Pitso Mosimane Apewa Tena Usukani wa Bafana Bafana

Global Publishers
September 1, 2026
0 views
0 Comments

Shirikisho la Soka la Afrika Kusini (SAFA) limemtangaza Pitso Mosimane kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Bafana Bafana.

Uteuzi huo unamrejesha Mosimane kwenye benchi la timu hiyo kwa mara ya pili, baada ya awali kuiongoza Bafana Bafana kati ya mwaka 2010 na 2012.

Mosimane anaingia kwenye nafasi hiyo akiwa miongoni mwa makocha wenye uzoefu mkubwa barani Afrika, kutokana na mafanikio aliyowahi kuyapata katika ngazi ya klabu na timu za taifa.

Kocha huyo sasa atakuwa na jukumu la kujenga kikosi imara cha Bafana Bafana na kuhakikisha timu hiyo inapata matokeo mazuri katika mashindano mbalimbali yajayo.

Katika kipindi chake cha kwanza kuiongoza Afrika Kusini, Mosimane alipata uzoefu muhimu wa kufanya kazi katika mazingira ya timu ya taifa, kabla ya kuendelea na safari yake ya ukocha katika klabu mbalimbali.

Katika majukumu yake mapya, anatarajiwa kufanya kazi kwa karibu na benchi lake la ufundi pamoja na viongozi wa SAFA kuhakikisha timu hiyo inafikia malengo yaliyowekwa.

Miongoni mwa majukumu makubwa yanayomsubiri Mosimane ni kuiandaa Bafana Bafana kwa ajili ya AFCON 2027, michuano ambayo Afrika Kusini inatarajiwa kushiriki.

Mosimane atatakiwa kujenga kikosi chenye ushindani na kuhakikisha timu hiyo inakuwa tayari kwa changamoto za michuano hiyo mikubwa ya soka barani Afrika.

Uteuzi wake unakuja baada ya kuondoka kwa Hugo Broos, ambaye aliiongoza Afrika Kusini katika Kombe la Dunia la FIFA 2026.

Sasa macho ya mashabiki wa Bafana Bafana yataelekezwa kwa Mosimane, ambaye anarudi kwenye benchi la timu hiyo akiwa na jukumu la kuendeleza ushindani na mafanikio ya Afrika Kusini katika soka la kimataifa.

Na Florah Anderson | GPL

MUME AUWAWA KWA KUDAI UNYUMBA MOROGORO

 

Na Lilian Kasenene, Morogoro 

Morogoro.FUNDI cherehani Jovita Bategeuye Budyo (30), mkazi wa Mafisa, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za kumuua mumewe, Abeli Charles (44), mfanyabiashara na mkazi wa Mafisa, Manispaa ya Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Andrew Kantimbo, tukio hilo lilitokea usiku wa Agosti 31, 2026, katika eneo la Mafisa, Kata ya Mafisa.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa mtuhumiwa na marehemu walikuwa wakiishi pamoja.

Aidha alisema wakati wakiwa wanajiandaa kula, kulitokea mgogoro ambao, kwa mujibu wa taarifa ya polisi, ulihusishwa na madai ya marehemu kunyimwa unyumba.

Mgogoro huo ulizua ugomvi mkubwa na inadaiwa mtuhumiwa alimpiga/kumkata marehemu kwa kitu chenye makali katika maeneo ya shingoni na kichwani, hali iliyosababisha majeraha makubwa na hatimaye kupelekea kifo chake.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limeendelea na uchunguzi wa tukio hilo na linamshikilia mtuhumiwa kwa hatua zaidi za kisheria.

Kamanda Kantimbo ametoa wito kwa wananchi kuepuka kutumia nguvu katika kutatua migogoro ya kifamilia na kijamii, badala yake kutumia njia salama za kumaliza tofauti na changamoto za mahusiano.

Pia amewataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha usalama unadumishwa, hasa kwa kuwalinda watoto, wazee, watu wenye ulemavu na makundi mengine yaliyo katika mazingira hatarishi.

Taarifa hiyo imetolewa Septemba 1, 2026, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro. ACP Kantimbo.

Mwisho

Rais Samia Aondoka Nchini Kwenda Zambia Kwa Uapisho Wa Hichilema

Global Publishers
September 1, 2026
936 views
0 Comments

Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiagana na Viongozi mbalimbali kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kabla ya kuondoka nchini, kuelekea Luzaka Zambia kuhudhuria Sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Zambia Mheshimiwa Hakainde Hichilema kufuatia ushindi alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa Zambia Uliofanyika tarehe 13 Agosti, 2026 ambapo Rais Hichilema alichaguliwa kwa Muhula mwengine wa Miaka mitano. Tarehe 01 Sept, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 1, 2026, ameondoka nchini kuelekea Lusaka, Zambia, kushuhudia sherehe za uapisho wa Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Rais Hichilema alichaguliwa tena katika Uchaguzi Mkuu wa Zambia uliofanyika Agosti 13, 2026, na amechaguliwa kuongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka mitano. Taarifa nyingine pia zimethibitisha kuwa uapisho huo umepangwa kufanyika Septemba 1, 2026.

Ziara ya Rais Samia nchini Zambia inaelezwa kuwa sehemu ya kuendeleza uhusiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Zambia, unaojengwa katika misingi ya umoja, mshikamano, ujirani mwema na ushirikiano wa kikanda.

Uhusiano kati ya Tanzania na Zambia umeendelea kuwa muhimu katika maeneo mbalimbali, ikiwemo biashara, usafirishaji na miundombinu, huku mataifa hayo yakishirikiana pia katika masuala ya maendeleo ya kikanda.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari S. Machumu.

Ndejembi Atua Kilimanjaro, Asalimiana Na Viongozi – Picha

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Deogratius Ndejembi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, leo tarehe 01 Septemba 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro leo, Jumanne, Septemba 1, 2026.

Mhe. Ndejembi alipowasili uwanjani hapo alipokelewa na kusalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kumpokea.

Ujio huo umefanyika leo Septemba 1, 2026, huku shughuli za kikazi za Makamu wa Rais zikiendelea katika mikoa mbalimbali nchini.

Mnyika Akabilia Maswali Mazito Mahakamani Katika Kesi Ya Lissu

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amekabiliana na maswali makali kutoka kwa Wakili wa Serikali, Katuga, wakati akiendelea kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.

Katika dodoso hilo, Mnyika alisisitiza kuwa jukumu lake ni kueleza kile anachokifahamu na alichokiona, huku akikataa baadhi ya madai yaliyowasilishwa na upande wa mashtaka.

Wakati mmoja, Wakili Katuga aliposema kazi yake ni kuonesha kwamba Mnyika ni mwongo, Mnyika alimjibu:

“Mimi kazi yangu ni kusema ukweli.”

Katika sehemu nyingine ya mahojiano, Mnyika aliulizwa kuhusu mkutano wa Aprili 3, 2025 na msimamo wa CHADEMA uliokuwa ukijulikana kwa kauli ya “No Reforms, No Election.”

Mnyika alisema mkutano huo ulikuwa na mada moja kuu iliyohusu msimamo wa chama kuhusu uchaguzi na mageuzi.

Alipoulizwa kuhusu kauli zinazohusishwa na kuhamasisha uasi, Mnyika alisema kwa uelewa wake wa kisiasa, uasi unaweza kumaanisha kupinga au kukataa jambo kwa nguvu kubwa, lakini alisisitiza kuwa katika muktadha alioueleza kulikuwa na njia za kidemokrasia.

Wakili Katuga alimuuliza Mnyika maana ya kuhamasisha uasi dhidi ya uchaguzi.

Mnyika alijibu kuwa kwake ilikuwa ni kukataa uchaguzi haramu kwa njia za kidemokrasia, huku akisisitiza kuwa neno “kidemokrasia” lilikuwa sehemu ya kauli yake.

Mnyika pia alitaja baadhi ya njia za kisiasa kama kususia uchaguzi na hatua nyingine zisizohusisha vurugu au fujo.

Alipoulizwa kama CHADEMA iliwahi kufungua kesi mahakamani kupinga uchaguzi, Mnyika alisema hakuwahi kufungua kesi hiyo.

Jaji: Shahidi unakumbushwa kwamba kiapo chako kinaendelea

Katuga: Unasema wewe ndio ulikiwakilisha chama kwenye kamati ya Bunge ya katiba na sheria?

Katuga: Waambie waheshimiwa kama unakumbuka au hukumbuki moja ya pendekezo ulilotoa ni kushirikishwa wakurugenzi kwenye maswala ya uchaguzi

Katuga: Waambie waheshimiwa kama unafahamu au hufahamu na mapendekezo yako yalipelekea wakurugenzi kuondolewa na kuwa maafisa wa uchaguzi

Katuga: Waambie waheshimiwa kama chama mlipata nafasi ya kutoa maoni ya mbele ya kamati hiyo kufanya maboresho ya sheria

Mnyika: Kwa kuwa nilizimiwa mic sikutoa maoni

Katuga: Ulitoa maoni kwenye mabadiliko ya kikatiba kabla ya mabadiliko

Katuga: Mada ni jambo linalojadiliwa bado unasimama na msimamo mada na ajenda ni vitu viwili tofauti

Mnyika: Ndio ni vitu viwili tofauti Katuga kwa tafsiri hii unaimbia mahakama mkutano wa tarehe tatu haukuwa na agenda ulikuwa na Mada

Mnyika: Ndio hakukuwa na ajenda ni mada

Katuga: Kwa kuwa hakukuwa na agenda na ni mada kiongozi alikuwa na uhuru wa kuzungumza jambo lolote alilolipanga na kuamua kutekeleza

Mnyika: Mkutano ulikuwa na mada moja tu ‘No reforms no election’

Katuga: Uliulizwa kama uasi ni kosa kisheria ukasema sio kosa na ukamnukuu Nyerere kuwa alisema vijana waasi dhidi ya Mifumo kandamizi

Katuga: Waambie majaji uelewa wako wa kisiasa neno uasi lina maana gani

Mnyika: Kupinga au kukataa kwa nguvu kubwa sana

Katuga: Kuhamasisha uasi dhidi ya uchaguzi tafsiri yake ni nini

Mnyika: Ni kukataaaa uchaguzi haramu kwa njia za kidemokrasia Katuga waambie waheshimiwa tafsiri yako ya uasi kama ndivyo ulivyowaambia waheshimiwa na kama kulikuwa na demokrasia

Mnyika: Nimesema na hayo maneno kidemokrasia yapo

Katuga: Mimi kazi yangu kuonesha ulivyo Muongo

Mnyika: Mimi kazi yangu kusema ukweli

Katuga: Hiyo tafsiri uliyoitoa ni kwa mujibu wa nani au nini?

Mnyika: Uelewa wangu kisiasa

Katuga: Mwaka Jana chama chako kilishiriki uchaguzi mkuu?

Mnyika: Tulizuiliwa kushiriki

Katuga: Waambie majaji kama unakumbuka ni kweli kwamba ulisikia mwenyekiti akiwaambia watia nia kama unategemea kuwa mbunge mwaka huu sahauni

Katuga: Mwenyekiti na yeye alisema yeye alikuwa na nia ya kugombea urais ila ame ahirisha

Mnyika: Hiyo sentensi siikumbuki

Katuga: Kama chama cha siasa na wewe ni mtendaji mkuu mlijiandaa kushiriki uchaguzi wa mwaka jana 2025?

Mnyika: Tulijiandaa vizuri sana

Katuga: Waambie majaji kama mlijiandaa kushiriki kwa mujibu wa katiba na marekebisho yaliyofanyika

Mnyika: Tulijiandaa kwa mujibu wa katiba iliyipo na mapungufu yake

Katuga: Unajua kuwa kwa haki hiyo waliyokuwa nayo CHADEMA na vyama vingine vilikuwa nayo?

Katuga: Mwenyekiti alisema tutazuia uchaguzi kwa njia ya kidemokrasia

Mnyika: Sikutumia moja kwa moja maneno unayoyasema ila nilieleza njia za kidemokrasia

Katuga: Sasa katika ushahidi wako waambie majaji kwamba njia zilizosemwa na mwenyekiti za kuzuia uchaguzi kidemoktasia ni njia moja, mbili, tatu,

Katuga: Waambie majaji kama kuhasisha uasi ni njia ya kidemokrasia kupinga uchaguzi usifanyike

Mnyika: Ndio ni njiaa ya kidemokrasia

Katuga: Umekubali kuwa vyama vingine vina haki ya kushiriki uchaguzi

Mnyika: Uchaguzi huru wa haki

Katuga: Waambie majaji ulikuwa wa aina gani

Mnyika: Haukuwa wa huru wala wa haki na jaji nyalali alisema…

Katuga: Sikilizaaaaa, Waambie majaji kwa maneno yako vilikuwa na haki ya kushiriki uchaguzi

Mnyika: Siwezi kuvitolea maoni vyama vingine

Katuga: Kwa elimu yako hiyo ni demokrasia gani itakayotumika kumzuia mtu anayeenda kupiga kura

Mnyika: Kuahirisha uchaguzi na njia nyingine za kidemokrasia

Katuga: Uliwahi kufungua kesi kupinga uchaguzi?

Katuga: Ni njia gani ya kidemokrasia isiyokuwa ya mahakamani inayoweza kumzuia mtu kupiga kura

Mnyika: Njia zipo nyingi, kususia uchaguzi na njia nyingine sio vurugu sio fujo wala sio nini

Katuga: Waambie majaji mtu anayekwenda kupiga kura kama hakuna zuio mahakamani njia pekee ya kumzuia ni kwa kutumia njia ya nguvu zote za uasi

Katuga: Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, Je inaruhusu mtu kuamini anacho amini

Katuga: Je katiba ya CHADEMA inaheshimu imani ya mtu ilimradi asivunje sheria?

Katuga: Je kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA inaelekeza mtu asiamini anachokiamini ilimradi asivunje sheria?

Katuga: Mwenyekiti aliposema tutakinukisha tutahamasisha uasi alilenga kufanyike mabadiliko ambayo nyie ndio mnaamini ni mabadiliko yanayofaa?

Mnyika: Sielewi umeuliza nini, rudia swali lako

Katuga: Mwenyekiti aliposema tutakunukisha, tutahamasisha uasi alilenga kufanyike mabadiliko ambayo nyie ndio mnaamini ni mabadiliko yanayofaaa?

Katuga: Baada ya mwenyekiti kupata kesi hii nani aliendeleza hamasa ya no reforms no election

Mnyika: Kamati kuu ya Chama, viongozi wa kamati kuu

Katuga: Je kiongozi aliyeongoza hii nia ni pamoja na makamo mwemyekiti?

Katuga: Makamo mwenyekiti anaitwa Nani?

Mnyika: John Wegesa Heche

Katuga: Waambie majaji kama na yeye ulikuwa unamuandalia press conference na mikutano

Mnyika: Hapana sikumuandalia

Katuga: Waambie majaji kama hao viongozi waliendelea kuhamasisha umma kuhusu nia hiyo ya kuzuia uchaguzi

Mnyika: Tarehe tisa mwezi wa sita ndio ilikuwa mwisho kabla ya kuzuiwa kufanyika shughuli za kisiasa

Katuga: Waambie majaji kama unajua makamo mwenyekiti bara aliwahikuongea na East Africa Radio kuhusu nia hiyo ya kuzuia uchaguzi

Katuga: Unajua kupitia hiyo redio alitangaza uchaguzi wa 2025 hautokuepo na mko determined?

Katuga: Waambie majaji kama unajua kwenye uchaguzi wa mwaka jana kulikuwa na jaribio la kuzuia uchaguzi kwa kufanya fujo

Mnyika: Kulikuwa na mauaji ndio ninachojua

Katuga: Kulikuwa na jaribio la kuzuai uchaguzi kwa kuchoma vituo na miundombinu mingine?

Katuga: Siku ya uchaguzi mwaka jana ulikuwa nchini au nje ya nchi

Katuga: Je ulijitokeza kupiga kura?

Katuga: Kwa imani hiyo imedhihirisha ile nia ya kuzuia uchaguzi

Katuga: Unajua au haujui kuna mali za watu zilichomwa moto?

Mnyika: Sijui nilisikia kwenye vyombo vya habari

Katuga: Unajua au haujui vituo vya mwendo kasi vilichomwa?

Mnyika: Nimeviona vimeungua

Katuga: Ni sahihi au sio sahihi kwa umma kutafsiri kauli zile na kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani

Katuga: Je, ni haki sio haki kwa umma kutafsiri waonavyo maneno ya mwenyekiti?

Katuga: Ni haki ya Jamii kuchochoke na kufanya vurugu

Katuga: Waambie majaji ni haki au sio haki

Katuga: Jaji chande alisema matukio ya 2025 yalipelekea vifo vya watu

Katuga: Waeleze majaji kama ulisikia akisema matukio yale yalihamasishwa na kutokana na maneno ya wanasiasa

Katuga: Kwa mujibu wa hotuba ya Jaji chande waambie majaji kama hotuba hii inafanana na kile kilichopelekea machafuko

Katuga: Waeleze majaji kama Lissu alihamasisha uasi ili kuwa na uchaguzi huru na wa haki

Katuga: Jaji chande aliposema vurugu zile zilitokana na maneno ya kudai sheria ya uchaguzi

Mnyika: Hapana hakuyasema na mwenyekiti hakuhusika na vurugu

Katuga: Uliwahi kuwa mbunge, je ni wakuteuliwa au kuchaguliwa?

Katuga: Kwa uzoefu wako kuhusu bunge unauelewa wa katiba na sheria?

Katuga: Waambie majaji mahakama ni chombo cha mwisho kwa mujibu wa sheria

Kikosi Cha Man City Cha 2023 Chaanza Kutoweka, Wabaki Wachezaji Wawili

Kikosi cha Manchester City kilichotwaa UEFA Champions League mwaka 2023 na kukamilisha Treble kinaendelea kuvunjika, huku wachezaji wengi waliokuwa sehemu ya timu hiyo wakiondoka klabuni hapo.

Manchester City iliandika historia mwaka 2023 baada ya kutwaa UEFA Champions League kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.

City ilishinda fainali dhidi ya Inter Milan kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Istanbul, Uturuki, huku Rodri akifunga bao pekee lililoipa timu hiyo taji la Ulaya na kukamilisha msimu wa Treble.

Miaka mitatu baadaye, sura ya kikosi hicho imebadilika kwa kiasi kikubwa.

WACHEZAJI WENGI WAMEONDOKA

Miongoni mwa nyota waliokuwa sehemu ya kikosi cha City kilichotwaa Champions League mwaka 2023 lakini ambao sasa wameondoka klabuni hapo ni Ederson, John Stones, Nathan Aké, Rodri, İlkay Gündoğan, Kevin De Bruyne, Jack Grealish na Bernardo Silva.

Kuondoka kwa nyota hao kunaashiria mwisho wa kizazi kilichokuwa msingi wa mafanikio makubwa ya Manchester City katika miaka ya nyuma.

 

WABAKI WAWILI TU

Baada ya Rodri kuondoka na kujiunga na Barcelona, idadi ya wachezaji waliosalia kutoka kwenye kikosi cha kwanza kilichoanza fainali ya Champions League mwaka 2023 imefikia wawili pekee.

Wachezaji hao ni Rúben Dias na Erling Haaland.

Hivyo, City sasa iko katika kipindi cha mabadiliko makubwa, huku mastaa waliokuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya klabu hiyo wakiondoka mmoja baada ya mwingine.

CITY YAJENGA KIZAZI KIPYA

Manchester City imeanza kujenga kikosi kipya kwa kufanya usajili wa wachezaji kadhaa wenye umri mdogo.

Miongoni mwa wachezaji waliowasili ni Ayyoub Bouaddi, Elliot Anderson na Allan Elias, ambao wanatarajiwa kuwa sehemu ya kizazi kipya cha klabu hiyo.

Mabadiliko hayo yanaashiria mwanzo wa sura mpya kwa Manchester City baada ya kipindi cha mafanikio makubwa kilichoipa klabu hiyo mataji mbalimbali, likiwemo taji lake la kwanza la Champions League na Treble ya mwaka 2023.

Kwa sasa, Rúben Dias na Erling Haaland ndio wachezaji wawili pekee waliosalia kutoka kwenye kikosi cha kwanza kilichoanza fainali ya Istanbul mwaka 2023, huku City ikiendelea kujenga timu mpya kwa ajili ya miaka ijayo.

Stori na Na Haika Urio | GPL – TUDACO

MOI YAANZISHA HUDUMA MAALUM YA KIHARUSI

 

Na Hamida Ramadhan,Matukio Daima Media Dodoma

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imeanzisha huduma maalum ya kutibu kiharusi (stroke), ikiwa ni sehemu ya hatua za kupanua huduma za kibingwa na ubingwa bobezi nchini.

Huduma hiyo ni miongoni mwa huduma mpya zilizoanzishwa na Taasisi hiyo, pamoja na upasuaji wa ubongo kupitia tundu la pua, tiba ya maumivu sugu ya mgongo na upasuaji wa magoti kwa njia ya matundu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya, amesema kuanzishwa kwa huduma hizo kumesaidia kupunguza wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Amesema huduma za kibingwa zilizoanzishwa na Taasisi hiyo zimewezesha kupunguza rufaa za wagonjwa wa mifupa kwa asilimia 98 na wagonjwa wa ubongo kwa asilimia 97.

Kwa mujibu wa Dkt. Ulisubisya, MOI imeendelea kuimarisha huduma za uchunguzi na matibabu kwa kutumia vifaa vya kisasa, ikiwamo MRI, CT Scan, Digital X-Ray, Ultrasound, Brain Lab na vifaa vya kisasa vya upasuaji wa ubongo na mgongo.

“Katika mwaka wa fedha 2025/2026, MOI ilihudumia wagonjwa 211,359, ambapo 202,000 walikuwa wagonjwa wa nje na 9,359 walilazwa ,” Amesema.

Aidha, Taasisi hiyo imeendelea kutoa huduma za fiziotherapia kwa wagonjwa wenye changamoto mbalimbali za kiafya, ikiwamo waliopata majeraha, kufanyiwa upasuaji na wenye matatizo ya mifupa na mishipa ya fahamu.

“Katika kipindi hicho, wagonjwa 71,819 walipatiwa huduma za fiziotherapia kwa lengo la kurejesha nguvu za misuli, uwezo wa kutembea na utendaji wa viungo vya mwili, ” Amesema.

Dkt. Ulisubisya amesema MOI itaendelea kuanzisha huduma mpya za kibingwa na ubingwa bobezi kwa kutumia teknolojia za kisasa, pamoja na kusogeza huduma karibu na wananchi kupitia programu za outreach na vituo vya satellite katika mikoa mbalimbali.

Mzunguko Mmoja Kuanzisha Mnyororo Wa Ushindi Ndani Ya Meridian Bonanza

Global Publishers
September 1, 2026
30 views
0 Comments

Burudani ya kasino mtandaoni imepata sura mpya baada ya Meridianbet kuendelea kukupa Meridian Bonanza, mchezo unaochanganya kasi, burudani na vipengele vinavyoweza kufanya kila mzunguko kuwa wa kusisimua. Ukiwa na muonekano wa kuvutia, sauti zenye kuongeza hamasa na mfumo rahisi wa kucheza, Meridian Bonanza imeandaliwa kuwapa wapenzi wa kasino uzoefu unaokaribia ladha ya kasino halisi.

Mchezo huu hauishii kwenye mwonekano wake pekee, bali umebeba vipengele vinavyoongeza msisimko kila unapocheza. Miongoni mwa vitu vinavyoutofautisha ni Ante Bet, inayokupa nafasi ya kuongeza dau na kufungua mizunguko ya bure. Ukichagua kizidishi cha x20, unaweza kufungua hadi mizunguko 100 ya bure, hivyo kuongeza muda wa kushuhudia kile ambacho kila mzunguko unaweza kuleta.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kisha kuna Tumble, kipengele kinachoweza kugeuza mzunguko mmoja kuwa mfululizo wa matukio ya kusisimua. Mara alama za ushindi zinapotokea, huondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na alama nyingine, hivyo nafasi ya kupata ushindi mwingine ndani ya mzunguko huo huendelea kuwepo hadi mfululizo unapokatika.

Lakini macho yote yanaelekezwa kwenye Scatter. Ukifanikiwa kupata alama hii maalumu, unafungua mizunguko 10 ya bure. Ndani ya mizunguko hiyo, kizidishi kinaweza kufika hadi X100, jambo linaloongeza zaidi msisimko wa mchezo na kufanya kila mzunguko kuwa na matarajio yake.

Meridian Bonanza ipo tayari kwa wapenzi wa kasino wanaotaka kujaribu burudani yenye kasi na vipengele vya kipekee. Jisajili Meridianbet, ingia kwenye Meridian Bonanza na uanze safari yako ya burudani.

Waamuzi Wanne wa Tanzania Wateuliwa Kusimamia Mechi ya CAF

Global Publishers
September 1, 2026
96 views
0 Comments

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limewateua rasmi waamuzi kutoka Tanzania kusimamia mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).

Uteuzi huo unaongeza heshima na kuonyesha kuongezeka kwa imani kwa waamuzi wa Tanzania katika medani ya soka la kimataifa barani Afrika.

WATASIMAMIA MECHI ALGERIA

Waamuzi hao watakuwa na jukumu la kusimamia mchezo wa hatua ya awali ya CAF Champions League kati ya JS Saoura ya Algeria na Horoya AC ya Guinea.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa Ijumaa, Septemba 4, 2026, katika Uwanja wa Miloud Hadefi, Algeria.

WAAMUZI WALIOTEULIWA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha waamuzi watakaowakilisha Tanzania katika mchezo huo pamoja na majukumu yao.

  • Nasir Salum (Siyah) – Mwamuzi wa kati, Zanzibar.
  • Mohamed Mkono – Mwamuzi msaidizi namba moja, Tanga.
  • Ally Ramadhani (Kibo) – Mwamuzi msaidizi namba mbili, Zanzibar.
  • Ahmed Arajiga – Mwamuzi wa akiba/mezani, Manyara.

Uteuzi huo unawapa waamuzi hao nafasi ya kuendelea kujenga uzoefu katika mashindano ya ngazi ya juu barani Afrika na pia kuiwakilisha Tanzania katika jukwaa la kimataifa.

Mchezo kati ya JS Saoura na Horoya AC unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku macho yakiwa pia kwa waamuzi hao wa Tanzania katika kuhakikisha mchezo unachezwa kwa kufuata sheria za soka.

Stori na Peter Jinanai | GPL

Waamuzi Watano wa Tanzania Wateuliwa Kusimamia Mechi za CAF

Global Publishers
September 1, 2026
12 views
0 Comments

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limewateua rasmi waamuzi kutoka Tanzania kusimamia mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).

Uteuzi huo unaongeza heshima na kuonyesha kuongezeka kwa imani kwa waamuzi wa Tanzania katika medani ya soka la kimataifa barani Afrika.

WATASIMAMIA MECHI ALGERIA

Waamuzi hao watakuwa na jukumu la kusimamia mchezo wa hatua ya awali ya CAF Champions League kati ya JS Saoura ya Algeria na Horoya AC ya Guinea.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa Ijumaa, Septemba 4, 2026, katika Uwanja wa Miloud Hadefi, Algeria.

WAAMUZI WALIOTEULIWA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha waamuzi watakaowakilisha Tanzania katika mchezo huo pamoja na majukumu yao.

  • Nasir Salum (Siyah) – Mwamuzi wa kati, Zanzibar.
  • Mohamed Mkono – Mwamuzi msaidizi namba moja, Tanga.
  • Ally Ramadhani (Kibo) – Mwamuzi msaidizi namba mbili, Zanzibar.
  • Ahmed Arajiga – Mwamuzi wa akiba/mezani, Manyara.

Uteuzi huo unawapa waamuzi hao nafasi ya kuendelea kujenga uzoefu katika mashindano ya ngazi ya juu barani Afrika na pia kuiwakilisha Tanzania katika jukwaa la kimataifa.

Mchezo kati ya JS Saoura na Horoya AC unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku macho yakiwa pia kwa waamuzi hao wa Tanzania katika kuhakikisha mchezo unachezwa kwa kufuata sheria za soka.

Stori na Peter Jinanai | GPL