Global Publishers
September 1, 2026
12 views
0 Comments

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limewateua rasmi waamuzi kutoka Tanzania kusimamia mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).
Uteuzi huo unaongeza heshima na kuonyesha kuongezeka kwa imani kwa waamuzi wa Tanzania katika medani ya soka la kimataifa barani Afrika.
WATASIMAMIA MECHI ALGERIA
Waamuzi hao watakuwa na jukumu la kusimamia mchezo wa hatua ya awali ya CAF Champions League kati ya JS Saoura ya Algeria na Horoya AC ya Guinea.
Mchezo huo umepangwa kuchezwa Ijumaa, Septemba 4, 2026, katika Uwanja wa Miloud Hadefi, Algeria.
WAAMUZI WALIOTEULIWA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha waamuzi watakaowakilisha Tanzania katika mchezo huo pamoja na majukumu yao.
- Nasir Salum (Siyah) – Mwamuzi wa kati, Zanzibar.
- Mohamed Mkono – Mwamuzi msaidizi namba moja, Tanga.
- Ally Ramadhani (Kibo) – Mwamuzi msaidizi namba mbili, Zanzibar.
- Ahmed Arajiga – Mwamuzi wa akiba/mezani, Manyara.
Uteuzi huo unawapa waamuzi hao nafasi ya kuendelea kujenga uzoefu katika mashindano ya ngazi ya juu barani Afrika na pia kuiwakilisha Tanzania katika jukwaa la kimataifa.
Mchezo kati ya JS Saoura na Horoya AC unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku macho yakiwa pia kwa waamuzi hao wa Tanzania katika kuhakikisha mchezo unachezwa kwa kufuata sheria za soka.
Stori na Peter Jinanai | GPL
