Matokeo ya Darasa la Saba 2026 Yapo Hapa, Asilimia 85.22 Wafulu, Yatangazwa na Necta

Global Publishers
November 4, 2026
1,866 views
0 Comments

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi kwa mwaka 2026, huku watahiniwa 970,876 wakifaulu kwa madaraja ya A, B na C, sawa na asilimia 85.22 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani huo.

Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Saidi Ally Mohamed, amesema jumla ya watahiniwa 1,139,273 walifanya mtihani huo, huku idadi kubwa ikiweza kupata madaraja yanayowawezesha kuhitimu elimu ya msingi.

Katika hatua nyingine, Profesa Saidi amesema watahiniwa 31 wamefutiwa matokeo kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo ukiukwaji wa kanuni na taratibu za mitihani.

Amefafanua kuwa kati ya watahiniwa hao, 26 wamefutiwa matokeo kwa kufanya udanganyifu wakati wa mtihani, huku wengine watano wakichukuliwa hatua kutokana na kuandika matusi kwenye karatasi za majibu.

Matokeo hayo yanakuja wakati wanafunzi, wazazi na walezi wakisubiri kujua hatua inayofuata ya safari ya elimu kwa wahitimu wa darasa la saba, ikiwemo nafasi za kujiunga na elimu ya sekondari.

BONYEZA HAPA KUTAZAMA MATOKEO >> MATOKEO YA DARASA LA SABA 2026

WAZAZI SHULE YA GOOD VICTORY IRINGA WAPONGEZA MATOKEO MAZURI YA DARASA LA SABA

NA MATUKIO DAIMA MEDIA, IRINGA

WAZAZI wa wanafunzi waliofanya mtihani wa Taifa wa kumaliza elimu ya msingi, darasa la saba mwaka 2026, katika Shule ya Good Victory iliyopo mjini  mkoani Iringa, wamepongeza matokeo mazuri yaliyopatikana na wanafunzi wa shule hiyo, ambapo wanafunzi wote 64 waliofanya mtihani huo wamefanikiwa kupata daraja A.

Wazazi hao wamesema matokeo hayo ni ishara ya ubora wa elimu inayotolewa shuleni hapo, juhudi za walimu katika kufundisha, usimamizi mzuri wa uongozi wa shule pamoja na ushirikiano uliopo kati ya walimu na wazazi katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.

Wakizungumza na Matukio Daima Media  kuhusu mafanikio hayo, Amina Sanga na John Ndelwa walisema wamefurahishwa na kuvutiwa na matokeo yaliyopatikana, wakieleza kuwa ni jambo la kujivunia kuona wanafunzi wote 64 wakifaulu kwa kupata daraja A.

Wamesema mafanikio hayo yanaonesha kuwa uwekezaji katika elimu, unapokwenda sambamba na nidhamu, maandalizi ya kutosha na ufuatiliaji wa karibu wa maendeleo ya wanafunzi, unaweza kuleta matokeo makubwa na yenye manufaa kwa jamii.

Aidha, wazazi hao wameeleza kuwa matokeo hayo yanaongeza imani kwa wazazi na walezi wanaotafuta shule zenye uwezo wa kuwajengea watoto wao msingi imara wa kitaaluma, huku wakisisitiza umuhimu wa kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na taasisi za elimu katika kulea na kuandaa kizazi chenye maarifa.

Shule ya Good Victory iliyopo katika Manispaa ya Iringa imeonesha kiwango kizuri cha ufaulu kupitia matokeo hayo, ambapo wanafunzi wote waliofanya mtihani wamepata daraja la juu zaidi, jambo linaloweka alama muhimu katika historia ya maendeleo ya taaluma ya shule hiyo.

Kwa upande mwingine, mafanikio hayo yanaibua umuhimu wa kuendelea kuimarisha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, kuhakikisha walimu wanapata ushirikiano unaostahili na wanafunzi wanapata malezi yanayowawezesha kutumia vizuri vipaji na uwezo wao katika masomo.

Wadau wa elimu wamekuwa wakisisitiza kuwa mafanikio ya mwanafunzi hayajengwi na juhudi za upande mmoja pekee, bali yanahitaji ushirikiano wa karibu kati ya shule, wazazi na jamii kwa ujumla. Ushirikiano huo husaidia kufuatilia maendeleo ya watoto, kutambua changamoto mapema na kutafuta suluhisho zinazoweza kuboresha kiwango cha ufaulu.

Matokeo ya Good Victory ya mwaka 2026 yanatoa taswira ya matumaini kwa wazazi na wanafunzi wengine, huku yakiongeza matarajio ya kuona shule hiyo ikiendelea kudumisha kiwango hicho cha ufaulu katika miaka ijayo.

Hata hivyo, pamoja na mafanikio hayo, ni muhimu kwa shule kuendelea kuweka mikakati ya kudumisha ubora wa elimu, kuwajengea wanafunzi uwezo wa kufikiri kwa kina, ubunifu, maadili mema na kujiandaa kukabiliana na changamoto za hatua zinazofuata za masomo.

Kwa wazazi, mafanikio hayo ni faraja na uthibitisho wa umuhimu wa kuchagua mazingira bora ya elimu kwa watoto wao. Kwa wanafunzi waliofaulu, ni mwanzo wa safari nyingine ya kitaaluma inayohitaji bidii, nidhamu na kujituma zaidi.

Walisema ufaulu wa wanafunzi wote 64 kupata daraja A katika mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka 2026 ni mafanikio makubwa kwa Shule ya Good Victory, wazazi na jamii ya Iringa, huku ukiweka matarajio mapya katika safari ya kuimarisha ubora wa elimu mkoani humo.

HAYATI SAMUEL SITTA ALITUACHIA DIRA YA UONGOZI, TUIISHI – MAKAMU WA RAIS

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amewataka Viongozi kuuenzi urithi wa aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Samuel John Sitta kwa kuishi misingi ya uadilifu, uwajibikaji na kujenga Taasisi imara.

 

Makamu wa Rais ametia ujumbe huo Novemba 3, 2026, katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma, alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,  kwenye kumbukizi ya miaka 10 ya kifo cha Samuel John Sitta na uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha na safari yake ya uongozi.

 

Makamu wa Rais amesema Hayati Samuel Sitta anakumbukwa kwa kutanguliza maslahi ya Taifa, kulinda hadhi ya Bunge na kusimamia heshima kwa taratibu na kanuni. Amesisitiza kuwa viongozi wanapaswa kuyatafsiri mafunzo hayo katika utendaji wao wa kila siku.

 

“Uongozi wa kweli si njia ya kujitafutia umaarufu, hadhi au manufaa binafsi bali ni wajibu, utumishi, na ni kujitoa kwa ajili ya wengine,” amesema.

 

Aidha, amewahimiza Watanzania, hususan viongozi, vijana na wanafunzi, kukisoma kitabu hicho chenye kurasa 217 ili kujifunza kuhusu utumishi wa umma, uzalendo na umuhimu wa Taasisi imara katika kulijenga Taifa.

 

“Taifa linalokumbuka wajenzi wake huhifadhi utambulisho wake; Taifa linaloheshimu utumishi huwahamasisha wengine kutumikia; na, Taifa linalohifadhi historia yake hulinda mustakabali wake” amesema Makamu wa Rais.

 

 

Kwa upande wake, Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azan Zungu, amesema Sitta ataendelea kukumbukwa kwa uchapakazi, uzalendo na mchango wake katika Bunge na Taifa kwa ujumla. Kwa upande wake Mjane wa Hayati Sitta, Mhe. Margaret Sitta, amemwelezea kuwa mpenda haki aliyethamini ubunifu, uwajibikaji na falsafa ya “viwango na kazi.”

 

Hafla hiyo imewakutanisha viongozi mbalimbali, familia na watu waliowahi kufanya kazi na Sitta, huku ujumbe mkuu ukiwa kuendeleza urithi wake kwa vitendo na kutanguliza maslahi ya wananchi.

HASIRA ZA NDEJEMBI KWA TAN ROADS SONGWE, ZAIFANYA TUNDUMA KUPUMUA

Na Moses Ng’wat, Tunduma.

MKUU wa Mkoa wa Songwe, Aboubakar Kunenge, leo Novemba 3, 2026, amefungua rasmi matumizi ya njia mbili za barabara ya njia nne katika eneo la Kituo cha Pamoja cha Forodha (OSBP) Tunduma, hatua inayotarajiwa kupunguza msongamano wa malori na kurahisisha usafirishaji wa mizigo katika mpaka huo.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache,

tangu Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, kutoa maelekezo kuhusu kasi ndogo ya utekelezaji wa mradi huo, yaliyokwenda sanjari na kutumbuliwa kwa aliyekuwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe, Mhandisi Frederick Mande

Kunenge amefungua njia hizo baada ya kutembelea eneo la mradi na kukagua maendeleo ya ujenzi, huku akiridhia magari makubwa ya mizigo kuanza kuzitumia baada ya wataalamu kuthibitisha kuwa zege limekomaa na lina uwezo wa kuhimili uzito wa magari hayo.

Akizungumza wakati wa kufungua barabara hiyo, amesema matumizi ya njia hizo yatawezesha magari yanayoingia na kutoka nchini kutumia njia hizo, hivyo kupunguza mwingiliano na msongamano uliokuwa ukikwamisha shughuli za usafirishaji katika mpaka huo.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja mpya wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe, Mhandisi Silvanus Mroka, amesema utekelezaji wa mradi mzima umefikia asilimia 76, huku mkandarasi akiendelea na ujenzi wa kilomita 1.275 zilizobaki kuelekea Mbeya.

Amesema njia mbili zilizobaki zinatarajiwa kufunguliwa Novemba 17, mwaka huu, hatua itakayokamilisha matumizi ya njia zote nne na kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo kupitia mpaka huo.

Ameongeza kuwa, Sehemu iliyofunguliwa ina urefu wa mita 400 na upana wa mita 14, kuanzia eneo la geti la Nakonde upande wa Zambia hadi mzunguko wa magari (Roundabout) upande wa Tunduma.

Baadhi ya madereva wanaotumia mpaka huo wameipongeza Serikali kwa kufungua njia hizo, wakieleza kuwa zitapunguza muda wa kusubiri, foleni, mizunguko mirefu ya magari na matumizi ya mafuta yaliyokuwa yakiongezeka kutokana na msongamano.

Kunenge amesema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu na kuweka mazingira rafiki kwa biashara na uwekezaji, huku akisisitiza wananchi kutumia fursa hiyo kuifanya Tunduma kuwa kitovu cha biashara na uchumi badala ya kuwa eneo la makazi pekee.

Mwisho.

Matokeo ya Darasa la Saba 2026 Yapo Hapa, Asilimia 85.22 Wafulu, Yatangazwa na Necta

Global Publishers
November 3, 2026
1,536 views
0 Comments

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi kwa mwaka 2026, huku watahiniwa 970,876 wakifaulu kwa madaraja ya A, B na C, sawa na asilimia 85.22 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani huo.

Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Saidi Ally Mohamed, amesema jumla ya watahiniwa 1,139,273 walifanya mtihani huo, huku idadi kubwa ikiweza kupata madaraja yanayowawezesha kuhitimu elimu ya msingi.

Katika hatua nyingine, Profesa Saidi amesema watahiniwa 31 wamefutiwa matokeo kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo ukiukwaji wa kanuni na taratibu za mitihani.

Amefafanua kuwa kati ya watahiniwa hao, 26 wamefutiwa matokeo kwa kufanya udanganyifu wakati wa mtihani, huku wengine watano wakichukuliwa hatua kutokana na kuandika matusi kwenye karatasi za majibu.

Matokeo hayo yanakuja wakati wanafunzi, wazazi na walezi wakisubiri kujua hatua inayofuata ya safari ya elimu kwa wahitimu wa darasa la saba, ikiwemo nafasi za kujiunga na elimu ya sekondari.

BONYEZA HAPA KUTAZAMA MATOKEO >> MATOKEO YA DARASA LA SABA 2026

Polisi Dar Yaonya Waliopanga Kuhamasisha Vurugu Siku ya Hukumu ya Lissu

Global Publishers
November 3, 2026
18 views
0 Comments

 

1003614578-1024x682 Polisi yaonya wanaohamasisha vurugu Novemba 6

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewaonya watu wanaodaiwa kuhamasishana ndani na nje ya Mkoa huo kwa lengo la kufanya fujo, vurugu na hujuma mbalimbali Novemba 6, 2026.

Jeshi hilo limesema halitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watakaobainika kujihusisha na mipango hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 03,2026, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, SACP Jumanne J. Muliro, amesema Jeshi hilo linaendelea kufuatilia kwa karibu kundi hilo na kwamba haitavumilia viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani katika Jiji la Dar es Salaam.

Amesema jeshi hilo litachukua hatua za haraka na za kisheria dhidi ya mipango yoyote itakayolenga kuvuruga amani, huku akiwataka wananchi kuheshimu utaratibu uliowekwa na Mahakama katika kufuatilia mashauri mbalimbali.

Katika hatua nyingine, SACP Muliro amesema katika kipindi cha Oktoba mwaka huu, Polisi Dar es Salaam ilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 67 wanaotuhumiwa kujihusisha na makosa mbalimbali ya jinai na kupata baadhi ya vitu vilivyoibwa.

Kuhusu mafanikio ya mashauri ya jinai yaliyofikishwa mahakamani kupitia Ofisi ya Mashitaka, Kamanda Murilo amesema baadhi ya watuhumiwa wamepatikana na hatia na kuhukumiwa vifungo mbalimbali vya jela.

Muliro amewashukuru wananchi wanaojitokeza kwa wingi kushiriki kampeni ya ‘Ongea na Kamanda’ inayoendelea jijini Dar es Salaam, akisema inalenga kujenga ushirikiano kati ya Polisi na wananchi katika kujadili changamoto za kiusalama katika maeneo yao na kuzitafutia ufumbuzi.

BARAZA LA HABARI TANZANIA LAJA NA MIKAKATI MIKUBWA

 

 

mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Keneth Simbaya  (wa tatu kushoto ) akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Kilolo Fredy Mwakibete aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Iringa katika mkutano wa baraza la Habari Tanzania (MCT) jana wakati wa mkutano mkuu wa 28 wa taasisi hiyo huku UTPC ikipongezwa kwa kulipa ada kwa wakati (Picha na Matukio Daima Media

NA MATUKIO DAIMA MEDIA 

IRINGA.

Baraza la Habari Tanzania (MCT) limeeleza mikakati ya kuimarisha uhai wa wanachama wake kwa kuboresha mfumo wa ada na kuanzisha vifurushi vya huduma vitakavyowawezesha wanachama kunufaika na mafunzo, msaada wa kisheria, usalama wa kimwili na kidijitali pamoja na fursa mbalimbali za kitaaluma.


Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 28 wa MCT uliofanyika mkoani Iringa, Katibu Mtendaji wa baraza hilo Ernest Sungura amesema changamoto zilizokuwepo kwa muda mrefu ni pamoja na mfumo wa ada ambao haukuwa ukitoa thamani ya moja kwa moja kwa wanachama pamoja na madeni yasiyo na tija, hali iliyosababisha taasisi hiyo kuweka mikakati mipya ya kuimarisha uendeshaji wake.

“Uimara wa MCT haupimwi kwa idadi ya wanachama pekee, bali ushiriki wao katika shughuli za baraza, uwajibikaji na manufaa wanayopata kupitia uanachama, akisisitiza kuwa wanachama wanapaswa kuona thamani ya huduma wanazopata ili waweze kuchangia ada kwa wakati na kwa hiari”alisema

Katika hatua nyingine, MCT imezindua kampuni tanzu ya Media Integrity Consulting Services, itakayokuwa mkono wa kibiashara wa baraza hilo kwa kujihusisha na tafiti za vyombo vya habari, ushauri wa mawasiliano, mafunzo ya kulipia, usimamizi wa matukio na huduma za ushauri, hatua inayolenga kupunguza utegemezi wa ada na misaada ya wahisani.

Ameeleza kuwa kampuni hiyo itatumia eneo la ardhi lenye ukubwa wa zaidi ya mita za mraba 65,000 lililopo Bagamoyo kwa shughuli za uwekezaji na uzalishaji, huku akiwahimiza wanachama na wawekezaji wengine kushiriki katika fursa zitakazotokana na eneo hilo kupitia ubia na uwekezaji wa pamoja.

Aidha, amesema MCT imeendelea na mazungumzo na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) ili kupata uelewa wa fursa za uwekezaji zinazoweza kutekelezwa katika eneo hilo, huku wawakilishi wa mamlaka hiyo wakitarajiwa kutoa maelezo kuhusu fursa zilizopo kwa wanachama.


Akizungumzia mustakabali wa taasisi hiyo, Sungura  amewataka wanachama kutambua kuwa viongozi na bodi zinazochaguliwa huwa na muda maalumu wa uongozi, lakini wanachama ndio msingi wa kudumu wa taasisi hiyo. Amewataka kutumia umoja wao kushiriki katika uwekezaji na kufanya maamuzi yatakayolinda maslahi ya MCT kwa muda mrefu.

“Nawahimiza wanahabari kuendelea kuzingatia maadili, kuwajibika katika ukusanyaji na utoaji wa taarifa pamoja na kulinda heshima ya taaluma,  uhuru wa habari hauwezi kudumu bila uwajibikaji na mifumo imara ya kujisimamia, Aidha, natoa wito kwa wajumbe wa mkutano huu kujadili kwa uwazi na kuweka maazimio yatakayotekelezeka kwa maslahi ya taasisi na tasnia ya habari kwa ujumla”alisema


Awali akifungua Mkutano huo Mkuu wa 28 wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) uliofanyika mkoani Iringa, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Fredy Atupele Mwakibete kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James amewaasa wanahabari  kuzingatia  maadili na weledi wa taaluma ya habari kwa kutoa taarifa sahihi, za ukweli na kuepuka kusambaza habari za uongo na upotoshaji, huku akisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa mazingira salama yatakayowawezesha waandishi kutekeleza majukumu yao bila hofu.

“Vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kuunganisha serikali na wananchi kwa kutoa elimu, kuhamasisha maendeleo na kusimamia uwajibikaji, hivyo amewataka wanahabari kuendelea kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia misingi ya taaluma”alisema 

Aidha, ameipongeza MCT kwa kuanzisha kampuni tanzu ya Media Intelligence Consulting Services, akieleza kuwa serikali ipo tayari kushirikiana nayo kwa kutumia huduma za utafiti na ushauri. Pia ameitaka taasisi hiyo kutumia eneo lake lenye ukubwa wa zaidi ya mita za mraba 65,000 lililopo Bagamoyo kwa uwekezaji na shughuli za uzalishaji zitakazoongeza mapato ya taasisi.

Akizungumzia fursa za Mkoa wa Iringa, amewahimiza wanahabari kutumia kalamu na taaluma zao kutangaza vivutio vya utalii na miradi ya maendeleo, ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Makumbusho ya Mkwawa, miradi ya umwagiliaji ya Isakalilo, ujenzi wa barabara ya mchepuo wa Igumbilo–Ihemi pamoja na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Iringa.


Kwa upande wake Mratibu wa Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani Deusdedit Hokororo –TISEZA amesema  wametambua mchango wa vyombo vya habari katika kuhamasisha uwekezaji nchini, ikieleza kuwa waandishi wa habari wamekuwa wadau muhimu katika kufikisha taarifa za fursa za uwekezaji kwa wananchi na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Hokororo amesema mafanikio yaliyopatikana katika kusajili zaidi ya miradi 3,500 ya uwekezaji yametokana na ushirikiano wa wadau mbalimbali, wakiwemo wanahabari ambao wamekuwa wakitangaza fursa na kuelimisha jamii kuhusu masuala ya uwekezaji.

“Vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kukuza uchumi wa nchi kwa kuhamasisha uwekezaji katika sekta mbalimbali, ikiwemo viwanda na usindikaji wa madini, hivyo kuwataka waandishi kuendelea kutumia maarifa na uzoefu wao kutangaza maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji”alisema

Aidha, ameeleza kufurahishwa na taarifa za MCT kumiliki eneo kubwa la ardhi Bagamoyo, lililopo karibu na eneo la uwekezaji la Bagamoyo, akiwahimiza viongozi na wanachama wa baraza hilo kulitumia eneo hilo kama fursa ya kujenga miradi itakayowaongezea kipato na kuimarisha taasisi yao.

Amesema TISEZA ipo tayari kushirikiana na MCT katika kutafuta wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, kuunganisha taasisi hiyo na wawekezaji pamoja na kusaidia kuweka mazingira yatakayowezesha eneo hilo kutumika kwa shughuli za kiuchumi kupitia uwekezaji wa moja kwa moja au ubia.

Mshambuliaji wa Tenerife Afariki Baada Ya Kugongana na Kipa Uwanjani

Mshambuliaji wa klabu ya CD Tenerife ya Hispania, Jesus de Miguel Alameda, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 30 baada ya kupata majeraha makubwa ya kichwa na kifua kufuatia kugongana na mlinda mlango wa FC Andorra, Jesus Owono, katika mchezo wa ligi daraja la pili nchini humo.

Tukio hilo lilitokea Jumatatu wakati timu hizo zikicheza mchezo uliokuwa ukielekea ukingoni kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2, ambapo dakika saba za nyongeza zilikuwa zimeongezwa.

Kwa mujibu wa taarifa za mchezo huo, Owono alikimbia kuelekea katikati ya uwanja kwa lengo la kuondoa mpira mrefu, lakini goti lake liligongana na mwili wa De Miguel, ambaye alianguka na kubaki bila kusogea uwanjani.

Madaktari waliokuwa uwanjani walitoa huduma ya kwanza kabla ya mshambuliaji huyo kukimbizwa hospitalini kwa gari la wagonjwa kutoka Uwanja wa Estadio Heliodoro Rodriguez Lopez.

Hali yake ilielezwa kuwa mbaya Jumatatu, hata hivyo ilizidi kuwa mbaya Jumanne asubuhi na hatimaye kufariki dunia saa 10:00 alfajiri kwa saa za Hispania.

Klabu ya Tenerife imethibitisha kifo hicho kupitia taarifa iliyosema imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mchezaji huyo, huku ikitoa pole kwa familia, ndugu, marafiki na mashabiki wa klabu hiyo.

Katika tukio hilo, mwamuzi wa mchezo alimpatia kipa Owono kadi nyekundu ya moja kwa moja kabla ya kusitisha mchezo kutokana na uzito wa tukio hilo.

Kifo cha De Miguel kimeibua majonzi makubwa katika ulimwengu wa soka, huku klabu ya FC Andorra, ambayo ilikuwa mpinzani wa Tenerife katika mchezo huo, nayo ikitoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu na klabu yake.

Aliyekuwa beki wa Barcelona na mmiliki mwenza wa FC Andorra, Gerard Pique, pamoja na Rais wa La Liga, Javier Tebas, ni miongoni mwa viongozi wa soka walioeleza masikitiko yao.

Nyota wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe, pia alitoa salamu za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii.

Kufuatia kifo hicho, Shirikisho la Soka la Hispania limetangaza kuahirishwa kwa michezo ya Kombe la Hispania iliyokuwa imepangwa kuchezwa Jumanne, ikiwa ni pamoja na michezo ya Copa del Rey na Copa de la Reina.

DSTV Yatangaza Vifurushi Vipya, Bei Kuanzia Shilingi 15,000

Global Publishers
November 3, 2026
474 views
0 Comments

Kampuni ya DStv imetangaza vifurushi vipya vya huduma zake nchini Tanzania, ikiwa na maboresho yanayowawezesha wateja kupata burudani kupitia vipindi mbalimbali vya televisheni, michezo na filamu.

Kwa mujibu wa tangazo la kampuni hiyo, vifurushi hivyo vitaanza kutumika rasmi Novemba 5, 2026, vikiwa katika viwango vinne tofauti vya malipo.

Vifurushi vilivyotangazwa ni Starter kinachogharimu Shilingi 15,000, Select Shilingi 25,000, Sports Shilingi 50,000 na Ultimate kinachogharimu Shilingi 118,000.

Kupitia vifurushi hivyo, wateja watapata fursa ya kufurahia maudhui mbalimbali yakiwemo burudani za ndani na nje ya nchi, michezo pamoja na mashindano mbalimbali ya kimataifa.

DStv imetumia kaulimbiu ya “Pata zaidi na zaidi” katika kutangaza mabadiliko hayo, huku ikisisitiza upatikanaji wa burudani kupitia huduma yake ya DStv.

Marekani Kuiondoa Rwanda na Afrika Kusini Kwenye Mpango wa AGOA

 

Utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump, umetangaza mpango wa kuiondoa Rwanda na Afrika Kusini katika mpango wa upendeleo wa kibiashara wa Marekani unaojulikana kama AGOA, kuanzia Januari Mosi mwaka 2027.

Uamuzi huo unatarajiwa kuathiri biashara kati ya nchi hizo na Marekani, kupitia mpango wa African Growth and Opportunity Act (AGOA), unaozipa nchi za Afrika zinazokidhi masharti fursa ya kuuza maelfu ya bidhaa katika soko la Marekani bila kutozwa ushuru wa forodha.

Mwakilishi wa Biashara wa Marekani, Jamieson Greer, amesema tathmini ya kila mwaka ya mpango huo imebaini kuwa Rwanda na Afrika Kusini zinakiuka baadhi ya masharti yanayohitajika ili kuendelea kunufaika na fursa hiyo.

Kwa mujibu wa Greer, serikali ya Marekani tayari imezifikishia nchi hizo taarifa kuhusu uamuzi huo, ikieleza kuwa kuna masuala yanayohusiana na vikwazo vya biashara na uwekezaji wa Marekani, usalama wa taifa pamoja na maslahi ya sera za kigeni.

Kwa upande wa Rwanda, Marekani imeeleza pia wasiwasi kuhusu masuala ya haki za binadamu, uhuru wa kisiasa, utawala wa sheria na haki za wafanyakazi.

Hatua hiyo inakuja wakati ambapo uhusiano kati ya Washington na Kigali ukiwa katika mvutano, kufuatia vikwazo vilivyowekwa na Wizara ya Fedha ya Marekani dhidi ya Wizara ya Ulinzi ya Rwanda.

Taarifa ya Reuters pia inaeleza kuwa Afrika Kusini iliingiza bidhaa zenye thamani ya takribani dola bilioni 1.7 za Marekani kupitia AGOA mwaka 2025, zikiwemo vipuri vya magari, matunda jamii ya machungwa na mvinyo.

Rwanda nayo inanufaika kupitia mauzo ya kahawa na madini.Hatua hiyo inaweza kuongeza gharama za bidhaa zitakazoingia katika soko la Marekani kutoka nchi hizo, endapo zitaanza kutozwa ushuru wa kawaida badala ya kunufaika na upendeleo wa AGOA.

Hata hivyo, Marekani imesema nchi hizo zinaweza kuchukua hatua zinazohitajika ili kukidhi vigezo vya mpango huo na kurejesha hadhi yake.