Makamu wa Rais Ndejembi Aungana na Waombolezaji Maziko ya Hafidh Ameir Hassan (Video +Picha)

Global Publishers
September 7, 2026
498 views
0 Comments


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameshiriki maziko ya Marehemu Hafidh Ameir Hassan, mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Maziko hayo yamefanyika leo, Jumatatu, Septemba 7, 2026, katika eneo la Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja.

Marehemu Hafidh Ameir Hassan amefariki dunia leo katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Zanzibar, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Maziko hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Viongozi Wakuu na Viongozi Wakuu Wastaafu, viongozi wa Serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa Mahakama na Bunge, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, pamoja na familia, ndugu, marafiki na waombolezaji kutoka ndani na nje ya nchi.

Matajiri wa Jiji Azam Fc na Namungo Kukipiga Leo Ligi Kuu ya NBC

Global Publishers
September 7, 2026
66 views
0 Comments

Klabu ya Azam FC leo Jumatatu, Septemba 7, 2026, inashuka dimbani kumenyana na Namungo FC katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya NBC, kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa 1:00 usiku, unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kuhitaji alama tatu muhimu ili kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi.

Kwenye msimamo kuelekea mtanange wa leo, timu hizi zinapishana kwa pointi na nafasi, kulingana na mwanzo wao wa msimu wa 2026/2027.

Azam FC,imecheza mechi tano,  inashika nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 11.

Azam FC inalenga kupata ushindi leo ili kuisogelea Yanga SC na Simba SC zilizopo kileleni mwa msimamo, kila moja ikiwa na pointi 15.

Namungo FC kwa upande wao, imecheza mechi tano, lakini inasuasua kwenye msimamo ikiwa na pointi tatu pekee.

Na Peter Jinanai



Dkt. Mwinyi Atoa Pole kwa Rais Samia Kufuatia Kifo cha Mumewe, Kuzikwa Leo Kizimkazi, Zanzibar

Global Publishers
September 7, 2026
852 views
0 Comments

Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mume wake, Marehemu Hafidh Ameir Hassan.

Marehemu Hafidh Ameir Hassan amefariki dunia leo, Septemba 7, 2026, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Zanzibar.

Katika salamu hizo, Rais Dkt. Mwinyi amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba huo na kuungana na Rais Dkt. Samia, familia, ndugu, jamaa pamoja na wote waliofikwa na msiba huo katika kipindi hiki cha majonzi.

Amesema kifo hicho ni pigo kubwa kwa familia na wote waliokuwa karibu na marehemu, huku akimuomba Mwenyezi Mungu amjaalie Rais Dkt. Samia pamoja na familia yake subira, nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu.

Marehemu Hafidh Ameir Hassan anatarajiwa kuzikwa leo Kizimkazi, Zanzibar, katika mazishi yatakayohudhuriwa na familia, ndugu, jamaa, viongozi mbalimbali wa kitaifa pamoja na wananchi.

Rais Dkt. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu aisamehe roho ya Marehemu Hafidh Ameir Hassan na amjaalie makazi mema Peponi.

Inna Lillahi wa Inna Ilayhi Raji’un.

Infantino Athibitisha Kugombea tena Urais wa FIFA Mwakani

Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA), Gianni Infantino, amethibitisha kuwa atagombea tena nafasi ya urais wa FIFA katika uchaguzi utakaofanyika Machi 2027, licha ya kukabiliwa na upinzani na shinikizo kutoka baadhi ya vyama vya soka duniani.

 

FIFA imethibitisha leo, Septemba 7, 2026, kwamba Infantino bado ana mpango wa kugombea muhula mwingine.

 

FIFA imesema kuwa hakuna kilichobadilika tangu Infantino alipotangaza mwezi Aprili kwamba angewania tena nafasi hiyo.

 

Infantino, mwenye umri wa miaka 56, amekuwa rais wa FIFA tangu mwaka 2016 na amewahi kuchaguliwa tena mwaka 2019 na 2023. Akishinda uchaguzi wa mwaka 2027, ataendelea kuiongoza FIFA hadi mwaka 2031 uamuzi wake wa kugombea tena unakuja wakati FIFA ikikabiliwa na mgawanyiko kuhusu uongozi wake.

 

Infantino amekosolewa baada ya mpango wa kuhusisha wawekezaji binafsi katika mashindano ya FIFA, ikiwemo Kombe la Dunia, kukataliwa na hatimaye kuachwa mpango huo uliibua upinzani kutoka kwa baadhi ya mashirikisho makubwa ya soka.

 

Miongoni mwa mashirikisho yaliyomkosoa Infantino ni UEFA, AFC na CONCACAF. Hata hivyo, bado anaungwa mkono na baadhi ya vyama vya soka, hususan barani Afrika kupitia CAF na Amerika Kusini kupitia CONMEBOL.

 

Kwa sasa, Infantino ndiye mgombea pekee aliyethibitishwa rasmi kwa uchaguzi huo, ingawa Victor Montagliani, rais wa CONCACAF, ametajwa kama mmoja wa viongozi wanaoweza kumpinga.

Wagombea wengine wana hadi Novemba 18, 2026 kuwasilisha nia zao,uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Machi 2027 mjini Rabat, Morocco, katika kongamano la FIFA.

 

Matokeo yake yanaweza kuwa na umuhimu mkubwa kwa mustakabali wa uongozi wa soka duniani kutokana na mgawanyiko uliopo ndani ya shirikisho hilo.

 

Kwa sasa, Infantino anaendelea na majukumu yake kama rais wa FIFA huku akitarajiwa kukabiliana na changamoto kubwa zaidi za kisiasa katika safari yake ya kutafuta muhula mwingine wa uongozi.

Na Ashura karimu



Jaji Warioba Aanguka Wakati Akihutubia Mkutano

Global Publishers
September 7, 2026
0 views
0 Comments

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, ameanguka ghafla wakati akizungumza katika mkutano wa kitaifa wa kutafakari hali ya kisiasa nchini Tanzania, ambapo alikuwa miongoni mwa wazungumzaji wakuu.

Tukio hilo limetokea wakati wa mkutano huo unaoandaliwa na Tanzania Centre for Democracy (TCD), na kusababisha shughuli za mkutano kusitishwa kwa muda.

Kufuatia tukio hilo, Mwenyekiti wa TCD, Dorothy Semu, ametangaza mapumziko mafupi ili kuruhusu hali kutulia na hatua zinazohitajika kuchukuliwa.

Hadi sasa, taarifa zaidi kuhusu hali ya kiafya ya Jaji Warioba baada ya kuanguka kwake hazijawekwa wazi.

Mkutano huo ulikuwa ukijadili hali ya kisiasa nchini pamoja na masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa demokrasia na siasa nchini Tanzania.

Zungusha, Kusanya, Shinda Na Pragmatic Play Drops & Wins 2026

Meridianbet imefungua ukurasa mpya wa burudani kwa wapenzi wa kasino kupitia Pragmatic Play Drops & Wins 2026, promosheni inayokupa zawadi na vizidishi vikubwa kwa mtindo unaoongeza msisimko kila unapocheza. Kama unapenda michezo ya kasino yenye nafasi ya kupata zawadi huku ukiendelea kuburudika, basi huu ni wakati wa kuingia kwenye michezo inayoshiriki na kuanza safari ya kukusanya. Kila mzunguko unakupeleka hatua moja karibu na zawadi inayokusubiri.

Sheria za mchezo huu ni rahisi na hazihitaji mambo mengi. Unachotakiwa kufanya ni kuweka dau kwenye michezo inayoshiriki, kisha kila raundi inayochezwa kwa fedha halisi itahesabiwa. Kadiri unavyoendelea kucheza, ndivyo unavyopata nafasi ya kukusanya vipande vya gurudumu. Ukifanikiwa kupata vipande vitatu vya gurudumu, unafungua mlango wa kupata zawadi, huku msisimko ukiendelea kuongezeka kila raundi inapozunguka.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kinachofanya promosheni hii kuwa ya kuvutia zaidi ni ukubwa wa zawadi zinazoweza kupatikana. Wachezaji wanaweza kukutana na vizidishi hadi x100,000 ya dau, huku mizunguko ya bure ikiwa pia miongoni mwa zawadi zinazoweza kupatikana. Hii ndiyo aina ya burudani inayofanya kila mzunguko kuwa na mvuto wake, kwa sababu huwezi kujua ni wakati gani mkusanyiko wako utakamilika na zawadi ikaingia.

Zaidi ya hapo, zawadi zinapatikana papo hapo kwenye michezo inayostahiki, na kila mchezaji anaweza kupata hadi zawadi mbili. Hivyo, ukianza safari yako leo, si lazima uridhike na zawadi moja pekee. Endelea kukusanya vipande, fuatilia maendeleo yako na uone kama bahati itakupa nafasi ya kufungua zawadi nyingine ndani ya promosheni hii inayosisimua.

Kwa hiyo, kama uko tayari kwa msisimko wa kila raundi na zawadi kubwa, Pragmatic Play Drops & Wins 2026 inakusubiri Meridianbet. Ingia kwenye michezo inayoshiriki, weka dau kwa fedha halisi, zungusha na anza kukusanya.

Real Sociedad Kuwasaka Pointi Tatu Uwanja Wa Martínez Valero

Elche watawapokea Real Sociedad katika uwanja wao wa nyumbani wa Martínez Valero, katika mechi ya round ya nne ya msimu mpya wa LaLiga. Mechi hii inatarajiwa kuwa na changamoto kubwa kwa wenyeji, ambao wataenda kupambana na timu iliyokuwa na historia ya ubora dhidi yao katika miaka ya hivi karibuni. Elche wanahitaji ushindi ili kuboresha nafasi yao ya awali kwenye msimimo wa ligi.

Elche wanaingia kwenye mechi hii wakiwa hawajapata matokeo mazuri hivi karibuni, baada ya kupoteza mechi yao ya awali kwa bao 3-2 dhidi ya Real Racing Club. Timu hiyo, inayoongozwa kwenye ulinzi na wachezaji kama Víctor Chust na David Affengruber, itahitajika kuimarisha mchezo wao wa nyuma endapo watataka kuzuia mashambulizi ya wageni wao. Elche wanajulikana kwa kucheza mpira mfupi wanapokuwa nyumbani, lakini msimu huu wameonekana kuwa vizuri katika mstari wa mbele.

Real Sociedad, kwa upande wao, wanaingia kwenye mechi hii na mchanganyiko wa matokeo walishinda dhidi ya Espanyol kwa bao 2-1 kabla ya kupata pigo kubwa la kufungwa mabao 4-1 na Real Madrid huko Bernabéu.

Timu hiyo ina wachezaji wenye vipaji kama Takefusa Kubo, Mikel Oyarzabal na Luka Sučić, ambao wanategemewa kuleta hatari kubwa mbele ya golo la Elche. Real Sociedad watakuwa na hamu ya kurejesha msimamo wao baada ya kushindwa vibaya dhidi ya mabingwa watetezi.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kihistoria, Real Sociedad wana ubora mkubwa dhidi ya Elche, wakiwa wameshinda mechi nane kati ya kumi za mwisho kati yao, huku Elche wakishinda mara moja tu na mechi moja kuishia sare. Hata katika mechi zao za hivi karibuni zaidi, Real Sociedad wameonyesha nguvu ya wazi, ikiwemo ushindi wa 3-1 uliopita msimu jana. Rekodi hii ya kihistoria inawapa Real Sociedad ukubwa kabla ya safari yao ya kwenda Elche.

Kwa ujumla, mechi hii inatarajiwa kuwa na uwiano fulani kutokana na Elche kuwa na faida ya kucheza nyumbani, lakini rekodi ya kihistoria na ubora wa jumla wa Real Sociedad unawapa wageni nafasi kubwa zaidi ya kuchukua pointi tatu. Elche watahitaji kuwa makini sana kiulinzi na kutumia vizuri fursa chache watakazopata mbele ili kuepuka kuendelea na msimu mgumu wa kuanzia.

Shigongo Aanza Safari Ya Soko La Kisasa La Bilioni 4 Buchosa – Video

Global Publishers
September 7, 2026
30 views
0 Comments

Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo, ameambatana na Madiwani pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Buchosa, akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo (DED), Benson Peter Mihayo, na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa, Isaac Mashimba, katika ziara ya kujifunza kuhusu ujenzi na uendeshaji wa masoko ya kisasa.

Ziara hiyo imefanyika katika Soko la Majengo jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utekelezaji wa ahadi ya Mbunge huyo ya kujenga soko la kisasa lenye thamani ya shilingi bilioni 4 ndani ya Jimbo la Buchosa.

Katika ziara hiyo, Shigongo akiwa pamoja na Madiwani na wataalamu wa Halmashauri ya Buchosa, wamekagua maendeleo ya ujenzi wa Soko la Majengo na kujifunza namna linavyoendeshwa na kusimamiwa.

Lengo ni kuhakikisha uzoefu na maarifa yatakayopatikana yanatumika katika utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa soko la kisasa katika Jimbo la Buchosa.

Shigongo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo la Buchosa, ikiwemo ujenzi wa soko hilo.

Breaking: Mume Wa Rais Samia, Hafidh Ameir Afariki Dunia – Video

Global Publishers
September 7, 2026
6 views
0 Comments

Mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Hafidh Ameir, amefariki dunia.

Taarifa za kifo cha Hafidh Ameir zimetangazwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, kupitia vyombo vya habari.

Hafidh Ameir alikuwa mume wa Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Ikulu, wamejaliwa watoto wanne.