MWENGE WA UHURU 2026: WANANCHI BUKOBA WAFUNGULIWA HUDUMA JANJA YA MAJI, MWANG’ONDA ATOA WITO.

Na Matukio Daima Media

BUKOBA, KAGERA 

 Wananchi zaidi ya 700 wa Kata ya Ijuganyondo, Halmashauri ya Bukoba, wameanza kunufaika na huduma ya maji safi na salama kufuatia uzinduzi wa Mradi wa Kituo Janja, huku Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Michael Wazo Mwang’onda, akiwataka wananchi kulinda na kutunza miundombinu hiyo ili iendelee kutoa huduma kwa muda mrefu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Mwang’onda amesema upatikanaji wa maji safi na salama ni sehemu muhimu ya kuboresha maisha ya wananchi, kwa kuwa unasaidia kuimarisha afya, usafi wa mazingira na kupunguza muda unaotumika kutafuta maji.

Amesema huduma hiyo pia itawawezesha wananchi kutumia muda wao katika shughuli za kiuchumi na kijamii, hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kaya na jamii kwa ujumla.

“Ni jukumu la wananchi kuhakikisha miundombinu hii inalindwa na kutunzwa ili iweze kudumu na kuendelea kutoa huduma kwa jamii kwa muda mrefu,” amesema Mwang’onda.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na Mhandisi kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA), Edmund Deus, ujenzi wa Kituo Janja umetokana na upanuzi wa mtandao wa mradi wa maji unaohudumia Kata za Ijuganyondo na Karabagine.

Deus amesema uzinduzi wa kituo hicho ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na muhimu za kijamii, sambamba na kuimarisha miundombinu inayolenga kuboresha ustawi wa wananchi na kuchochea maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa upande wao, wananchi wa Kata ya Ijuganyondo wameeleza kufurahishwa na ujio wa mradi huo, wakisema huduma ya maji inayopatikana karibu na makazi yao itawasaidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji iliyokuwa ikiikabili jamii hiyo.

Wamesema upatikanaji wa maji karibu utawapunguzia muda na nguvu zinazotumika kutafuta maji, huku ukitoa fursa kwa jamii kuelekeza muda zaidi katika shughuli za uzalishaji na maendeleo.

Uzinduzi wa Kituo Janja unaongeza kasi ya jitihada za Serikali za kusogeza huduma muhimu za kijamii karibu na wananchi, hasa katika maeneo ambayo yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama.

Wakati huo huo, Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 zinaendelea katika Mkoa wa Kagera, zikiwa na kauli mbiu:

“Tanzania ni yetu sote, Tushikamane.”

Kupitia kauli hiyo, Mwenge wa Uhuru unaendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, kutunza miradi ya Serikali na kuimarisha mshikamano katika jamii.

Dortmund Yaanza Safari Ya Dfb Cup Dhidi Ya Hebc Hamburg

Leo Jumanne, tarehe 1 Septemba 2026, saa 21:45, uwanja wa Volksparkstadion jijini Hamburg utakuwa jukwaa la mechi ya raundi ya kwanza ya Kombe la DFB kati ya HEBC Hamburg na Borussia Dortmund. Hii ni mechi ya kihistoria kwa klabu ya HEBC, ambayo haijashiriki mashindano ya Kombe la Ujerumani tangu mwaka 1935 miaka 91 iliyopita.

HEBC Hamburg ni klabu ndogo inayochezea ligi ya tano ya Ujerumani, Oberliga Hamburg. Wamefika raundi hii kwa kushinda Kombe la Mkoa wa Hamburg (Hamburger Pokal), jambo lililowawezesha kukutana na timu kubwa ya ligi kuu. Kwa sababu uwanja wao wa nyumbani hubeba mashabiki wachache tu kwa kawaida, mechi hii ililazimika kuhamishiwa Volksparkstadion.

Kwa upande wa Dortmund, msimu unaanza kwa ratiba ngumu na mikutano miwili mfululizo dhidi ya timu za Hamburg. Baada ya kuanza msimu wa Bundesliga kwa kuipokea HSV, sasa Kombe linawapeleka Volksparkstadion kukutana na HEBC, timu ya Oberliga. Chochote kisichokuwa ushindi wa Dortmund kingekuwa mshangao mkubwa, hasa ikizingatiwa kwamba timu ya kocha Niko Kovac, licha ya maandalizi magumu ya awali, imekuwa katika hali nzuri hivi karibuni.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kabla ya mechi hii, Dortmund ilionyesha nguvu zake za msimu mpya kwa kuanza kampeni ya Bundesliga kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Hamburger SV nyumbani. Aidha, timu hiyo ilikuwa na maandalizi ya kuvutia msimu wa kiangazi baada ya kufunga msimu uliopita katika nafasi ya pili ya Bundesliga, mabao 16 nyuma ya mabingwa Bayern Munich. Hata hivyo, Dortmund ilipoteza fainali ya Supercup ya Franz Beckenbauer kwa mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao wakubwa, Bayern Munich, tarehe 22 Agosti.

Kihistoria mechi hii ni ya kipekee kwa sababu HEBC Hamburg na Borussia Dortmund hazijawahi kukutana hapo awali, hivyo leo itakuwa mwanzo wa rekodi yao ya ana kwa ana. Ingawa kitaalamu nafasi ya HEBC kuendelea mbele ni ndogo sana dhidi ya jitu la Bundesliga, usiku huu utabaki kuwa historia kwa wachezaji wa Eimsbüttel kutoka viwanja vya udongo na mashabiki wachache, hadi mwanga wa fluji na viti 57,000 vya Volksparkstadion. Huu ndio uzuri wa Kombe la DFB fursa ya wasiokuwa na jina kukutana na mabingwa, hata kama kwa jioni moja tu.

WANANCHI BUKOBA WAFUNGULIWA HUDUMA JANJA YA MAJI, MWANG’ONDA ATOA WITO.

Na Matukio Daima Media -BUKOBA, KAGERA 

Wananchi zaidi ya 700 wa Kata ya Ijuganyondo, Halmashauri ya Bukoba, wameanza kunufaika na huduma ya maji safi na salama kufuatia uzinduzi wa Mradi wa Kituo Janja, huku Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Michael Wazo Mwang’onda, akiwataka wananchi kulinda na kutunza miundombinu hiyo ili iendelee kutoa huduma kwa muda mrefu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Mwang’onda amesema upatikanaji wa maji safi na salama ni sehemu muhimu ya kuboresha maisha ya wananchi, kwa kuwa unasaidia kuimarisha afya, usafi wa mazingira na kupunguza muda unaotumika kutafuta maji.

Amesema huduma hiyo pia itawawezesha wananchi kutumia muda wao katika shughuli za kiuchumi na kijamii, hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kaya na jamii kwa ujumla.

“Ni jukumu la wananchi kuhakikisha miundombinu hii inalindwa na kutunzwa ili iweze kudumu na kuendelea kutoa huduma kwa jamii kwa muda mrefu,” amesema Mwang’onda.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na Mhandisi kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA), Edmund Deus, ujenzi wa Kituo Janja umetokana na upanuzi wa mtandao wa mradi wa maji unaohudumia Kata za Ijuganyondo na Karabagine.

Deus amesema uzinduzi wa kituo hicho ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na muhimu za kijamii, sambamba na kuimarisha miundombinu inayolenga kuboresha ustawi wa wananchi na kuchochea maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa upande wao, wananchi wa Kata ya Ijuganyondo wameeleza kufurahishwa na ujio wa mradi huo, wakisema huduma ya maji inayopatikana karibu na makazi yao itawasaidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji iliyokuwa ikiikabili jamii hiyo.

Wamesema upatikanaji wa maji karibu utawapunguzia muda na nguvu zinazotumika kutafuta maji, huku ukitoa fursa kwa jamii kuelekeza muda zaidi katika shughuli za uzalishaji na maendeleo.

Uzinduzi wa Kituo Janja unaongeza kasi ya jitihada za Serikali za kusogeza huduma muhimu za kijamii karibu na wananchi, hasa katika maeneo ambayo yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama.

Wakati huo huo, Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 zinaendelea katika Mkoa wa Kagera, zikiwa na kauli mbiu:

“Tanzania ni yetu sote, Tushikamane.”

Kupitia kauli hiyo, Mwenge wa Uhuru unaendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, kutunza miradi ya Serikali na kuimarisha mshikamano katika jamii

Polisi Arusha Wamkamata Godlisten Malisa, Aachiwa Kwa Dhamana

Global Publishers
September 1, 2026
6 views
0 Comments

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limemkamata Godlisten Elisante Malisa pamoja na mwenzake kwa tuhuma za jinai zilizokuwa zikichunguzwa dhidi yao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi, Malisa na mwenzake walikamatwa jana, Agosti 31, 2026, majira ya usiku mkoani Arusha.

Baada ya kukamatwa, wawili hao walifanyiwa mahojiano kuhusiana na tuhuma zilizokuwa zikichunguzwa dhidi yao.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa baada ya mahojiano, Malisa na mwenzake waliachiwa kwa dhamana, huku wakisubiri kukamilishwa kwa taratibu nyingine za kisheria.

Taarifa hiyo haijaeleza kwa undani aina ya kosa la jinai linalochunguzwa wala hatua nyingine zitakazochukuliwa dhidi yao, zaidi ya kueleza kuwa taratibu za kisheria zinaendelea.

HASARA YA MGOMO WA WAFANYAKAZI WA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA NCHINI KENYA

Baada ya zaidi ya saa 18 za mazungumzo, wadau katika sekta ya usafiri wa anga nchini Kenya wamekubaliana kusitisha mgomo uliodumu kwa siku mbili.

Katika taarifa iliyochapishwa mapema Jumanne, Waziri wa Uchukuzi wa Umma nchini Kenya, Davis Chirchir, amesema: “Kufuatia makubaliano yaliyofikiwa, KAWU inatangaza kusitisha mgomo huo mara moja na kuwaelekeza wafanyakazi walioathirika kurejea katika majukumu yao ya kawaida.”

Kwa sasa, pande zote zimeahidi kujitolea kurejesha haraka shughuli za kawaida za usafiri wa anga, kudumisha amani ya viwanda na kutatua malalamiko yoyote yaliyosalia au yatakayojitokeza baadaye kupitia mazungumzo, upatanishi na mifumo iliyoanzishwa kisheria.

Hata hivyo, baadhi ya watu tuliozungumza nao wameeleza hofu ya kukumbwa na ucheleweshaji wa safari kutokana na safari nyingi kuahirishwa awali. Wengi wana hofu kuwa itachukua muda kabla ya hali ya kawaida kurejea.

Taarifa hii imekuja kama afueni kwa maelfu ya wasafiri waliokwama katika viwanja vya ndege si tu nchini Kenya bali pia katika maeneo mengine duniani. Maelfu ya wasafiri walikwama katika miji kama Doha, London na Johannesburg wakisubiri safari ambazo zilitarajiwa kutua Nairobi au kuunganishwa kupitia Nairobi, baada ya kuahirishwa kwa zaidi ya saa sita.

Kwa mujibu wa Chama cha Wahudumu wa Usafiri wa Anga nchini Kenya (KAAO), Shirika la Mashirika ya Ndege Afrika (AFRAA) na Shirikisho la Utalii nchini Kenya (KTF), hasara iliyopatikana katika siku mbili za mgomo huenda ikafikia dola bilioni moja za Marekani, sawa na ilivyoshuhudiwa mwezi Februari mwaka huu wakati Chama cha Wafanyakazi wa Viwanja vya Ndege nchini Kenya (KAWU) kilipoitisha mgomo mwingine.

Kulingana na mwandishi huru na mtaalamu wa masuala ya uchumi, Julian Amboko, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) una umuhimu mkubwa kwa wasafiri wengi, hasa kutoka Afrika Magharibi ambao hutegemea Kenya Airways kwa usafiri wao. Kwa sababu hiyo, safari nyingi kutoka eneo hilo hupitia Nairobi, huku wengi wakitumia uwanja huo kuunganisha safari kuelekea Ulaya, Mashariki ya Kati, Asia na mataifa ya Kusini mwa Afrika.

Wengi wameulizia iwapo viwanja vingine vya ndege katika ukanda wa Afrika Mashariki vinaweza kuziba pengo linaloachwa wazi wakati wa matatizo kama yale yaliyoshuhudiwa nchini Kenya katika siku mbili zilizopita.

Kulingana na Amboko, ikiwa Kenya haitafanya juhudi za kupanua JKIA au kujenga uwanja mpya wa ndege, upanuzi wa viwanja vya ndege na ujenzi wa viwanja vipya katika mataifa jirani unaweza kuiondoa JKIA katika nafasi yake ya sasa kama kitovu kikuu cha usafiri wa anga katika ukanda huo kwa kuzingatia idadi ya wasafiri wanaopita katika uwanja huo kila siku.

Baada ya mazungumzo ya siku nzima, Waziri wa Uchukuzi wa Umma nchini Kenya, Davis Chirchir, alitangaza kwamba pande hizo zilikubaliana kuwa ada za wakala zinazoshikiliwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Kenya (KAA) zitarejeshwa kwa KAWU mara moja.

Kuhusu masuala ya Mkataba wa Majadiliano ya Pamoja (CBA) wa KCAA, Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC) imejitolea kuwashirikisha wahusika ndani ya mfumo husika wa kisheria na kiudhibiti, kwa kuzingatia uwezo wa mashirika ya serikali yanayohusika kulipa.

Suala la mkataba wa utambuzi kati ya KAWU na Jambojet linasubiri maelekezo ya mahakama. Pande hizo zimesema zinaheshimu mchakato unaoendelea wa kimahakama na zitaendelea kuongozwa na matakwa yote ya kisheria na kiutaratibu yanayohusiana na suala hilo.

Huku mgomo ukisitishwa kwa sasa, pande husika zinatarajiwa kuendelea kufanya vikao vya kutatua malalamiko yaliyosalia ya wafanyakazi hao katika wiki chache zijazo.

Kwa sasa, kampuni kama Kenya Airways na Jambojet zimetangaza kurejelewa kwa safari za ndege, huku wasafiri wengi wakielekea viwanjani kuthibitisha iwapo wataweza kusafiri kwa muda uliopangwa.

Mbeto: Jussa Usithubutu Kuwagombanisha Watanzania Kwa Utashi wa Kisiasa

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC ya CCM Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis, amemtaka Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa Ladu, kuacha kutumia misamiati ya Utanganyika na Uzanzibari kwa kile alichodai kuwa ni juhudi za kuwagawa na kuwagombanisha Watanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi zake Kisiwandui, Mbeto amesema Utanzania ni msingi wa umoja, mshikamano na udugu kati ya Watanganyika na Wazanzibari, ambao umeendelea kudumu kwa zaidi ya miaka 62 tangu Muungano wa mwaka 1964.

Mbeto amesema ameshangazwa na kile alichokiita mwenendo wa kisiasa wa Jussa wa kuibua tofauti kati ya wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar, akidai kuwa hatua hiyo ni aina ya “fitna za siasa za uke wenza.”

Mbeto amesema kwa wiki kadhaa Jussa amekuwa akijionesha kuwa na mapenzi makubwa kwa Zanzibar huku akiwakebehi wananchi wa Tanzania Bara, bila kuzingatia kuwa miongoni mwao wapo pia wanachama na wafuasi wa ACT-Wazalendo.

Amedai kuwa mwenendo huo unalenga kujenga taswira kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anapendwa zaidi na Wazanzibari kuliko wananchi wa Tanzania Bara.
“Mwambieni Jussa aachane na aina ya siasa za uke wenza. Rais Dkt. Samia tangu aingie madarakani amekuwa kipenzi cha Watanzania wote. Aina ya uongozi wake haina tofauti na viongozi wenzake waliomtangulia,” alisema Mbeto.

Mbeto amesema Rais Samia si kiongozi wa Wazanzibari pekee, bali ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo hakuna haja ya kutumia tofauti za kisiasa na kimaeneo kujaribu kuwagombanisha wananchi.

Akizungumzia historia ya uongozi nchini, Mbeto amesema viongozi waliowahi kuongoza Tanzania hawakujifunga katika maeneo yao ya kuzaliwa, bali waliongoza nchi nzima.
“Julius Nyerere hakuwa Rais wa Butiama, Ali Hassan Mwinyi hakuiongoza Mangapwani wala Benjamin Mkapa hakuwa Rais wa Lupaso. Kadhalika, Jakaya Kikwete hakuitwa Rais wa Msoga, John Magufuli hakuitawala Chato na Dkt. Samia si Rais wa Kizimkazi,” alisisitiza.

Amesema mifano hiyo inaonesha umuhimu wa kutenganisha maeneo ambayo viongozi wamezaliwa na nafasi zao za kitaifa, akisisitiza kuwa viongozi wa Tanzania wamekuwa wakiongoza nchi nzima.

Mbeto amemtaka Jussa kutambua hatua ambayo Watanzania wamefikia katika kujenga umoja na mshikamano, akisema hakuna mtu wala kundi lenye uwezo wa kuwagawa na kuwarudisha katika hali ya kabla ya Muungano wa mwaka 1964.

Ameeleza kuwa fikra za kuamini Tanzania inaweza kugawanyika kwa misingi ya maeneo au tofauti za kisiasa ni “ndoto za mchana na njozi za jinamizi.”
“Jussa acha fikra mgando kwa kudhani utafanikiwa kuwagawa Watanzania kwa utashi wako wa kisiasa. Waulize baba na kaka zako waliojaribu kufanya mtihani huo walifikia wapi,” alisema.

Mbeto amesema vyama vya siasa vinaweza kuwa na mitazamo na misimamo tofauti, lakini tofauti hizo hazipaswi kutumiwa kama sababu ya kuwagawa wananchi kwa misingi ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Amesema CCM, ACT-Wazalendo na vyama vingine vya siasa vina haki ya kuwa na tofauti zao za kisiasa, lakini hakuna sababu ya kutumia tofauti hizo kuwagonganisha viongozi au kuchochea migawanyiko miongoni mwa wananchi.
“Si Jussa, ACT-Wazalendo wala wenzake ambao wamewahi kuwa na upendo kwa CCM. Hivyo, majaribu yoyote ya kutaka kuwagonganisha viongozi au kuwafitini, ngoma hiyo itapasukia kwake,” alimaliza.

Baada Ya Miaka 30; Keefe D Akutwa na Hatia ya Mauaji ya Tupac Shakur

Mahakama nchini Marekani imemkuta na hatia Duane “Keffe D” Davis kwa kosa la mauaji ya mwanamuziki maarufu wa Hip Hop, Tupac Shakur, katika tukio lililotokea takribani miaka 30 iliyopita huko Las Vegas, Nevada.

Davis amepatikana na hatia baada ya kesi hiyo iliyohusu kifo cha Tupac, ambaye alipigwa risasi mjini Las Vegas mwaka 1996 na kufariki siku chache baadaye kutokana na majeraha aliyoyapata.

Katika hoja za kuhitimisha kesi hiyo, upande wa mashtaka ulidai kuwa Davis alikuwa mmoja wa viongozi wa kundi la South Side Compton Crips na kwamba alihusika katika kupanga na kusimamia tukio lililosababisha kifo cha Tupac Shakur.

Mwendesha mashtaka pia alikitaja kitabu cha kumbukumbu za maisha ya Davis kama sehemu muhimu ya ushahidi uliowasilishwa mahakamani.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, maelezo yaliyomo katika kitabu hicho kuhusu tukio hilo yanaweza kuchukuliwa kama kukiri kwa Davis kuhusu kile alichokijua na nafasi yake katika tukio lililosababisha kuuawa kwa Tupac.

UTETEZI WAPINGA USHAHIDI

Kwa upande mwingine, mawakili wa Davis walipinga hoja za upande wa mashtaka, wakisema maelezo yaliyotolewa na mteja wao kuhusu tukio hilo katika kitabu chake yalikuwa “hadithi ya kubuni.”

Utetezi pia ulieleza kuwepo kwa mapungufu katika uchunguzi wa kesi hiyo, ukiwemo upotevu wa baadhi ya kumbukumbu muhimu za uchunguzi.

Aidha, mawakili hao walidai kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaomuunganisha Davis na mauaji ya Tupac Shakur.

Baada ya kupatikana na hatia, Davis anatarajiwa kurejea mahakamani Oktoba 13 kwa ajili ya kusomewa hukumu yake.

Davis tayari ameeleza kuwa ana mpango wa kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Kifo cha Tupac Shakur kimeendelea kuwa miongoni mwa matukio makubwa na yenye utata katika historia ya muziki wa Hip Hop, huku uchunguzi wa mauaji yake ukiendelea kwa miongo kadhaa kabla ya Davis kukabiliwa na mashtaka.

Stori na Na; Lailath Burhan | GPL – TUDACO

Keefe D Akutwa na Hatia ya Mauaji ya Tupac Shakur

Rais Samia Kwenda Zambia Kushuhudia Uapisho wa Hichilema leo Septemba 1, 2026

Global Publishers
September 1, 2026
60 views
0 Comments

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 1, 2026, anatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Lusaka, Zambia, kushuhudia sherehe za uapisho wa Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Rais Hichilema alichaguliwa tena katika Uchaguzi Mkuu wa Zambia uliofanyika Agosti 13, 2026, na amechaguliwa kuongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka mitano. Taarifa nyingine pia zimethibitisha kuwa uapisho huo umepangwa kufanyika Septemba 1, 2026.

Ziara ya Rais Samia nchini Zambia inaelezwa kuwa sehemu ya kuendeleza uhusiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Zambia, unaojengwa katika misingi ya umoja, mshikamano, ujirani mwema na ushirikiano wa kikanda.

Uhusiano kati ya Tanzania na Zambia umeendelea kuwa muhimu katika maeneo mbalimbali, ikiwemo biashara, usafirishaji na miundombinu, huku mataifa hayo yakishirikiana pia katika masuala ya maendeleo ya kikanda.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari S. Machumu.

Rais Samia Kwenda Zambia Kushuhudia Uapisho Wa Hichilema Leo

Global Publishers
September 1, 2026
0 views