Manchester United Yakamilisha dili la Carlos Baleba kwa Bilioni 253

Global Publishers
August 22, 2026
414 views
0 Comments

MANCHESTER: Manchester United imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa Brighton, Carlos Baleba, kwa ada ya jumla ya pauni milioni 70 sawa na  TSh bilioni 253.2.

Manchester United imekubali kulipa pauni milioni 65 pamoja na pauni milioni 5 zitakazotokana na vigezo maalum vya mkataba, huku Brighton ikikubali ofa hiyo.

Baleba, mwenye umri wa miaka 22, amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu na uhamisho wa kwenda Old Trafford, na sasa amefanya hatua muhimu kuelekea kujiunga na kikosi cha Manchester United.

Mchezaji huyo alisafiri kwenda Manchester Ijumaa usiku kwa ajili ya vipimo vya afya, hatua ambayo inatarajiwa kutanguliwa na kusaini mkataba wake mpya.

Baleba anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano, ukiwa na chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi. Brighton pia imeweka kipengele cha kupata sehemu ya fedha endapo mchezaji huyo atauzwa na Manchester United hapo baadaye.

Hata hivyo, kiungo huyo kwa sasa yuko nje ya uwanja kutokana na jeraha la kifundo cha mguu alilolipata katika mchezo wa kirafiki wa maandalizi ya msimu dhidi ya Strasbourg.

Mazungumzo kati ya Manchester United na Brighton yalirejea baada ya vipimo kuonyesha kuwa jeraha hilo, alilolipata mwanzoni mwa Agosti, halikuwa kubwa kama ilivyohofiwa awali.

Baleba anatarajiwa kurejea uwanjani mwishoni mwa Septemba, huku Manchester United ikimtarajia kuongeza nguvu na ushindani katika eneo la kiungo.

Usajili huo unaongeza chaguo la kocha Michael Carrick katika eneo la kiungo, wakati Manchester United ikiendelea kujenga kikosi chenye ushindani zaidi kwa msimu mpya.

Mradi mpya kupunguza msongamano bandari ya Dar – HabariLeo

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema eneo la Kurasi Logistics Park linatarajiwa kuanza kutumika kama sehemu ya upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam (Port Extension) kuanzia Novemba mwaka huu, hatua inayolenga kupunguza msongamano bandarini na kuongeza ufanisi wa huduma za mizigo.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya eneo hilo, Prof. Mbarawa amesema Serikali imekubaliana kulitumia eneo hilo si kama Kituo Kikuu cha Mizigo ya Nchi Kavu (ICD), bali kama sehemu ya bandari ambako shughuli za ukaguzi, uondoaji wa mizigo na huduma nyingine za Serikali zitafanyika.

Amesema matumizi ya eneo hilo kama Port Extension yatawezesha baadhi ya makontena kushushwa katika Bandari ya Dar es Salaam na kuhamishiwa Kurasi Logistics Park, ambako taratibu za ukaguzi na uondoshaji wa mizigo zitafanyika.

“Lengo kubwa ni kuhakikisha tunatumia eneo hili kama sehemu ya bandari ili kupunguza sana msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam. Mzigo utashukia pale bandarini, lakini clearance yote itafanyika hapa,” amesema Prof. Mbarawa.

Ameeleza kuwa ili mpango huo utekelezwe kwa ufanisi, Serikali imeweka masharti kadhaa, ikiwemo kuwepo kwa mobile scanners katika eneo hilo ili mizigo inayohamishiwa Kurasi ikaguliwe bila kulazimika kurudi bandarini.

Pia, amesema barabara inayounganisha Bandari ya Dar es Salaam na Kurasi Logistics Park itapaswa kutambuliwa kama Customs Bonded Road, ili kuwezesha usafirishaji salama wa mizigo kutoka bandarini hadi eneo hilo chini ya usimamizi wa mamlaka husika.

Prof. Mbarawa amesema Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imeelekezwa kushirikiana na TARURA, TANROADS na Halmashauri kuhakikisha barabara hiyo inakuwa maalumu kwa ajili ya usafirishaji wa mizigo kutoka bandarini kwenda Kurasi.

“Mzigo ukitoka bandarini hautapita kwenye scanner pale. Utakuja kuscaniwa hapa. Ili kufanya hivyo, lazima barabara ile iwe Customs Bonded Road, TRA iweidhinishe na iwekwe mifumo ya ulinzi na ufuatiliaji,” amesema.

Kwa mujibu wa Waziri Mbarawa, awali eneo hilo lilikuwa limekusudiwa zaidi kwa ajili ya kuhifadhia makontena, lakini Serikali sasa inalenga kulifanya kuwa sehemu ya shughuli za bandari ili kuongeza uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam kuhudumia mizigo inayoongezeka.

Amesema kwa kuanzia, eneo hilo litatumika kuhudumia makontena ya mizigo inayoingia nchini (import containers), huku mpango wa kushughulikia mizigo ya nje (export containers) ukifuatia baada ya changamoto zilizopo kutatuliwa.

Prof. Mbarawa amesema endapo maandalizi yataenda kama yalivyopangwa, kufikia Novemba eneo hilo litakuwa limekamilika kwa matumizi kama Port Extension, huku TPA, TRA na taasisi nyingine za Serikali zitakazohusika na huduma za mizigo zikiwa na uwepo katika eneo hilo.

Ameongeza kuwa hatua hiyo itasaidia wananchi kupata mizigo yao kwa haraka zaidi, huku ikipunguza msongamano wa magari na makontena katika Bandari ya Dar es Salaam na kuongeza ufanisi wa bandari hiyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Abed Galus Abed, amesema kuongezeka kwa shughuli za bandari na ukuaji wa mji kumeongeza changamoto za msongamano wa malori na mizigo katika maeneo yanayozunguka bandari.

Amesema Serikali imeendelea kuweka miundombinu kama Kurasi Logistics Park ili kuwa na uwezo wa kuhifadhi malori na mizigo kabla ya kuondoka katika Bandari ya Dar es Salaam.

Abed amesema ongezeko la shughuli za bandari limekuwa kubwa, akieleza kuwa katika kipindi cha miaka ya karibuni kumekuwa na ongezeko la takribani tani milioni sita za mizigo, hali ambayo imeongeza shinikizo kwenye miundombinu ya barabara.

Ameahidi kuwa mamlaka husika itatekeleza maelekezo yaliyotolewa na Waziri Mbarawa ili kuhakikisha eneo hilo linaanza kutoa huduma na kusaidia kupunguza msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam.

Tanzania Yaendelea Kung’ara Miss World, Latricia Ian Afuzu Top 60

Global Publishers
August 22, 2026
486 views
0 Comments

Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Miss World 2026, Latricia Ian, amefanikiwa kuingia kwenye orodha ya warembo 60 bora katika kipengele cha Top Model, hatua inayomuweka katika nafasi nzuri ya kuwania ushindi wa kipengele hicho nchini Vietnam.

Ian amefuzu miongoni mwa washiriki kutoka mataifa mbalimbali duniani, akiendelea kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo yanayowakutanisha warembo kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, fainali ya kipengele cha Top Model inatarajiwa kufanyika Agosti 28, 2026, ambapo warembo hao 60 watashindana katika hatua ya mwisho ya kipengele hicho.

Mbali na Top Model, washiriki wote 111 wanaowakilisha mataifa yao watapata nafasi ya kutembea kwenye jukwaa katika kuwania World Designer Award, huku wakionyesha mitindo na utambulisho wa maeneo yao ya kijiografia.

Kwa upande wa Tanzania, kufuzu kwa Latricia Ian katika Top 60 ni hatua nyingine muhimu katika safari yake ya Miss World 2026, huku akitarajiwa kuendelea kupambana katika hatua zinazofuata za mashindano hayo.

Macho ya mashabiki wa Tanzania sasa yanaelekezwa Agosti 28, wakati Ian atakapokuwa akiwakilisha Tanzania katika hatua ya fainali ya Top Model.

Stori na Ilankize Godfrey | GPL – TUDACO

Kairuki apongeza upanuzi huduma za intaneti – HabariLeo

DAR ES SALAAM: Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, amesema upanuzi wa huduma za intaneti kupitia mkongo wa Taifa wa fiber optic ni hatua muhimu ya kufungua fursa za elimu, ajira, biashara, ubunifu na huduma bora kwa wananchi

Kairuki amesema hayo Leo wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa Fiber Mlangoni kwa Mteja (FTTH) wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), akieleza kuwa mradi huo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kujenga uchumi wa kidijitali na kuhakikisha teknolojia inakuwa chachu ya maendeleo ya wananchi.

Amesema Serikali inataka kuona miundombinu hiyo ikimuwezesha mwanafunzi kujifunza kwa kutumia teknolojia, mfanyabiashara kufikia masoko mapya na taasisi za umma kutoa huduma kwa wananchi kwa haraka, kwa gharama nafuu na kwa ufanisi zaidi.

Ameongeza kuwa huduma za intaneti zenye kasi pia zinaweza kupunguza gharama na muda ambao wananchi hutumia kusafiri kufuata huduma mbalimbali, hususan pale huduma hizo zinapopatikana kupitia mifumo ya kidijitali.

Aidha amesema hadi Juni 2026, idadi ya watumiaji wa intaneti nchini ilifikia milioni 62.7, huku matumizi ya data yakiongezeka hadi kufikia petabyte 1,041 huku matumizi ya fiber majumbani bado yako katika kiwango cha chiniu ikilinganishwa na idadi kubwa ya watumiaji wa intaneti nchini, akitaja kuwa watumiaji wa fiber majumbani walikuwa takribani 178,904.

Kwa upande Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Moremi Marwa amesema kutokana na ongezeko la mahitaji ya huduma za intaneti na umuhimu wa mawasiliano katika shughuli za kiuchumi na kijamii, TTCL imeanzisha awamu ya pili ya mradi huo ili kuhakikisha huduma za Fiber Mlangoni kwa Mteja zinapatikana katika maeneo mbalimbali nchini.

Ameeleza kuwa katika awamu ya pili, TTCL inalenga kujenga takribani maunganisho 400,000 ya Home Pass, hatua ambayo inatarajiwa kuongeza jumla ya uwezo wa mtandao wa shirika hadi kufikia takribani maunganisho 750,000 ifikapo Juni 2027.

Aidha, amesema mpango wa TTCL ni kufikisha idadi hiyo hadi takribani maunganisho milioni moja ifikapo Juni 2028, ikiwa sehemu ya mpango wa miaka mitatu wa shirika katika kuimarisha huduma za mawasiliano nchini.

Mradi wa Julius Nyerere Watikisa Sekta ya Nishati kwa MW 2,115

Global Publishers
August 22, 2026
78 views
0 Comments

Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) umeingia katika hatua muhimu katika historia ya sekta ya nishati nchini Tanzania, baada ya kufikia uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 za umeme.

Mradi huo uliopo Rufiji, Mkoa wa Pwani, unatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho, Agosti 22, 2026, katika hafla itakayowakutanisha viongozi pamoja na wadau mbalimbali.

JNHPP umegharimu takribani Shilingi trilioni 7.452, huku ukielezwa kuwa miongoni mwa miradi mikubwa zaidi ya uzalishaji umeme kutekelezwa nchini kwa kutumia fedha za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Nishati, mradi huo tayari umeanza kutoa mchango mkubwa katika Gridi ya Taifa. Katika kipindi kilichoishia Mei 31, 2026, JNHPP ulichangia takribani asilimia 44.9 ya umeme wote uliozalishwa na kuingizwa kwenye gridi.

Uwezo huo unatarajiwa kusaidia kukidhi ongezeko la mahitaji ya umeme nchini, ambayo yalifikia kiwango cha juu cha takribani MW 2,199.06 Februari 4, 2026.

Mradi wa Julius Nyerere unatarajiwa kuwa na nafasi kubwa katika kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini, pamoja na kusaidia shughuli za uzalishaji, biashara na ukuaji wa uchumi.

Uzinduzi rasmi wa mradi huo kesho unatajwa kuwa hatua muhimu katika historia ya sekta ya nishati Tanzania, huku Serikali ikiendelea kuweka mkazo katika kuongeza uzalishaji wa umeme na kuimarisha uwezo wa Gridi ya Taifa.

Stori na Anifa Mwegelo | GPL – TUDACO

Dogo Janja Afunguka Kuhusu Ndoa yake na Irene Uwoya – Video

Global Publishers
August 22, 2026
42 views
0 Comments

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende maarufu Dogo Janja, amefunguka kuhusu historia ya uhusiano wake na staa wa Bongo Movie, Irene Uwoya, akieleza ukweli kuhusu ndoa yao iliyowahi kuzungumziwa kwa kiasi kikubwa katika tasnia ya burudani.

Dogo Janja aliingia katika muziki akiwa katika umri mdogo na baadaye akawa miongoni mwa wasanii waliojitengenezea jina katika muziki wa Bongo Fleva. Uhusiano wake na Irene Uwoya uliwahi kuvuta perhatian kubwa kutokana na tofauti ya umri kati yao.

Taarifa za wakati huo zilieleza kuwa wawili hao walifunga ndoa ya Kiislamu, huku maisha yao ya ndoa yakifuatiliwa kwa karibu na mashabiki na vyombo vya habari vya burudani.

Katika mahojiano yaliyowahi kuchapishwa, Dogo Janja pia aliwahi kusema kuwa alimuoa Uwoya akiwa na umri wa miaka 22.

Hata hivyo, ndoa hiyo haikudumu kwa muda mrefu, na baadaye wawili hao wakaachana huku kila mmoja akiendelea na maisha yake.

Kwa miaka kadhaa, suala la iwapo ndoa hiyo ilikuwa ya kweli au la limeendelea kuibua mijadala, huku taarifa mbalimbali za wakati huo zikithibitisha kuwa wawili hao waliishi kama wanandoa.

Sasa, Dogo Janjaro anaeleza upande wake kuhusu historia hiyo na namna alivyowahi kuingia kwenye ndoa akiwa bado kijana katika safari yake ya muziki.

Roboti Yaanguka Kwa Hitilafu ya Umeme Wakati wa Mazoezi

Global Publishers
August 22, 2026
60 views
0 Comments

Beijing, China — Maandalizi ya mashindano ya World Humanoid Robot Games 2026 yamekumbwa na tukio lisilotarajiwa baada ya roboti kutoka kampuni ya Unitree kupata hitilafu wakati wa majaribio.

Roboti hiyo ilionekana kushindwa kusimama kwa usawa baada ya kukimbia kwa kasi, kabla ya kuporomoka chini na kupata hitilafu kwenye mfumo wake wa umeme.

Tukio hilo limeibua mjadala kuhusu changamoto zinazokabili watengenezaji wa roboti humanoid, hususan katika kuhakikisha vifaa hivyo vinaweza kudhibiti kasi na kusimama kwa usalama vinapofanya shughuli zinazofanana na za binadamu.

Hata hivyo, hadi sasa hakuna taarifa rasmi inayoonyesha kuwa roboti hiyo imeharibika kabisa kutokana na tukio hilo.

Wataalamu wa teknolojia wanaeleza kuwa matukio ya aina hiyo yanaweza kujitokeza wakati wa majaribio ya roboti, hasa katika hatua za kujaribu uwezo wake wa kukimbia, kubadilisha mwelekeo na kudhibiti mwendo kwa kasi.

World Humanoid Robot Games 2026 inatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kuonyesha maendeleo katika teknolojia ya roboti humanoid, huku kampuni na washiriki kutoka maeneo mbalimbali duniani wakijiandaa kuonyesha uwezo na ubunifu wao.

Tukio hilo pia linaonyesha kuwa licha ya maendeleo makubwa katika teknolojia ya roboti, bado kuna changamoto za kiufundi zinazohitaji kutatuliwa ili roboti ziweze kufanya kazi kwa usalama na ufanisi zaidi.

Stori na Clever Alphonce

Miaka 11 Baada Ya Kustaafu, Ronaldinho Arejea Kwenye Soka

Milan, Italia — Mwanasoka nguli wa Brazil, Ronaldinho Gaúcho, anatarajiwa kurejea rasmi uwanjani akiwa na umri wa miaka 46, miaka 11 baada ya kucheza mchezo wake wa mwisho wa soka la ushindani.

Ronaldinho amefikia makubaliano na Ravenna FC, klabu ya Italia inayoshiriki Serie C, ambapo atahusishwa na klabu hiyo si tu kama mwekezaji, bali pia kama mchezaji.

Mpango huo unalenga kumrudisha nyota huyo wa zamani uwanjani kwa mara nyingine, huku akipewa nafasi ya kuandika ukurasa wa mwisho wa safari yake ya soka kwa kujaribu kufunga bao akiwa amevalia jezi ya Ravenna.

Hata hivyo, hadi sasa tarehe rasmi ya mchezo ambao Ronaldinho atarejea uwanjani haijatangazwa.

Ronaldinho, ambaye alistaafu soka baada ya kucheza mchezo wake wa mwisho akiwa na Fluminense mwaka 2015, sasa anarejea katika kipindi ambacho Ravenna inashiriki Serie C, daraja la tatu la soka nchini Italia.

Klabu hiyo pia inalenga kutumia jina na umaarufu wa Ronaldinho kuongeza mvuto wake kimataifa na kusaidia katika mpango wake wa kujenga upya timu.

Ronaldinho ni miongoni mwa wanasoka walioacha alama kubwa katika historia ya mchezo huo. Akiwa na Barcelona, alitwaa Ballon d’Or mwaka 2005 na kusaidia klabu hiyo kushinda UEFA Champions League mwaka 2006.

Pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Brazil kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 2002, akicheza pamoja na nyota wengine wakubwa wa kizazi chake.

Iwapo atashuka uwanjani kama ilivyopangwa, kurejea kwa Ronaldinho akiwa na miaka 46 kutakuwa tukio la kipekee kwa mashabiki wa soka duniani, hasa wale waliovutiwa na kipaji chake cha kipekee wakati wa enzi zake.

STORI NA RAZAKU RAMADHAN, GPL – TUDACO

Siri Nzito! Ndege Ya Malaysia Iliyopotea Angani, Haijulikani Ilipoelekea-Video

Shechambo Chris
August 21, 2026
948 views
0 Comments

Tarehe 8 Machi 2014, ndege ya Malaysia Airlines aina ya Boeing 777 iliondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur kuelekea Beijing, China.

Ndani ya ndege hiyo kulikuwa na watu 239, abiria 227 pamoja na wafanyakazi 12 wa ndege,safari ilianza kawaida, bila taarifa yoyote ya tatizo kubwa. takribani dakika 40 baada ya kuruka, ndege hiyo ilipotea kwenye mifumo ya kawaida ya rada.

Maneno ya mwisho yaliyosikika kutoka kwenye chumba cha marubani yalikuwa “Good night, Malaysian three seven zero.” Kisha mawasiliano yakakatika.

Lakini kilichofuata ndicho kilichoufanya ulimwengu kuanza kujiuliza maswali makubwa.

Transponder ya ndege ilizimwa, na ndege ikaacha kufuata njia yake ya kawaida kuelekea Beijing, badala yake, Boeing 777  ilibadilisha mwelekeo na kuanza kuruka kuelekea magharibi.

Kwa muda mfupi, ndege hiyo iliendelea kuonekana kwenye mifumo ya rada za kijeshi. Hata hivyo, hakuna mawasiliano ya kawaida yaliyokuwa yakipatikana kutoka kwenye ndege .

Swali likawa moja Kwa nini ndege iliyokuwa na watu 239 ilibadilisha njia ghafla na kutoweka bila kutoa tahadhari?



Luizer awasihi wanawake kutunza ngozi – HabariLeo

MSANII wa muziki wa dansi, Luizer Nyoni Mbutu, amewashauri mabinti na wanawake kuthamini na kutunza ngozi zao kwa kuepuka matumizi ya bidhaa zinazoweza kuathiri afya ya ngozi. Akizungumza na Daily News Digital, Luizer amesema amewahi kukumbana na changamoto hiyo baada ya kushawishiwa na rafiki yake kutumia bidhaa iliyosababisha ngozi yake kuharibika.

Amesema licha ya kuwa si rahisi kuacha matumizi ya bidhaa hiyo, kwa sasa ngozi yake imeanza kuimarika na kurejea katika hali yake ya awali.Kutokana na uzoefu huo, amewataka wanawake kujipenda na kutokubali shinikizo la kubadilisha mwonekano wa ngozi zao kwa kutumia bidhaa bila kufahamu madhara yake.

“Akili za kuambiwa changanya na zako. Uzuri si kujichubua, ni wewe mwenyewe kukipenda na kuithamini ngozi uliyonayo,” amesema Luizer. Amesisitiza umuhimu wa kuchagua bidhaa salama na kuwa makini na ushauri wanaoupata kuhusu utunzaji wa ngozi. SOMA: Mungu ndiye nguvu ya mafanikio