Global Publishers
November 4, 2026
42 views
0 Comments

Chama cha Democrat kimefanikiwa kupata udhibiti wa Seneti na Baraza la Wawakilishi la Marekani, hatua inayokipa chama hicho ushawishi mkubwa katika Bunge la Congress kwa kipindi kilichosalia cha urais wa Donald Trump.
Ushindi huo umetokana na matokeo ya uchaguzi wa katikati ya muhula (Midterm Elections), ambapo Democrat wamefanikiwa kushinda katika majimbo na maeneo mbalimbali yaliyokuwa yakishikiliwa na chama cha Republican.
Miongoni mwa maeneo yaliyotajwa ni majimbo ya Texas, Kansas na Ohio, ambako wagombea wa Democrat wamepata ushindi katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi.

Kwa upande wa Seneti, Democrat wamefanikiwa kushinda viti muhimu katika majimbo yaliyokuwa yakiongozwa na Republican, ikiwemo Kansas, Texas, Iowa, Ohio, Maine, North Carolina na South Carolina.
Katika Baraza la Wawakilishi, Democrat pia wamefanikiwa kupata udhibiti wa baraza hilo, hali inayowapa mamlaka ya kusimamia ajenda za Bunge la Congress na kuimarisha uangalizi wa shughuli za utawala wa Rais Donald Trump.
Kwa mujibu wa Associated Press, ushindi huo unatarajiwa kuleta mabadiliko katika uwiano wa kisiasa nchini Marekani katika kipindi cha miaka miwili iliyosalia ya urais wa Trump.
