Halmashauri ya Chunya Yatangaza Nafasi 14 za Ajira, Mwisho wa Maombi Sept 13, 2026

Chunya, Mbeya — Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ametangaza nafasi 14 za ajira kwa Watanzania wenye sifa, katika kada za Udereva na Uandishi wa Ofisi.

Tangazo hilo lenye Kumb. Na. CDS/S.10/39 VOL IV/22, la tarehe 31 Agosti 2026, limetolewa baada ya Halmashauri kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Nafasi zilizotangazwa

Halmashauri imetangaza nafasi zifuatazo:

  • Dereva Daraja la II — nafasi 9
  • Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II — nafasi 5

Dereva Daraja la II — nafasi 9

Waombaji wa nafasi hii watakuwa na jukumu la kukagua magari kabla na baada ya safari, kuwapeleka watumishi katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya safari za kikazi, kufanya matengenezo madogo ya magari na kutunza daftari la safari (log book).

Majukumu mengine ni kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali, kufanya usafi wa gari pamoja na kutekeleza majukumu mengine watakayopewa na wasimamizi wao.

Sifa za mwombaji

Mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) pamoja na leseni ya udereva ya Daraja E au C, ambayo ameitumia kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.

Pia anatakiwa kuwa na vyeti vya mafunzo vilivyomuwezesha kupata daraja husika la leseni na awe amehudhuria Basic Driving Course inayotolewa na VETA au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

Mshahara: TGS B

Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II — nafasi 5

Majukumu ya nafasi hii ni pamoja na kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri; kupokea wageni na kuwaelekeza sehemu wanakoweza kupata msaada; kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, vikao na safari za mkuu wake.

Mwandishi pia atahusika na kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika, kupokea na kusambaza majalada kwa maofisa husika, kukusanya na kuyatunza majalada, kupanga dondoo za vikao na kuandaa mahitaji ya ofisi.

Sifa za mwombaji

Mwombaji anatakiwa kuwa na elimu ya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita, pamoja na Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Aidha, anatakiwa kuwa amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza kwa maneno 100 kwa dakika moja, pamoja na kuwa na mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email na Publisher.

Mshahara: TGS C

Masharti muhimu ya waombaji

Waombaji wote wanapaswa kuwa raia wa Tanzania, wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 45.

Waombaji wanatakiwa kuambatanisha Curriculum Vitae (CV) yenye maelezo kamili, anuani inayotumika, namba za simu, barua pepe pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wanaoaminika.

Vyeti vya elimu na taaluma vinapaswa kuwa vimehakikiwa na kuthibitishwa na Mwanasheria/Wakili kwa mujibu wa masharti ya tangazo.

Halmashauri imesisitiza kuwa testimonial, provisional result, statement of result pamoja na Form IV na Form VI result slips havitakubaliwa.

Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanapaswa kuhakikisha vyeti vyao vinatambuliwa na mamlaka husika, ikiwemo TCU, NECTA na NACTE.

Aidha, waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa wawe na kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Jinsi ya kutuma maombi

Maombi yote yanatakiwa kutumwa kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal).

Recruitment Portal: portal.ajira.go.tz

Barua ya maombi inapaswa kusainiwa na kuelekezwa kwa:

Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Chunya,
S.L.P 73,
Chunya.

Mwisho wa kutuma maombi

Mwisho wa kutuma maombi ni Septemba 13, 2026.

Halmashauri imeonya kuwa maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu uliowekwa katika tangazo hayatazingatiwa, huku utoaji wa taarifa au sifa za kughushi ukisababisha wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.

Tangazo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji (W) wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.

SEO title: Halmashauri ya Chunya yatangaza nafasi 14 za ajira

Meta description: Halmashauri ya Wilaya ya Chunya imetangaza nafasi 14 za ajira kwa Dereva Daraja la II na Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II. Mwisho wa maombi ni Septemba 13, 2026.

Wezesha Mzawa Insurance Broker Watangaza Nafasi Nne za Kazi

Kampuni ya Wezesha Mzawa Insurance Broker Limited imetangaza nafasi za kazi kwa Watanzania wenye sifa na uzoefu katika sekta ya bima, mauzo, masoko, biashara, uhasibu na nyanja zinazohusiana.

Nafasi zilizotangazwa ni Business Development Executive, Accountant pamoja na Insurance Sales Executives, huku waombaji wakitakiwa kutimiza vigezo vilivyowekwa kwa kila nafasi.

1. Business Development Executive

Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Kwanza katika Insurance and Risk Management, Sales and Marketing, Business Administration au fani nyingine inayohusiana, pamoja na uzoefu wa angalau miaka miwili katika sekta ya bima, maendeleo ya biashara, mauzo au masoko.

2. Accountant

Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Kwanza katika Accounting au Finance, pamoja na uzoefu wa angalau miaka miwili katika sekta ya bima. Sifa ya CPA ni nyongeza.

3. Insurance Sales Executives

Waombaji wanatakiwa kuwa na Cheti katika Insurance and Risk Management, Sales, Marketing, Business Administration au fani nyingine inayohusiana.

Uzoefu katika sekta ya bima na kazi za mauzo ni nyongeza.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi yao pamoja na viambatisho muhimu vilivyothibitishwa kupitia barua pepe au kwa anuani ya ofisi ya kampuni kabla ya Septemba 30, 2026.

Wezesha Mzawa Insurance Broker Limited
P.O. Box 7534, Sinza Mori
Global Group House/Building, Opposite Wanyama Hotel
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: [email protected]

Watoto wa Wakulima, Wafugaji Kupewa Nafasi Kwenye Ufadhili wa Masomo Algeria

Serikali imeeleza kuwa inalenga kupanua wigo wa fursa za elimu ya juu kwa Watanzania, ikiwemo kuhakikisha wanafunzi kutoka familia za wakulima na wafugaji wanapata nafasi ya kusoma nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Septemba 11, 2026, akieleza kuhusu fursa mpya za masomo zilizopatikana nchini Algeria.

Kwa mujibu wa Prof. Mkenda, Tanzania imepata nafasi 150 za ufadhili wa masomo nchini Algeria kwa wanafunzi waliofanya vizuri. Serikali ya Algeria itagharamia ada za masomo, huku Serikali ya Tanzania ikigharamia fedha za kujikimu kwa wanafunzi hao kupitia utaratibu wa Samia Scholarship.

Waziri amesema fursa hizo ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa na Serikali kuongeza idadi ya Watanzania wanaopata nafasi za elimu ya juu katika vyuo vya nje ya nchi.

Ameeleza pia kuwa, kati ya wanafunzi 1,000 waliotangazwa kupata Samia Scholarship, tayari wanafunzi 10 wamechaguliwa kwenda kusoma Moscow, nchini Urusi.

Prof. Mkenda amesema majina ya wanafunzi 150 watakaopata nafasi za kwenda kusoma Algeria yatachapishwa kwenye tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, pamoja na maelekezo kuhusu uwasilishaji wa nyaraka na taratibu nyingine zinazohitajika kabla ya safari.

Ameongeza kuwa Serikali inataka fursa hizo zisibaki kwa kundi moja pekee, bali zinufaishe wanafunzi kutoka mazingira na makundi mbalimbali ya jamii, wakiwemo watoto wa wakulima na wafugaji.

Kwa upande mwingine, wanafunzi watakaofanikiwa kupata nafasi hizo wametakiwa kujiandaa kujifunza lugha ya Kifaransa, kwa kuwa lugha hiyo hutumika katika sehemu kubwa ya masomo nchini Algeria.

Hatua hiyo inaongeza wigo wa fursa za elimu ya juu nje ya nchi zinazopatikana kwa wanafunzi wa Kitanzania kupitia mipango ya Serikali ya ufadhili wa masomo.

Harmonize Amtembelea Rais Samia Kizimkazi Kutoa Baada ya Kufiwa na Mumewe – Picha

Global Publishers
September 12, 2026
0 views
0 Comments

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’, amemfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba wa mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.

Harmonize alifika nyumbani kwa Rais Samia, Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, Septemba 11, 2026, baada ya Rais kuwasili nyumbani kwake kufuatia msiba huo.

Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Septemba 7, 2026, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar.

Katika ziara hiyo, Harmonize alitoa pole na faraja kwa Rais Samia pamoja na familia katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

Sevilla Kuikabili Valencia, Nani Kuibuka na Ushindi?

Klabu ya Sevilla itakuwa mwenyeji wa Valencia katika mchezo wa raundi ya tano ya LALIGA msimu wa 2026/27, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Ramón Sánchez-Pizjuán. Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 22:00 jioni.

Sevilla inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na pointi saba baada ya kucheza michezo minne, ikiwa imeshinda michezo miwili, sare moja na kupoteza mmoja. Timu hiyo ilianza msimu kwa ushindi dhidi ya Rayo Vallecano na Athletic Bilbao, kabla ya kufungwa na Atletico Madrid na kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Espanyol.

Kwa upande wa Valencia, hali ni tofauti baada ya kuanza msimu kwa kusuasua. Wakiwa na pointi moja pekee, Valencia wako nafasi ya mwisho baada ya sare moja na vipigo vitatu, huku wakifunga bao moja tu na kuruhusu mabao tisa. Kipigo cha mwisho cha 5-0 dhidi ya Barcelona kimeongeza presha kwa kocha Carlos Corberán.

Kocha Corberán mwenyewe alikiri hali hiyo baada ya mechi, akisema kwamba dhidi ya timu kubwa kama Barcelona, kila kitu lazima kiende sawasawa ili kupata matokeo mazuri, jambo ambalo halikutokea kwao siku hiyo.

Kwa sasa Valencia wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa hawana ushindi katika mechi michezo minne, huku baadhi ya ripoti zikieleza kuwa wana changamoto kubwa ya majeruhi kambini kwao.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Sevilla pia itakosa baadhi ya wachezaji muhimu. Arouna Sangante hatacheza kutokana na kadi nyekundu aliyopata dhidi ya Espanyol, huku Rubén Vargas akiwa nje kutokana na majeraha. Valencia nayo ina changamoto kubwa za majeraha, akiwemo Mouctar Diakhaby, ambaye ameongezeka kwenye orodha ya wachezaji wanaokosekana.

Kwa ujumla, mchezo huu unatarajiwa kuwa muhimu kwa kila timu. Sevilla itatafuta pointi tatu mbele ya mashabiki wake ili kuendelea kupanda kwenye msimamo, wakati Valencia itahitaji matokeo mazuri ili kuondokana na mwanzo mbaya wa msimu. Historia ya hivi karibuni inaibeba Valencia matumaini, kwani Sevilla haijaifunga katika mechi sita zilizopita kati yao.

Kisa cha Kushangaza! Siku ya Harusi, Ukweli wa Wazazi Wake Wafichuka – Video

Global Publishers
September 11, 2026
6 views
0 Comments


Siku ya harusi yake, aliamini wazazi wake ni maskini na walikuwa wakimwaibisha mbele ya watu.

Lakini hakujua kuwa ukweli ulikuwa tofauti kabisa — wazazi wake walikuwa miongoni mwa wanandoa matajiri zaidi duniani! 

Kumbe, kwa miaka yote walikuwa wakimjaribu ili kujua tabia yake halisi. Cha kushangaza zaidi, yeye alikuwa amejifanya kutowajua wazazi wake kwa muda wote huo.

Sasa siri imefichuka!

Je, nini kitatokea kwa mke wake kutoka familia ya kitajiri? Na ndoa yao itaishia wapi baada ya ukweli huu kujulikana?

 

*MAKAMU WA RAIS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO*

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameagiza Mamlaka na Taasisi zinazohusika kuchukua hatua za haraka kujiandaa ili kuzuia na kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño zinazotarajiwa kuanza mwezi Oktoba 2026.

 

Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo, mara baada ya kupokea taarifa ya utayari na maandalizi ya Serikali kufuatia tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kuhusu mvua za El- nino, katika kikao kilichofanyika Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza na Viongozi pamoja na timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Wizara ya Ujenzi pamoja na Taasisi zilizochini ya Wizara hizo, Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa taasisi zote zinazohusika, kufanya kazi kwa pamoja na kuchukua hatua za tahadhari mapema ili kuzuia au kupunguza athari zinazoweza kutokea kwa wananchi kufuatia ujio wa mvua hizo.

 

Pia amesisitiza umuhimu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kushirikishwa katika maandalizi hayo ili kuwa na nguvu kazi ya kutosha pamoja na kuimarisha uwezo wa Serikali wa kuzuia, kupunguza na kukabiliana kwa haraka na athari zinazoweza kujitokeza.

 

“Ifanyike kampeni ya haraka, mikondo na mifereji ya maji izibuliwe, na barabara ziandaliwe,” amesisitiza Makamu wa Rais.

 

Aidha, ameelekeza taka, tope na udongo unaotolewa baada ya kuzibua mitaro na mifereji katika maeneo mbalimbali kuondolewa mara moja na kutupwa katika maeneo yaliyotengwa, badala ya kuachwa kandokando ya barabara ambako unaweza kurejea kwenye mifereji wakati mvua zinapoanza.

 

Makamu wa Rais pia ameagiza mamlaka husika kuwasimamia wakandarasi wanaotekeleza miradi ya ujenzi wa barabara, kuchukua hatua za haraka kusambaza vifusi vilivyorundikwa katika maeneo yenye shughuli za ujenzi, akisisitiza kuwa kazi hiyo haipaswi kusubiri hadi mvua zianze kunyesha kwani husababisha usumbufu na kero kwa wananchi.

 

Amesema katika maeneo yenye miradi ya ujenzi wa barabara ni lazima kuwe na mipango madhubuti itakayohakikisha barabara zinaendelea kupitika kwa urahisi na usalama, ili shughuli za ujenzi zisigeuke kuwa chanzo cha usumbufu au kuongeza athari kwa wananchi wakati wa mvua.

 

Katika kikao hicho, Makamu wa Rais alipokea taarifa kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe; pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya.

 

Taarifa ziliyowasilishwa katika kikao hicho zimeeleza kuwa maandalizi yanaendelea vizuri kupitia Kamati ya Kitaifa iliyoundwa kuratibu hatua za kuzuia, kudhibiti na kukabiliana na majanga yanayoweza kujitokeza katika kipindi cha mvua za El Niño.

 

Miongoni mwa maeneo yaliyopewa kipaumbele ni kufanya tathmini ya makazi yaliyopo mabondeni na maeneo mengine yenye hatari ya mafuriko, kuongeza elimu na tahadhari kwa umma, kufanya tathmini ya masoko na maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu, pamoja na kuendesha kampeni za usafi wa mazingira.

 

Hatua nyingine ni kuzibua mitaro, mifereji na mikondo ya maji, kulinda njia za asili za maji, kudhibiti maji taka na kufanya ukaguzi wa madaraja pamoja na miundombinu mingine muhimu ili kubaini maeneo yenye hatari na kuchukua hatua kabla ya mvua kuanza.

 

Serikali pia imeweka mkazo katika kuwa na mpango shirikishi wa dharura utakaowezesha Taasisi mbalimbali kuratibu hatua za uokoaji na utoaji wa huduma muhimu endapo kutatokea mafuriko au majanga mengine yanayohusiana na mvua hizo.

 

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

11 Septemba 2026

Dar es Salaam.

Libasse Gueye Mchezaji Bora Agosti, Manqoba Kocha Bora Ligi Kuu

Global Publishers
September 11, 2026
0 views
0 Comments

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Libasse Gueye, ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Agosti wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/27, huku kocha wa Young Africans, Manqoba Mngqithi, akichaguliwa kuwa Kocha Bora wa Mwezi huo.

Gueye alionesha kiwango kizuri katika mwezi huo, akishinda tuzo hiyo mbele ya Maxi Nzengeli wa Young Africans na Oscar Mwangaja wa Mbeya City.

Katika michezo mitano ambayo Simba ilicheza mwezi Agosti, Gueye alitoa mchango mkubwa kwa timu yake, iliyoshinda michezo yote mitano na kufunga bao moja kati ya mabao yaliyofungwa na Simba katika kipindi hicho.

Kwa upande wa Manqoba Mngqithi, kocha huyo aliiongoza Young Africans kushinda michezo yote mitano iliyocheza mwezi Agosti, hivyo kuiweka timu hiyo kileleni mwa msimamo wa ligi.

Kocha wa Yanga, Manqoba Mngqithi Kocha Bora wa Mwezi.

Wakati huo huo, Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemtangaza Meneja wa Uwanja wa Bukombe, mkoani Geita, Deogratius Dayan, kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Agosti.

Tuzo hiyo imekuja kutokana na namna alivyofanya vizuri katika usimamizi wa matukio ya michezo pamoja na kushughulikia masuala mbalimbali yanayohusu miundombinu ya uwanja.

Aidha, Kamati hiyo imeteua mabao matatu yaliyofungwa katika mwezi Agosti kuwania Bao Bora la Mwezi. Mabao hayo ni la Shekhan Hamis (Singida BS dhidi ya Polisi Tanzania), Robert Mathias (Geita Gold dhidi ya Kagera Sugar) na Hija Shamhe (Mbeya City dhidi ya Mashujaa).

 

KLINIKI YA VIWANGO TBS YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO NA MWENGE

  Na Mwandishi Wetu.

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kusogeza huduma na elimu kuhusu viwango, ubora na usalama wa bidhaa karibu na wananchi kupitia Kliniki ya Viwango, hatua inayolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo na kuwawezesha wafanyabiashara kuzingatia matakwa ya viwango.

Akizungumza wakati wa Kliniki hiyo inayoendelea Kariakoo na Mwenge Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Yusuph, kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ameipongeza TBS kwa kuendelea kuwafikishia wananchi huduma hizo, akisema zina mchango mkubwa katika kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa, kusambazwa na kuuzwa nchini zinakidhi viwango vinavyotakiwa.

Yusuph amesema huduma zinazotolewa na TBS, ikiwemo upimaji, ukaguzi, usajili wa bidhaa na majengo pamoja na elimu kwa umma, ni muhimu katika kulinda afya za wananchi na kujenga imani katika bidhaa zinazouzwa sokoni.

Amesema usalama wa chakula na bidhaa si jukumu la Serikali pekee, bali ni wajibu wa kila mmoja, huku akiwataka wafanyabiashara kuhakikisha bidhaa wanazozalisha na kuuza ni salama na zinakidhi matakwa ya viwango.

“Bidhaa zenye ubora humjengea mfanyabiashara jina zuri, kuongeza imani kwa mlaji na kufungua fursa zaidi za biashara,” amesema.

Kwa upande wake, Meneja wa Usajili wa Bidhaa na Majengo wa TBS, Habakuki Kalebo, amesema usalama wa vyakula na vipodozi ni wajibu wa wadau wote, hivyo wafanyabiashara wanapaswa kuhakikisha bidhaa zao ni salama na zinakidhi viwango vinavyotakiwa.

Kalebo amesema kwa mujibu wa mwongozo wa TBS, wafanyabiashara wa chakula na vipodozi wanapaswa kusajili maeneo yao ya biashara, yakiwemo maduka, maghala, hoteli, migahawa na maeneo mengine yanayohusika na biashara ya vyakula na vipodozi.

Amewataka wafanyabiashara kutumia fursa ya Kliniki ya Viwango kupata elimu na huduma za usajili, akisisitiza kuwa viwango ni sehemu muhimu ya ulinzi wa afya za wananchi, bidhaa na uaminifu katika soko.

“Tunawashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kupata huduma hii kwa karibu na elimu kuhusu mahitaji ya viwango,” amesema.

Ameongeza kuwa Kliniki ya Viwango imefanyika Kariakoo na Mwenge na itaendelea katika mikoa mbalimbali ambako TBS ina ofisi za kanda.

Kalebo amesema TBS inaendelea kushirikiana na halmashauri nchini katika kutoa huduma za usajili na ukaguzi wa maeneo ya biashara za vyakula na vipodozi, kuanzia ngazi za chini hadi taifa.

Akizungumza kama mmoja wa wanufaika wa Kliniki hiyo, mfanyabiashara Sajobe amesema huduma hiyo imewarahisishia wafanyabiashara kupata huduma za TBS bila kulazimika kwenda mbali.

Alisema awali wafanyabiashara walilazimika kufuata huduma hizo katika maeneo mengine, lakini uwepo wa kliniki Kariakoo umewarahisishia kushughulikia changamoto zao kwa haraka.

“Nimenufaika zaidi kwa sababu wamenirahisishia kusajili kwa haraka bidhaa zote ninazoagiza kutoka nje. Nimefanikiwa kusajili bidhaa nyingi kwa muda mfupi na zoezi limekuwa rahisi zaidi,” amesema.

Kliniki hiyo imekuwa pia fursa kwa wafanyabiashara kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu viwango, usajili na usalama wa bidhaa, huku TBS ikiendelea kusisitiza ushirikiano kati yake, wafanyabiashara, wananchi na mamlaka za Serikali katika kuhakikisha bidhaa zinazowafikia walaji ni salama na zenye ubora.