Global Publishers September 15, 2026 0 views 0 Comments
Peri-menopauzi, menopauzi na mabadiliko yanayohusishwa na andropauzi yanaweza kuathiri afya, mahusiano, kujiamini, tija na mazingira ya kazi. Pamoja na hayo, mada hizi bado hujadiliwa kwa siri, kwa aibu au wakati mwingine hazizungumzwi kabisa.
Ni wakati wa kubadilisha hilo.
Ungana nasi kwa jioni ya maarifa, mazungumzo ya wazi na suluhisho za vitendo, ukishirikiana na wanawake na wanaume, wataalamu wa afya, viongozi wa kampuni, wataalamu wa Rasilimali Watu (HR), wajasiriamali na wadau wa mabadiliko.
Kwa pamoja tutajadili namna ya:
🗣️ Kuvunja ukimya na kupinga dhana potofu.
💡 Kuongeza uelewa kuhusu peri-menopauzi, menopauzi na andropauzi.
🤝 Kujenga mazingira ya kazi yenye uelewa na msaada.
❤️ Kukuza afya, ustawi na mahusiano bora.
🌱 Kuandaa jamii kwa mtazamo chanya kuhusu kuzeeka kwa afya.
UELEWA. MAANDALIZI. MSAADA.
Tuvunje ukimya. Tubadilishe mtazamo wa mazungumzo. Tujenge mustakabali wenye afya bora, heshima na unaojumuisha kila mtu.
🚨 SHIRIKI KATIKA MAZUNGUMZO. SHIRIKI KATIKA MABADILIKO. 🚨
Dar es Salaam. Shahidi John Heche ameiambia mahakama kuwa Tundu Lissu hakuwahi kuwapa maelekezo ya namna ya kuzuia Uchaguzi Mkuu, kuhamasisha uasi au kufanya vitendo vya kuvuruga uchaguzi.
Heche ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na Wakili Katuga, katika sehemu ya mahojiano iliyolenga kuchunguza kauli na misimamo ya viongozi wa CHADEMA kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Akijibu swali la Katuga kama Lissu aliwaambia njia za kuzuia uchaguzi, Heche alisema: “Hakutuambia.”
Alipoulizwa kama Lissu aliwaambia njia za kuhamasisha uasi, shahidi huyo alijibu tena: “Hakutuambia.”
Aidha, alipoulizwa kama Lissu aliwahi kutaja njia ya kukinukisha, Heche alisema: “Hakusema.”
Hata hivyo, katika mahojiano hayo Heche alikiri kwamba alimsikia mwenyekiti wa chama akisema, “tutazuia uchaguzi.”
Pia alikiri kuwa mwenyekiti alisema “mahakamani hakuendeki” na kwamba polisi wanaingiza kura feki.
“No Reforms, No Election”
Kabla ya kufikia hoja hizo, Katuga alimuuliza Heche kama baada ya Lissu kukamatwa aliendeleza nia ya kuzuia uchaguzi.
Heche hakukubaliana na swali hilo, akisema alichokiendeleza kilikuwa msimamo wa “No Reforms, No Election.”
Alipoulizwa tena kama msimamo huo ulikuwa nia ya kuzuia uchaguzi, Heche alijibu:
“Hicho unachouliza siyo kweli.”
Katuga aliendelea kumkabili kuhusu kauli zinazodaiwa kutolewa kupitia vyombo vya habari kwamba uchaguzi wa 2025 hautafanyika.
Katika maswali hayo, Heche alisema mara kadhaa “sikumbuki”, ikiwemo alipoulizwa kuhusu mahojiano yake na East Africa Radio na kauli zinazodaiwa kutolewa kuhusu kutoshiriki uchaguzi na kutofanyika kwa uchaguzi.
Mahakama yakataa kusikiliza sauti
Wakati Katuga akiomba Heche akumbushwe kwa kutumia rekodi ya sauti ya mahojiano yake ya East Africa Radio, Lissu alipinga hatua hiyo na kurejea kifungu cha 177(1) na (2) cha Sheria ya Ushahidi.
Majaji, kwa mujibu wa mwenendo uliowasilishwa mahakamani, waliamua kwamba Heche akumbushwe bila kusikiliza sauti hiyo.
Baada ya kukumbushwa, Heche bado alisema hakumbuki baadhi ya kauli alizoulizwa.
Ushahidi kuhusu Oktoba 29
Katuga pia alimhoji Heche kuhusu hotuba ya Jaji Chande na matukio ya Oktoba 29.
Heche alisema anakumbuka kwamba katika hotuba hiyo ilielezwa kuwa matukio hayo yalipangwa na kuratibiwa, lakini alisema hakumbuki baadhi ya vipengele vingine alivyoulizwa.
Alikanusha kuwa anakumbuka kama alisema hotuba hiyo ilieleza kwamba fujo za Oktoba 29 zililenga kuzuia uchaguzi.
Aidha, hakukumbuka baadhi ya maelezo kuhusu idadi ya askari waliouawa.
Mkutano wa CHADEMA
Katika sehemu nyingine ya ushahidi, Heche alikiri kwamba alihudhuria mkutano wa CHADEMA ambapo mwenyekiti wa chama taifa alikuwa mzungumzaji mkuu.
Heche alisema naye alizungumza katika mkutano huo kwa muda wa takribani nusu saa, ingawa hakukumbuka kwa usahihi alichokizungumza.
Katuga alitaka kujua kama kulikuwa na hotuba rasmi iliyoandaliwa na mwenyekiti kwa ajili ya mkutano huo. Heche alisema hafahamu.
Pia alisema mikutano ya CHADEMA si yote huhifadhi kumbukumbu.
Hoja inayobaki mbele ya mahakama
Ushahidi wa Heche umeibua tofauti kati ya msimamo wa kisiasa wa “No Reforms, No Election” na madai kwamba kulikuwa na mpango au maelekezo ya moja kwa moja ya kuzuia uchaguzi.
Wakati Heche akikiri kusikia baadhi ya kauli kali kuhusu uchaguzi, amesisitiza kwamba Lissu hakuwahi kuwapa maelekezo ya namna ya kuzuia uchaguzi au kuhamasisha uasi.
Hivyo, mahojiano ya Katuga yanaendelea kulenga kubaini kama kauli na matendo yaliyotajwa mahakamani yanaonyesha msimamo wa kisiasa pekee au yanaweza kuhusishwa na madai ya njama ya kuzuia uchaguzi.
NANTERRE, UFARANSA — Mwanamuziki mashuhuri wa Canada, Céline Dion, amerejea jukwaani kwa kishindo baada ya zaidi ya miaka sita bila kufanya tamasha kamili, huku akiwavutia mashabiki si kwa sauti yake pekee bali pia kwa mwonekano wake uliopambwa kwa vito vya thamani kubwa.
Dion, mwenye umri wa miaka 58, alifanya onyesho lake la kwanza katika residency yake nchini Ufaransa Jumamosi, Septemba 12, katika Plenitude Arena, Nanterre. Tamasha hilo lilikuwa sehemu ya ratiba ya maonyesho 26 anayotarajiwa kufanya nchini humo.
Mwimbaji huyo wa hit song “My Heart Will Go On” alionekana akiwa amevalia gauni jeusi maalumu kutoka Dior, huku shingoni akiwa amevaa mkufu mkubwa wa almasi uliotengenezwa na kampuni ya vito ya Boucheron.
Mkufu huo, unaojulikana kama The Address, una almasi yenye uzito wa karati 10.1, pamoja na almasi nyingine za aina mbalimbali. Boucheron ilieleza kuwa utengenezaji wa mkufu huo ulichukua takribani saa 1,107.
Dion pia alivaa pete ya Fuzzy, the Leopard Cat, iliyotengenezwa kwa dhahabu na kupambwa kwa vito, ikiwa na jiwe la kijani la tourmaline lenye uzito wa karati 18.17.
Katika video zilizoonyeshwa wakati wa tamasha, Dion pia alionekana akiwa amevalia mkufu mwingine wa Boucheron uitwao Tattoo, uliotengenezwa kwa smoky quartz yenye uzito wa karati 580 na almasi adimu yenye uzito wa karati 1.74.
Kwa ujumla, mkusanyiko wa vito alivyovaa Dion ulifanya mwonekano wake kuwa miongoni mwa mambo yaliyozungumziwa zaidi katika usiku huo.
Hata hivyo, kilichogusa zaidi mashabiki ni hisia za Dion alipofungua tamasha hilo kwa wimbo “On Ne Change Pas.” Sekunde chache baada ya kuanza kuimba, alionekana kuzidiwa na hisia na kusimama huku akifuta machozi.
Baadaye aliweka mkono kifuani na kuunganisha mikono yake, ishara iliyotafsiriwa kama namna ya kuwashukuru mashabiki waliokuja kumuunga mkono.
Baada ya kuimba wimbo “Destin,” Dion alizungumza na mashabiki wake kwa Kifaransa na kisha kwa Kiingereza, akiwashukuru kwa kusafiri kutoka maeneo mbalimbali ya dunia ili kushuhudia kurejea kwake jukwaani.
Kurudi kwa Dion kunakuja baada ya kukumbwa na changamoto ya kiafya. Mnamo Desemba 2022, alitangaza kuwa alikuwa amegundulika kuwa na ugonjwa wa stiff-person syndrome, hali iliyomlazimisha kupunguza shughuli zake za muziki na kuahirisha baadhi ya maonyesho.
Kwa kurejea kwake jukwaani nchini Ufaransa, Dion ameanza ukurasa mpya wa kazi yake ya muziki huku mashabiki wakisubiri kuona maonyesho yake yanayofuata katika residency hiyo.
Mbali na kipaji chake cha muziki, usiku huo pia ulimweka kwenye uangalizi wa ulimwengu wa mitindo, kutokana na mchanganyiko wa gauni jeusi la Dior na vito vya Boucheron vyenye thamani na uzito mkubwa.
Uwanja wa ushindani umefunguliwa Meridianbet na safari ya kuwania mkwanja inaanza kupitia Expanse Cash Rush Challenge, mashindano yanayokuja na mfuko wa zawadi wenye thamani ya TZS 6,000,000. Kuanzia sasa hadi Septemba 22, 2026, wachezaji watakuwa na nafasi ya kuingia kwenye mbio hizi maalum huku wakilenga kujihakikishia nafasi miongoni mwa washindi 20 watakaotwaa zawadi.
Katika mashindano haya, Expanse imeandaa michezo 20 ya kusisimua ambayo itakuwa uwanjani kwa washiriki. Kwa dau la kuanzia TZS 1,000 pekee, kila mchezaji anapata nafasi ya kuanza safari yake bila kuhitaji dau kubwa. Hata hivyo, kadri changamoto inavyoendelea, ushindani unazidi kupanda na kila hatua inaweza kuwa muhimu katika kutengeneza nafasi nzuri kwenye mbio za zawadi.
Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Kipengele kinachofanya Cash Rush Challenge kuvutia zaidi ni kwamba jumla ya dau utakazocheza ndicho kipimo kinachokuweka kwenye mbio za ushindi. Hivyo, si suala la kuingia na kucheza mara moja, bali ni kushiriki kwenye mbio na kuacha jumla ya dau zako zifanye kazi katika safari ya kuelekea kileleni.
Kwa jumla ya TZS 6 milioni kwenye mfuko wa zawadi na nafasi kwa washindi 20, kila mshiriki ana sababu ya kuongeza umakini na kufuatilia mbio hadi siku ya mwisho. Kuanzia sasa hadi 22, Expanse Cash Rush inageuka kuwa uwanja wa ushindani ambao kila mchezaji anataka kuona jina lake likiwa miongoni mwa waliotamba zaidi.
Usiache mbio zipite pembeni yako ukiwa na Meridianbet. Chagua mchezo wako kati ya michezo 20 ya Expanse, anza kwa dau la kuanzia TZS 1,000, na shiriki katika Cash Rush Challenge. Milioni 6 zipo kwenye mfuko wa zawadi, washindi ni 20, na mbio tayari zimeanza.
Je unajua kuwa leo ndiyo ile siku ambayo unaweza ukaondoka na pesa za kutosha kutoka Meridianbet?. Mechi kibao za ushindi zipo kwaajili yako hivyo suka jamvi na ubashiri leo.
Kama kawaida kule Hispania, LALIGA itaendelea kutakuwa na mechi nyingi lakini hapa tutaangalia mechi ya Elche dhidi ya Real Madrid ambapo kila timu inahitaji ushindi wa pointi 3 ili kuendelea kujiweka sawa kwenye msimamo wa ligi kuu.
Elche mpaka sasa kwenye mechi tano ambazo amecheza ameambulia pointi 2 pekee huku wenyeji wao wakiondoka na ppointi 12 kwenye msimamo wa ligi baada ya kupata ushindi mnono kwenye mechi yao iliyopita. Nani kushinda leo?. Jisajili hapa.
Vijana hao wa Mourinho wanahitaji kupambania taji la ligi kuu ambalo hawajalipata kwa muda sasa huku wakiwa wamewekeza kwenye usajili wa wachezaji wenye uwezo mkubwa ambao kwa pamoja wanaweza kuisaidia timu kufika malengo yao.
Msimu uliopita kwenye mechi mbili za ligi walipokutana, Real aliondoka na pointi 4 ambapo mechi ya kwanza walitoa sare na ya pili wakashinda. Je leo hii nani unampa beti yako ya ushindi?. Suka jamvi hapa.
Pesa kubwa ipo kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno,Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Meridianbet wao wanampa nafasi ya ushindi Mourinho na vijana wake, lakini pia mechi hii imepewa machaguo zaidi ya 1000. Beti sasa.
Carabao Cup Raundi ya 3 kule Uingereza itaendelea ambapo mechi zipo kibao za kukufanya uwe mshindi kikosi cha Iraola Liverpool kitaumana dhidi ya Tottenham Spurs ambao wameanza msimu vibaya sana wakiwa hawajashinda mechi yoyote hadi sasa , lakini pia bila kufunga bao lolote.
Chini ya Iraola Liverpool bado inajitafuta kwani imekuwa haina matokeo ya kushawishi sana tena hawa baada ya kutoa suluhu kwenye mechi yao wakiwa Anfield. Hii ni mechi ambayo Jogoo anahitaji kushinda ili kuthibitisha kwa mashabiki zao kuwa mpia una matokeo matatu.
Spurs licha ya kufanya usajili mkubwa msimu huu timu bado haipati matokeo mzuri, ambapo De Zerbi sasa ana kibarua kizito cha kufanya kipindi ambacho bado mechi hazijachanganya.
Mara ya mwisho kukutana timu hizi mbili, walitoa sare huku nafasi kubwa ya kupata ushindi pale Meridianbet anapewa Liver. Je wewe unampa nani nafasi kubwa ya kupata ushindi?. Suka jamvi hapa.
Nao Ipswich watapepetana dhidi ya Arsenal ambao ni mabingwa watetezi wa ligi na vinara wa ligi hadi sasa huku nafasi ya kuondoka na mpunga ikiwa nje kabisa.
Hii nii mechi ambayo inakutanisha timu mbili zenye uwezo tofauti ambapo vijana wa Arteta wako kwenye kiwango bora sana si kwenye ligi tuu, bali kwenye mashindano yote ambapo wenyeji wao kwenye ligi hadi sasa wamekusanya pointi 6 kwenye mechi 4 huku wakiwa wameshinda mechi mbili na kupoteza mbili pia.
Kwa upande wa Arsenal wao wameshinda mechi zote nne ambazo wamecheza huku wakiwa wameruhusu bao moja hadi sasa, na ni moja ya timu ambazo zinasifika kwa kujilinda zaidi hivyo ni ngumu mpinzani kupata goli.
Global Publishers September 15, 2026 18 views 0 Comments
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameanza ziara nchini Hispania na kutembelea klabu ya FC Barcelona, ambako amekutana na Rais wa klabu hiyo, Joan Laporta.
Katika ziara hiyo, Makonda amefanya mazungumzo na viongozi wa Barcelona kuhusu fursa za ushirikiano katika maendeleo ya soka, kukuza vipaji, maendeleo ya kiufundi pamoja na maandalizi ya Tanzania kuelekea AFCON 2027.
Mazungumzo hayo pia yameangazia namna uzoefu na mfumo wa soka wa Barcelona unavyoweza kusaidia katika kuimarisha maendeleo ya mchezo wa soka nchini Tanzania.
Aidha, Makonda amemkabidhi Rais wa Barcelona, Joan Laporta, salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba wa mume wake, Marehemu Hafidh Ameir Hassan, pamoja na kumkabidhi barua ya rambirambi kwa ajili ya kumfikishia Rais Samia.
Makonda pia anatarajiwa kushuhudia mchezo wa FC Barcelona dhidi ya Racing Santander, utakaochezwa Jumatano, Septemba 16, 2026, katika uwanja wa Spotify Camp Nou.
Kwa kifupi: Ziara hiyo inalenga zaidi katika kujenga ushirikiano wa kimichezo kati ya Tanzania na FC Barcelona, hususan katika maendeleo ya vipaji na soka la Tanzania kuelekea AFCON 2027.
Global Publishers September 15, 2026 0 views 0 Comments
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameanza ziara nchini Hispania na kutembelea klabu ya FC Barcelona, ambako amekutana na Rais wa klabu hiyo, Joan Laporta.
Katika ziara hiyo, Makonda amefanya mazungumzo na viongozi wa Barcelona kuhusu fursa za ushirikiano katika maendeleo ya soka, kukuza vipaji, maendeleo ya kiufundi pamoja na maandalizi ya Tanzania kuelekea AFCON 2027.
Mazungumzo hayo pia yameangazia namna uzoefu na mfumo wa soka wa Barcelona unavyoweza kusaidia katika kuimarisha maendeleo ya mchezo wa soka nchini Tanzania.
Aidha, Makonda amemkabidhi Rais wa Barcelona, Joan Laporta, salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba wa mume wake, Marehemu Hafidh Ameir Hassan, pamoja na kumkabidhi barua ya rambirambi kwa ajili ya kumfikishia Rais Samia.
Makonda pia anatarajiwa kushuhudia mchezo wa FC Barcelona dhidi ya Racing Santander, utakaochezwa Jumatano, Septemba 16, 2026, katika uwanja wa Spotify Camp Nou.
Kwa kifupi: Ziara hiyo inalenga zaidi katika kujenga ushirikiano wa kimichezo kati ya Tanzania na FC Barcelona, hususan katika maendeleo ya vipaji na soka la Tanzania kuelekea AFCON 2027.
Watu wengi hawajui adhabu zinazotolewa na mahakama. Baadhi yao hujua adhabu mbili tu, kufungwa aukunyongwa kulingana na kosa la mtu alilolitenda. Kwa taarifa yako elewa kwamba kuna adhabu saba ambazo mahakama huruhusiwa na sharia kuzitoa, fuatilia hapa:
1. ADHABU YA KIFO (DEATH PENALTY) Adhabu hii hutolewa kwa wenye makosa makubwa kama kuua kwa kukusudia (murder). Kifungu cha 26 Kanuni za Adhabu kinasema kuwa mtu atakapohukumiwa adhabu ya kifo basi adhabu hiyo itatekelezwa kwa kunyongwa kwa kitanzi mpaka mtu huyo atakapokufa.
Baadhi ya nchi adhabu ya kifo hutekelezwa kwa kupigwa risasi na nyingine kudungwa sindano ya sumu. Sisi kwetu ni kitanzi/kamba shingoni kwa kuning’inizwa mpaka roho itoke. Pamoja na hayo, adhabu hii inapingwa sana na mashirika ya haki za binadamu pamoja na wanaharakati wengine duniani kote.
2. ADHABU YA KIFUNGO (IMPRISONMENT) Adhabu ya kifungo hutolewa kwa muda tofauti kutegemea na aina ya kosa alilotenda mtu. Yapo makosa watu hufungwa miaka saba, mwaka mmoja, miezi, mpaka thelathini lakini pia kipo kifungo cha maisha. Kifungo kimegawanyika mara mbili.
Kipo kifungo cha ndani na kipo cha nje. Kifungo cha ndani ni kifungo ambacho mtu anakuwa ndani ya uzio maalum ambao haruhusiwi kutoka huku ukihudumiwa na askari magereza. Hii huitwa jela (jail). Hataruhusiwa kutoka humo mpaka muda maalum uliosemwa na mahakama utakapoisha.
Aidha, kifungu cha nje wakati mwingine huitwa kifungo cha masharti. Ni kifungo ambacho mtuhumiwa hazuiliwi katika jela isipokuwa atapewa masharti kadhaa atakayotakiwa kutekeleza akiwa nje ya jela.
Anaweza kuwa anaishi nyumbani kwake lakini kwa sharti la kuripoti sehemu fulani kila siku au vinginevyo, anaweza kuzuiwa kusafiri nje ya mkoa wilaya au vinginevyo, anaweza kupewa sharti la kutotenda kosa ndani ya mwaka, miaka au vinginevyo n.k. Kubwa hapa ni kuwa kifungo hiki mtu anakuwa nje lakini kwa masharti maalum kama vile kufanya kazi za kijamii kama mahakama itakavyoona.
3. ADHABU YA KUCHAPWA VIBOKO (CORPORAL PUNISHMENT) Hakimu au jaji anaweza, kwa mamlaka aliyonayo, kuamuru mtuhumiwa kuchapwa bakora. Adhabu hii inaweza kutolewa ikiwa kama adhabu inayojitegemea au kama nyongeza baada ya adhabu nyingine. Maana yake ni kuwa unaweza kuhukumiwa kifungo na viboko au viboko pekee na huchapwa na askari wa jeshi la magereza baada ya kupimwa na daktari kuthibitisha afya yake.
4. ADHABU YA FAINI (FINE) Hii nayo inaweza kuwa adhabu inayojitegemea au inayotumika kama adhabu ya nyongeza baada ya kuwa imetolewa adhabu nyingine. Faini huhusisha malipo ya fedha ambayo yatalipwa kwa utaratibu maalum utakaowekwa na Mahakama.
5. ADHABU YA KUNYANG’ANYWA MALI (FORFEITURE) Mahakama inaweza kuamuru mali ya mtuhumiwa kunyang’anywa baada ya kupatikana na hatia. Mali kunyang’anywa ni sehemu ya adhabu. Mara nyingi mali zinazonyang’anywa ni zile zilizotumika katika uhalifu. Gari au pikipiki kutumika katika wizi ambao umethibitishwa inaweza kunyang’anywa. Hii ni pamoja na mali nyingine kama nyumba, meli, n.k. Mara nyingi adhabu hii hutolewa kwa wale wanaopatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya au kuzihifadhi majumbani.
6. ADHABU YA KULIPA FIDIA (COMPENSATION) Fidia ni tofauti na faini. Fidia ni kulipia kile ulichoharibu, kupoteza au hasara uliyosababisha. Fidia ni mpaka kiwepo kitu kilichosababisha hasara, upotevu, au uharibifu. Pesa inayolipwa kufidia hasara, uharibifu ndiyo inayoitwa fidia. Aidha, faini hulipwa bila kuhitaji kuwepo kitu kilichoharibika au kusababishiwa hasara.
7. ADHABU YA KUTUNZA AMANI NA KUWA NA TABIA NJEMA (PEACE KEEPING & BE OF GOOD BEHAVIOUR) Mara nyingi adhabu hii hutolewa kwa wenye makosa madogo madogo. Hatutarajii mtu aibe, aue au abake halafu adhabu yake iwe kuhakikisha anatunza amani na kuwa na tabia njema mtaani. Ifahamike kuwa adhabu hii hutekelezwa mtu akiwa nje. Ni sawa na kifungo cha nje kwa sharti la kutunza amani na kuwa mtu mwema mtaani. Endapo mtu huyu atatenda kosa jingine katika kipindi hiki cha uangalizi basi atapewa adhabu nyingine kubwa zaidi.
Matthew Rhys ameshinda tuzo ya mwigizaji bora wa kiume katika tamthilia ya vichekesho.
LOS ANGELES — Tamasha la 78 la Tuzo za Emmy limefanyika Jumatatu, Septemba 14, 2026, katika ukumbi wa Peacock Theater mjini Los Angeles, huku vipindi vya televisheni ‘Widow’s Bay’ na ‘The Pitt’ vikiwa miongoni mwa vilivyoibuka na ushindi mkubwa.
Sherehe hizo ziliongozwa na mwigizaji Mariska Hargitay na kurushwa moja kwa moja kupitia NBC na Peacock, zikihudhuriwa na baadhi ya majina makubwa katika tasnia ya televisheni.
‘Widow’s Bay’ ilitwaa tuzo ya Outstanding Comedy Series, huku Matthew Rhys akishinda tuzo ya mwigizaji bora wa kiume katika tamthilia ya vichekesho. Stephen Root naye alishinda tuzo ya mwigizaji msaidizi bora wa kiume, huku Kate O’Flynn akitwaa tuzo ya mwigizaji msaidizi bora wa kike.
Kipindi hicho pia kilishinda tuzo za uandishi bora na uongozi bora (directing) katika kitengo cha comedy, na kukifanya kuwa miongoni mwa washindi wakubwa wa usiku huo.
Kwa upande mwingine, ‘The Pitt’ ilitwaa tuzo ya juu ya Outstanding Drama Series. Noah Wyle alishinda tuzo ya mwigizaji bora wa kiume katika drama kwa nafasi yake katika kipindi hicho.
‘The Pitt’ pia ilipata uteuzi kadhaa katika vitengo vya waigizaji wasaidizi, huku ushindani mkubwa ukiwa miongoni mwa waigizaji wake.
Katika tuzo nyingine za drama, Rhea Seehorn alishinda Outstanding Lead Actress in a Drama Series kwa ‘Pluribus’, wakati Tom Pelphrey alitwaa tuzo ya mwigizaji msaidizi bora wa kiume kwa ‘Task’. Allison Janney naye alishinda tuzo ya mwigizaji msaidizi bora wa kike kwa ‘The Diplomat’.
Rhea Seehorn ameshinda Outstanding Lead Actress in a Drama Series kwa ‘Pluribus
Vince Gilligan alipewa tuzo ya uandishi bora wa drama kwa kipindi cha ‘Pluribus’, huku Saul Metzstein akishinda tuzo ya directing bora kwa ‘Slow Horses’.
Katika kitengo cha tamthilia maalum, ‘DTF St. Louis’ ilitwaa tuzo ya Outstanding Limited or Anthology Series. Matthew Rhys aliongeza ushindi mwingine kwa kutwaa tuzo ya mwigizaji bora wa kiume katika limited series au movie kwa ‘The Beast in Me’.
Sally Field naye alishinda tuzo ya mwigizaji bora wa kike katika kitengo hicho kwa ‘Remarkably Bright Creatures’.
Kwa upande wa vipindi vya mashindano ya uhalisia, ‘The Traitors’ ilitwaa tuzo ya Outstanding Reality Competition Program, ikiwashinda ‘Dancing with the Stars’, ‘RuPaul’s Drag Race’, ‘Survivor’ na ‘Top Chef’.
Sally Field naye ameshinda tuzo ya mwigizaji bora wa kike katika kitengo hicho kwa ‘Remarkably Bright Creatures’.
Katika kitengo cha variety series, ‘The Late Show with Stephen Colbert’ iliibuka mshindi, ikishinda programu zilizokuwa zikichuana nazo kama ‘The Daily Show’, ‘Jimmy Kimmel Live!’, ‘Last Week Tonight with John Oliver’ na ‘Saturday Night Live’.
Tuzo hizo za Emmy za mwaka huu zilifuatia Creative Arts Emmys zilizotolewa Septemba 5 na 6, ambapo washindi wengine akiwemo Shailene Woodley, David Harbour, Linda Cardellini, Betty Gilpin na marehemu Rob Reiner walitambuliwa.
Mariska Hargitay, ambaye alikuwa mwenyeji wa sherehe kuu za mwaka huu, pia alikuwa miongoni mwa washindi baada ya kutwaa tuzo mbili za Emmy kwa filamu yake ya maandishi ‘My Mom Jayne’.
Kwa ujumla, usiku wa Emmy 2026 uliendelea kuonyesha ushindani mkubwa katika televisheni, huku ‘Widow’s Bay’ ikitawala upande wa comedy na ‘The Pitt’ ikifanya vizuri katika upande wa drama.
Outstanding Comedy Series
Abbott Elementary The Bear Hacks Margo’s Got Money Troubles Nobody Wants This Only Murders in the Building Shrinking Widow’s Bay – WINNER
Outstanding Lead Actor in a Comedy Series
Yahya Abdul-Mateen II – Wonder Man Steve Carell – Rooster Matthew Rhys – Widow’s Bay – WINNER Jason Segel – Shrinking Martin Short – Only Murders in the Building
Outstanding Lead Actress in a Comedy Series
Quinta Brunson – Abbott Elementary Ayo Edebiri – The Bear Elle Fanning – Margo’s Got Money Troubles Lisa Kudrow – The Comeback Jean Smart – Hacks – WINNER
Outstanding Supporting Actor in a Comedy Series
Colman Domingo – The Four Seasons Paul W. Downs – Hacks Harrison Ford – Shrinking Nick Offerman – Margo’s Got Money Troubles Stephen Root – Widow’s Bay – WINNER Michael Urie – Shrinking Tyler James Williams – Abbott Elementary
Outstanding Supporting Actress in a Comedy Series
Dale Dickey – Widow’s Bay Hannah Einbinder – Hacks Janelle James – Abbott Elementary Kate O’Flynn – Widow’s Bay – WINNER Michelle Pfeiffer – Margo’s Got Money Troubles Megan Stalter – Hacks Jessica Williams – Shrinking
Outstanding Writing for a Comedy Series
Abbott Elementary, “Team Building” – Quinta Brunson The Chair Company, “Life Goes by Too F**king Fast, It Really Does” – Tim Robinson, Zach Kanin The Comeback, “Valerie Does It All” – Michael Patrick King, Lisa Kudrow Hacks, “Hacks (Finale)” – Lucia Aniello, Paul W. Downs, Jen Statsky Jury Duty Presents: Company Retreat, “Mergers and Acquisitions” – Anthony King Widow’s Bay, “Welcome to Widow’s Bay!” – Katie Dippold – WINNER
Outstanding Directing for a Comedy Series
Abbott Elementary, “Ballgame” – Randall Einhorn The Bear, “Bears” – Christopher Storer The Chair Company, “Life Goes by Too F**king Fast, It Really Does.” – Andrew DeYoung Hacks, “Hacks (Finale)” – Lucia Aniello The Ms. Pat Show, “Give It Arrest” – Mary Lou Belli Widow’s Bay, “Welcome to Widow’s Bay!” – Hiro Murai – WINNER
Outstanding Lead Actor in a Drama Series
Sterling K. Brown – Paradise Gary Oldman – Slow Horses Mark Ruffalo – Task Rufus Sewell – The Diplomat Noah Wyle – The Pitt – WINNER
Outstanding Lead Actress in a Drama Series
Carrie Coon – The Gilded Age Chase Infiniti – The Testaments Keri Russell – The Diplomat Rhea Seehorn – Pluribus – WINNER Zendaya – Euphoria
Outstanding Supporting Actor in a Drama Series
Patrick Ball – The Pitt Billy Crudup – The Morning Show Shawn Hatosy – The Pitt Gerran Howell – The Pitt Jack Lowden – Slow Horses Tom Pelphrey – Task – WINNER Carlos-Manuel Vesga – Pluribus
Outstanding Supporting Actress in a Drama Series
Taylor Dearden – The Pitt Fiona Dourif – The Pitt Allison Janney – The Diplomat – WINNER Katherine LaNasa – The Pitt Sepideh Moafi – The Pitt Julianne Nicholson – Paradise Karolina Wydra – Pluribus
Outstanding Writing for a Drama Series
The Diplomat, “Amagansett” – Peter Ackerman, Debora Cahn The Pitt, “1:00 P.M.” – Kirsten Pierre-Geyfman, R. Scott Gemmill The Pitt, “12:00 P.M.” – Valerie Chu Pluribus, “We Is Us” – Vince Gilligan – WINNER Slow Horses, “Scars” – Will Smith Task, “A Still Small Voice” – Brad Ingelsby
Outstanding Directing for a Drama Series
The Gilded Age, “My Mind Is Made Up” – Salli Richardson Whitfield Paradise, “Exodus” – Hanelle M. Culpepper The Pitt, “12:00 P.M.” – Noah Wyle Pluribus, “We Is Us” – Vince Gilligan Slow Horses, “Scars” – Saul Metzstein – WINNER Task, “Out Beyond Ideas of Wrongdoing and Rightdoing, There Is a River.” – Salli Richardson Whitfield
Outstanding Limited or Anthology Series
All Her Fault The Beast in Me Beef DTF St. Louis – WINNER Love Story: John F. Kennedy Jr. and Carolyn Bessette
Outstanding Lead Actor in a Limited or Anthology Series or Movie
Riz Ahmed – Bait Jason Bateman – Black Rabbit Charlie Hunnam – Monster: The Ed Gein Story Oscar Isaac – Beef Matthew Rhys – The Beast in Me – WINNER
Outstanding Lead Actress in a Limited or Anthology Series or Movie
Claire Danes – The Beast in Me Sally Field – Remarkably Bright Creatures – WINNER Carey Mulligan – Beef Sarah Pidgeon – Love Story: John F. Kennedy Jr. & Carolyn Bessette Sarah Snook – All Her Fault
Outstanding Reality Competition Program
Dancing with the Stars RuPaul’s Drag Race Survivor Top Chef The Traitors – WINNER
Outstanding Variety Series
The Daily Show Jimmy Kimmel Live! Last Week Tonight with John Oliver The Late Show with Stephen Colbert – WINNER Saturday Night Live
MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA
MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)
1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA
2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM
3:TUZO YA AFYA
4:TUZO YA MPIGA PICHA
AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .