Kitawaka EPL Wikiendi Hii, Macho Yatakuwa Liverpool, United, Arsenal

Ligi Kuu ya England, Premier League, inaendelea wikiendi hii kwa michezo mbalimbali huku timu kubwa zikitarajiwa kushuka dimbani kuwania pointi muhimu katika mbio za mapema za msimu wa 2026/27.

Miongoni mwa michezo inayosubiriwa kwa hamu ni Liverpool dhidi ya Nottingham Forest, huku Liverpool ikilenga kuendeleza kasi nzuri na kuhakikisha inapata matokeo yatakayoipa nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.

Nayo Tottenham Hotspur itakuwa mwenyeji wa Newcastle United katika mchezo mwingine unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Timu hizo zinahitaji pointi tatu ili kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.

Macho pia yataelekezwa kwenye mchezo wa Brighton dhidi ya Chelsea, ambapo Chelsea itakuwa ikitafuta ushindi muhimu dhidi ya Brighton. Mchezo huo unatarajiwa kuwa na mvuto kutokana na ushindani wa timu hizo katika soka la England.

Katika mchezo mwingine mkubwa, Aston Villa itakutana na Arsenal, huku Arsenal ikitarajiwa kuwa na kazi ya kuhakikisha inapata matokeo mazuri katika uwanja wa Villa.

Kwa upande wa Manchester United, timu hiyo itakuwa ugenini dhidi ya Ipswich Town katika mchezo utakaokuwa muhimu kwa kikosi hicho, hasa baada ya kuanza msimu kwa matokeo yasiyoridhisha.

Wakati huo huo, michezo mingine ya wikiendi itawakutanisha Bournemouth na Everton, Sunderland na Fulham, pamoja na Leeds United dhidi ya Brentford.

Kwa ujumla, wikiendi hii inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku kila timu ikisaka pointi tatu katika hatua za mwanzo za msimu wa Premier League.

Mechi za EPL wikiendi hii — 29–31 Agosti 2026

Ijumaa, Agosti 28

  • Crystal Palace vs Manchester City — saa 4:00 usiku (Tanzania)

Jumamosi, Agosti 29

  • Liverpool vs Nottingham Forest — saa 2:30 jioni
  • Bournemouth vs Everton — saa 5:00 jioni
  • Coventry City vs Hull City — saa 5:00 jioni
  • Tottenham Hotspur vs Newcastle United — saa 7:30 usiku

Jumapili, Agosti 30

  • Sunderland vs Fulham
  • Brighton vs Chelsea
  • Leeds United vs Brentford
  • Aston Villa vs Arsenal

Jumatatu, Agosti 31

  • Ipswich Town vs Manchester United

Ratiba hii ni ya wikiendi ya pili ya Premier League 2026/27.

Wiki hii ndani ya DStv ni special sana! Usikose kutazama episode mpya ya kipindi cha A List, mechi za kukatana na shoka za ligi ya England, bila kusahau Jumapili kuanzia saa 4:00 tunaanza kuitazama series mpya ya Spinners ikiwa na lugha ya Kiswahili.

Aunty Ezekiel Afichua Siri Za Mastaa, “Zamani Tulitoka Na Wanaume Wakubwa”

Global Publishers
August 28, 2026
18 views
0 Comments

Msanii wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel, amefunguka kuhusu maisha ya mahusiano ya mastaa wenzake, akieleza namna baadhi yao walivyokuwa wakitoka na wanaume waliowazidi umri kipindi cha nyuma, tofauti na ilivyo sasa.

Aunty Ezekiel amesema zamani mastaa hao walikuwa wakiingia kwenye mahusiano kwa misingi ya mapenzi, huku wakitoka na wanaume waliowazidi umri, lakini kwa sasa mambo yamebadilika na baadhi yao wameanza kutoka na vijana wadogo.

Kauli hiyo ameitoa huku akiwapa stori mastaa wenzake, Wema Sepetu (Wolper), Kajala Masanja na Irene Uwoya, akizungumzia mwenendo wa mahusiano yao na namna ulivyobadilika kwa miaka ya hivi karibuni.

Aunty Ezekiel ameeleza kuwa kipindi cha nyuma ilikuwa jambo la kawaida kwa mastaa hao kuwa katika mahusiano na wanaume wenye umri mkubwa kuliko wao, lakini sasa baadhi yao wamekuwa wakihusishwa na vijana wenye umri mdogo.

Kauli hiyo imezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii, huku mashabiki wakisubiri kuona namna mastaa hao watakavyoitikia kauli hiyo ya Aunty Ezekiel.

Weekend hii ndani ya DStv ni special sana! Usikose kutazama episode mpya ya kipindi cha A List, mechi za kukatana na shoka za ligi ya England, bila kusahau Jumapili kuanzia saa 4:00 tunaanza kuitazama series mpya ya Spinners ikiwa na lugha ya Kiswahili.

Lipia mapema kifurushi chako kwa kupiga *150*53# ili usipitwe na burudani hii ya kukatana na shoka.

Mwang’oda aagiza usimamizi miradi ya CSR – HabariLeo

GEITA: KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mwaka 2026, Wazo Michael Mwang’oda, ameagiza viongozi wa serikali kushiriki, kufuatilia na kusimamia kikamirifu miradi ya Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR).

Mwang’oda ametoa maagizo hayo alipoongoza msafara wa mbio za mwenge kutembelea, kukagua na kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya Lwamugasa wilayani Geita.

Amesema fedha za CSR zinazotolewa na makampuni ni fedha halali za watanzania kwa kuwa zinatolewa kwa mjibu wa sheria za nchi na hivo miradi ushiriki wa viongozi wa serikali ni jambo muhimu.

“CSR inatolewa kwa mjibu wa sheria, kwa ajili ya kurudisha kwa wananchi, kwa kuwa wanarudisha kwa jamii, basi serikali isimamie kwa ukaribu, tusiwaachie wadau wetu wa maendeleo peke yao”, amesema.

Aidha, ameagiza kituo cha afya Lwamugasa kuunganishiwa umeme ili kuruhusu miundombinu iliyojengwa na serikali kuanza kutoa huduma za afya kwa wananchi kusudiwa wa eneo la Lwamugasa.

Amesema haina afya kuona ujenzi wa miundombinu yote umekamilika, vifaa tiba vimenunuliwa na watoa huduma za afya wameajiliwa lakini kituo cha afya hakitoshelezi kutoa huduma kwa kukosa umeme.

“Kitakwimu kata hii ina zaidi ya wananchi elfu 72, niombe wanaohusika waweze kuleta umeme mahala hapa ili huduma zingine zianze kutolewa katika kituo hiki”, amesema.

Naibu Waziri wa Tamisemi na Mbunge wa Jimbo la Busanda, Dk Jafari Rajabu Self amesema kituo cha afya Lwamugasa kinatarajia kuhudumia takribani wananchi 72,000 wa kata ya Lwamugasa.

 

“Kati ya wananchi hao elfu 72, wapo kina mama wanaojifungua kwa mwezi, wastani wa kina mama 250 na Lwamugasa hapakuwa kabisa na kituo cha afya.

Awali Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Lwamugasa, Charles Anthony amesema mradi umegharimu takribani sh bilioni 1.24 kati yake sh milioni 565 ni fedha za CSR kutoka kampuni ya Bucreef.

Kagera yapokea vifaa kilimo cha umwagiliaji – HabariLeo

KAGERA: Mkoa wa Kagera, kupitia Tume ya Umwagiliaji umepokea vifaa vya umwagiliaji kutoka Wizara ya Kilimo, vyenye thamani ya Sh bilioni 1.2 ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha wakulima wadogo kuendelea na uzalishaji wa mazao bila kutegemea mvua.

Lengo la hatua hiyo ni kuongeza uzalishaji wa kilimo kwa kuwawezesha wakulima kutumia teknolojia ya umwagiliaji na hivyo kupunguza utegemezi wa mvua katika shughuli zao za kilimo na Kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahya Ramadhani Kido, ndiye aliyekabidhi vifaa hivyo kwa vikundi 146 vya wakulima,wa mkoa wa Kagera huku akisisitiza umuhimu wa kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuongeza tija na uzalishaji wa mazao

Amesema vifaa hivyo vinatarajiwa kuwa chachu ya kuimarisha kilimo cha umwagiliaji na kuongeza uhakika wa uzalishaji wa chakula kwa ngazi ya kaya na Taifa kwa ujumla kwa misimu mbalimbali kwa ukanda wa mkoa wa Kagera na Kanda ya Ziwa.

Amezitaka Mamulaka za serikali za mitaa kuhakikisha zinasimamia vikundi hivyo na kuvisajili kisheria na kutoa taarifa za uzalishaji baada ya muda mfupi ,kutoa mafunzo namna ya kutumia vifaaa hivyo Kwa weledi na kutunga sheria ndogo ndogo kwa vikundi vyenye nia ovu ya kukodisha vifaa hivyo au kuviuza kinyume na matakwa

Taarifa iliyotolewa na Mhandisi wa tume ya umwagiliaji mkoani Kagera Said Mbiru alisema kuwa vikundi vilivyopokea vifaa ni 146 vyenye uwezo wa wakulima 2193

Alisema vifaa hivyo vinauwezo wa kurusha maji Lita 80,000 kwa saa na kumwagilia hekari 28 kwa saa.

Alisema hiyo ni awamu ya kwanza Kwa wakulima wadogo kupata vifaa hivyo na awamu ya pili itahusisha wakulima wengi zaidi kwenye vikundi vyao .

Katibu wa itikadi na uenezi chama Cha mapinduzi CCM Hamimu Mahamud amesema ilani ya chama Cha mapinduzi ya mwaka 2025-2030 inasema kuwa serikali itaendelea kuwajali wananchi wake wakiwemo wakulima kwa kuhamasisha kwa vitendo kilimo cha umwagiliaji bila kusubiri mvua.

Amesema ni vyema wakulima wakashikama na kujiuga kwenye vikundi ili wapate kuhudumiwa kwa pamoja kama kupewa mitaji,dhana za kilimo pembejeo na mbolea na kwa njia hiyo wakulima wanakuwa wamenufaika na utekelezaji wa ilani ya chama Cha mapinduzi.

Mwakilishi wa vikundi vya wakulima Recho Chacha kutoka kikundi Cha Kinyerere Kagya Amesema serikali imefanya jambo kubwa kwa wakati uliopo kutokana na majira kubadilika badilika na kukosekana kwa mvua za uhakika.

Amewasilisha ombi la wakulima la kupewa trecta ndogo za kilimo ili kupiga hatua kubwa za kuingia katika wakulima wakubwa na kudai kuwa jembe la mkono linachosha na matokeo yanakuwa kidogo .

Mikakati yasukwa kuvutia wawekezaji wakubwa Ulaya – HabariLeo

DAR ES SALAAM: Tanzania inalenga kuvutia mitaji mikubwa zaidi kutoka Ulaya kwa kuimarisha mazingira ya uwekezaji kwa sekta binafsi, hatua inayotarajiwa kuongeza ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo ameeleza hayo leo Agosti 27, Dar es Salaam, katika mkutano wa mashauriano kati ya Serikali na wawakilishi wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Umoja wa Ulaya (EU).

Katika mkutano huo, pande hizo zimejadili fursa mbalimbali za uwekezaji, na namna ya kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa nchini ili kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika soko la dunia.

Prof. Mkumbo amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi na wawekezaji, huku ikilenga kutumia fursa zilizopo kuongeza uzalishaji, ajira na kukuza uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake, Balozi wa Ireland nchini Tanzania na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Ulaya, Nicola Brennan, amesema EU ina dhamira ya kuendelea kuwekeza na kushirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi.

Amesema utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 utasaidia kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji, hivyo kuongeza fursa za Tanzania kuvutia mitaji mikubwa kutoka Ulaya na kuimarisha nafasi yake kama nguvu ya kiuchumi katika Afrika Mashariki.

Majirani jengeni utamaduni wa kutambuana – HabariLeo

MOROGORO; Watanzania wameombwa kujenga utamaduni wa watu majirani kutambuana na inapotokea jirani yako humuelewi vizuri toa taarifa mapema kwa viongozi wa serikali ya mtaa au polisi.

Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 27, 2026 na Kamishna wa Polisi Jamii Tanzania, Alex Mkama alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua Banda la Polisi Jamii katika Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni linalofanyika mkoani Mororgoro na kueleza kwa njia hiyo itasaidia kupunguza baadhi ya vitendo vya jinai.

Pia ametaka jamii itilie mkazo suala la maadili kuanzia ngazi ya familia, kwani maadili ndio yanayofanya watu wawajibike, wachukie rushwa na kuupuka vitendo vya uhalifu.

Ameitaka jamii kujenga tabia ya kutambua majirani zao na pale wanapoona wageni wanaowatilia mashaka watoe taarifa polisi au kwa viongozi wa serikali..

Kwa upande wake Mrakibu Mwandamizi wa Polisi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Kanisheni ya Polisi Jamii Dk, Ezekiel Kyogo, amesema wameshiriki tamasha hilo kwa lengo la kutoa elimu Kwa jamii.

Amesema matukio mengi ya jinai chimbuko lake ni kukosekana maadili, hivyo kupitia elimu hiyo wataweza kurejesha jamii kwenye maadili.

Naye Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro,  Pendo Meshurie amesema kupitia tamasha hilo wamekuwa wakitoa elimu ya kupambana na vitendo vya ukatili kupitia sanaa zikiwemo nyimbo na vipeperushi.

Bahasha yenye jina la Makamu wa Rais Mteule yatua bungeni – HabariLeo

DODOMA; Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, leo Agosti 28 , 2026 amepokea rasmi jina la Makamu wa Rais Mteule, Deogratius John Ndejembi, lililopendekezwa na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Jina hilo limewasilishwa kwa Spika na Katibu wa Rais Balozi Ali Jabir Mwadini akiwa ameambatana na Mpambe wa Rais (ADC) Brigedia Jenerali, Nyamburi Mashauri kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge.

Mapokezi ya Jina hilo yameshuhudiwa na Naibu Spika, Daniel Sillo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, pamoja na Katibu wa Bunge , Baraka Leonard.Wengine ni Wenyeviti wa Bunge, Deogratius Mwanyika, Najma Giga na Cecilia Pareso.

MADIWANI CHUNYA WAONYWA KUTIMIZA WAJIBU WAO.

Na Samwel Mpogole – Mbeya.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Mbaraka Alhaji Batenga amewataka madiwani kutambua wajibu wao wa kuwawakilisha wananchi kwa kuhakikisha wanahudhuria vikao vya Baraza la Madiwani na kushiriki kikamilifu katika kufanya maamuzi ya maendeleo.

Hayo yanajiri baada ya zaidi ya madiwani 10 kutoshiriki kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kilichokutana kujadili na kupitisha hesabu za mwisho za Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Mbali na suala la mahudhurio, Mkuu huyo wa Wilaya amewataka madiwani kuhakikisha wanabaini maeneo yenye changamoto ya maji na kuweka mipango maalumu ya uchimbaji wa mabwawa, akisisitiza kuwa mitambo ya uchimbaji ipo na hivyo kinachohitajika ni kuwasilisha maombi ya maeneo yenye uhitaji.

Pia, amewataka madiwani kushirikiana na wananchi na watendaji katika kujiandaa kupokea wahitimu wa darasa la saba na darasa la sita wanaotarajiwa kujiunga na elimu ya sekondari, ambapo Halmashauri ina uhitaji wa vyumba vya madarasa 141 na matundu ya vyoo 577, huku zaidi ya shilingi bilioni tatu zikihitajika kukidhi mahitaji hayo.

Kadhalika, madiwani wametakiwa kusimamia upangaji bora wa huduma za kibiashara, ikiwemo kutenga maeneo rasmi kwa ajili ya shughuli za wachomeleaji na ujenzi wa parking, ili kuhakikisha mji wa Chunya unakuwa salama na wenye mpangilio.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Bwana Kelvin Shinshi, amewaagiza madiwani kuhakikisha wanasimamia vyema wananchi wanaowawakilisha na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo katika maeneo yao.

Amesema Halmashauri tayari imeanza kuchukua hatua za kutekeleza mipango ya kukabiliana na changamoto ya maji katika maeneo mbalimbali, huku akisisitiza kuwa kila diwani ana wajibu wa kuhakikisha mahitaji ya wananchi yanafikishwa na kufanyiwa kazi.

Kuhusu mahudhurio ya vikao, Mwenyekiti huyo amesema uvunjifu wa nidhamu unaosababishwa na kutohudhuria vikao hautaendelea kuvumiliwa, na kwamba hatua za kinidhamu zitaanza kuchukuliwa dhidi ya madiwani watakaokiuka kanuni na taratibu za mahudhurio.

Kwa upande wake, Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Chunya, Francis Michael, amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha kunakuwa na usimamizi madhubuti na wa ufanisi wa mapato ya Halmashauri, ili fedha zinazokusanywa zitumike kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.

Amesema usimamizi wa mapato kwa uadilifu utasaidia kuzuia upotevu wa fedha na kuhakikisha rasilimali zinazokusanywa zinatumika kutekeleza miradi ya maendeleo na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Jina la Makamu wa Rais Mteule lilivyowasilishwa bungeni – HabariLeo

DODOMA; Picha za matukio mbalimbali, wakati Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, akipokea rasmi leo Agosti 28, 2026 jina la Makamu wa Rais Mteule, Deogratius John Ndejembi, lililopendekezwa na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM).


Jina hilo limewasilishwa kwa Spika na Katibu wa Rais, Balozi Ali Jabir Mwadini akiwa ameambatana na Mpambe wa Rais (ADC) Brigedia Jenerali, Nyamburi Mashauri kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge.

Mapokezi ya jina hilo yameshuhudiwa na Naibu Spika, Daniel Sillo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, pamoja na Katibu wa Bunge , Baraka Leonard.Wengine ni Wenyeviti wa Bunge, Deogratius Mwanyika, Najma Giga na Cecilia Pareso

MIMI SIO MAKAMU WA RAIS WA CCM,NI WA VYAMA VYOTE – NDEJEMBI

NA MATUKIO DAIMA MEDIA

DODOMA. Makamu wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amesema baada ya kuthibitishwa na Bunge kwa kura zote 304 sawa na asilimia 100, atakuwa Makamu wa Rais wa Watanzania wote bila kujali vyama vyao vya siasa.

Ndejembi amesema hayo leo Agosti 28, 2026, muda mfupi baada ya kuthibitishwa na Wabunge kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema atatekeleza majukumu yake kwa unyenyekevu na kuhakikisha anakuwa kiungo kati ya Serikali na Watanzania wote, huku akisisitiza kuwa atafanya kazi kwa kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Ninakuwa ni Makamu wa Rais wa Watanzania wote, nakuwa Makamu wa Rais si wa wana CCM peke yake, nakuwa Makamu wa Rais wa Watanzania wa vyama vyote.”

Amesema atatumia nafasi hiyo kwa unyenyekevu mkubwa katika kumsaidia Rais na kuwa kiungo cha Watanzania wote.

“Nitajitahidi kwa unyenyekevu mkubwa sana kumsaidia Mheshimiwa Rais, kuwa kiungo wa Watanzania wote kama vile mapenzi yake yatakavyotaka, kwa sababu nafanya kazi chini yake.”amesema