TBS YAONYESHA BIDHAA ZISIZOKIDHI VIWANGO MAONYESHO YA WIKI YA MWANAKATAVI

 Na Mwandishi Wetu.

KATAVI: Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kuimarisha juhudi za kuwajengea wananchi uelewa kuhusu ubora na usalama wa bidhaa zinazotumika katika maisha ya kila siku, kwa kuonesha bidhaa zisizokidhi viwango katika Maonesho ya Wiki ya Mwanakatavi yanayofanyika mkoani Katavi.

Kupitia maonesho hayo, TBS imeonesha baadhi ya bidhaa ambazo hazikidhi viwango vinavyotakiwa, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuwawezesha wananchi kuzitambua, kuepuka matumizi yake na kufanya maamuzi sahihi wanaponunua bidhaa sokoni.

Hatua hiyo inalenga kuongeza uelewa wa umma kuhusu umuhimu wa kuzingatia ubora wa bidhaa, sambamba na kuwajengea wananchi utamaduni wa kuwa makini katika ununuzi na matumizi ya bidhaa mbalimbali zinazopatikana katika soko.

Akizungumza kuhusu juhudi hizo, Meneja wa TBS Kanda ya Magharibi, Bw. Hamisi Seleleko, amesema kuwa shirika hilo linaendelea kutekeleza majukumu yake ya kusimamia viwango vya bidhaa kwa kufanya ukaguzi na doria katika maeneo mbalimbali ya Kanda ya Magharibi ili kudhibiti usambazaji na uuzaji wa bidhaa zisizokidhi viwango.

Amesema ukaguzi huo ni sehemu ya jitihada za kuhakikisha bidhaa zinazowafikia walaji zinazingatia matakwa ya viwango vinavyotakiwa, huku hatua za kutoa elimu kwa umma zikiendelea kuwa muhimu katika kuimarisha ulinzi wa mlaji.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TBS, kuendelea kwa doria hizo kumechangia kupungua kwa bidhaa zisizokidhi viwango katika maeneo yanayosimamiwa na shirika hilo, hali inayoonesha umuhimu wa kuendeleza usimamizi wa soko pamoja na ushirikiano kati ya mamlaka husika, wafanyabiashara na wananchi.

Aidha, wananchi wametakiwa kuwa makini wanaponunua bidhaa kwa kuhakikisha wanachunguza taarifa muhimu zilizowekwa kwenye vifungashio, hali ya bidhaa na alama za viwango pale inapohusika, badala ya kufanya maamuzi ya ununuzi kwa kuzingatia bei pekee.

Wananchi pia wanahimizwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika wanapobaini bidhaa zinazotia shaka kuhusu ubora wake, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.

Ushiriki wa TBS katika Maonesho ya Wiki ya Mwanakatavi unaendelea kuwa fursa ya kuifikisha huduma ya elimu kwa wananchi moja kwa moja, kwa kuwawezesha kujifunza kuhusu viwango, kutambua bidhaa zisizokidhi matakwa ya ubora na kuelewa wajibu wao katika kulinda afya, usalama na maslahi yao kama walaji.

Kupitia maonesho hayo, TBS imewajengea wananchi uelewa wa kutambua na kuepuka matumizi ya vipodozi visivyo salama, huku ikiwataka kuwa makini wanaponunua bidhaa mbalimbali.

Aidha, TBS imetoa elimu kwa wajasiriamali wadogo kuhusu umuhimu wa kupata alama ya ubora ya TBS kwa bidhaa wanazozalisha na kuuza, ikieleza kuwa alama hiyo huongeza imani ya walaji na kufungua fursa za masoko ndani na nje ya nchi.

Meneja wa TBS Kanda ya Magharibi, Bw. Hamisi Seleleko, amesema shirika hilo linaendelea kufanya ukaguzi na doria katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uuzaji na usambazaji wa bidhaa zisizokidhi viwango.

TBS inaendelea kuwataka wananchi kuzingatia ubora na usalama wa bidhaa wanazonunua, huku wajasiriamali wakihimizwa kuzingatia viwango ili kuongeza ushindani wa bidhaa zao katika soko.

Harusi ya Kijana Yatima Yashangaza Wengi! Maelfu Wahudhuria Kutoka Mtandaoni

Kijana mwenye umri wa miaka 24 nchini China amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya maelfu ya watu asiowafahamu kujitokeza kuhudhuria harusi yake Oktoba 31, 2026 kufuatia mwaliko alioutoa kupitia mitandao ya kijamii.

Xiao Xiao Xu, mkazi wa Zhaotong, Mkoa wa Yunnan, nchini China, aliamua kuwaalika watu asiowafahamu kwenye harusi yake baada ya kuwa na hofu kuwa sherehe hiyo isingekuwa na wageni wa kutosha kutokana na kukosa ndugu wengi wa karibu.

Xiao alipoteza baba yake akiwa na umri wa miaka mitatu, huku mama yake akiolewa tena miaka miwili baadaye. Alipofikisha umri wa miaka saba, pia alimpoteza bibi yake, hali iliyomfanya kukulia katika mazingira magumu akitegemea zaidi msaada wa kaka yake mkubwa.

Kutokana na changamoto za maisha, aliacha shule akiwa bado katika elimu ya sekondari ya chini na kuanza kufanya kazi mbalimbali ikiwemo ujenzi na udereva wa usafirishaji. Katika kipindi cha miaka kadhaa, alifanikiwa kuweka akiba ya Yuan 160,000 za China kwa ajili ya kugharamia harusi yake na msichana anayempenda, Chuichui.

Hata hivyo, kadiri siku ya harusi ilivyokuwa ikikaribia, alianza kuwa na wasiwasi kuhusu idadi ya wageni watakaohudhuria, akihofia kuwa ndugu zake wasingetosha kujaza hata meza tatu za wageni.

Kutokana na hali hiyo, Xiao aliamua kutumia mitandao ya kijamii kutoa mwaliko wa kipekee kwa watu mbalimbali, akiwaomba wajitokeze nyumbani kwake kusherehekea siku yake ya ndoa.

Kwa mshangao wake, mwaliko huo ulisambaa kwa kasi na kuwafikia maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali, huku wakazi wa kijiji chake pamoja na watu asiowafahamu wakijitokeza kwa wingi kuunga mkono harusi hiyo.


Msaada uliotolewa haukuishia kwenye kuhudhuria pekee, kwani baadhi ya watu walijitolea kupika chakula cha wageni, wengine wakaleta vyakula na mahitaji mbalimbali yaliyohitajika kufanikisha sherehe hiyo.

Aidha, watu mbalimbali walijitolea magari ya harusi, huku mmoja wao akitoa gari aina ya Maybach kwa ajili ya maharusi.

Wengine walishiriki kupamba nyumba na kuandaa mazingira ya sherehe, ikiwemo kutoa mishumaa ya harusi.

Watu wema bado wanaishi 🎉

Kichapo cha Chelsea Chazua Hasira Man United, Viongozi Washambuliwa

Mashabiki wa klabu ya Manchester United wameonyesha hasira zao kwa mmiliki mwenza wa klabu hiyo, Sir Jim Ratcliffe, pamoja na viongozi wengine wa juu wa timu hiyo, kufuatia kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Stamford Bridge.

Mashabiki hao walioisindikiza timu yao jijini London hawakuficha hasira zao, huku wakisikika wakiimba nyimbo za kumkashifu Ratcliffe kwa lugha chafu, wakimlinganisha na familia ya Glazer ambayo imekuwa ikikosolewa kwa muda mrefu na mashabiki wa United.

Katika nyimbo hizo, mashabiki walionyesha wazi kuwa hawamtambui Ratcliffe kama kiongozi tofauti na wamiliki waliomtangulia, wakieleza kutoridhishwa na mwenendo wa klabu hiyo chini ya uongozi wake.

Mkurugenzi wa masuala ya soka wa Manchester United, Jason Wilcox, naye alikuwa miongoni mwa viongozi waliolengwa na mashabiki hao, akitajwa kwa majina mbalimbali ya kumkosoa kutokana na hali ya timu hiyo. Afisa Mtendaji Mkuu, Omar Berrada, pia alikuwa miongoni mwa viongozi waliokosolewa.

Hasira hizo zimeongezeka baada ya Manchester United kuendelea kukabiliwa na matokeo yasiyoridhisha, huku mashabiki wakionekana kupoteza uvumilivu dhidi ya uongozi wa klabu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya mchezo huo, kocha Michael Carrick naye amekuwa chini ya shinikizo kubwa, huku mustakabali wake ukiendelea kuzungumziwa baada ya timu hiyo kushindwa kupata matokeo yaliyotarajiwa.

Kipigo cha Chelsea kimeongeza presha kwa United, ambayo sasa inakabiliwa na maswali kuhusu mwelekeo wa timu, usajili wa wachezaji na maamuzi ya viongozi wanaosimamia klabu hiyo.

Katika mchezo huo, Chelsea ilionekana kuwa bora kwa takwimu kadhaa, ikimiliki mpira kwa asilimia 58 dhidi ya 42 za Manchester United, huku pia ikipiga mashuti 19 dhidi ya 12 ya wapinzani wao.

Kwa mashabiki wa Manchester United, tatizo halionekani kuwa matokeo ya uwanjani pekee, bali pia ni kutoridhishwa na namna klabu inavyoendeshwa, hali inayozidi kuongeza mvutano kati yao na viongozi wa juu wa timu hiyo.

Netanyahu Atingishwa, Tel Aviv Yalipuka kwa Maandamano, Shinikizo la Kumuondoa Laongezeka

Global Publishers
November 1, 2026
30 views
0 Comments

Maelfu ya wananchi wameandamana katika jiji la Tel Aviv nchini Israel, wakimtaka kiongozi wa upinzani, Gadi Eisenkot, kuingia makubaliano ya kisiasa na vyama vingine ili kuunda serikali mpya na kumng’oa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu madarakani.

Maandamano hayo yanafanyika kufuatia matokeo ya uchaguzi yaliyoonyesha kuwa kambi inayomuunga mkono Netanyahu imepata viti 53, huku kambi ya Eisenkot ikipata viti 48 katika bunge la Israel.

Kwa upande mwingine, vyama vinavyowakilisha raia wa Kipalestina nchini Israel vimepata jumla ya viti 19, idadi inayovifanya kuwa na nafasi muhimu katika maamuzi ya kuunda serikali ijayo.

Kwa mujibu wa mgawanyo huo, kambi yoyote kati ya hizo mbili haina viti vya kutosha kuunda serikali peke yake, kwani inahitaji angalau viti 61 kati ya 120 vya bunge la Israel.

Hali hiyo imeongeza shinikizo kwa Eisenkot kutafuta ushirikiano na vyama vya Kiarabu ili kuunganisha nguvu na kupata wingi wa viti vinavyohitajika kuunda serikali.

Iwapo vyama hivyo vitakubaliana kushirikiana, vinaweza kupata jumla ya viti 67, hatua inayoweza kuzuia Netanyahu kuendelea kushikilia madaraka.

Maandamano hayo yanaashiria kuongezeka kwa shinikizo la kisiasa nchini Israel, huku mustakabali wa serikali ijayo ukitegemea uwezo wa wapinzani wa Netanyahu kufikia makubaliano ya pamoja.

Serikali Ya Netanyahu Yatingishwa, Vyama vya Kiarabu Kumng’oa Madarakani

Global Publishers
November 1, 2026
6 views
0 Comments

Maelfu ya wananchi wameandamana katika jiji la Tel Aviv nchini Israel, wakimtaka kiongozi wa upinzani, Gadi Eisenkot, kuingia makubaliano ya kisiasa na vyama vingine ili kuunda serikali mpya na kumng’oa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu madarakani.

Maandamano hayo yanafanyika kufuatia matokeo ya uchaguzi yaliyoonyesha kuwa kambi inayomuunga mkono Netanyahu imepata viti 53, huku kambi ya Eisenkot ikipata viti 48 katika bunge la Israel.

Kwa upande mwingine, vyama vinavyowakilisha raia wa Kipalestina nchini Israel vimepata jumla ya viti 19, idadi inayovifanya kuwa na nafasi muhimu katika maamuzi ya kuunda serikali ijayo.

Kwa mujibu wa mgawanyo huo, kambi yoyote kati ya hizo mbili haina viti vya kutosha kuunda serikali peke yake, kwani inahitaji angalau viti 61 kati ya 120 vya bunge la Israel.

Hali hiyo imeongeza shinikizo kwa Eisenkot kutafuta ushirikiano na vyama vya Kiarabu ili kuunganisha nguvu na kupata wingi wa viti vinavyohitajika kuunda serikali.

Iwapo vyama hivyo vitakubaliana kushirikiana, vinaweza kupata jumla ya viti 67, hatua inayoweza kuzuia Netanyahu kuendelea kushikilia madaraka.

Maandamano hayo yanaashiria kuongezeka kwa shinikizo la kisiasa nchini Israel, huku mustakabali wa serikali ijayo ukitegemea uwezo wa wapinzani wa Netanyahu kufikia makubaliano ya pamoja.

Fahamu Kwanini Hoteli Kubwa Hupandisha Bendera za Mataifa Mbalimbali?

Huenda umewahi kutembelea hoteli mbalimbali na kukutana na bendera zenye rangi tofauti zikiwa zimepeperushwa kwenye nguzo zilizopo mbele ya hoteli hizo. Hata hivyo, si watu wengi wanaofahamu maana ya bendera hizo, sababu za hoteli kuzipeperusha na vigezo vinavyotumika kuruhusu hoteli kutumia alama hizo.

Kwa kawaida, bendera zinazowekwa katika maeneo ya hoteli zinaweza kuwa na maana tofauti kulingana na aina yake na matumizi yaliyokusudiwa. Baadhi hutumika kuonyesha utambulisho wa hoteli, nchi ambazo wageni wake wanatoka au kuashiria shughuli maalumu zinazofanyika katika eneo hilo.

Aidha, baadhi ya hoteli hupeperusha bendera za mataifa mbalimbali kama ishara ya ukarimu wa kimataifa, hasa wakati wa kupokea wageni kutoka nchi hizo, mikutano ya kimataifa au ziara za viongozi mbalimbali.

Hata hivyo, ni muhimu kutofautisha bendera za mapambo na utambulisho na alama rasmi za uainishaji wa hoteli. Upeperushaji wa bendera hauimaanishi moja kwa moja kuwa hoteli husika ina hadhi ya nyota tano au imekidhi viwango vyote vya ubora vinavyotakiwa.

Nchini Tanzania, hoteli za kitalii hupitia utaratibu wa usajili, ukaguzi na uainishaji unaozingatia vigezo mbalimbali vinavyohusiana na ubora wa huduma na miundombinu. Uainishaji huo hutumia mfumo wa nyota kuanzia nyota moja hadi tano.

SIFA ZA HOTELI KUPEWA NYOTA MOJA HADI TANO

NYOTA MOJA (ONE STAR)

Hii ni hoteli inayokidhi mahitaji ya msingi ya malazi. Inapaswa kuwa na vyumba vinavyokidhi viwango vya chini vya ubora, vitanda vinavyofaa, mazingira safi, huduma za msingi za wageni na kuhakikisha usalama wao. Pamoja na huduma kuwa za kawaida, usafi na ubora wa msingi havipaswi kuathiriwa.

NYOTA MBILI (TWO STARS)

Hoteli ya nyota mbili inatakiwa kuwa na huduma zilizoimarika zaidi ya zile za nyota moja. Inapaswa kuwa na vyumba vyenye vifaa vinavyofaa, samani zenye ubora wa kuridhisha, mazingira mazuri, huduma za ziada zinazopatikana kulingana na mahitaji ya wageni na kiwango kizuri cha usafi.

NYOTA TATU (THREE STARS)

Hoteli ya nyota tatu inapaswa kuwa na huduma za kiwango cha kati kwenda juu, ikiwemo vyumba vyenye ubora mzuri, samani za kisasa, huduma za chakula na vinywaji, mapokezi yenye ufanisi na wafanyakazi wenye ujuzi wa kuhudumia wageni. Pia, inatarajiwa kuwa na miundombinu inayokidhi mahitaji mbalimbali ya wateja.

NYOTA NNE (FOUR STARS)

Hizi ni hoteli zinazotakiwa kutoa huduma za kiwango cha juu. Zinapaswa kuwa na vyumba vyenye ubora wa hali ya juu, samani na vifaa vya kisasa, migahawa yenye huduma bora, maeneo ya mapumziko, huduma za ziada na wafanyakazi wenye weledi wa hali ya juu.

Pia, ubunifu wa majengo, mandhari, usafi, usalama na namna wageni wanavyohudumiwa vinapaswa kuonyesha kiwango cha juu cha ubora.

NYOTA TANO (FIVE STARS)

Hii ni hoteli inayotakiwa kuonyesha ubora wa hali ya juu katika maeneo yote ya utoaji huduma. Inapaswa kuwa na vyumba vya kifahari, vifaa vya kisasa, migahawa yenye huduma za kiwango cha juu, huduma binafsi kwa wageni kulingana na mahitaji yao, miundombinu bora na wafanyakazi wenye weledi wa hali ya juu.

Hoteli za daraja hili zinatarajiwa kuwa na huduma nyingi na zinazoweza kukidhi mahitaji tofauti ya wageni, pamoja na kuzingatia kwa umakini kila kipengele cha huduma na mazingira.

MAMBO MENGINE YANAYOPIMWA KABLA YA HOTELI KUPEWA NYOTA

Mbali na ubora wa vyumba na huduma, kuna mambo mengine yanayozingatiwa wakati wa kufanya tathmini ya hoteli. Miongoni mwa mambo hayo ni:

  1. Usafi: Hali ya usafi wa vyumba, mabafu, migahawa, majiko na maeneo yote ya hoteli.
  2. Usalama: Uwepo wa mifumo ya ulinzi, vifaa vya kuzima moto, njia za dharura na taratibu za kulinda wageni.
  3. Miundombinu: Ubora wa majengo, mifumo ya maji, umeme, hewa na vifaa vingine muhimu.
  4. Huduma kwa wateja: Uwezo wa wafanyakazi kupokea, kuhudumia na kutatua changamoto za wageni kwa weledi.
  5. Chakula na vinywaji: Ubora wa huduma za migahawa, maandalizi ya chakula, usafi wa jikoni na namna wageni wanavyohudumiwa.
  6. Wafanyakazi: Ujuzi, mafunzo, muonekano na weledi wa wafanyakazi katika maeneo mbalimbali ya hoteli.
  7. Mazingira na mandhari: Muonekano wa hoteli, mpangilio wa maeneo yake, utunzaji wa mazingira na hali ya kuvutia kwa wageni.
  8. Huduma za ziada: Uwepo wa huduma kama bwawa la kuogelea, ukumbi wa mikutano, mazoezi, spa na huduma nyingine kulingana na daraja la hoteli.

NANI HUTOA NYOTA KWA HOTELI?

Nchini Tanzania, uainishaji wa hoteli za kitalii hufanyika kupitia mamlaka za serikali zinazohusika na usimamizi wa sekta ya utalii, kwa kuzingatia viwango vya kitaifa na vya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Mchakato huo unahusisha ukaguzi wa hoteli kwa kutumia vigezo vilivyowekwa, kutathmini ubora wa miundombinu na huduma zinazotolewa kabla ya kupewa daraja linalostahili.

Hivyo, hoteli haiwezi kujipa yenyewe hadhi ya nyota tano bila kupitia utaratibu rasmi wa tathmini na uainishaji.

JE, HOTELI YENYE NYOTA TANO LAZIMA IPEPERUSHE BENDERA?

Jibu ni hapana. Kupeperusha bendera si kigezo kinachothibitisha hoteli kuwa na nyota tano. Bendera zinaweza kutumika kwa ajili ya utambulisho, mapambo, kuonyesha mataifa ya wageni au shughuli maalumu.

Kwa hiyo, unapokutana na hoteli yenye bendera nyingi mbele yake, usihitimishe moja kwa moja kuwa ina hadhi ya juu kuliko hoteli nyingine. Kinachothibitisha daraja lake ni cheti au utambuzi rasmi wa uainishaji unaotolewa baada ya ukaguzi.

Kwa ujumla, mfumo wa utoaji nyota unalenga kuhakikisha hoteli zinatoa huduma zinazokidhi viwango vya ubora, usalama na matarajio ya wageni, huku ukisaidia kukuza ushindani na sekta ya utalii nchini.

Mielekeo 7 ya Teknolojia Itakayobadilisha Dunia Mwaka 2027

Mielekeo 7 ya Teknolojia Itakayobadilisha Dunia Mwaka 2027 – TeknoKona Teknolojia Tanzania

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_1-bc9efc15c341-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-js-js-front-end-breeze-prefetch-links.min-81119a57b31d-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-js-jquery-jquery.min-6836d82c2675-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-js-jquery-jquery-migrate.min-2346c86992b8-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-weglot-dist-front-js-9226ba194f92-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_2-a785a75a34a1-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_3-323462673fc7-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_4-6add049d5794-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-youtube-embed-plus-scripts-ytprefs.min-41b8ef8d5516-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_5-dc5440dbebd1-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_6-d510bf7efb2d-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_7-2f6ca4f1f852-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_8-89743c229303-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_9-f4af2ae5dc4a-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_10-e9d1e2357471-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_11-e4923f14768c-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_12-2e1d956dbb67-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_13-92a0d29ebd3b-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_14-b6e2dd7ea1fa-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_15-3419b0a9d48d-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-assets-js-fluent-forms-elementor-widget-fb18c7abb132-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-js-dist-hooks.min-1e6013aecb3f-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-js-dist-i18n.min-8a672a7b3338-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_16-94c4eed60653-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-swv-js-index-8d0927242d72-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_17-32e62a28f1ce-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-includes-js-index-e8b7e8c92e4e-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-assets-js-SmoothScroll.min-132b02aee8b7-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-wp-includes-js-comment-reply.min-5e27e6025459-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_18-a2aa12e87f3f-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-assets-js-main-a7415881660e-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-assets-js-webpack.runtime.min-bb61ccabd4bc-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-assets-js-frontend-modules.min-1c2486988462-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_19-592979563c5d-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-jquery-ui-core.min-bbe779825618-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_20-6b83ebba7c99-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-assets-js-frontend.min-562b3159aee7-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-js-js-front-end-breeze-lazy-load.min-ce1a9bcfcae0-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_21-1c580bd2ffb2-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_22-2d4471d05cd5-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-wp-content-copy-protector-js-activity-tracker-9e0626ce27a9-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-youtube-embed-plus-scripts-fitvids.min-a18894311799-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_23-04c99766675b-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-dist-js-public.min-3e807f9c1e46-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-akismet-_inc-akismet-frontend-632bfb5d2300-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_24-5ed549545e8d-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-ank-simplified-ga-assets-front-end.min-888431ccbdc3-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853

https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/cache/breeze-minification/js/breeze_mielekeo-teknolojia-mwaka-2027-1-49035-inline_script_25-7da672e85abf-cv1fe5108f103784f0.js?ver=1793503853