Europa League Kuamua! Salah Aongoza Trabzonspor Kwenye Mechi ya Marudiano

Ferencváros watawapokea Trabzonspor katika uwanja wa Groupama Arena, jijini Budapest, Hungary, Alhamisi Agosti 27, 2026, saa 21:30, katika mechi ya marudiano ya raundi ya kufuzu (play-off) ya UEFA Europa League msimu wa 2026/27. Ushindi katika mchezo huu utampeleka mshindi hatua ya makundi ya mashindano hayo.

Mechi ya kwanza iliyochezwa Trabzon, Uturuki, ilishuhudia Ferencváros wakishinda kwa bao 1-0. Bao pekee la mechi lilifungwa na Kristoffer Zachariassen kupitia kichwa katika dakika ya 17, akihudumiwa na Oliver Nagy.

Trabzonspor walimalizia mechi hiyo wakiwa na wachezaji 10 baada ya Chibuike Nwaiwu kuonyeshwa kadi nyekundu muda mfupi kabla ya mwisho wa mechi, jambo litakalomkosesha mchezo huu wa marudiano kwa sababu ya adhabu.

Mechi hiyo ya kwanza pia iliashiria mwanzo wa historia mpya kwa Trabzonspor, kwani nyota maarufu Mohamed Salah alicheza mchezo wake wa kwanza barani Ulaya kwa klabu hiyo baada ya kuhamia kutoka Liverpool.

Ingawa hakufunga bao, Salah alionyesha hatari kadhaa, ikiwemo jaribio lililomlazimu kipa Dénes Dibusz kufanya kazi mapema mechini. Matarajio ni kwamba ataanza tena mechi hii ya marudiano akiwa na hamu ya kufunga bao lake la kwanza la Ulaya.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Ferencváros, mabingwa watetezi wa ligi ya Hungary, wameonyesha uthabiti mkubwa msimu huu wa kufuzu, wakipita raundi tatu za awali kabla ya kufika hatua hii, wakiwemo dhidi ya Górnik Zabrze. Timu hiyo pia haijashindwa katika mechi zao za ughaibuni barani Ulaya msimu huu, jambo linalowapa Ferencváros faida ya kucheza nyumbani wakiwa na ubora wa bao moja.

Trabzonspor watahitaji kufunga angalau mabao mawili bila kujibiwa ili kufuzu, jambo litakalokuwa gumu zaidi baada ya kupoteza mchezaji mmoja kwa kadi nyekundu na kucheza ughaibuni dhidi ya timu isiyoshindwa nyumbani.

Hata hivyo, uwepo wa Salah na wachezaji wengine wenye uzoefu kama Paul Onuachu unaweza kuwapa matumaini ya kupata matokeo mazuri. Kwa ujumla, Ferencváros wanaingia mechini wakiwa vipendwa zaidi kufuzu, ingawa ubora mdogo wa bao moja unamaanisha mechi hii bado iko wazi kwa mshangao.

Watanzania 173 Warejea Nchini kwa Hiari Kutoka Afrika Kusini

Shechambo Chris
August 27, 2026
6 views
0 Comments

Raia 173 wa Tanzania waliokuwa wakiishi katika mkoa wa KwaZulu-Natal, Afrika Kusini, wamewasili nchini leo, Agosti 27, 2026, baada ya Serikali kuwawezesha kurejea kwa hiari.

Kundi hilo limesafirishwa kwa ndege maalumu kupitia ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Zoezi hilo liliratibiwa baada ya Serikali, kupitia Ubalozi wa Tanzania mjini Pretoria, kutoa wito kwa Watanzania waliokuwa tayari kurejea nyumbani kujisajili na kukamilisha taratibu za safari.

Mpango huo unatarajiwa kutekelezwa kwa awamu katika maeneo mbalimbali ya Afrika Kusini, kwa lengo la kuwawezesha Watanzania wanaohitaji kurejea nchini kufanya hivyo kwa usalama na utaratibu.

Miongoni mwa walionufaika na zoezi hilo ni Watanzania wasio na pasipoti, waliopoteza pasipoti zao au ambao muda wa matumizi ya pasipoti zao umeisha, pamoja na watoto waliozaliwa nchini Afrika Kusini.

Kwa wale wasio na pasipoti, Serikali imewawezesha kupata hati za dharura za kusafiria ili kuwawezesha kurejea nchini.

Hatua hiyo imekuja wakati kukiwa na ongezeko la hisia na maandamano dhidi ya wahamiaji nchini Afrika Kusini, hali ambayo imesababisha baadhi ya mataifa ya Afrika kuchukua hatua za kuwawezesha raia wao kurejea nyumbani.

Serikali ya Tanzania imeeleza kuwa zoezi hilo ni la hiari na linalenga kuwawezesha wananchi kurejea nchini kwa usalama na kwa kufuata taratibu.

Kurejea kwa raia hao ni sehemu ya juhudi za Serikali, kupitia uwakilishi wake wa kidiplomasia nchini Afrika Kusini, kuwasaidia Watanzania wanaohitaji kurejea nyumbani.

Ubalozi wa Tanzania mjini Pretoria pia hutoa huduma za dharura, masuala ya pasipoti na huduma nyingine za kibalozi kwa raia wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Na Ilankize Godfrey



*WMA WAKAGUA USAHIHI WA VIPIMO KWENYE VIWANDA VYA MABATI MKOANI MWANZA*

Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Mwanza umezitaka kampuni zinazojihusisha na uzalishaji wa mabati kuhakikisha zinazingatia matakwa ya sheria ya vipimo na viwango vya ubora vilivyowekwa, ili kulinda haki na fedha za wananchi.

Akizungumza mapema leo Agosti 27, 2026 mara baada ya zoezi la ukaguzi wa kushtukiza katika baadhi ya viwanda vya uzalishaji wa mabati mkoani Mwanza, Meneja wa Mkoa wa Wakala huo, Karim Zuberi, amesema kupitia kaguzi na taarifa zinazotolewa na wananchi, ndani ya kipindi cha mwaka huu, tayari wamebaini na kuchukua hatua dhidi ya wazalishaji watano waliobainika kuzalisha mabati yasiyokuwa na vipimo sahihi.

Zuberi amesema wananchi wanapaswa kuwa makini wanaponunua mabati na kutoa taarifa kwa mamlaka husika pindi wanapohisi kuuziwa bidhaa zisizokuwa na vipimo sahihi, akiwataka pia wafanyabiashara kuacha tabia ya kuwapotosha wateja kuhusu vipimo vya unene wa mabati.

Amesema baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakitoa taarifa zisizo sahihi kwa wateja kwa kuwafanya waamini kuwa kadri namba ya ‘Gauge’ inavyokuwa kubwa ndivyo bati linavyokuwa bora, wakati kinyume chake ndicho sahihi, ambapo bati lenye namba ndogo ya “Gauge’ huwa na unene mkubwa zaidi.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa wananchi kupata taarifa sahihi kuhusu viwango vya bidhaa wanazonunua ili kuepuka udanganyifu unaoweza kusababisha hasara, hususan katika ujenzi wa makazi na miundombinu mingine.

Kwa upande wake, Biyolelo Ndaisaba, mmoja wa viongozi wa kampuni inayojihusisha na uzalishaji wa bidhaa hizo mkoani Mwanza, amesema udanganyifu katika vipimo vya mabati ni sawa na kuhujumu jasho la wananchi wanaotumia fedha zao kujenga makazi na kuendeleza shughuli nyingine.

Amesema kampuni yao imeendelea kuwa kinara katika kuzingatia usahihi wa vipimo vinavyotakiwa kisheria, akisisitiza kuwa wazalishaji wote wana wajibu wa kuhakikisha bidhaa wanazozipeleka sokoni zinakidhi viwango kwa manufaa ya walaji.

Wakala wa Vipimo Mkoa wa Mwanza unaendelea na zoezi la ukaguzi wa bidhaa mbalimbali, linalofanyika kwa utaratibu wa kawaida pamoja na ukaguzi wa kushtukiza, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wananchi wanalindwa dhidi ya bidhaa zisizokidhi vipimo sahihi.

Shigongo Ahoji Serikali Kuhusu Barabara za Mitaa Nyehunge – Video

Global Publishers
August 27, 2026
12 views
0 Comments

Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo, amehoji Bungeni jijini Dodoma kuhusu hatua za Serikali katika kuboresha barabara za mitaa katika eneo la Nyehunge, Buchosa mkoani Mwanza, ambazo kwa sasa hazikidhi viwango vinavyohitajika.

Shigongo ametoa hoja hiyo Bungeni akiitaka Serikali kueleza ni lini itachukua hatua za kuzirekebisha barabara hizo ili ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi na kurahisisha usafiri katika eneo hilo.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, amesema Serikali inalifahamu suala hilo na tayari inalishughulikia.

Prof. Shemdoe amesema kuwa Serikali itaendelea kutafuta na kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo, huku akieleza kuwa fedha zitakapopatikana, barabara hizo zitajengwa kwa kiwango cha lami.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuboresha miundombinu ya barabara za mitaa na kuongeza ubora wa huduma za usafiri kwa wananchi.

Uboreshaji wa barabara hizo unatarajiwa kuwa na mchango katika kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa pamoja na kuchochea shughuli za kiuchumi katika eneo la Buchosa.

Dkt. Mwigulu Ampongeza Ndejembi, Aeleza Mikakati ya Serikali Kuhusu Mawasiliano na Usafiri – Vudeo

Global Publishers
August 27, 2026
30 views
0 Comments

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amempongeza Mheshimiwa Deogratius Ndejembi kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dkt. Mwigulu ametoa pongezi hizo leo, Agosti 27, 2026, akiwa Bungeni Dodoma, akimtakia Mheshimiwa Ndejembi kila la heri katika kutekeleza majukumu mapya aliyopewa kwa ajili ya kulitumikia Taifa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuimarisha huduma za mawasiliano katika maeneo yenye shughuli kubwa za kiuchumi ambayo bado yanakabiliwa na changamoto za kimawasiliano.

Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi na wafanyabiashara katika maeneo hayo wanapata huduma bora na za uhakika za mawasiliano, jambo litakalosaidia kuimarisha mazingira ya biashara na shughuli za kiuchumi.

Akizungumzia sekta ya usafirishaji, Dkt. Mwigulu amesema Serikali inaendelea kusisitiza mabasi kuanzia safari zao katika standi rasmi, badala ya kuchukua abiria kiholela njiani.

Waziri Mkuu ameyasema hayo mapema leo, Agosti 27, 2026, Bungeni Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge.

Amesisitiza umuhimu wa waendeshaji wa mabasi kuzingatia taratibu na kanuni za usafirishaji ili kuhakikisha abiria wanapata huduma salama na yenye utaratibu.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, utekelezaji wa taratibu hizo ni muhimu katika kuboresha huduma za usafiri wa abiria na kuhakikisha usalama wa wasafiri pamoja na watumiaji wengine wa barabara.

Hatua hizo ni sehemu ya jitihada za Serikali katika kuboresha huduma kwa wananchi, kuimarisha mazingira ya shughuli za kiuchumi na kuhakikisha huduma za usafiri na mawasiliano zinapatikana kwa ufanisi zaidi.

Tanzania yaandaa ziara ujumbe wa ADDI – HabariLeo

DAR ES SALAAM: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeandaa ziara maalumu ya ujumbe kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Diaspora wa Kiafrika (ADDI) katika Makumbusho ya Taifa la Tanzania, jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo iliyofanyika Agosti 26, 2026, imelenga kuwapa wageni fursa ya kujifunza historia, utamaduni na urithi wa Tanzania, pamoja na kuimarisha diplomasia ya utamaduni.

Ujumbe huo uliongozwa na Mwanzilishi na Rais wa ADDI, Balozi Arikana Chihombori-Quao kutoka Zimbabwe, ambaye amewataka Waafrika kuwa wamoja, kushikamana na kudumisha amani, akisisitiza umuhimu wa umoja katika kulinda na kuendeleza urithi wa Afrika.

Kwa upande wake, Muhifadhi Kiongozi wa Makumbusho na Nyumba za Utamaduni, Dk. Aloyce Mwambwiga, amewahimiza wananchi na wageni kutoka nje ya nchi kutembelea Makumbusho ya Taifa ili kujifunza zaidi kuhusu historia, utamaduni na urithi wa Tanzania.

Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za kuendeleza diplomasia ya utamaduni na kuitangaza Tanzania kupitia historia na urithi wake kwa wageni kutoka ndani na nje ya nchi.

S/SGT Mongo Apewa Tuzo, Milioni 1 na Madereva wa Malori – Video

Global Publishers
August 27, 2026
78 views
0 Comments

Iringa, Agosti 25, 2026 — Umoja wa Madereva wa Malori nchini umemtunuku S/SGT Mongo cheti cha pongezi, tuzo pamoja na fedha taslimu Shilingi milioni moja, kwa kutambua mchango wake katika kurahisisha mtiririko wa magari na kuimarisha usalama barabarani.

Tuzo hiyo imetolewa kama ishara ya kuthamini utendaji wake katika kutekeleza majukumu ya usimamizi wa usalama barabarani, hususan katika maeneo yenye msongamano wa magari ya mizigo.

Akizungumza baada ya tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, amempongeza S/SGT Mongo kwa utendaji wake na kuwataka madereva kuendelea kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani.

Kamanda Bukumbi amesisitiza kuwa usalama barabarani ni jukumu la kila mtumiaji wa barabara, hivyo madereva wanapaswa kuwa waangalifu, kuheshimu sheria na kuhakikisha magari yao yanakuwa katika hali salama wakati wote.

Kwa upande wake, S/SGT Mongo amewashukuru madereva hao kwa kutambua juhudi zake na kusema kuwa tuzo hiyo imempa hamasa zaidi ya kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi, uadilifu na kujituma.

Aidha, amemshukuru Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Camillus Wambura kwa uongozi wake na mchango katika kuwawezesha askari kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

S/SGT Mongo amesema utambuzi huo ni motisha kwake na kwa askari wengine kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi na kuhakikisha usalama wa watumiaji wote wa barabara.

Tukio hilo linaendelea kuonyesha umuhimu wa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na wadau wa usafirishaji katika kuboresha usalama barabarani na kuhakikisha mtiririko mzuri wa magari katika barabara za Tanzania.

Mwakioja atekeleza ahadi, akabidhi pampu ya maji Lanzoni – HabariLeo

TANGA: MBUNGE wa Jimbo la Mkinga, Twaha Mwakioja, ametekeleza ahadi yake baada ya kukabidhi pampu ya maji kwa ajili ya Shule ya Sekondari Lanzoni, pamoja na kutoa fedha taslimu na vifaa mbalimbali vya maendeleo na michezo katika wilaya hiyo.

​Katika ziara yake iliyofanyika katika Kata ya Mhinduro, Mbunge Mwakioja alikabidhi pampu hiyo inayolenga kupunguza kero ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji shuleni hapo, sambamba na kutoa Sh 300,000 kwa ajili ya ukarabati wa vyoo katika Shule ya Msingi Bamba Mavengero.

​”Leo nimekuja kutekeleza ahadi zangu baada ya kubaini changamoto mbalimbali kwenye shule zetu. Ninaamini misaada hii itasaidia kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia kwa vijana wetu,” alisema Mwakioja alipokuwa akizungumza na wananchi.

​Mbali na sekta ya elimu, Mbunge huyo aligusa nyanja nyingine muhimu kwa jamii ya Mkinga kwa kutoa misaada wa

​Viti 20 kwa kikundi cha wanakijiji cha Muheza ili kurahisisha shughuli zao za kijamii na Sh 500,000 kwa Klabu ya Mpira wa Miguu ya St. Augustino FC (inayomilikiwa na Kanisa Anglikana Mhinduro) ikiwa ni hamasa kwa vijana kujihusisha na michezo.

 

​Katika ziara hiyo, Mwakioja alipata fursa ya kusikiliza na kupokea kero mbalimbali za wananchi, kukutana na makundi ya vijana, pamoja na kushiriki katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Mhinduro.

​Akihutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi, aliainisha mafanikio mbalimbali ya kimaendeleo yaliyopatikana jimboni humo tangu alipoingia madarakani. Alisisitiza kuwa siri ya maendeleo ya haraka inatokana na ushirikiano thabiti kati ya wananchi, viongozi wa Chama, na Serikali.

Madereva wa Malori S/SGT Mongo, Wampa Tuzo na Sh Milioni 1 – Video

Global Publishers
August 27, 2026
18 views
0 Comments

Iringa, Agosti 25, 2026 — Umoja wa Madereva wa Malori nchini umemtunuku S/SGT Mongo cheti cha pongezi, tuzo pamoja na fedha taslimu Shilingi milioni moja, kwa kutambua mchango wake katika kurahisisha mtiririko wa magari na kuimarisha usalama barabarani.

Tuzo hiyo imetolewa kama ishara ya kuthamini utendaji wake katika kutekeleza majukumu ya usimamizi wa usalama barabarani, hususan katika maeneo yenye msongamano wa magari ya mizigo.

Akizungumza baada ya tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, amempongeza S/SGT Mongo kwa utendaji wake na kuwataka madereva kuendelea kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani.

Kamanda Bukumbi amesisitiza kuwa usalama barabarani ni jukumu la kila mtumiaji wa barabara, hivyo madereva wanapaswa kuwa waangalifu, kuheshimu sheria na kuhakikisha magari yao yanakuwa katika hali salama wakati wote.

Kwa upande wake, S/SGT Mongo amewashukuru madereva hao kwa kutambua juhudi zake na kusema kuwa tuzo hiyo imempa hamasa zaidi ya kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi, uadilifu na kujituma.

Aidha, amemshukuru Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Camillus Wambura kwa uongozi wake na mchango katika kuwawezesha askari kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

S/SGT Mongo amesema utambuzi huo ni motisha kwake na kwa askari wengine kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi na kuhakikisha usalama wa watumiaji wote wa barabara.

Tukio hilo linaendelea kuonyesha umuhimu wa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na wadau wa usafirishaji katika kuboresha usalama barabarani na kuhakikisha mtiririko mzuri wa magari katika barabara za Tanzania.

Mbappe Apiga Hat Trick Madrid Ikiibuka na Ushindi Mnono Dhidi ya Sociedad

Shechambo Chris
August 27, 2026
0 views
0 Comments

Real Madrid jana usiku Agosti 26, iliibuka na ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya Real Sociedad katika mchezo wa La Liga uliopigwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu, huku Kylian Mbappé akiwa shujaa wa mchezo baada ya kufunga magoli matatu (hat-trick)

 

Madrid ilianza kwa kasi na Mbappe akifungia bao la kwanza dakika ya 40, baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Federico Valverde na kumalizia kwa ustadi.

Hata hivyo, Real Sociedad ilisawazisha kupitia Luka Sučić dakika ya 44, hivyo timu hizo zikaenda mapumziko zikiwa sare ya 1-1.

 

Kipindi cha pili kilikuwa cha Madrid, Mbappe alifunga bao lake la pili dakika ya 60, baada ya kucheza vizuri na Jude Bellingham ndani ya eneo la hatari na kumalizia kwa shuti la chini.

Dakika 68, Real Madrid iliongeza bao la tatu kupitia Vinícius Júnior, aliyemalizia pasi ya Jude Bellingham na kuifanya Madrid kuongoza 3-1.

 

Mbappe hakutosheka na mabao mawili, dakika ya 80, Mfaransa huyo alikamilisha hat-trick yake baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Vinicius Junior na kumchambua kipa Alex Remiro kwa kumtupia mpira juu yake.

 

Pia ulikuwa ushindi muhimu kwa Jose Mourinho ambaye amerejea Santiago Bernabeu baada miaka 13.

 

Na Haika Urio DaTU.