Skip to content
-
Subscribe to our newsletter & never miss our best posts. Subscribe Now!
Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

  • Home
  • Privacy Policy
  • Sample Page
  • Home
  • Privacy Policy
  • Sample Page
Close

Search

  • https://www.facebook.com/
  • https://twitter.com/
  • https://t.me/
  • https://www.instagram.com/
  • https://youtube.com/
Subscribe
Habari

Madereva wa Malori S/SGT Mongo, Wampa Tuzo na Sh Milioni 1 – Video

By admin
August 27, 2026 2 Min Read
Comments Off on Madereva wa Malori S/SGT Mongo, Wampa Tuzo na Sh Milioni 1 – Video

Global Publishers
August 27, 2026
18 views
0 Comments

Iringa, Agosti 25, 2026 — Umoja wa Madereva wa Malori nchini umemtunuku S/SGT Mongo cheti cha pongezi, tuzo pamoja na fedha taslimu Shilingi milioni moja, kwa kutambua mchango wake katika kurahisisha mtiririko wa magari na kuimarisha usalama barabarani.

Tuzo hiyo imetolewa kama ishara ya kuthamini utendaji wake katika kutekeleza majukumu ya usimamizi wa usalama barabarani, hususan katika maeneo yenye msongamano wa magari ya mizigo.

Akizungumza baada ya tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, amempongeza S/SGT Mongo kwa utendaji wake na kuwataka madereva kuendelea kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani.

Kamanda Bukumbi amesisitiza kuwa usalama barabarani ni jukumu la kila mtumiaji wa barabara, hivyo madereva wanapaswa kuwa waangalifu, kuheshimu sheria na kuhakikisha magari yao yanakuwa katika hali salama wakati wote.

Kwa upande wake, S/SGT Mongo amewashukuru madereva hao kwa kutambua juhudi zake na kusema kuwa tuzo hiyo imempa hamasa zaidi ya kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi, uadilifu na kujituma.

Aidha, amemshukuru Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Camillus Wambura kwa uongozi wake na mchango katika kuwawezesha askari kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

S/SGT Mongo amesema utambuzi huo ni motisha kwake na kwa askari wengine kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi na kuhakikisha usalama wa watumiaji wote wa barabara.

Tukio hilo linaendelea kuonyesha umuhimu wa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na wadau wa usafirishaji katika kuboresha usalama barabarani na kuhakikisha mtiririko mzuri wa magari katika barabara za Tanzania.

Author

admin

Follow Me
Other Articles
Previous

Mbappe Apiga Hat Trick Madrid Ikiibuka na Ushindi Mnono Dhidi ya Sociedad

Next

Mwakioja atekeleza ahadi, akabidhi pampu ya maji Lanzoni – HabariLeo

Recent Posts

  • Kesi ya Uhaini ya Lissu Yaendelea leo;- Maswali Mazito Yaibuka Katika Dodoso la Serikali
  • Nafasi za Kazi Wezesha Mzawa Microfinance – Loan Officer, Mwisho wa Maombi Agosti 31, 2026
  • Safari Mpya Imeanza! Fahamu Mchezo wa 3 Fisher Cats Meridianbet
  • Europa League Kuamua! Salah Aongoza Trabzonspor Kwenye Mechi ya Marudiano
  • Watanzania 173 Warejea Nchini kwa Hiari Kutoka Afrika Kusini

Recent Comments

  1. A WordPress Commenter on Hello world!

Archives

  • August 2026

Categories

  • Burudani
  • Habari
  • Magazeti
  • Michezo
  • Siasa
Copyright 2026 — Habarimpya. All rights reserved. Blogsy WordPress Theme