Wezesha Mzawa Insurance Broker Watangaza Nafasi Nne za Kazi

Kampuni ya Wezesha Mzawa Insurance Broker Limited imetangaza nafasi za kazi kwa Watanzania wenye sifa na uzoefu katika sekta ya bima, mauzo, masoko, biashara, uhasibu na nyanja zinazohusiana.

Nafasi zilizotangazwa ni Business Development Executive, Accountant pamoja na Insurance Sales Executives, huku waombaji wakitakiwa kutimiza vigezo vilivyowekwa kwa kila nafasi.

1. Business Development Executive

Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Kwanza katika Insurance and Risk Management, Sales and Marketing, Business Administration au fani nyingine inayohusiana, pamoja na uzoefu wa angalau miaka miwili katika sekta ya bima, maendeleo ya biashara, mauzo au masoko.

2. Accountant

Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Kwanza katika Accounting au Finance, pamoja na uzoefu wa angalau miaka miwili katika sekta ya bima. Sifa ya CPA ni nyongeza.

3. Insurance Sales Executives

Waombaji wanatakiwa kuwa na Cheti katika Insurance and Risk Management, Sales, Marketing, Business Administration au fani nyingine inayohusiana.

Uzoefu katika sekta ya bima na kazi za mauzo ni nyongeza.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi yao pamoja na viambatisho muhimu vilivyothibitishwa kupitia barua pepe au kwa anuani ya ofisi ya kampuni kabla ya Septemba 30, 2026.

Wezesha Mzawa Insurance Broker Limited
P.O. Box 7534, Sinza Mori
Global Group House/Building, Opposite Wanyama Hotel
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: [email protected]

Tulia Ackson Amfariji Rais Samia Baada ya Msiba wa Mumewe – Picha

Global Publishers
September 13, 2026
480 views
0 Comments

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Uyole, Tulia Ackson, amemfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Tulia amefika Kizimkazi kufuatia msiba wa mume wa Rais Samia, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan, aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, Septemba 7, 2026.

Katika kipindi hiki cha majonzi, viongozi, ndugu, jamaa na Watanzania mbalimbali wameendelea kutoa pole na kushirikiana na Rais Samia pamoja na familia yake katika kuomboleza msiba huo.

Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan ameacha pengo kubwa kwa familia na watu waliokuwa karibu naye.

 

Singida Black Stars Yathibitisha Mabadiliko ya Uongozi wa Klabu

Global Publishers
September 13, 2026
6 views
0 Comments

Uongozi wa Klabu ya Singida Black Stars umetangaza mabadiliko ya uongozi baada ya Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Ndg. Kassano Jonathan, kuomba kujiuzulu nafasi yake.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Septemba 13, 2026, uongozi wa klabu umesema umekubali ombi hilo na kumteua Ndg. Tabitha Kidawawa kuwa Mtendaji Mkuu mpya wa Singida Black Stars, akisaidiwa na Naibu wake, Muhibu Kanu.

Aidha, uongozi wa klabu umemshukuru Kassano Jonathan kwa mchango wake mkubwa katika kipindi chote alichohudumu, huku ukimtakia kila la heri katika hatua zake zijazo.

Uongozi umeeleza kuwa unaamini mabadiliko hayo yataisaidia Singida Black Stars kuendelea kuwa nyumbani kwa wanyumbani wake na kufikia malengo yake.

Simba Yatinga Hatua ya Pili CAFCL kwa Kishindo, Yaifumua Mighty Wanderers bao 6-1

Global Publishers
September 13, 2026
0 views
0 Comments

Simba SC imefanikiwa kusonga mbele hadi hatua ya pili ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Mighty Wanderers ya Malawi.

Ushindi huo umeifanya Simba kufuzu kwa jumla ya mabao 7-1 baada ya matokeo ya michezo miwili katika hatua ya kwanza ya awali.

Katika mchezo huo, Simba ilianza kwa kasi na kufunga bao la kwanza dakika ya 7 kupitia Clatous Chama, kabla ya Cheikh Gueye kuongeza la pili dakika ya 26. Chama alifunga bao lake la pili katika mchezo huo dakika ya 34 na kuifanya Simba kwenda mapumziko ikiwa mbele.

Gueye alirejea tena kwenye orodha ya wafungaji dakika ya 69, huku Makgwala akifunga dakika ya 87. Morice alikamilisha ushindi wa Simba kwa bao la dakika ya 90+3.

Mighty Wanderers ilipata bao lake pekee kupitia Kaliati dakika ya 43.

FT: Simba SC 🇹🇿 6-1 🇲🇼 Mighty Wanderers

⚽ 07’ — Chama
⚽ 26’ — Gueye
⚽ 34’ — Chama
⚽ 43’ — Kaliati
⚽ 69’ — Gueye
⚽ 87’ — Makgwala
⚽ 90+3’ — Morice

Agg: Simba SC 7-1 Mighty Wanderers

Baada ya matokeo hayo, Simba SC sasa itakutana na FC de Agosto de Akonibe ya Guinea ya Ikweta katika hatua ya pili ya awali ya CAF Champions League.

KUNDI LA IRINGA VISION LASHEREHEKEA MIAKA MIWILI KWA KUTOA MSAADA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA HURUMA CENTER

NA MATUKIO DAIMA MEDIA, IRINGA

KUNDI la Iringa Vision

limeadhimisha miaka miwili tangu kuanzishwa kwake kwa kutoa msaada wa chakula na fedha kwa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Watoto Yatima cha Huruma Centre, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kusaidia makundi yenye uhitaji katika jamii.

Msaada huo umetolewa na wanachama wa kundi hilo kwa lengo la kushirikiana na watoto wa kituo hicho katika maadhimisho ya miaka miwili ya Iringa Vision Group, sambamba na kuonesha upendo na kuwapa faraja watoto hao.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa Iringa Vision Group, Eliza Chusi, alisema chakula na fedha zilizotolewa katika kituo hicho zimepatikana kupitia michango ya wanachama wa kundi hilo.

Chusi alisema wanachama walikubaliana kutumia sehemu ya maadhimisho yao kuwakumbuka watoto yatima badala ya kujikita katika sherehe pekee. Alisema hatua hiyo imelenga kuonesha kuwa jamii ina wajibu wa kuwajali na kuwasaidia watu wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali za maisha.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, miaka miwili ya uwepo wa Iringa Vision Group imekuwa na mafanikio makubwa katika kuimarisha ushirikiano na mshikamano miongoni mwa wanachama wake.

Alisema maadhimisho hayo yamewapa nafasi ya kutafakari walikotoka, mafanikio waliyopata na namna wanavyoweza kuendelea kutumia umoja wao kuleta manufaa kwa wanachama pamoja na jamii inayowazunguka.

“Tumetoa msaada wa chakula na fedha kwa watoto wa Kituo cha Huruma Centre. Msaada huu umetokana na michango ya wanachama wetu kwa ajili ya kuadhimisha miaka miwili tangu kuanzishwa kwa kundi letu,” alisema Chusi.

Mwenyekiti huyo aliishukuru Huruma Center kwa kuendelea kuwalea na kuwahudumia watoto yatima, akisema jukumu la kuwasaidia watoto hao halipaswi kuachiwa viongozi na walezi wa kituo pekee.

Alisema wananchi, wafanyabiashara, taasisi mbalimbali na makundi ya kijamii wanapaswa kushirikiana kuhakikisha watoto wanaoishi katika mazingira yenye changamoto wanapata mahitaji muhimu, malezi bora na matumaini ya kufikia malengo yao.

Chusi alitoa rai kwa jamii kuendelea kuwakumbuka watoto yatima, wajane na wazee wasiojiweza kwa kuwapatia misaada kulingana na uwezo wao.

Alisema baadhi ya watu katika makundi hayo wanakabiliwa na changamoto nyingi, hivyo wanahitaji faraja, upendo na msaada wa jamii ili waweze kuendesha maisha yao kwa matumaini.

Aidha, alieleza kuwa msaada si lazima uwe mkubwa, bali hata mchango mdogo unaotolewa kwa moyo wa upendo unaweza kuleta mabadiliko katika maisha ya mtu mwenye uhitaji.

Alisema Iringa Vision Group itaendelea kuyajali makundi yenye uhitaji na kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazolenga kuisaidia jamii.

“Tunatoa rai kwa jamii kuendelea kuwakumbuka watoto yatima, wajane na wazee wasiojiweza. Sisi kama Iringa Vision Group tutaendelea kuyajali makundi haya na kutoa msaada pale tutakapopata nafasi ya kufanya hivyo,” alisema Chusi.

Kwa upande wake, Katibu wa Iringa Vision Group, Nevice Katindasa, alisema kundi hilo lina wanachama zaidi ya 54 ambao wameunganishwa kwa lengo la kusaidiana wakati wa shida na raha.

Katindasa alisema tangu kuanzishwa kwa kundi hilo, wanachama wameendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali yanayowahusu, huku wakihakikisha kuwa umoja wao unaleta manufaa pia kwa wananchi wengine.

Alisema Iringa Vision Group halikuanzishwa kwa ajili ya maslahi ya wanachama pekee, bali lina dhamira ya kushirikiana na jamii katika kutoa msaada kwa makundi yenye uhitaji, yakiwamo ya watoto yatima.

Katibu huyo alisema kutoa msaada kwa Huruma Center

ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya kundi hilo na kwamba wanachama wataendelea kuandaa shughuli nyingine za kijamii kulingana na mahitaji na uwezo wao.

“Dhamira ya kundi letu ni kusaidiana wakati wa shida na raha, lakini pia kusaidia jamii. Tunapopata nafasi na uwezo wa kuwafikia watoto yatima au watu wengine wenye uhitaji, tunafanya hivyo kwa moyo mmoja,” alisema Katindasa.

Aidha, Katindasa aliwakaribisha wananchi wengine kutoka maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa wa Iringa kujiunga na kundi hilo ili kuongeza nguvu ya ushirikiano na kupanua wigo wa shughuli zake.

Alisema kuongezeka kwa wanachama kutasaidia kuimarisha mshikamano na kuwezesha kundi kuwafikia watu wengi zaidi wanaohitaji msaada.

Katindasa alisema milango ya Iringa Vision Group iko wazi kwa wananchi wenye nia njema na utayari wa kushirikiana na wengine wakati wa matatizo na furaha.

Aliongeza kuwa mshikamano ni msingi muhimu wa maendeleo ya jamii, kwa sababu unapunguza changamoto zinazoweza kumlemea mtu mmoja na kujenga moyo wa kujitolea.

Kuwa maadhimisho hayo ya miaka miwili yamekuwa na ujumbe wa kuhimiza upendo, mshikamano na uwajibikaji wa jamii kwa watoto yatima pamoja na makundi mengine yenye uhitaji.

Viongozi wa kundi hilo wameahidi kuendeleza umoja uliopo miongoni mwa wanachama na kuhakikisha Iringa Vision Group inaendelea kuwa sehemu ya jitihada za kuisaidia jamii ya Mkoa wa Iringa.

Kwa upande wake Rahabu Gavile akishukuru kwa niaba ya mkuu wa kituo hicho mchungaji Upendo Sanga alisema mchango huu ni mkubwa na kuomba jamii kuendelea kusaidia kituo hicho .

Alisema kituo kina zaidi ya watoto 90 na kuwa kwa sasa watoto wengi wapo masomoni na waliobaki wanaendelea na masomo katika shule ya kituo hicho.

TAZAMA TUKIO ZIMA HAPA

BONYEZA LINK HII KISHA PIGA KURA ZOTE NNE BAADA YA KUFUNGUA NENDA SEHEMU

BONYEZA HAPA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA PIGA KURA ZOTE NNE

 IMEANDIKWA PIGA KURA KISHA BONYEZA SEHEMU IMEANDIKWA NDIO

MATUKIO DAIMA MEDIA IMETEULIWA KUWANIA TUZO ZA SKA2026 TUNAOMBA KURA YAKO WAWEZA KUPIGA KURA KIRAHISI KULIKO KUPITIA LINK HII

NAOMBA SANA SAPOTI YENU WADAU ZIMEBAKI SIKU 17 PEKEE KUENDELEA KUPIGA KURA KILA SIKU TUPIGE WOTE KWA MATUKIO DAIMA MEDIA🙏🙏🙏

Old Trafford Kitawaka leo! Man United na Man City Kukutana Kwenye Derby Kali

Global Publishers
September 13, 2026
72 views
0 Comments

Manchester United na Manchester City wanatarajiwa kukutana katika mchezo wa kusisimua wa Premier League leo Jumapili, Septemba 13, 2026, kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Mchezo huo ni derby ya 199 kati ya timu hizo mbili na utakuwa mtihani mkubwa kwa makocha Michael Carrick wa United na Enzo Maresca wa City.

Manchester City wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na mwanzo bora wa msimu, baada ya kushinda michezo yote mitatu ya Premier League, huku pia wakianza kampeni yao ya Champions League kwa ushindi dhidi ya Porto.

Erling Haaland naye anaonekana kuwa katika kiwango kizuri baada ya kufunga mabao mawili kwenye ushindi huo wa 2-0.

Kwa upande wa Manchester United, msimu umeanza kwa matokeo yasiyotabirika, ikiwemo kupoteza dhidi ya Hull City na sare ya 2-2 dhidi ya Everton.

Hata hivyo, ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Sabah katika Champions League unaweza kuwapa morali kuelekea derby hiyo, huku United wakitarajia kutumia faida ya kucheza mbele ya mashabiki wao Old Trafford.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa vita kubwa ya ufundi na nguvu, huku City wakitaka kuendeleza rekodi yao nzuri ya mwanzo wa msimu na United wakitafuta ushindi utakaowapa msukumo mpya.

Kwa historia na ushindani wa derby hii, dakika 90 za Old Trafford zinatarajiwa kuwa na presha kubwa kutoka mwanzo hadi mwisho.

Piga *150*53# kulipia Tshs. 40,000 tu tukupeleke COMPACT utazame mechi hii ndani ya 223 DSTV.

Stori na Mputa Ngaga | GPL

Video: Diamond na Zuchu Watikisa Kawe! Shughuli ya Mtoto Wao Yawa Gumzo

Global Publishers
September 13, 2026
6 views
0 Comments


Shughuli ya mtoto wa Diamond Platnumz na Zuchu imefanyika usiku wa kuamkia leo Jumapili Septemba 13, 2026 katika Ukumbi wa St. Laurent, Kawe jijini Dar es Salaam, huku hali ya furaha na shamrashamra ikitawala katika tukio hilo.

Tukio hilo limewakutanisha watu mbalimbali, wakiwemo wasanii, ndugu, marafiki na wageni waalikwa, ambao wamejitokeza kushiriki katika siku hiyo maalum.

Ukumbi wa St. Laurent umeonekana kupambwa kwa ajili ya shughuli hiyo, huku wageni wakifurahia pamoja na familia katika mazingira yaliyojaa furaha na bashasha.

Diamond na Zuchu, ambao ni miongoni mwa majina makubwa katika muziki wa Tanzania, wameendelea kuvuta hisia za mashabiki kila wanapoonekana pamoja katika matukio mbalimbali.

Kwa upande wa mashabiki, tukio hilo limekuwa gumzo mitandaoni, huku picha na video mbalimbali zisambaa kwenye mitandao zikionyesha namna shughuli hiyo inavyokwenda.

Mali Zenye Utata Zakamatwa Oysterbay! TRA na Polisi Wachunguza – Video

Global Publishers
September 13, 2026
12 views
0 Comments


Mwenyekiti wa Mtaa wa Oysterbay, Mololo Abel Mwaisumo, amesema upekuzi uliofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi umebaini kuwepo kwa mali za raia wa China zinazotiliwa shaka.

Mwaisumo amesema mali hizo zimekamatwa na mamlaka husika kwa ajili ya uchunguzi, huku akieleza kuwa bado haijafahamika kwa undani mali hizo zinahusishwa na kosa gani.

Amesema uchunguzi unaendelea ili kubaini aina ya mali zilizokamatwa, umiliki wake pamoja na mazingira yaliyopelekea kukamatwa kwake.

Mwenyekiti huyo amewataka wananchi na wasamaria wema kuendelea kutoa taarifa kwa mamlaka husika pale wanapobaini au kulihisi jambo lolote linaloweza kuwa na viashiria vya ukiukwaji wa sheria.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa wananchi kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa kwa wakati, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa baada ya uchunguzi kukamilika.