BALOZI SIRRO AHIMIZA WATANZANIA KUKATA BIMA

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma 

Mkuu wa mkoa Kigoma  Balozi Simon Sirro  amewataka Watanzania kubadili mtazamo wao kuhusu bima na kuanza kuiona kama sehemu ya maandalizi ya maisha badala ya kuichukulia kuwa gharama isiyo na umuhimu.

Balozi Sirro alisema hayo wakati akizindua kampeni ya utoaji elimu na uhamasishaji jamii kujiunga na huduma za bima za maisha na mali zinazotolewa na Shirika la Bima la Taifa (NIC) ambapo alibainisha kuwa bima ya maisha na mali ni muhimu kwa maisha ya Watanzania kabla hawajapata majanga.

Katika hotuba ya Mkuu huyo wa mkoa iliyotolewa na  Mkuu wa wilaya Kigoma,DkRashid Chuachua alisema kuwa  wananchi wanapaswa kuhakikisha wanaweka mipango ya kulinda maisha yao, familia, mali na shughuli za uzalishaji kwa kuchagua aina ya bima inayokidhi mahitaji yao kutoka NIC.

Awali Mkurugenzi wa idara ya mawasiliano  na masoko wa shirika hilo, Karim Meshack alimesema kuwa elimu  na ufahamu duni wa umuhimu wa bima umechangia idadi kubwa ya watanzania kushindwa kukata bima za maisha na mali  na hivyo kuathirika yanapotokea majanga ambapo kwa sasa ni asilimia tano tu ya watanzania ndiyo wamejiunga na huduma hiyo.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa  changamoto kubwa ni baadhi ya wananchi kutotambua kuwa bima ni kinga muhimu ya maisha, mali na shughuli zao za kiuchumi, badala yake wengi huanza kufikiria kuhusu bima baada ya kukumbwa na ajali au kupata hasara ambapo alisema kuwa bima inaweza kumsaidia mtu, familia au mfanyabiashara kukabiliana na athari za kifedha zinazoweza kujitokeza baada ya kutokea tukio lisilotarajiwa.

Kwa sasa  alisema kuwa katika awamu hii ya kampeni hiyo kwa mikoa ya Magharibi na kanda ya ziwa itakayochukua siku 12 alisema kuwa watafika maeneo mbalimbali ya mkoa Kigoma kampeni inayojulikana kama NIC Kitaa na kwamba bima ya mali na maisha ni muhimu kwa maisha ya Mtanzania kabla na anapopata majanga.

Mwisho.

Maduro Aonekana kwa Mara ya Kwanza Akiwa Gerezani Marekani

Aliyekuwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza akiwa ndani ya gereza nchini Marekani, miezi kadhaa baada ya kukamatwa na kupelekwa nchini humo.

Picha hizo, ambazo zimeibua gumzo kubwa, zinamuonyesha Maduro akiwa amevalia mavazi ya kijivu huku akiinua mikono yake na kuonyesha ishara ya ushindi.

Hii ni mara ya kwanza kwa umma kumuona akiwa ndani ya Metropolitan Detention Center (MDC) iliyopo Brooklyn, New York, ambako anashikiliwa wakati akiendelea kukabiliwa na mchakato wa kisheria nchini Marekani.

Katika ujumbe ulioambatana na picha hizo kwenye mitandao yake ya kijamii, Maduro amesema yeye pamoja na watu wake wanaendelea kuwa imara. Pia ametoa shukrani kwa familia yake na wafuasi wake kwa maombi pamoja na mshikamano wanaoendelea kumuonyesha.

Hata hivyo, jambo lililozua maswali zaidi ni muda ambao picha hizo zilipigwa na muda zilipotangazwa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, picha hizo zinaonekana kuwa zilipigwa Juni 25, 2026, lakini zikawekwa hadharani Agosti 30, 2026, hali ambayo imeongeza mjadala kuhusu mazingira na sababu za kucheleweshwa kwa kuchapishwa kwake.

Maduro kwa sasa anakabiliwa na mashtaka nchini Marekani, ambayo ameyakana, huku kesi yake ikiendelea kufuatiliwa kwa karibu na jumuiya ya kimataifa.

Kuonekana kwake kwa mara ya kwanza akiwa gerezani kumeongeza mjadala kuhusu mustakabali wake wa kisiasa, pamoja na athari ambazo kesi hiyo inaweza kuwa nazo kwa siasa za Venezuela.

Kwa sasa, macho yanaendelea kuelekezwa kwenye hatua zinazofuata za kesi yake nchini Marekani na namna zitakavyoweza kuathiri mustakabali wa Maduro pamoja na hali ya kisiasa nchini Venezuela.

Stori na Mwajabu Abdallah | GPL 

Nafasi za Kazi Wezesha Mzawa Microfinance – Loan Officer, Mwisho wa Maombi Agosti 31, 2026

Global Publishers
August 31, 2026
9,042 views
0 Comments

We are seeking a motivated, experienced Loan officer/ Credit officer to join our growing company. In this position, you will evaluate and approve or deny loan applications. You will act as liaison between financial institutions, individuals, and businesses applying for loans as well as process loan applications, solicit loans, and act as intermediary for creditors and borrowers.

Loan Officer Job Duties:

  • Evaluates loan applications and documentation by confirming credit worthiness.
  • Improves loan applications and documentation by informing applicant of additional requirements.
  • Rejects loans by explaining deficiencies to applicants.
  • Approves loans by issuing checks or forwarding applications to loan committee.
  • Completes loan contracts by explaining provisions to applicant; obtaining signatures and notarizations; collecting fees.
  • Helps customers by answering questions; responding to requests.
  • Maintains customer confidence by keeping loan information confidential.
  • Accomplishes Company mission by completing related results as needed.

Qualification;

  • Bachelor of finance, economics, Marketing, Business, Banking or related field
  • Experience in the relevant field will be an added advantage
  • Proficient computer skills, including Microsoft Office Suite
  • Able to analyze financial records and transfer data

Additional Knowledge, Skills & Abilities

  • Excellent customer service skills, attentiveness, and information retention.
  • Detail oriented, high degree of accuracy.
  • Familiar with banking regulations and responsibilities relating to each including a working.
  • Self-starter, ability to work independently.
  • Strong communication & organizational skills.
  • Competence with computers.
  • Ability to work in a fast-paced environment & under pressure as needed.
  • The ability to make sound decisions. This may include making on-the-spot decisions regarding customer transactions; weighing customer satisfaction issues with the Bank’s exposure to loss or fraud and the ability to think through and rationalize decisions.

All applications should be filed through the following email address or the physical address with necessary certified attachments befor August 31, 2026.

WEZESHA MZAWA MICROFINANCE,

P.O.BOX 7534, SINZA-MORI,

OPPOSITE WANYAMA HOTEL

DAR ES SALAAM, TANZANIA.

EMAIL: [email protected]

Majalila & Kilimanjaro FC Za Katavi Zapokea Vifaa Vya Michezo Kutoka Meridianbet

Global Publishers
August 31, 2026
36 views
0 Comments

Mchezo wa soka katika manispaa ya Tanganyika, Katavi umeendelea kupata nguvu mpya baada ya Meridianbet kufanya zoezi jingine la uwajibikaji kwa jamii (CSR), likilenga kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana. Kampuni hiyo imekabidhi vifaa maalum vya michezo, ikiwemo jezi za mpira na mipira, kwa timu za Majalila FC na Kilimanjaro FC. Hatua hiyo imepokelewa kama nyongeza muhimu kwa timu hizo katika kuendelea na shughuli zao za michezo na kuwapa vijana mazingira bora ya kushiriki soka.

Kwa vijana wanaoishi na ndoto za kuwa mastaa wa soka, kila mpira, kila jezi na kila nafasi ya kucheza inaweza kuwa sehemu ya safari kuelekea mafanikio. Meridianbet imeamua kugusa eneo hilo moja kwa moja kwa kuhakikisha timu hizo zinapata vifaa vinavyoweza kuongeza hamasa na kurahisisha ushiriki wa vijana katika michezo. Zaidi ya ushindani wa uwanjani, msaada huo unalenga kuimarisha mshikamano, nidhamu na mahusiano miongoni mwa wanajamii kupitia nguvu ya michezo.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Akizungumza kuhusu hatua hiyo, mwakilishi wa Meridianbet, Nancy Ingram, amesema kampuni inatambua mchango mkubwa wa michezo katika kujenga jamii yenye afya na umoja. “Tunatambua umuhimu wa michezo katika kuleta afya, umoja na kuimarisha mahusiano ya kijamii,” alisema. Kauli hiyo inaweka wazi msimamo wa Meridianbet wa kuendelea kushirikiana na jamii katika kujenga mazingira yanayowawezesha vijana kutumia vipaji vyao kwa njia chanya.

Vilevile amesisitiza kuwa Meridianbet imekuwa mstari wa mbele kusaidia ukuaji wa michezo katika jamii, kwa lengo la kuhakikisha vijana wanapata nafasi ya kushiriki bila vikwazo visivyo vya lazima. Kwa Majalila FC na Kilimanjaro FC, msaada huu haujaja tu kama vifaa, bali pia kama ishara ya kuaminiwa na kupewa hamasa ya kupambana zaidi. Sasa ni zamu ya wachezaji kugeuza msaada huo kuwa nguvu ya kufanya vizuri zaidi wanaposhuka dimbani.

Hatua ya Meridianbet ndani ya Katavi ni mfano mwingine wa namna sekta binafsi inavyoweza kuwa sehemu ya safari ya maendeleo ya michezo nchini. Majalila FC na Kilimanjaro FC wamepata nyenzo mpya, huku vijana wa Tanganyika Municipal wakipokea ujumbe kwamba vipaji vyao vina nafasi ya kukua.

Miamaba ya Ulaya Uwanjani Barça na Arsenal Kusaka Ushindi Leo

Mechi kali zinatarajiwa kupigwa kwenye viwanja mbalimbali huku tayari Meridianbet wakiwa wamekuwekea Odds za kuvutia. Je nani unampendelea zaidi kukupatia matokeo?. Jisajili hapa.

Ligi kuu kule Hispania yaani LALIGA itaendelea ambapo Barcelona atakipiga dhidi ya  Rayo Vallecano ambapo mabingwa hao watetezi wanataka kuanza msimu wakiwa na kasi nzuri katika harakati za kutetea ubingwa wao.

Chini ya Hansi Flick wanaingia kwenye mchezo wakiwa na kikosi chenye uwezo mkubwa wa kutawala mpira. Mfumo wao unategemea pasi za haraka, pressing baada ya kupoteza mpira na kutumia kasi ya wachezaji wa pembeni.

Kitu muhimu zaidi kitakuwa kufungua ulinzi wa Rayo, kwa sababu Rayo si timu rahisi.  Barca wanahitaji kufanya kazi ya ziada kuhakikisha wanafungua nafasi za kalbu hiyo na kuweza kupata magoli. Beti hapa.

Barcelona wanahitaji kuzungusha mpira kwa haraka na kutumia nafasi kati ya mabeki na viungo wa Rayo.

Lakini pia mchezo huu pia unaweza kuwa muhimu kwa Rodri, ambaye anatarajiwa kupata dakika zake za kwanza Barcelona baada ya kujiunga kutoka Manchester City. Flick amesema anatarajiwa kucheza dakika chache na uzoefu wake unaweza kusaidia Barcelona kuongeza udhibiti wa kiungo.

Je pesa yako unaiweka kwa nani kati ya hizi timu mbili?. Ingia kwenye akaunti yako na usuka jamvi la ushindi siku ya leo.

Piga pesa kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

EPL kule Uingereza kutakuwa na mtanange wa kukata na shoka ambapo mabingwa watetezi wa ligi hiyo Arsenal watakuwa ugenini kupepetana dhidi ya Aston Villa ambao walishangazwa kwenye mechi yao ya kwanza kwa kipigo kizito.

Vijana wa Mikel Arteta wameendelea kuuthibitishia ulimwengu kuwa mafanikio ya msi u uliyopita, hayakuja kwa bahati mbaya bali kwa kujituma na uwezo mkubwa ambao wachezaji walionesha hivyo hii mechi pia wanahitaji kwenda kufanya maajabu makubwa kabisa pale Villa Park.

Meridianbet kama kawaida wao wanampa nafasi kubwa The Gunners kuondoka na ushindi siku ya leo kutokana na kiwango ambacho anacho, lakini je vijana wa Unai watakubali kupoteza mechi ya pili mfululizo kwenye ligi?. Odds kubwa zipo hapa. Jisajili hapa.

Takwimu zinaonesha kuwa msimu uliopita kwenye mechi mbili walizokutana, kila mtu alishinda nyumbani kwake, hivyo kila timu iliondoka na pointi 3 kwenye mechi mbili walizokutana. Je safari hii itakuwaje?

Arsenal wamejiimarisha sana kwenye msimu huu kwa kuleta wachezaji wenye uwezo mkubwa akiwemo Tzolis ambaye alionesha kiwango bora kabisa kwenye mechi ya kwanza  na wachezaji wengine wakifanya vyema kabisa na kuihakikishia ushindi klabu hiyo ya London.

Lakini pia unaweza ukaweka machaguo zaidi ya 1000 kwenye mtanange huu wa leo ambapo hapo utakuwa na nafasi ya kushinda kabisa, lakini pia unaweza ukatumia BET BUILDER kufanya ubashiri mechi hii.

Msichana Wa Miaka 14 Auawa Akirekodi Tiktok, Kijana Wa Miaka 17 Akamatwa

Msichana mwenye umri wa miaka 14, Zytina Mason-Brown, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi.

Washington, D.C. — Kifo cha kutatanisha cha Zytina Mason-Brown, msichana mwenye umri wa miaka 14, kimechukua mwelekeo mpya baada ya kijana wa miaka 17 kukamatwa na kushtakiwa kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga risasi mwaka 2025.

Zytina alipigwa risasi Mei 21, 2025, katika nyumba moja iliyopo Benning Road, Washington, D.C., wakati ambapo inadaiwa alikuwa akirekodi video za TikTok.

Kwa mujibu wa Polisi wa Metropolitan Police Department (MPD), polisi walifika katika eneo hilo majira ya saa 5:08 jioni baada ya kupokea taarifa kuhusu tukio la ufyatuaji risasi.

Walipofika, walimkuta Zytina akiwa hana fahamu na hapumui, huku akiwa amejeruhiwa vibaya kwa risasi. Alitangazwa kuwa amefariki dunia eneo la tukio.

Uchunguzi wa Ofisi ya Mchunguzi Mkuu wa Vifo baadaye uliainisha kifo chake kama mauaji.

MASHTAKA YAIBUA MAELEZO MAPYA

Zaidi ya mwaka mmoja baada ya tukio hilo, polisi walimkamata kijana mwenye umri wa miaka 17 mnamo Agosti 26, 2026, na kumfungulia shtaka la mauaji akiwa na silaha.

Mpelelezi wa polisi aliieleza mahakama kuwa kijana huyo alikuwa na umri wa miaka 15 wakati tukio hilo lilipotokea.

Awali, kijana huyo aliwaambia polisi kuwa Zytina alijipiga risasi kwa bahati mbaya wakati akichezea bunduki ambayo alidai aliipata kutoka kwa mjomba wake.

Wakati huo, kulikuwa na msichana mwingine katika chumba hicho ambaye alithibitisha maelezo hayo.

Hata hivyo, miezi kadhaa baadaye, shahidi huyo alibadilisha maelezo yake na kutoa simulizi tofauti kuhusu kilichotokea.

Kwa mujibu wa maelezo yake mapya, Zytina alikuwa akirekodi video za TikTok wakati kijana huyo alipoanza kucheza karibu naye. Inadaiwa Zytina alimsukuma kijana huyo ili aondoke karibu naye.

Shahidi huyo alidai kuwa baada ya kusukumwa, kijana huyo alimpiga Zytina risasi.

Baada ya mlio wa risasi, mama wa kijana huyo alianza kugonga mlango wa chumba hicho. Kwa mujibu wa shahidi, kijana huyo alimwambia asimweleze mtu yeyote kuhusu kilichotokea.

Polisi waliitwa na uchunguzi ukaendelea.

Shahidi huyo naye alikamatwa mwezi Juni kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kwa mamlaka, baada ya awali kutoa maelezo ambayo polisi walidai hayakuwa ya kweli.

Kesi hiyo sasa inaendelea mahakamani, huku kijana huyo akikabiliwa na shtaka la mauaji ya daraja la pili akiwa na silaha.

Kumbuka: Maelezo kuhusu namna Zytina alivyopigwa risasi yanatokana na ushahidi uliowasilishwa mahakamani na madai ya shahidi; hayajathibitishwa kuwa ukweli wa mwisho wa kesi.

Iran Yashambulia Kambi Mbili Za Marekani Nchini Jordan

Shechambo Chris
August 31, 2026
72 views
0 Comments

Iran  imefanya mashambulizi kwenye kambi mbili za kijeshi za Marekani nchini Jordan, kwa kutumia makombora ya ndege zisizo na rubani (drones), ikiwa ni hatua ya kulipiza kisasi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Iran, mashambulizi hayo yalilenga kambi za kijeshi za Marekani za King Hussein na Al-Azraq nchini Jordan.

Hatua hiyo imekuja baada ya Marekani kufanya mashambulizi dhidi ya maeneo ya kijeshi ya Iran katika kisiwa cha Larak, kusini mwa Iran.

Tehran imesema mashambulizi yake dhidi ya vituo vya Marekani yalikuwa jibu la moja kwa moja kwa operesheni hiyo ya Marekani.

Kwa upande wa Jordan, jeshi la nchi hiyo limesema mifumo yake ya ulinzi wa anga ilinasa makombora yaliyoelekezwa katika maeneo yake, mamlaka za Jordan zimeripoti kuwa hakuna vifo wala majeruhi vilivyothibitishwa kutokana na mashambulizi hayo.

Marekani imekuwa na uwepo wa kijeshi nchini Jordan, ambayo ni mshirika muhimu wa Washington katika Mashariki ya kati,kwa sababu hiyo mashambulizi hayo yameongeza wasiwasi kuhusu uwezekano wa mvutano kati ya Marekani na Iran kuenea zaidi katika eneo hilo.

Marekani imesema mashambulizi yake dhidi ya Larak yalilenga kuzuia vitisho kwa usafiri wa meli katika eneo la Strait of Hormuz, njia muhimu kwa usafirishaji wa mafuta duniani.

Iran, kwa upande wake, imekosoa vikali hatua hiyo ya Marekani na kuahidi kujibu mashambulizi yoyote dhidi ya maeneo yake.

Na Tereza Muga



ABIRIA WALALA JKIA HUKU MGOMO WA WAFANYAKAZI WA SEKTA YA ANGA UKIENDELEA

 

Mamia ya abiria wamekwama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi tangu Jumapili.

Wasafiri hao, ambao walitarajiwa kusafiri kupitia uwanja mkubwa zaidi wa ndege nchini Kenya, walilala katika maeneo ya mapokezi ya uwanja huo wakisubiri maelekezo kutoka kwa mashirika ya ndege.

Siku ya Jumatatu asubuhi, mashirika kadhaa ya ndege yalikuwa yakishughulikia taratibu za kuwapeleka abiria wao kwenye hoteli.

Hii ni baada ya wafanyakazi wa usafiri wa anga, chini ya Chama cha Wafanyakazi wa Usafiri wa Anga cha Kenya (KAWU), kuanza mgomo wao Jumapili, wakitangaza kupunguzwa kwa muda kwa shughuli katika viwanja vya ndege vya Kenya.

Wafanyakazi hao wanadai ustawi ulioboreshwa, mazingira bora ya kazi na utekelezaji wa marupurupu ya ajira yaliyokubaliwa hapo awali.

Kuanzia JKIA jijini Nairobi hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Moi huko Mombasa, shughuli zilisimama Jumapili.

Katibu Mkuu wa KAWU Moss Ndiema alisema wanachama waliacha kazi zao katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Kenya, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege vya Kenya na Jambojet, na hawangeendelea hadi malalamiko ya chama hicho dhidi ya yote matatu yatakapotatuliwa

Marekani Yashambulia Iran, Drone Yaangushwa Mlango wa Hormuz

WASHINGTON — Marekani imetekeleza mashambulizi dhidi ya Iran baada ya vikosi vyake kushambulia vizindua viwili vya roketi katika Kisiwa cha Larak, kilichopo kwenye Mlango wa Hormuz, hatua inayotajwa kuwa mashambulizi ya kwanza ya Marekani dhidi ya Iran tangu mwishoni mwa Julai.

Kisiwa cha Larak, kilichopo karibu na Bandari ya Bandar Abbas, kina umuhimu mkubwa kimkakati kutokana na nafasi yake katika njia za meli zinazopita kwenye Mlango wa Hormuz, eneo muhimu kwa usalama wa usafirishaji wa baharini na usambazaji wa nishati duniani.

Baada ya mashambulizi hayo, vyombo vya habari vya Iran viliripoti kuwa Iran ilijibu kwa kushambulia vituo viwili vya kijeshi vya Marekani vilivyopo Jordan.

Wakati huo huo, Shirika la Habari la Mehr limeripoti kuwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limeangusha ndege isiyo na rubani ya Marekani aina ya MQ-9 katika eneo la Mlango wa Hormuz.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, drone hiyo iliangushwa kwa makombora ya ulinzi wa anga na kuanguka katika maji ya Ghuba.

TRUMP ADOKEZA KHARG ISLAND YASHAMBULIWA

Rais wa Marekani, Donald Trump, usiku wa Jumapili alitoa ujumbe mfupi kwenye mitandao ya kijamii akidai kuwa Kisiwa cha Kharg, ambacho ni kitovu muhimu cha nishati nchini Iran, kilikuwa kikishambuliwa.

Trump alidai kuwa eneo hilo lilikuwa “likilipuliwa,” huku ujumbe huo ukiambatana na video iliyotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili bandia (AI).

Hata hivyo, hadi wakati huo hakukuwa na uthibitisho mwingine huru uliothibitisha kuwa Kisiwa cha Kharg, kilichopo umbali wa mamia ya kilomita kutoka Larak, kilikuwa kikishambuliwa.

Ikulu ya Marekani pamoja na Wizara ya Ulinzi ya Marekani hazikutoa majibu ya haraka kuhusu madai hayo, huku Iran pia ikiwa haijatoa tamko rasmi kuhusu ujumbe wa Trump.

UAE YAANGUSHA DRONE ILIYOTOKA IRAN

Katika tukio jingine, Wizara ya Ulinzi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imesema vikosi vyake vya anga vilikabiliana na drone iliyokuwa ikiruka katika maji yake ya eneo na ambayo ilidaiwa kutoka Iran.

Wizara hiyo imesema vikosi vya UAE viko katika hali ya tahadhari kubwa na mifumo yake ya ulinzi wa anga inaendelea kufuatilia anga la nchi hiyo saa nzima.

Serikali ya UAE pia imewataka wananchi kupata taarifa kuhusu hali hiyo kupitia vyanzo rasmi pekee.

MAREKANI YAONGEZA SHINIKIZO LA KIUCHUMI KWA IRAN

Hatua hizo za kijeshi zimekuja baada ya wiki kadhaa ambazo utawala wa Trump ulikuwa umeongeza shinikizo la kiuchumi dhidi ya Iran na washirika wake wa kibiashara kupitia vikwazo vya kifedha.

Waziri wa Hazina wa Marekani, Scott Bessent, amesema Washington inaweza kutangaza vikwazo vipya vya aina ya secondary sanctions kila wiki, huku hatua za awali zikilenga taasisi za kifedha.

Bessent amesema Marekani iko tayari kutumia shinikizo kubwa la kifedha dhidi ya watu na taasisi zinazohusishwa na Iran iwapo Tehran haitabadilisha msimamo wake.

Kauli hiyo imetolewa wakati Bessent akijiandaa kushiriki mikutano ya Kundi la G20 mjini Asheville, North Carolina, ambapo anatarajiwa kukutana na mawaziri wenzake kutoka mataifa mbalimbali duniani.

CHINA YAWEKWA KWENYE MIZANI YA VIKWAZO

China nayo imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu kutokana na kuwa mshirika mkubwa wa kibiashara wa Iran na mnunuzi muhimu wa mafuta yake.

Bessent amesema atakutana na maafisa wa China katika mkutano wa G20 na kwamba “chaguzi zote ziko mezani” kuhusu uwezekano wa kuchukua hatua dhidi ya Beijing kutokana na kuendelea kununua mafuta kutoka Iran.

Hata hivyo, amekanusha madai kwamba utawala wa Trump unasita kuikabili China, akisema mataifa hayo mawili yana maslahi ya pamoja katika kuhakikisha Mlango wa Hormuz unafunguliwa tena na kuzuia Iran kutengeneza silaha ya nyuklia.

Hatua za Marekani zinaashiria kuongezeka kwa mchanganyiko wa shinikizo la kijeshi na kiuchumi dhidi ya Tehran, huku Mlango wa Hormuz ukiendelea kuwa kitovu cha mvutano kutokana na umuhimu wake katika biashara na usafirishaji wa nishati duniani.