Skip to content
-
Subscribe to our newsletter & never miss our best posts. Subscribe Now!
Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

  • Home
  • Privacy Policy
  • Sample Page
  • Home
  • Privacy Policy
  • Sample Page
Close

Search

  • https://www.facebook.com/
  • https://twitter.com/
  • https://t.me/
  • https://www.instagram.com/
  • https://youtube.com/
Subscribe
Habari

Mikakati yasukwa kuvutia wawekezaji wakubwa Ulaya – HabariLeo

By admin
August 28, 2026 2 Min Read
Comments Off on Mikakati yasukwa kuvutia wawekezaji wakubwa Ulaya – HabariLeo

DAR ES SALAAM: Tanzania inalenga kuvutia mitaji mikubwa zaidi kutoka Ulaya kwa kuimarisha mazingira ya uwekezaji kwa sekta binafsi, hatua inayotarajiwa kuongeza ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo ameeleza hayo leo Agosti 27, Dar es Salaam, katika mkutano wa mashauriano kati ya Serikali na wawakilishi wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Umoja wa Ulaya (EU).

Katika mkutano huo, pande hizo zimejadili fursa mbalimbali za uwekezaji, na namna ya kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa nchini ili kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika soko la dunia.

Prof. Mkumbo amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi na wawekezaji, huku ikilenga kutumia fursa zilizopo kuongeza uzalishaji, ajira na kukuza uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake, Balozi wa Ireland nchini Tanzania na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Ulaya, Nicola Brennan, amesema EU ina dhamira ya kuendelea kuwekeza na kushirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi.

Amesema utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 utasaidia kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji, hivyo kuongeza fursa za Tanzania kuvutia mitaji mikubwa kutoka Ulaya na kuimarisha nafasi yake kama nguvu ya kiuchumi katika Afrika Mashariki.

Author

admin

Follow Me
Other Articles
Previous

Majirani jengeni utamaduni wa kutambuana – HabariLeo

Next

Kagera yapokea vifaa kilimo cha umwagiliaji – HabariLeo

Recent Posts

  • Tanzania, DR Congo wakubaliana kuwarejesha wakimbizi – HabariLeo
  • POLISI YAWATAKA WANANCHI KUWAJUA JIRANI ZAO
  • Kitawaka EPL Wikiendi Hii, Macho Yatakuwa Liverpool, United, Arsenal
  • Aunty Ezekiel Afichua Siri Za Mastaa, “Zamani Tulitoka Na Wanaume Wakubwa”
  • Mwang’oda aagiza usimamizi miradi ya CSR – HabariLeo

Recent Comments

  1. A WordPress Commenter on Hello world!

Archives

  • August 2026

Categories

  • Burudani
  • Habari
  • Magazeti
  • Michezo
  • Siasa
Copyright 2026 — Habarimpya. All rights reserved. Blogsy WordPress Theme