DODOMA YASIMAMA KUMSUBIRI RAIS SAMIA, NGOMA ZA ASILI KUTAWALA

Wananchi na vikundi mbalimbali vya ngoma za asili wakionesha burudani na shamrashamra za furaha wakati wakisubiri mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, hapa Stesheni ya SGR Dodoma.

Rais Samia atazindua rasmi  majengo ya Ofisi, Wizara, Taasisi za Serikali, na barabara za lami katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, Oktoba 30, 2026.