Macho Yote Brighton! Arsenal Yalenga Kuendeleza Kasi EPL

Global Publishers
September 19, 2026
48 views
0 Comments

Ni siku nyingine tena ya kushuhudia miamba kibao ikishuka dimbani leo kwenye Ligi kuu ya EPL. Je ni Arsenal kujihakikishia nafasi ya kwanza kwenye msimamo au Brighton watawashika shati mabingwa hao? Jisajili na ubashiri hapa.

Brighton & Hove Albion leo Jumamosi Septemba 19 wataikaribisha Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu England, EPL, utakaopigwa kuanzia saa 17:00 jioni. Pambano hilo linatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa vikosi hivyo na umuhimu wa pointi tatu.

Arsenal wataingia uwanjani wakiwa na lengo la kuendeleza kasi yao nzuri ya mwanzo wa msimu. Kikosi hicho cha Mikel Arteta kimeonyesha ushindani mkubwa katika michezo ya awali na sasa kitakuwa na kazi ya kuhakikisha kinapata matokeo mazuri dhidi ya Brighton kwenye uwanja wao.

Kwa upande wa Brighton, mchezo huo utakuwa nafasi ya kutumia faida ya kucheza mbele ya mashabiki wao. Timu hiyo pia imeonyesha uwezo wa kupata matokeo, jambo linalofanya Arsenal kutarajiwa kukutana na upinzani mkubwa katika dakika zote 90.

Macho pia yataelekezwa kwa safu za ushambuliaji za timu zote, huku kila upande ukihitaji kutumia nafasi utakazopata. Brighton wanahitaji kuwa makini katika kuzuia mashambulizi ya Arsenal.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kwa ujumla, pambano hili linatarajiwa kuwa moja ya michezo yenye mvuto katika ratiba ya EPL mwishoni mwa wiki. Brighton watakuwa wakisaka pointi mbele ya mashabiki wao, huku Arsenal wakilenga kuondoka na matokeo yatakayowaweka katika mwendo mzuri wa msimu.

Ndejembi Atoa Agizo Mto Ng’ombe, Taka Ziondolewe Haraka – Picha

Global Publishers
September 19, 2026
0 views
0 Comments


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, tarehe 18 Septemba 2026, amefanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Mto Ng’ombe, Tandale jijini Dar es Salaam, kukagua hali ya usafi wa mazingira na maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza katika kipindi cha mvua.

Akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Waziri wa TAMISEMI pamoja na viongozi wa Wilaya ya Kinondoni, Ndejembi ameelekeza Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha mto huo unasafishwa na taka zilizorundikana kandokando ya Mto Ng’ombe zinaondolewa haraka na mazingira yanaendelea kuwekwa katika hali ya usafi.

Amewaagiza Viongozi wa Halmshauri, kupitia maafisa mazingira na maafisa maendeleo, kuendelea kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuzingatia usafi na ukusanyaji wa taka. Amesema ni muhimu kwa Halmashauri kuweka miundombinu mizuri ya kukusanya taka na kuzichukua kwa wakati ili wananchi wasitupe taka hizo katika maeneo yasiyofaa.

Vilevile, ameelekeza mamlaka za Wilaya ya Kinondoni kuweka utaratibu wa maeneo rasmi ya kutupa taka ili wananchi wawe na sehemu zinazotambulika kwa ajili ya kuhifadhi taka, hatua itakayosaidia kudhibiti utupaji holela na uchafuzi wa mazingira.

Akizungumza na wananchi wanaoishi pembezoni mwa Mto Ng’ombe, Makamu wa Rais amewataka kuzingatia usafi wa mazingira na kubadili tabia ya utupaji taka holela, akisisitiza kuwa utunzaji wa mazingira unahitaji ushiriki wa Serikali na wananchi kwa pamoja.

Aidha, Makamu wa Rais ameelekeza madaraja yanayokatiza maeneo ya Pakacha na Sokoni katika Mto Kiboko yanapitika wakati wa mvua, ili wananchi waendelee kufanya shughuli zao za kijamii na kiuchumi bila kukwamishwa na changamoto za miundombinu.

MKARUDI NA USHINDI- ADA- MLINGA*

Dodoma
TIMU za Maliasili Sports Club  zimetakiwa kuhakikisha  zinacheza kwa nguvu, juhudi na maarifa  michezo yote katika Michuano ya SHIMIWI 2026 ili kuhakikisha zinaipatia Wizara ya Maliasili na Utalii ushindi wa hali ya juu. 
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo Bi. Violeth Mlinga wakati akiiaga timu hiyo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi kabla ya  kuanza safari yao kuelekea Moshi,  Mkoani Kilimanjaro. 
Bi. Mlinga amesisitiza kuwa, Wizara hiyo imeiamini Club hiyo hivyo wachezaji wana wajibu wa kuzingatia weledi na taratibu zote za Utumishi wa Umma ili kulinda taswira ya Wizara hiyo ili kuibuka na matokeo chanya ambayo ni ushindi kwa timu zote. 
Ameongeza kuwa, ushiriki wa Wizara hiyo katika michuano hayo ni sehemu ya kuongeza wigo si tu wa kutangaza shughuli za Wizara bali  kujenga pia uhusiano mwema wa kiutumishi na Wizara zingine kwa maslahi mapana ya taifa kwa ujumla. 
Naye Mkwenyekiti wa Club hiyo Bw. Elia Mtalemwa, amesema Club hiyo imejiandaa vyema na kuwa lengo kuu ni kurudi na ushindi katika michezo yote kama walivyoelekezwa. 
Pamoja na kuushukuru uongozi wa Wizara kwa mchango mkubwa katika maandalizi na ushiriki wa Club hiyo, amesema  timu zote zimejiandaa vyema na kuwa lengo lao kuu ni ushindi kwenye michezo yote. 
Maliasili Sports Club, inaelekea Moshi Mkoani Kilimanjaro kuungana na Wizara zingine kuoneshana ubabe katika Michuano ya SHIMIWI itakayoanza hivi karibuni.

 

MAKAMU WA RAIS AAGIZA MAWAZIRI WATATU KUTATUA MGOGORO WA MIPAKA PUGU NDANI YA SIKU SABA

Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amewaagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Waziri wa Maliasili na Utalii kufika ndani ya siku saba katika Dampo la Pugu kwa ajili ya kutatua mgogoro wa muda mrefu wa wananchi kuhusu mipaka ya kiutawala na mpaka wa Msitu wa Kazimzumbwi.

Makamu wa Rais ametoa agizo hilo Septemba 18, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na wananchi wa Pugu mara baada ya kufanya ziara katika Dampo la Pugu, linalohudumia Mkoa wa Dar es Salaam kwa kupokea taka, na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi wa eneo hilo.

“Nikiwa Dampo kuna wazee wangu waliwasilisha malalamiko juu ya kubuguziwa katika Msitu wa Kazimzumbwi, wakidai hawajui kama wako eneo gani la utawala, Pwani au Dar es Salaam. Hivyo, ninawaelekeza Mawaziri wa TAMISEMI, Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wa Maliasili na Utalii kuhakikisha ndani ya siku saba wawe wamefika hapa kutatua changamoto hiyo ya wananchi kubuguziwa,” amesema Mhe. Ndejembi.

Aidha, Mhe. Ndejembi amewataka mawaziri hao watakapofika katika eneo hilo kuzungumza na wananchi na kuhakikisha katika kutatua changamoto hiyo wanatumia taarifa rasmi ya Serikali kuhusu mipaka ya kiutawala, yaani Government Notice (GN) iliyochapishwa katika Gazeti la Serikali, kama msingi wa kubaini mipaka husika.

Akizungumza kwa niaba ya mawaziri wenzake, Waziri wa Nchi, OWM–TAMISEMI, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, ameahidi kutekeleza maelekezo hayo ya Makamu wa Rais kwa kufika katika eneo hilo ndani ya siku saba na kuzungumza na wananchi kwa ajili ya kutafuta suluhisho la mgogoro huo.

“Mhe. Makamu wa Rais, tumepokea maelekezo yako ya kutatua mgogoro huu wa wananchi wa mipaka ya kiutawala na Msitu wa Kazimzumbwi ndani ya siku saba. Hivyo, mimi Prof. Riziki Shemdoe, Waziri wa TAMISEMI, Dkt. Akwilapo, Waziri wa Ardhi, na Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Maliasili, tutakuja kuzungumza na wananchi ili kutatua mgogoro huo,” amesema Prof. Shemdoe.

Aidha, Prof. Shemdoe ameahidi kutekeleza maelekezo ya Makamu wa Rais ya kuzisimamia Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam kuleta vitendea kazi, ikiwemo tingatinga (bulldozer), kwa ajili ya kuboresha mazingira na kuongeza ufanisi wa huduma ya upokeaji wa taka katika Dampo la Pugu.

Prof. Shemdoe amesema tayari amemwelekeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuanza kufuatilia utekelezaji wa agizo hilo ili kuhakikisha vitendea kazi vinapatikana na hatua zinazohitajika zinachukuliwa.

Prof. Shemdoe ametumia fursa hiyo kumshukuru na kumpongeza Makamu wa Rais, Mhe. Deogratius Ndejembi, kwa kufanya ziara katika Dampo la Pugu, kusikiliza kero za wananchi na kutoa maelekezo ya hatua za haraka kuchukuliwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa dampo hilo linalohudumia Mkoa wa Dar es Salaam.

CCM Yapongeza ACT-Wazalendo Kuwasilisha Jina la Makamu wa Kwanza

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimepongeza uteuzi wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, kikisema hatua hiyo imekamilisha muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kisiwandui, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo Zanzibar, Khamis Mbeto Hamisi, amesema CCM imempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kutekeleza matakwa ya Katiba.

Mbeto pia amepongeza Chama cha ACT-Wazalendo kwa kuwasilisha jina la mgombea kwa nafasi hiyo, akisema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa misingi ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Amesema kwa mujibu wa Ibara ya 39 ya Katiba ya Zanzibar, Serikali hiyo inatakiwa kuwa na Makamu wa Kwanza na Makamu wa Pili wa Rais, pamoja na majukumu yao yaliyoainishwa kikatiba.

Kwa mujibu wa Mbeto, ACT-Wazalendo sasa inapaswa kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa kuzingatia Katiba na sheria za Zanzibar.

Amesema CCM inatarajia viongozi watakaounda Serikali hiyo, wakiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais na mawaziri, kufanya kazi kwa kuzingatia maslahi ya wananchi, Dira ya Taifa ya 2050 pamoja na mipango ya maendeleo ya Zanzibar.

Mbeto amesisitiza umuhimu wa viongozi wa kisiasa kutumia kauli zinazojenga umoja na mshikamano, huku akivitaka vyama vya siasa na wafuasi wao kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii ili kuepuka kauli zinazoweza kuleta mgawanyiko.

Amesema licha ya vyama kuendelea na shughuli zao za kisiasa, wanapaswa kutambua kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa inalenga kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar.

CCM imesema iko tayari kushirikiana na viongozi wote wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, wakiwemo Rais, Makamu wa Kwanza wa Rais, Makamu wa Pili wa Rais, mawaziri na watendaji wengine, katika kuhakikisha serikali inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Mbeto amesema ushirikiano huo unalenga kuimarisha umoja, mshikamano na maendeleo ya Zanzibar, huku akiwataka viongozi na wananchi kutumia fursa hiyo kujenga mazingira yatakayowezesha Zanzibar kupata maendeleo zaidi.

Makamu wa Rais Ndejembi Aungana na Wananchi Kufanya Mazoezi Dar

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi ameungana na wananchi mbalimbali kufanya mazoezi ya asubuhi katika barabara ya fukwe za Coco beach kuelekea Daraja la Tanzanite, Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 19 Septemba 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameungana na wananchi mbalimbali kufanya mazoezi ya asubuhi katika barabara ya fukwe za Coco Beach kuelekea Daraja la Tanzanite, jijini Dar es Salaam.

Mazoezi hayo yamefanyika leo, Septemba 19, 2026, yakishirikisha wananchi katika kuimarisha afya na kuhamasisha mtindo bora wa maisha.

Taifa Stars Kuanza Kampeni ya AFCON 2027 Dhidi ya Guinea-Bissau

Global Publishers
September 19, 2026
978 views
0 Comments

TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inatarajiwa kuanza kampeni yake ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 kwa mchezo dhidi ya Guinea-Bissau.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Septemba 18, 2026, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Septemba 25, 2026 katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Baada ya mchezo huo, Taifa Stars inatarajiwa kusafiri Septemba 26 kuelekea Casablanca, Morocco, kwa ajili ya mchezo wa pili wa kampeni hiyo dhidi ya Madagascar.

Madagascar imechagua Morocco kuwa eneo la kuchezea kama mwenyeji wa mchezo huo, ambao unatarajiwa kufanyika Septemba 29, 2026.

Mbali na michezo hiyo ya kufuzu AFCON, Taifa Stars pia inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Ghana.

Mchezo huo wa kirafiki umepangwa kuchezwa Oktoba 4, 2026 jijini Casablanca, Morocco, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya timu hiyo kwa michezo yake ijayo.

Taifa Stars sasa inaelekeza nguvu katika maandalizi ya mchezo wa kwanza dhidi ya Guinea-Bissau, huku ikitarajiwa kutumia michezo hiyo kujenga msingi mzuri katika safari ya kuwania nafasi ya kushiriki AFCON 2027.

Stori Na Clever Alphonce | GPL -TUDACO

Wezesha Mzawa Insurance Broker Watangaza Nafasi Nne za Kazi

Kampuni ya Wezesha Mzawa Insurance Broker Limited imetangaza nafasi za kazi kwa Watanzania wenye sifa na uzoefu katika sekta ya bima, mauzo, masoko, biashara, uhasibu na nyanja zinazohusiana.

Nafasi zilizotangazwa ni Business Development Executive, Accountant pamoja na Insurance Sales Executives, huku waombaji wakitakiwa kutimiza vigezo vilivyowekwa kwa kila nafasi.

1. Business Development Executive

Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Kwanza katika Insurance and Risk Management, Sales and Marketing, Business Administration au fani nyingine inayohusiana, pamoja na uzoefu wa angalau miaka miwili katika sekta ya bima, maendeleo ya biashara, mauzo au masoko.

2. Accountant

Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Kwanza katika Accounting au Finance, pamoja na uzoefu wa angalau miaka miwili katika sekta ya bima. Sifa ya CPA ni nyongeza.

3. Insurance Sales Executives

Waombaji wanatakiwa kuwa na Cheti katika Insurance and Risk Management, Sales, Marketing, Business Administration au fani nyingine inayohusiana.

Uzoefu katika sekta ya bima na kazi za mauzo ni nyongeza.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi yao pamoja na viambatisho muhimu vilivyothibitishwa kupitia barua pepe au kwa anuani ya ofisi ya kampuni kabla ya Septemba 30, 2026.

Wezesha Mzawa Insurance Broker Limited
P.O. Box 7534, Sinza Mori
Global Group House/Building, Opposite Wanyama Hotel
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: [email protected]

MAGAZETINI LEO JUMAMOSI SEPT 19/2026:DCI KINGAI AMKATALIA LISU

 

 MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA 

 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)

1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

 

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

3:TUZO YA AFYA

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .