Golugwa Kuendelea Kutoa Ushahidi wa Kumtetea Lissu leo – Video

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Amani Golugwa, leo Septemba 3, 2026, anaendelea kutoa ushahidi wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.

Golugwa alianza kutoa ushahidi wake jana, Septemba 2, 2026, akiwa shahidi wa tatu wa upande wa utetezi, baada ya shahidi wa pili, ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, kukamilisha ushahidi wake.

Katika ushahidi wake jana, Golugwa aliongozwa na Lissu na kueleza mambo mbalimbali, ikiwemo chimbuko la kampeni ya “No Reforms, No Election” ya CHADEMA, matukio yaliyohusiana na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024 pamoja na ripoti mbalimbali za kimataifa zilizotoa madai kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa mwaka 2025.

Aidha, Golugwa alieleza namna uongozi ndani ya CHADEMA unavyopatikana pamoja na majukumu yanayohusishwa na nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho.

Katika mwendelezo wa ushahidi wake leo, Golugwa ataendelea kuongozwa na Lissu katika kutoa utetezi wake.

Kesi hiyo yenye namba 19605/2025 inasikilizwa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru.

Lissu anakabiliwa na shtaka la uhaini chini ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code), Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania, kama ilivyorekebishwa mwaka 2023.

Lissu: Unasema kwamba mkutano uliandaliwa na Sekretariet, waeleze waheshimiwa majaji hii Sekretariet ni akina nani?

Golugwa: Hii Sekretariet ninayoizungumzia ni Katibu Mkuu wa Chama, Manaibu Katibu wawili kwa maana ya Bara na Zanzibar, Makatibu wa Mabaraza matatu ya chama, BAWACHA, BAVICHA na BAZECHA.Pia Wakurugenzi wa Chama pamoja na wataalam wawili ambao wameteuliwa na Mwenyekiti kuwa sehemu ya Sekretariet ya chama.

Lissu: Jumla watu wangapi hapo kwa hesbau yako

Golugwa:14 Lissu: Kwa muundo wa Chama Sekretariet ya Chadema ni chombo cha aina gani?

Golugwa: Sekretariet ya Chadema ndicho chombo cha kiutendaji kinachofanya kazi kila siku za kichama kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama

Lissu:Sasa Shahidi umesema Katibu Miuu alikuja na wazo kwamba muandae mkutano muwaandae watia nia hao watia nia ni akina nani?

Golugwa: Hao watia nia ni wanachama wa Chadema ambao aidha walipitishwa kuwa wagombea kwenye uchaguzi wa 2020 katika nafasi za udiwani, ubunge na Urais na kwamba bado nia yao ya kutaka kugombea nafasi hizo bado walikuwa nayo. Na wengine katika kundi hilo la watia nia ni wale ambao hawajawahi kugombea wala kupitishwa kwenye nafasi hizo nilizozitaja kwa maana mwaka 2025 na wao wakataka kutia nia wapitishwe kugombea nafasi hizo. Hao ndio watia nia.

Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji hao watia nia walikua wanatia nia ya kugombea nafasi gani

Golugwa:Waheshimiwa majaji hao watia nia walikuwa wanatia nia ya kugombea kwenye uchaguzi wa mwaka 2025.

Lissu:Waeleze waheshimiwa majaji lengo la kuwaita hao watia nia kwenye huo mkutano wa tarehe 3 Aprili lilikuwa lengo gani?

Golugwa: Lengo lilikuwa ni kuwaeleza na kuwafafanulia juu ya msimamo wa Chama uliopitishwa na mkutano kwa maana ya wazo la No Reforms No Elections, na msimamo huo ukawa umefafanuliwa na Kamati Kuu ya chama kwa kuazimiwa hilo ndilo lilikuwa lengo.

Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji unaposema No Reform No Elections, huu msimamo ulikuwa unahusu nini hasa?

Golugwa: Msimamo huu ulianza au ulizaliwa baada ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024.

Nikiwa Katibu wa Kanda ya Kaskazini, Katibu Mkuu alituambia Makatibu wa Kanda atuandikie ripoti ya uchaguzi wa Serikali za mitaa jinsi ulivyofanyika, na mimi kama mtendaji ambaye nilikuwa sehemu ya uchaguzi huo kwa kusimamia kanda ya Kaskazini nilitoa ripoti kwa kuonesha madudu mengi ya hivyo yaliyojitokeza.

Na Katibu Mkuu alitutaka tuandike maoni yetu ya kuhusiana na nini chama kifanye kutokana na hayo yaliyojitokeza, kwa hivyo mimi kwenye ripoti niliandika na waheshimiwa majaji naomba nitumie maneno exactly maneno niliyoandika yalikuwa maneno makali “Kwa ushenzi huu niliouona chama kisishiriki uchaguzi mwingine wowote mpaka kushinikiza mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi”.

Na Makatibu wenzangu kutoka katika kanda 9 kila mmoja kwa lugha yake wote tulitoa taarifa au ripoti yenye pendekezo zinazofanana na ndipo Kamati Kuu ikaketi ikayachakata mapendekezo ya Makatibu wa Kanda na wajumbe wenyewe wa Kamati Kuu ikatafakari kwa jinsi wanavyojua, basi nadhani tarehe 10 Desemba 2024, Mwenyekiti wa Chama wakati huo Mh. Freeman Mbowe akatoa tamko rasmi la chama, msimamo wa Kamati Kuu yaliyoazimiwa kwamba hatutakuwa tayari kwenda kwenye uchaguzi mwingine wowote bila mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi.

Lissu: Shahidi hebu waeleze waheshimiwa majaji kwa kifupi ni ushenzi gani uliouona.

Golugwa: Waheshimiwa majaji ushenzi ni mwingi.

Lissu: Waeleze majaji kwa ufahamu wako taarifa ya watazamaji wa uchaguzi wa SADC walisemaje juu ya huo uchaguzi.

Shahidi: Walisema uchaguzi wa Tanzania umeshindwa kukidhi Vigezo vya chaguzi kwa viwango vya chaguzi za kidemokrasia. Pia kulikuwa na Vitisho kwa viongpzi wa vyama vya upinzani na hivyo mazingira ya kiushindani hayakuwa sawa. Pia hakukuwa na uwazi katika mchakato mzima wa uchaguguzi. Kulikiwa na udanganyifu katika mchakato wa uchaguzi vurugu Siku ya uchaguzi hivyo uchaguzi wa Tanzania umekosa uhalali wa kuitwa uchaguzi.

Lissu: Waeleze Majaji watazamani wa Uchagauzi huo wa Jumuiya ya Ulaya EU walisemaje juu ya uchaguzi huo

Shahidi: Watazamaji wa Jumuiya ya Ulaya kwanza walisema wamesikitishwa na matukio ya vurugu yaliyotokea siku ya uchaguzi na kupelekea kuvuruga uchaguzi na wamesikitishwa na uharibifu wa mali na wamesikitishwa na mtandao kuzimwa mawasiliano na wamesikitishwa na taarifa za mauaji.

Madeleka Atoa Msaada wa Milioni 1 Kwa Watoto wa Mjane – Video

Global Publishers
September 3, 2026
30 views
0 Comments

Wakili Peter Madeleka.

Wakili Peter Madeleka ameguswa na changamoto ya mama mjane, Asha Mbaraka anayeuguza watoto wake wawili wanaosumbuliwa na ugonjwa wa figo, taarifa zilizoibuliwa na Global TV.

Global TV iliripoti habari za mjane huyo mara kadhaa ambapo Watanzania walikuwa wakimsaidia kwa kidogo walichojaliwa ambapo leo, Madeleka ameonesha kuguswa na kumkabidhi mjane huyo kiasi cha shilingi milioni moja, fedha taslimu.

Spika Zungu Awakalia Kooni Watendaji wa TAMISEMI Uchafu katika Jiji la Dar – Video

Global Publishers
September 3, 2026
48 views
0 Comments

Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Zungu, amewataka watendaji wa Serikali, hususan wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kubadili haraka mtazamo wao na kuacha kuchelewesha utekelezaji wa miradi ya ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP).

Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo, Alhamisi, Septemba 3, 2026, Zungu amesema hivi karibuni Rais alitoa maelekezo na kukemea hali ya uchafu katika Jiji la Dar es Salaam, lakini changamoto kubwa imekuwa kwa watendaji wa TAMISEMI ambao, kwa mujibu wake, wamekuwa kikwazo katika kutafuta suluhisho la tatizo hilo.

Amesema halmashauri za Dar es Salaam na miji mingine mikubwa nchini zinapobuni miradi ya PPP kwa ajili ya kuboresha usafi wa miji na kuiwasilisha TAMISEMI kwa ajili ya kushughulikiwa, majibu kutoka ofisi hiyo yamekuwa yakichelewa au kutotolewa kabisa.

Zungu amesema hali hiyo imekuwa ikiwakatisha tamaa wawekezaji wanaohitaji kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi ya usafi, na matokeo yake miji hiyo imeendelea kukabiliwa na changamoto ya uchafu.

Ametoa wito kwa watendaji hao kubadili fikra na kuhakikisha miradi ya PPP inayowasilishwa inashughulikiwa kwa wakati ili kutoa fursa kwa sekta binafsi kushiriki katika kutatua changamoto zinazozikabili halmashauri.

Jay-Z Kufanya Onyesho London Kusherehekea Miaka 30 ya Muziki

Global Publishers
September 3, 2026
30 views
0 Comments

LONDON, UINGEREZA — Rapper na mfanyabiashara maarufu wa Marekani, Jay-Z, anatarajiwa kufanya maonyesho mawili makubwa katika Uwanja wa Tottenham Hotspur jijini London, Septemba 4 na 5, 2026, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanza rasmi kwa safari yake katika tasnia ya muziki.

Maonyesho hayo, yanayofahamika kama JAŸ-Z 30, yataadhimisha miaka 30 tangu kutolewa kwa albamu yake ya kwanza, Reasonable Doubt, iliyochangia kumweka Jay-Z miongoni mwa wasanii wakubwa na wenye ushawishi katika historia ya muziki wa Hip Hop.

Mbali na kuadhimisha miaka 30 ya Reasonable Doubt, matamasha hayo pia yatahusisha kumbukumbu ya miaka 25 tangu kutolewa kwa albamu yake nyingine yenye mafanikio makubwa, The Blueprint.

Jay-Z, ambaye jina lake halisi ni Shawn Carter, amekuwa mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa katika muziki wa Hip Hop kwa zaidi ya miongo mitatu, huku akipanua mafanikio yake kupitia muziki, biashara na uwekezaji.

Mashabiki wa msanii huyo nchini Uingereza na sehemu nyingine duniani wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia maonyesho hayo, ambayo yameongeza msisimko kutokana na Jay-Z kutokuwa na ratiba kubwa ya matamasha ya mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni.

Maonyesho hayo ya London yanatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya Jay-Z kuangazia safari yake ya miaka 30 katika muziki pamoja na mchango wake katika maendeleo na ukuaji wa Hip Hop duniani.

Stori na Erick Elibariki | GPL

UMOJA WA MATAIFA WAONYA KUHUSU EL NIÑO ‘KUBWA ZAIDI’ HUKU NCHI ZIKIJIANDAA KWA ATHARI

 

Dunia imeingia katika “eneo hatari la hali mbaya ya hewa” huku athari za El Niño zikianza kuhisiwa duniani kote, mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameonya.

Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) limetoa data ya hivi karibuni kuhusu hali ya hewa mbaya zaidi kwa zaidi ya miaka 70 na huenda ikadumu hadi angalau Februari 2027.

El Niño hubadilisha mifumo ya hali ya hewa kote ulimwenguni, ikisukuma baadhi ya maeneo kwenye ukame huku mengine yakipata vimbunga vikali na mafuriko.

Watabiri wa hali ya hewa pia wanasema El Niño itaongeza hali ya joto katika baadhi ya maeneo, ikija na kuongeza kiwango cha juu cha joto linaloongezeka kote duniani kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na binadamu.

“El Niño inazidi kuwa kubwa mbele ya macho yetu. Sayansi haiachi nafasi ya shaka: sayari iko katika maji yasiyojulikana, na maji hayo yanaongeza joto,” Guterres alisema.

BBC ilizungumza na serikali na wanasayansi kuhusu hatua zinazochukuliwa duniani kote ili kupunguza hatari ya vifo, kuhama makazi na uharibifu wa mazingira.

Mifumo ya tahadhari za mapema imeimarishwa na kupelekwa kwa usaidizi wa kimatibabu wa awali, lakini nguvu ya tukio hili maalum imeibua wasiwasi mkubwa hasa kwa makundi yaliyo katika mazingira magumu.

WMO – shirika la Umoja wa Mataifa – limesema limechukua “uhamasishaji mkubwa” kujaribu kusambaza utabiri wake wa matukio mabaya ya hali ya hewa, yanayohusiana na El Niño, kwa jamii nyingi iwezekanavyo.

Katibu Mkuu wa WMO Celeste Saulo alionya: “El Niño ina uwezo wa kuleta pigo kubwa kwa jamii na uchumi kote ulimwenguni.”

SERIKALI IMEENDELEA KUCHUKUA ATUA ZA KUIMARISHA SEKTA YA ELIMU

Serikali imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha sekta ya elimu kwa kuongeza miaka ya elimu ya lazima, kupanua fursa za elimu ya sekondari na kuimarisha mafunzo ya ufundi ili kuwapa vijana uwezo wa kushiriki kikamilifu katika soko la ajira.  

Akizungumza Septemba 02, 2026 jijini Dodoma na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema maandalizi ya utekelezaji wa miaka 10 ya elimu ya lazima kuanzia mwaka 2028 yanaendelea, hatua itakayohitaji miundombinu, walimu na nafasi za kutosha katika shule za sekondari.  

Prof. Mkenda amebainisha kuwa mpango huo utasababisha ongezeko kubwa la wanafunzi watakaoingia sekondari, hivyo Serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha wanafunzi wote wanaostahili wanapata nafasi ya kuendelea na masomo.  

Aidha, ameongeza kuwa  Serikali inaendelea kuimarisha mfumo wa elimu wenye mikondo ya elimu ya jumla na elimu ya amali, ili wanafunzi wapate maarifa na stadi zinazowawezesha kuajirika au kujiajiri.  

Katika mazungumzo hayo, Prof. Mkenda ameeleza kuwa Serikali inajenga vyuo vya ufundi katika maeneo mbalimbali na kuimarisha mafunzo ya ufundi ili kukidhi mahitaji ya vijana na uchumi wa Taifa.  

Prof. Mkenda ameongeza kuwa Serikali inawekeza katika masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati pamoja na teknolojia mpya kama akili bandia (AI), ujifunzaji wa mashine na usalama wa mtandao, ili kuandaa wataalamu wa kisasa.  

Amesisitiza  umuhimu wa ushiriki wa sekta binafsi katika kupanua fursa za elimu, hususan katika ujenzi wa miundombinu na utoaji wa elimu ya amali.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, amesema kuwa Serikali inatazama uwezekano wa kuboresha vivutio vya kisera vitakavyoongeza uwekezaji wa sekta binafsi katika elimu.  

Naye Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Marianne Young, amepongeza juhudi za Tanzania na kuahidi kuendeleza ushirikiano katika elimu na na mafunzo ya  ufundi, ikiwemo kuunganisha taasisi za Tanzania na vyuo vikuu vya Uingereza katika maeneo ya teknolojia ya kisasa na mazingira.

 

*AFISA UGAVI WMA AHAMASISHA UHAKIKI VIFAA VYA VIPIMO BAADA YA UNUNUZI*

 *MWANZA* 

Wakala wa Vipimo (WMA) umetoa wito kwa Maafisa wanaosimamia  ununuzi na ugavi katika taasisi za umma na binafsi kuhakikisha vifaa vyote vinavyohusiana na vipimo vinawasilishwa WMA kwa ajili ya uhakiki kabla ya kupelekwa kwa watumiaji.

Akizungumza leo Septemba 2, 2026 katika Maonesho ya 21 ya  Biashara ya Afrika Mashariki yanayoendelea katika Uwanja wa Furahisha  jijini Mwanza, Afisa Ugavi wa WMA, Bi. Rehema Komba amesema ni vema taasisi zinapokamilisha ununuzi wa vifaa vya kivipimo,  zisivipeleke moja kwa moja kwa watumiaji bila kuhakikiwa, kwani inaweza lkupelekea hasara kwa serikali na wananchi.

“Tunasimamia mchakato wa manunuzi, lakini baada ya vifaa kufika, tuzikumbushe taasisi zetu kupeleka kwanza Wakala wa Vipimo kwa uhakiki. Msiogope kuchelewa kwa siku chache, bali ogopeni hasara ya miaka,”  amesema.

Akifafanua, Bi. Rehema ametoa mfano wa Mamlaka na Kampuni za Maji, ambapo amesema maafisa ugavi katika Mamlaka hizo  wanapaswa kushauri na kuhakikisha mita zote mpya za maji baada ya kununuliwa zinapita WMA kwa uhakiki  kabla ya kufungwa kwa wateja.

“Kama kila afisa ugavi atatoa ushauri huu mara baada ya kukamilisha manunuzi, tutakuwa tumepiga hatua kubwa kuhakikisha kuna biashara ya haki na ulinzi wa walaji nchini” ameongeza.

Mtaalamu huyo wa Ugavi amesema WMA ina mitambo ya kisasa inayowezesha kutoa huduma ya uhakiki wa haraka hali  inayoepusha usumbufu kwa taasisi wakati wa kutoa huduma.

Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yameanza tarehe  28 Agosti na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 6 Septemba, 2026.

 

Msako wa TANESCO! Wateja Wanaotumia Umeme Bila Kulipa Wakamatwa

Global Publishers
September 3, 2026
72 views
0 Comments

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ubungo jijini Dar es Salaam limeendelea na operesheni yake maalum ya kuwabaini na kuwachukulia hatua wateja ambao wanatumia umeme bila kulipia wakiwa wameunganishiwa umeme na vishoka mtaani kinyume na utaratibu.

Katika operesheni hiyo TANESCO Mkoa wa Ubungo imekamata baadhi ya wateja wake katika maeneo ya Mabibo External,Mburahati na Kimara Kilungure na miongoni mwa wateja hao wamekuwa wakitumia umeme wa TANESCO bila kulipia kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Akizungumza Septemba 2, 2026 wakati wa operesheni hiyo fundi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ubungo Salum Bure amesema wamewakamata wateja ambao wamechepusha umeme kupitia vishoka.

“Katika eneo la Mtaa wa Amani uliopo Mabibo External kuna mteja tumekuta amechepusha umeme na mara ya mwisho amenunua umeme Agosti mwaka 2025.

Hivyo kwa zaidi ya mwaka mmoja halipi umeme na ameunganishiwa na kishoka.

“Pia katika Mtaa wa Tanzanite uliopo Kimara Kirungule kuna mteja amekuwa akiliibia Shirika letu kwa kutumia umeme ambao haulipii na yeye amechepusha umeme kupitia vishoka,”amesema na kuongeza wateja wote ambao watabainika wameunganisha umeme kinyume na utaratibu hatua za kisheria zitachukuliwa

Bure amesema operesheni inayoendelea sasa inatokana na maelekezo ya Mkurugenzi wa Shirika hilo la TANESCO huku akitumia nafasi hiyo kuwataka wale wote wenye tabia ya kutumia umeme bila kuulipia waaache na wale wenye changamoto wafike katika ofisi zao kutoa taarifa.

Pia amewaomba wananchi wanapobaini baadhi yao kwa wamejiunganishia Umeme kinyume na utaratibu kwa kutumia vishoka kutoa Taarifa TANESCO kupitia namba ambayo unapiga bure ambayo ni 180

Kwa upande wake Mjumbe wa shina namba 10 katika Mtaa wa Amani eneo la Mabibo External Rose Peter amesema TANESCO wamefika katika eneo lake kukagua wale ambao wanaiba umeme kwa kujiunganishia bila utaratibu na kweli wamemkamata watu waliojiunganishia umeme bila utaratibu.

“Kwahiyo kwa wananchi wenzangu nitoe rai tuache tabia ya kuiibia TANESCO umeme .Hii iwe onyo kwa wote ambao wanaiba umeme na ushauri wangu tutumie mita zetu vizuri.”

Wasira Akutana na Wabunge wa CCM katika Makao Makuu ya Chama

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM – Bara), Stephen Wasira, amekutana na kuzungumza na Kamati ya Wabunge wa CCM, Septemba 2,  2026, katika Ukumbi wa White House Makao Makuu ya Chama jijini Dodoma.

Katika kikao hicho Wasira aliambatana na ujumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro.