Skip to content
-
Subscribe to our newsletter & never miss our best posts. Subscribe Now!
Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

  • Home
  • Privacy Policy
  • Sample Page
  • Home
  • Privacy Policy
  • Sample Page
Close

Search

  • https://www.facebook.com/
  • https://twitter.com/
  • https://t.me/
  • https://www.instagram.com/
  • https://youtube.com/
Subscribe
Habari

UEFA Yaandaa Kesi ya Jinai Dhidi ya Infantino, Mashabiki Wamlipua

By admin
August 28, 2026 1 Min Read
Comments Off on UEFA Yaandaa Kesi ya Jinai Dhidi ya Infantino, Mashabiki Wamlipua

Global Publishers
August 28, 2026
66 views
0 Comments

Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) linajiandaa kuanzisha mchakato wa kisheria nchini Uswisi dhidi ya Rais wa FIFA, Gianni Infantino, kwa tuhuma za usimamizi mbaya wa fedha, huku mashabiki wakimzomea na kumtukana wakati akiwakabidhi kombe washindi wa mashindano nchini Vietnam.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, nyaraka za kisheria zinaonyesha kuwa UEFA pamoja na wahusika wengine wanajiandaa kuwasilisha madai ya jinai dhidi ya Infantino na huenda viongozi au washauri wengine wa FIFA, wakihusisha suala hilo na tuhuma za “criminal mismanagement”.

Hatua hiyo inahusishwa na mpango uliokuwa ukihusisha FIFA kuuza hisa katika Kombe la Dunia, mpango ambao Infantino aliusitisha baada ya UEFA kutishia kususia mashindano hayo.

Wakati huo huo, Infantino alikumbana na hali ya aibu nchini Vietnam baada ya mashabiki waliokuwa kwenye Uwanja wa My Dinh National Stadium, Hanoi, kumtukana kwa lugha chafu alipokuwa akiwasilisha kombe baada ya Vietnam kuifunga Thailand na kutwaa ubingwa wa ASEAN.

Video kutoka uwanjani ilionyesha baadhi ya mashabiki wakimuita Infantino kwa matusi kwa lugha ya Kiingereza, huku rais huyo wa FIFA akitabasamu na kuwapungia mkono.

Infantino mwenye umri wa miaka 56 baadaye alielezea ziara hiyo kupitia Instagram, akisema matukio kama hayo yanaakisi kile ambacho FIFA inasimamia.

Infantino anatarajiwa kugombea tena nafasi ya urais wa FIFA katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Machi 2027.

Author

admin

Follow Me
Other Articles
Previous

OUT na Mzumbe Watangaza Nafasi 6 za Kazi, Mwisho wa Maombi Agosti 31

Next

WAZIRI MKUU: NDEJEMBI ANATOSHA KUMSAIDIA RAIS

Recent Posts

  • Rais Samia Atuma Rambirambi Kifo cha Mfalme wa Norway
  • KINGU: NDEJEMBI NI KIJANA MZALENDO, MCHAPAKAZI
  • Msukuma Asimulia Ndejembi Alivyopokea Taarifa za Uteuzi wa Makamu wa Rais – Video
  • Jamhuri Yakamilisha Kumuhoji Lissu Katika Kesi ya Uhaini Leo – Video
  • Mafuriko Yaua Watu 100 Nepal, Zaidi ya 1500 Hawajulikani Walipo

Recent Comments

  1. A WordPress Commenter on Hello world!

Archives

  • August 2026

Categories

  • Burudani
  • Habari
  • Magazeti
  • Michezo
  • Siasa
Copyright 2026 — Habarimpya. All rights reserved. Blogsy WordPress Theme