Sababu 7 Kwanini Wagonjwa wa Pressure Wanatumia Kitunguu Saumu

High blood pressure (hypertension) ni sababu kubwa ya magonjwa ya moyo, kiharusi na uharibifu wa figo. Kwa muda mrefu, tiba asili zimekuwa zikisisitiza umuhimu wa lishe na mimea tiba katika kuzuia na kudhibiti shinikizo la damu  na miongoni mwa mimea iliyopewa utafiti mkubwa zaidi ni kitunguu saumu.

Zaidi ya maelfu ya tafiti zimechunguza uwezo wa kitunguu saumu kusaidia mwili kupambana na magonjwa mbalimbali, na matokeo mengi yanaonyesha kinaweza kuwa msaada muhimu katika afya ya moyo.

Kwa nini kitunguu saumu ni muhimu kwenye hypertension?

Kitunguu saumu (Allium sativum) kimehusishwa kwa muda mrefu na faida za mfumo wa moyo na mishipa ya damu. Utafiti unaonyesha kwamba kinaweza kusaidia kupunguza shinikizo la damu, hasa kwa watu ambao tayari wana hypertension.

Siri kubwa ipo kwenye kiungo chake mahsusi kinachoitwa allicin kinachotokea unapokikata au kukiponda.

Allicin:

  • Hulegeza na kupanua mishipa ya damu,

  • Huongeza uzalishaji wa nitric oxide,

  • na hivyo hupunguza msukumo wa damu kwenye kuta za mishipa.

Matokeo ya tafiti kadhaa yameonyesha kupungua kwa wastani wa karibu 8–9 mmHg kwa shinikizo la juu (systolic) na 5–6 mmHg kwa shinikizo la chini (diastolic), jambo linaloonyesha kwamba kitunguu saumu kinaweza kuwa nyongeza nzuri sambamba na matibabu ya kawaida.

Jinsi kinavyofanya kazi ndani ya mwili

Mbali na kulegeza mishipa, allicin pia huchochea kutengenezwa kwa misombo kama hydrogen sulfide na nitric oxide inayosaidia mishipa kuwa laini na kupanuka zaidi.

Kwa upande mwingine, kitunguu saumu huchochea utoaji wa maji na chumvi ya ziada mwilini, hali inayosaidia kupunguza shinikizo la damu kwa njia ya asili.

Ushahidi wa tafiti za kitabibu

Katika tafiti zilizohusisha wagonjwa wenye shinikizo lisilodhibitika, matumizi ya aged garlic extract kwa miezi kadhaa yalionyesha kupungua kwa shinikizo la damu kwa kiwango kinachoonekana kitabibu.

Utafiti mwingine ulionyesha pia kupungua kwa mkusanyiko wa mafuta kwenye mishipa ya moyo, hivyo kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo kwa walio kwenye hatari kubwa.

Faida nyingine zinazohusishwa na kitunguu saumu

Mbali na shinikizo la damu, tafiti zimehusisha kitunguu saumu na:

  • kupunguza kolesteroli mbaya,

  • kusaidia udhibiti wa sukari mwilini,

  • na kupunguza hatari ya baadhi ya saratani kutokana na misombo yake ya sulfur.

Hata hivyo, si kila utafiti unafanana — hivyo ushahidi unaendelea kukua.

Namna salama ya kukiongeza kwenye lishe

  • Kila mara, kikate au kiponde ili kuamsha allicin kabla ya kupika au kukila.

  • Ongeza kwenye vyakula kama supu, saladi au mboga.

  • Virutubisho vya aged garlic extract vinapatikana; mara nyingi hutumika kati ya 600–1,200 mg kwa siku.

Lakini ni muhimu kuzungumza na daktari kabla ya kuanza virutubisho, hasa kama tayari unatumia dawa za shinikizo au dawa za kupunguza damu kuganda.

Hitimisho

Kitunguu saumu kinaonyesha uwezo wa kusaidia kupunguza shinikizo la damu kwa kuboresha afya ya mishipa na kupunguza mzigo kwa moyo. Hata hivyo, kinapaswa kutumika kama kiunga cha lishe na nyongeza ya matibabu, si mbadala wa dawa alizoandikiwa mgonjwa.

Kabla ya kufanya mabadiliko yoyote ya matibabu shauriana na mtaalamu wa afya.

Aishi na Uvimbe Miaka 20 Aomba Msaada wa Matibabu, Afunguka Mazito -Video

Global Publishers
September 3, 2026
1,890 views
0 Comments

Usemi wa Kiswahili “Kabla hujafa hujaumbika” unaakisi kwa kiasi kikubwa maisha ya Ester Juma, mwenye umri wa miaka 32, mkazi wa Tabata Barakuda jijini Dar es Salaam, ambaye kwa zaidi ya miaka 20 amekuwa akiishi na uvimbe mkubwa usoni.

Ester anapitia wakati mgumu huku akihangaika kutafuta fedha kwa ajili ya matibabu na upasuaji wa kuondoa uvimbe huo ambao umeathiri kwa kiasi kikubwa maisha yake ya kila siku.

Akizungumza kuhusu hali yake, Ester amesema amekuwa akikumbana na changamoto mbalimbali anapokuwa katika maeneo ya umma. Anaeleza kuwa baadhi ya watoto humkimbia wanapomuona, huku wakati mwingine hata mtoto wake mwenyewe akimuogopa kutokana na mabadiliko ya sura yake.

Changamoto hiyo, amesema, imemfanya kuishi maisha yenye maumivu na msongo mkubwa huku akiwa na matumaini ya kupata msaada wa matibabu.

Ester amesema aliwahi kufika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kupata matibabu, lakini hakufanikiwa kuanza mchakato huo baada ya kushindwa kupata Shilingi 450,000 zinazohitajika kwa ajili ya vipimo.

Kwa sasa, Ester anaendelea kuomba msaada kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kupata fedha za vipimo na hatimaye kufanyiwa upasuaji.

Mtu yeyote aliyeguswa na hali ya Ester na angependa kumsaidia anaweza kuchangia kupitia namba 0760 780914, jina Magoli Juma.

Yanga Yamtumia Fabrizio Romano Kutambulisha Jezi za Ligi Ya Mabingwa

Global Publishers
September 3, 2026
0 views
0 Comments

Klabu ya Yanga imemtumia mwandishi maarufu wa habari za michezo duniani, hususan taarifa za usajili wa wachezaji, Fabrizio Romano, kutambulisha jezi zake zitakazotumika katika michuano ya CAF Champions League msimu wa 2026/2027.

Romano, raia wa Italia, amejizolea umaarufu mkubwa duniani kupitia taarifa zake za usajili wa wachezaji na kauli yake maarufu “Here We Go”. Katika tukio hilo, ametumika kuitambulisha jezi ya Yanga ya michuano ya kimataifa, hatua inayotajwa kuwa sehemu ya mkakati wa klabu hiyo kukuza na kuitangaza chapa yake katika soko la kimataifa.

Yanga, ambayo ni moja ya wawakilishi wa Tanzania katika CAF Champions League msimu wa 2026/2027, imeendelea kuweka mkazo katika kuongeza mwonekano wa klabu hiyo kwenye jukwaa la kimataifa, sambamba na dhamira yake ya kufanya vizuri katika michuano ya Afrika.

Uamuzi wa kutumia jina kubwa kama Romano katika utambulisho huo umeipa Yanga fursa ya kufikisha utambulisho wa klabu na jezi zake kwa hadhira kubwa ya mashabiki wa soka duniani.

PPRA Yatangaza Nafasi 10 za Ajira Katika Kada za TEHAMA

Dodoma, Septemba 1, 2026 — Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS), kwa niaba ya Public Procurement Regulatory Authority (PPRA), imetangaza nafasi 10 za ajira kwa Watanzania wenye sifa na uwezo unaohitajika.

Tangazo hilo lenye Kumb. Na. JA.9/16/01/54 limetolewa tarehe 1 Septemba 2026, likiwa na nafasi katika kada mbalimbali za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Nafasi zilizotangazwa

  1. ICT Officer II (Software Development – Frontend) — Nafasi 3
  2. ICT Officer II (Software Development – Backend) — Nafasi 4
  3. ICT Officer II (Artificial Intelligence Applications) — Nafasi 2
  4. ICT Officer II (Systems Analyst) — Nafasi 1

 

ICT Officer II – Software Development (Frontend)

Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa na Shahada ya Computer Science, Software Engineering, Information Technology, Information Systems, Computer Engineering au sifa inayolingana nayo kutoka taasisi inayotambuliwa.

Mwombaji anatakiwa kuwa na uzoefu wa vitendo katika miradi ya kutengeneza programu au portfolio inayoweza kuthibitisha uwezo wake. Pia anatakiwa kuwa na ujuzi wa Angular, TypeScript, HTML5, Tailwind CSS na teknolojia za kisasa za utengenezaji wa interfaces.

Aidha, anapaswa kuwa na ujuzi wa kutengeneza applications za simu kwa kutumia Flutter na Dart, kuunganisha mifumo na REST APIs na GraphQL, pamoja na kutumia Git, GitHub au GitLab.

Ujuzi wa UI/UX kwa kutumia Figma au zana nyingine zinazohusiana nao utakuwa faida ya ziada.

Mshahara: PPRA 5

ICT Officer II – Software Development (Backend)

Nafasi hizi zinahitaji mwombaji mwenye Shahada ya Computer Science, Software Engineering, Information Technology, Information Systems au Computer Engineering kutoka taasisi inayotambuliwa.

Mwombaji anatakiwa kuwa na ujuzi wa Java 21 au zaidi, Spring Boot, Spring Data JPA, Hibernate, REST APIs, GraphQL, PostgreSQL, RabbitMQ na mifumo ya asynchronous na event-driven architecture.

Ujuzi wa Kubernetes, Redis, Spring Security, OAuth2, JWT, JUnit 5, GraphiQL na Postman utakuwa faida ya ziada.

Mshahara: PPRA 5

ICT Officer II – Artificial Intelligence Applications

Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa na Shahada ya Computer Science, Software Engineering, Artificial Intelligence, Data Science au taaluma nyingine inayohusiana na teknolojia.

Mwombaji anatakiwa kuwa na ujuzi wa Python, TypeScript au JavaScript, pamoja na uzoefu katika AI execution pipelines, RESTful APIs, JSON na asynchronous programming.

Pia anatakiwa kuwa na uzoefu wa kutumia au kusanidi Large Language Models (LLMs) zinazoweza kuendeshwa ndani ya mifumo kama Ollama, LM Studio, vLLM au LocalAI, au kutumia huduma za LLM za mtandaoni kama OpenAI, Gemini au Anthropic.

Ujuzi wa prompt engineering, structured outputs, JSON schemas, function calling, tool use, agentic AI workflows, embeddings, vector databases na Retrieval-Augmented Generation (RAG) utahitajika kulingana na mahitaji ya nafasi.

Mshahara: PPRA 5

ICT Officer II – Systems Analyst

Nafasi hii inahitaji mwombaji mwenye Shahada ya Computer Science, Information Systems, Information Technology, Software Engineering, Computer Engineering, Business Information Systems au sifa inayolingana nayo.

Mwombaji anatakiwa kuwa na uelewa au uzoefu wa vitendo katika systems analysis, enterprise information systems, user requirements gathering, system testing, ICT user support, business process analysis na technical documentation.

Ujuzi katika cybersecurity, enterprise applications na Government ICT systems utakuwa faida ya ziada.

Mshahara: PPRA 5

Masharti muhimu ya maombi

PSRS imesema waombaji wote lazima wawe raia wa Tanzania na wasizidi umri wa miaka 45.

Waombaji wanatakiwa kuambatanisha nakala zilizothibitishwa za vyeti vyao vya elimu na taaluma, transcripts, vyeti vya usajili wa kitaaluma pale inapohitajika, pamoja na cheti cha kuzaliwa.

Aidha, Form IV na Form VI result slips, testimonials na partial transcripts hazitakubalika.

Mwombaji anatakiwa pia kupakia picha ya Passport Size ya hivi karibuni katika Recruitment Portal na kutaja referees watatu wenye mawasiliano yanayoaminika.

Waombaji wenye vyeti vya elimu vya nje ya Tanzania wanatakiwa kuhakikisha vyeti hivyo vimetambuliwa na mamlaka husika, ikiwemo TCU, NECTA au NACTVET.

Jinsi ya kutuma maombi

Maombi yote yanatakiwa kuwasilishwa kupitia Recruitment Portal ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Recruitment Portal: portal.ajira.go.tz

Barua ya maombi inapaswa kuandikwa kwa Kiswahili au Kiingereza, kusainiwa na kuelekezwa kwa:

Secretary,
President’s Office, Public Service Recruitment Secretariat,
P.O. Box 2320,
Mahakama Street, Tambukareli,
Dodoma.

Mwisho wa kutuma maombi

Mwisho wa kutuma maombi ni Septemba 14, 2026.

PSRS imesema ni waombaji watakaoteuliwa pekee ndio watakaofahamishwa kuhusu tarehe ya usaili.

Aidha, mwombaji atakayewasilisha vyeti vya kughushi au taarifa za uongo atachukuliwa hatua za kisheria.

Maombi yatakayowasilishwa kupitia njia nyingine tofauti na Recruitment Portal hayatazingatiwa.

Chanzo: Public Service Recruitment Secretariat (PSRS), Tangazo Kumb. Na. JA.9/16/01/54, Septemba 1, 2026.

MIILI WALIOKUFA AJALI YA MELI KIGOMA YAAGWA, YASAFIRISHWA DRC

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Mkuu wa wilaya Kigoma Dk.Rashid Chuachua ameongoza viongozi wa serikali za Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (RDC) na Burundi kuaga miili ya watu sita waliofariki katika ajali ya kuteketea kwa moto kwa meli ya Mv.Pasific kwenye bandari ya Kigoma usiku wa Agosti 28 mwaka huu 

Miili hiyo imeagwa katika hospitali ya mkoa Kigoma Maweni na kusafirishwa kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) ambapo Mkuu huyo wa wilaya Kigoma akimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma, Balozi Simon Sirro alisema kuwa serikali ya mkoa Kigoma kwa niaba ya serikali ya Tanzania inatoa pole kwa ndugu,jamaa, marafiki na serikali ya DRC kwa kuondokewa na watu hao ambao walikuwa wakifanya kazi ya kusadia kusafirisha abiria na mali kutoka Tanzania kwenda DRC.

Dk.Chuachua alisema kuwa serikali ya Tanzania kupitia vyombo vya ulinzi na usalama na kikosi cha zimamoto walichukua hatua madhubuti kuhakikisha kwanza wanapambana na moto lakini pia kuhakikisha wanaokoa maisha na mwisho kutafuta miili ya watu waliokuwepo kwenye meli hiyo na kwamba mapenzi ya Mwenyezi Mungu yametimizwa hadi leo miili hii inaposafirishwa kwenda DRC kwa mazishi.

Kwa upande wake Katibu wa CCM mkoa Kigoma, Christopher Pallangyo akitoa salamu za Katibu Mkuu wa CCM,Dk,Asha Rose Migiro alisema kuwa chama kimeguswa na msiba huo na kinatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki na serikali ya DRC kwani nchi hizi mbili ni ndugu na marafiki tukishirikiana kwa mambo mengi kwa manufaa ya nchi hizo mbili na watu wake.

Naye Balozi Mdogo wa ubalozi wa Burundi mkoani Kigoma, Kekenwa Jeremeah alisema kuwa serikali ya nchi hiyo imaungama na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Tanzania kwani marehemu walikuwa wakifanya kazi ambayo imekuwa ikiziunganisha nchi hizo kupitia ziwa Tanganyika.

Akizungumza katika ibada hiyo ya kuaga miili Balozi mdogo wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika ubalozi mdogo wa DRC Kigoma, Loius Kinyamba alisema kuwa serikali ya nchi hiyo imepokea kwa masikitiko makubwa vifo vya mabaharia hao na inatoa pole kwa ndugu wa marehemu hao.

Pamoja na hilo Balozi huyo amesema kuwa watafuatilia kwa kina sababu za tukio hilo na kuchukua hatua lakini pia akitoa wito kwa manahodha na wamiliki wa meli kuhakikisha wanawasilisha majina ya abiria wote wanaosafiri kweny meli zao, aina ya mizigo wanayosafirisha na uzito wake wakieleza maeneo ambayo mizigo na abiria hao wanakwenda akieleza kuwepo kwa udhaifua wa kupatikana kwa taarifa muhimu za meli hiyo zinazpopata ajali.

Mwisho.

 

SERIKALI YAIMARISHA UHIMILIVU BEI ZA MAFUTA NCHINI

Na Matukio Daima Media 

SERIKALI imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha bei za mafuta nchini zinakuwa himilivu na zinalinda maslahi ya wananchi, ikiwa ni pamoja na kuimarisha usimamizi wa soko na kuhakikisha upatikanaji wa mafuta kwa wakati katika maeneo mbalimbali nchini.

Hatua hizo zimechangia kupunguza athari za mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia.

Kwa mwezi Septemba 2026, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei za mafuta hali inayotarajiwa kuleta unafuu kwa watumiaji.

Bei ya petroli imepungua kwa shilingi 102 kwa lita, huku bei ya dizeli ikishuka kwa shilingi 101 kwa lita.

EWURA imeonya kuwa wauzaji wa mafuta watakaokiuka bei elekezi watachukuliwa hatua kali za kisheria, na kwamba wakaguzi wa Mamlaka hiyo tayari wapo kazini katika maeneo mbali mbali kuhakikisha sheria na taratibu zinafuatwa. Watumiaji wa mafuta wameshauriwa kuchukua risiti wanaponunua mafuta, kwani nyaraka hizo hutumika kama ushahidi kunapokuwa na changamoto yoyote.

JUDITH LAIZER ASHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA KWA KUWAFIKIA WATOTO WENYE MAHITAJI MOROGORO

Matukio Daima Media, Morogoro 

 Katibu wa Jumuiya ya Wanawake, UWT, Morogoro Mjini, Judith Laizer, ameamua kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa namna tofauti, baada ya kutumia sehemu ya siku hiyo kwa yeye na familia yake kuwafikia watoto yatima na wenye mahitaji maalum wanaolelewa katika Kituo cha Agape, Kihonda, Manispaa ya Morogoro.

Katika maadhimisho hayo, Judith alishirikiana na watoto hao kukata keki na kula pamoja, huku akiwapatia baadhi ya mahitaji ya kibinadamu. 

Hatua hiyo ilifanya siku yake ya kuzaliwa kuwa ya kipekee, huku watoto hao wakipata fursa ya kufurahia na kusherehekea pamoja naye.

Judith amesema kwake, kusherehekea siku ya kuzaliwa siyo tu kukusanyika na familia na marafiki, bali pia ni fursa ya kushirikiana furaha na watu wengine, hususan watoto wanaohitaji upendo, faraja na msaada kutoka kwa jamii.

Baada ya shughuli hizo katika kituo cha Agape,na kutoa wito kwa jamii kuwakumbuka watoto Wenye uhitaji kwa mahitaji mbalimbali ya kibinadamu.

Mlezi wa Kituo cha Agape aliyejitambulisha kwa jina la Mama Tina, Raia wa Kigeni aliyelowea nchini  kwa miaka mingi, amesema kituo hicho kina watoto zaidi ya 40 ambapo wengine wako shule za bweni, na wamewalea watoto ambao wengine kwasasa wameshafikia hatua ya kujitegemea na wengine wanasoma elimu ya juu.

Akatoa wito kwa watu wenye mapenzi mema kuwatembelea watoto kituoni hapo na kuwapatia msaada wa mahitaji kikiwemo chakula, Vifaa vya shule, mavazi na mahitaji mengine muhimu ya kijamii.

Kwa upande wake Judith aliendelea na sherehe ndogo nyumbani kwake maeneo ya Kihonda akiwa ndugu, jamaa na Marafiki wachache, akihimiza Umoja na mshikamano katika kufikia mafanikio yeyote kwa kila mtanzania.

Mwisho