Mchora Katuni Kinyagulo Tuzo ‘King Kinya’ Afariki Dunia Morogoro

Global Publishers
September 17, 2026
0 views
0 Comments

Mchora katuni maarufu nchini, Kinyagulo Tuzo almaarufu King Kinya, amefariki dunia leo, Septemba 17, 2026 baada ya kuugua kwa kipindi kifupi.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rasilimali Watu ya Kampuni ya MCL aliyokuwa akiifanyia kazi kama mchora katuni wa magazeti, imethibitisha taarifa za kifo cha King Kinya.

Kaka wa marehemu, Kiondo Mjema, amenukuliwa akisema King Kinya alianza kuugua akiwa nyumbani Tabata mwanzoni mwa Julai, 2026 hali iliyomfanya kukaa ndani kwa muda kabla ya kupelekwa Morogoro.

Amesema akiwa Morogoro hali yake ilizidi kuwa mbaya na baadaye alipelekwa hospitalini, ambako alilazwa kwa takriban wiki moja kabla ya kuruhusiwa kurejea nyumbani.

“Alipotoka hospitali aliambiwa arudi tena kwa ajili ya ufuatiliaji. Juzi alirudi hospitalini baada ya kusumbuliwa na tumbo, kuharisha na kutapika, akapewa dawa na kuruhusiwa kurudi nyumbani,” amesema.

Kwa mujibu wa Kiondo, hali ya marehemu ilizidi kuwa mbaya usiku wa kuamkia jana Septemba 15, 2026, akilalamikia maumivu makali ya tumbo na kichwa pamoja na kutapika na kuharisha, ambapo alifariki dunia.

Kiondo amesema msiba upo Kimara Kona na mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa Septemba 18, 2026 saa 10 jioni katika makaburi ya Mwananyamala.

MADEREVA WMA WASHIRIKI KONGAMANO LA CHAMA CHAO KITAIFA

🔶 *WAAHIDI UTENDAJI MAHIRI ZAIDI* 

*Na WMA  – DODOMA.* 

Baadhi ya madereva kutoka Wakala wa Vipimo (WMA) wanashiriki Kongamano la Tano la Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania (MST-TGDU) linaloendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Kongamano hilo la kitaifa lililoanza Septemba 12 limewakutanisha mamia ya madereva wa Serikali kutoka mikoa yote nchini, ambapo pamoja na mambo mengine wanajadili mustakabali wa taaluma yao, changamoto wanazokutana nazo barabarani na namna ya kuimarisha nidhamu na weledi kazini.

Kwa mujibu wa waandaaji, kongamano hili ni zaidi ya mkutano wa kawaida; ni darasa huru la kubadilishana uzoefu, kujifunza mbinu mpya za uendeshaji salama, matunzo ya vyombo vya moto vya Serikali na umuhimu wa uwajibikaji katika kulinda mali za umma.

Akizungumza kwa niaba ya madereva wa WMA, Dereva Mkuu kutoka WMA Mkoa wa Dodoma, Bw. John Jumbe amesema ushiriki wao umewapa fursa ya kipekee kujifunza na kuona thamani ya taaluma yao.

 “Tumefurahi sana kushiriki kongamano hili. Tumebadilishana uzoefu na wenzetu kutoka taasisi nyingine na tumejifunza mengi kuhusu uwajibikaji, usalama barabarani na namna ya kuwa mabalozi wazuri wa WMA na Serikali kwa ujumla. Tutaenda kuyafanyia kazi tuliyojifunza,” amesema Bw. Mhando.

Ushiriki wa WMA katika kongamano hilo unaakisi dhamira ya Wakala inayoongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Bw. Alban Mark Kihulla, ya kuendelea kuwawezesha watumishi wake katika ngazi zote ili kuhakikisha wanatoa huduma bora na yenye tija kwa wananchi.

 

Kaulimbiu ya Kongamano hilo linalotarajiwa kuhitimishwa Septemba 19, 2026 ni ‘Dereva wa Serikali, Nguvu Moja, Sauti Moja, Kulinda Amani ya Nchi ni Jukumu letu pia.’

 

WIZARA NA BRELA ZAFANYA TATHMINI YA KATAZO LA BIASHARA 15 KWA WAGENI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhe. Balozi Waziri Rajab Salum, leo tarehe 16 Septemba 2026 amefanya kikao kazi na taasisi wezeshi kwa biashara ikiwemo BRELA, TISEZA, TANTRADE, FCC, TPA, TASAC, Idara ya Uhamiaji, Idara ya Kazi na Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Uchukuzi pamoja na Halmashauri za Dar es Salaam na Mwanza kwa lengo la kujadili na kufanya maboresho katika utekelezaji wa katazo la biashara 15 ambazo haziruhusiwi kwa wageni nchini.

Akizungumza katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Balozi Waziri alisema hatua hiyo imekuja kufuatia maoni na malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali, hivyo Wizara imeona umuhimu wa kuyafanyia tathmini ili kubaini maeneo yanayohitaji maboresho na kuhakikisha utekelezaji unazingatia malengo yaliyokusudiwa.

Mhe. Balozi Waziri alisema mapendekezo ya kikao na tathmini itawasilishwa kwa Waziri wa Viwanda na Biashara kwa hatua zaidi za na kutoa mwelekeo wa utekelezaji wake huku akisisitiza kuwa Serikali, kupitia Wizara inalenga kulinda na kuimarisha sekta ya biashara nchini kwa kuweka misingi imara ya kiuchumi na kujenga mazingira wezeshi yatakayowawezesha Watanzania kunufaika na fursa za biashara

Aidha, Balozi Waziri alisisitiza umuhimu wa kuzingatia utu katika utekelezaji wa katazo hilo, akibainisha kuwa pamoja na wajibu wa Serikali kusimamia na kutekeleza sheria, utekelezaji wake unapaswa kufanyika kwa kuzingatia utu na kuepusha usumbufu usio wa lazima kwa wahusika.

Baada ya kukamilika kwa tathmini na majadiliano, kikao hicho kilifikia hatua ya kupitisha mapendekezo yaliyofanyiwa maboresho, ambayo sasa yanawasilishwa kwa Waziri wa Viwanda na Biashara kwa ajili ya kutoa mwelekeo wa mwisho kuhusu hatua zinazofuata katika utekelezaji wa katazo hilo.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa utekelezaji wa katazo la biashara 15 unakwenda sambamba na sera, sheria na taratibu za Serikali, huku ukizingatia maslahi ya Taifa na mazingira wezeshi kwa Watanzania kushiriki kikamilifu katika shughuli za biashara.

 

KUPIGA KURA ZA SAMIA KALAMU AWARDS 2026 KWA MATUKIO DAIMA PEKEE INGIA HAPA

 

MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA 

 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)

1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

3:TUZO YA AFYA

 

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .

TANZANIA NA UJERUMANI ZAJADILI FURSA ZA UWEKEZAJI NA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. James Millya (Mb.), amekutana na ujumbe wa ujumbe wa Serikali na wafanyabiashara 30 waandamizi kutoka Ujerumani ulioongozwa na Waziri  wa Masuala ya Shirikisho, Ulaya na Kimataifa Mhe. Manfred Pentz. Mkutano huo uliofanyika Septemba 16, 2026 katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam ulilenga kujadili fursa za uwekezaji na kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania, Ujerumani na ukanda wa Afrika Mashariki.

Akizungumza katika majadiliano hayo, Waziri Manfred Pentz amebainisha kuwa Ujerumani inaona fursa kubwa za kiuchumi nchini Tanzania na katika ukanda huo, hususan kwenye maeneo ya uhamishaji wa teknolojia, ubunifu na upatikanaji wa masoko. Hata hivyo, alisisitiza umuhimu wa kutatua changamoto za kodi, sera, vikwazo visivyo vya kikodi na miundombinu ili kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.

Kwa upande wake, Mhe. Millya amethibitisha utayari wa Tanzania kushirikiana na wawekezaji kutoka Ujerumani, akieleza kuwa nchi ina utulivu mkubwa wa kisiasa na fursa lukuki. Amebainisha kuwa sekta za kimkakati zinazotoa fursa hizo ni pamoja na sekta ya madini, utalii, mazingira na rasilimali za asili, ambazo zipo tayari kupokea mitaji na ushirikiano mpya.

Naye Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Annett Günther amesisitiza haja ya kuhamisha ushirikiano huo kutoka kwenye majadiliano kwenda kwenye utekelezaji wa vitendo wa miradi ya maendeleo. Ameongeza kuwa jukwaa la Invest East Africa Forum litatumika kama fursa muhimu ya kupokea na kushughulikia kwa pamoja changamoto mbalimbali zinazowakabili wawekezaji wanaoingia katika ukanda huo.

Ushirikiano kati ya pande hizo mbili unazidi kupanuka katika sekta za kisasa, ikiwemo teknolojia ya Akili Bandia (AI), kufuatia kusainiwa kwa Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya Ujerumani na Afrika Mashariki. Mkataba huo unalenga kusaidia ujumuishaji, uwezeshaji na ukuaji wa teknolojia ya AI ili kuchochea maendeleo endelevu ya kiuchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

 

Chanuo Nchakali Afunguka Kiki ya Ndoa na YJ Kiboko – Video

Global Publishers
September 17, 2026
1,338 views
0 Comments

Msanii wa filamu Bongo, Chanuo Nchakali, amefunguka kuhusu sakata la kiki ya ndoa kati yake na msanii wa Bongofleva, YJ Kiboko, akieleza namna suala hilo lilivyomtokea puani na kumfanya ashambuliwe vikali na mashabiki.

Chanuo amesema kiki hiyo ilisababisha mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki, huku baadhi yao wakimshambulia kwa maneno kutokana na kuamini kuwa uhusiano huo ulikuwa wa kweli.

Msanii huyo ameeleza kwa undani kilichotokea na namna alivyokabiliana na presha kutoka kwa mashabiki baada ya taarifa hizo kusambaa.

Jinsi ya Kusikia Sauti Halisi ya Video za YouTube Badala ya Tafsiri ya AI

Global Publishers
September 17, 2026
1,866 views
0 Comments

YouTube imeanza kutumia teknolojia ya kutafsiri sauti kwa kutumia Akili Bandia (AI Dubbing) kwenye baadhi ya video, hali inayowafanya baadhi ya watazamaji kusikia sauti iliyotafsiriwa badala ya sauti halisi ya mtengenezaji wa maudhui.

Ikiwa unataka kusikia sauti ya asili ya video, unaweza kufanya hatua zifuatazo:

  1. Fungua video unayotaka kutazama kwenye YouTube.
  2. Bofya alama ya Mipangilio (Settings) yenye umbo la gia (⚙️).
  3. Chagua Audio Track (Njia ya Sauti), ikiwa chaguo hilo linapatikana.
  4. Badili kutoka lugha iliyotafsiriwa kwenda Original au lugha ya awali ya video.

Baada ya kufanya mabadiliko hayo, video itaanza kucheza kwa sauti halisi iliyorekodiwa na mtayarishaji wa maudhui.

Hata hivyo, si video zote zina chaguo la kubadili sauti. Endapo huoni kipengele cha Audio Track, ina maana mtengenezaji wa video hajawasha huduma hiyo au video hiyo inapatikana katika toleo moja tu la sauti.

Huduma ya AI Dubbing inalenga kuwafikia watazamaji wa lugha mbalimbali, lakini YouTube bado inatoa uwezekano wa kurejea kwenye sauti ya awali pale ambapo mtayarishaji amewezesha chaguo hilo.

Fahamu Safari ya Louis Vuitton, Kijana Maskini wa Kijijini Aliyejenga Chapa Yenye Thamani Kubwa Duniani

Louis Vuitton alikuwa mmoja wa watu muhimu katika historia ya mitindo ya kifahari duniani. Jina lake limeendelea kuwa alama ya ubora kupitia kampuni ya Louis Vuitton inayojulikana kwa mabegi, mikoba, nguo, viatu na bidhaa za kifahari.

Kuzaliwa na Utoto

Louis Vuitton alizaliwa tarehe 4 Agosti 1821 katika kijiji cha Anchay, Jura, Ufaransa. Alizaliwa katika familia ya kawaida; baba yake, Xavier Vuitton, alikuwa mkulima na mtengenezaji wa masanduku, huku mama yake, Corinne Gaillard, akiwa mshonaji wa kofia na mfanyakazi wa mikono.

Maisha yake ya utotoni yalikuwa magumu. Baada ya mama yake kufariki akiwa bado mdogo na baadaye kumpoteza baba yake, Louis akiwa na umri wa takribani miaka 13 aliamua kuondoka nyumbani na kuanza safari ya kutafuta maisha bora.

Kijiji cha Anchay, Jura, Ufaransa alipozaliwa Louis Vuitton alizaliwa tarehe 4 Agosti 1821.

Safari ya Kuelekea Paris

Akiwa kijana, Louis alitembea kwa miguu zaidi ya kilomita 400 kutoka kijijini kwao hadi Paris, safari iliyochukua muda mrefu. Alipofika Paris mwaka 1837 akiwa na umri wa miaka 16, alianza kufanya kazi kama mwanafunzi wa fundi wa kutengeneza masanduku (box maker) chini ya fundi maarufu Monsieur Maréchal.

Wakati huo, kutengeneza masanduku ilikuwa kazi ya kifahari kwa sababu matajiri walihitaji maboksi maalumu kwa ajili ya kuhifadhi na kusafirisha nguo, vito na vitu vya thamani wanaposafiri.

Kuanzishwa kwa Louis Vuitton

Baada ya miaka mingi ya kujifunza na kuboresha ujuzi wake, Louis Vuitton alifungua biashara yake mwenyewe mwaka 1854 mjini Paris.

Alimuoa Clémence-Émilie Parriaux mwaka 1854, na walipata mtoto mmoja aitwaye Georges Ferréol Vuitton.

Alianzisha duka lake katika eneo la Rue Neuve-des-Capucines, karibu na Place Vendôme, likiwa miongoni mwa maeneo ya kifahari Paris.

Ubunifu wake mkubwa ulikuwa kutengeneza masanduku ya kusafiria yenye:

  • Muundo mwepesi lakini imara
  • Uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu
  • Umbo bapa juu ili yaweze kupangwa vizuri kwenye usafiri
  • Ubora wa hali ya juu kuliko masanduku ya kawaida yaliyokuwa na umbo la duara

Ubunifu huo ulifanya bidhaa zake kupendwa na wafalme, matajiri na wasafiri mashuhuri.

Mafanikio Makubwa

Louis Vuitton alijenga sifa kubwa kutokana na ubunifu na ubora wa bidhaa zake. Miongoni mwa mafanikio yake ni:

1. Kuwa mtengeneza masanduku wa familia za kifalme

Alipata umaarufu baada ya kuwa mtengeneza masanduku anayependwa na watu wa tabaka la juu nchini Ufaransa, akiwemo malkia wa Ufaransa Eugénie de Montijo.

2. Ubunifu wa turubai maalumu

Kampuni yake ilianza kutumia vifaa maalumu vya kufunika maboksi yake, vilivyosaidia kutambulika na kuwa vigumu kuigwa.

3. Kuanzisha urithi wa kifahari

Baada ya kifo chake, familia yake iliendeleza biashara hiyo na kuifanya kuwa moja ya chapa kubwa zaidi za mitindo duniani.

Kifo Chake

Louis Vuitton alifariki dunia tarehe 27 Februari 1892 akiwa na umri wa miaka 70. Aliacha kampuni iliyokuwa imeanza kuwa na jina kubwa katika sekta ya bidhaa za kifahari.

Urithi wa Louis Vuitton Leo

Leo hii, jina la Louis Vuitton linawakilisha:

  • Ubora wa hali ya juu
  • Ubunifu wa kifahari
  • Hadhi na mafanikio
  • Chapa yenye thamani kubwa duniani

Kampuni yake imeendelea kukua na kuwa sehemu ya kundi kubwa la bidhaa za kifahari duniani, ikitengeneza bidhaa zinazotumiwa na watu maarufu, wafanyabiashara wakubwa na wapenzi wa mitindo kote duniani.

Kutoka kijana aliyekimbia maisha magumu kijijini hadi kuunda moja ya chapa maarufu zaidi duniani, safari ya Louis Vuitton ni mfano wa ubunifu, uvumilivu na kujenga thamani kupitia ujuzi.

Mpigie Kura Godmuya, Kura Yako Ni Ushindi! – Tuzo za Samia Kalamu Awards 2026

Global Publishers
September 17, 2026
2,226 views
0 Comments

Mtangazaji wa @globaltvonline na @255globalradio, Godfrey Nathan @godmuya ameteuliwa kuwania tuzo za Samia Kalamu Awards 2026.

Sasa Godmuya anaomba support yako, mfuatiliaji wa Global TV, kwa kumpigia kura ili kufanikisha ushindi wake.

🗳️ MPIGIE KURA: GODFREY LUHILABAKE NATHAN
🔢 Kodi: 260246

Kura yako ni mchango mkubwa kwa Godmuya katika safari hii ya tuzo.

🙏 Piga kura, share na mwambie mwingine apige kura!