RESTLESS YASAIDIA WANAFUNZI WA MAZINGIRA MAGUMU KIGOMA

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 Zaidi ya wanafunzi 8000 ambao ni watoto na vijana Balehe wanaoishi mazingira hatarishi kutoka mikoa ya Kigoma, Songwe na Tabora wamenufaika na elimu kupitia vifaa vinavyotolewa kwa lengo la kukabiliana na changamoto za utoro zinazowakabili wanafunzi hao.

Mradi huu wa Elimu unaotekelezwa na Shirika la Restless Development kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF), kwa ufadhiliwa na Global Affairs Canada  ambapo kwa mkoa wa Kigoma Mradi umefanikiwa kutoa  seti za 295 za taulo za kike zinazotumika na kutupa, seti 1447 taulo za kike za kufua na kutumika tena, chupi za kike dazeni 250 na sabuni za kufulia dazeni 250 ambazo zinalenga kuwasaidia wanafunzi wa kike kujisitiri hata kipindi cha hedhi pasipo kukosa masomo yao.

Mratibu wa Mradi wa Elimu  kutoka Shirika lanRestless Development,  John Maftah akizungumza wakati wa ugawaji wa misaada hiyo alisema kuwa Jumla ya wanafunzi 3367 wakiwemo wanafunzi 77 wenye ulemavu kutoka shule 42 za Msingi na sekondari wamenufaika katika mkoa wa Kigoma kutoka halmashauri nne ambazo ni Kigoma Vijijini, Buhigwe, Kakonko na Uvinza.

Maftaha alisema kuwa pia wamefanikiwa kutoa magunia 271 ya mahindi na magunia 100 ya maharage kuwezesha wanafunzi kupata chakula shuleni kutokana   na ukosefu wa chakula kuwa miongoni mwa sababu kuu ya utoro na wanafunzi kuacha masomo wakitoa pia counter book boksi 111, rim za karatasi boksi 128, kalamu za wino boksi 53 na magodoro 75

Akizungumzia wakati wa kukabidhi vifaa na mahitaji hayo katika shule za sekondari ya Nyamuhoza iliopo Halmashauri ya wilaya Kigoma Meneja miradi wa Shirika hilo,  Ridhione Juma alisema kuwa Shirika la Restless Development linatekeleza mradi huo kukabiliana na baadhi ya vichochezi vinavyosababisha wanafunzi kuwa watoro au kuacha masomo akibainisha kuwa msaada uliotolwa ni mdogo ukilinganiisha na mahitaji hivyo bado jitihada zinahitajika kutoka kwa wadau mbalimbali.

Ridhiaone alisema kuwa Sambamba na hilo  shirika lemtoa  elimu ya uongozi na stadi za maisha, kufundisha elimu ya hedhi salama kwa wanafunzi wa kike na kiume ili kujua mabadiliko ya miili yao lakini pia kujua njia za kujiweka safi wakati wa hedhi na kuondoa unyanyapaa shuleni ili kutengeneza mazingira saidizi kwa wanafunzi wa kike hasa wanapokuwa kipindi cha hedhi.

Baadhi ya wanafunzi waliopokea vifaa hivyo akiwemo Mwanafunzi Josephina Pomeni kutoka shule ya Sekondari Kidahwe halmashauri ya wilaya Kigoma  aliishukuru Shirika la Restless Development kwa vifaa hivyo na utekelezaji wa mradi huo ambao unawezesha wanafunzi kukabiliana na changamoto za utoro au kuacha masomo.

Aidha akipokea vifaa hivyo Afisa Maendeleo ya Jamii wa halmashauri ya Wilaya ya kigoma, Joyce Bakunda amesema kuwa upatikanaji wa chakula na mahitaji haya ya shule   utawasaidia wanafunzi kujisomea kwa utulivu na kuwa na uhakiwa wa kula shuleni

Mwisho.

CHUO KIKUU CHA HARVEST MISSION CHAMTUNUKU PhD MCHUNGAJI MSTAAFU SAMWEL MWAHALENDE

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA,IRINGA

MCHUNGAJI Mstaafu wa kanisa la Pentecostal Holiness Mission  ( PHM), Samwel Mwahalende, ametunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Harvest Mission cha Texas, Marekani, ikiwa ni kutambua mchango wake wa muda mrefu katika kulitumikia Kanisa na jamii.

Akizungumza muda mfupi baada ya kutunukiwa shahada hiyo, Mwahalende alimshukuru Mungu kwa kumwezesha kufikia hatua hiyo, akisema safari yake ya huduma imekuwa na changamoto mbalimbali, lakini hakuwahi kukata tamaa katika kulitumikia Kanisa, Taifa na jamii inayomzunguka.

“Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kufikia siku hii. Nimefanya kazi katika mazingira mbalimbali, wakati mwingine bila malipo ya kutosha, lakini sikuwahi kukata tamaa kulitumikia Taifa langu na Kanisa,” alisema.

Mwahalende alisema kutunukiwa shahada hiyo kumefungua ukurasa mpya katika maisha yake, huku akieleza kuwa ni heshima kubwa kwake sasa kutambulika kama Dkt. Samwel Mwahalende baada ya miaka mingi ya kutambulika kama Mchungaji Mstaafu Samwel Mwahalende.

“Leo, kama mnavyoona, jina langu limebadilika na kuwa Dkt. Samwel Mwahalende. Hii ni mara yangu ya kwanza kutamka hivyo, kwa sababu awali nilikuwa nikijitambulisha kama Mchungaji Mstaafu Samwel Mwahalende,” alisema.

Alisema huduma yake ya Kikristo imemfikisha katika nchi mbalimbali nje ya Tanzania, zikiwemo Zambia, Malawi na Kenya, ambako amepata fursa ya kuhubiri na kuzitumikia jamii mbalimbali.

Mwahalende pia aliishukuru familia yake, hususan mke wake, ambaye alimwelezea kuwa moja ya nguzo muhimu katika safari yake ya maisha na huduma.

“Mke wangu amekuwa shujaa kwangu. Katika safari yangu yote ya maisha na kazi ya Mungu, amekuwa miongoni mwa watu ambao daima wamesimama nami,” alisema.

Pia aliwashukuru wanafamilia, watoto, marafiki na wageni wengine waliosafiri kutoka maeneo mbalimbali kushuhudia tukio hilo, akisema uwepo wao uliifanya siku hiyo kuwa ya kipekee katika maisha yake.

Akizungumzia maisha yake katika Mkoa wa Iringa, Mwahalende alisema ameshuhudia mabadiliko makubwa tangu alipofika mkoani humo mwaka 1972 na amekuwa akijitahidi kutoa mchango wake katika maendeleo ya jamii.

Mbali na huduma ya dini, alisema amewahi kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii na maendeleo, ikiwemo kushika nafasi za uongozi wa jamii ambako alifanya kazi kwa karibu na wananchi katika kutatua changamoto mbalimbali.

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Harvest Mission International Tanzania, Balozi Prof. Isaack Yona Mpema, amewataka waliotunukiwa shahada za uzamivu pamoja na Watanzania kwa ujumla kuwa mabalozi wa amani na kulinda utulivu uliopo nchini.

Prof. Mpema alisema amani ni tunu muhimu ya Taifa ambayo haipaswi kuchukuliwa kwa kawaida, akionya kuwa migogoro inayoshuhudiwa katika baadhi ya nchi za Afrika na maeneo mengine duniani mara nyingi huanza na mambo yanayoonekana kuwa madogo, ambayo yakipuuzwa hugeuka kuwa migogoro mikubwa.

Alitaja hali katika baadhi ya nchi, zikiwemo Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kuwa funzo muhimu kwa Tanzania kuhusu umuhimu wa kulinda amani na kushughulikia changamoto zinapojitokeza kabla hazijawa kubwa.

“Jamii inapaswa kutambua kuwa amani ikipotea si rahisi kuirejesha. Kila mwananchi ana wajibu wa kulinda amani kwa vitendo na si kwa maneno pekee,” alisema Prof. Mpema.

Alisema moja ya misingi ya amani ya kudumu ni kuhakikisha haki inatendeka kuanzia ngazi ya familia, mtaa, kata na tarafa hadi Taifa.

Prof. Mpema aliwataka Watanzania kuzingatia haki, kuheshimiana na kushirikiana, huku wakiiunga mkono Serikali katika juhudi zake za kulinda amani, umoja na mshikamano wa Taifa.

Alisisitiza kuwa mtu anayependa amani hawezi kwa makusudi kumuumiza, kumsumbua au kumkandamiza mtu mwingine, akisema upendo na amani vinapaswa kuonekana katika maisha ya kila siku ya wananchi.

Kwa mujibu wake, vitendo vya ukandamizaji, unyanyasaji na kutotenda haki vinaweza kuzaa chuki na hatimaye kusababisha migogoro ndani ya jamii.

Prof. Mpema pia aliwataka waajiri na viongozi kulinda haki na maslahi ya wafanyakazi, hususan vijana ambao wakati mwingine wanaweza kufanyiwa vitendo visivyo vya haki kutokana na hofu ya kupoteza ajira zao.

Alisema waajiri wana wajibu wa kuwatendea haki wafanyakazi wao na kuhakikisha haki na maslahi yao yanalindwa kwa mujibu wa sheria na misingi ya utu.

Aidha, alionya kuwa vitendo vinavyoweza kuonekana kuwa vidogo vinaweza kuwa na madhara makubwa iwapo vitapuuzwa, hivyo akawataka viongozi na wananchi kutumia nafasi zao kujenga upendo, haki na mshikamano katika jamii.

“Taifa ambalo watu wake wanapendana na kuheshimiana linakuwa na mazingira salama kwa maendeleo endelevu,” alisema.

Kwa upande wake, Dkt. Matilda Manase Seme, ambaye pia alikuwa miongoni mwa waliotunukiwa shahada hiyo, alisema ameipokea kwa unyenyekevu mkubwa na kumshukuru Mwenyezi Mungu pamoja na Chuo Kikuu cha Harvest Mission kwa kutambua mchango wake katika jamii.

“Shahada hii kwangu si heshima ya kawaida tu, bali ni wito na jukumu la ziada la kulitumikia Kanisa, Taifa na jamii kwa moyo wa kujitolea,” alisema Dkt. Seme.

Alisema kutambuliwa huko kumeongeza dhamira yake ya kutumia elimu, maarifa na uzoefu wake katika kuwahudumia watu wengine.

Kwa mujibu wa Dkt. Seme, kutunukiwa shahada hiyo ni sawa na kukabidhiwa jukumu jingine la kutekeleza, ambalo ameahidi kulifanya kwa uaminifu na unyenyekevu.

Alikipongeza Chuo Kikuu cha Harvest Mission kwa kutambua watu kutoka katika nyanja mbalimbali za maisha na kuthamini michango yao katika jamii.

Dkt. Seme alisema kutunukiwa heshima hiyo baada ya kuhudumu katika maeneo mbalimbali, ikiwemo utumishi wa umma, ni hatua kubwa katika maisha yake na itakuwa chachu ya kuendelea kulitumikia Taifa na jamii kwa uadilifu, upendo na kujitolea.

TAZAMA VIDEO YA TUKIO HILI BOFYA LINK HII

Maono ya Rais Samia Yajenga Kizazi cha Sayansi na Teknolojia, GEL Yaeleza..

WhatsApp%20Image%202026-08-29%20at%2010.34.50%20PM

KUNDI lingine la mamia ya wanafunzi wa Kitanzania wameondoka nchini Jumamosi kuelekea vyuo vikuu mbalimbali kuanza masomo ya elimu ya juu.

Wanafunzi hao walioondoka kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Terminal 3, jijini Dar es Salaam, wengi wao wamechagua programu zinazohusiana na sayansi, teknolojia na taaluma zinazohitajika katika dunia ya sasa, zikiwemo Computer Engineering, Cyber Security, Artificial Intelligence, Civil Engineering, programu mbalimbali za afya, sheria na biashara.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Meneja wa Tawi la Dar es Salaam, Micky Musa, amesema kuondoka kwa wanafunzi hao ni sehemu ya mpango mpana wa kuwaunganisha vijana wa Tanzania na fursa za elimu ya kimataifa.

WhatsApp%20Image%202026-08-29%20at%2010.34.49%20PM

Alisema mbali na India, Global Education Link inaendelea kuwaandaa wanafunzi wengine wanaotarajiwa kuelekea nchini China, huku wengine wakiwa katika hatua mbalimbali za maandalizi ya kwenda kusoma Malaysia, Marekani na Uingereza.

“Kadiri muda unavyokwenda Watanzania wataendelea kuona makundi mengine ya wanafunzi yakiondoka. Tunawaomba vijana wenye ndoto ya kusoma nje ya nchi wafike katika ofisi zetu zilizopo Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Mwanza na Arusha. Muda bado upo. Njoo na matokeo yako, nasi Global Education Link tupo tayari kukusaidia kuifanya ndoto yako kuwa uhalisia,” amesema.

WhatsApp%20Image%202026-08-29%20at%2010.34.51%20PM

Musa pia amewataka wazazi na walezi wenye vijana wanaotamani kupata elimu nje ya nchi kutumia ofisi za Global Education Link kupata ushauri kuhusu uchaguzi wa vyuo, programu za masomo, udahili, visa na maandalizi ya safari.

Miongoni mwa wanafunzi walioondoka ni vijana wanaokwenda kusomea Computer Science Engineering, Artificial Intelligence na Cyber Security, wakisema wamechagua taaluma hizo kutokana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia na umuhimu wake katika maendeleo ya uchumi wa kisasa.

Cardi B Avamia Jalada la Vogue Arabia, Aonyesha Mvuto wa Kiarabu

Msanii wa kimataifa kutoka Marekani, Cardi B, amepewa nafasi ya kipekee kwenye jalada la toleo la Septemba 2026 la Vogue Arabia, katika picha iliyozua gumzo kutokana na mtindo wake wa kipekee wenye mguso wa utamaduni wa Kiarabu.

Jalada hilo, lililotolewa Agosti 27, 2026, linamuonyesha Cardi B akiwa amevalia vazi la kifahari lenye mchanganyiko wa rangi nyeusi na kijani, huku akiwa ameshikilia tufaha.

Kinachovutia zaidi ni ujumbe ulioandikwa kwenye jalada hilo, “Assalamu Alaikum, Cardi B”, ambao umeongeza mvuto wa picha hiyo na kuonyesha namna msanii huyo anavyoendelea kuhusishwa na utamaduni wa eneo la Arabia.

Katika toleo hilo, Vogue Arabia imemzungumzia Cardi B kwa upana, ikigusa safari yake ya muziki, mitindo, umaarufu pamoja na maisha yake nje ya jukwaa akiwa mama.

Jarida hilo limemuelezea kama msanii mwenye uwezo mkubwa wa kubadilika kimtindo bila kupoteza utambulisho wake.

Cardi B naye ameonyesha furaha yake kupitia mitandao ya kijamii, ambapo amewashukuru Vogue Arabia pamoja na mpiga picha na mkurugenzi wa ubunifu Szilveszter Makó kwa kazi hiyo.

Mwonekano wake umeendelea kuzungumziwa na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii, wengi wakimpongeza kwa kuonekana tofauti na vile walivyozoea kumuona kwenye matukio mbalimbali.

Cardi B si mgeni katika eneo la Mashariki ya Kati. Amewahi kutembelea Saudi Arabia na kutumbuiza katika tamasha la MDLBEAST Soundstorm jijini Riyadh.

Safari hiyo pia ilimpa nafasi ya kueleza hisia zake kuhusu watu na utamaduni wa Saudi Arabia, huku akionyesha kuvutiwa na baadhi ya vipengele vya utamaduni huo.

Kwa jalada hili la Vogue Arabia, Cardi B anaendelea kuonyesha kuwa ushawishi wake hauishii kwenye muziki pekee, bali pia unaendelea kukua katika mitindo, utamaduni na burudani ya kimataifa.

Stori na Nasra Kassim | GPL – TUDACO

*MAKAMU WA RAIS AWASALIMU WANANCHI WA CHAMWINO*

AAHIDI KUFANYA KAZI KWA UADILIFU, UTII NA UZALENDO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumpa dhamana ya kuwa msaidizi namba moja na kuahidi utii, uadilifu, uzalendo na uchapaji kazi.

 

Makamu wa Rais amesema hayo, wakati akiwasalimu wananchi wa Jimbo la Chamwino, waliojitokeza kumpokea kwa wingi nje ya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, mara baada ya kuapishwa kuwa Makamu wa Rais. Amesema ataendelea kufanya kazi ya kumsaidia Mhe.  Rais kwa uadilifu na kuwatumikia watanzania wote ili kuharakisha maendeleo.

 

Aidha Makamu wa Rais amesema ataendelea kuwawakilisha vyema vijana hapa nchini na kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha Tanzania inazidi kusonga mbele katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

 

Akitoa salamu zake kwa wananchi hao, Makamu wa Rais amewahakikishia kuendelea kutekeleza majukumu yake mapya kwa uadilifu, bidii na kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.

 

“Wana sitawazingua, na Mama sitamzingua,” amesema Ndejembi, katika ujumbe uliosisitiza dhamira yake ya kutekeleza wajibu aliopewa na kuendelea kuwa mwaminifu na mwakilishi mwema wa vijana.

 

Makamu wa Rais amewasalimu wananchi wa Jimbo la Chamwino ikiwa ni

jimbo alilolitumikia kabla ya kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais.