Rais Samia Apewa Pole na Viongozi Mbalimbali Baada Ya Kifo Cha Mumewe – Picha

Global Publishers
September 8, 2026
72 views
0 Comments

Felix Antoine Tshisekedi Tshilombo, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akimfariji Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 08 Septemba, 2026 kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Sept, 2026.

Viongozi, wageni mbalimbali, viongozi wa dini, wasanii na watu kutoka kada tofauti wamefika Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, kumfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba wa mumewe, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.

Rais Samia amewasili nyumbani kwake Kizimkazi leo, Septemba 8, 2026, baada ya mumewe kufariki dunia Septemba 7, 2026 katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar.

Mtume Boniface Mwamposa pamoja na Mchungaji Tony Kapola wakimfariji Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 08 Septemba, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan, aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Sept, 2026.

Miongoni mwa waliomtembelea Rais Samia ni Rais wa Jamhuri ya Burundi, Evariste Ndayishimiye, ambaye alifika kutoa pole kufuatia msiba huo.

Viongozi wa dini pia wameungana na waombolezaji kumfariji Rais Samia, akiwemo Mtume Boniface Mwamposa pamoja na Mchungaji Tony Kapola.

Evariste Ndayishimiye, Rais wa Jamhuri ya Burundi akimfariji Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 08 Septemba, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Sept, 2026.

Aidha, wasanii mbalimbali wamefika Kizimkazi kutoa pole na kumfariji Rais Samia katika kipindi hiki cha majonzi.

Msiba huo umeendelea kuwakutanisha viongozi na wageni mbalimbali wanaofika Kizimkazi kutoa pole kwa Rais Samia na familia ya Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.

Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali wakimfariji Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 08 Septemba, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan, aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Sept, 2026.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Afrika CDC) Dkt. Jean Kaseya akimfariji  Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 08 Septemba, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan, aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Sept, 2026.
Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali wakimfariji Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 08 Septemba, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan, aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Sept, 2026.

 

Rais Samia Apewa Pole Za Viongozi Mbalimbali Baada Ya Kifo Cha Mumewe – Picha

Global Publishers
September 8, 2026
0 views
0 Comments

Viongozi, wageni mbalimbali, viongozi wa dini, wasanii na watu kutoka kada tofauti wamefika Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, kumfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba wa mumewe, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.

Rais Samia amewasili nyumbani kwake Kizimkazi leo, Septemba 8, 2026, baada ya mumewe kufariki dunia Septemba 7, 2026 katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar.

Miongoni mwa waliomtembelea Rais Samia ni Rais wa Jamhuri ya Burundi, Evariste Ndayishimiye, ambaye alifika kutoa pole kufuatia msiba huo.

Viongozi wa dini pia wameungana na waombolezaji kumfariji Rais Samia, akiwemo Mtume Boniface Mwamposa pamoja na Mchungaji Tony Kapola.

Aidha, wasanii mbalimbali wamefika Kizimkazi kutoa pole na kumfariji Rais Samia katika kipindi hiki cha majonzi.

Msiba huo umeendelea kuwakutanisha viongozi na wageni mbalimbali wanaofika Kizimkazi kutoa pole kwa Rais Samia na familia ya Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.

Ikulu Yatoa Onyo Dhidi Ya Taarifa Feki Za Shughuli Za Rais Samia

Global Publishers
September 8, 2026
6 views
0 Comments

Ikulu imeonya umma dhidi ya kusambaza taarifa za uongo zinazohusu shughuli za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, zikieleza kuwa taarifa rasmi hutolewa kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Katika taarifa iliyotolewa Zanzibar leo, Septemba 8, 2026, Kurugenzi hiyo imesema imebaini uwepo wa taarifa zinazotengenezwa kwa sura ya taarifa rasmi na kusambazwa mitandaoni zikidaiwa kutoka Ikulu au kuhusishwa na Rais.

Ikulu imesema taarifa zote rasmi kuhusu shughuli za Rais hutolewa kupitia tovuti na kurasa rasmi za Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ikiwemo Instagram @ikulu_mawasiliano, Facebook @ikulu.mawasiliano pamoja na tovuti ya Ikulu.

Kurugenzi hiyo imesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuthibitisha taarifa kuhusu Rais kupitia vyanzo rasmi kabla ya kuzipokea au kuzisambaza, ili kuepuka kueneza taarifa za upotoshaji.

Aidha, Ikulu imekumbusha kuwa utengenezaji na usambazaji wa taarifa za uongo kwa kutumia jina, nembo au utambulisho wa Rais bila ruhusa ni kosa kwa mujibu wa Vifungu vya 15 na 16 vya Sheria ya Makosa ya Mtandao, Sura ya 443.

Taarifa hiyo imesainiwa na Bakari S. Machumu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Dai Dai ya Shakira na Burna Boy Yafikisha Views Bilioni Moja YouTube

Wimbo “Dai Dai” wa mwanamuziki wa Colombia, Shakira, akishirikiana na staa wa Afrobeats kutoka Nigeria, Burna Boy, umeendelea kufanya vizuri duniani baada ya video yake rasmi kufikisha zaidi ya views bilioni moja kwenye YouTube.

Mafanikio hayo yamefikiwa ndani ya takribani miezi minne tangu video hiyo itoke, hatua inayoufanya “Dai Dai” kuwa miongoni mwa nyimbo zilizofanya vizuri zaidi katika mwaka 2026.

Kwa mujibu wa taarifa zinazohusiana na mafanikio ya wimbo huo, “Dai Dai” imekuwa video ya kwanza ya muziki iliyotolewa mwaka 2026 kufikisha views bilioni moja kwenye YouTube, ikiwa ni hatua kubwa kwa Shakira na Burna Boy.

Taarifa kuhusu tarehe ya kutolewa kwa wimbo huo pia imefanyiwa marekebisho, ambapo “Dai Dai” ilitolewa rasmi Mei 15, 2026, badala ya Mei 23 kama ilivyodaiwa awali. FIFA ilithibitisha tarehe hiyo na kuutaja wimbo huo kama sehemu rasmi ya muziki wa Kombe la Dunia la FIFA 2026.

“Dai Dai” umeunganisha mitindo mbalimbali ya muziki, ikiwemo Afrobeats, Latin pop, dance-pop na reggaeton, huku ujumbe wake ukilenga kuhamasisha umoja, ujasiri na shauku ya soka.

Nafasi yake katika kampeni ya muziki ya Kombe la Dunia imeupa wimbo huo jukwaa kubwa zaidi la kimataifa, na kuchangia kuufikisha kwa mashabiki wa muziki na soka katika sehemu mbalimbali duniani.

Mbali na mafanikio yake kwenye YouTube, wimbo huo pia umeonyesha kufanya vizuri kwenye chati za kimataifa, huku taarifa mbalimbali zikieleza kuwa umefikia nafasi za juu katika masoko kadhaa duniani.

Mirabaha Kusaidia Elimu ya Watoto

Mafanikio ya “Dai Dai” pia yana upande wa kijamii. FIFA imesema mapato ya mirabaha yanayotokana na wimbo huo yanaelekezwa kwenye FIFA Global Citizen Education Fund, mfuko unaolenga kusaidia upatikanaji wa elimu bora na fursa za michezo kwa watoto duniani.

Kwa Shakira, mafanikio ya “Dai Dai” yanaendeleza historia yake ya kushirikishwa katika muziki unaohusishwa na Kombe la Dunia, miaka kadhaa baada ya kufanya vizuri kupitia “Waka Waka (This Time for Africa)” wakati wa Kombe la Dunia la 2010.

Kwa upande wa Burna Boy, ushirikiano huo ni hatua nyingine inayoonyesha namna Afrobeats inavyoendelea kupata nafasi kubwa katika jukwaa la muziki wa kimataifa.

Kwa kufikisha zaidi ya views bilioni moja ndani ya kipindi kifupi, “Dai Dai” imejiweka miongoni mwa mafanikio makubwa ya muziki wa mwaka 2026, huku Shakira na Burna Boy wakiendelea kuvuna matunda ya ushirikiano wao wa kimuziki.

Polisi Yakamata Watuhumiwa 418 Kwa Makosa Mbalimbali, Wakifikishwa Mahakamani

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limekamata jumla ya watuhumiwa 418 kwa makosa mbalimbali katika kipindi cha kuanzia Agosti 12 hadi Septemba 7, 2026, ikiwa ni sehemu ya misako na operesheni za kukabiliana na uhalifu mkoani humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, kati ya watuhumiwa hao, 118 wamekamatwa wakiwa na vitu mbalimbali vinavyodhaniwa kuwa vya uhalifu, ikiwemo mirungi kilo 46 na gramu 805, bangi kilo 3, mafuta ya dizeli dumu 39, box 24 za marumaru (tiles), debe 15 za mpunga, kuku 127, pombe ya moshi lita 5, vipande 30 vya magamba ya kakakuona, pamoja na vifaa mbalimbali vya elektroniki.

Vitu vingine vilivyokamatwa ni majiko manne ya gesi, feni tano, mashine moja ya aluminium, betri nne za gari zenye thamani ya Sh1.8 milioni, sim tank mbili zenye ujazo wa lita 5,000, simu ndogo 26, televisheni tano, laptop moja aina ya Dell, kompyuta mbili aina ya HP, smartphone mbili, redio mbili, power bank moja, blender moja, friji moja, mashine mbili za kunyolea, saa mbili za mkononi na pikipiki 45.

Aidha, Polisi mkoani Dodoma imewashikilia watuhumiwa 16 kwa kesi ya kuharibu miundombinu ya barabara ya mzunuko Ring Road, watuhumiwa saba kwa kuharibu mazingira, mmoja kwa kubaka, wanne kwa mauaji, wanne kwa ramli chonganishi, wawili kwa ukatili dhidi ya mtoto, wawili kwa wizi wa mifugo, huku watuhumiwa 41 wakikabiliwa na kesi za uvunjaji na wengine 211 kwa makosa mbalimbali.

Katika hatua nyingine, kwa upande wa kikosi cha Usalama Barabarani, Jeshi la Polisi limeendelea kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara, wakiwemo mashuleni, vijiji vya bodaboda, stendi za mabasi na maeneo mengine.

Hatua hizo zimeelezwa kuwa sehemu ya jitihada za kukabiliana na makosa ya barabarani. Katika kipindi hicho, madereva 15,018 wamekamatwa kwa makosa mbalimbali, ambapo madereva watatu wamefungiwa leseni kwa muda wa miezi mitatu na mmoja kwa miaka mitano kwa makosa ya kuendesha kwa uzembe na kusababisha ajali, kuzidisha abiria na mwendo kasi, huku madereva 10 wakifikishwa mahakamani.

Polisi Dodoma Yakamata Watuhumiwa 418 Kwa Makosa Mbalimbali, Madereva 10 Wakifikishwa Mahakamani.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limekamata jumla ya watuhumiwa 418 kwa makosa mbalimbali katika kipindi cha kuanzia Agosti 12 hadi Septemba 7, 2026, ikiwa ni sehemu ya misako na operesheni za kukabiliana na uhalifu mkoani humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, kati ya watuhumiwa hao, 118 wamekamatwa wakiwa na vitu mbalimbali vinavyodhaniwa kuwa vya uhalifu, ikiwemo mirungi kilo 46 na gramu 805, bangi kilo 3, mafuta ya dizeli dumu 39, box 24 za marumaru (tiles), debe 15 za mpunga, kuku 127, pombe ya moshi lita 5, vipande 30 vya magamba ya kakakuona, pamoja na vifaa mbalimbali vya elektroniki.

Vitu vingine vilivyokamatwa ni majiko manne ya gesi, feni tano, mashine moja ya aluminium, betri nne za gari zenye thamani ya Sh1.8 milioni, sim tank mbili zenye ujazo wa lita 5,000, simu ndogo 26, televisheni tano, laptop moja aina ya Dell, kompyuta mbili aina ya HP, smartphone mbili, redio mbili, power bank moja, blender moja, friji moja, mashine mbili za kunyolea, saa mbili za mkononi na pikipiki 45.

Aidha, Polisi mkoani Dodoma imewashikilia watuhumiwa 16 kwa kesi ya kuharibu miundombinu ya barabara ya mzunuko Ring Road, watuhumiwa saba kwa kuharibu mazingira, mmoja kwa kubaka, wanne kwa mauaji, wanne kwa ramli chonganishi, wawili kwa ukatili dhidi ya mtoto, wawili kwa wizi wa mifugo, huku watuhumiwa 41 wakikabiliwa na kesi za uvunjaji na wengine 211 kwa makosa mbalimbali.

Katika hatua nyingine, kwa upande wa kikosi cha Usalama Barabarani, Jeshi la Polisi limeendelea kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara, wakiwemo mashuleni, vijiji vya bodaboda, stendi za mabasi na maeneo mengine.

Hatua hizo zimeelezwa kuwa sehemu ya jitihada za kukabiliana na makosa ya barabarani. Katika kipindi hicho, madereva 15,018 wamekamatwa kwa makosa mbalimbali, ambapo madereva watatu wamefungiwa leseni kwa muda wa miezi mitatu na mmoja kwa miaka mitano kwa makosa ya kuendesha kwa uzembe na kusababisha ajali, kuzidisha abiria na mwendo kasi, huku madereva 10 wakifikishwa mahakamani.

Meridian Icy Fruits: Mchanganyiko wa Barafu, Matunda na Teknolojia Kwenye Slot Mpya

Global Publishers
September 8, 2026
18 views
0 Comments

Meridianbet imefungua mlango wa burudani nyingine ya kisasa kupitia Meridian Icy Fruits, mchezo wa sloti unaokuja na mchanganyiko usio wa kawaida wa barafu na matunda yanayong’aa. Mandhari yake imeundwa kwa mtindo unaovutia macho na kutoa hisia ya mazingira ya baridi, huku teknolojia ya kidijitali ikiunganisha kila kipengele kwa mwonekano mmoja. Ni mchezo uliobuniwa kuleta uzoefu wa kuona na kusikia unaotofautiana na michezo mingine ya sloti.

Katika moyo wa mchezo huu kuna alama ambazo mashabiki wanaweza kuzitambua kwa urahisi. Matunda yanaonekana pamoja na kengele na Lucky 7, huku kila alama ikiwa sehemu ya muundo wa mchezo. Mchanganyiko wa alama hizi za kawaida na muonekano wa kisasa unafanya mchezo uwe rahisi kufuatilia, hasa kwa mtumiaji anayefungua ukurasa mpya wa michezo ya sloti za kidijitali.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kwa upande wa mfumo wa mchezo, Meridian Icy Fruits imekuja na mistari 40 ya ushindi inayoruhusu mchanganyiko mbalimbali wa alama kuonekana katika kila mzunguko. Hii ina maana kwamba skrini inaweza kubadilika mara kwa mara kadri alama zinavyopangwa upya. Mfumo huo unaongeza mabadiliko kwenye mchezo na kuufanya kila mzunguko kuwa na taswira yake ndani ya muundo wa jumla.

Sauti na uhuishaji nao wamepewa nafasi yao maalumu. Muziki unaendana na mazingira ya barafu, huku harakati za alama zikitoa hisia ya mchezo unaoendelea kuishi kwenye skrini. Uhuishaji huo wa kisasa unaongeza mwingiliano kati ya mtumiaji na mchezo, na kufanya uzoefu usiwe wa kutegemea picha pekee bali pia sauti na miondoko inayotokea wakati wa mchezo.

Kwa kifupi, Meridian Icy Fruits ni mchanganyiko wa ubunifu, teknolojia na burudani ya kisasa ya sloti. Kuanzia matunda yanayong’aa, kengele na Lucky 7, hadi mistari 40 ya ushindi pamoja na mandhari ya barafu, kila kipengele kimejengwa kuongeza mvuto wa mchezo.

Real Madrid, Inter, Dortmund na Villarreal Kitawaka Ligi ya Mabingwa

Kama kawaida ile siku tuliyokuwa tunaingoja imefika kwani ni siku maalumu ya kwenda kuishuhudia Ligi ya Mabingwa. Wababe wengi kushuka uwanjani kumenyana kusaka pointi 3. Je wewe unasubiri nini kujipigia mkwanja?

Tukianza na kule Santiago Bernabeu itapigwa mechi ya Real Madrid dhidi ya Inter Milan, ambapo wakali wa ubashiri wanampa nafasi kubwa ya kushinda vijana wa Mourinho kwasababu ya kuwepo nyumbani.

Real Madrid wanahitaji kurejesha heshima yao mbele ya mashabili baada ya kupoteza mechi iliyopita wakiwa ugenini na kufanya baadhi ya mashabiki kuwa na hofu juu ya kiwango ambacho walikionesha.

Vijana hao wa Mourinho wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na kumbukumbu nzuri katika siku za ufunguzi wa Champions League. Wameshinda mechi 17 kati ya 19 za kwanza za kampeni zao za Champions League, jambo linaloonyesha uwezo wao wa kuanza mashindano haya kwa nguvu. Jisajili hapa.

Tengeneza pesa kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Inter wanaingia Bernabéu wakiwa katika hali nzuri zaidi kwa upande wa matokeo. Wameshinda mechi zao tatu za kwanza za Serie A, na ushindi wao mkubwa zaidi ulikuwa ule wa 3-2 dhidi ya Napoli baada ya kuwa nyuma kwa mabao mawili. Lautaro Martínez alifunga mabao mawili huku Marcus Thuram akifunga bao jingine.

Pia Inter wanaonekana kuwa na faida kwenye midfield kwa sababu Real Madrid wameathiriwa na majeraha na suspensions. Barella, Çalhanoğlu na wachezaji wengine wa Inter wanaweza kujaribu kutumia udhaifu huo kwa kutawala eneo la kati.

Je nani unampa nafasi ya kuondoka na ushindi siku ya leo?. Tengeneza jamvi lako la ushindi na ubeti sasa.

Lakini pia mtanange mwingine ni huu wa  Borussia Dortmund dhidi ya Villarreal ambapo kila timu inahitaji kushinda kwenye mechi yao ya kwanza ambapo mchezo huu utapigwa pale Signal Iduna Park na wenyeji ndio wanapewa nafasi nzuri ya kuondoka na ushindi.

Huu ni wakati wa BVB kuthibitisha kwamba wanaweza kuonesha kiwango bora licha ya kusua sua kwenye ligi kuu kule Ujerumani. Baada ya kuanza msimu kwa changamoto, wameweza kujikusanyia kasi kupitia matokeo mazuri na kiwango bora cha ushambuliaji. Ushindi wao kwenye mechi iliyopita inawapa kujiamini kuelekea mchezo huu.

Wachezaji wenye uwezo mkubwa pia wanao kama vile Serhou Guirassy, Nmecha, Bellingham na wengine wengi ambao kwa pamoja wanafanya kikosi kuwa bora zaidi.

Vilevile Villarreal wao wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na mambo mengi ya kuyafanyia kazi. Mwanzo wao wa msimu wa La Liga haujawa mzuri kama walivyotarajia, huku matokeo yao yakionyesha kwamba bado wanatafuta uthabiti. Jisajili hapa.

Kipigo cha 3-2 dhidi ya Deportivo La Coruña katika mchezo wao wa mwisho kimeongeza maswali kuhusu uwezo wao wa kulinda lango, hasa wanapokutana na timu yenye kasi na nguvu ya kushambulia kama Dortmund.

Hata hivyo, Villarreal hawapaswi kuchukuliwa kama timu rahisi. Wana uzoefu wa kucheza katika mashindano ya Ulaya na wana uwezo wa kuleta matatizo kupitia umiliki wa mpira, pasi za haraka na mashambulizi ya kushtukiza. Nani kushinda mechi hii?. Bashiri sasa.

Halikadhalika nao FC Porto watakuwa kibaruani dhidi ya Manchester, mechi ambayo itapigwa katika uwanja wa City itachezwa katika uwanja wa Estádio do Dragão, ikiwa ni mechi ya kwanza ya hatua ya ligi ya UEFA Champions League 2026/27 kati yao.

Hii ni mechi inayokutanisha timu mbili zinazoingia kwenye Champions League zikiwa na mwanzo mzuri wa msimu. Porto wamekuwa na matokeo mazuri ndani ya ligi yao, huku City pia wakiwa wameanza kampeni yao ya ndani kwa kiwango cha juu. ESPN inaeleza kuwa timu zote mbili zimeanza msimu wa ligi zikiwa na rekodi ya ushindi wa asilimia 100.

Porto wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na faida kubwa ya kucheza nyumbani. Estádio do Dragão ni uwanja ambao mara nyingi huweka presha kubwa kwa timu pinzani, hasa katika usiku wa Champions League.

Porto pia wameanza vizuri msimu, wakiwa wameshinda mechi zao tatu mfululizo katika mashindano mbalimbali, huku ushindi wao ukiambatana na uwezo mzuri wa kufunga. Zaidi ya hapo, wamekuwa na rekodi nzuri nyumbani katika Champions League, wakishinda nne kati ya mechi zao sita zilizopita za michuano hiyo wakiwa Dragão.

Wakati City wao wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na confidence kubwa. Chini ya Enzo Maresca, wameanza msimu kwa kiwango kizuri na wamekuwa na rekodi nzuri kwenye ligi.

City wana faida kubwa kwenye ubora wa midfield. Uwezo wao wa kutawala possession, kuzungusha mpira na kuwalazimisha Porto kukaa chini unaweza kuwa sehemu muhimu ya mchezo. Wanapokuwa na mpira kwa muda mrefu, Porto watalazimika kutumia nguvu nyingi katika pressing na ulinzi.

Takwimu zinaonesha kuwa mechi 4 za mwisho kukutana City wameshinda 3 na sare moja, hivyo hii ni nafasi ya wenyeji kulipa kisasi. Je wataweza mbele ya vijana hawa wa Marsca?. Odds kubwa zipo hapa. Beti sasa

TRA United Yamfukuza Kocha Ndayiragije Baada Ya Mwanzo Mbaya

Global Publishers
September 8, 2026
420 views
0 Comments

Klabu ya TRA United SC imethibitisha kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba na Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije, kwa makubaliano ya pande zote mbili kuanzia Septemba 7, 2026.

Kupitia taarifa yake, uongozi wa klabu hiyo umemshukuru Ndayiragije kwa mchango wake mkubwa, weledi na huduma aliyotoa kwa timu katika kipindi chote alichokuwa sehemu ya klabu hiyo.

TRA United imemtakia kocha huyo kila la kheri na mafanikio katika hatua inayofuata ya maisha na taaluma yake ya ukocha.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, klabu itaendelea kuwafahamisha wanachama, mashabiki na wadau wake kuhusu hatua zaidi zitakazochukuliwa kuhusiana na uongozi wa benchi la ufundi.

Uamuzi huo unakuja baada ya mwenendo usioridhisha wa TRA United katika michezo mitano ya mwanzo, ambapo timu hiyo imekusanya alama tatu, bila kupata ushindi, ikipoteza michezo miwili na kutoka sare mara tatu.https://youtu.be/gbIBVH4WGP8

Shahidi wa Nne Kesi ya Uhaini Lissu Kuendelea Kutoa Ushahidi leo

Dar es Salaam: Shahidi wa nne katika kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Brenda Rupia, leo Septemba 8, 2026 anaendelea kutoa ushahidi wa utetezi dhidi ya Lissu.

Jana, Septemba 7, 2026, Rupia alianza kutoa ushahidi wake ambapo Lissu alimhoji kuhusu mkutano uliofanyika Aprili 3, 2025, ukiwemo ulikuwa na lengo gani na nani aliyeandaa mkutano huo.

Katika majibu yake, Rupia alieleza kuwa mkutano huo ulilenga kuwakutanisha watia nia wa Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa ajili ya kujadili msimamo wa chama wa “No Reforms, No Election”.

Alisema uamuzi wa kufanyika kwa mkutano huo ulifanywa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, pamoja na Sekretarieti ya chama, akisisitiza kuwa mkutano huo haukuandaliwa na Tundu Lissu kama inavyodaiwa.

Rupia pia alieleza kuwa Kurugenzi ya Mawasiliano na Uenezi chini yake ndiyo iliyohusika na kuandaa taarifa kwa umma pamoja na kuwaalika waandishi wa habari kuhudhuria mkutano huo.

Hata hivyo, alisema waandishi wa habari walioalikwa hawakupewa maelekezo yoyote ya kikazi wala kuagizwa kurusha matangazo ya moja kwa moja kutoka katika mkutano huo.

Katika ushahidi wake, Rupia alisisitiza kuwa Lissu alihudhuria mkutano huo kama mzungumzaji mkuu kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, na kwamba hakuhusika katika ualikaji wa vyombo vya habari.

Aidha, shahidi huyo alieleza kuwa umiliki wa maudhui yote ya habari yaliyorekodiwa siku hiyo ulikuwa chini ya vyombo vya habari vilivyohudhuria, na si CHADEMA au viongozi wake.