Rais Samia Apiga Kura Uchaguzi Mdogo Wa Ubunge Chamwino

Global Publishers
November 4, 2026
18 views
0 Comments

 Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipiga kura kwenye Kituo cha kupigia kura cha Ofisi ya Kijiji cha Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 04 Novemba, 2026 katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Chamwino. Uchaguzi huo unafanyika kufuatia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Deogratius Ndejembi kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepiga kura katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Chamwino, uliofanyika leo, Novemba 4, 2026, mkoani Dodoma.

Dkt. Samia amepiga kura katika Kituo cha Kupigia Kura cha Ofisi ya Kijiji cha Chamwino, ambako wananchi wa jimbo hilo wanashiriki katika uchaguzi huo kumchagua mwakilishi wao mpya katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uchaguzi huo mdogo umefanyika kufuatia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Dkt. Deogratius Ndejembi, kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na hivyo kuacha nafasi hiyo wazi.

Uchaguzi huo ni sehemu ya mchakato wa kidemokrasia unaowawezesha wananchi wa Chamwino kupata mwakilishi mpya atakayewasilisha na kutetea maslahi yao katika Bunge.

Beno Malisa Amuomba Radhi Rais Samia Baada ya Kutenguliwa – Video

Global Publishers
November 4, 2026
84 views
0 Comments

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Beno Malisa.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Beno Malisa, amemuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akieleza kuwa aliteleza katika utekelezaji wa majukumu yake wakati akihudumu katika nafasi hiyo.

Malisa ametoa kauli hiyo Novemba 3, 2026, wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora iliyofanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Malisa amekiri kuwepo kwa mapungufu katika utekelezaji wa majukumu yake na kumuomba radhi Rais Samia, huku akieleza kuwa amepokea uamuzi wa kumuondoa katika nafasi hiyo kwa heshima.

Malisa alitenguliwa katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Oktoba 28, 2026, na nafasi yake kuchukuliwa na Angelina Mabula, ambaye anatarajiwa kuendelea na majukumu ya kuongoza mkoa huo.

Mbeto: CCM Kitaendelea Kubeba Matumaini ya Watanzania bila Kuyumbishwa

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar,Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis.

Chama Cha Mapinduzi kimewahakikishia Wananchi kuwa kitabaki na umadhubuti wake wa kubeba matumaini ya Wananchi wote bila kujali imani zao za dini,Itikadi za Kisiasa au kabila zao.

Pia chama hicho kimewataka Wananchi kuwa hodari wa kuvipekua Vyama vya Siasa kabla kufikia maamuzi ya kuvifuata , kujiunga navyo na kuviunga mkono .

Maelezo hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar,Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis huku akiwasisitiza Watanzania wote kuendelea kulinda Amani na utulivu wa nchi yao.

Mbeto alisema uzoefu wa CCM katika medani za madaraka, uongozi, kisiasa na kiutawala , ni mkubwa usiolingana na viongozi wa Vyama vingine.

Alisema chama cha Siasa kilichoshika madaraka ya Utawala kwa miaka zaidi ya sitini, bila shaka chama hicho hakifanani kwa lolote na Vyama vichanga vinavyoibuka na kufa kama uyoga nyakati za masika.

“Vyama vingi vitaendelea kuibuka
,kuishi kwa muda ,vitayumba hatimae vitakufa. CCM kwa upeo wa viongozi wake na uzoefu wake kitabaki na uhai wake na kudumu “Alisema Mbeto

Aidha, Katibu huyo Mwenezi,! alieleza ndio maana CCM kinaweza kujadili masuala yake mazito ya kisiasa, kukabiliana na chamgamoto kadhaa za ndani na nje kwa umakini na kufikia kutoa maamuzi magumu.

“Vyama vichanga vyote vya Kisiasa haviwezi kupata ustawi na uwezo wa kuhimili misukosuko . CCM imepitia mengi makubwa lakini hakikutikisika katika kupigania maslahi mapana ya Taifa” Alisema.

Akisisitiza zaidi, Katibu huyo Mwenezi aliendelea kuutaja uzoefu na uwezo mkubwa wa kiutawala na kisiasa, alidai CCM kinapotaka kutoa maamuzi yake ,hutanguliza kwanza utaifa si kitu kingine.

“CCM si chama kinachofuga wanachama mamluki na wasaliti. Ni chama kinachoamini na kufuata Siiasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Hujitegemea kifikra , kimawazo,kiakili na kuamini katika Sera na misimamo yake “Alifafanua Mbeto .

Akizungumza kwa undani, Mbeto alisema CCM hakiwezi kutikiswa kwa namna yoyote na Vyama vilivyoundwa Mwaka 1992 huku vyama hivyo vikidhani vimeshapata mbavu na uwezo wa kuongoza nchi.

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

TNCC YAONYA UTAPELI KUDHOOFISHA BIASHARA KIGOMA NA DRC

Na Fadhili Abdallah, Kigoma

CHEMBA ya Taifa ya biashara  (TNCC) mkoani Kigoma imewataka wafanyabiashara wa mkoa huo kuimarisha uaminifu na uadilifu  katika kufanya biashara na wafanyabiashara wenzao kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ili kukuza uhusiano wa kibiashara baina ya nchi hizo mbili.

Meneja wa TNCC Mkoa wa Kigoma, Prosper Guga, alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma, akieleza kuwepo kwa  malalamiko ya baadhi ya wafanyabiashara kutoka DRC kuhusu kutapeliwa na wenzao wa Kigoma akieleza kuwa yanaweza kuathiri ushirikiano wa kibiashara baina ya nchi hizo.

Alisema ni muhimu wafanyabiashara kuzingatia maadili, uaminifu na kutimiza makubaliano wanayoingia na wenzao  kwa kuwa biashara ya kuvuka mpaka  inategemea zaidi kujenga mahusiano ya muda mrefu na kuaminiana ambapo alisema kuwa TNCC imeingia makubaliano na Chemba ya biashara ya DRC kusaidia kukuza biashara na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa nchi hizo.

Akieleza hali hiyo alisema kuwa TNCC imeanza kulipatia ufumbuzi suala la Mfanyabiashara wa DRC na wenzake waliotapeliwa milioni Zaidi ya 90 mwaka 2024 ambapo katika kulifuatilia jambo hilo tayari mfanyabiashara huyo wa Kigoma ameanza kulipa deni hilo kwa juzi kutoa kiasi cha milioni 20.

Kwa upande wake, mfanyabiashara mmoja kutoka DRC,Anne Shilwalwa Maombi  alisema alikuwa anashirikiana na Mfanyabiashara mmoja waa Kigoma ambaye alikuwa akimletea unga wa ngano kutoka Dar es Salaam kuleta Kigoma na yeye kupeleka DRC ambapo baadaye alimuamini na kumpatia kiasi cha milioni 90 mwaka 2024 kuwa wakala wao lakini mfanyabiashaara huyo  alitumia fedha hizo kwa manufaa yake badala ya kutekeleza makubaliano hali iliyosababisha usumbufu mkubwa na kuyumbisha shughuli zao za biashara.

Maombi alisema kuwa tangu mwaka 2024 amehangaika maeneo mbalimbali ikiwemo polisi lakini hakupata mafanikio hadi mwezi uliopita alipoenda ofisi za TNCC ambapo baada ya kueleza changamoto yake ilifanyiwa kazi na wiki hii amepatiwa kiasi cha shilingi milioni 20 ikiwa sehemu ya fedha alizokuwa ametapeliwa.

Kutokana na hilo Mfanyabiashara huyo  aliishukuru TNCC kwa kuingilia kati na kusimamia suala hilo, akisema kuwa hatua hiyo imeanza kuleta matumaini ya taasisi hiyo katika kusimamia changamoto za wafanyabiashara wa nchi hizo mbili.

Mwisho.

Trump Apata Pigo! Democrat Wachukua Seneti na Bunge la Wawakilishi, Mitaa Yafungwa!

Global Publishers
November 4, 2026
462 views
0 Comments

Chama cha Democrat kimefanikiwa kupata udhibiti wa Seneti na Baraza la Wawakilishi la Marekani, hatua inayokipa chama hicho ushawishi mkubwa katika Bunge la Congress kwa kipindi kilichosalia cha urais wa Donald Trump.

Ushindi huo umetokana na matokeo ya uchaguzi wa katikati ya muhula (Midterm Elections), ambapo Democrat wamefanikiwa kushinda katika majimbo na maeneo mbalimbali yaliyokuwa yakishikiliwa na chama cha Republican.

Miongoni mwa maeneo yaliyotajwa ni majimbo ya Texas, Kansas na Ohio, ambako wagombea wa Democrat wamepata ushindi katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa makadirio ya matokeo yaliyotolewa Democrat inatarajiwa kupata viti 229 katika Bunge la Wawakilishi dhidi ya 164 vya Republican, huku viti 218 vikihitajika ili kupata udhibiti wa chombo hicho cha kutunga sheria.

Katika Seneti, Democrat inatarajiwa kupata viti 54 dhidi ya 43 vya Republican, na hivyo kuvuka idadi ya viti 51 vinavyohitajika kudhibiti chombo hicho. Matokeo hayo yanaonesha Democrat imeongeza viti saba, huku Republican ikipoteza idadi hiyo.

Aidha, katika uchaguzi wa magavana, Democrat imefanikiwa kupata viti 26 na kuongeza viti vinne, huku Republican ikipata viti 19.

Ushindi huo unaashiria mabadiliko makubwa ya nguvu za kisiasa nchini Marekani, huku chama cha Democrat kikitarajiwa kuwa na ushawishi mkubwa katika Bunge la Congress kwa kipindi kilichosalia cha utawala wa Rais Donald Trump.

Wananchama wa Democrat wamefungu mitaa wakiendelea kusherekea ushindi huo.

Trump Apata Pigo! Democrat Wachukua Seneti na Bunge la Wawakilishi

Global Publishers
November 4, 2026
408 views
0 Comments

Chama cha Democrat kimefanikiwa kupata udhibiti wa Seneti na Baraza la Wawakilishi la Marekani, hatua inayokipa chama hicho ushawishi mkubwa katika Bunge la Congress kwa kipindi kilichosalia cha urais wa Donald Trump.

Ushindi huo umetokana na matokeo ya uchaguzi wa katikati ya muhula (Midterm Elections), ambapo Democrat wamefanikiwa kushinda katika majimbo na maeneo mbalimbali yaliyokuwa yakishikiliwa na chama cha Republican.

Miongoni mwa maeneo yaliyotajwa ni majimbo ya Texas, Kansas na Ohio, ambako wagombea wa Democrat wamepata ushindi katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa makadirio ya matokeo yaliyotolewa Democrat inatarajiwa kupata viti 229 katika Bunge la Wawakilishi dhidi ya 164 vya Republican, huku viti 218 vikihitajika ili kupata udhibiti wa chombo hicho cha kutunga sheria.

Katika Seneti, Democrat inatarajiwa kupata viti 54 dhidi ya 43 vya Republican, na hivyo kuvuka idadi ya viti 51 vinavyohitajika kudhibiti chombo hicho. Matokeo hayo yanaonesha Democrat imeongeza viti saba, huku Republican ikipoteza idadi hiyo.

Aidha, katika uchaguzi wa magavana, Democrat imefanikiwa kupata viti 26 na kuongeza viti vinne, huku Republican ikipata viti 19.

Ushindi huo unaashiria mabadiliko makubwa ya nguvu za kisiasa nchini Marekani, huku chama cha Democrat kikitarajiwa kuwa na ushawishi mkubwa katika Bunge la Congress kwa kipindi kilichosalia cha utawala wa Rais Donald Trump.

Wananchama wa Democrat wamefungu mitaa wakiendelea kusherekea ushindi huo.

Democrat Wateka Seneti na Bunge la Wawakilishi, Trump Kupata Upinzani Mkali

Global Publishers
November 4, 2026
42 views
0 Comments

Chama cha Democrat kimefanikiwa kupata udhibiti wa Seneti na Baraza la Wawakilishi la Marekani, hatua inayokipa chama hicho ushawishi mkubwa katika Bunge la Congress kwa kipindi kilichosalia cha urais wa Donald Trump.

Ushindi huo umetokana na matokeo ya uchaguzi wa katikati ya muhula (Midterm Elections), ambapo Democrat wamefanikiwa kushinda katika majimbo na maeneo mbalimbali yaliyokuwa yakishikiliwa na chama cha Republican.

Miongoni mwa maeneo yaliyotajwa ni majimbo ya Texas, Kansas na Ohio, ambako wagombea wa Democrat wamepata ushindi katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi.

Kwa upande wa Seneti, Democrat wamefanikiwa kushinda viti muhimu katika majimbo yaliyokuwa yakiongozwa na Republican, ikiwemo Kansas, Texas, Iowa, Ohio, Maine, North Carolina na South Carolina.

Katika Baraza la Wawakilishi, Democrat pia wamefanikiwa kupata udhibiti wa baraza hilo, hali inayowapa mamlaka ya kusimamia ajenda za Bunge la Congress na kuimarisha uangalizi wa shughuli za utawala wa Rais Donald Trump.

Kwa mujibu wa Associated Press, ushindi huo unatarajiwa kuleta mabadiliko katika uwiano wa kisiasa nchini Marekani katika kipindi cha miaka miwili iliyosalia ya urais wa Trump.

EWURA Yatangaza Bei Mpya za Mafuta, Petroli Dar Yapanda

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli zitakazoanza kutumika kuanzia leo, Jumatano, Novemba 4, 2026, saa 6:01 usiku.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na EWURA, bei za mafuta katika soko la dunia zilipungua kidogo mwezi Oktoba 2026 ikilinganishwa na mwezi Septemba, hata hivyo, bei hizo zimeendelea kuwa juu kutokana na mgogoro unaoendelea Mashariki ya Kati, ambako Tanzania hununua sehemu kubwa ya mafuta yake.

EWURA imeeleza kuwa ongezeko la gharama za usafirishaji na bima, pamoja na gharama za uagizaji wa mafuta, limechangia kuendelea kwa bei hizo kuwa juu.

Katika bei mpya zilizotangazwa, petroli kwa rejareja jijini Dar es Salaam itauzwa kwa Shilingi 4,083 kwa lita, dizeli Shilingi 4,128 na mafuta ya taa Shilingi 4,117.

Kwa upande wa Mkoa wa Tanga, petroli itauzwa kwa Shilingi 4,149 kwa lita, dizeli Shilingi 4,194 na mafuta ya taa Shilingi 4,183.

Mkoani Mtwara, petroli itauzwa kwa Shilingi 4,186 kwa lita, dizeli Shilingi 4,231 na mafuta ya taa Shilingi 4,220.

Aidha, EWURA imetangaza bei za jumla ambapo jijini Dar es Salaam petroli itauzwa kwa Shilingi 3,935.23 kwa lita, dizeli Shilingi 3,979.98 na mafuta ya taa Shilingi 3,969.83.

Mkoani Tanga, bei za jumla ni Shilingi 3,931.19 kwa lita ya petroli na Shilingi 3,974.06 kwa dizeli, huku Mtwara petroli ikiuzwa kwa Shilingi 3,930.70 na dizeli Shilingi 3,972.94 kwa lita.

Katika hatua nyingine, EWURA imeelekeza kuwa bei za rejareja za mafuta katika maeneo mbalimbali nchini zizingatie viwango vilivyoainishwa kwenye jedwali namba tatu la taarifa hiyo, huku wafanyabiashara wanaouza mafuta kwa jumla wakitakiwa kuzingatia bei zilizoainishwa kwenye jedwali namba mbili.

Mamlaka hiyo imesisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wafanyabiashara watakaobainika kukiuka agizo hilo.

PDPC YAZIDI KUIMARISHA USALAMA WA TAARIFA BINAFSI, KUJENGA MAZINGIRA RAFIKI YA BIASHARA NA UWEKEZAJI

 Katika uchumi wa kidijitali, taarifa binafsi zimekuwa rasilimali muhimu kwa shughuli za biashara, uwekezaji na utoaji wa huduma. Hata hivyo, thamani yake haiwezi kutenganishwa na wajibu wa kulinda faragha na haki za wananchi. Ulinzi wa taarifa binafsi hujenga uaminifu katika matumizi ya teknolojia, hupunguza hatari za matumizi mabaya ya taarifa na kuchangia mazingira yanayofaa kwa biashara na uwekezaji.

Kutokana na umuhimu huo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, iliridhia Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Sura ya 44 (PDPA), iliyotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2022 na kuwezesha kuanzishwa kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) tarehe 1 Mei, 2023. Hatua hizi zimeweka msingi wa kisheria na kitaasisi wa kusimamia ukusanyaji, uchakataji, uhifadhi na matumizi ya taarifa binafsi katika sekta za umma na binafsi.

Akizindua rasmi PDPC tarehe 3 Aprili 2024, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alisisitiza kuwa faragha ni sehemu ya utu na staha ya mwanadamu. Aidha, alielekeza taasisi zote zinazokusanya na kuchakata taarifa binafsi kujisajili na kuzingatia sheria. Maelekezo hayo yalielekeza msisitizo si kwenye teknolojia pekee, bali pia kwenye uwajibikaji wa taasisi na haki za wananchi katika mazingira ya kidijitali.

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeendelea kusimamia utekelezaji wa sera na sheria katika eneo hili. Akifunga mafunzo ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi (DPOs) jijini Arusha tarehe 5 Januari 2026, Waziri mwenye dhamana ya Wizara hiyo, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb), alisisitiza umuhimu wa taasisi kujisajili PDPC na kuweka mifumo salama ya usimamizi wa taarifa. 

Kwa upande wa utekelezaji, PDPC chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mkuu Dkt. Emmanuel Lameck Mkilia, imeendelea kutoa elimu, kusajili wadhibiti na wachakataji wa taarifa binafsi, kushughulikia malalamiko na kusimamia uzingatiaji wa sheria. Akizungumza kwenye mafunzo ya DPOs jijini Mbeya tarehe 11 Februari 2026, Dkt. Mkilia alionya kuwa ukiukaji wa misingi ya ukusanyaji na uchakataji wa taarifa unahatarisha faragha, usalama na haki za wananchi. Tume pia ilitangaza kuanza kwa ukaguzi wa lazima tarehe 28 Agosti 2026 ili kuimarisha uzingatiaji wa matakwa ya sheria.

Hadi kufikia Oktoba 2026, zaidi ya taasisi 15,000 zilikuwa zimesajiliwa; malalamiko zaidi ya 445 yalikuwa yamepokelewa na kushughulikiwa; na vibali 121 vya usafirishaji wa taarifa binafsi nje ya Tanzania vilikuwa vimetolewa. Hatua hizi zinaonyesha kuimarika kwa taratibu za usimamizi, uwajibikaji na ufuatiliaji wa uchakataji wa taarifa binafsi nchini.

Uhusiano kati ya ulinzi wa taarifa binafsi na uwekezaji unatokana na hitaji la wawekezaji kuwa na uhakika wa usalama wa taarifa, uzingatiaji wa masharti ya kisheria na uwezo wa taasisi kulinda haki za wateja. Uwepo wa mfumo wa kisheria wa ulinzi wa taarifa unaweza kuongeza imani ya biashara zinazotegemea huduma za kidijitali na kubadilishana taarifa ndani na nje ya nchi. Hivyo, utekelezaji wa PDPA ni sehemu ya mazingira mapana yanayowezesha biashara, ingawa si sababu pekee inayoamua kiwango cha uwekezaji.

Kwa mujibu wa taarifa ya mwenendo wa uwekezaji nchini kwa mwaka 2021–2025 iliyotolewa na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi (TISEZA) tarehe 7 Januari 2026, miradi iliyosajiliwa iliongezeka kutoka 252 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 3.7 mwaka 2021 hadi miradi 915 yenye thamani ya dola bilioni 10.95 mwaka 2025. Mwaka 2024, thamani ya uwekezaji iliyotajwa ilifikia dola bilioni 9.3. Takwimu hizi zinaonyesha ukuaji wa uwekezaji katika kipindi ambacho Tanzania pia iliimarisha mifumo yake ya kidijitali na kisheria, ikiwemo ulinzi wa taarifa binafsi.

Ili manufaa ya mfumo huu yaendelee kuonekana, taasisi zinapaswa kujisajili inapohitajika, kuweka hatua za kiufundi na kiutawala za kulinda taarifa, kutoa taarifa kwa uwazi kuhusu matumizi ya taarifa na kushughulikia haki na malalamiko ya wananchi. Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi wana nafasi muhimu katika kuratibu uzingatiaji wa sheria, kutoa ushauri kwa menejimenti na kufuatilia mienendo ya uchakataji wa taarifa ndani ya taasisi.

Wananchi nao wanapaswa kufahamu haki zao na kuwa waangalifu wanapotoa taarifa binafsi, hususani kupitia huduma za mtandaoni. Kwa kushirikiana na wadau, PDPC itaendelea kuimarisha elimu kwa umma, ukaguzi, usimamizi wa malalamiko na ufuatiliaji wa utekelezaji wa sheria. Hatua hizi ni muhimu katika kujenga uchumi wa kidijitali unaoaminika, unaolinda utu na faragha ya mwananchi na kusaidia Tanzania kuwa na mazingira salama na yanayotabirika kwa uwekezaji.

Ronaldo, Messi Waongoza Orodha ya Wanamichezo Matajiri Zaidi Duniani

Global Publishers
November 4, 2026
1,176 views
0 Comments

Mwanasoka wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo, ameendelea kutawala ulimwengu wa michezo kwa upande wa mapato, akiongoza orodha ya wanamichezo wanaoingiza fedha nyingi zaidi duniani kwa mwaka 2026, kwa mujibu wa jarida la Forbes.

Ronaldo, anayeichezea klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia, anakadiriwa kuingiza takribani Shilingi bilioni 793.5 za Tanzania kwa mwaka, kupitia mshahara wake wa soka, mikataba ya matangazo, udhamini na shughuli mbalimbali za kibiashara.

Katika nafasi ya pili yupo bondia wa Mexico, Canelo Álvarez, anayekadiriwa kuingiza Shilingi bilioni 449.7 kwa mwaka, huku mwanasoka Lionel Messi wa Inter Miami akishika nafasi ya tatu kwa mapato ya takribani Shilingi bilioni 370.3.

Nyota wa mpira wa kikapu wa Marekani, LeBron James, anashika nafasi ya nne akiwa na mapato ya Shilingi bilioni 364.5, akifuatiwa na mchezaji wa baseball wa Japan, Shohei Ohtani, anayekadiriwa kuingiza Shilingi bilioni 337.5 kwa mwaka.

ORODHA YA WANAMICHEZO 10 WANAOINGIZA FEDHA NYINGI ZAIDI DUNIANI

  1. Cristiano Ronaldo (Soka) – Shilingi bilioni 793.5.
  2. Canelo Álvarez (Ndondi) – Shilingi bilioni 449.7.
  3. Lionel Messi (Soka) – Shilingi bilioni 370.3.
  4. LeBron James (Mpira wa Kikapu) – Shilingi bilioni 364.5.
  5. Shohei Ohtani (Baseball) – Shilingi bilioni 337.5.
  6. Stephen Curry (Mpira wa Kikapu) – Shilingi bilioni 329.8.
  7. Jon Rahm (Gofu) – Shilingi bilioni 283.0.
  8. Karim Benzema (Soka) – Shilingi bilioni 275.1.
  9. Kevin Durant (Mpira wa Kikapu) – Shilingi bilioni 274.6.
  10. Lewis Hamilton (Formula 1) – Shilingi bilioni 264.5.

Kwa ujumla, orodha hiyo inaonesha namna sekta ya michezo inavyoendelea kuwa moja ya maeneo yenye mzunguko mkubwa wa fedha duniani, huku wanamichezo wakinufaika si tu na mishahara na zawadi za mashindano, bali pia mikataba ya matangazo, udhamini na uwekezaji wa kibiashara.