Serikali Yatangaza Nafasi Mpya za Ajira kwa Wenye Shahada za Uzamili

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) imetangaza nafasi nne (4) za kazi katika Shule ya Sheria Tanzania (Law School of Tanzania – LST) na Chuo cha Elimu ya Biashara (College of Business Education – CBE).

Tangazo hilo lenye Kumbukumbu Na. JA.9/16/01/62 la Oktoba 29, 2026, linatoa fursa kwa Watanzania wenye sifa stahiki kuomba nafasi hizo za kitaaluma.

Nafasi zilizotangazwa ni kama ifuatavyo:

1. SHULE YA SHERIA TANZANIA (LST)

Shule ya Sheria Tanzania imetangaza nafasi tatu za Wakufunzi Wasaidizi (Assistant Lecturers), katika maeneo yafuatayo:

  • Assistant Lecturer (Conveyancing) – Nafasi 1.

  • Assistant Lecturer (Alternative Dispute Resolution and Quasi Judicial Practice) – Nafasi 1.

  • Assistant Lecturer (Practical Aspects of Commercial Law) – Nafasi 1.

Sifa za waombaji:

Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Uzamili ya Sheria (Master’s Degree in Law) kutoka taasisi inayotambulika, yenye GPA isiyopungua 3.8.

Aidha, anatakiwa kuwa Wakili anayefanya kazi za uwakili kwa kipindi kisichopungua miaka mitano, na awe amehudhuria na kufaulu Stashahada ya Uzamili ya Sheria katika Law School of Tanzania au kukamilisha programu ya mafunzo ya awali ya uwakili (Internship Programme).

Pia, anatakiwa kuwa na Shahada ya Kwanza ya Sheria yenye GPA isiyopungua 3.5.

Uzoefu katika ufundishaji, tafiti na huduma za ushauri wa kitaalamu utakuwa nyongeza ya sifa.

Mshahara: PHTS 1.

2. CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA (CBE)

Chuo cha Elimu ya Biashara kimetangaza nafasi moja ya Mkufunzi Msaidizi katika fani ya:

– Assistant Lecturer (Networking) – Nafasi 1.

Sifa za waombaji:

Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Uzamili (NTA Level 9) au sifa inayolingana nayo, pamoja na Shahada ya Kwanza katika mojawapo ya fani zifuatazo:

GPA ya Shahada ya Uzamili haitakiwi kuwa chini ya 4.0 au kiwango kinacholingana na B+, na Shahada ya Kwanza haitakiwi kuwa chini ya 3.8.

Mwombaji anatakiwa pia kuwa amesomea fani zinazofanana au zinazohusiana katika ngazi zote mbili za elimu.

Mshahara: PHTS 2.

MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI

PSRS imeeleza kuwa waombaji wote wanapaswa kuzingatia masharti yafuatayo:

  1. Awe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na asiwe na umri unaozidi miaka 45.

  2. Kuwasilisha nakala zilizothibitishwa za vyeti vya elimu na matokeo (transcripts).

  3. Kuwasilisha vyeti vya usajili na mafunzo ya kitaaluma pale inapohitajika.

  4. Kuwasilisha cheti cha kuzaliwa.

  5. Kupakia picha mpya ya Passport Size katika mfumo wa maombi.

  6. Kutaja wadhamini watatu (referees) wenye mawasiliano yanayoaminika.

  7. Vyeti vya elimu vilivyopatikana nje ya nchi lazima vitambuliwe na mamlaka husika kama TCU, NECTA au NACTVET.

  8. Waombaji wenye sifa zinazohitaji GPA wanapaswa kuambatanisha cheti cha uthibitisho wa ukokotoaji wa GPA kutoka TCU.

Watumishi walioajiriwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba nafasi hizo, kwa mujibu wa masharti ya tangazo. Aidha, wastaafu wa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba.

MWISHO WA MAOMBI: NOVEMBA 11,  2026

PSRS imeeleza kuwa waombaji watakaofanikiwa kuingia katika orodha fupi (shortlisted candidates) ndio watakaofahamishwa tarehe ya usaili.

Pia, imeonya kuwa uwasilishaji wa vyeti vya kughushi au taarifa za uongo utasababisha kuchukuliwa kwa hatua za kisheria.