ASAS APOKELEWA KWA KISHINDO SONGWE

 

Na Moses Ng’wa, Songwe

MJUMBE wa Kamati Kuu (MCC) na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe, Salim Faraj Abri maarufu Asas, amepokelewa kwa kishindo mkoani Songwe leo Novemba 6, 2026, alipowasili kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Asas amepokelewa katika ofisi za CCM za Mkoa zilizopo Vwawa, Wilaya ya Mbozi, na wajumbe wa Kamati za Siasa za CCM za Mkoa na Wilaya, kabla ya kuanza kwa shughuli mbalimbali zilizopangwa katika ziara yake hiyo.

Miongoni mwa shughuli hizo ni kushiriki kikao maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Songwe, ambacho atahudhuria akiwa katika nafasi yake ya mlezi wa chama mkoani humo.

Aidha, anatarajiwa kuimarisha uhai wa chama katika ngazi mbalimbali na kuhimiza viongozi kuimarisha usimamizi wa shughuli za CCM katika maeneo yao.

Baada ya kukamilisha ziara yake mkoani Songwe, kesho Novemba 7, 2026, Asas anatarajiwa kuelekea mkoani Mbeya kuendelea na majukumu yake ya ulezi wa CCM katika mikoa hiyo miwili.