Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imeongoza vikao vya Kamati ya Fedha na Utawala pamoja na Kamati ya Misitu na Nyuki, vilivyolenga kupitia utekelezaji wa majukumu ya Wakala katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027, kuanzia Julai hadi Septemba 2026.
Vikao hivyo vimefanyika tarehe 15 Oktoba 2026 katika Ukumbi wa Karume, Julius Nyerere Leadership School, Manispaa ya Kibaha.
Lengo la vikao hivyo lilikuwa kutathmini utekelezaji wa majukumu ya TFS katika kulinda, kusimamia na kuhifadhi rasilimali za misitu na nyuki.
Aidha, Bodi hiyo inatarajia kufanya kikao chake maalumu cha 50 kesho, tarehe 16 Oktoba 2026, kujadili masuala mbalimbali yanayohusu utendaji, ufanisi na maendeleo ya Wakala.





