Jina la Makamu wa Rais Mteule lilivyowasilishwa bungeni – HabariLeo

DODOMA; Picha za matukio mbalimbali, wakati Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, akipokea rasmi leo Agosti 28, 2026 jina la Makamu wa Rais Mteule, Deogratius John Ndejembi, lililopendekezwa na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM).


Jina hilo limewasilishwa kwa Spika na Katibu wa Rais, Balozi Ali Jabir Mwadini akiwa ameambatana na Mpambe wa Rais (ADC) Brigedia Jenerali, Nyamburi Mashauri kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge.

Mapokezi ya jina hilo yameshuhudiwa na Naibu Spika, Daniel Sillo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, pamoja na Katibu wa Bunge , Baraka Leonard.Wengine ni Wenyeviti wa Bunge, Deogratius Mwanyika, Najma Giga na Cecilia Pareso

MIMI SIO MAKAMU WA RAIS WA CCM,NI WA VYAMA VYOTE – NDEJEMBI

NA MATUKIO DAIMA MEDIA

DODOMA. Makamu wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amesema baada ya kuthibitishwa na Bunge kwa kura zote 304 sawa na asilimia 100, atakuwa Makamu wa Rais wa Watanzania wote bila kujali vyama vyao vya siasa.

Ndejembi amesema hayo leo Agosti 28, 2026, muda mfupi baada ya kuthibitishwa na Wabunge kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema atatekeleza majukumu yake kwa unyenyekevu na kuhakikisha anakuwa kiungo kati ya Serikali na Watanzania wote, huku akisisitiza kuwa atafanya kazi kwa kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Ninakuwa ni Makamu wa Rais wa Watanzania wote, nakuwa Makamu wa Rais si wa wana CCM peke yake, nakuwa Makamu wa Rais wa Watanzania wa vyama vyote.”

Amesema atatumia nafasi hiyo kwa unyenyekevu mkubwa katika kumsaidia Rais na kuwa kiungo cha Watanzania wote.

“Nitajitahidi kwa unyenyekevu mkubwa sana kumsaidia Mheshimiwa Rais, kuwa kiungo wa Watanzania wote kama vile mapenzi yake yatakavyotaka, kwa sababu nafanya kazi chini yake.”amesema

WARAGHABISHI WACHOCHEA MAENDELEO KIGOMA – Matukio Daima Habari

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Mkakati wa uraghabishi unaotekelezwa na wananchi wa mitaa 10 ya manispaa ya Kigoma Ujiji kwa uratibu wa Shirika lisilo la kiserikali la TWAWEZA unaelezwa kuchochea wananchi kwenye mitaa hiyo kushiriki kwenye mikutano ya maendeleo sambamba na kushiriki kwenye utekelezaji wa miradi inayoibuliwa kwenye mtaa yao.

Mthamini Binafsi aliyepewa kazi na TWAWEZA kutathmini utekelezaji wa mradi huo uliotekelezwa kwa miaka minane katika manispaa ya Kigoma Ujiji, Kapongola Nganyanyuka alisema hayo akiwasilisha taarifa yake ya tathmini wakati wa kufunga mradi huo ambao umefikia mwisho. 

Nganyanyuka alisema kuwa katika  utekelezaji wa mtadi huo wananchi wamekuwa na hamasa ya kuhudhuria mikutano ya mitaa yao, kuibua mawazo mbalimbali yakiwemo ya miradi ya maendeleo, kupanga na kushiriki katika utekelezaji wa miradi hiyo huku wakiwa na uwezo wa kuomba taarifa ya hali ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Baadhi ya wananchi (waraghabishi) walioshiriki katika mpango wa kutoa elimu kwa jamii kiwemo Mwenyekiti wa Waraghabishi (WAMCU) mkoa Kigoma,  John Edward alisema kuwa baada ya kuona mradi unafikia mwisho waliamua kuunda umoja huo ili kuendeleza kazi hiyo kwa kuendelea kutafuta fedha kutoka vyanzo vingine.

Edward alisema kuwa kwa kipindi cha uratibu wa TWAWEZA walichofanya kazi kumekuwa na mabadiliko makubwa na mwamko kwa jamii kujitokeza kwenye mikutano na shughuli za maendeleo.

Naye Shekhe Omari Hussein kutoka kata ya Buzebazeba alisema kuwa mradi huo umeleta mabadiliko makubwa kwenye fikra za wananchi kuhusu dhana ya kuibua,kupanga  na kutekeleza miradi na kuwa  chachu ya kuwafanya wananchi kuwa na umiliki kamili wa miradi kwa kuifanya miradi hiyo kama sehemu ya maisha yao.

Akieleza kuhusu utekelezaji wa mradi huo ambao umefikia mwisho Mratibu wa mkoa Kigoma wa mradi huo, Esther Prosper alisema kuwa mradi ulilenga kuwajengea uwezo waraghabishi kuifikia jamii kubwa wanaoishi nayo kuwa na uwezo wa kushiriki mikutano, kuchangia mada na kuwa washiriki wa maamuzi wa mikutano hiyo ikiwemo kuibua, kupanga na kushiriki shughuli za maendeleo na kwamba miaka minane ya mradi huo wameridhika na mafanikio yaliyofikiwa.

Mwisho.

Mkuu wa CIA Afanya Ziara ya Siri Moscow, Putin Apewa Onyo Kali

Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), John Ratcliffe, ameripotiwa kufanya ziara ya siri mjini Moscow kwa kutumia ndege ya kijeshi ya Marekani, huku akikutana na viongozi wakuu wa ujasusi wa Urusi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na The Wall Street Journal na The New York Times, Ratcliffe alipeleka ujumbe mzito kwa Moscow kuhusu vita vya Ukraine na mahusiano ya Urusi na NATO.

Inadaiwa kuwa katika mazungumzo hayo, Ratcliffe aliionya Urusi kutoshambulia nchi wanachama wa NATO, huku taarifa nyingine zikisema aliiambia Moscow kutathmini upya msimamo wake katika vita vya Ukraine na kutafuta makubaliano kabla hali yake ya kijeshi na kiuchumi haijawa mbaya zaidi.

Ratcliffe aliripotiwa kukutana na Aleksandr Bortnikov, mkuu wa shirika la usalama la ndani la Urusi, FSB. Rais wa Urusi, Vladimir Putin, hakukutana moja kwa moja na Ratcliffe, lakini alielezwa kuhusu mazungumzo hayo.

Ziara hiyo ilifanyika baada ya ndege ya kijeshi ya Marekani aina ya C-17 Globemaster III kutua katika Uwanja wa Ndege wa Vnukovo, Moscow, ikitokea Riga nchini Latvia.

Baada ya ndege hiyo kutua, msafara wa magari yenye namba za kidiplomasia za Marekani ulionekana ukielekea katikati ya Moscow, jambo lililoibua taharuki na maswali kuhusu sababu ya ziara hiyo ya ghafla.

Rais Donald Trump baadaye aliielezea safari hiyo kama ziara ya “semi-routine”, lakini akaashiria kuwa huenda kukawa na matokeo muhimu kutokana na mazungumzo hayo.

Ziara ya Ratcliffe inakuja wakati jitihada za kidiplomasia za kumaliza vita vya Ukraine zikiwa bado zinaendelea, huku Marekani ikijaribu kuishawishi Moscow na Kyiv kuelekea makubaliano ya kusitisha mapigano.

Safari hiyo pia inakumbusha ziara ya aliyekuwa Mkurugenzi wa CIA, William Burns, mjini Moscow mwaka 2021, ambapo aliripotiwa kumuonya Putin kuhusu madhara ya kuivamia Ukraine.

USHIRIKIANO WA NHIF NA ZHSF WAVUTIA KAMATI YA BAJETI YA BARAZA LA WAWAKILISHI

 

Na Matukio Daima Media , Dodoma

Kamati ya Bajeti ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar imeupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kazi kubwa inayofanya katika kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma za bima ya afya nchini, pamoja na ushirikiano wake na Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF).

Pongezi hizo zimetolewa leo, Agosti 26, 2026, na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Mariam Hamis Said, wakati Kamati hiyo pamoja na Menejimenti za ZHSF na NHIF ilipotembelea Makao Makuu ya NHIF kwa ajili ya kujifunza namna Mfuko huo unavyoendesha na kutoa huduma kwa wanachama.

Mhe. Mariam amesema ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa, kwa kuwa Kamati imepata fursa ya kuelezwa na kujionea kwa vitendo mifumo na huduma zinazotolewa na NHIF, kupitia ziara kwenye Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH).

Pamoja na kutoa pongezi kwa NHIF, Kamati hiyo ilipata fursa ya kutaka kufahamu kwa kina masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji na maendeleo ya Mfuko, ikiwemo namna NHIF inavyopambana na udanganyifu, utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, pamoja na hatua zinazochukuliwa kuhakikisha wanachama wanapata huduma bora na kwa wakati.

Aidha, Kamati ilitaka kufahamu namna matumizi ya TEHAMA yameboresha utendaji wa NHIF na kusaidia kupunguza gharama za uendeshaji, pamoja na namna uwekezaji unavyosaidia kuimarisha Mfuko. 

Masuala mengine yaliyotiliwa mkazo ni pamoja na vyanzo vya mapato ya Mfuko, viashiria vinavyotumika kupima mafanikio na uendelevu wa NHIF, pamoja na mafunzo na uzoefu ambao Mfuko umeupata katika kipindi cha miaka 25 ya utekelezaji wa majukumu yake.

Amesema ushirikiano kati ya NHIF na ZHSF umeleta matokeo makubwa katika hatua mbalimbali za uanzishaji na uendelezaji wa ZHSF, huku akieleza kuwa uzoefu na msaada uliotolewa na NHIF umeiwezesha Zanzibar kuanza na kuendelea vizuri katika safari ya kuimarisha huduma za bima ya afya.

“Kamati inapongeza NHIF na ZHSF kwa mashirikiano makubwa wanayoyafanya ambayo yamewezesha ZHSF kuanza na kuendelea vizuri,” amesema Mhe. Mariam.

Ameongeza kuwa kazi iliyofanywa na NHIF katika kusaidia uanzishaji wa ZHSF ilihitaji uvumilivu na kujitolea kwa kiwango kikubwa, akieleza kuwa Zanzibar imenufaika na uzoefu wa NHIF katika kujenga mfumo wa bima ya afya.

“Kazi iliyofanywa na NHIF ni kazi iliyofanyika kwa uvumilivu mkubwa, lakini kwa kutubeba Zanzibar katika uanzishaji wa Mfuko wetu,” amesema.

Aidha, Mhe. Mariam ameipongeza Menejimenti ya NHIF kwa kuwawezesha kutembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa, ambako wamejionea namna wanachama wa NHIF wanavyopokelewa na kuhudumiwa.

Amesema ziara hiyo imewapa fursa ya kuona kwa vitendo ubora wa huduma zinazotolewa, hususan huduma za kibingwa na kibingwa bobezi, ambayo ni mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika kuboresha huduma za afya nchini.

“Tumejionea namna wanachama wa NHIF wanavyopokelewa na kuhudumiwa. Hakika kazi hii ni kubwa na nzuri ambayo kwa ujumla tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, ambapo huduma za kibingwa na kibingwa bobezi zinapatikana hapa nchini,” amesema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dkt. Irene Isaka, amesema Mfuko utaendelea kushirikiana kwa karibu na ZHSF ili kuhakikisha wananchi na wanachama wanapata huduma bora za afya kwa wakati na kwa ufanisi.

Dkt. Isaka amesema NHIF itaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika kwa ZHSF, hususan katika maeneo ya uzoefu, mifumo ya utoaji huduma na masuala mengine ya kitaalamu, kwa lengo la kuimarisha huduma za bima ya afya kwa wananchi wa Zanzibar.

Amesema ushirikiano huo ni sehemu ya dhamira ya NHIF ya kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa wananchi popote walipo nchini, huku mifuko hiyo ikiendelea kujifunza na kubadilishana uzoefu katika kuboresha huduma kwa wanachama.

Ziara hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu baina ya taasisi zinazohusika na utoaji wa huduma za bima ya afya Tanzania Bara na Zanzibar.

MWISHO.

Video: Wabunge 324 Wamthibitisha Ndejembi kuwa Makamu wa Rais

Global Publishers
August 28, 2026
48 views
0 Comments

Wabunge 324 wamepiga kura za “Ndiyo” kumthibitisha Makamu wa Rais Mteule, Deogratius John Ndejembi, kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kura hiyo imefanyika leo, Agosti 28, 2026, katika kikao cha Bunge jijini Dodoma, kufuatia jina la Ndejembi kuwasilishwa kwa ajili ya uthibitisho.

Katika mchakato huo, hakukuwa na kura ya “Hapana” wala kura iliyoharibika, hivyo Ndejembi amepata uungwaji mkono wa asilimia 100 ya kura zilizopigwa.

Uthibitisho huo unafungua njia kwa Ndejembi kuapishwa rasmi na kuanza majukumu yake kama Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hatua ya Mwisho kwa Ndejembi Bungeni, Waziri Ammwagia Sifa (Picha +Video)

Global Publishers
August 28, 2026
90 views
0 Comments

Makamu wa Rais Mteule na Waziri wa Nishati, Deogratius John Ndejembi, leo Agosti 28, 2026, amehudhuria Kikao cha Tatu cha Mkutano wa Nne wa Bunge la Kumi na Tatu kinachoendelea jijini Dodoma.

Katika kikao hicho, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amewasilisha hoja ya kumthibitisha Ndejembi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hatua hiyo imekuja baada ya Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, kutangaza kuwa amepokea jina la Makamu wa Rais Mteule lililowasilishwa kwake na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge.

Ndejembi, ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Chamwino na Waziri wa Nishati, alipendekezwa na Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushika nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, kujiuzulu nafasi hiyo.

Endapo Bunge litamthibitisha, Ndejembi ataingia rasmi katika nafasi ya Makamu wa Rais na kuanza kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais Samia Atuma Rambirambi Kifo cha Mfalme wa Norway

Shechambo Chris
August 28, 2026
6 views
0 Comments

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa wananchi na Serikali ya Norway kufuatia kifo cha aliyekuwa Mfalme wa taifa hilo, Harald V, aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 89.

Kupitia ujumbe wake rasmi, Rais Samia ameeleza kusikitishwa kwake na taarifa hizo huku akiihakikishia familia ya kifalme na wananchi wa Norway kuwa Tanzania ipo pamoja nao katika kipindi hiki cha simanzi kuu.

“Nimesikitishwa sana na taarifa za kifo cha Mheshimiwa Mfalme Harald V wa Norway. Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatuma rambirambi zetu za dhati kabisa kwa Mheshimiwa Mfalme Haakon VIII, Familia ya Kifalme, na wananchi wa Ufalme wa Norway,” alisema Rais Samia.

Mfalme Harald V, aliyekuwa mfalme wa umri mkubwa zaidi barani Ulaya, amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Oslo (Rikshospitalet). Kufuatia msiba huo, Mwana wa Mfalme, Prince Haakon, anatarajiwa kuchukua mikoba ya uongozi kama Mfalme mpya wa taifa hilo.

Ikumbukwe kuwa Tanzania na Norway zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu wa kidiplomasia na kiuchumi, na ujumbe wa Rais Samia unadhihirisha mshikamano thabiti kati ya mataifa haya mawili.

 

Na Hasina Thabit

KINGU: NDEJEMBI NI KIJANA MZALENDO, MCHAPAKAZI

 

Mbunge wa Ikungi Magharibi, Elibariki Kingu amemmwagia sifa Makamu wa Rais mteule, Deogratius Ndejembi akisema ni kijana mchapakazi, mwenye uzalendo ndani yake na anayeling’arisha Taifa.

Kingu ameyasema hayo leo Agosti 28, 2026 jijini Dodoma wakati akichangia hoja ya kumthibitisha ndejembi kwenye nafasi ya Makamu wa Rais, iliyotolewa na Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba.

Amesema Taifa limepata kijana mwenye kaliba ya unyeyekevu na kujishusha kwa kila mtu na nidhamu katika kazi anazofanya kila siku.

“Ndejembi ni kijana mchapakazi mwenye commitment ya uzalendo ndani yake. Wakati dunia inapita kwenye misukosuko ya kupanda kwa bei ya mafuta, ni kijana huyu Ndejembi aliisimamia Serikali kuhakikisha shirika letu la TPDC (Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania) linapata uhakika wa kupata mafuta kwa kipindi chote ambacho dunia inapita katika misukosuko.

“Ni kwa uzalendo huo wa kijana huyu, ameweza kuling’arisha taifa katika medani za kimataifa. Leo anapokuwa nje ya nchi tunaona uwakilishi wake na utulivu wake namna anavyoliwakilisha taifa letu,” amesema Kingu.

Msukuma Asimulia Ndejembi Alivyopokea Taarifa za Uteuzi wa Makamu wa Rais – Video

Global Publishers
August 28, 2026
870 views
0 Comments

Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku ‘Msukuma’, amesimulia namna Deogratius Ndejembi alivyopokea taarifa za kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Msukuma ametoa simulizi hiyo wakati akizungumza kuhusu uteuzi wa Ndejembi, ambaye Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua na kumpendekeza kushika nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa Msukuma, namna Ndejembi alivyopokea taarifa hizo inaonyesha hali aliyokuwa nayo baada ya kupata taarifa za uteuzi huo.

Ndejembi amependekezwa kushika nafasi hiyo baada ya mchakato uliofanywa na CCM, huku hatua inayofuata ikiwa ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupokea na kuthibitisha uteuzi huo kwa mujibu wa Katiba.