MASAJI ZA SALUNI CHANZO CHA KUPOOZA NA KUHARIBU UTI WA MGONGO

 

Wataalamu wa upasuaji wa ubongo na uti wa mgongo wameonya wananchi kuacha tabia ya kufanyiwa masaji, kuvutwa au “kukunjwa” shingo na watu wasio na utaalamu, wakiwamo baadhi ya vinyozi, wakisema kitendo hicho kinaweza kuharibu uti wa mgongo na kusababisha kupooza mwili.

Utaratibu huo umetajwa kuwafanya baadhi ya wanaume kuwa na maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo yanayosambaa hadi miguuni, pamoja na maumivu ya shingo na mabega.

Onyo hilo limetolewa jana, Septemba 11, 2026, na Karanjit Singh Narang, daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na uti wa mgongo kutoka Hospitali ya Medanta nchini India, aliyeko Dar es Salaam kwa ajili ya kambi ya matibabu inayolenga kutoa elimu na ushauri kwa wagonjwa wenye matatizo ya ubongo, uti wa mgongo na shingo.

Katika baadhi ya maeneo nchini, masaji ya shingo baada ya kunyoa nywele ni huduma inayotolewa na baadhi ya vinyozi.

Amesema kuwa shinikizo au mjongeo mkali wa shingo unaweza kuathiri mishipa inayopita katika eneo hilo. 

Uharibifu huo unaweza kusababisha madhara makubwa ya mishipa ya fahamu, ikiwamo kupoteza uwezo wa baadhi ya viungo kufanya kazi.

Career Opportunities – Wezesha Mzawa Insurance Broker Limited

WEZESHA MZAWA INSURANCE BROKER LIMITED is seeking motivated and experienced professionals to join its team in the following positions:

1️⃣ INSURANCE UNDERWRITING/CLAIMS OFFICER

We are seeking a motivated and experienced Insurance Underwriting/Claims Officer to join our Insurance Broking Firm.

🎓 Minimum Academic Qualification:
Bachelor of Science in Insurance and Risk Management, with at least two years of relevant working experience.

2️⃣ BUSINESS DEVELOPMENT EXECUTIVE

We are seeking a motivated and experienced Business Development Executive to join our Insurance Broking Firm.

🎓 Minimum Academic Qualification:
Bachelor’s Degree in Insurance and Risk Management, Sales and Marketing, Business Administration, or any other related field, with at least two years of working experience in the insurance industry, business development, sales, or marketing.

3️⃣ ACCOUNTANT

We are seeking a motivated and experienced Accountant to join our Insurance Broking Firm.

🎓 Minimum Academic Qualification:
Bachelor’s Degree in Accounting or Finance, with at least two years of working experience in the insurance industry.

📌 CPA qualification is an added advantage.

4️⃣ INSURANCE SALES EXECUTIVES

We are seeking motivated and experienced Insurance Sales Executives to join our Insurance Broking Firm.

🎓 Minimum Academic Qualification:
Certificate in Insurance and Risk Management, Sales, Marketing, Business Administration, or any other related field.

📌 Experience in the insurance industry and sales is an added advantage.

📅 APPLICATION DEADLINE: SEPTEMBER 30, 2026

All applications should be submitted via the email address below or delivered to the physical address, accompanied by the necessary certified documents, before the application deadline.

🏢 WEZESHA MZAWA INSURANCE BROKER LIMITED
P.O. BOX 7534, SINZA MORI,
GLOBAL GROUP HOUSE (OPPOSITE WANYAMA HOTEL),
DAR ES SALAAM, TANZANIA.

📧 EMAIL: [email protected]

Mfalme Oyo Azikwa Karambi, Uganda Yamuaga Kiongozi Wake wa Kifalme

FORT PORTAL, UGANDA: Mfalme Oyo Nyimba Kabamba Iguru Rukidi IV wa Ufalme wa Tooro, magharibi mwa Uganda, amezikwa katika Makaburi ya Kifalme ya Karambi, kufuatia kifo chake kilichotokana na saratani mwezi uliopita.

Mfalme Oyo, ambaye alitawazwa Septemba 12, 1995 baada ya kifo cha baba yake, amezikwa Septemba 12, miaka 31 baada ya kutawazwa kwake. Alikuwa ametawala Ufalme wa Tooro tangu akiwa na umri wa miaka mitatu.

Mazishi yake yamefanyika kwa kuzingatia mila na desturi za kifalme za Tooro, huku hafla ya mwisho ya kumzika ikiwa ya faragha na kuhudhuriwa na familia pamoja na marafiki wachache wa karibu.

Wananchi na vyombo vya habari hawakuruhusiwa kushuhudia hatua za mwisho za mazishi, huku kamera zikizuiwa katika eneo la kaburi.

Mapema asubuhi, saa 3:16 kwa saa za eneo hilo, jeneza lililobeba mwili wa Mfalme Oyo, likiwa limefunikwa kwa rangi rasmi za Ufalme wa Tooro, njano na bluu, liliondolewa katika Ikulu ya Karuziika mjini Fort Portal kwa safari yake ya mwisho.

Maelfu ya waombolezaji walikusanyika katika Kanisa Kuu la St. John, kanisa lililojengwa na babu wa Mfalme Oyo, Omukama Rukidi III, na ambako marehemu mfalme alibatizwa.

Mazishi hayo yalihudhuriwa pia na maafisa wa serikali, viongozi waandamizi pamoja na wawakilishi kutoka falme na tawala za machifu wa jadi kutoka Uganda, Kenya, Sudan Kusini, Nigeria na Eswatini.

Kwa mujibu wa mila za Tooro, Omusuna, msimamizi mkuu wa masuala ya kifalme anayehusika na mazishi ya wafalme, aliongoza taratibu za mazishi.

Miongoni mwa desturi zilizotekelezwa ni mfalme mpya kutupa punje tisa za kahawa kaburini, ikiwa ni ishara maalumu katika taratibu za kifalme za Tooro.

Mzozo wa Urithi Wazua Mvutano

Kifo cha Mfalme Oyo kimeibua mvutano ndani ya familia ya kifalme kuhusu mrithi wa kiti cha ufalme.

Mama yake na baadhi ya wanafamilia wamepinga uteuzi wa Edward Rukidi Kijanangoma, mwandishi wa habari wa televisheni, kuwa mrithi wa kiti hicho, wakisisitiza kuwa mtoto wa marehemu mfalme ndiye anayepaswa kurithi nafasi hiyo.

Hata hivyo, Baraza la Wazee wa Tooro limeunga mkono uamuzi wa ukoo wa kifalme wa kumteua Edward Rukidi Kijanangoma kuwa kiongozi ajaye wa Ufalme wa Tooro.

Akizungumza wakati wa ibada ya mazishi, Mkuu wa Ukoo wa Kifalme, Omusuuga Charles Kamurasi, alisema uamuzi huo umefanyika kwa kuzingatia sheria, mila na desturi za Tooro.

“Tunaye mfalme mpya, Edward Rukidi Kijanangoma. Kila hatua tuliyochukua imezingatia sheria na kuongozwa na mila na desturi za Tooro. Tudumishe amani na tutulie,” alisema Kamurasi.

Uganda Yafanya Mazishi ya Kitaifa

Serikali ya Uganda ilimfanyia Mfalme Oyo mazishi ya kitaifa na kutangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kwa heshima yake.

Katika taratibu hizo, marehemu mfalme alipewa heshima ya kupigwa mizinga tisa, ishara ya heshima inayotolewa kwa viongozi na watu mashuhuri wa taifa.

Mamia ya waombolezaji walijipanga kando ya barabara kuelekea Makaburi ya Kifalme ya Karambi, wakimsindikiza Mfalme Oyo katika safari yake ya mwisho.

Mazishi hayo yamehitimisha utawala wa Mfalme Oyo, aliyekuwa miongoni mwa wafalme waliotawala kwa muda mrefu zaidi barani Afrika, baada ya kuvikwa taji akiwa na umri wa miaka mitatu.

Museveni Atoa Heshima

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amemtaja Mfalme Oyo kuwa kiongozi wa kitamaduni aliyekuwa akiwahamasisha wananchi wake kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Katika ujumbe wa rambirambi uliowasilishwa na Naibu Spika wa Bunge, Thomas Tayebwa, Museveni amesema marehemu mfalme alidumisha uhusiano mzuri na Serikali huku akihamasisha maendeleo na kuhifadhi utamaduni.

Aidha, Museveni ametoa wito kwa Waganda kuongeza juhudi katika mapambano dhidi ya saratani na magonjwa yanayoweza kuzuilika.

Amewataka wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu visababishi vya magonjwa hayo pamoja na hatua zinazoweza kuchukuliwa katika kuyazuia.

Yanga Yatinga Hatua ya Pili CAFCL Kwa Ushindi wa Jumla wa 3-2

Global Publishers
September 12, 2026
0 views
0 Comments

YANGA imefanikiwa kutinga hatua ya pili ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) baada ya kuiondoa Gaborone United ya Botswana kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 katika michezo miwili.

Yanga imemaliza kazi hiyo kwa ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Gaborone, Botswana.

Katika mchezo wa marudiano, Yanga ilianza kwa kasi na kupata bao la kwanza dakika ya saba kupitia mshambuliaji wao Shalulile, kabla ya Touré kuongeza bao la pili dakika ya 83.

Gaborone United ilijibu dakika ya 86 kupitia Ditsele, lakini bao hilo halikutosha kuzuia Yanga kusonga mbele baada ya timu hizo kumaliza dakika 180 kwa jumla ya mabao 3-2.

Hatua inayofuata itakuwa mtihani mwingine kwa Yanga, ambayo sasa itakutana na CFFA FC ya Madagascar katika hatua ya pili ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ushindi huo umeendeleza matumaini ya Yanga katika safari yake ya kuwania nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa ya klabu barani Afrika.

Mpigie Kura Godmuya, Kura Yako Ni Ushindi! – Tuzo za Samia Kalamu Awards 2026

Global Publishers
September 12, 2026
1,788 views
0 Comments

Mtangazaji wa @globaltvonline na @255globalradio, Godfrey Nathan @godmuya ameteuliwa kuwania tuzo za Samia Kalamu Awards 2026.

Sasa Godmuya anaomba support yako, mfuatiliaji wa Global TV, kwa kumpigia kura ili kufanikisha ushindi wake.

🗳️ MPIGIE KURA: GODFREY LUHILABAKE NATHAN
🔢 Kodi: 260246

Kura yako ni mchango mkubwa kwa Godmuya katika safari hii ya tuzo.

🙏 Piga kura, share na mwambie mwingine apige kura!

Viongozi Mbalimbali Wamfariji Rais Samia Kizimkazi – Picha

Global Publishers
September 12, 2026
24 views
0 Comments

KIZIMKAZI, ZANZIBAR: Viongozi mbalimbali wa dini, taasisi za umma na binafsi pamoja na makundi mbalimbali wameendelea kumfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.

Viongozi hao wamefika nyumbani kwa Rais Samia Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, Septemba 11 na 12, 2026, kwa ajili ya kutoa pole na kumfariji katika kipindi hiki cha majonzi.

Miongoni mwa waliofika ni Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Prof. Mohamed Janabi, ambaye alifika Kizimkazi kutoa pole kwa Rais Samia na familia yake.

Aidha, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, ni miongoni mwa viongozi wa dini waliomtembelea Rais Samia na kumpa pole kufuatia msiba huo.

Viongozi mbalimbali kutoka taasisi za umma na binafsi pia wamefika nyumbani hapo kuungana na Rais Samia pamoja na familia katika kipindi hiki cha maombolezo.

Mbali na viongozi hao, mabondia kutoka Mafia Boxing nao wamefika Kizimkazi kutoa pole na faraja kwa Rais Samia kufuatia msiba wa mume wake.

Maalim Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Septemba 7, 2026, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar.

Ziara hizo za viongozi na makundi mbalimbali zinaendelea kuonyesha mshikamano na kutoa faraja kwa Rais Samia na familia yake katika kipindi hiki cha majonzi. 

Rais Mstaafu Kikwete Awasili Tabora Kukagua Zahanati za JMKF

Global Publishers
September 12, 2026
0 views
0 Comments

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanzilishi pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF), Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amewasili mkoani Tabora leo Jumamosi, Septemba 12, 2026, kwa ziara ya siku nne.

Katika ziara hiyo, Dkt. Kikwete atatembelea na kukagua zahanati zilizojengwa na JMKF kwa lengo la kusaidia juhudi za Serikali katika kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa maeneo ya pembezoni.

Zahanati hizo zimejengwa kwa lengo la kuwahudumia zaidi ya wakazi 36,000 katika vijiji viwili pamoja na jamii zinazozunguka maeneo hayo.

Mbali na kukagua miundombinu hiyo ya afya, Dkt. Kikwete anatarajiwa pia kuangalia utekelezaji wa Mradi wa Jamii Salama (Mobile Antenatal Care Outreach), unaolenga kusogeza huduma za afya kwa wajawazito karibu na jamii.

Dkt. Kikwete amepokelewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Upendo Wella, pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa huo.

Ziara hiyo inatarajiwa kutoa fursa ya kutathmini maendeleo ya miradi hiyo, pamoja na namna inavyosaidia kuongeza upatikanaji wa huduma muhimu za afya kwa wananchi wa maeneo yanayozunguka vijiji hivyo.

DC RUKIA AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO

Wananchi wa Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya uwezekano wa kunyesha kwa mvua kubwa katika kipindi kijacho kufuatia taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mwenendo wa hali ya hewa na uwezekano wa mvua za El Niño.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Mhe. Rukia Zuberi ambapo amesema wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi, yakiwemo mabondeni, maeneo ya jirani milima au mito, pamoja na maeneo yenye uwezekano wa kukumbwa na mafuriko au maporomoko ya ardhi, wanashauriwa kuchukua hatua tahadhari mapema, ikiwemo kuhama maeneo hayo, kuweka akiba ya chakula na mahitaji muhimu kwa matumizi wakati wa mvua hizo.

Pia amewahimiza wananchi kuhakikisha kuwa mitaro, mifereji na njia za maji zinakuwa safi na hazijazibwa na taka, ili kuwezesha maji kupita kwa urahisi hatua inayolenga kupunguza uwezekano wa maji kujaa katika maeneo ya makazi, kusababisha mafuriko na uharibifu wa mali na kuhatarisha maisha ya watu.

Kuhusu watoto, wazazi na walezi wametakiwa kuwa waangalifu na kutowaruhusu kwenda shuleni wakati mvua zinapokuwa kubwa na mazingira yakiwa hatarishi huk, viongozi katika maeneo mbalimbali wakielekezwa kusimamia utekelezaji wa tahadhari hizo, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usafi wa njia za maji unafanyika kwa wakati.

TMA imesema mvua hizo zinatarajiwa kuanza kunyesha kuanzia mwishoni mwa Septemba 2026 na kuendelea hadi Januari 2027, Wananchi wa Mwanga wametakiwa kuendelea kufuatilia taarifa rasmi kutoka TMA na Serikali, pamoja na kuzingatia maelekezo yatakayotolewa ili kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo.