Benfica Kuendeleza Ubabe Wake Dhidi ya Alverca Usiku wa Leo

Ligi Kuu ya Ureno, Primeira Liga, itaendelea Jumatatu, Novemba 2, 2026, kwa mchezo kati ya Benfica na Alverca utakaopigwa saa 23:15 usiku, katika dimba la Estádio da Luz jijini Lisbon. Benfica watakuwa wenyeji wa mchezo huo wakiwa na lengo la kuendeleza matokeo mazuri na kuongeza pointi muhimu katika mbio za kuwania nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi.

Benfica wanaingia katika mchezo huo wakiwa na rekodi nzuri ya hivi karibuni, baada ya kuichapa Santa Clara mabao 2-1 katika mchezo wao uliopita wa ligi. Kikosi hicho kina uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga, huku mshambuliaji Vangelis Pavlidis akiwa miongoni mwa wachezaji muhimu katika safu ya ushambuliaji. Benfica watatarajia kutumia faida ya uwanja wao ili kuanza mchezo kwa nguvu na kupata mabao mapema.

Kwa upande wa Alverca, timu hiyo inakabiliwa na changamoto ya kucheza ugenini dhidi ya mpinzani mwenye uzoefu mkubwa katika mashindano ya Ureno. Katika mchezo wao uliopita wa ligi, Alverca walipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Arouca, hivyo watakuwa na jukumu la kuboresha kiwango chao, hasa katika safu ya ushambuliaji. Ushirikiano wa wachezaji na umakini wa safu ya ulinzi vitakuwa muhimu ili kuzuia mashambulizi ya wenyeji.

Hiyo leo hiyoo Odds kubwa zipo kwenye mchezo huu jisajili Leo na tandika jamvi lako leo na ufurahie ushindi.

Benfica wabashikilia nafasi ya pili wakiwa na pointi 22 baada ya mechi tisa, huku Alverca wakishika nafasi ya nane kwa pointi 11. Tofauti hiyo inaonyesha umuhimu wa mchezo huu kwa pande zote mbili, kwani Benfica wanahitaji kuendelea kukusanya pointi ili kubaki kwenye ushindani wa juu, wakati Alverca wanataka kuboresha nafasi yao kwenye msimamo wa ligi.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

 

Historia ya michezo yao ya hivi karibuni pia inaipa Benfica matumaini, baada ya kushinda mechi zao mbili zilizopita za ligi dhidi ya Alverca. Hata hivyo, matokeo ya zamani hayawezi kuamua kitakachotokea uwanjani, hivyo Benfica watahitaji kuonyesha ubora wao, huku Alverca wakitafuta namna ya kuwashangaza wenyeji.

Wageni AFCON kunufaika mfumo malipo ya kidijitali – HabariLeo

DAR ES SALAAM: Wananchi na wageni watakaoingia nchini wakati wa mashindano ya AFCON watanufaika na kurahisishwa kwa huduma za mafuta, gesi na mahitaji mengine ya magari kupitia mfumo wa malipo ya kidijitali unaolenga kuongeza usalama na kurahisisha usimamizi wa matumizi.

Kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania imezindua mfumo mpya wa kadi za malipo za kidijitali utakaotumika katika vituo vyake 130 vilivyosambaa nchini, ukiwawezesha wateja kulipia huduma mbalimbali kupitia mfumo mmoja.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa kampuni hiyo, Getrude Mpangile, amesema mfumo huo umeboreshwa ili kuwawezesha wateja kulipia mafuta, gesi, huduma za kubadilisha mafuta ya injini na kuosha magari.

Amesema kupitia programu ya TotalEnergies Mobility, watumiaji wataweza kufuatilia miamala na matumizi yao kwa wakati, hatua inayolenga kuongeza uwazi na udhibiti wa matumizi.

Mfumo huo pia unaendana na juhudi za kukuza matumizi ya teknolojia katika sekta binafsi na kuboresha utoaji wa huduma, sambamba na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ya kuimarisha uchumi, kuvutia uwekezaji na kupanua fursa za biashara.

Kwa upande wao, watumiaji wa kadi hizo, Nishit Mdessa na Thabit Binzou, wamesema mfumo huo unarahisisha usimamizi wa matumizi, kuongeza usalama na kupunguza uwezekano wa matumizi ya mafuta yasiyoidhinishwa.

Wamesema mfumo huo unatarajiwa kuwa na manufaa kwa wasafiri na wadau wa utalii, hususan katika kipindi cha AFCON, ambapo idadi ya wageni na mahitaji ya huduma za usafiri yanatarajiwa kuongezeka.

Mabula Aapishwa Kuwa RC wa Tabora Ikulu ya Chamwino, Dodoma – Video

Global Publishers
November 2, 2026
72 views
0 Comments


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Novemba 2, 2026, amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nafasi mbalimbali za uongozi serikalini na katika tume mbalimbali.



Uapisho huo umefanyika katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma, ambapo miongoni mwa walioapishwa ni Angeline Lubala Mabula kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Dunford George Mpelumbe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Wengine ni Omar Ali Omar, aliyeapishwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, pamoja na Jaji Mstaafu Wilfred Peter Dyansobera, aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, sambamba na Makamishna wa Tume hiyo.

Mabula Aapishwa Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ikulu ya Chamwino – Video

Global Publishers
November 2, 2026
0 views
0 Comments


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Novemba 2, 2026, amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nafasi mbalimbali za uongozi serikalini na katika tume mbalimbali.

Uapisho huo umefanyika katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma, ambapo miongoni mwa walioapishwa ni Angeline Lubala Mabula kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Dunford George Mpelumbe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Wengine ni Omar Ali Omar, aliyeapishwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, pamoja na Jaji Mstaafu Wilfred Peter Dyansobera, aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, sambamba na Makamishna wa Tume hiyo.

Ajali ya Ndege Yauwa Watu Tisa Baada Kuanguka na Kuteketea Kwa Moto, Gavana wa Florida Afunguka

Watu tisa wamefariki dunia baada ya ndege binafsi waliyokuwa wakisafiria kuanguka katika eneo la Palm Beach, jimbo la Florida nchini Marekani, katika ajali iliyosababisha ndege hiyo kuteketea kwa moto.

Ajali hiyo imetokea Jumapili jioni, Novemba 1, 2026, katika eneo lililopo umbali wa takribani kilomita 12 kutoka makazi ya mapumziko ya Mar-a-Lago yanayomilikiwa na Rais wa Marekani, Donald Trump.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa, ndege hiyo inayodaiwa kuwa aina ya Learjet 60 ilikuwa imebeba watu tisa na ilikuwa ikisafiri kutoka jimbo la Texas kuelekea Bahamas kabla ya kuanguka.

Hadi sasa, utambulisho wa watu waliokuwa ndani ya ndege hiyo haujatangazwa rasmi na mamlaka husika.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Marekani (FAA) imesema imetuma timu ya wataalamu katika eneo la tukio kwa ajili ya kufanya uchunguzi utakaobaini chanzo cha ajali hiyo.

Picha zilizopatikana katika eneo la ajali zinaonyesha mabaki ya ndege yaliyoteketea kwa moto pamoja na shimo kubwa lililotokana na nguvu ya ndege kugonga ardhi.

Wakati huohuo, ripoti za vyombo vya habari nchini Marekani pamoja na uchambuzi wa takwimu za safari ya ndege zinaashiria kuwa ndege hiyo ilikuwa ikipoteza mwinuko kwa kasi kubwa, inayokadiriwa kufikia mamia ya futi kwa sekunde, kabla ya kuanguka.

Video ambayo bado haijathibitishwa rasmi na mamlaka, iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kuonekana kurekodiwa kupitia kamera ya gari, inaonyesha ndege hiyo ikianguka kwa ghafla.

Katika video hiyo, magari yanaonekana yakiendelea na safari katika barabara ya makazi kabla ndege hiyo haijaanguka, na muda mfupi baadaye kutokea mlipuko mkubwa ulioambatana na moto na vipande vya mabaki kurushwa hewani.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano ulioitishwa kufuatia ajali hiyo, Gavana wa Florida, Ron DeSantis, amesema video ya tukio hilo inashtua kutokana na namna ndege hiyo ilivyoanguka na kusababisha mlipuko mkubwa.

“Unapoitazama video hii, kwa kweli inashtua sana. Ni kana kwamba kombora linashuka kutoka angani, kisha kunatokea mlipuko mkubwa na vipande vya mabaki kurushwa kila upande,” amesema DeSantis.

Kwa sasa, uchunguzi wa mamlaka za anga unaendelea kubaini mazingira yaliyopelekea ajali hiyo, huku familia za wahanga zikisubiri taarifa rasmi kuhusu utambulisho wa ndugu zao.

Ajali ya Ndege Yauwa Watu Tisa Baada Kuanguka na Kuteketea Kwa Moto

Watu tisa wamefariki dunia baada ya ndege binafsi waliyokuwa wakisafiria kuanguka katika eneo la Palm Beach, jimbo la Florida nchini Marekani, katika ajali iliyosababisha ndege hiyo kuteketea kwa moto.

Ajali hiyo imetokea Jumapili jioni, Novemba 1, 2026, katika eneo lililopo umbali wa takribani kilomita 12 kutoka makazi ya mapumziko ya Mar-a-Lago yanayomilikiwa na Rais wa Marekani, Donald Trump.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa, ndege hiyo inayodaiwa kuwa aina ya Learjet 60 ilikuwa imebeba watu tisa na ilikuwa ikisafiri kutoka jimbo la Texas kuelekea Bahamas kabla ya kuanguka.

Hadi sasa, utambulisho wa watu waliokuwa ndani ya ndege hiyo haujatangazwa rasmi na mamlaka husika.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Marekani (FAA) imesema imetuma timu ya wataalamu katika eneo la tukio kwa ajili ya kufanya uchunguzi utakaobaini chanzo cha ajali hiyo.

Picha zilizopatikana katika eneo la ajali zinaonyesha mabaki ya ndege yaliyoteketea kwa moto pamoja na shimo kubwa lililotokana na nguvu ya ndege kugonga ardhi.

Wakati huohuo, ripoti za vyombo vya habari nchini Marekani pamoja na uchambuzi wa takwimu za safari ya ndege zinaashiria kuwa ndege hiyo ilikuwa ikipoteza mwinuko kwa kasi kubwa, inayokadiriwa kufikia mamia ya futi kwa sekunde, kabla ya kuanguka.

Video ambayo bado haijathibitishwa rasmi na mamlaka, iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kuonekana kurekodiwa kupitia kamera ya gari, inaonyesha ndege hiyo ikianguka kwa ghafla ikiwa imeelekeza sehemu yake ya mbele chini.

Katika video hiyo, magari yanaonekana yakiendelea na safari katika barabara ya makazi kabla ndege hiyo haijaanguka, na muda mfupi baadaye kutokea mlipuko mkubwa ulioambatana na moto na vipande vya mabaki kurushwa hewani.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano ulioitishwa kufuatia ajali hiyo, Gavana wa Florida, Ron DeSantis, amesema video ya tukio hilo inashtua kutokana na namna ndege hiyo ilivyoanguka na kusababisha mlipuko mkubwa.

“Unapoitazama video hii, kwa kweli inashtua sana. Ni kana kwamba kombora linashuka kutoka angani, kisha kunatokea mlipuko mkubwa na vipande vya mabaki kurushwa kila upande,” amesema DeSantis.

Kwa sasa, uchunguzi wa mamlaka za anga unaendelea kubaini mazingira yaliyopelekea ajali hiyo, huku familia za wahanga zikisubiri taarifa rasmi kuhusu utambulisho wa ndugu zao.

Mitambo 41 yarudishwa baada ya agizo la Kadogosa – HabariLeo

SHINYANGA: Agizo la Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa, alilolitoa Oktoba 2026 mkoani Shinyanga, limeanza kutekelezwa baada ya vifaa na mitambo ya ujenzi kuanza kurejeshwa katika maeneo ya miradi husika, hatua inayolenga kuhakikisha kazi zinaendelea kwa kasi na kukamilika kwa wakati.

Waziri Kadogosa alitoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Msalala, wilayani Kahama, ambapo alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha vifaa na mitambo inayohitajika katika utekelezaji wa miradi inapatikana na kubaki katika maeneo ya kazi ili kuepusha ucheleweshaji.

Alieleza kutoridhishwa na tabia ya baadhi ya wakandarasi kuhamisha vifaa na mitambo kutoka mradi mmoja kwenda mwingine kwa lengo la kukidhi masharti ya malipo ya awali ya maandalizi ya mradi, yanayojulikana kama ‘Mobilization’.

Kwa mujibu wa Waziri Kadogosa, tabia hiyo inaweza kusababisha miradi kutokamilika kwa wakati na kuisababishia Serikali gharama zisizo za lazima, ikiwamo kulipia tena usafirishaji wa vifaa na mitambo kutoka eneo moja kwenda jingine.

Utekelezaji wa agizo hilo umeanza pia katika mradi wa ujenzi wa barabara ya mchepuo ya Iringa (Iringa Bypass), yenye urefu wa kilomita 7.3.

Hadi Oktoba 29, 2026, mkandarasi wa mradi huo alikuwa amerejesha mitambo 41 kati ya 65 inayohitajika kwa mujibu wa mkataba, sawa na asilimia 63 ya mitambo iliyotakiwa kuwepo katika eneo la mradi.

Aidha, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ulimwita mkandarasi huyo katika kikao cha kawaida cha mradi kilichopangwa kufanyika Oktoba 30, 2026, kwa lengo la kusisitiza umuhimu wa kuendelea na utekelezaji wa kazi mara baada ya kurejesha mitambo hiyo.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha mitambo inayohitajika inabaki katika eneo la mradi na hivyo kuongeza kasi ya utekelezaji wa kazi, kuzuia ucheleweshaji na kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati kwa mujibu wa mkataba.

Arteta Aandika Historia Anfield, Arsenal Yashinda Baada Ya Miaka 14

Arsenal imeandika historia mpya katika Ligi Kuu England baada ya kuifunga Liverpool bao 1-0 kwenye dimba la Anfield, na kupata ushindi wake wa kwanza ugenini dhidi ya wapinzani hao katika kipindi cha miaka 14.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Kai Havertz katika kipindi cha kwanza, likiipa Arsenal alama tatu muhimu na kuendeleza harakati zake za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu England.

Ushindi huo ni wa kihistoria kwa kikosi cha kocha Mikel Arteta, ambaye alikuwa nahodha wa Arsenal mara ya mwisho timu hiyo ilipoifunga Liverpool ugenini kwa mabao 2-0 mwaka 2012.

Tangu wakati huo, Arsenal ilikuwa imecheza michezo 16 katika mashindano mbalimbali bila kupata ushindi kwenye uwanja wa Anfield, kabla ya kuvunja rekodi hiyo kupitia mchezo huo.

Akizungumza baada ya mchezo, Arteta amesema anajivunia ushindi huo, akieleza kuwa ulikuwa na umuhimu mkubwa kwa klabu na mashabiki wake kutokana na muda mrefu ambao timu hiyo ilikuwa haijashinda katika uwanja huo.

“Ninajivunia sana. Imepita miaka 14, huo ni muda mrefu. Nina uhakika tumewafanya wote wanaohusishwa na klabu hii kujivunia leo, si kwa ushindi pekee bali pia kwa namna tulivyoupata na ari tuliyoonyesha,” amesema Arteta.

Ushindi huo umekuja siku nne baada ya Arsenal kupata kipigo cha kushangaza kutoka kwa Fleetwood Town ya Ligi ya Daraja la Pili, katika mchezo wa Kombe la Carabao, matokeo ambayo Arteta amesema yaliwapa wachezaji wake msukumo wa kurejea kwa nguvu.

Katika mchezo dhidi ya Liverpool, Arsenal ilionyesha uimara mkubwa wa safu yake ya ulinzi, hasa baada ya kupata bao la kuongoza, huku Liverpool wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara bila kufanikiwa kupata bao.

Hata hivyo, kipindi cha pili Arsenal iliendelea kulinda lango lake kwa umakini mkubwa na kuzuia Liverpool kupata shuti lolote lililoelekezwa langoni.

Matokeo hayo yameifanya Arsenal kufikisha alama tatu zaidi ya timu inayofuatia katika msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo tisa, huku ikiwa na alama mbili zaidi ikilinganishwa na ilipokuwa katika hatua kama hiyo msimu uliopita ilipotwaa ubingwa.

Licha ya mafanikio hayo, safu ya ushambuliaji ya Arsenal bado haijafikia kiwango kinachotarajiwa, ikiwa imefunga mabao 14 pekee katika michezo tisa ya ligi.

Arteta pia amekuwa akikabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa baadhi ya wachezaji muhimu wa ushambuliaji, akiwemo Bukayo Saka aliye majeruhi, huku Max Dowman akiwa nje kutokana na adhabu ya kadi nyekundu. Viktor Gyokeres na Kai Havertz nao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kutopata kiwango bora.

Hata hivyo, uimara wa safu ya ulinzi unaonekana kuwa moja ya silaha muhimu za Arsenal katika mbio za kutetea taji lake, baada ya kuruhusu mabao 27 pekee msimu uliopita.

Arteta amesema ushindi dhidi ya Liverpool ni sehemu ya changamoto ambazo amekuwa akitamani kuzitimiza, akitaja pia ushindi dhidi ya Chelsea na Manchester United katika viwanja vyao kama sehemu ya malengo yake.

Kwa upande mwingine, Manchester City inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi, huku kukiwa na suala la rufaa yake dhidi ya tuhuma za kukiuka kanuni za kifedha za Ligi Kuu England.

Arsenal sasa inaendelea na kampeni yake ya kutetea ubingwa ikiwa na matumaini ya kuendeleza matokeo mazuri na kuongeza pengo dhidi ya wapinzani wake katika mbio za kuwania taji.

Balozi wa Marekani Afunguka Hatma ya Netanyahu Kuunda Serikali

Balozi wa Marekani nchini Israel, Mike Huckabee

Balozi wa Marekani nchini Israel, Mike Huckabee, amesema matokeo ya uchaguzi nchini Israel yaliyoonesha Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kupata uungwaji mkono mkubwa kuliko ilivyotarajiwa yamebadilisha mwelekeo wa siasa za nchi hiyo, huku hatua inayofuata ikiwa ni mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha Newsmax, Huckabee amesema kambi ya Netanyahu imepata viti 53, ikilinganishwa na viti 48 vya kambi ya kiongozi wa upinzani Eisenkot, lakini hakuna upande uliofikia viti 61 vinavyohitajika ili kupata wingi wa kuunda serikali katika Bunge la Israel lenye viti 120.

Amesema matokeo hayo yalikuwa tofauti na matarajio ya wengi waliodhani kuwa kambi ya mabadiliko ingeibuka na ushindi katika uchaguzi huo.

Huckabee ameeleza kuwa hatua inayofuata itakuwa ni Rais wa Israel kumpa Netanyahu au Eisenkot nafasi ya kwanza ya kujaribu kuunda serikali, ambapo watakuwa na siku 42 za kutafuta uungwaji mkono wa wabunge wasiopungua 61.

Amesisitiza kuwa matokeo ya uchaguzi pekee hayaamui nani atakuwa Waziri Mkuu, bali uwezo wa kiongozi kupata washirika wa kutosha kuunda serikali.

Serikali ya umoja na nafasi ya vyama vya Waarabu

Akizungumzia uwezekano wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa kati ya Netanyahu na Eisenkot, Huckabee amesema kauli zinazotolewa na wanasiasa wakati wa kampeni hazipaswi kuchukuliwa kuwa msimamo wa mwisho wakati wa mazungumzo ya kuunda serikali.

Amesema baadhi ya wanasiasa wanaweza kubadili misimamo yao wanapokabiliwa na uwezekano wa kubaki nje ya serikali kwa kipindi cha miaka minne.

Hata hivyo, kuhusu msimamo wa Netanyahu wa kutovitaka vyama vya Waarabu katika serikali yake, Huckabee ameuelezea kuwa ni muhimu, akitoa hoja kuhusu baadhi ya kauli za wanasiasa wa Kiarabu kuhusu Israel na shambulio la Hamas la Oktoba 7.

Kwa mujibu wa Huckabee, vyama vya Waarabu vilipata viti 19 katika uchaguzi huo, lakini amesema baadhi ya wanasiasa waliochaguliwa wamekuwa na misimamo inayozua maswali kuhusu ushiriki wao katika serikali.

Uchunguzi wa madai ya kuingiliwa kwa uchaguzi

Huckabee pia amezungumzia uchunguzi wa madai ya kuwepo kwa ushawishi wa fedha kutoka nje ya Israel katika uchaguzi huo, hususan katika jamii za Waarabu.

Amesema uchunguzi unaohusisha vyombo vya usalama unaendelea na kwamba madai hayo ni mazito, lakini amesisitiza kuwa bado hakuna matokeo yaliyothibitishwa hadharani.

Ameeleza kuwa kuingiliwa kwa uchaguzi kutoka nje, iwapo kutathibitishwa, kunaweza kuwa na athari kubwa katika matokeo ya uchaguzi na hali ya kisiasa nchini humo.

Huckabee azikosoa nchi za Ulaya

Katika mahojiano hayo, Huckabee pia amezikosoa baadhi ya serikali za Ulaya kwa kile alichokiita kujaribu kuingilia maamuzi ya Israel kuhusu namna ya kuendesha mambo yake ya ndani.

Amesema viongozi wa Ulaya wanapaswa kuelekeza nguvu zaidi katika kushughulikia changamoto za usalama na machafuko katika nchi zao.

Marekani na Israel kuendelea kushirikiana

Kuhusu uhusiano wa Marekani na Israel, Huckabee amesema ushirikiano wa mataifa hayo una umuhimu mkubwa katika usalama wa taifa la Marekani, hususan katika kubadilishana taarifa za kiintelijensia na kuzuia Iran kupata silaha za nyuklia.

Amesema taarifa za kiintelijensia zinazoshirikishwa kati ya nchi hizo zimekuwa zikisaidia kuokoa maisha ya Wamarekani.

Amepongeza pia msimamo wa Rais Donald Trump kuhusu Iran, akisema hatua zilizochukuliwa na Marekani ni sehemu ya kukabiliana na vitisho vya muda mrefu kutoka kwa utawala wa Tehran.

Huckabee amehitimisha kwa kusisitiza kuwa uhusiano wa Marekani na Israel una umuhimu wa kimkakati na kiusalama, licha ya mijadala ya kisiasa inayoendelea ndani ya Marekani kuhusu kiwango cha ushirikiano huo.