
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amekabiliana na maswali makali kutoka kwa Wakili wa Serikali, Katuga, wakati akiendelea kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.
Katika dodoso hilo, Mnyika alisisitiza kuwa jukumu lake ni kueleza kile anachokifahamu na alichokiona, huku akikataa baadhi ya madai yaliyowasilishwa na upande wa mashtaka.
Wakati mmoja, Wakili Katuga aliposema kazi yake ni kuonesha kwamba Mnyika ni mwongo, Mnyika alimjibu:
“Mimi kazi yangu ni kusema ukweli.”
Katika sehemu nyingine ya mahojiano, Mnyika aliulizwa kuhusu mkutano wa Aprili 3, 2025 na msimamo wa CHADEMA uliokuwa ukijulikana kwa kauli ya “No Reforms, No Election.”

Mnyika alisema mkutano huo ulikuwa na mada moja kuu iliyohusu msimamo wa chama kuhusu uchaguzi na mageuzi.
Alipoulizwa kuhusu kauli zinazohusishwa na kuhamasisha uasi, Mnyika alisema kwa uelewa wake wa kisiasa, uasi unaweza kumaanisha kupinga au kukataa jambo kwa nguvu kubwa, lakini alisisitiza kuwa katika muktadha alioueleza kulikuwa na njia za kidemokrasia.
Wakili Katuga alimuuliza Mnyika maana ya kuhamasisha uasi dhidi ya uchaguzi.
Mnyika alijibu kuwa kwake ilikuwa ni kukataa uchaguzi haramu kwa njia za kidemokrasia, huku akisisitiza kuwa neno “kidemokrasia” lilikuwa sehemu ya kauli yake.
Mnyika pia alitaja baadhi ya njia za kisiasa kama kususia uchaguzi na hatua nyingine zisizohusisha vurugu au fujo.
Alipoulizwa kama CHADEMA iliwahi kufungua kesi mahakamani kupinga uchaguzi, Mnyika alisema hakuwahi kufungua kesi hiyo.
Jaji: Shahidi unakumbushwa kwamba kiapo chako kinaendelea
Katuga: Unasema wewe ndio ulikiwakilisha chama kwenye kamati ya Bunge ya katiba na sheria?
Katuga: Waambie waheshimiwa kama unakumbuka au hukumbuki moja ya pendekezo ulilotoa ni kushirikishwa wakurugenzi kwenye maswala ya uchaguzi
Katuga: Waambie waheshimiwa kama unafahamu au hufahamu na mapendekezo yako yalipelekea wakurugenzi kuondolewa na kuwa maafisa wa uchaguzi
Katuga: Waambie waheshimiwa kama chama mlipata nafasi ya kutoa maoni ya mbele ya kamati hiyo kufanya maboresho ya sheria
Mnyika: Kwa kuwa nilizimiwa mic sikutoa maoni
Katuga: Ulitoa maoni kwenye mabadiliko ya kikatiba kabla ya mabadiliko
Katuga: Mada ni jambo linalojadiliwa bado unasimama na msimamo mada na ajenda ni vitu viwili tofauti
Mnyika: Ndio ni vitu viwili tofauti Katuga kwa tafsiri hii unaimbia mahakama mkutano wa tarehe tatu haukuwa na agenda ulikuwa na Mada
Mnyika: Ndio hakukuwa na ajenda ni mada
Katuga: Kwa kuwa hakukuwa na agenda na ni mada kiongozi alikuwa na uhuru wa kuzungumza jambo lolote alilolipanga na kuamua kutekeleza
Mnyika: Mkutano ulikuwa na mada moja tu ‘No reforms no election’
Katuga: Uliulizwa kama uasi ni kosa kisheria ukasema sio kosa na ukamnukuu Nyerere kuwa alisema vijana waasi dhidi ya Mifumo kandamizi
Katuga: Waambie majaji uelewa wako wa kisiasa neno uasi lina maana gani
Mnyika: Kupinga au kukataa kwa nguvu kubwa sana
Katuga: Kuhamasisha uasi dhidi ya uchaguzi tafsiri yake ni nini
Mnyika: Ni kukataaaa uchaguzi haramu kwa njia za kidemokrasia Katuga waambie waheshimiwa tafsiri yako ya uasi kama ndivyo ulivyowaambia waheshimiwa na kama kulikuwa na demokrasia
Mnyika: Nimesema na hayo maneno kidemokrasia yapo
Katuga: Mimi kazi yangu kuonesha ulivyo Muongo
Mnyika: Mimi kazi yangu kusema ukweli
Katuga: Hiyo tafsiri uliyoitoa ni kwa mujibu wa nani au nini?
Mnyika: Uelewa wangu kisiasa
Katuga: Mwaka Jana chama chako kilishiriki uchaguzi mkuu?
Mnyika: Tulizuiliwa kushiriki
Katuga: Waambie majaji kama unakumbuka ni kweli kwamba ulisikia mwenyekiti akiwaambia watia nia kama unategemea kuwa mbunge mwaka huu sahauni
Katuga: Mwenyekiti na yeye alisema yeye alikuwa na nia ya kugombea urais ila ame ahirisha
Mnyika: Hiyo sentensi siikumbuki
Katuga: Kama chama cha siasa na wewe ni mtendaji mkuu mlijiandaa kushiriki uchaguzi wa mwaka jana 2025?
Mnyika: Tulijiandaa vizuri sana
Katuga: Waambie majaji kama mlijiandaa kushiriki kwa mujibu wa katiba na marekebisho yaliyofanyika
Mnyika: Tulijiandaa kwa mujibu wa katiba iliyipo na mapungufu yake
Katuga: Unajua kuwa kwa haki hiyo waliyokuwa nayo CHADEMA na vyama vingine vilikuwa nayo?
Katuga: Mwenyekiti alisema tutazuia uchaguzi kwa njia ya kidemokrasia
Mnyika: Sikutumia moja kwa moja maneno unayoyasema ila nilieleza njia za kidemokrasia
Katuga: Sasa katika ushahidi wako waambie majaji kwamba njia zilizosemwa na mwenyekiti za kuzuia uchaguzi kidemoktasia ni njia moja, mbili, tatu,
Katuga: Waambie majaji kama kuhasisha uasi ni njia ya kidemokrasia kupinga uchaguzi usifanyike
Mnyika: Ndio ni njiaa ya kidemokrasia
Katuga: Umekubali kuwa vyama vingine vina haki ya kushiriki uchaguzi
Mnyika: Uchaguzi huru wa haki
Katuga: Waambie majaji ulikuwa wa aina gani
Mnyika: Haukuwa wa huru wala wa haki na jaji nyalali alisema…
Katuga: Sikilizaaaaa, Waambie majaji kwa maneno yako vilikuwa na haki ya kushiriki uchaguzi
Mnyika: Siwezi kuvitolea maoni vyama vingine
Katuga: Kwa elimu yako hiyo ni demokrasia gani itakayotumika kumzuia mtu anayeenda kupiga kura
Mnyika: Kuahirisha uchaguzi na njia nyingine za kidemokrasia
Katuga: Uliwahi kufungua kesi kupinga uchaguzi?
Katuga: Ni njia gani ya kidemokrasia isiyokuwa ya mahakamani inayoweza kumzuia mtu kupiga kura
Mnyika: Njia zipo nyingi, kususia uchaguzi na njia nyingine sio vurugu sio fujo wala sio nini
Katuga: Waambie majaji mtu anayekwenda kupiga kura kama hakuna zuio mahakamani njia pekee ya kumzuia ni kwa kutumia njia ya nguvu zote za uasi
Katuga: Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, Je inaruhusu mtu kuamini anacho amini
Katuga: Je katiba ya CHADEMA inaheshimu imani ya mtu ilimradi asivunje sheria?
Katuga: Je kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA inaelekeza mtu asiamini anachokiamini ilimradi asivunje sheria?
Katuga: Mwenyekiti aliposema tutakinukisha tutahamasisha uasi alilenga kufanyike mabadiliko ambayo nyie ndio mnaamini ni mabadiliko yanayofaa?
Mnyika: Sielewi umeuliza nini, rudia swali lako
Katuga: Mwenyekiti aliposema tutakunukisha, tutahamasisha uasi alilenga kufanyike mabadiliko ambayo nyie ndio mnaamini ni mabadiliko yanayofaaa?
Katuga: Baada ya mwenyekiti kupata kesi hii nani aliendeleza hamasa ya no reforms no election
Mnyika: Kamati kuu ya Chama, viongozi wa kamati kuu
Katuga: Je kiongozi aliyeongoza hii nia ni pamoja na makamo mwemyekiti?
Katuga: Makamo mwenyekiti anaitwa Nani?
Mnyika: John Wegesa Heche
Katuga: Waambie majaji kama na yeye ulikuwa unamuandalia press conference na mikutano
Mnyika: Hapana sikumuandalia
Katuga: Waambie majaji kama hao viongozi waliendelea kuhamasisha umma kuhusu nia hiyo ya kuzuia uchaguzi
Mnyika: Tarehe tisa mwezi wa sita ndio ilikuwa mwisho kabla ya kuzuiwa kufanyika shughuli za kisiasa
Katuga: Waambie majaji kama unajua makamo mwenyekiti bara aliwahikuongea na East Africa Radio kuhusu nia hiyo ya kuzuia uchaguzi
Katuga: Unajua kupitia hiyo redio alitangaza uchaguzi wa 2025 hautokuepo na mko determined?
Katuga: Waambie majaji kama unajua kwenye uchaguzi wa mwaka jana kulikuwa na jaribio la kuzuia uchaguzi kwa kufanya fujo
Mnyika: Kulikuwa na mauaji ndio ninachojua
Katuga: Kulikuwa na jaribio la kuzuai uchaguzi kwa kuchoma vituo na miundombinu mingine?
Katuga: Siku ya uchaguzi mwaka jana ulikuwa nchini au nje ya nchi
Katuga: Je ulijitokeza kupiga kura?
Katuga: Kwa imani hiyo imedhihirisha ile nia ya kuzuia uchaguzi
Katuga: Unajua au haujui kuna mali za watu zilichomwa moto?
Mnyika: Sijui nilisikia kwenye vyombo vya habari
Katuga: Unajua au haujui vituo vya mwendo kasi vilichomwa?
Mnyika: Nimeviona vimeungua
Katuga: Ni sahihi au sio sahihi kwa umma kutafsiri kauli zile na kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani
Katuga: Je, ni haki sio haki kwa umma kutafsiri waonavyo maneno ya mwenyekiti?
Katuga: Ni haki ya Jamii kuchochoke na kufanya vurugu
Katuga: Waambie majaji ni haki au sio haki
Katuga: Jaji chande alisema matukio ya 2025 yalipelekea vifo vya watu
Katuga: Waeleze majaji kama ulisikia akisema matukio yale yalihamasishwa na kutokana na maneno ya wanasiasa
Katuga: Kwa mujibu wa hotuba ya Jaji chande waambie majaji kama hotuba hii inafanana na kile kilichopelekea machafuko
Katuga: Waeleze majaji kama Lissu alihamasisha uasi ili kuwa na uchaguzi huru na wa haki
Katuga: Jaji chande aliposema vurugu zile zilitokana na maneno ya kudai sheria ya uchaguzi
Mnyika: Hapana hakuyasema na mwenyekiti hakuhusika na vurugu
Katuga: Uliwahi kuwa mbunge, je ni wakuteuliwa au kuchaguliwa?
Katuga: Kwa uzoefu wako kuhusu bunge unauelewa wa katiba na sheria?
Katuga: Waambie majaji mahakama ni chombo cha mwisho kwa mujibu wa sheria
