Doumbia Aandaliwa Kuikabili Mighty Wanderers Ligi ya Mabingwa Afrika

Global Publishers
September 12, 2026
0 views
0 Comments

Mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Doumbia, ni miongoni mwa wachezaji wanaoendelea na mazoezi maalumu kuelekea mchezo wa marudiano wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) dhidi ya Mighty Wanderers ya Malawi.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Septemba 13, 2026, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, huku Simba SC ikiwa na faida ya ushindi wa bao 1-0 iliyoupata katika mchezo wa kwanza ugenini.

Bao pekee la Simba SC katika mchezo huo lilifungwa na Anicet Oura dakika ya 65, hivyo Wekundu wa Msimbazi kuhitaji matokeo yatakayowavusha kwenda hatua inayofuata.

Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, anaendelea kuwaandaa wachezaji wake kwa mchezo huo, akiwemo Oura, Doumbia, Clatous Chama, Ellie Mpanzu na Hussen Abel.

Barker amesema mchezo huo hautakuwa rahisi kutokana na Mighty Wanderers kuhitaji ushindi wakiwa ugenini, akisisitiza kuwa Simba bado haijafuzu licha ya kushinda mchezo wa kwanza.

“Wapinzani wetu wanatambua kwamba wamepoteza mchezo wa kwanza, hivyo wanakuja kwenye mchezo wakiwa wanahitaji ushindi. Tunawaheshimu wapinzani kutokana na ubora walionao kwani kazi bado inaendelea.”

Amesema pia kikosi chake kinaendelea kufanyia kazi makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa kwanza ili kuhakikisha kinafanya vizuri zaidi katika mchezo wa marudiano.

“Makosa ambayo yamepita tunafanyia kazi ili kuwa bora zaidi. Hauwezi kuwa mchezo rahisi. Matokeo ya mwisho yataamua nani ambaye atafuzu hatua inayofuata. Hata sisi bado hatujafuzu, tunapambana kuhakikisha tunafanikisha malengo yetu.”

Stori na Lunyamadzo Mlyuka

Iñaki Williams Aaga Black Stars, Aendelea na Athletic Club

Global Publishers
September 12, 2026
0 views
0 Comments

Mshambuliaji na nahodha wa Athletic Club, Iñaki Williams, ametangaza kustaafu kucheza soka la kimataifa akiwa na umri wa miaka 32.

Williams ametangaza uamuzi huo leo, Septemba 11, 2026, kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, akifunga rasmi ukurasa wa miaka minne akiwa na timu ya taifa ya Ghana, Black Stars.

Mchezaji huyo aliamua kubadili uaminifu wake wa kimataifa kutoka Hispania kwenda Ghana mwaka 2022. Kabla ya hapo, Williams aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Hispania mchezo mmoja wa kirafiki mwaka 2016.

Katika kipindi chake akiwa na Ghana, Williams amecheza jumla ya mechi 28 na kufunga mabao mawili, huku akiiwakilisha nchi hiyo katika Kombe la Dunia mara mbili pamoja na michuano ya AFCON.

Akizungumzia uamuzi wake wa kustaafu soka la kimataifa, Williams amesema Ghana ilimpa zaidi ya mpira wa miguu, kwani ilimsaidia kurejea karibu zaidi na asili yake na kupata fahari ya kuvaa jezi ya taifa.

Mchezo wake wa mwisho akiwa na Black Stars ulikuwa dhidi ya Colombia katika Kombe la Dunia, ambapo Ghana ilipoteza kwa bao 1-0 na kutolewa katika hatua ya 32 bora.

Hata hivyo, uamuzi huo unahusu soka la kimataifa pekee, kwani Williams bado anaendelea na shughuli zake za soka la klabu akiwa na Athletic Club ya Hispania.

STORI NA DIDAS DIDAS, GPL -TUDACO

Book Of Dead, Crystal Hall Na Wengine Wengi Watua Meridianbet

Global Publishers
September 12, 2026
0 views
0 Comments

Burudani ya kasino mtandaoni imepata sura mpya baada ya Meridianbet kuileta Play’n GO, mtoa huduma anayejulikana kimataifa kwa michezo ya kasino yenye ubunifu na muundo wa kisasa. Ujio huu umeongeza nguvu kwenye jukwaa la Meridianbet, huku wachezaji wakipewa nafasi ya kugundua michezo yenye hadithi, wahusika na mazingira yaliyobuniwa kwa namna ya kipekee.

Kwenye orodha hiyo kuna majina kama Book of Dead, Hot Dog Heist, Flying Pigs, Crystal Hall na Cats and Cash, kila mmoja akiwa na utambulisho wake. Mchezo mmoja unaweza kukupeleka kwenye hadithi ya kusisimua, mwingine ukakupa mazingira ya kuchekesha, huku mwingine ukija na muonekano wa kisasa unaovutia. Tofauti hizo ndizo zinazofanya mkusanyiko huu kuwa na ladha mbalimbali kwa wachezaji wenye mapendeleo tofauti.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Play’n GO imejenga sifa yake kupitia michezo inayoweka mkazo kwenye ubunifu na simulizi. Ndani ya michezo hiyo, picha, sauti, wahusika na mfumo wa uchezaji huunganishwa ili kuunda mazingira yanayomfanya mchezaji ajisikie kama sehemu ya tukio. Hivyo, kila raundi inakuwa nafasi ya kugundua kinachoendelea, huku uzoefu wa kidijitali ukipewa msisimko unaozidi ule wa mchezo wa kawaida.

Meridianbet imeongeza michezo hiyo huku ikiendelea kuweka mazingira yanayolenga usalama na burudani kwa wachezaji. Wachezaji wanaweza kujaribu michezo mbalimbali na kufurahia uzoefu unaotolewa.

Mlango wa Play’n GO umefunguliwa rasmi ndani ya Meridianbet, na wapenzi wa burudani ya kidijitali wana nafasi ya kuingia na kugundua ulimwengu mpya wa michezo. Book of Dead, Flying Pigs, Cats and Cash na wengine wanasubiri kutoa ladha zao tofauti kwa wachezaji.

Diamond na Zuchu Kufanya Sherehe ya Siku 40 ya Mtoto Wao Leo

Global Publishers
September 12, 2026
36 views
0 Comments

Familia ya Diamond Platnumz na Zuchu leo, Jumamosi Septemba 12, 2026, inatarajiwa kufanya sherehe ya siku 40 ya mtoto wao wa kike, katika hafla itakayofanyika St. Laurent Garden- Kawe jijini Dar es Salaam.

Diamond Platnumz ametangaza tarehe na eneo la hafla hiyo kupitia mitandao yake ya kijamii, huku tukio hilo likija takribani siku 40 baada ya Zuchu kujifungua mtoto huyo Agosti 2, 2026.

Mtoto huyo ni wa kwanza kwa Zuchu, huku akiwa mtoto wa tano kwa Diamond Platnumz.

Sherehe hiyo inatarajiwa kuwa na mvuto zaidi baada ya watoto wa Diamond na Zari Hassan, Tiffah na Nillan, kuwasili Tanzania wakitokea Afrika Kusini Septemba 9, 2026, kwa ajili ya kushiriki katika tukio hilo la kifamilia.

Kwa sasa, macho ya mashabiki wa Diamond na Zuchu yameelekezwa St. Laurent Garden, ambako familia hiyo inatarajiwa kukutana kusherehekea hatua hiyo muhimu katika maisha ya mtoto wao.

Stori na Razaku Ramadhan | GPL -TUDACO

Liverpool Yamlaza Fulham Anfield, Isak Aongoza Mashambulizi

Klabu ya Liverpool inaendelea na kampeni yao ya ligi kuu ya EPL ambapo itakuwa mwenyeji wa Fulham katika mchezo wa Ligi Kuu England (EPL) utakaopigwa leo Jumamosi, Septemba 12, 2026, kuanzia saa 17:00 jioni katika Uwanja wa Anfield.

Liverpool inajiamini zaidi baada ya kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya Ipswich Town katika mchezo uliopita wa ligi kuu, ambapo mshambuliaji wao Alexander Isak alifunga mabao mawili ndani ya dakika tisa za mwanzo. Isak tayari ameanza kuonyesha ubora wake na kuwa miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuleta tofauti dhidi ya Fulham.

Liverpool wanaingia kwenye mechi hii wakiwa na matokeo mchanganyiko waliweza kufunga mabao 2-0 dhidi ya Ipswich Town wiki iliyopita, lakini kabla ya hapo walitoka sare 2-2 dhidi ya Nottingham Forest nyumbani na pia sare 2-2 dhidi ya Newcastle United. Kwa sasa Liverpool wapo nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 5 kutokana na kushinda mchezo mmoja na sare mbili.

Kwa upande wa Fulham, mambo yamekuwa magumu mwanzoni mwa msimu chini ya kocha mpya Álvaro Arbeloa. Timu hiyo imepoteza michezo yote mitatu ya EPL hadi sasa, ikiwemo kichapo cha 3-2 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wao wa mwisho, huku ikiruhusu jumla ya mabao saba.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Hata hivyo, Fulham bado ina wachezaji wenye uwezo wa kuleta changamoto, akiwemo Joshua King ambaye amekuwa sehemu muhimu ya mashambulizi yao. Arbeloa, ambaye aliwahi kuichezea Liverpool, atarejea Anfield akiwa na jukumu la kujaribu kuibadilisha hali ya timu yake na kupata pointi tatu za kwanza ndani ya msimu huu.

Kwa Liverpool, ushindi unaweza kuendelea kuwaweka katika nafasi nzuri mwanzoni mwa msimu, huku Fulham ikihitaji matokeo chanya ili kuondokana na mwanzo mbaya. Mchezo huo unatarajiwa kuwa na presha kubwa kwa wageni, hasa kutokana na ubora wa Liverpool nyumbani na kiwango kinachoendelea kuonyeshwa na Isak pamoja na safu yao ya ushambuliaji.

Chege na Mbosso Waungana Kwenye Wimbo Mpya ‘Ubaya’ – Video

Global Publishers
September 12, 2026
6 views
0 Comments

Msanii mkongwe wa Bongo Flava, Chege Chigunda, ameachia rasmi wimbo wake mpya unaoitwa “Ubaya”, akiwa amemshirikisha mwanamuziki Mbosso katika ushirikiano unaogusa kwa kina upande wa maumivu na changamoto zinazojitokeza katika mahusiano ya kimapenzi.

Wimbo huo unaangazia masuala ya usaliti, kuvunjika kwa uaminifu, maumivu ya moyo na madhara yanayoweza kumpata mtu anayempenda mwenza ambaye hatimizi matarajio ya mapenzi.

Katika “Ubaya”, Chege anakuja na uzoefu wake wa muda mrefu katika muziki, huku Mbosso akiongeza sauti yake yenye hisia, jambo linaloufanya ushirikiano huo kuwa na ladha ya kipekee kwa mashabiki wa Bongo Flava.

Video rasmi ya wimbo huo tayari imeachiwa kupitia YouTube, ikiwa na jina “Mbosso X Chege – UBAYA Official Video”, huku wimbo huo ukianza kupokelewa na mashabiki muda mfupi baada ya kutolewa.

“Ubaya” unaingia sokoni ukiwakutanisha wasanii hao wawili wenye mitazamo na uzoefu tofauti katika muziki, huku ujumbe wake ukilenga zaidi watu waliowahi kupitia maumivu, usaliti na changamoto mbalimbali katika mapenzi.

Stori na Razaku Ramadhan | GPL

Clara Luvanga Atembelea Yanga Baada ya Kusajiliwa Washington Spirit

Global Publishers
September 12, 2026
18 views
0 Comments

Mshambuliaji wa Tanzania, Clara Luvanga

Mshambuliaji wa Tanzania, Clara Luvanga, ametembelea klabu yake ya zamani ya Young Africans (Yanga), ikiwa ni muda mfupi baada ya kukamilisha uhamisho wake wa kihistoria kwenda Washington Spirit ya Marekani.

Luvanga, ambaye alikulia katika mfumo wa Yanga Princess, amerejea katika mazingira ya klabu hiyo wakati akianza ukurasa mpya wa safari yake ya soka katika ligi ya wanawake nchini Marekani.

Septemba 9, 2026, Washington Spirit ilitangaza kumsajili Luvanga kutoka Al-Nassr ya Saudi Arabia kwa mkataba wa miaka minne.

Uhamisho huo umeweka historia kwa Luvanga kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza katika National Women’s Soccer League (NWSL), ligi ya juu ya soka la wanawake nchini Marekani.

Kabla ya kuhamia Marekani, Luvanga alitumia misimu mitatu akiichezea Al-Nassr, ambapo msimu wa 2025/26 aliweka rekodi ya kuvutia kwa kufunga mabao 24 na kutwaa tuzo ya mfungaji bora wa ligi.

Ziara yake Yanga imekuja wakati jina lake likizidi kupata umaarufu katika soka la kimataifa, huku hatua yake ya kujiunga na Washington Spirit ikiwa miongoni mwa mafanikio makubwa katika historia ya soka la wanawake Tanzania.

Stori na Anifa Mwegelo | GPL -TUDACO

Fahamu Faida 7 Muhimu za Kula Machungwa Kila Siku


Machungwa ni miongoni mwa matunda yanayopatikana kwa urahisi na yanayopendwa na watu wengi, lakini nyuma ya ladha yake tamu kuna hazina kubwa ya virutubisho muhimu kwa afya ya binadamu. Kula machungwa mara kwa mara kunaweza kuwa hatua ndogo yenye matokeo makubwa katika kuboresha afya yako kwa ujumla.

Moja ya faida kuu ya machungwa ni uwezo wake wa kuimarisha kinga ya mwili. Tunda hili lina kiwango kikubwa cha vitamini C, kirutubisho kinachosaidia mwili kupambana na magonjwa mbalimbali, hasa yale ya maambukizi kama mafua. Kwa mtu anayekula machungwa mara kwa mara, mwili hupata uwezo mkubwa wa kujilinda dhidi ya maradhi.

Mbali na hilo, machungwa yana mchango mkubwa katika kuboresha afya ya ngozi. Vitamini C husaidia katika uzalishaji wa collagen, ambayo ni muhimu kwa ngozi kuwa imara, laini na yenye mwonekano mzuri. Hii ina maana kuwa kula machungwa kunaweza kusaidia kuchelewesha dalili za kuzeeka kama vile mikunjo.

Katika upande wa mmeng’enyo wa chakula, machungwa yana nyuzinyuzi (fiber) ambazo husaidia kuboresha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Hii husaidia kuzuia matatizo kama kufunga choo na kuhakikisha chakula kinameng’enywa vizuri mwilini.

Pia, machungwa yana mchango mkubwa katika kulinda afya ya moyo. Virutubisho vilivyomo ndani yake husaidia kupunguza kiwango cha mafuta mabaya (cholesterol) mwilini na hivyo kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo. Kwa watu wanaojali afya ya moyo wao, kuongeza machungwa katika lishe ni uamuzi mzuri.

Zaidi ya hayo, machungwa yana maji kwa wingi, jambo linalosaidia kuupa mwili unyevu wa kutosha na kuzuia upungufu wa maji mwilini. Hii ni muhimu hasa katika maeneo yenye joto kali ambapo mwili hupoteza maji kwa urahisi.

Kwa upande wa nishati, machungwa hutoa sukari ya asili ambayo huupa mwili nguvu kwa haraka bila madhara makubwa kama yale ya sukari zilizoongezwa viwandani. Hii hufanya machungwa kuwa chaguo bora la vitafunwa vya afya.

Vilevile, machungwa yanaweza kusaidia katika kudhibiti uzito wa mwili. Kwa kuwa yana kalori chache lakini yana nyuzinyuzi nyingi, husaidia mtu kushiba kwa muda mrefu na kupunguza ulaji wa kupita kiasi.

Kwa ujumla, machungwa si tunda la kawaida tu bali ni sehemu muhimu ya lishe bora. Kujenga tabia ya kula machungwa mara kwa mara kunaweza kuwa njia rahisi lakini yenye manufaa makubwa katika kuboresha afya yako ya kila siku.