Ushirikiano kuimarisha mapambano usafirishaji haramu wa binadamu – HabariLeo

DAR ES SALAAM: Tanzania na Misri zitaendelea kuimarisha ushirikiano katika kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu pamoja na magendo ya wahamiaji, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed Mahmoud, amesema.

Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya siku tano yanayolenga kuwajengea uwezo maofisa wanaohusika na mapambano dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu kutoka Wizara na taasisi mbalimbali.

Ayoub amesema Serikali inatambua umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na uhalifu huo unaovuka mipaka, hususan katika kubadilishana taarifa, uzoefu na mbinu za kiutendaji.

Amebainisha kuwa jumla ya maofisa, wakaguzi na askari 69 wa vyeo mbalimbali kutoka Tanzania wamepata mafunzo nchini Misri katika kipindi cha mwaka 2024 hadi 2025, hatua inayodhihirisha kuendelea kuimarika kwa ushirikiano kati ya nchi hizo katika kujenga uwezo wa watendaji.

Amesema changamoto za uhamaji wa watu pamoja na kuongezeka kwa mitandao ya uhalifu inayojihusisha na usafirishaji haramu wa binadamu zinahitaji nchi kuendelea kushirikiana