SERIKALI YAWEKA USAWA KATIKA ELIMU MAFINGA IRINGA:SHALOM ROBERT

 

Wananchi wa Mji wa Mafinga Wilayani Mufindi Mkoani Iringa wameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kujenga shule ya Serikali ya mchepuo wa kiingereza hali inayoweka usawa kwa watoto wote kupata elimu bora.

Mdau wa maendeleo ambaye pia ni Mwanahabari Ndg.Shalom Robert akiwa mgeni wa heshima katika Mahafali ya Tatu ya Shule ya Chief Mkwawa English Medium amesema  jitihada za Serikali kuweka usawa kwa watoto kwa kujenga shule hiyo kunawafanya hadi wananchi wenye uchumi wa chini kuwapeleka watoto wao kupata elimu bora.

Aidha Robert Amesema shule hiyo imefanikiwa kupokea watoto wa Mama Lishe,Machinga,Wakulima na hata Wafugaji ambao wasingeweza kuwasomesha watoto wao kwenye shule ya mchepuo wa Kiingereza.

Ofisa Elimu Msingi Halmashauri ya Mji wa Mafinga Doroth Kobelo amesema ujenzi wa shule hiyo umepunguza mzigo kwa wazazi waliotamani kuwapeleka watoto wao English medium kwani ada yake ni nafuu na kila mzazi anaweza kumudu.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Chief Mkwawa English Medium Mwalimu James Kelela amesema shule hiyo imekuwa kimbilio la wazazi wengi kwani serikali imewekeza  miundombinu bora ya kujifunzia hali inayopelekea wazazi wengi kupeleka watoto wao hapo.

Katika mahalafi hayo shalom amechangia vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni mbili ili kuwafanya watoto wapate elimu bora pamoja na Michezo.

SHALOM ROBERT:SERIKALI YAWEKA USAWA KATIKA ELIMU MAFINGA IRINGA

MATUKIO DAIMA MEDIA

MAFINGA.Wananchi wa Mji wa Mafinga Wilayani Mufindi Mkoani Iringa wameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kujenga shule ya Serikali ya mchepuo wa kiingereza hali inayoweka usawa kwa watoto wote kupata elimu bora.

Mdau wa maendeleo ambaye pia ni Mwanahabari Ndg.Shalom Robert akiwa mgeni wa heshima katika Mahafali ya Tatu ya Shule ya Chief Mkwawa English Medium amesema  jitihada za Serikali kuweka usawa kwa watoto kwa kujenga shule hiyo kunawafanya hadi wananchi wenye uchumi wa chini kuwapeleka watoto wao kupata elimu bora.

Aidha Robert Amesema shule hiyo imefanikiwa kupokea watoto wa Mama Lishe,Machinga,Wakulima na hata Wafugaji ambao wasingeweza kuwasomesha watoto wao kwenye shule ya mchepuo wa Kiingereza.

Ofisa Elimu Msingi Halmashauri ya Mji wa Mafinga Doroth Kobelo amesema ujenzi wa shule hiyo umepunguza mzigo kwa wazazi waliotamani kuwapeleka watoto wao English medium kwani ada yake ni nafuu na kila mzazi anaweza kumudu.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Chief Mkwawa English Medium Mwalimu James Kelela amesema shule hiyo imekuwa kimbilio la wazazi wengi kwani serikali imewekeza  miundombinu bora ya kujifunzia hali inayopelekea wazazi wengi kupeleka watoto wao hapo.

Katika mahalafi hayo shalom amechangia vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni mbili ili kuwafanya watoto wapate elimu bora pamoja na Michezo.

NCHI ZA EAC ZATAKIWA KUJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO

Na, Matukio Daima Media Nairobi, Kenya

Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimetakiwa kuimarisha ushirikiano na kuchukua hatua za haraka kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño, zikiwemo mafuriko, maporomoko ya ardhi, uharibifu wa miundombinu na kuathirika kwa biashara na maisha ya kawaida ya wananchi.

Wito huo umetolewa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Dharura wa Wataalamu wa Sekta Mbalimbali kuhusu Maandalizi na Mwitikio wa Kikanda dhidi ya Mvua Zinazotarajiwa za El Niño Kali, unaofanyika Nairobi, Kenya, kuanzia Novemba 4 hadi 6, 2026.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wa wataalamu  umeongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Brigedia Jenerali Hosea Ndagala.

Akifungua mkutano huo Mratibu wa Mradi wa Pamoja wa Sekta Mbalimbali wa Usalama wa Chakula na Lishe wa Uganda, Bw.Julius Twinamatsiko amesema utabiri unaonesha uwezekano wa mvua kunyesha kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2026, hali inayohitaji maandalizi ya haraka na hatua za pamoja.

Amezitaka nchi wanachama kubaini maeneo hatarishi katika miundombinu ya usafirishaji, kuandaa njia mbadala, kuhakikisha upatikanaji wa chakula na malisho ya mifugo, pamoja na kuimarisha huduma za afya na ufuatiliaji wa magonjwa yanayoweza kuenea kutokana na mafuriko.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Sekretarieti ya EAC amesisitiza kuwa athari za El Niño zinaweza kuhatarisha amani, usalama na maendeleo ya kiuchumi, hivyo juhudi za kila nchi zinapaswa kuunganishwa kupitia mpango wa pamoja wa kikanda.

Mkutano huo unalenga kutathmini uwezo wa nchi wanachama kukabiliana na athari zinazotarajiwa, kubaini mapungufu na kuandaa mpango wa uratibu wa kikanda utakaosaidia kulinda maisha ya wananchi, huduma muhimu na shughuli za biashara katika Afrika Mashariki.

MWISHO

Watakiwa kuhama maeneo hatarishi kuepuka athari za El Nino Mbeya – HabariLeo

MBEYA; Kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kwa takribani dakika 30 na kusababisha nyumba 21 kusombwa na maji huku kaya 43 zikikosa makazi katika Kata ya Nzovwe, jijini Mbeya, Mkuu wa Mkoa huo, Jumanne Sagini, amewaagiza wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi kuhama mara moja kwa muda ili kunusuru maisha yao.

Akizungumza baada ya kuwatembelea waathirika wa mafuriko hayo, Sagini ameonya kuwa madhara yaliyotokea ni ishara ya hatari inayoweza kujitokeza zaidi endapo mvua kubwa zinazotabiriwa zitaendelea kunyesha huku wananchi wakiendelea kukaa katika maeneo hatarishi.

“Serikali imekuwa ikizungumzia uwepo wa mvua za El Niño, lakini baadhi ya watu wamekuwa wakifanya mizaha badala ya kuchukua tahadhari na kumuomba Mungu,sasa tumeona mvua ya nusu saa tu imesababisha madhara haya,Je, kama ingenyesha kwa saa saba hali ingekuwaje?” Amehoji Sagini.

Kutokana na hali hiyo, mkuu huyo wa mkoa ameagiza kamati ya maafa kuhakikisha kaya zilizoathirika zinapata msaada wa haraka wa chakula na magodoro, akieleza kuwa baadhi ya waathirika wamelazimika kuhifadhiwa na ndugu pamoja na majirani.

Aidha amethibitisha  kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha katika tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kuchukua tahadhari dhidi ya mvua zinazoendelea kunyesha ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

Amesema tayari Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)imeanza kuchukua hatua za kuboresha maeneo hatarishi, ikiwemo kushughulikia mtaro unaotajwa kuchangia mafuriko hayo baada ya maji kujaa na kufurika.

Kwa upande wake, mmoja kati ya waathirika wa tukio hilo, Innocent Mwongole, ameiomba Serikali kuhakikisha mtaro huo unafanyiwa marekebisho na vifusi vinavyotokana na shughuli za ujenzi wa barabara vinaondolewa ili kuzuia mafuriko mengine yasitokee.

Mvuvi Mkongwe Aingia Meridianbet na Safari Mpya ya Cash ‘Em All

Uvuvi ni kazi inayohitaji moyo wa subira, mikakati na uwezo wa kusubiri wakati sahihi kabla ya kuvuta chambo. Kwa mvuvi mwenye uzoefu, hakuna kitu kinachosisimua kama kuhisi samaki mkubwa ameingia kwenye mtego. Lakini safari hii, Meridianbet imeleta mabadiliko katika simulizi hilo kupitia mchezo wa Legendary Fisherman Cash ‘Em All, unaochukua mazingira ya uvuvi wa baharini na kuyageuza kuwa burudani ya kasino. Badala ya kusubiri samaki ajitokeze majini, hapa macho yako yataelekezwa kwenye pesa, zawadi na vipengele maalumu vinavyoufanya mchezo uwe na msisimko wake wa kipekee.

Mhusika mkuu wa mchezo huu ni mvuvi mwenye ndevu nyingi, sigara mdomoni na mwonekano wa mtu ambaye ana historia ndefu ya kupambana na samaki wakubwa. Anaonekana kama mtu anayejua siri zote za bahari, huku sura yake ikikupa picha ya mvuvi ambaye amewahi kukutana na changamoto nyingi katika safari zake. Mhusika huyo anaonekana kwenye nembo ya mchezo na pia kwenye Collect Symbol, jambo linalomfanya kuwa sehemu muhimu ya utambulisho wa Legendary Fisherman Cash ‘Em All. Ni aina ya ubunifu unaoufanya mchezo kuwa na tabia yake tofauti na kuleta mazingira ya uvuvi kwenye skrini yako.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kama ilivyo kwenye mashindano ya uvuvi, ambapo kila mshiriki anasubiri tukio kubwa litakalobadilisha matokeo, mchezo huu nao una kipengele kinachobeba msisimko mkubwa. Cash ‘Em All ndiyo sehemu inayovutia zaidi, hasa pale Money Symbols zinapoanza kujitokeza. Wachezaji wanakutana na viwango vitatu vya thamani vinavyojulikana kama Bronze, Silver na Gold. Kila kiwango kina matokeo tofauti, hivyo safari ya mchezo inakuwa na mabadiliko yanayoweza kuongeza burudani. Hapa ndipo unapoweza kuelewa kwa nini kila alama inayojitokeza inahitaji kufuatiliwa kwa makini.

Lakini mchezo hauishii kwenye alama za pesa pekee. Mystery Symbols na Level Up Symbols vinaongeza ladha nyingine kwa kuwa vinaweza kuboresha kipengele cha Cash ‘Em All. Pia, Progression Meter ni sehemu muhimu inayofuatilia maendeleo ya mchezo kadiri mizunguko inavyoendelea. Vipengele hivi vinaifanya Legendary Fisherman Cash ‘Em All kuwa na safari yenye hatua mbalimbali, huku kila mzunguko ukiendelea kuleta matarajio mapya. Kwa wapenzi wa kasino wanaopenda michezo yenye mandhari ya kipekee na vipengele vya ziada, huu ni mchezo unaostahili kujaribiwa.

Meridianbet inaendelea kukuletea michezo mbalimbali inayochanganya ubunifu, burudani na msisimko wa kipekee. Sasa ni zamu yako kuingia kwenye safari ya Legendary Fisherman Cash ‘Em All na kumfuata mvuvi huyu mkongwe katika ulimwengu wa alama za pesa na jackpot. Fungua akaunti yako Meridianbet, ingia kwenye mchezo na ujionee burudani inayokusubiri.

TAKUKURU MOROGORO YATATUA CHANGAMOTO YA MAJI SGR YA JAKAYA KIKWETE

Na Lilian Kasenene, Morogoro 

Matukio Daima Media 

TAASISI ya kupambana na kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) imefanikiwa kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji katika stesheni ya SGR ya Jakaya Kikwete .

Afisa mwandamizi wa TAKUKURU  mkoa wa Morogoro Casius  Kiaro amesema hayo wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

“Kwa Utatuzi wa changamoto hii ya maji katika stesheni tunatarajia utasaidia kuokoa zaidi ya sh milioni 106.08 kwa mwaka zilizokuwa zikitumika kununua na kusafirisha maji kwa magari maalumu,” bouser” alisema Kiaro .

Alisema kabla ya hatua hiyo stesheni  ilikuwa inatumia sh milioni 2.21 kwa wiki sawa na sh milioni 8.24 kwa mwezi kwa ajili ya kununua maji kwenye magari  kwani hawakuwa na huduma ya maji ya uhakika kwa matumizi ya stesheni na mabehewa.

Bw Kiaro alisema TAKUKURU kupitia  mpango wake wa ufuatiliaji wa huduma za kijamii ilibaini changamoto inayoikabili stesheni hiyo na kuamua kuitafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na SGR na MORUWASA.

Naye meneja wa kanda namba moja  MORUWASA Injinia Gidion Chahe alisema kwa  sasa stesheni hiyo matumizi yake ya maji ni kati ya lita milioni   mbili hadi milioni nne kwa siku na wamekuwa wakifunguliwa maji mara mbili kwa wiki.

Alisema ili kuwa na uhakika zaidi wa maji stesheni hiyo kwa kushirikiana na MORUWASA wanajenga matanki yatakayoweza kuhifadhi maji mengi  na kwa muda wa siku  kati ya tatu hadi tano.

Kaimu Meneja wa wa stesheni ya Jakaya Kikwete,  Salvatory Kimaro alisema hivi sasa kituo hicho kinahudumia abiria wengi tofauti na walivyoanza,  hivyo na mahitaji ya maji yanazidi kuongezeka.

” Wakati tunaanza tulikuwa na safari chache na mahitaji ya maji ilikuwa ni lita 6000 ila sasa safari zimeongezeka…. abiria wameongezeka mahitaji ya maji kwa sasa ni lita 152,000 kwa wiki”  alisema Kimaro.

MWISHO.

Fenerbahçe Kuikabili Liverpool, Usiku wa Miamba Ya Ulaya leo!

Mashabiki wa soka wanatarajia kushuhudia pambano lenye mvuto mkubwa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Fenerbahçe ya Uturuki itakapokuwa mwenyeji wa Liverpool ya England katika mchezo wa hatua ya ligi utakaopigwa leo Jumatano, kwenye dimba la Şükrü Saracoğlu, jijini Istanbul.

Fenerbahçe inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na jukumu kubwa la kurekebisha mwenendo wake kwenye mashindano hayo. Katika michezo mitatu iliyopita, timu hiyo imeanza kwa sare ya 1-1 dhidi ya AS Roma, ikakubali kichapo cha mabao 6-0 kutoka kwa Aston Villa kabla ya kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Slavia Prague. Hivyo, kucheza nyumbani kunakuwa nafasi muhimu kwa kikosi hicho kutafuta ushindi na kurejesha matumaini ya kusonga mbele.

Kwa upande wa Liverpool, The Reds wanaingia Istanbul wakiwa na mwanzo mzuri katika kampeni hii ya Champions League. Wamekusanya pointi tisa baada ya kushinda michezo yote mitatu ya awali dhidi ya Atlético Madrid (2-1), LASK (6-3) na Villarreal (4-3). Rekodi hiyo inaonyesha ubora wa safu yao ya ushambuliaji, ingawa kuruhusu mabao katika michezo hiyo miwili ya mwisho ni jambo ambalo benchi la ufundi litahitaji kulifanyia kazi.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Macho yatakuwa kwa nyota wa Liverpool kama Mohamed Salah, Florian Wirtz na Alexander Isak, ambao wanaweza kuwa sehemu muhimu ya mipango ya kuisumbua ngome ya wenyeji. Hata hivyo, Fenerbahçe nayo ina wachezaji wenye uwezo wa kubadilisha matokeo ya mchezo, akiwemo Ederson, N’Golo Kanté na Jhon Durán. Kwa Liverpool, ushindi wa ugenini utaendeleza mwenendo wao mzuri, huku Fenerbahçe ikihitaji kutumia nguvu ya mashabiki wake kupata matokeo.

Kinachoongeza ladha ya mchezo huu ni kwamba timu zote zina malengo tofauti lakini yenye uzito sawa. Fenerbahçe inataka kujinasua katika nafasi za chini za msimamo, wakati Liverpool inalenga kuendelea kuimarisha nafasi yake katika timu zinazowania kufuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora. Kwa hiyo, kila dakika ya mchezo inaweza kuwa na umuhimu mkubwa, kuanzia mbinu za makocha hadi uwezo wa wachezaji kutumia nafasi wanazozipata.

Istanbul itawaka moto! Je, Fenerbahçe itatumia faida ya uwanja wake kuwazuia The Reds au Liverpool itaendeleza ubabe wake na kuondoka na pointi tatu muhimu? Jiandae kushuhudia burudani ya soka la kiwango cha juu, ushindani na vita ya pointi katika usiku wa Champions League. Mchezo huu ni sehemu ya machaguo mengi yanayokusubiri Meridianbet, hivyo jiunge leo na uwe sehemu ya washindi wa leo.

UDSM kujadili nafasi ya vijana Afrika – HabariLeo

DAR ES SALAAM: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kupitia Ndaki ya Sayansi za Jamii, kimeandaa Mkutano wa Kimataifa wa Sauti ya Sayansi za Jamii (VSS2026), utakaowakutanisha wanataaluma, watafiti na vijana kujadili nafasi ya kizazi cha Gen Z katika kuamua mustakabali wa jamii za Afrika.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Novemba 5 na 6, 2026, katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ukiwa na kaulimbiu isemayo “Kutafakari Upya Leo na Kesho: Kizazi cha Gen Z na Harakati za Kijamii Barani Afrika.”

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Ndaki ya Sayansi za Jamii ya UDSM, Dk. Richard Sambaiga, amesema mkutano huo unalenga kutoa jukwaa la kujadili mchango, nafasi na changamoto zinazowakabili vijana wa kizazi hicho katika maendeleo ya jamii.

Amesema mijadala hiyo itajikita katika nafasi ya vijana kwenye uongozi, utawala, uwajibikaji wa taasisi za umma na ushiriki wao katika mijadala ya kitaifa, pamoja na namna wanavyoweza kuchangia kujenga jamii yenye uwazi na ushirikishwaji.

Aidha, amesema mkutano huo utajadili mchango wa teknolojia za kidijitali na mitandao ya kijamii katika kuibua mijadala, kusambaza taarifa, kuhamasisha mabadiliko ya kijamii na kuwawezesha vijana kushiriki katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazoikabili jamii.

Masuala mengine yatakayojadiliwa ni pamoja na changamoto za ajira, fursa za kiuchumi, mazingira ya kujipatia kipato, jinsia, mahusiano ya kijamii, utambulisho, tofauti za kipato, mabadiliko ya tabianchi, utamaduni, elimu na uzalishaji wa maarifa.

Dk. Sambaiga amesema mkutano huo utashirikisha wanataaluma, watafiti, vijana, wawakilishi wa asasi za kiraia na wadau mbalimbali kutoka Tanzania, nchi nyingine za Afrika na nje ya bara hilo kwa lengo la kubadilishana uzoefu na mawazo kuhusu nafasi ya kizazi cha Gen Z katika kuunda mustakabali wa jamii za Afrika.

Amesema kupitia mkutano huo, wanatarajia sauti, mawazo, matarajio na mahitaji ya vijana kupata nafasi katika mijadala na maamuzi yanayohusu maendeleo ya jamii na mustakabali wa bara la Afrika.

Familia ya Lissu Yatangaza Ratiba ya Mazishi ya Mzee Alute

Global Publishers
November 4, 2026
24 views
0 Comments

Familia ya marehemu Alute Mughwai Lissu imetangaza ratiba ya shughuli za kuuaga na kuzika mwili wa marehemu, ambapo ibada ya kuuaga itafanyika Jumatatu, Novemba 9, 2026, jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari Novemba 3, 2026, msemaji wa familia, Vincent Lissu Mughwai, ambaye ni mdogo wa marehemu, amesema ibada hiyo itafanyika katika Kanisa la Mtakatifu Teresa kuanzia saa saba mchana.

Amesema baada ya ibada ya kuuaga, mwili wa marehemu utasafirishwa kuelekea mkoani Singida kwa ajili ya mazishi.

Kwa mujibu wa Vincent, mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumanne, Novemba 10, 2026, katika Kijiji cha Mahambe, ambacho ni nyumbani kwa marehemu na familia yake.

Katika hatua nyingine, Vincent amethibitisha kuwa ratiba ya familia kwenda mahakamani Ijumaa, Novemba 6, 2026, kusikiliza hukumu ya kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Antipas Lissu, haijabadilika.

Amesema familia itashiriki shughuli hiyo ya mahakamani kama ilivyopangwa kabla ya kuendelea na taratibu nyingine za kuuaga na mazishi ya marehemu.

Familia imeendelea na maandalizi ya kuhakikisha shughuli zote za kumuaga na kumzika marehemu zinafanyika kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa.

Nandy vs Zuchu: Fahamu Ukweli wa Mafanikio Unaofichwa na Followers na Views

Wakati mashabiki wa muziki wakiendelea kuwalinganisha Nandy na Zuchu kuhusu nani mwenye mafanikio makubwa zaidi, safari zao zinaibua mjadala mpana unaozidi idadi ya mashabiki, watazamaji wa YouTube na umaarufu wa mitandaoni.Katika tasnia ya muziki, mafanikio hayaishii kwenye kutoa nyimbo zinazofanya vizuri, kujaza matamasha au kuwa na mamilioni ya wafuasi kwenye mitandao ya kijamii. Kwa wasanii wa kizazi cha sasa, uwezo wa kujenga biashara, kumiliki chapa, kuwekeza na kuanzisha mifumo inayoweza kuendelea kuingiza kipato nje ya muziki ni sehemu muhimu ya kupima mafanikio.

Katika eneo hilo, Nandy, anayefahamika pia kama The African Princess, ana safari inayostahili kuangaliwa kwa jicho tofauti.

Kwa zaidi ya miaka 10 tangu aanze kujijengea jina katika muziki, Nandy ameendelea kupanua wigo wa shughuli zake kutoka kuwa mwimbaji hadi kuwa mjasiriamali, mmiliki wa lebo na mwandaaji wa matamasha.

Hata hivyo, hilo halimaanishi kuwa Zuchu hana mafanikio yake. Msanii huyo naye amejijengea jina kubwa ndani na nje ya Tanzania, akitumia muziki na ushirikiano wa kibiashara kujenga chapa yake.

SAFARI ZAO ILIVYOANZA

Nandy na Zuchu wana historia inayogusana tangu waliposhiriki mashindano ya TECNO Own The Stage mwaka 2015 nchini Nigeria.

Nandy alifanikiwa kushika nafasi ya pili katika mashindano hayo, hatua iliyomfungulia milango ya kujenga jina lake katika muziki wa Afrika Mashariki. Mwaka 2016 aliingia rasmi kwenye soko la muziki kupitia wimbo wake Nagusagusa.

Kwa upande wa Zuchu, jina lake lilipata umaarufu mkubwa zaidi mwaka 2020 baada ya kusainiwa na lebo ya WCB Wasafi inayomilikiwa na Diamond Platnumz. Alitambulishwa rasmi sokoni kupitia EP yake ya I Am Zuchu, iliyokuwa mwanzo wa safari yake kubwa katika muziki.

Tofauti ya mazingira hayo ya kazi imekuwa sehemu muhimu ya mjadala kuhusu safari zao, hasa katika suala la umiliki na uendeshaji wa biashara ya muziki.

NANDY NA UMILIKI WA LEBO YAKE

Moja ya hatua kubwa katika safari ya Nandy ni kuanzisha lebo yake ya muziki, The African Princess Label, mwaka 2023.

Kupitia lebo hiyo, Nandy alijitanua kutoka kuwa msanii anayefanya muziki wake pekee hadi kuwa mtu anayeshiriki katika kukuza na kusimamia vipaji vya wasanii wengine.

Miongoni mwa wasanii walioingia kwenye mfumo huo ni Yammi, ambaye alianza safari yake kupitia EP ya Three Hearts.

Hatua hii inampa Nandy nafasi mbili ndani ya tasnia: kuwa msanii anayezalisha kazi zake na wakati huohuo kuwa mmiliki wa biashara inayoweza kuwekeza katika vipaji vingine.

Kwa upande wa Zuchu, yeye ni msanii aliyesainiwa chini ya WCB Wasafi. Hivyo, tofauti inayoweza kuonekana hapa ni kwamba Nandy ameanzisha na kuendesha lebo yake, wakati Zuchu anafanya kazi ndani ya mfumo wa lebo ambayo hakumiliki.

Ni tofauti ya kimuundo inayopaswa kuzingatiwa wakati wa kuchambua safari zao, bila kupuuza mafanikio ambayo kila mmoja ameyapata katika mazingira yake.

MITANDAO YA KIJAMII: NANDY ANAONGOZA INSTAGRAM, ZUCHU TIKTOK NA YOUTUBE

Katika zama ambazo mitandao ya kijamii imekuwa sehemu muhimu ya biashara ya muziki, idadi ya wafuasi inaweza kuonyesha ukubwa wa ushawishi wa msanii katika jukwaa husika.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotajwa za Chartmetric za Novemba 2026, Nandy alikuwa na takribani wafuasi milioni 10.7 Instagram, huku Zuchu akiwa na milioni 7.6.

Hata hivyo, hali ni tofauti katika majukwaa mengine.

Zuchu anaongoza TikTok akiwa na takribani wafuasi milioni saba, dhidi ya milioni 2.7 wa Nandy.

Katika YouTube, Zuchu naye anaongoza kwa kuwa na subscribers takribani milioni tano, wakati Nandy akiwa na milioni 1.9.

Takwimu hizi zinaonyesha kuwa kila msanii ana eneo ambalo amejijengea nguvu zaidi. Nandy ana ushawishi mkubwa Instagram, huku Zuchu akiwa na ukubwa mkubwa zaidi TikTok na YouTube.

ALBAMU NA KAZI ZILIZOJENGA MAJINA YAO

Nandy amekuwa na safari ndefu katika utoaji wa kazi za muziki. Mwaka 2018 alitoa albamu yake ya The African Princess, iliyosaidia kuimarisha utambulisho wake katika soko la muziki.

Baadaye aliendelea kutoa EP mbalimbali zikiwemo Taste, Maturity na Wanibariki, huku akiendelea kujenga chapa yake kupitia jina la The African Princess.

Kwa upande wa Zuchu, EP yake ya I Am Zuchu ya mwaka 2020 ilikuwa hatua muhimu katika kumtambulisha rasmi kwa mashabiki. Kupitia kazi hiyo na nyimbo zilizofuata, aliweza kujenga nafasi yake katika muziki wa Tanzania na Afrika Mashariki.

Tofauti kubwa hapa ni namna kila mmoja alivyojenga chapa yake. Nandy ameifanya The African Princess kuwa sehemu ya utambulisho wake wa kisanii na kibiashara, huku Zuchu akijijengea jina lake ndani ya mfumo wa WCB Wasafi.

YOUTUBE: ZUCHU ANA NGUVU KUBWA YA WATAZAMAJI

Licha ya Nandy kuwa na mafanikio katika umiliki wa lebo na biashara, Zuchu ana takwimu kubwa zaidi katika upande wa watazamaji wa YouTube.

Kwa mujibu wa takwimu zilizoripotiwa Novemba 2025, Zuchu alikuwa amefikisha zaidi ya watazamaji bilioni moja katika video zake, wakati Nandy akiwa na zaidi ya milioni 306.

Takwimu zilizotajwa za Novemba 2026 zinaonyesha Zuchu akiwa amefikisha zaidi ya watazamaji bilioni 1.3 kwenye chaneli yake, huku Nandy akiwa na zaidi ya milioni 375.

Hizi ni takwimu zinazoonyesha ukubwa wa matumizi ya kazi za Zuchu kwenye jukwaa hilo la kidijitali.

Kwa upande wa biashara ya muziki, watazamaji wengi wanaweza kuongeza thamani ya chapa ya msanii kupitia matangazo, usambazaji wa kazi na fursa mbalimbali za kibiashara.

Hivyo, mafanikio ya Zuchu kwenye YouTube ni sehemu muhimu ya mjadala huu na hayawezi kupuuzwa.

NANDY: MUZIKI KAMA CHANZO CHA KUJENGA BIASHARA

Moja ya mambo yanayovutia katika safari ya Nandy ni namna ambavyo amejaribu kupanua shughuli zake nje ya muziki.

Mbali na The African Princess Label, amekuwa akihusishwa na biashara ya vipodozi kupitia chapa ya Shushi Products.

Pia amehusishwa na biashara ya malazi kupitia Naya Villa, inayotangaza huduma za nyumba za kifahari za kupangisha kwa muda mfupi.

Hizi ni shughuli zinazoonyesha namna wasanii wanavyoweza kutumia umaarufu wao kujenga biashara katika sekta nyingine.

Nandy pia ameendesha tamasha lake la Nandy Festival, ambalo limekuwa jukwaa la kukutanisha wasanii, burudani na kukuza vipaji mbalimbali.

Kwa hatua hiyo, ameongeza nafasi yake ndani ya tasnia kutoka kuwa mtu anayehusika na utengenezaji wa muziki hadi kuwa sehemu ya uandaaji wa majukwaa ya burudani.

MAGARI NA MALI ZA NANDY

Katika upande wa mali binafsi, Nandy amewahi kuhusishwa na umiliki wa magari mbalimbali ya kifahari.

Taarifa zilizochapishwa na Global Publishers mwaka 2019 na 2021 zilimtaja kuwa na magari yakiwemo Range Rover Evoque, Land Rover Discovery, BMW X1, Mercedes-Benz E-Class, Toyota Alphard, Toyota Harrier na Toyota Noah.

Hata hivyo, taarifa hizo ni za miaka iliyopita na hazithibitishi kuwa magari yote hayo bado yako chini ya umiliki wake.

Pia Nandy aliwahi kuripotiwa kuwazawadia wazazi wake nyumba, hatua iliyotajwa kuwa sehemu ya mafanikio yake na namna alivyotumia matunda ya kazi yake kuwasaidia watu wa karibu.

Ni muhimu kutofautisha taarifa za mali zilizowahi kuripotiwa na thamani halisi ya utajiri wa mtu, ambayo inahitaji nyaraka na taarifa za kifedha zilizothibitishwa.

ZUCHU NAYE ANAVYOJENGA MAISHA NJE YA MUZIKI

Kwa upande wa Zuchu, mafanikio yake hayaishii kwenye muziki pekee. Tangu alipoingia rasmi kwenye soko mwaka 2020, ameendelea kujijengea thamani kupitia kazi za muziki na mikataba ya kibiashara.

Mwaka 2021, gazeti la The Citizen liliripoti kuwa Zuchu alikuwa amekataa mkataba wa matangazo ya pombe uliokuwa na thamani ya Sh milioni 250.

Pia amekuwa akihusishwa na ushirikiano wa kibiashara na chapa mbalimbali, zikiwemo Darling Hair na Tridea Cosmetics.

Katika upande wa magari, Zuchu aliwahi kujinunulia Range Rover mwaka 2023. Aidha, taarifa za Mwanaspoti za mwaka 2022 zilieleza kuwa alikuwa amefanikiwa kumiliki magari matano, yakiwemo mawili aliyoyatoa zawadi kwa mama yake na meneja wake.

Novemba 2026, Zuchu alitangaza kujinunulia Bentley Continental GT V8 Azure, akieleza kuwa gari hilo lilikuwa ndoto yake ya muda mrefu na mafanikio yaliyotokana na muziki.

Pia mwaka 2025 alionyesha nyumba ya vyumba vitano aliyokuwa akiijenga kwa ajili ya mama yake, Khadija Kopa, ikiwa ni sehemu ya kutimiza ndoto yake ya kumzawadia mzazi wake makazi bora.

Taarifa nyingine za mwaka 2026 zimemhusisha na uwekezaji wa vyumba viwili vya kifahari Zanzibar, ingawa umiliki na thamani ya uwekezaji huo vinahitaji uthibitisho wa ziada.

Mafanikio hayo yanaonyesha namna Zuchu naye anavyotumia muziki na chapa yake kujenga maisha na kupanua vyanzo vya mapato.

NANDY NA ZUCHU: NANI ANAPASWA KUHESHIMIWA ZAIDI?

Kwa kuangalia safari zao, ni wazi kuwa Nandy na Zuchu wana mafanikio katika maeneo tofauti.

Nandy ana historia ndefu zaidi katika muziki, ameanzisha lebo yake, amejihusisha na biashara ya vipodozi na malazi, ameandaa tamasha lake na kuendelea kujenga chapa ya The African Princess.

Kwa upande mwingine, Zuchu ana mafanikio makubwa katika YouTube na TikTok, amejenga ushawishi mkubwa wa kidijitali, amefanya mikataba ya kibiashara na kuonyesha mafanikio yake kupitia ununuzi wa mali mbalimbali.

Hata hivyo, kuna jambo moja ambalo mara nyingi husahaulika katika mijadala ya aina hii: si kila msanii ana safari inayofanana na ya mwingine.

Nandy amekuwa akijenga mfumo wake wa biashara na lebo yake, wakati Zuchu amefanya safari yake kubwa ndani ya mfumo wa WCB Wasafi, ambao umekuwa na mchango katika kukuza kazi zake.

Hiyo haimaanishi kuwa mafanikio ya mmoja yanapaswa kupunguza thamani ya mwingine.

Lakini pia, kumlinganisha Nandy na Zuchu kwa kuangalia followers, views au umaarufu pekee ni kuacha nje sehemu muhimu ya safari ya Nandy, hususan katika umiliki wa biashara na kujenga mifumo ya kukuza vipaji vingine.

Kwa kweli, mafanikio ya msanii hayapaswi kupimwa kwa idadi ya magari, nyumba au watazamaji pekee. Yanapaswa pia kuangaliwa kwa uwezo wa kujenga chapa, kumiliki biashara, kuwekeza, kutengeneza ajira na kuacha mfumo utakaoweza kuendelea kufanya kazi hata pale msanii anapokuwa hayupo jukwaani.

MAISHA YA MAPENZI: NANDY NA BILLNASS, ZUCHU NA DIAMOND

Mbali na mafanikio ya muziki na biashara, maisha yao binafsi pia yamekuwa sehemu ya mijadala ya mashabiki.

Nandy yupo kwenye ndoa na msanii mwenzake, Billnass, ambaye pia ni sehemu ya tasnia ya muziki. Muunganiko wao umekuwa ukivutia kutokana na namna wanavyounganisha maisha ya familia na shughuli zao za kisanii na kibiashara.

Kwa upande wa Zuchu, amekuwa akihusishwa kimapenzi na Diamond Platnumz, ambaye ni mmiliki wa WCB Wasafi, lebo anayoifanyia kazi. Uhusiano wao umekuwa ukivuta hisia za mashabiki na kuendelea kuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, maisha ya mapenzi ya wasanii hayapaswi kuwa kipimo pekee cha mafanikio yao. Kilicho muhimu zaidi ni kutambua kazi, juhudi, uwekezaji na mchango ambao kila mmoja ameutoa katika tasnia ya burudani.

Kwa hiyo, kumlinganisha Nandy na Zuchu si tatizo lenyewe, lakini kumhukumu Nandy kwa vigezo vya umaarufu wa mitandaoni pekee ni kupuuza sehemu kubwa ya safari yake. Nandy ana historia yake, uwekezaji wake na mfumo wake alioujenga kwa miaka mingi. Zuchu naye ana mafanikio yake yanayostahili kutambuliwa.

Mwisho wa siku, muziki si mashindano ya nani ana followers wengi, bali pia ni uwezo wa kutumia kipaji kujenga biashara, kuwekeza na kuacha alama ndani ya tasnia.