Waziri Mkuu Afunga Mkutano wa Makambi ya Waadventista Kinyerezi

Global Publishers
September 19, 2026
6 views
0 Comments


Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo (Jumamosi, Septemba 19, 2026) ameshiriki Ibada Kuu na Kufunga Mkutano wa Makambi ya Kanisa la Waadventista Sabato, yaliyofanyika kwa siku saba, Kinyerezi jijini Dar es Salaam

Akizungumza na waumini wa kanisa hilo Dkt. Mwigulu amewasihi waumini wa kanisa hilo kuendelea kudumisha amani na kusimamia maadili ya watoto huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kulinda uhuru wa wananchi kuabudu kwa kadri ya imani zao.

Trump Awapiga Marufuku CNN, MS NOW na Politico Ikulu ya Marekani

Washington, D.C. — Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuwa waandishi wa habari kutoka vyombo vya CNN, MS NOW na Politico wamepigwa marufuku kuingia Ikulu ya Marekani, huku akionya kuwa vyombo vingine vya habari vinaweza kufuatia.

Trump alitoa tangazo hilo kupitia mtandao wake wa Truth Social Ijumaa, Septemba 18, 2026. Alivituhumu vyombo hivyo kwa kile alichokiita kuripoti habari za uongo na taarifa zisizo za kweli kuhusu yeye, utawala wake na Marekani.

Trump aliandika kuwa vyombo vya habari havipaswi kuruhusiwa “kuandika au kuripoti habari za kubuni na uongo” vinapomzungumzia Rais wa Marekani au utawala wake. Pia aliongeza kuwa “vyombo vingine vya habari vya uongo” vinaweza kufuatia.

Haikufahamika mara moja kwa nini Trump alivichagua CNN, MS NOW na Politico pekee. Vyombo hivyo pia havikuwa vimetolewa maelezo ya kina kuhusu sababu maalumu za kuchukuliwa hatua hiyo.

Baada ya tangazo hilo, Brian Stelter, mchambuzi mkuu wa masuala ya vyombo vya habari wa CNN, alisema kwenye televisheni kuwa bado haikuwa wazi kama marufuku hiyo ilikuwa imetekelezwa kikamilifu.

CNN, kwa upande wake, ilisema inasimama nyuma ya timu yake ya waandishi wa habari walioko Ikulu na kwamba inaamini wana haki ya kikatiba ya kufanya kazi zao bila kuingiliwa na serikali.

Katika mahojiano yaliyofuata katika Ikulu, mwandishi alimuuliza Trump jinsi anavyoweza kuendana na Katiba ya Marekani, hasa kifungu cha Kwanza kinacholinda uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari.

Trump alijibu kuwa anaiheshimu Katiba, huku akiendelea kuvikosoa vyombo hivyo na kuvishutumu kwa kuwa na taarifa anazoziita za uongo.

Trump alisema Marekani inahitaji habari za “uaminifu, haki na ukweli,” na akasisitiza kuwa nchi inahitaji pia vyombo vya habari vilivyo huru na vya haki.

Hatua hiyo imezua mjadala kuhusu uhusiano kati ya Ikulu ya Marekani na vyombo vya habari, pamoja na mipaka ya mamlaka ya serikali katika kuwapatia waandishi wa habari fursa ya kufikia rais na shughuli za Ikulu.

Katika kipindi chake cha pili madarakani, Trump amekuwa akikosoa mara kwa mara waandishi na vyombo vya habari vinavyoripoti kuhusu utawala wake kwa namna asiyoikubali.

Utawala wake pia umewahi kuchukua hatua zinazowazuia au kuwabana baadhi ya waandishi wa habari, huku kukiwa na mijadala na kesi za kisheria kuhusu uhuru wa vyombo vya habari na haki ya serikali kudhibiti upatikanaji wa maeneo ya serikali.

Suala kubwa linalotarajiwa kujadiliwa kisheria ni iwapo serikali inaweza kuzuia chombo cha habari kupata fursa ya kuripoti kutoka Ikulu kwa sababu ya mtazamo au maudhui ya taarifa zake. Uamuzi wa mwisho kuhusu uhalali wa hatua hiyo unaweza kutegemea mahakama.

Serikali Yatoa Tahadhari Athari za El Niño Katika Mvua Za Vuli

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imetoa tahadhari kuhusu uwezekano wa kutokea kwa athari zinazohusishwa na hali ya El Niño katika kipindi cha mvua za Vuli za miezi ya Oktoba hadi Desemba 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo, tarehe 18 Agosti 2026, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitoa rasmi utabiri wa msimu wa mvua za Vuli (Oktoba–Desemba 2026), ambao unaashiria kuwepo kwa viwango vikubwa vya hali ya El Niño kwenye eneo kubwa la Bahari ya Pasifiki.

Hali hiyo inatarajiwa kuchangia ongezeko la mvua za Vuli za mwaka 2026 kuwa juu ya wastani katika baadhi ya maeneo nchini.

Wizara imesema baadhi ya athari zinazoweza kujitokeza kutokana na hali hiyo ni pamoja na mafuriko, maporomoko ya ardhi, kujaa kwa mito na mifereji, uharibifu wa miundombinu ya barabara, reli, madaraja na majengo, pamoja na uharibifu wa mali na mazao.

Aidha, imeonya kuwa kuna uwezekano wa kuongezeka kwa hatari ya magonjwa yanayotokana na matumizi ya maji yasiyo salama.

Kutokana na hali hiyo, Wizara imetoa wito kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoa elimu na tahadhari kwa wananchi kuhusu athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Niño.

Maafisa hao wametakiwa pia kuwatambua wananchi walio katika mazingira hatarishi, hususan watoto, wazee na watu wenye ulemavu, pamoja na kufanya maandalizi ya utoaji wa msaada wa kisaikolojia na kijamii kwa wananchi watakaoathiriwa na mvua hizo.

Kwa upande wa wazazi, walezi, walimu na jamii kwa ujumla, Wizara imewataka kuchukua tahadhari mapema kwa kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa, kuepuka kuvuka mito au maeneo yaliyofunikwa na maji na kutoa usaidizi kwa watu wenye ulemavu na wazee wasiojiweza.

Wananchi pia wametakiwa kutoruhusu watoto kucheza karibu na mifereji, mitaro, mito, makalavati, madaraja na maeneo ambayo maji yanapita kwa kasi.

Aidha, wametakiwa kusafisha mitaro na mifereji ya kupitisha maji ili kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo, pamoja na kuhakikisha wanapata maji salama ya kunywa na kupikia wakati wote.

Wizara imewataka pia wakazi wanaoishi katika maeneo ya mabondeni, karibu na mito na maeneo yenye historia ya mafuriko au maporomoko ya ardhi kuwa waangalifu zaidi na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, ikiwemo kuhama mapema endapo wataelekezwa kufanya hivyo.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Charles F. Komba, Septemba 19, 2026.

Iran Yamnyonga Mtu Aliyetiwa Hatiani kwa Ujasusi wa Mossad

Global Publishers
September 19, 2026
0 views
0 Comments

Tehran, Iran — Iran imetekeleza hukumu ya kifo dhidi ya Hoseyn Paderan, aliyepatikana na hatia ya kufanya ujasusi na kushirikiana na shirika la ujasusi la Israel, Mossad, vyombo vya habari vya Iran vimeripoti.

Hukumu hiyo ilitekelezwa baada ya rufaa ya Paderan kukataliwa na Mahakama ya Juu ya Iran kuthibitisha hukumu hiyo.

Kwa mujibu wa mahakama ya Iran, Paderan alikamatwa kwa tuhuma za kuipa Mossad taarifa za siri zinazohusiana na masuala ya kijeshi.

Mamlaka zilidai kuwa alikusanya taarifa kuhusu vituo vya kijeshi na maafisa wa kijeshi, ikiwemo baadhi ya taarifa zao binafsi, kisha kuzifikisha kwa mtu aliyekuwa akimshughulikia upande wa Mossad.

Mahakama pia ilidai kuwa Paderan alipokea malipo kwa njia ya fedha za Euro kwa ajili ya taarifa alizokuwa akitoa.

Mamlaka zilisema katika upekuzi wa nyumba yake vilipatikana vitu mbalimbali, ikiwemo daftari lenye taarifa zinazohusiana na makombora lililowekwa alama ya “siri ya juu”, vifaa vya kuhifadhi taarifa vilivyosimbwa kwa njia fiche, vifaa vya mawasiliano pamoja na vifaa vya kupiga picha na video.

Iran imekuwa ikichukua hatua kali dhidi ya watu wanaowatuhumu kwa kufanya ujasusi kwa niaba ya Israel, hasa katika kipindi ambacho mvutano kati ya Tehran na Tel Aviv umeendelea kuwa mkubwa.

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MTO NG’OMBE, AAGIZA TAKA ZIONDOLEWE HARAKA*

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amefanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Mto Ng’ombe, Tandale jijini Dar es Salaam, kukagua hali ya usafi wa mazingira na maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza katika kipindi cha mvua.

 

Akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Waziri wa TAMISEMI pamoja na viongozi wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Ndejembi ameelekeza Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha mto huo unasafishwa na taka zilizorundikana kandokando ya Mto Ng’ombe zinaondolewa haraka na mazingira yanaendelea kuwekwa katika hali ya usafi.

 

Amewaagiza Viongozi wa Halmshauri, kupitia maafisa mazingira na maafisa maendeleo, kuendelea kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuzingatia usafi na ukusanyaji wa taka. Amesema ni muhimu kwa Halmashauri kuweka miundombinu mizuri ya kukusanya taka na kuzichukua kwa wakati ili wananchi wasitupe taka hizo katika maeneo yasiyofaa.

 

Vilevile, ameelekeza mamlaka za Wilaya ya Kinondoni kuweka utaratibu wa maeneo rasmi ya kutupa taka ili wananchi wawe na sehemu zinazotambulika kwa ajili ya kuhifadhi taka, hatua itakayosaidia kudhibiti utupaji holela na uchafuzi wa mazingira.

 

Akizungumza na wananchi wanaoishi pembezoni mwa Mto Ng’ombe, Makamu wa Rais amewataka kuzingatia usafi wa mazingira na kubadili tabia ya utupaji taka holela, akisisitiza kuwa utunzaji wa mazingira unahitaji ushiriki wa Serikali na wananchi kwa pamoja.

 

Aidha, Makamu wa Rais ameelekeza madaraja yanayokatiza maeneo ya Pakacha na Sokoni katika Mto Kiboko yanapitika wakati wa mvua, ili wananchi waendelee kufanya shughuli zao za kijamii na kiuchumi bila kukwamishwa na changamoto za miundombinu.

 

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

19 Septemba 2026

Dar es Salaam.

 

Meridianbet Yaleta Burudani Mpya ya Kasino Kupitia Fortune Farm

Global Publishers
September 19, 2026
54 views
0 Comments

Mchezo mpya unapofika kwenye ulimwengu wa kasino, mashabiki hutafuta kitu kinachoweza kuongeza ladha ya burudani yao. Fortune Farm ya Meridianbet inakuja na simulizi la shamba lenye fursa, gurudumu la bonasi na ngazi za ushindi zinazoweza kubadilisha mwelekeo wa kila mzunguko. Hapa, unaingia ukiwa na dau lako na matarajio ya kufurahia safari inayokupa nafasi ya kufuatilia matokeo hatua kwa hatua. Ni mazingira yanayojumuisha mandhari ya shamba na msisimko wa kasino kwa namna inayovutia.

Msingi wa mchezo huu ni mfumo wake wa ngazi tatu za Wilds. Kuna 3 Wilds Level 1, 4 Wilds Level 2 na 5 Wilds Level 3, kila moja ikiwa na vizidishi vinavyoweza kuongeza thamani ya ushindi. Unapofuatilia gurudumu la bonasi, kila ngazi inakuwa sehemu ya safari yenye matarajio. Mzunguko mmoja unaweza kukupeleka kwenye hatua nyingine ya mchezo, na hivyo kuongeza hamu ya kuona kama bahati itakufungulia mlango wa bonasi inayofuata.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Fortune Farm inavutia pia kwa mfumo wake wa kuongeza ushindi. Kila bonasi inayopatikana inaweza kuongeza thamani juu ya ile iliyotangulia, na kuifanya safari ya mchezo kuwa na mfuatano wa kipekee. Kwa lugha ya shamba, ni kama kuona mavuno yakiongezeka kadri msimu unavyoendelea. Mfumo huu unaweza kuleta msisimko kwa wachezaji wanaopenda kufuatilia mabadiliko ya thamani ya ushindi.

Kwa mtu anayependa kasino yenye mfumo wa bonasi unaoleta matarajio mapya, Fortune Farm inatoa nafasi ya kujaribu uzoefu tofauti. Mandhari ya shamba, gurudumu la bonasi na Wilds tatu zinaunda safari inayoweza kukufanya ufuatilie kila hatua kwa hamu.

Meridianbet inakualika kuijua Fortune Farm na kufurahia safari yake ya kasino. Ingia kwenye jukwaa, chagua mchezo na uone namna mfumo wa bonasi na vizidishi unavyofanya kazi. Fortune Farm imefungua milango yake, na sasa unaweza kuanza safari ya kuichunguza kwa mtindo wako mwenyewe.

WAZIRI MKUU AFUNGA MKUTANO WA MAKAMBI YA WAADVENTISTA

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo (Jumamosi, Septemba 19, 2026) ameshiriki Ibada Kuu na Kufunga Mkutano wa Makambi ya Kanisa la Waadventista Sabato, yaliyofanyika kwa siku saba, Kinyerezi jijini Dar es Salaam

Akizungumza na waumini wa kanisa hilo Dkt. Mwigulu amewasihi waumini wa kanisa hilo kuendelea kudumisha amani na kusimamia maadili ya watoto huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kulinda uhuru wa wananchi kuabudu kwa kadri ya imani zao.

 

JKT Yaweka Mkazo Uzalendo wa Kidijitali, Mabele Atoa Maagizo kwa Vijana – Video

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, amesema somo la Uzalendo na Uzalendo wa Kidijitali katika silabasi za mafunzo ya JKT litaendelea kuboreshwa ili kuwaelimisha vijana kuhusu umuhimu wa kutumia mitandao ya kijamii kwa usahihi na kwa manufaa ya Taifa.

Meja Jenerali Mabele amesema hayo Septemba 18, 2026, wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Mujibu wa Sheria kupitia Operesheni Linda Amani na vijana wa kujitolea kupitia Operesheni Nishati Safi katika Kikosi cha Kanembwa JKT, mkoani Kigoma.

Amesema mafunzo hayo yana nafasi kubwa katika kuwajenga vijana kuwa wazalendo, wenye nidhamu na wanaotambua wajibu wao katika ujenzi na ulinzi wa Taifa, ikiwemo matumizi sahihi ya teknolojia na mitandao ya kijamii.

Akiwasilisha salamu za Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Brigedia Jenerali Lawrence Lugenge, Meja Jenerali Mabele amewapongeza vijana hao kwa kukubali kujiunga na JKT na kuwataka kuyaendeleza kwa vitendo maarifa na mafunzo waliyoyapata.

Kwa upande wake, Mkuu wa Tawi la Mafunzo JKT, Brigedia Jenerali Peter Mnyani, amewapongeza wahitimu hao kwa kuwa watiifu na kuzingatia taratibu wakati wote wa mafunzo.

Naye Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar, Kanali Makame Daima, amewataka vijana hao kuendelea kuulinda na kuuenzi Muungano wa Tanzania.

Akitoa taarifa ya mafunzo hayo, Kamanda wa Kikosi cha Kanembwa JKT, Kanali Mantage Nkombe, amesema vijana wote waliohitimu wamepatiwa mafunzo ya kinadharia na vitendo kwa kuzingatia silabasi husika na wamefaulu kwa viwango vinavyokubalika ndani ya JKT.

Zoezi la kufunga mafunzo ya JKT lilianza rasmi Septemba 8, 2026 katika vikosi mbalimbali vya mafunzo vya JKT. Kwa mara ya kwanza, mafunzo hayo yamefanyika kwa kuwakutanisha vijana kutoka makundi mawili, ambao ni vijana wa kujitolea kupitia Operesheni Nishati Safi na vijana wa Mujibu wa Sheria.

Macho Yote Brighton! Arsenal Yalenga Kuendeleza Kasi EPL

Global Publishers
September 19, 2026
48 views
0 Comments

Ni siku nyingine tena ya kushuhudia miamba kibao ikishuka dimbani leo kwenye Ligi kuu ya EPL. Je ni Arsenal kujihakikishia nafasi ya kwanza kwenye msimamo au Brighton watawashika shati mabingwa hao? Jisajili na ubashiri hapa.

Brighton & Hove Albion leo Jumamosi Septemba 19 wataikaribisha Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu England, EPL, utakaopigwa kuanzia saa 17:00 jioni. Pambano hilo linatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa vikosi hivyo na umuhimu wa pointi tatu.

Arsenal wataingia uwanjani wakiwa na lengo la kuendeleza kasi yao nzuri ya mwanzo wa msimu. Kikosi hicho cha Mikel Arteta kimeonyesha ushindani mkubwa katika michezo ya awali na sasa kitakuwa na kazi ya kuhakikisha kinapata matokeo mazuri dhidi ya Brighton kwenye uwanja wao.

Kwa upande wa Brighton, mchezo huo utakuwa nafasi ya kutumia faida ya kucheza mbele ya mashabiki wao. Timu hiyo pia imeonyesha uwezo wa kupata matokeo, jambo linalofanya Arsenal kutarajiwa kukutana na upinzani mkubwa katika dakika zote 90.

Macho pia yataelekezwa kwa safu za ushambuliaji za timu zote, huku kila upande ukihitaji kutumia nafasi utakazopata. Brighton wanahitaji kuwa makini katika kuzuia mashambulizi ya Arsenal.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kwa ujumla, pambano hili linatarajiwa kuwa moja ya michezo yenye mvuto katika ratiba ya EPL mwishoni mwa wiki. Brighton watakuwa wakisaka pointi mbele ya mashabiki wao, huku Arsenal wakilenga kuondoka na matokeo yatakayowaweka katika mwendo mzuri wa msimu.

Ndejembi Atoa Agizo Mto Ng’ombe, Taka Ziondolewe Haraka – Picha

Global Publishers
September 19, 2026
0 views
0 Comments


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, tarehe 18 Septemba 2026, amefanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Mto Ng’ombe, Tandale jijini Dar es Salaam, kukagua hali ya usafi wa mazingira na maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza katika kipindi cha mvua.

Akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Waziri wa TAMISEMI pamoja na viongozi wa Wilaya ya Kinondoni, Ndejembi ameelekeza Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha mto huo unasafishwa na taka zilizorundikana kandokando ya Mto Ng’ombe zinaondolewa haraka na mazingira yanaendelea kuwekwa katika hali ya usafi.

Amewaagiza Viongozi wa Halmshauri, kupitia maafisa mazingira na maafisa maendeleo, kuendelea kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuzingatia usafi na ukusanyaji wa taka. Amesema ni muhimu kwa Halmashauri kuweka miundombinu mizuri ya kukusanya taka na kuzichukua kwa wakati ili wananchi wasitupe taka hizo katika maeneo yasiyofaa.

Vilevile, ameelekeza mamlaka za Wilaya ya Kinondoni kuweka utaratibu wa maeneo rasmi ya kutupa taka ili wananchi wawe na sehemu zinazotambulika kwa ajili ya kuhifadhi taka, hatua itakayosaidia kudhibiti utupaji holela na uchafuzi wa mazingira.

Akizungumza na wananchi wanaoishi pembezoni mwa Mto Ng’ombe, Makamu wa Rais amewataka kuzingatia usafi wa mazingira na kubadili tabia ya utupaji taka holela, akisisitiza kuwa utunzaji wa mazingira unahitaji ushiriki wa Serikali na wananchi kwa pamoja.

Aidha, Makamu wa Rais ameelekeza madaraja yanayokatiza maeneo ya Pakacha na Sokoni katika Mto Kiboko yanapitika wakati wa mvua, ili wananchi waendelee kufanya shughuli zao za kijamii na kiuchumi bila kukwamishwa na changamoto za miundombinu.