*TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA*

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba Wakala wa Vipimo (WMA) kuanzisha Klabu za Vipimo katika shule za Mkoa huo.

Ombi hilo wamelitoa jana Jumamosi, Agosti 29, 2026 walipotembelea banda la WMA katika Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayoendelea viwanja vya Furahisha, Jijini Mwanza.

Ili kuthibitisha kiu yao ya elimu ya vipimo, mwanafunzi mmoja kutoka Shule ya Msingi Ghana, Ibrahim Omary, alijitolea na kupewa fursa ya kutoa elimu ya vipimo kwa wanafunzi wenzake na wananchi waliotembelea banda hilo. Aliifanya kazi hiyo kwa ufasaha mkubwa na kupata pongezi.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Ibrahim alisema: 

“Tuliona kwenye vyombo vya habari wanafunzi wenzetu jijini Dodoma ambao wako katika Klabu za Vipimo wakitoa elimu ya vipimo, tukavutiwa sana. Nasi tunaomba WMA waanzishe klabu hizo kwa shule za Mwanza ili nasi tupate elimu hiyo kwa kina.”

Wanafunzi hao wameahidi kuwa mabalozi wa WMA katika jamii zao kwa kuelimisha wenzao, familia na majirani kuhusu umuhimu wa matumizi sahihi ya vipimo. Wengi wao wamesema ndoto yao ni kuwa Maafisa Vipimo.

Akijibu ombi hilo, Meneja Mawasiliano wa WMA, Bi. Veronica Simba amewaahidi wanafunzi hao kuwa Wakala utaanzisha Klabu za Vipimo katika shule za Mkoa wa Mwanza na hatua kwa hatua katika mikoa mingine yote nchini.

“Lengo letu ni kufikisha elimu ya vipimo kwa watoto tangu awali. Kupitia klabu hizi tunajenga kizazi cha wafanyabiashara na watumiaji wanaojali haki na usawa katika biashara,” amesema Bi. Simba.

Wanafunzi na wananchi wengine wameendelea kufurika katika banda la WMA katika siku ya pili ya maonesho hayo. Wamesema wameridhishwa na elimu wanayopata kuhusu umuhimu wa matumizi sahihi ya vipimo.

Maonesho hayo yameanza tarehe 28 Agosti 2026 na yanahitimishwa tarehe 6 Septemba 2026 yakiwa na  kaulimbiu “Usalama na Amani ni Kichocheo cha Biashara na  Uwekezaji hapa Nchini”.  

Katika  Maonesho hayo, WMA inatumia kaulimbiu isemayo “Vipimo Sahihi ni Msingi wa Usalama, Amani na  Uwekezaji wa Biashara ”.

Mawakili wa Mtoto wa Rwakatare Watoa Tahadhari Kuhusu Mali za Mirathi – Video

Global Publishers
August 30, 2026
24 views
0 Comments

Mawakili Nicholas Mugarura, Mwesigwa Muhingo na David Saire Manoti, wanaomwakilisha mmoja kati ya watoto wa marehemu Mchungaji Getrude Rwakatare wametoa taarifa kuhusu mgogoro wa mirathi ya marehemu.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mmoja wa mawakili hao, David Saire Manoti, amesema marehemu Mchungaji Rwakatare alikuwa kiongozi maarufu wa Kanisa la Assemblies of God, Mikocheni B, Mlima wa Moto, pamoja na kuwa Mbunge wa Kuteuliwa na Rais.

Amesema baada ya kifo cha mama Rwakatare aliyefariki dunia Aprili 20, 2020, Shauri la Mirathi Na. 32 la mwaka 2020 lilifunguliwa katika Mahakama Kuu ya Dar es Salaam na baadaye kuhamishiwa Mahakama Kuu, Kituo Jumuishi cha Haki Temeke.

Katika shauri hilo, watoto wa marehemu waliteuliwa kuwa wasimamizi wa mirathi.

Manoti amesema marehemu Mchungaji Rwakatare alikuwa akimiliki shule kadhaa ambazo, kupitia hati maalum ya ugawaji wa mali za mirathi (Accounts of Estate) ya Novemba 26, 2024, na baada ya kuidhinishwa na Mahakama Kuu, ziligawanywa kwa watoto wake.

Amesema kila mtoto aligawiwa shule tatu. Hata hivyo, kwa upande wa mtoto mmoja, Tibe Kenneth Rwakatare, utekelezaji wa ugawaji huo umekumbana na changamoto kubwa na kuonya kuwa watu wasinunue mali za marehemu mpaka ufumbuzi wa utata huo utakapopatikana.

Mourinho Amkingia Kifua Mbappe Kwenye Bio za Ballon d’Or

MADRID, Hispania: Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho, amesema mshambuliaji wa timu hiyo, Kylian Mbappe, ndiye anayestahili kushinda tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu, akisisitiza kuwa tuzo hiyo inapaswa kutolewa kwa mchezaji bora zaidi duniani badala ya kuzingatia mafanikio ya timu katika Kombe la Dunia au Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mourinho ametoa kauli hiyo Jumamosi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa Real Madrid dhidi ya Malaga katika Ligi Kuu ya Hispania.

“Wachezaji bora duniani wapo wawili, watatu au wanne, na tunawajua. Wapo hapa,” amesema Mourinho.

Kocha huyo amesema kwa mtazamo wake, Mbappe ndiye anayestahili zaidi tuzo hiyo kutokana na mafanikio yake binafsi msimu huu, akirejea rekodi ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa kuwa mfungaji bora wa muda wote katika historia ya Kombe la Dunia.

Mbappe ni miongoni mwa wagombea wa tuzo hiyo baada ya kumaliza msimu uliopita akiwa mfungaji bora wa La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na Kombe la Dunia 2026, licha ya kutwaa bila ubingwa mkubwa wa timu.

Wachezaji wengine wanaowania tuzo hiyo ni pamoja na mshambuliaji wa England, Harry Kane, kiungo wa Hispania na bingwa wa Kombe la Dunia, Rodri, pamoja na nyota wa Paris Saint-Germain, Ousmane Dembele na Khvicha Kvaratskhelia.

Mbappe aliendelea kuonyesha ubora wake baada ya kufunga mabao matatu katika ushindi wa Real Madrid wa 4-1 dhidi ya Real Sociedad Jumatano.

Akizungumzia vigezo vya Ballon d’Or, Mourinho amesema mafanikio ya timu pekee hayapaswi kuwa msingi wa kumpa mchezaji tuzo hiyo.

“Huwezi kumpa mchezaji Ballon d’Or kwa sababu tu ameshinda Ligi ya Mabingwa au Kombe la Dunia,” amesema.

Mourinho ametaja baadhi ya wachezaji waliowahi kushinda tuzo hiyo kama mifano ya wachezaji ambao walikuwa na kiwango cha kipekee binafsi, akiwemo Diego Maradona, Ronaldinho, Ronaldo Nazario, Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Zinedine Zidane.

Amesema endapo tuzo hiyo ingelenga zaidi mafanikio ya kushinda Ligi ya Mabingwa, basi ingepewa kocha wa Paris Saint-Germain, Luis Enrique, huku kwa upande wa timu ya taifa ya Hispania ikistahili kwenda kwa Luis de la Fuente.

Kwa mujibu wa Mourinho, Ballon d’Or inapaswa kumtambua mchezaji bora zaidi duniani kwa kiwango chake binafsi, na si tu mafanikio ya timu aliyochezea.

Rais wa Iran Akiri Vikwazo vya Marekani Vinaumiza Uchumi

TEHRAN, Iran: Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amekiri kuwa vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Marekani vinaendelea kuathiri uchumi wa nchi hiyo, siku chache baada ya kusema kuwa hatua hizo hazitakuwa na mafanikio.

Akizungumza na televisheni ya taifa ya Iran Ijumaa usiku, Pezeshkian amesema baadhi ya watu wamekuwa wakidai kuwa vikwazo hivyo havina madhara yoyote, lakini hali halisi ni tofauti.

“Wengine wanasema vikwazo havina athari kabisa; kwa watu hao, kwa kweli sijui niseme nini,” Pezeshkian amesema.

Amesema Iran kwa sasa iko katika hali ya vita na hivyo wananchi wanapaswa kukubaliana na mazingira magumu yanayoikabili nchi hiyo.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Waziri wa Hazina wa Marekani, Scott Bessent, kutangaza mipango ya kuongeza shinikizo la kiuchumi dhidi ya Iran, akionya nchi zitakazokataa kushiriki katika kampeni hiyo.

Hatua hizo mpya zinaendeleza vikwazo vilivyowekwa na Marekani na washirika wake tangu mwaka 2018, baada ya Rais Donald Trump wa wakati huo kuiondoa Marekani katika makubaliano ya kimataifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Pezeshkian amesema katika miezi ya hivi karibuni, kiwango cha bidhaa zinazoingia na kutoka nchini Iran zimepungua kwa asilimia 25 hadi 35, akidai hali hiyo inatokana pia na zuio la majini la Marekani katika bandari za Iran.

Kutokana na kupungua kwa biashara, Rais huyo amesema kuna haja ya kuongeza bei ya mafuta ya petroli nchini Iran ili kukabiliana na hali hiyo.

Ameeleza kuwa bei ya moja ya viwango vya matumizi ya mafuta inaweza kuongezwa kutoka tomani 5,000 hadi tomani 10,000.

Iran ni miongoni mwa nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi duniani na imekuwa ikitoa ruzuku kubwa kwa mafuta ya petroli, jambo linalofanya suala la kuongeza bei kuwa nyeti kisiasa.

Hata hivyo, siku hiyo hiyo Pezeshkian alisisitiza kuwa vikwazo vipya vya Marekani “havitatimiza chochote,” akisema Iran itaendelea kukabiliana na shinikizo la kiuchumi.

Kauli zake za hivi karibuni zinaashiria mabadiliko ya msimamo kuhusu ukubwa wa athari za vikwazo hivyo, huku serikali ya Iran ikikabiliwa na changamoto za biashara, uagizaji wa mafuta na hali ya uchumi wa ndani.

Chadema Yaweka Nguvu Kwenye Kesi ya Lissu, Baraza Kuu Laahirishwa

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amesema chama hicho hakitakuwa tayari kushiriki katika mazungumzo yoyote iwapo Mwenyekiti wake, Tundu Lissu, ataendelea kuwa gerezani.

Heche ameyasema hayo leo, Agosti 29, 2026, katika Kikao Maalumu cha Kamati Kuu ya CHADEMA kilichofanyika katika Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.

Amesema msimamo wa chama ni kwamba Lissu, ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi ya uhaini, ndiye anayebeba dira ya CHADEMA na hivyo anapaswa kuwa sehemu inayoongoza aina yoyote ya mazungumzo yatakayofanyika.

Heche amesema CHADEMA haiwezi kuingia katika mazungumzo chini ya vitisho au kushurutishwa, akisisitiza kuwa viongozi wa chama hicho hawako tayari kushiriki mazungumzo kwa kulazimishwa.

Aidha, amesema viongozi wa CHADEMA wanaoshikiliwa kwa makosa ambayo ameyataja kuwa ni “uongo” wanapaswa kuachiliwa, huku akitaka kupatikana kwa msuluhishi wa kitaifa au kimataifa anayeaminika ili kusaidia kuwakutanisha wahusika na kuwezesha mchakato wa mazungumzo.

Naibu Katibu Mkuu Bara wa CHADEMA, Amani Golugwa.

CHADEMA yaahirisha Baraza Kuu

Katika kikao hicho, Kamati Kuu ya CHADEMA imeazimia kuahirisha kikao cha Baraza Kuu la chama hicho kilichokuwa kifanyike Septemba 15, 2026.

Naibu Katibu Mkuu Bara wa CHADEMA, Amani Golugwa, amesema uamuzi huo umetolewa baada ya Kamati Kuu kujadili, miongoni mwa mambo mengine, maandalizi ya Baraza Kuu pamoja na mwenendo wa kesi inayomkabili Lissu.

Golugwa amesema tarehe mpya ya kufanyika kwa kikao hicho bado haijawekwa na itapangwa baadaye.

Kamati Kuu yaweka nguvu kwenye kesi ya Lissu

Kuhusu kesi hiyo, Kamati Kuu imewaelekeza viongozi wakuu wa chama kuelekeza nguvu katika kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika mchakato wa kesi hiyo.

Pia, CHADEMA imesema itaendelea kuongeza nguvu katika madai yake ya Katiba Mpya, sambamba na kuendelea kushinikiza kuachiwa kwa Mwenyekiti wake, ikisisitiza msimamo wa chama kuwa Lissu hana hatia.

CHADEMA yakusanya Sh milioni 302

Katika kikao hicho, Kamati Kuu pia imepokea taarifa kuhusu kampeni ya uchangishaji fedha ya “Tone kwa Tone” kuelekea Baraza Kuu la chama.

Kwa mujibu wa taarifa iliyowasilishwa kwenye kikao hicho, jumla ya Sh milioni 302 zimekusanywa kupitia zoezi hilo.

Kamati Kuu imewapongeza na kuwashukuru wanachama wote walioshiriki katika uchangishaji huo.

Fahamu Faida 7 Muhimu za Kula Machungwa Kila Siku


Machungwa ni miongoni mwa matunda yanayopatikana kwa urahisi na yanayopendwa na watu wengi, lakini nyuma ya ladha yake tamu kuna hazina kubwa ya virutubisho muhimu kwa afya ya binadamu. Kula machungwa mara kwa mara kunaweza kuwa hatua ndogo yenye matokeo makubwa katika kuboresha afya yako kwa ujumla.

Moja ya faida kuu ya machungwa ni uwezo wake wa kuimarisha kinga ya mwili. Tunda hili lina kiwango kikubwa cha vitamini C, kirutubisho kinachosaidia mwili kupambana na magonjwa mbalimbali, hasa yale ya maambukizi kama mafua. Kwa mtu anayekula machungwa mara kwa mara, mwili hupata uwezo mkubwa wa kujilinda dhidi ya maradhi.

Mbali na hilo, machungwa yana mchango mkubwa katika kuboresha afya ya ngozi. Vitamini C husaidia katika uzalishaji wa collagen, ambayo ni muhimu kwa ngozi kuwa imara, laini na yenye mwonekano mzuri. Hii ina maana kuwa kula machungwa kunaweza kusaidia kuchelewesha dalili za kuzeeka kama vile mikunjo.

Katika upande wa mmeng’enyo wa chakula, machungwa yana nyuzinyuzi (fiber) ambazo husaidia kuboresha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Hii husaidia kuzuia matatizo kama kufunga choo na kuhakikisha chakula kinameng’enywa vizuri mwilini.

Pia, machungwa yana mchango mkubwa katika kulinda afya ya moyo. Virutubisho vilivyomo ndani yake husaidia kupunguza kiwango cha mafuta mabaya (cholesterol) mwilini na hivyo kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo. Kwa watu wanaojali afya ya moyo wao, kuongeza machungwa katika lishe ni uamuzi mzuri.

Zaidi ya hayo, machungwa yana maji kwa wingi, jambo linalosaidia kuupa mwili unyevu wa kutosha na kuzuia upungufu wa maji mwilini. Hii ni muhimu hasa katika maeneo yenye joto kali ambapo mwili hupoteza maji kwa urahisi.

Kwa upande wa nishati, machungwa hutoa sukari ya asili ambayo huupa mwili nguvu kwa haraka bila madhara makubwa kama yale ya sukari zilizoongezwa viwandani. Hii hufanya machungwa kuwa chaguo bora la vitafunwa vya afya.

Vilevile, machungwa yanaweza kusaidia katika kudhibiti uzito wa mwili. Kwa kuwa yana kalori chache lakini yana nyuzinyuzi nyingi, husaidia mtu kushiba kwa muda mrefu na kupunguza ulaji wa kupita kiasi.

Kwa ujumla, machungwa si tunda la kawaida tu bali ni sehemu muhimu ya lishe bora. Kujenga tabia ya kula machungwa mara kwa mara kunaweza kuwa njia rahisi lakini yenye manufaa makubwa katika kuboresha afya yako ya kila siku.

Airtel Kuanzisha Fursa Lab Tanga, Kuwaongezea Vijana Ujuzi wa Kidijitali

Tanga. Airtel Tanzania imepanga kuanzisha kituo cha Airtel Fursa Lab katika Shule ya Sekondari Magaoni, mkoani Tanga, ikiwa ni hatua inayolenga kuwaongezea vijana fursa za kujifunza teknolojia, ubunifu na ujasiriamali.

Kituo hicho kitakuwa na mfumo wa darasa janja (Smart Class) na kinatarajiwa kuwapa wanafunzi na vijana mazingira ya kujifunza, kufanya majaribio na kuendeleza mawazo ya kibunifu yanayoweza kusaidia kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.

Akizungumza wakati wa Wiki ya Taifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu iliyofanyika Tanga, Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, amesema kituo hicho ni sehemu ya jitihada za kampuni hiyo kuwawezesha vijana kutumia teknolojia kwa tija.

“Kituo hiki kipya kitatoa mazingira ambayo vijana na wabunifu wataweza kujifunza, kufanya majaribio na kuendeleza mawazo yao,” amesema Mmbando.

Amesema kupitia Fursa Lab, vijana wataweza kupata mafunzo katika teknolojia, ujasiriamali na maeneo mbalimbali ya ujuzi wa kidijitali, huku wakipewa nafasi ya kugeuza mawazo yao kuwa miradi yenye suluhisho kwa jamii.

Fursa Lab kuwajengea vijana uwezo

Mpango wa Airtel Fursa Lab ulianzishwa mwaka 2020 kupitia ushirikiano kati ya Airtel Africa Foundation na Dar es Salaam Technology and Business Incubator (DTBi).

Tangu kuanzishwa kwake, zaidi ya watu 5,800, wakiwemo wanafunzi, walimu, vijana, wajasiriamali na wanawake, wamenufaika na mafunzo kupitia mpango huo.

Lengo la Fursa Lab ni kusaidia kuziba pengo kati ya upatikanaji wa teknolojia na uwezo wa kuitumia kwa ajili ya elimu, biashara na ubunifu.

Wanafunzi watumia teknolojia kutatua changamoto

Uzoefu kutoka Airtel Fursa Lab iliyopo Shule ya Sekondari Kijitonyama, Dar es Salaam, unaonyesha namna wanafunzi wanavyoweza kutumia teknolojia kubuni suluhisho kwa changamoto zinazowazunguka.

Miongoni mwa miradi iliyobuniwa ni programu inayomsaidia msichana kufuatilia mzunguko wa hedhi na kupata taarifa muhimu kuhusu afya yake.

Mwanafunzi Angel Swai naye amewahi kubuni wazo linalotumia akili mnemba katika udhibiti wa taa za barabarani, baada ya kutumia vifaa na rasilimali zilizopo katika kituo hicho kujaribu na kuendeleza wazo lake.

Miradi hiyo inaonyesha msisitizo wa Fursa Lab katika kuwasaidia vijana kwenda zaidi ya kujifunza nadharia na kuwapa nafasi ya kutumia teknolojia katika kutengeneza suluhisho halisi.

Ubunifu kuunganishwa na biashara

Kituo kinachotarajiwa kuanzishwa Magaoni pia kitasaidia kuwaunganisha vijana na fursa za biashara kupitia programu zinazolenga kukuza ujasiriamali na ubunifu.

Programu hizo zinaendeshwa kwa ushirikiano wa Airtel Tanzania, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia DTBi, pamoja na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

Kupitia mafunzo hayo, wabunifu watapata uelewa kuhusu haki miliki na namna ya kulinda mawazo yao, huku mafunzo ya ujasiriamali yakilenga kuwajengea uwezo wa kutumia teknolojia kuanzisha na kukuza biashara.

Mmbando amesema Airtel inalenga kuwawezesha vijana na wajasiriamali kutumia vituo hivyo kujenga ujuzi na kubadilisha mawazo yao kuwa bidhaa na huduma zenye thamani kiuchumi.

Mbali na kituo cha Magaoni, Airtel pia inapanga kuanzisha kituo kingine cha Fursa Lab katika eneo la Usagara, Tanga, hatua inayotarajiwa kuongeza zaidi fursa za kujifunza kidijitali na ubunifu kwa vijana wa mkoani humo.

Hatua hiyo inaendelea kuonyesha umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta binafsi, taasisi za Serikali na wadau wa teknolojia katika kuwaandaa vijana kwa fursa zinazotokana na uchumi wa kidijitali.

Baraza la Wazazi CCM Launga Mkono Nchimbi Kuvuliwa Uanachama – Video

Global Publishers
August 30, 2026
24 views
0 Comments

Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Wazazi la CCM Taifa, Ally Salum Hapi

Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Wazazi la CCM Taifa, Ally Salum Hapi, amesoma azimio la Jumuiya hiyo la kuunga mkono uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wa kumvua uanachama aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi.

Azimio hilo limesomwa Agosti 29, 2026, katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Wazazi yaliyofanyika jijini Mwanza.

Akisoma azimio hilo, Hapi amesema uamuzi huo umezingatia tamko na maamuzi yaliyofanywa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, pamoja na jukumu la Jumuiya ya Wazazi la kusimamia maadili katika jamii.

Amesema Jumuiya hiyo imeona umuhimu wa kuunga mkono uamuzi huo kutokana na wajibu wake wa kuhimiza na kusimamia maadili ndani ya jamii na chama.

Hapi amesema azimio hilo limepitishwa kwa kauli moja na wajumbe wote, baada ya Jumuiya ya Wazazi kufanya kikao chake Agosti 28, 2026.

Hatua hiyo imekuja katika kipindi ambacho uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuhusu uanachama wa Dkt. Nchimbi umeendelea kuzua mjadala ndani na nje ya chama.

SILLO: MICHEZO ITAJENGA AFYA, KUIMARISHA MAANDALIZI YA AFCON

 . 

Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma

NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daniel Sillo, amesema Bunge lipo tayari kushirikiana na Serikali katika kufanikisha mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), akisisitiza umuhimu wa michezo katika kujenga afya, umoja, udugu na nidhamu.

Sillo ameyasema hayo wakati wa Bonanza la Bunge lililowakutanisha wabunge, wizara na taasisi mbalimbali jijini Dodoma, ambapo aliwataka washiriki kutumia michezo kama sehemu ya kujenga afya bora na kuimarisha mahusiano baina yao.

Amesema michezo ina nafasi kubwa katika kupunguza msongo wa mawazo, jambo alilolieleza kuwa ni muhimu kwa wabunge kutokana na majukumu yao ya kutunga sheria, kuisimamia Serikali na kufanya maamuzi yanayogusa maisha ya wananchi.

“Nimefurahishwa kuona idadi kubwa ya washiriki katika michezo ya leo. Michezo hupunguza msongo wa mawazo na mwili wenye afya ni suluhisho muhimu katika kufanya maamuzi mazuri,” amesema Sillo.

Sillo amewapongeza washindi pamoja na washiriki wote wa bonanza hilo, huku akiishukuru Benki ya NMB kwa kuwezesha kufanyika kwa shughuli hiyo na kuchangia katika kuimarisha afya na ustawi wa wabunge.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Wateja Binafsi wa NMB, Filbert Mponzi, amesema benki hiyo imeendelea kuboresha huduma zake za kifedha, ikiwemo kuwezesha wananchi kupata mikopo kwa njia ya kidijitali.

 Mponzi pia ametajwa katika taarifa za hivi karibuni za NMB kuhusu huduma za kifedha kwa wafanyabiashara.

Amesema kupitia huduma ya NMB Mkononi, mteja anaweza kupata mkopo wa MshikoFasta kwa kutumia simu yake bila kulazimika kufika benki au kupitia taratibu ndefu za maombi, huku tathmini ya uwezo wa kukopa ikifanyika kwa kuzingatia historia ya miamala ya mteja.

Mponzi amesema mteja wa kawaida anaweza kukopa hadi Sh milioni mbili bila kujaza fomu wala kuweka dhamana, akieleza kuwa huduma hiyo inalenga kupunguza changamoto ya wananchi kukosa mikopo kutokana na masharti magumu ya dhamana.

“Mkopo huu ni suluhisho kwa wananchi wetu, wakiwemo wabunge, mamalishe, bodaboda na wafanyabiashara wengine. Hakuna dhamana inayohitajika, tunaangalia miamala yako,” amesema.

Aidha, Mponzi amesema NMB imeboresha huduma zake kwa wajasiriamali, ambao wanaweza kupata mikopo ya hadi Sh milioni tano bila dhamana, huku tathmini ikizingatia taarifa za miamala ya biashara zao.

Amesema NMB pia imehamia kwenye mfumo mpya wa kibenki baada ya kutumia mfumo wa awali kwa takribani miaka 15, hatua ambayo amesema itaiwezesha benki hiyo kutoa huduma za kisasa na zenye ufanisi zaidi, hususan katika eneo la huduma za kidijitali.

“NMB tumeingia kwenye mfumo mpya. Tunatarajia kuona mambo mazuri zaidi katika huduma zote kutokana na kuingia kwenye mfumo huu mkubwa,” amesema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Machano Ali Machano, aliipongeza NMB kwa mchango wake kwa Bunge, akisema wabunge wanatambua na kuthamini ushirikiano unaotolewa na benki hiyo katika shughuli mbalimbali, ikiwemo michezo.

Machano amesema mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki yanatarajiwa kufanyika jijini Arusha mwezi Desemba mwaka huu, yakishirikisha wabunge kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amesema Tanzania, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo NMB, inapaswa kutumia mashindano hayo kama fursa ya kuimarisha ushirikiano na nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, huku akisisitiza umuhimu wa maandalizi mazuri.

Wapewa elimu mafuta, gesi asilia Tamasha la Utamaduni – HabariLeo

MOROGORO; Wananchi mbalimbali wamejitokeza kwenye banda la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) na kupewa elimu juu ya usimamizi wa shughuli za utafutaji na uendelezaji wa mafuta na gesi asiia.

PURA ni sehemu ya taasisi mbalimbali zilizoshiriki kwenye Tamasha la Nne la Taifa la Utamaduni, Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro na lilikuwa kivutio kikubwa kwa wananchi.

Akizungumza kwenye banda hilo, Mjiolojia kutoka PURA, Lukelo Matimbwi amewaeleza masuala mbalimbali ikiwemo tafiti zinazofanyika kuhusu masuala ya gesi asilia na pia viasharia vya uwepo wa nishati hiyo kwa baadhi ya maeneo.