Mbunge ashauri uwekezaji zaidi NM-AIST – HabariLeo

ARUSHA: SERIKALI imeshauriwa kuongeza uwekezaji na kutumia kikamilifu uwezo wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) katika tafiti, ubunifu na kubadilisha matokeo ya tafiti hizo kuwa bidhaa na huduma za kibiashara zitakazochochea maendeleo ya uchumi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Ushauri huo umetolewa na Mbunge wa Msalala, Mabula Magangila, wakati akichangia mjadala kuhusu maendeleo ya sayansi na teknolojia katika ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo iliyotembelea taasisi hiyo kujionea shughuli za utafiti na utekelezaji wa programu ya Samia Scholarship.

Amesema NM-AIST inaaminika barani Afrika kutokana na mchango wake katika tafiti, ubunifu na kukuza uwezo wa wataalamu, hivyo Serikali inapaswa kuwekeza zaidi ili matokeo ya kazi hizo yaonekane na kunufaisha jamii.

Amesisitiza kuwa uwekezaji wa Serikali katika taasisi za sayansi na teknolojia unapaswa kuelekezwa pia katika kubuni bidhaa na teknolojia zinazoweza kuzalishwa na kuuzwa kibiashara, akieleza kuwa sekta binafsi haiwezi kuchukua nafasi ya Serikali katika uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya utafiti.

Hata hivyo, ameshauri kuwekwa kwa mifumo itakayowezesha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi ili kuendeleza bunifu na kuzifanya kuwa fursa za kiuchumi.

Akizungumzia miundombinu ya teknolojia ya taarifa, amesema vituo vya kuhifadhi na kusimamia taarifa za kidijitali vinaweza kuwa chanzo muhimu cha mapato kwa taifa endapo vitaendelezwa kwa ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi.

Ameeleza kuwa Tanzania inaweza kutumia miundombinu hiyo kutoa huduma za kuhifadhi na kulinda taarifa kwa taasisi za ndani na nje ya nchi, ikiwemo masoko ya Afrika na kimataifa, na hivyo kuongeza mapato kupitia mauzo ya huduma za teknolojia. Pia ameipongeza NM-AIST kwa kazi na uwekezaji unaofanyika, akisema ni msingi muhimu wa kuimarisha uwezo wa Tanzania katika sayansi, teknolojia na ubunifu.

Takukuru kukamilisha majengo 93 nchi nzima – HabariLeo

ARUSHA: TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inatarajia kukamilisha ujenzi wa majengo 93 ya ofisi katika maeneo mbalimbali nchini ifikapo Julai 2027, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kusogeza huduma karibu na wananchi.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila, alisema hayo wilayani Karatu mkoani Arusha wakati wa uzinduzi wa jengo la taasisi hiyo lililojengwa kwa gharama ya Sh milioni 405, kutoka bajeti ya awali ya Sh milioni 421.

Alisema serikali imeendelea kuiwezesha taasisi hiyo kwa fedha za ujenzi wa miundombinu ya ofisi pamoja na mafunzo ya kuwawezesha watumishi kutekeleza majukumu yao kwa kutumia mifumo ya kisasa.

Zawadi Ngailo Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha.

Alisema kuwa ifikapo mwaka 2030, kila wilaya nchini inatarajiwa kuwa na jengo la TAKUKURU lenye hadhi inayolingana na majukumu ya taasisi hiyo, hatua inayolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.

Chalamila alisema uwekezaji huo hauishii kwenye miundombinu pekee, bali pia unahusisha kuimarisha idara za operesheni na uchunguzi ili kuongeza ufanisi katika kuzuia na kupambana na rushwa.

Akizungumzia gharama za ujenzi wa jengo la Karatu, alisema matumizi ya Sh milioni 405 badala ya bajeti ya Sh milioni 421, na kubaki kwa Sh milioni 15, yanaonesha umuhimu wa kuzingatia thamani ya fedha katika utekelezaji wa miradi ya umma.

Alizitaka halmashauri nchini kuzingatia misingi hiyo katika usimamizi wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Aidha, alisema TAKUKURU imeingiza elimu ya uzalendo, uadilifu, maadili na mapambano dhidi ya rushwa katika mitaala ya shule za msingi, sekondari na vyuo vya kati ili kujenga jamii inayozingatia misingi hiyo tangu ngazi za awali za elimu.

Baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la ofisi ya Takukuru wilaya ya Karatu

Alisema elimu hiyo inalenga kuwajengea wanafunzi uelewa wa madhara ya kutoa na kupokea rushwa pamoja na umuhimu wa kutekeleza majukumu kwa kuzingatia maadili.

Aliongeza kuwa taasisi hiyo inaendelea kuhamasisha uanzishwaji wa klabu za wapinga rushwa katika shule, vyuo, taasisi za dini na makundi mbalimbali ya kijamii ili kuongeza ushiriki wa wananchi katika mapambano dhidi ya vitendo hivyo.

Katika hatua nyingine, Chalamila alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wananchi na kuzitaka halmashauri kuweka wazi taarifa za miradi ya maendeleo kwenye mbao za matangazo ili wananchi waweze kufuatilia utekelezaji wake na kujiridhisha kama thamani ya fedha imezingatiwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Lameck Karanga, alisema tangu kuanzishwa kwa wilaya hiyo, TAKUKURU ilikuwa ikitoa huduma katika nyumba za kupanga, hivyo kukamilika kwa jengo hilo kutaimarisha upatikanaji wa huduma za taasisi hiyo.

Naye Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha, Zawadi Ngailo, alisema ujenzi wa jengo hilo ulianza Februari mwaka huu na kukamilika Agosti mwaka huu kwa kuzingatia muda na taratibu za manunuzi.

Alisema taasisi hiyo ilipata kiwanja cha ujenzi mwaka 2012 na kukamilisha taratibu za umiliki, huku Mkoa wa Arusha ukiwa na majengo manne ya ofisi yanayomilikiwa na TAKUKURU.

Binance Yafidia Takribani Asilimia 90 ya Fedha Zilizoibwa, FBI Yaitaja Korea Kaskazini

Binance Yafidia Takribani Asilimia 90 ya Fedha Zilizoibwa, FBI Yaitaja Korea Kaskazini – TeknoKona Teknolojia Tanzania

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_1-bc9efc15c341-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-js-js-front-end-breeze-prefetch-links.min-81119a57b31d-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-js-jquery-jquery.min-6836d82c2675-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-js-jquery-jquery-migrate.min-2346c86992b8-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-weglot-dist-front-js-9226ba194f92-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_2-a785a75a34a1-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_3-323462673fc7-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_4-6add049d5794-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-youtube-embed-plus-scripts-ytprefs.min-41b8ef8d5516-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_5-dc5440dbebd1-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_6-d510bf7efb2d-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_7-2f6ca4f1f852-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_8-89743c229303-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_9-f4af2ae5dc4a-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_10-e9d1e2357471-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_11-e4923f14768c-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_12-2e1d956dbb67-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_13-92a0d29ebd3b-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_14-b6e2dd7ea1fa-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_15-3419b0a9d48d-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-assets-js-fluent-forms-elementor-widget-fb18c7abb132-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-js-dist-hooks.min-1e6013aecb3f-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-js-dist-i18n.min-8a672a7b3338-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_16-94c4eed60653-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-swv-js-index-8d0927242d72-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_17-32e62a28f1ce-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-includes-js-index-e8b7e8c92e4e-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-assets-js-SmoothScroll.min-132b02aee8b7-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-wp-includes-js-comment-reply.min-5e27e6025459-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_18-a2aa12e87f3f-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-assets-js-main-a7415881660e-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-assets-js-webpack.runtime.min-bb61ccabd4bc-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-assets-js-frontend-modules.min-1c2486988462-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_19-592979563c5d-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-jquery-ui-core.min-bbe779825618-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_20-9246e262c231-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-assets-js-frontend.min-562b3159aee7-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-js-js-front-end-breeze-lazy-load.min-ce1a9bcfcae0-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_21-1c580bd2ffb2-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_22-e8f29744624c-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-wp-content-copy-protector-js-activity-tracker-9e0626ce27a9-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-youtube-embed-plus-scripts-fitvids.min-a18894311799-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_23-04c99766675b-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-dist-js-public.min-3e807f9c1e46-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-akismet-_inc-akismet-frontend-632bfb5d2300-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_24-5ed549545e8d-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-ank-simplified-ga-assets-front-end.min-888431ccbdc3-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_binance-wizi-dola-bilioni-6-3-korea-kaskazini-1-49038-inline_script_25-7da672e85abf-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793527387

Meridianbet Yaleta Mchezo Mpya wa 25 Magic Plums Wenye Grand Jackpot ya X1000

Global Publishers
November 1, 2026
48 views
0 Comments

Wapenzi wa burudani za kasino mtandaoni, kuna mchezo mpya unaostahili kufahamika. Meridianbet imeongeza 25 Magic Plums kutoka Wazdan kwenye jukwaa lake kwa uzinduzi wa kipekee wa mapema. Mchezo huu unapatikana kuanzia sasa hadi Novemba 10, 2026, ukiwaletea wachezaji muonekano wa kuvutia na vipengele vinavyoongeza msisimko. Kinachovutia zaidi ni safari kuelekea mchezo wa bonasi na Grand Jackpot yenye thamani ya mara 1,000 ya dau husika.

Katika michezo ya ushindani, kila hatua huleta matarajio ya kuona kitakachofuata. Ndivyo ilivyo pia katika 25 Magic Plums, ambako mizunguko inaambatana na picha angavu na muundo wenye mvuto. Mchezo huu umetengenezwa ili kutoa uzoefu unaochanganya urahisi wa kufurahia muonekano wake na msisimko wa kuchunguza vipengele mbalimbali. Kupitia Meridianbet, wapenzi wa michezo ya kasino wana nafasi ya kuifahamu burudani hii mpya.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jisajili leo kwa kutembelea tovuti ya MERIDIANBET au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Miongoni mwa vipengele muhimu ni Chance Level, kinachosaidia kufupisha safari kuelekea bonasi. Hapo ndipo mvuto wa Grand Jackpot ya x1000 unapoongezeka, kwani mchezo unatoa uwezekano wa kufikia hatua hiyo kulingana na matokeo yake.

Mbali na Chance Level, mchezo huu una kipengele cha Cash Out kinachoongeza matukio ya kuvutia wakati wa mchezo wa kawaida. Mchanganyiko huu unaifanya 25 Magic Plums kuwa chaguo jipya kwa wanaopenda michezo yenye vipengele tofauti na muonekano unaovutia. Meridianbet inaendelea kupanua burudani inayopatikana kwenye jukwaa lake, ikiwaruhusu wateja kuchunguza michezo mbalimbali kwa kuzingatia mipaka yao ya matumizi.

Sasa ni wakati wa kugundua 25 Magic Plums kupitia Meridianbet. Mchezo huu unapatikana kwa uzinduzi wa mapema hadi Novemba 10, 2026. Tembelea Meridianbet, jifunze namna mchezo unavyofanya kazi na ufurahie burudani yake huku ukitengeneza faida kubwa wakati wa mchezo.

Vita Ya Ubingwa EPL! Liverpool Kuikaribisha Arsenal Anfield Leo

Global Publishers
November 1, 2026
36 views
0 Comments

Mchezo wa Ligi Kuu ya England (EPL) kati ya Liverpool na Arsenal unatarajiwa kupigwa leo Jumapili, katika uwanja wa Anfield, kuanzia saa 19:30 usiku. Hili ni pambano muhimu kwa timu zote mbili, ambazo zinahitaji alama tatu ili kuimarisha nafasi zao katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi hiyo.

Liverpool wataingia katika mchezo huo wakiwa na matumaini ya kutumia faida ya uwanja wao wa nyumbani kupata ushindi. Kikosi hicho kimeonyesha uwezo mzuri katika michezo yake ya hivi karibuni ya ligi, ikiwemo ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Brighton. Hata hivyo, majeraha ya baadhi ya wachezaji, akiwemo Dominik Szoboszlai na Hugo Ekitike, yanaweza kuwa changamoto katika maandalizi ya mchezo huo.

Kwa upande wa Arsenal, kikosi cha kocha Mikel Arteta kitakuwa na dhamira ya kupata matokeo mazuri ugenini ili kuendelea kuwa katika nafasi nzuri ya kuwania taji. Arsenal wamekuwa na matokeo mazuri katika michezo yao ya hivi karibuni, ikiwemo ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Everton. Hata hivyo, kutokuwepo kwa Bukayo Saka kutokana na jeraha la paja kunaweza kuathiri mipango yao ya kushambulia.

Katika mchezo huo, vita ya kiungo na matumizi ya nafasi za kufunga mabao vitakuwa mambo muhimu yatakayoweza kuamua matokeo. Liverpool wanaweza kutumia kasi ya mashambulizi yao na sapoti ya mashabiki wa Anfield, huku Arsenal wakitegemea umiliki wa mpira, pasi za haraka na ubunifu wa wachezaji wao wa mbele. Timu itakayokuwa makini zaidi katika safu ya ulinzi na kutumia nafasi zake kwa ufanisi itakuwa na nafasi nzuri ya kupata ushindi.

 

Kwa habari na taarifa mbalimbali za michezo usisite kutembelea meridianbet ili upate mambo yote yanayotokea na kuendelea kwenye ulimwengu wakimichezo, ikiwemo michuano mikubwa ya Africa, Ulaya na ile ya falme za kiaarabu zote zinapatikana hapa.

Kwa kuzingatia ubora wa vikosi hivyo na ushindani wa Ligi Kuu ya England, mashabiki wanatarajia mchezo wenye kasi na ushindani mkubwa kwa dakika zote 90. Ushindi kwa Liverpool utawasaidia kupunguza pengo la alama dhidi ya Arsenal, wakati wageni hao wakilenga kuimarisha nafasi yao katika mbio za ubingwa. Hivyo, pambano hilo linatarajiwa kuwa miongoni mwa michezo inayovuta hisia za mashabiki wa soka mwishoni wikiendi hii.

Chadema Yatuma Salamu za Pole kwa Familia ya Lissu Baada ya Kifo cha Kaka Yake

Global Publishers
November 1, 2026
24 views
0 Comments

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kifo cha Alute Mughwai Lissu, ambaye ni kaka wa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Tundu Lissu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho leo Jumapili, Novemba 1, 2026, Alute amefariki dunia alfajiri ya leo akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha, jijini Arusha.

CHADEMA kimeeleza kuwa kifo hicho kimetokea katika kipindi kigumu kwa familia ya Lissu, ikiwa ni siku chache kabla ya hukumu ya kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu, inayotarajiwa kutolewa Ijumaa, Novemba 6, 2026.

Kupitia taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, chama hicho kimetoa pole kwa Tundu Lissu, familia, ndugu, jamaa, marafiki, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) pamoja na Watanzania wote waliofikwa na msiba huo.

Aidha, CHADEMA kimeeleza kuwa kinaungana na familia katika kipindi hiki cha maombolezo, huku kikiwaombea nguvu, faraja na uvumilivu katika kukabiliana na msiba huo.

Chama hicho kimesema kinaendelea kuwasiliana na familia kuhusu maandalizi na ratiba ya ibada ya mazishi, na kitaendelea kutoa taarifa kadiri kitakavyopokea maelekezo zaidi kutoka kwa familia.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.

Mhandisi Mashauri Jofrey afunguka fursa Tanzania, Urusi – HabariLeo

URUSI: Uhusiano kati ya Tanzania na Urusi unaingia katika sura mpya, huku fursa katika biashara, uwekezaji, elimu, sayansi, teknolojia, nishati, kilimo na viwanda zikionekana kuwa maeneo muhimu ya kuunganisha urafiki wa muda mrefu na mahitaji ya maendeleo ya sasa.

Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan, nchini Urusi mwezi Juni 2026, pamoja na ushiriki wa Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Lameck Nchemba, katika Mkutano wa Tatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Afrika na Urusi uliofanyika Moscow mwezi Oktoba 2026, imeendelea kuweka msukumo katika uhusiano huo.

Hata hivyo, nyuma ya mikutano ya viongozi na diplomasia ya kimataifa kuna swali muhimu: Tanzania inaweza kufanya nini ili fursa zinazotokana na uhusiano huo ziwafikie vijana, wanafunzi, wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla?

Mhandisi Mashauri Jofrey Sabwoya, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Diaspora nchini Urusi na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Tanzania nchini humo, anaangazia fursa hizo, nafasi ya diaspora na namna Tanzania inaweza kutumia uzoefu, maarifa na teknolojia kutoka Urusi kuharakisha maendeleo yake.

𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐍𝐃𝐎 𝐖𝐀 𝐃𝐈𝐏𝐋𝐎𝐌𝐀𝐒𝐈𝐀 𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐍𝐀 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈 𝐊𝐔𝐅𝐔𝐀𝐓𝐈𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐕𝐈𝐎𝐍𝐆𝐎𝐙𝐈 𝐇𝐀𝐎.

Kwa mtazamo wake, Mhandisi Mashauri Jofrey Sabwoya anaona uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Urusi ukiendelea kuimarika na sasa ukiingia katika hatua mpya yenye mwelekeo mkubwa wa kiuchumi, kiteknolojia na kimkakati. Anasema uhusiano huo umejengwa katika misingi ya kihistoria, urafiki, kuheshimiana na kutambua mamlaka ya kila taifa.

Anaeleza kuwa tangu miaka ya mwanzo ya uhuru wa mataifa mengi ya Afrika, Urusi ilikuwa miongoni mwa washirika waliounga mkono harakati za ukombozi wa bara hilo na kujenga ushirikiano na mataifa yaliyokuwa yakijitafutia nafasi katika jumuiya ya kimataifa.

Hata hivyo, anasema fursa iliyopo sasa ni kubadilisha uhusiano huo kutoka katika urafiki wa kihistoria na kisiasa pekee kwenda kwenye ushirikiano unaozalisha manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi. Kwa mujibu wake, ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan, nchini Urusi mwezi Juni 2026, pamoja na ushiriki wa Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, katika Mkutano wa Tatu wa Afrika na Urusi mwezi Oktoba 2026, ni ishara muhimu ya kuendelea kuimarika kwa mahusiano hayo katika ngazi za juu za uongozi.

Rais Dk Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Rais wa Urusi, Vladamir Putin, katika Ikulu ya Urusi wakati wa ziara aliyoifanya Juni 2026 nchini humo.

Mhandisi Mashauri anaona matukio hayo yakifungua fursa za kuimarisha ushirikiano katika maeneo mbalimbali yenye umuhimu kwa maendeleo ya Tanzania, ikiwemo biashara, uwekezaji, elimu, nishati, madini, kilimo, viwanda na teknolojia. Kwa mtazamo wake, hatua muhimu ni kuhakikisha fursa zinazotokana na mahusiano hayo zinatafsiriwa kuwa matokeo yanayoweza kuonekana na wananchi, badala ya kubaki katika mikutano, makubaliano na diplomasia ya ngazi za juu.

Akizungumzia nafasi yake kama Katibu wa CCM Diaspora nchini Urusi, anasema anaamini diaspora ina wajibu wa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuimarisha mahusiano hayo kupitia diplomasia ya wananchi, kuitangaza Tanzania na kujenga mazingira mazuri ya ushirikiano kati ya Watanzania na Warusi. Ujumbe wake mkuu ni kwamba Tanzania na Urusi hazipaswi kubaki kuwa marafiki wa kihistoria pekee, bali zinapaswa kuwa washirika wa maendeleo ya sasa na ya baadaye.

𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐈𝐍𝐀𝐀𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐀 𝐍𝐈𝐍𝐈 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐍𝐃𝐎 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐌𝐊𝐀𝐊𝐀𝐓𝐈 𝐁𝐀𝐈𝐍𝐀 𝐘𝐀 𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐇𝐈𝐙𝐎?

Mhandisi Mashauri Jofrey Sabwoya anaona ziara mbili za viongozi waandamizi wa Tanzania nchini Urusi mwaka 2026 kuwa na umuhimu mkubwa katika kuonesha dhamira ya taifa kupanua ushirikiano wake wa kimataifa na kutumia diplomasia kama nyenzo ya kuharakisha maendeleo. Anasema ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan, nchini humo mwezi Juni mwaka huu ilikuwa ya kihistoria, ikiwa ni ziara ya pili ya Rais wa Tanzania nchini Urusi baada ya ile ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, iliyofanyika Oktoba 1969.

Kwa mujibu wa Sabwoya, ziara hiyo ilikuwa na nafasi muhimu katika historia ya kidiplomasia ya mataifa hayo mawili, kwa kuwa iliwapa viongozi fursa ya kujadili mustakabali wa mahusiano yao na kuimarisha maeneo ya ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote. Aidha, anasema ziara ya Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba, mwezi Oktoba 2026, aliyemwakilisha Rais katika Mkutano wa Tatu wa Afrika na Urusi, imeonesha mwendelezo wa juhudi za Tanzania za kuimarisha ushirikiano huo katika mfumo mpana wa mahusiano kati ya Afrika na Urusi.

Mhandisi Mashauri Jofrey Sabwoya, Katibu wa CCM Diaspora Urusi, akimkaribisha na kuzungumza na  Waziri Mkuu Dk Mwigulu Lameck Nchemba wakati wa ziara yake nchini Urusi.

Akifafanua umuhimu wa ziara hizo, Sabwoya anazitaja kuwa na mwelekeo katika maeneo matatu muhimu, ambayo ni diplomasia ya uchumi, ushirikiano wa kimkakati na diplomasia ya matokeo. Anasema kupitia diplomasia ya uchumi, Tanzania inaweza kutumia mahusiano yake ya kimataifa kuvutia mitaji, wawekezaji, teknolojia na masoko mapya ya bidhaa zake. Katika ushirikiano wa kimkakati, anaona umuhimu wa kupanua wigo wa washirika katika sekta za nishati, madini, usafirishaji, kilimo, elimu na viwanda. Hata hivyo, anasisitiza kuwa mazungumzo ya viongozi yanapaswa kuzaa miradi, ajira, biashara, mafunzo na fursa zinazogusa maisha ya wananchi.

Anasisitiza kuwa Tanzania ina sera ya kushirikiana na mataifa mbalimbali kwa kuzingatia maslahi yake ya kitaifa, hivyo kuimarisha uhusiano na Urusi hakumaanishi kuachana na washirika wengine, bali ni kupanua wigo wa fursa za maendeleo. Kwa mtazamo wake, ziara hizo zinatoa nafasi ya kuifanya diplomasia ya Tanzania kuwa daraja la kuunganisha nchi na fursa za uwekezaji, biashara, teknolojia na maendeleo ya wananchi.

𝐅𝐔𝐑𝐒𝐀 𝐒𝐈𝐓𝐀 𝐙𝐀 𝐊𝐈𝐌𝐊𝐀𝐊𝐀𝐓𝐈 𝐀𝐌𝐁𝐀𝐙𝐎 𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐈𝐓𝐀𝐍𝐔𝐅𝐀𝐈𝐊𝐀 𝐍𝐀 𝐔𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈𝐀𝐍𝐎 𝐇𝐔𝐎

Mhandisi Mashauri Jofrey Sabwoya anasema uzoefu alioupata wakati akiishi na kujifunza nchini Urusi umemwezesha kubaini maeneo sita ya kimkakati ambayo Tanzania inaweza kuyatumia kupanua ushirikiano na taifa hilo kwa manufaa ya uchumi wake.

Anayataja maeneo hayo kuwa ni nishati na umeme, madini na utafiti wa kijiolojia, kilimo na usalama wa chakula, viwanda na teknolojia, teknolojia za kidijitali na akili bandia pamoja na usafirishaji na miundombinu ya biashara.

Katika eneo la nishati na umeme, Sabwoya anasema Urusi ina uzoefu katika uzalishaji wa umeme, uhandisi wa nishati na teknolojia ya nyuklia kwa matumizi ya amani, ambao Tanzania inaweza kuutumia kuongeza utaalamu, kuendeleza miundombinu ya nishati na kujenga uwezo wa wataalamu wake. Pia anaona sekta ya madini kuwa na nafasi kubwa ya ushirikiano, akieleza kuwa uzoefu wa Urusi katika utafiti wa kijiolojia, teknolojia za uchimbaji na usindikaji unaweza kusaidia Tanzania kuongeza thamani ya madini kama dhahabu, urani, nikeli na shaba ndani ya nchi badala ya kutegemea kuuza malighafi pekee. Hata hivyo, anasisitiza kuwa miradi ya nishati inapaswa kuzingatia usalama, gharama, utunzaji wa mazingira na mahitaji ya wananchi.

Akizungumzia kilimo na usalama wa chakula, anasema Tanzania inaweza kunufaika na uzoefu wa Urusi katika uzalishaji wa nafaka, mitambo ya kilimo na teknolojia za uzalishaji wa pembejeo. Anataja fursa za ushirikiano katika upatikanaji wa mbolea, teknolojia za uzalishaji wake, mitambo ya kisasa, tafiti za mbegu bora, uhifadhi na uchakataji wa mazao pamoja na uwekezaji katika viwanda vya kusindika mazao. Kwa maoni yake, ushirikiano huo unapaswa kulenga kuongeza uzalishaji wa mkulima, kupunguza upotevu wa mazao na kumwezesha kupata masoko yenye tija.

Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Lameck Nchemba katika kikao na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, kilicholenga kutafuta fursa za masoko kwa bidhaa za Tanzania nchini Urusi.

Katika sekta ya viwanda na teknolojia, Sabwoya anasema uwezo wa Urusi katika uhandisi, utengenezaji wa mashine, kemikali, dawa na vifaa vya kisayansi unaweza kuwa fursa ya kuvutia wawekezaji kuanzisha viwanda nchini Tanzania.

Anataja viwanda vya mbolea, dawa, vifaa vya kilimo na uchakataji wa madini kuwa miongoni mwa maeneo yanayoweza kupewa kipaumbele. Pia anaona umuhimu wa ushirikiano katika teknolojia za kidijitali na akili bandia, ikiwemo programu za kompyuta, usalama wa mifumo ya taarifa, roboti na uchambuzi wa takwimu, pamoja na kuboresha usafirishaji wa bidhaa, mifumo ya ugavi, taratibu za forodha na mifumo salama ya malipo ya biashara kati ya mataifa hayo mawili. Anasema kwa kuunganisha rasilimali za Tanzania na teknolojia, maarifa na uzoefu wa Urusi, nchi hizo zinaweza kujenga ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote.

𝐒𝐎𝐊𝐎 𝐋𝐀 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈: 𝐅𝐔𝐑𝐒𝐀 𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀𝐁𝐈𝐀𝐒𝐇𝐀𝐑𝐀 𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀

Akizungumzia fursa za biashara, Mhandisi Mashauri Jofrey Sabwoya anasema soko la Urusi ni eneo ambalo wafanyabiashara wengi wa Tanzania bado hawajalitumia kikamilifu, licha ya kuwa na nafasi ya kupanua mauzo ya bidhaa na huduma za Tanzania. Anaeleza kuwa soko hilo linaweza kuwa miongoni mwa maeneo mapya ya kukuza biashara za Watanzania na kuongeza wigo wa masoko ya bidhaa zinazozalishwa nchini.

Anataja maeneo matano yenye fursa, ambayo ni mazao ya kilimo na bidhaa za chakula, utalii, bidhaa za madini na vito, ushirikiano wa viwanda na uwekezaji wa pamoja pamoja na huduma za kitaalamu na biashara za kidijitali.

Katika eneo la mazao ya kilimo na chakula, Sabwoya anasema Tanzania inaweza kuongeza mauzo ya kahawa, chai, korosho, viungo, matunda na bidhaa nyingine za kilimo katika soko la Urusi. Hata hivyo, anasisitiza umuhimu wa kuhakikisha bidhaa hizo zinakidhi viwango vya ubora, usalama wa chakula, vifungashio na masharti ya uingizaji bidhaa katika soko hilo. Pia anaitaja sekta ya utalii kuwa na nafasi ya kuvutia wageni wengi zaidi kutoka Urusi kwa kuitangaza Tanzania kupitia vivutio vyake vya kipekee, vikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Mlima Kilimanjaro, Zanzibar na utajiri wa utamaduni. Anaona ushirikiano na kampuni za utalii, mawakala wa safari na mashirika ya ndege kuwa njia mojawapo ya kufungua fursa hiyo.

“Katika eneo la madini na vito, Tanzania inaweza kupanua nafasi yake katika soko la kimataifa kwa kuuza vito, madini yaliyoongezwa thamani na bidhaa zinazotokana na rasilimali zake, kwa kuzingatia sheria za biashara na viwango vya kimataifa,” anasema.

Aidha, anaona uwezekano wa wafanyabiashara wa Tanzania kuingia ubia na kampuni za Urusi katika uwekezaji wa viwanda, hususan vya usindikaji wa chakula, uzalishaji wa mbolea, dawa na teknolojia za kilimo. Kwa upande wa huduma za kitaalamu na biashara za kidijitali, anataja fursa katika teknolojia, elimu, tafsiri na ushauri wa biashara zinazoweza kuunganisha kampuni za mataifa hayo mawili.

Hata hivyo, Sabwoya anasema ili wafanyabiashara wa Tanzania wanufaike kikamilifu na fursa hizo, wanahitaji kuwa na taarifa sahihi za soko, washirika wanaoaminika, uelewa wa lugha na maarifa ya taratibu za kisheria na kibiashara. Anaeleza kuwa jumuiya ya Watanzania wanaoishi Urusi inaweza kuwa kiungo muhimu katika kuwaunganisha wafanyabiashara wa nchi hizo mbili, kutoa taarifa za fursa na kuwaelekeza katika taasisi husika. Anasema anatamani kuona mfanyabiashara wa Tanzania anapofika Urusi tayari ana taarifa sahihi, bidhaa yenye ubora, mshirika wa biashara na mpango wa kuingia sokoni, badala ya kuanza kutafuta mahitaji hayo baada ya kuwasili nchini humo.

𝐄𝐋𝐈𝐌𝐔 𝐍𝐀 𝐔𝐓𝐀𝐅𝐈𝐓𝐈: 𝐅𝐔𝐑𝐒𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐀𝐍𝐃𝐀𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐀𝐀𝐋𝐀𝐌𝐔 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎 𝐘𝐀 𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀

Mhandisi Mashauri Jofrey Sabwoya anaitaja elimu kuwa miongoni mwa nguzo muhimu za kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Urusi, akisisitiza kuwa ushirikiano katika eneo hilo haupaswi kuishia katika kuwapeleka wanafunzi kusoma nje ya nchi, bali kuwa mkakati mpana wa kujenga rasilimali watu wenye maarifa, ujuzi, ubunifu na uwezo wa kutatua changamoto za maendeleo ya taifa.

“Urusi ina historia na uzoefu katika elimu ya sayansi, teknolojia, tiba, uhandisi, hisabati, fizikia, kemia na tafiti mbalimbali za kitaalamu, hivyo Tanzania inaweza kutumia fursa hiyo kuandaa wataalamu katika sekta muhimu kwa maendeleo yake,” anasema Mhandisi Sabwoya

Anapendekeza nchi hizo mbili kuongeza nafasi za ufadhili wa masomo katika ngazi za Shahada, Uzamili na Uzamivu, hususan katika fani zenye uhitaji mkubwa nchini, pamoja na kuimarisha tafiti za pamoja kati ya vyuo vikuu katika maeneo ya madini, nishati, kilimo, tiba, mazingira na teknolojia.

Aidha, anasisitiza umuhimu wa kubadilishana wahadhiri na watafiti ili kujenga mazingira ya kubadilishana maarifa, uzoefu na kufanya tafiti za pamoja. Anataja pia lugha kuwa daraja muhimu la mawasiliano na ushirikiano, akipendekeza kuhamasishwa kwa ufundishaji wa lugha ya Kirusi nchini Tanzania na Kiswahili nchini Urusi ili kurahisisha mawasiliano katika biashara na shughuli za kitaaluma. Sambamba na hilo, anasema programu za elimu zinapaswa kuzingatia mahitaji ya soko la ajira na kuandaa wataalamu wenye uwezo wa kuchangia katika uchumi na kutatua changamoto za maendeleo.

Akizungumzia nafasi ya Shirikisho la Wanafunzi wa Tanzania nchini Urusi, Sabwoya anasema lina wajibu wa kuwaunganisha wanafunzi, kuwasaidia kupata taarifa sahihi, kuhamasisha nidhamu ya kitaaluma na kujenga mahusiano kati yao na taasisi mbalimbali. Pia anasisitiza umuhimu wa kuwaandaa wanafunzi kimasomo na kimaadili ili watumie maarifa wanayoyapata kwa manufaa ya taifa.

𝐃𝐈𝐀𝐒𝐏𝐎𝐑𝐀: 𝐃𝐀𝐑𝐀𝐉𝐀 𝐋𝐀 𝐊𝐔𝐈𝐌𝐀𝐑𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐇𝐔𝐒𝐈𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐍𝐀 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈

Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Urusi ina nafasi muhimu katika kuimarisha uhusiano wa mataifa hayo mawili kupitia diplomasia ya wananchi, inayowezesha watu, wafanyabiashara, wanafunzi na wataalamu kushiriki katika kujenga mahusiano ya kimataifa.

Mhandisi Mashauri Jofrey Sabwoya anasema katika diplomasia ya kisasa, jukumu la kuimarisha ushirikiano wa nchi haliwezi kubaki mikononi mwa Serikali pekee, bali linahitaji pia mchango wa jumuiya za diaspora.

Anasema Watanzania wanaoishi Urusi wana nafasi ya kipekee kwa kuwa wanaelewa mazingira ya Tanzania na wakati huo huo wanafahamu mazingira ya kijamii, kiutamaduni, kielimu na kibiashara ya Urusi, hali inayowawezesha kuwa daraja la kuunganisha fursa za mataifa hayo. Kwa mujibu wake, jumuiya hiyo inaweza kutumia nafasi yake kuanzisha mtandao wa wafanyabiashara wa Tanzania na Urusi kwa ajili ya kubadilishana taarifa za bidhaa, huduma, masoko na fursa za uwekezaji, pamoja na kuitangaza Tanzania kupitia mitandao ya kijamii, maonesho na mikutano ya kitamaduni.

Mhandisi Mashauri Jofrey Sabwoya akiwa katika picha na Fredrick Ibrahim Kibuta, Balozi wa Tanzania Shirikisho la Urusi, wakati wa uwakilishi wa wanafunzi wa Kitanzania nchini Urusi.

Aidha, anapendekeza kuimarishwa kwa mahusiano ya kijamii na kitamaduni kupitia matukio yanayotangaza Kiswahili, muziki, vyakula na urithi wa Tanzania, sambamba na kujenga mtandao wa wanafunzi na wataalamu utakaowezesha kubadilishana maarifa na uzoefu. Anasema juhudi hizo zinapaswa kuambatana na ushirikiano wa karibu kati ya jumuiya hiyo, Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, taasisi za biashara, vyuo vikuu na wadau wengine, pamoja na kuanzisha mfumo wa kukusanya na kusambaza taarifa za ufadhili wa masomo, biashara, uwekezaji, mafunzo na masoko kwa Watanzania.

“Jumuiya ya diaspora isiishie kuwa jumuiya ya kukutana katika shughuli za kijamii pekee, inapaswa pia kuwa mtandao wa maarifa, fursa, uwekezaji na mchango wa maendeleo ya taifa,” anasema Sabwoya, akisisitiza umuhimu wa kila Mtanzania anayeishi Urusi kushiriki kuitangaza Tanzania, kuunganisha fursa na kujenga urafiki kati ya wananchi wa mataifa hayo mawili,” anasema.

𝐌𝐀𝐊𝐔𝐁𝐀𝐋𝐈𝐀𝐍𝐎 𝐍𝐀 𝐅𝐔𝐑𝐒𝐀 𝐙𝐈𝐓𝐀𝐕𝐘𝐎𝐆𝐄𝐔𝐊𝐀 𝐌𝐀𝐓𝐎𝐊𝐄𝐎 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈

Anasema hatua inayofuata baada ya ziara hizo ni kuhakikisha kwamba mazungumzo na makubaliano yanageuzwa kuwa mipango madhubuti ya utekelezaji. Anasema kuna hatua saba muhimu zinazopaswa kuchukuliwa.
Kwanza, kuweka mfumo wa utekelezaji wa makubaliano. Kila makubaliano yanayofikiwa kati ya Tanzania na Urusi yanapaswa kuwa na mpango wa utekelezaji, taasisi zinazowajibika, muda wa utekelezaji na matokeo yanayotarajiwa.

“Hatupaswi kuridhika na kusainiwa kwa mikataba pekee; tunapaswa kufuatilia utekelezaji wake na kupima manufaa yake.
Pili, Kuimarisha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano wa Tanzania na Urusi. Tume hii inapaswa kuwa na jukumu muhimu la kufuatilia utekelezaji wa miradi, kutambua changamoto za kibiashara na kiutawala na kuibua maeneo mapya ya ushirikiano,” anasema.

Tatu, anasema kuongeza ushiriki wa sekta binafsi. Serikali ziweke mazingira mazuri kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa nchi zote mbili kushirikiana.

“Hii ni pamoja na kuboresha upatikanaji wa taarifa za uwekezaji, mifumo ya malipo, usafirishaji na taratibu za kibiashara,”

Pia anataja kipaumbele katika miradi yenye manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi. Tuwe na miradi inayogusa maisha ya watu, kama vile:
* Viwanda vya mbolea na pembejeo za kilimo.
* Teknolojia za kuongeza uzalishaji na usalama wa chakula.
* Viwanda vya kuongeza thamani ya madini.
* Miradi ya nishati na umeme.
* Mafunzo ya kitaalamu kwa vijana.
* Ushirikiano wa kisayansi na kiteknolojia.

“Tano, Kuimarisha ushirikiano wa elimu na ajira. Nafasi za ufadhili wa masomo ziendane na mahitaji ya taifa. Pia, tuweke mifumo ya kuwasaidia wahitimu kutumia utaalamu wao katika taasisi na sekta mbalimbali nchini Tanzania,”

Sita, Kutumia diaspora kama rasilimali ya maendeleo. Watanzania wanaoishi Urusi wanapaswa kushirikishwa katika kutafuta fursa za biashara, uwekezaji, elimu, teknolojia na utalii.

Anasema wanapaswa kujenga mfumo unaowaunganisha Watanzania walioko nje ya nchi na taasisi za Serikali pamoja na sekta binafsi ili maarifa na mitandao waliyonayo iweze kuwa na manufaa kwa taifa.

Jambo jingine ni kuweka mfumo wa uwajibikaji na tathmini ya matokeo. Ni muhimu kuwepo kwa tathmini ya mara kwa mara inayopima idadi ya miradi iliyoanzishwa, uwekezaji ulioingia, ajira zilizozalishwa, wanafunzi walionufaika na ongezeko la biashara kati ya nchi hizi mbili. Kwa kufanya hivyo, wananchi wataweza kuona thamani halisi ya diplomasia.

“Ningependa kusisitiza kwamba ziara ya Mheshimiwa Rais na ushiriki wa Mheshimiwa Waziri Mkuu katika Mkutano wa Afrika na Urusi ni fursa muhimu kwa taifa letu. Sasa ni wakati wa kuendeleza mazungumzo hayo na kuyabadilisha kuwa utekelezaji wenye manufaa kwa pande zote.
Tunahitaji kutoka kwenye diplomasia ya mikutano kwenda kwenye diplomasia ya matokeo; kutoka kwenye makubaliano kwenda kwenye miradi; na kutoka kwenye fursa kwenda kwenye manufaa halisi kwa wananchi,” anamaliza kiongozi huyo.

Makala hii imeandaliwa kwa ushirikiano na Mhandisi Mashauri Jofrey Sabwoya, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Diaspora nchini Urusi na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Tanzania nchini humo.

Mawasiliano: sabwoyajofrey@gmail.com
+255626724744

Kaka wa Tundu Lissu afariki dunia – HabariLeo

ARUSHA; Wakili Alute Lissu ambaye ni kaka wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amefariki dunia.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali mkoani Arusha zinaeleza kuwa, Wakili Alute alifariki usiku wa kuamkia leo mkoani humo.

Vyombo mbalimbali vya habari vimemkariri Rose Masesa ambaye ni dada wa marehemu akithibitisha kufariki kwa ndugu yake na kueleza msiba upo nyumbani kwa marehemu jijini Arusha.

RATIBA YA MAZISHI YA KAKA WA TUNDU LISSU YASOGEZWA MBELE KUSUBIRI HUKUMU YA TUNDU LISSU

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA, ARUSHA

Familia ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, imetangaza kifo cha kaka yao, Wakili Alute Lissu Mughwai, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Jumapili, Novemba 1, 2026, katika Hospitali ya Selian mkoani Arusha.

Akizungumza kwa niaba ya familia, Dkt. Vincent Mughwai amesema marehemu alikuwa akiugua kwa muda mrefu na katika siku za karibuni alikuwa amelazwa hospitalini hapo, kabla ya hali yake kuzorota na kufariki dunia majira ya saa nane usiku.

Amesema familia imepokea msiba huo kwa huzuni kubwa, hasa kutokana na nafasi aliyokuwa nayo Alute kama msemaji wa familia na mmoja wa viongozi wakuu wa ukoo.

Aidha, Dkt. Vincent amesema familia inatarajia kufanya mazishi mkoani Singida, lakini tarehe rasmi itatangazwa baada ya familia kukutana na kukamilisha taratibu za msiba.

Ameeleza kuwa familia inapanga kusogeza mbele shughuli za mazishi ili kuwawezesha ndugu kushiriki katika usomaji wa hukumu ya kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu, unaotarajiwa kufanyika Ijumaa, Novemba 6, 2026, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa maelezo yake, familia inatarajia kutoa taarifa zaidi kuhusu ratiba na taratibu za mazishi baada ya kufanya mashauriano.

Marehemu Alute Lissu Mughwai alikuwa wakili wa muda mrefu na amewahi kuwa msemaji wa familia ya Tundu Lissu katika masuala mbalimbali.

MATUKIO DAIMA MEDIA — HABARI WAKATI WOTE.

ALUTE MUGHWAI, KAKA WA MWENYEKITI WA CHADEMA TUNDU LISSU, AFARIKI DUNIA

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA

Wakili Alute Mughwai, ambaye ni kaka wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Novemba 1, 2026.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na dada yake, aitwaye Rose Masesa.

Hata hivyo, chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana, huku taarifa zikieleza kuwa alikuwa jijini Arusha.

MATUKIO DAIMA MEDIA – HABARI WAKATI WOTE