DKT. MWIGULU MGENI RASMI HARAMBEE YA MAENDELEO YA KKKT*

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo, Jumatatu Oktoba 5, 2026, ni mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia maendeleo ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, ikiwemo kuboresha vituo vya huduma na shughuli za diakonia.

Harambee hiyo inafanyika katika viwanja vya Tanga Beach Resort, jijini Tanga, kwa lengo la kuhamasisha waumini na wadau kuchangia uimarishaji wa huduma na miradi ya maendeleo ya Dayosisi hiyo.