Global Publishers September 17, 2026 1,338 views 0 Comments
Msanii wa filamu Bongo, Chanuo Nchakali, amefunguka kuhusu sakata la kiki ya ndoa kati yake na msanii wa Bongofleva, YJ Kiboko, akieleza namna suala hilo lilivyomtokea puani na kumfanya ashambuliwe vikali na mashabiki.
Chanuo amesema kiki hiyo ilisababisha mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki, huku baadhi yao wakimshambulia kwa maneno kutokana na kuamini kuwa uhusiano huo ulikuwa wa kweli.
Msanii huyo ameeleza kwa undani kilichotokea na namna alivyokabiliana na presha kutoka kwa mashabiki baada ya taarifa hizo kusambaa.
Nafasi za kazi kila siku Tanzania, Serikalini, Makampuni na Taasisi mbalimbali tembelea website yetu ya Global Publishers muda wote bonyeza hapa Publishers muda wote bonyeza hapa
Global Publishers September 17, 2026 1,866 views 0 Comments
YouTube imeanza kutumia teknolojia ya kutafsiri sauti kwa kutumia Akili Bandia (AI Dubbing) kwenye baadhi ya video, hali inayowafanya baadhi ya watazamaji kusikia sauti iliyotafsiriwa badala ya sauti halisi ya mtengenezaji wa maudhui.
Ikiwa unataka kusikia sauti ya asili ya video, unaweza kufanya hatua zifuatazo:
Fungua video unayotaka kutazama kwenye YouTube.
Bofya alama ya Mipangilio (Settings) yenye umbo la gia (⚙️).
Chagua Audio Track (Njia ya Sauti), ikiwa chaguo hilo linapatikana.
Badili kutoka lugha iliyotafsiriwa kwenda Original au lugha ya awali ya video.
Baada ya kufanya mabadiliko hayo, video itaanza kucheza kwa sauti halisi iliyorekodiwa na mtayarishaji wa maudhui.
Hata hivyo, si video zote zina chaguo la kubadili sauti. Endapo huoni kipengele cha Audio Track, ina maana mtengenezaji wa video hajawasha huduma hiyo au video hiyo inapatikana katika toleo moja tu la sauti.
Huduma ya AI Dubbing inalenga kuwafikia watazamaji wa lugha mbalimbali, lakini YouTube bado inatoa uwezekano wa kurejea kwenye sauti ya awali pale ambapo mtayarishaji amewezesha chaguo hilo.
Louis Vuitton alikuwa mmoja wa watu muhimu katika historia ya mitindo ya kifahari duniani. Jina lake limeendelea kuwa alama ya ubora kupitia kampuni ya Louis Vuitton inayojulikana kwa mabegi, mikoba, nguo, viatu na bidhaa za kifahari.
Kuzaliwa na Utoto
Louis Vuitton alizaliwa tarehe 4 Agosti 1821 katika kijiji cha Anchay, Jura, Ufaransa. Alizaliwa katika familia ya kawaida; baba yake, Xavier Vuitton, alikuwa mkulima na mtengenezaji wa masanduku, huku mama yake, Corinne Gaillard, akiwa mshonaji wa kofia na mfanyakazi wa mikono.
Maisha yake ya utotoni yalikuwa magumu. Baada ya mama yake kufariki akiwa bado mdogo na baadaye kumpoteza baba yake, Louis akiwa na umri wa takribani miaka 13 aliamua kuondoka nyumbani na kuanza safari ya kutafuta maisha bora.
Kijiji cha Anchay, Jura, Ufaransa alipozaliwa Louis Vuitton alizaliwa tarehe 4 Agosti 1821.
Safari ya Kuelekea Paris
Akiwa kijana, Louis alitembea kwa miguu zaidi ya kilomita 400 kutoka kijijini kwao hadi Paris, safari iliyochukua muda mrefu. Alipofika Paris mwaka 1837 akiwa na umri wa miaka 16, alianza kufanya kazi kama mwanafunzi wa fundi wa kutengeneza masanduku (box maker) chini ya fundi maarufu Monsieur Maréchal.
Wakati huo, kutengeneza masanduku ilikuwa kazi ya kifahari kwa sababu matajiri walihitaji maboksi maalumu kwa ajili ya kuhifadhi na kusafirisha nguo, vito na vitu vya thamani wanaposafiri.
Kuanzishwa kwa Louis Vuitton
Baada ya miaka mingi ya kujifunza na kuboresha ujuzi wake, Louis Vuitton alifungua biashara yake mwenyewe mwaka 1854 mjini Paris.
Alimuoa Clémence-Émilie Parriaux mwaka 1854, na walipata mtoto mmoja aitwaye Georges Ferréol Vuitton.
Alianzisha duka lake katika eneo la Rue Neuve-des-Capucines, karibu na Place Vendôme, likiwa miongoni mwa maeneo ya kifahari Paris.
Ubunifu wake mkubwa ulikuwa kutengeneza masanduku ya kusafiria yenye:
Muundo mwepesi lakini imara
Uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu
Umbo bapa juu ili yaweze kupangwa vizuri kwenye usafiri
Ubora wa hali ya juu kuliko masanduku ya kawaida yaliyokuwa na umbo la duara
Ubunifu huo ulifanya bidhaa zake kupendwa na wafalme, matajiri na wasafiri mashuhuri.
Mafanikio Makubwa
Louis Vuitton alijenga sifa kubwa kutokana na ubunifu na ubora wa bidhaa zake. Miongoni mwa mafanikio yake ni:
1. Kuwa mtengeneza masanduku wa familia za kifalme
Alipata umaarufu baada ya kuwa mtengeneza masanduku anayependwa na watu wa tabaka la juu nchini Ufaransa, akiwemo malkia wa Ufaransa Eugénie de Montijo.
2. Ubunifu wa turubai maalumu
Kampuni yake ilianza kutumia vifaa maalumu vya kufunika maboksi yake, vilivyosaidia kutambulika na kuwa vigumu kuigwa.
3. Kuanzisha urithi wa kifahari
Baada ya kifo chake, familia yake iliendeleza biashara hiyo na kuifanya kuwa moja ya chapa kubwa zaidi za mitindo duniani.
Kifo Chake
Louis Vuitton alifariki dunia tarehe 27 Februari 1892 akiwa na umri wa miaka 70. Aliacha kampuni iliyokuwa imeanza kuwa na jina kubwa katika sekta ya bidhaa za kifahari.
Urithi wa Louis Vuitton Leo
Leo hii, jina la Louis Vuitton linawakilisha:
Ubora wa hali ya juu
Ubunifu wa kifahari
Hadhi na mafanikio
Chapa yenye thamani kubwa duniani
Kampuni yake imeendelea kukua na kuwa sehemu ya kundi kubwa la bidhaa za kifahari duniani, ikitengeneza bidhaa zinazotumiwa na watu maarufu, wafanyabiashara wakubwa na wapenzi wa mitindo kote duniani.
Kutoka kijana aliyekimbia maisha magumu kijijini hadi kuunda moja ya chapa maarufu zaidi duniani, safari ya Louis Vuitton ni mfano wa ubunifu, uvumilivu na kujenga thamani kupitia ujuzi.
Global Publishers September 17, 2026 2,028 views 0 Comments
Location: Dar es Salaam, Tanzania Salary: TSh 700,000 kwa mwezi
Kampuni inakaribisha maombi kutoka kwa watu wenye uwezo, uwajibikaji na bidii kwa nafasi ya Supervisor. Mwombaji atakayefanikiwa atakuwa na jukumu la kusimamia shughuli za kila siku pamoja na kuhakikisha timu inafanya kazi kwa ufanisi na kufikia malengo yaliyowekwa.
Sifa za Mwombaji
Awe na kiwango cha chini cha elimu cha Diploma.
Awe anaishi Dar es Salaam kwa sasa.
Uzoefu wa kazi katika nafasi ya usimamizi au uongozi utakuwa ni faida.
Awe na uwezo mzuri wa mawasiliano na kushirikiana na watu.
Awe na uwezo wa kusimamia na kuhamasisha timu.
Awe mwaminifu, mwenye nidhamu na anayewajibika.
Awe na uwezo wa kufanya kazi chini ya presha na kufikia malengo.
Ujuzi wa msingi wa matumizi ya kompyuta utakuwa ni faida.
Majukumu Makuu
Kusimamia na kuratibu shughuli za kila siku.
Kusimamia na kufuatilia utendaji wa wafanyakazi.
Kuandaa ripoti za kila siku na kila wiki.
Kuhakikisha sera na taratibu za kampuni zinafuatwa.
Kushughulikia changamoto za wateja na wafanyakazi kwa weledi.
Kuhakikisha malengo na shughuli za kila siku zinafikiwa.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Waombaji wenye sifa wanatakiwa kutuma CV zao kupitia barua pepe:
AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .
Global Publishers September 16, 2026 0 views 0 Comments
Mashabiki wa michezo, Meridianbet imeleta sababu nyingine ya kuongeza msisimko kwenye burudani yako. Safari hii zawadi ni simu tatu mpya kabisa za Samsung Galaxy A26, ambazo zitatua mikononi mwa washindi watatu watakaopatikana kupitia promosheni maalum. Kwa mchezaji anayependa soka, michezo mbalimbali au kasino, hii ni fursa ya kuburudika huku ukijiweka kwenye nafasi ya kushinda zawadi.
Ili kuingia kwenye kinyang’anyiro, wachezaji wanapaswa kuwa na akaunti ya Meridianbet na kushiriki kupitia tovuti au App kwa kuzingatia masharti ya promosheni. Hivyo, kama ulikuwa tayari unaendelea na shughuli zako za kubashiri, au michezo ya kasino sasa kuna sababu nyingine ya kuifanya safari yako iwe na msisimko zaidi.
Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Kitu cha kuvutia zaidi ni kwamba promosheni hii haijawekwa kwa kundi moja pekee la wachezaji. Wanaopenda kubashiri michezo na wale wanaofurahia kasino wote wanaweza kushiriki, mradi tu wafuate masharti yaliyowekwa. Mwisho wa promosheni, majina ya washiriki wanaokidhi vigezo yataingia kwenye droo, huku washindi watatu wakipata Samsung Galaxy A26 mpya kabisa.
Lakini kabla ya kuanza kuota kuhusu simu mpya mfukoni, kuna masharti muhimu ya kuzingatia. Kila mtumiaji anaruhusiwa nafasi moja pekee kwa kila anuani, huku dau za Turbocash na System Ticket zikiwa nje ya promosheni hii. Kwa hiyo, hakikisha kila hatua unayochukua inafuata masharti ili usikose nafasi yako kwenye kinyang’anyiro cha zawadi.
Hatua inayofuata iko mikononi mwako. Jisajili au ingia Meridianbet, endelea kufurahia michezo yako pendwa na jiweke kwenye nafasi ya kuwania mojawapo ya Samsung Galaxy A26 tatu. Washindi watakuwa watatu, lakini nafasi ya kuwa mmoja wao inaanza na wewe kushiriki kwa usahihi.
Deportivo La Coruña itakuwa mwenyeji wa Sevilla katika mchezo wa LaLiga utakaopigwa leo Jumatano, Septemba 16, kwenye Uwanja wa Abanca-Riazor. Kuanzia majira ya saa 20:00 usiku, ukiwa ni mchezo wa raundi ya 6 ya La Liga msimu huu.
Deportivo inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na mwanzo mzuri tangu waliporejea LaLiga, ikiwa bado haijapoteza katika michezo yake ya mwanzo. Kikosi hicho cha Antonio Hidalgo kimeonyesha ushindani mkubwa, huku Pierre-EmerickAubameyang akiwa mmoja wa wachezaji wanaoleta tofauti baada ya kuanza msimu kwa kufunga mara kwa mara.
Deportivo de A Coruña, hali ya timu kwa sasa ni ya kuridhisha. Katika raundi 4 za ligi, timu hii ilipata ushindi mechi 2 na sare 3, ikiwa haijafungwa hata mara moja, ikiwa na pointi 9 ikishika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi.
Katika mchezo wa raundi ya 5, Deportivo ilishinda ugenini 3-2 dhidi ya Villarreal, hali ya mashambulizi ni nzuri. Mshambuliaji waoAubameyang amefunga mabao 4 na kutoa pasi 2 za mabao katika raundi 4 za ligi, akiwa mchezaji muhimu zaidi wa timu.
Kwa upande wa Sevilla, imeanza msimu kwa nguvu. Katika raundi 5 za ligi, Sevilla ilipata ushindi mechi 3 na kufungwa mchezo 1, ikiwa na pointi 10 ikishika nafasi ya tano kwenye msumamo wa ligi.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Hata hivyo, Sevilla inakabiliwa na tatizo la majeraha ya wachezaji, Mlinzi MsenegalArouna Sangante kutokana na jeraha la kifundo cha mguu hatakuwa katika mchezo huu, wakati Rubén Vargas pia anaendelea kukosekana kutokana na jeraha.
Rekodi ya michezo ya timu hizi mbili, Sevilla ina faida kubwa. Katika michezo 5 ya mwisho, Sevilla ilipata ushindi kwenye michezo 3 na sare 2, Deportivo haikupata ushindi wowote.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na uwezo wa Deportivo kutumia faida ya uwanja wa nyumbani na kasi waliyonayo katika mashambulizi. Sevilla, kwa upande mwingine, itahitaji kutumia uzoefu wake na kuwa makini dhidi ya safu ya ushambuliaji ya wenyeji, hasa Aubameyang ambaye tayari ameonyesha kuwa tishio kubwa msimu huu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amepokea mwaliko wa kushiriki katika dua maalum ya kuwaombea viongozi wa nchi na kuliombea Taifa kutokana na matarajio ya mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya El Niño
Rais Dkt. Mwinyi amepokea mwaliko huo leo, tarehe 16 Septemba 2026, Ikulu Zanzibar, alipokutana na uongozi wa Almadrasat Swifat Nabawiyatil Karimah, Msolopa Kilimani.
Dua hiyo inatarajiwa kufanyika Ijumaa, tarehe 18 Septemba 2026, ikilenga kumuomba Mwenyezi Mungu kuwalinda viongozi, Taifa na wananchi wake, pamoja na kuliepusha Taifa na madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua kubwa.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameridhia ombi la madrasa hiyo la kuongeza nafasi za Hijja kutoka tatu zilizotolewa mwaka jana hadi sita mwaka huu.
Rais Dkt. Mwinyi ameipongeza taasisi hiyo kwa kuendelea kushiriki katika shughuli za kumuombea Mwenyezi Mungu amani, ustawi na maendeleo ya nchi, huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano wa kijamii na kiroho.
Naye, Amir Mkuu wa Almadrasat Swifat Nabawiyatil Karimah, Alhaj Sheikh Muhammad Salum Muhammed, amemshukuru Rais Dkt. Mwinyi kwa kupokea mwaliko huo na kukubali ombi la kuongeza nafasi za Hijja kutoka tatu hadi sita, akieleza kuwa hatua hiyo imepokelewa kwa shukrani kubwa na uongozi wa madrasa.