Meridianbet Yaja na Zawadi za Samsung Galaxy A26 kwa Washindi Watatu

Global Publishers
September 16, 2026
0 views
0 Comments

Mashabiki wa michezo, Meridianbet imeleta sababu nyingine ya kuongeza msisimko kwenye burudani yako. Safari hii zawadi ni simu tatu mpya kabisa za Samsung Galaxy A26, ambazo zitatua mikononi mwa washindi watatu watakaopatikana kupitia promosheni maalum. Kwa mchezaji anayependa soka, michezo mbalimbali au kasino, hii ni fursa ya kuburudika huku ukijiweka kwenye nafasi ya kushinda zawadi.

Ili kuingia kwenye kinyang’anyiro, wachezaji wanapaswa kuwa na akaunti ya Meridianbet na kushiriki kupitia tovuti au App kwa kuzingatia masharti ya promosheni. Hivyo, kama ulikuwa tayari unaendelea na shughuli zako za kubashiri, au michezo ya kasino sasa kuna sababu nyingine ya kuifanya safari yako iwe na msisimko zaidi.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kitu cha kuvutia zaidi ni kwamba promosheni hii haijawekwa kwa kundi moja pekee la wachezaji. Wanaopenda kubashiri michezo na wale wanaofurahia kasino wote wanaweza kushiriki, mradi tu wafuate masharti yaliyowekwa. Mwisho wa promosheni, majina ya washiriki wanaokidhi vigezo yataingia kwenye droo, huku washindi watatu wakipata Samsung Galaxy A26 mpya kabisa.

Lakini kabla ya kuanza kuota kuhusu simu mpya mfukoni, kuna masharti muhimu ya kuzingatia. Kila mtumiaji anaruhusiwa nafasi moja pekee kwa kila anuani, huku dau za Turbocash na System Ticket zikiwa nje ya promosheni hii. Kwa hiyo, hakikisha kila hatua unayochukua inafuata masharti ili usikose nafasi yako kwenye kinyang’anyiro cha zawadi.

Hatua inayofuata iko mikononi mwako. Jisajili au ingia Meridianbet, endelea kufurahia michezo yako pendwa na jiweke kwenye nafasi ya kuwania mojawapo ya Samsung Galaxy A26 tatu. Washindi watakuwa watatu, lakini nafasi ya kuwa mmoja wao inaanza na wewe kushiriki kwa usahihi.

Deportivo La Coruna Dhidi ya Sevilla, Nani kubeba pointi Tatu?

Deportivo La Coruña itakuwa mwenyeji wa Sevilla katika mchezo wa LaLiga utakaopigwa leo Jumatano, Septemba 16, kwenye Uwanja wa Abanca-Riazor. Kuanzia majira ya saa 20:00 usiku, ukiwa ni mchezo wa raundi ya 6 ya La Liga msimu huu.

Deportivo inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na mwanzo mzuri tangu waliporejea LaLiga, ikiwa bado haijapoteza katika michezo yake ya mwanzo. Kikosi hicho cha Antonio Hidalgo kimeonyesha ushindani mkubwa, huku Pierre-Emerick Aubameyang akiwa mmoja wa wachezaji wanaoleta tofauti baada ya kuanza msimu kwa kufunga mara kwa mara.

Deportivo de A Coruña, hali ya timu kwa sasa ni ya kuridhisha. Katika raundi 4 za ligi, timu hii ilipata ushindi mechi 2 na sare 3, ikiwa haijafungwa hata mara moja, ikiwa na pointi 9 ikishika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi.

Katika mchezo wa raundi ya 5, Deportivo ilishinda ugenini 3-2 dhidi ya Villarreal, hali ya mashambulizi ni nzuri. Mshambuliaji wao Aubameyang amefunga mabao 4 na kutoa pasi 2 za mabao katika raundi 4 za ligi, akiwa mchezaji muhimu zaidi wa timu.

Kwa upande wa Sevilla, imeanza msimu kwa nguvu. Katika raundi 5 za ligi, Sevilla ilipata ushindi mechi 3 na kufungwa mchezo 1, ikiwa na pointi 10 ikishika nafasi ya tano  kwenye msumamo wa ligi.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Hata hivyo, Sevilla inakabiliwa na tatizo la majeraha ya wachezaji, Mlinzi Msenegal Arouna Sangante kutokana na jeraha la kifundo cha mguu hatakuwa katika mchezo huu, wakati Rubén Vargas pia anaendelea   kukosekana kutokana na jeraha.

Rekodi ya michezo ya timu hizi mbili, Sevilla ina faida kubwa. Katika michezo 5 ya mwisho, Sevilla ilipata ushindi kwenye michezo 3 na sare 2, Deportivo haikupata ushindi wowote.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na uwezo wa Deportivo kutumia faida ya uwanja wa nyumbani na kasi waliyonayo katika mashambulizi. Sevilla, kwa upande mwingine, itahitaji kutumia uzoefu wake na kuwa makini dhidi ya safu ya ushambuliaji ya wenyeji, hasa Aubameyang ambaye tayari ameonyesha kuwa tishio kubwa msimu huu.

 

 

 

RAIS DKT. MWINYI APOKEA MWALIKO WA DUA MAALUM YA KULIOMBEA TAIFA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amepokea mwaliko wa kushiriki katika dua maalum ya kuwaombea viongozi wa nchi na kuliombea Taifa kutokana na matarajio ya mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya El Niño

Rais Dkt. Mwinyi amepokea mwaliko huo leo, tarehe 16 Septemba 2026, Ikulu Zanzibar, alipokutana na uongozi wa Almadrasat Swifat Nabawiyatil Karimah, Msolopa Kilimani.

Dua hiyo inatarajiwa kufanyika Ijumaa, tarehe 18 Septemba 2026, ikilenga kumuomba Mwenyezi Mungu kuwalinda viongozi, Taifa na wananchi wake, pamoja na kuliepusha Taifa na madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua kubwa.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameridhia ombi la madrasa hiyo la kuongeza nafasi za Hijja kutoka tatu zilizotolewa mwaka jana hadi sita mwaka huu.

Rais Dkt. Mwinyi ameipongeza taasisi hiyo kwa kuendelea kushiriki katika shughuli za kumuombea Mwenyezi Mungu amani, ustawi na maendeleo ya nchi, huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano wa kijamii na kiroho.

Naye, Amir Mkuu wa Almadrasat Swifat Nabawiyatil Karimah, Alhaj Sheikh Muhammad Salum Muhammed, amemshukuru Rais Dkt. Mwinyi kwa kupokea mwaliko huo na kukubali ombi la kuongeza nafasi za Hijja kutoka tatu hadi sita, akieleza kuwa hatua hiyo imepokelewa kwa shukrani kubwa na uongozi wa madrasa.

 

MASILE SACCOS YAWATAKA WANACHAMA KUREJESHA MIKOPO KWA WAKATI, YATANGAZA UCHAGUZI DESEMBA

Na Samwel Mpogole – Mbeya

Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Masile SACCOS kilichopo Jijini Mbeya kimefanya Mkutano Mkuu wa Mwaka, ambapo wanachama wamejadili mwenendo wa chama, changamoto zinazokikabili pamoja na hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika kukiendeleza.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkaguzi Mshauri wa Vyama vya Ushirika Kanda ya Mbeya, CPA Edson Pascal, amewataka wanachama wa Masile SACCOS kuhakikisha wanarejesha mikopo kwa wakati na kwa usahihi.

CPA Pascal amesema urejeshaji wa mikopo kwa wakati ni muhimu katika kuhakikisha chama kinaendelea kuwa na uwezo wa kutoa huduma za mikopo kwa wanachama wengine, pamoja na kuimarisha uendeshaji wa SACCOS.

Kwa upande wake, Meneja wa Masile SACCOS, Rodina Mbwaga, amesema pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika uendeshaji wa chama, ni muhimu kwa wanachama na viongozi kushirikiana katika kuzitafutia ufumbuzi.

Mbwaga amewataka wanachama kutoa ushirikiano kwa uongozi na kutoa maoni pamoja na ushauri pale inapohitajika, akisisitiza kuwa milango ya chama ipo wazi kwa wanachama.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Masile SACCOS, Venance Mlozi, amewataka wanachama kujiandaa kushiriki katika uchaguzi wa chama unaotarajiwa kufanyika Desemba 29, 2026.

Mlozi amesema ushiriki wa wanachama katika uchaguzi huo ni sehemu ya kutekeleza wajibu wao katika uendeshaji wa chama, huku akiwataka kusoma na kuelewa kanuni pamoja na taratibu zinazohusu uchaguzi.

Baadhi ya wanachama walioshiriki mkutano huo wameeleza kufurahishwa na mwenendo wa Masile SACCOS, wakisema huduma zinazotolewa na chama hicho zimeendelea kuwapa fursa za kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.

Wanachama hao wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi na kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za chama, wakisisitiza umuhimu wa mshikamano katika kuhakikisha Masile SACCOS inaendelea kukua na kuwanufaisha wanachama wake.

 

WIZARA YA MADINI YAJA NA SHERIA KUSIMAMIA TAALUMA YA WAJIOLOJIA

*Sheria kuanzisha Bodi ya Wajiolojia kusimamia na kuratibu taaluma nchini*

*Serikali kutenga asilimia 10 ya mapato ya madini kwa utafiti wa jiosayansi*

*Taarifa sahihi za jiolojia kuimarisha uwekezaji na kuwalinda wadau wa madini*

Wizara ya Madini imewasilisha pendekezo la kuanzishwa kwa Sheria ya Usimamizi wa Wajiolojia nchini katika Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri, hatua inayolenga kuweka mfumo madhubuti wa kusimamia taaluma hiyo na kuhakikisha taarifa za jiosayansi zinazotolewa nchini zinakuwa sahihi na zenye kuaminika.

Hayo yamebainishwa leo, Septemba 16, 2026, jijini Mwanza na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wajiolojia Tanzania (TGS).

Dkt. Kiruswa amesema endapo Sheria hiyo itapitishwa, itaanzishwa Bodi ya Wajiolojia itakayokuwa na jukumu la kusimamia, kuratibu na kuimarisha taaluma hiyo, ikiwemo kuweka viwango vya kitaaluma na kuhakikisha wataalamu wanaohusika na shughuli za jiosayansi wanatambulika na kuwajibika ipasavyo.

Amesema hatua hiyo ni muhimu kutokana na umuhimu wa taarifa za jiosayansi katika shughuli za utafutaji, uchimbaji na uwekezaji katika sekta ya madini, huku akieleza kuwa kumekuwa na baadhi ya taarifa zisizo sahihi zinazotolewa na watu wasio waaminifu au wasiokuwa na weledi na ujuzi unaohitajika, hali ambayo imekuwa ikisababisha hasara kwa baadhi ya wadau wa sekta hiyo.

“Ni muhimu kuwa na chombo kitakachosimamia taaluma hii ili kuhakikisha taarifa za jiosayansi zinazotokana na tafiti zinazofanywa nchini zinakuwa za uhakika na zinatolewa na wataalamu wenye sifa, weledi na uwajibikaji,” amesema Dkt. Kiruswa.

Katika hatua nyingine, Dkt. Kiruswa amesema Serikali imefanya uamuzi wa kutenga asilimia 10 ya makusanyo yatokanayo na mapato yasiyo ya kodi katika sekta ya madini kwa ajili ya shughuli za utafiti wa madini nchini, ambapo fedha hizo zinakadiriwa kufikia takribani Sh bilioni 140.

Amesema fedha hizo zitawezesha Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kuongeza kasi ya tafiti za jiosayansi na kuzalisha taarifa nyingi na sahihi zitakazosaidia kubainisha rasilimali zilizopo nchini na kuweka msingi imara wa uwekezaji katika sekta ya madini.

Dkt. Kiruswa amesema Wizara ya Madini itaendelea kushirikiana na Jumuiya ya Wajiolojia Tanzania katika kuimarisha taaluma hiyo na kuhakikisha wataalamu wa ndani wanashiriki kikamilifu katika tafiti na shughuli za jiosayansi zinazolenga kuongeza manufaa ya rasilimali za madini kwa Taifa.

Ameeleza kuwa hatua hiyo inakwenda sambamba na vipaumbele vya Wizara vinavyotokana na Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050 na Sera ya Madini, ambavyo ni pamoja na kuongeza utafiti na upatikanaji wa taarifa sahihi za jiolojia, kuongeza thamani madini, kuunganisha sekta ya madini na sekta nyingine za uchumi, kurasimisha na kuboresha uchimbaji mdogo, pamoja na kuimarisha usimamizi wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake, Rais wa Jumuiya ya Wajiolojia Tanzania, Prof. Alisante Mshiu, amesema Mkutano Mkuu wa Mwaka ulianza Septemba 14, 2026, ukiwa na dhima ya “Matumizi ya Suluhisho za Jiosayansi kwa Ukuaji wa Viwanda, Uhakika wa Upatikanaji wa Nishati, Kuelekea Matumizi ya Nishati Safi na Maendeleo Stahimilivu Tanzania.”

Amesema mkutano huo umelenga kutoa fursa kwa wataalamu kubadilishana uzoefu na maarifa katika nyanja mbalimbali za jiosayansi, kwa lengo la kuongeza matumizi ya taaluma hiyo katika kutatua changamoto za maendeleo, kukuza uchumi na kuongeza manufaa yatokanayo na rasilimali zilizopo nchini.

NIDA KUANZA KUWASAJILI WATOTO CHINI YA MIAKA 18″ – DKT MWIGULU.

*_● Awasihi Watanzania kuchukua Vitambulisho vyao vya Uraia._*

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) itaanza kuchukua hatua za kuwasajili na kuwatambua watoto walio chini ya umri wa miaka 18, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mfumo wa utambulisho wa Taifa.

Dkt. Mwigulu amesema hatua hiyo itamuwezesha kila Mtanzania kutambulika kuanzia hatua za mwanzo za maisha yake pamoja na kuondoa pengo lililokuwepo katika mfumo wa utambulisho kati ya mtoto anapozaliwa na anapofikisha umri wa miaka 18.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo, Jumatano, Septemba 16, 2026, wakati akiwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Utambulisho Duniani, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

“Mfumo huu utasaidia kupunguza usumbufu wa kutumia nyaraka au vitambulisho vingi wakati wa kupata huduma mbalimbali, kwa kuwa taarifa muhimu za mwananchi zitaendelea kutambulika na kuhifadhiwa katika mfumo mkuu wa Taifa wa utambuzi” amesema.

Aidha, Dkt. Mwigulu amewataka Watanzania ambao tayari wamesajiliwa na vitambulisho vyao vya Taifa vimekamilika kwenda kuvichukua, akisisitiza kuwa utambulisho ni msingi muhimu wa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

“Kitambulisho chenyewe kama nchi tumeingia gharama, tumeahirisha baadhi ya shughuli za maendeleo ili tutoe vitambulisho. Lakini tunapokuwa tumetoa kitambulisho, halafu mhusika haendi kuchukua, haya ni mambo ambayo yanakwamisha malengo mapana,” amesema.

Amesema kwa sasa NIDA imeboresha utaratibu wa kuwafahamisha wananchi pale vitambulisho vyao vinapokuwa tayari, ikiwemo kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS), hivyo hakuna sababu kwa wananchi waliokwishaandikishwa kuacha vitambulisho vyao kwa muda mrefu bila kuvichukua.

“Niendelee kusisitiza wananchi wote ambao wako tayari na vitambulisho vyao, basi waende kuvichukua. Lengo letu ni kuona kuwa hakuna Mtanzania anayeachwa nyuma katika kupata vitambulisho vya Taifa,” amesema.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwigulu amesema Serikali imeendelea kufanya maboresho katika mfumo wa utambulisho wa Taifa ili kuhakikisha unakidhi mahitaji ya sasa ya kiteknolojia, usalama wa taarifa na utoaji wa huduma kwa wananchi.

“Serikali imeendelea kuboresha mfumo wa utambulisho ili kupunguza utegemezi wa vitambulisho vingi kwa huduma mbalimbali na kuelekea katika mfumo ambao taarifa muhimu za mwananchi zinapatikana kupitia mfumo mkuu wa Taifa wa utambuzi,” amesema.

Naye, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema NIDA imefanya mapitio ya jumla ya vitambulisho vilivyotolewa katika ofisi zake na vituo 10 vya usajili vilivyopo katika kila wilaya, bila kuhusisha vituo 156 vilivyotajwa awali.

Amesema hadi sasa jumla ya watu 27,520,835 wamesajiliwa, ambapo watu 23,515,667 wamekwishapatiwa Namba za Utambulisho wa Taifa. Aidha, vitambulisho 21,526,635 vimezalishwa, huku bado kukiwa na idadi ya vitambulisho ambavyo havijachukuliwa na wananchi waliostahili kuvipata.

Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji, amesema jamii inapaswa kuacha dhana kwamba NIDA ni taasisi inayotoa kadi pekee, kwa kuwa utambulisho wa Taifa ni msingi wa upatikanaji wa huduma na utambulisho wa mwananchi katika maisha yake yote.

Amesema NIDA inaendelea kuboresha kitambulisho cha Taifa ili kiwe cha kidijitali na kiweze kuhusisha taarifa muhimu za huduma mbalimbali za kijamii, ikiwemo cheti cha kuzaliwa, bima ya afya, TIN, leseni ya udereva na taarifa nyingine muhimu, huku taarifa za kiafya kama kundi la damu zikitarajiwa kusaidia wakati wa dharura, kwa kuzingatia uthibitisho wa kitabibu.

Kanji amesema usajili wa watoto tangu wanapozaliwa ni muhimu kwa sababu utamwezesha kila mtoto kutambulika na kupata huduma za kijamii kwa urahisi katika hatua zote za maisha. Amesema zoezi hilo litaanza kwa majaribio katika wilaya za Kilolo, Lungu na Kusini Unguja, kabla ya kupanuliwa katika maeneo mengine nchini

 

WAZIRI MKUU AWASILI ARUSHA, KUFUNGUA KONGAMANO LA WANAMIPANGO

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasili mkoani Arusha leo Jumatano, Septemba 16, 2026, ambapo amepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Arusha na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makalla, pamoja na viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali.

Dkt. Mwigulu yupo mkoani Arusha kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kikazi, ikiwemo kufungua rasmi Kongamano la Kitaifa la Wanamipango, litakalofanyika kesho Alhamisi, Septemba 17, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).

 

MAKAMU WA RAIS MHE. NDEJEMBI AENDELEZA DIPLOMASIA YA TANZANIA – VIENNA

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi amefanya mikutano miwili ya pande mbili (bilateral meetings) pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa 70 wa Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA) Jijini Vienna, Austria, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Tanzania kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika maeneo mbalimbali ya maendeleo.

 

Katika mkutano wake na Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Bw. Rafael Mariano Grossi, mazungumzo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano katika matumizi ya sayansi na teknolojia ya nyuklia kwa madhumuni ya amani na maendeleo, hususan matibabu ya saratani, kilimo na usalama wa chakula, lishe, maendeleo ya wataalamu pamoja na maandalizi ya Tanzania kuelekea matumizi ya nishati ya nyuklia kama nyongeza ya vyanzo vya uzalishaji umeme nchini siku zijazo.

 

Aidha, Makamu wa Rais amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Vienna (UNOV) na Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), Dkt. Monica Juma. Mazungumzo yaliyolenga kuendeleza ushirikiano baina ya Tanzania na UNODC katika juhudi za kudhibiti dawa za kulevya.

 

Makamu wa Rais, Mhe. Ndejembi, yuko Jijini Vienna, Austria, akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano Mkuu wa 70 wa Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA), unaowakutanisha Viongozi na Wawakilishi wa Nchi wanachama kujadili masuala mbalimbali yanayohusu matumizi salama na ya amani ya sayansi na teknolojia ya nyuklia.

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

16 Septemba 2026

Vienna – Austria

 

DCI Kingai Kutinga Ijumaa Hii Kutoa Ushahidi Kesi ya Lissu, Heche Amaliza..

Mshtakiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amemaliza kumuuliza maswali ya re-examination shahidi wake, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche, katika kesi inayosikilizwa mbele ya Jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu, likiongozwa na Jaji Dustan Ndunguru.

Baada ya kumaliza kumuuliza Heche maswali ya re-examination, Lissu aliliomba Jopo la Majaji maelekezo kuhusu mashahidi ambao Mahakama ilitoa summons kwa ajili yao.

“Waheshimiwa Majaji, niliomba summons kwa ajili ya mashahidi, kwa hiyo nataka kujua majibu kuwa mashahidi hao wako wapi na tunakwendaje mbele,” alisema Lissu.

Lissu alieleza pia kuwa anahitaji kukutana na mashahidi hao kabla hawajafika mahakamani ili kuwaandaa kwa ajili ya kutoa ushahidi.

Alisema hawezi kuwaweka mashahidi kizimbani bila kwanza kukutana nao na kuwaelekeza namna ya kuendesha ushahidi wao.

Kwa mujibu wa Lissu, Mahakama ndiyo eneo pekee analoweza kukutana na mashahidi hao kwa kuwa hana sehemu nyingine ya kuwaandalia, huku akisema hawezi kwenda maofisini kwao au gerezani.

Jaji Ndunguru alisema Mahakama ilitarajia upande wa Lissu kutoa taarifa iwapo ana shahidi au hana, kwa kuwa summons tayari zilitolewa na Mahakama.

Jaji alisema Mahakama ingepumzika ili Msajili awasilishe taarifa kuhusu utekelezaji wa summons hizo.

Baada ya mapumziko, Lissu alirejea mahakamani na kueleza kuwa alikuwa amekutana na Msajili wa Mahakama ambaye alimpatia taarifa kuhusu summons za mashahidi.

Kwa mujibu wa Lissu, Msajili alimweleza kuwa mashahidi wote walipelekewa summons Dodoma, ingawa nakala za summons hizo hazikuweza kuhifadhiwa baada ya kubainika kuwa baadhi ya mashahidi walikuwa nje ya nchi.

Lissu alisema mmoja wa mashahidi hao, ambaye ni Kamishna wa Polisi na Mkuu wa Upelelezi katika Jeshi la Polisi (DCI), alitarajiwa kurejea nchini siku hiyo.

Alisema Msajili alimwahidi kuwa siku ya Ijumaa Kamishna huyo atakuwepo Mahakamani kwa ajili ya kutekeleza wito uliotolewa na Mahakama.

Lissu alieleza kuwa mashahidi wengine wawili waliotajwa ni Mkuu wa Majeshi, Jenerali Jacob Mkunda, na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Camillius Wambura, ambao wakati huo haikufahamika ni lini wangerejea nchini.

Kutokana na hali hiyo, Lissu alipendekeza kesi hiyo iahirishwe hadi Ijumaa saa 8:30 mchana, ili muda wa asubuhi autumie kukutana na kushauriana na shahidi anayetarajiwa kufika, pamoja na kuchukua maelezo yake.

Alisema endapo mashahidi hao hawatakuja kabisa, suala hilo litakuwa mikononi mwa Mahakama kwa kuwa ni Mahakama iliyotoa summons hizo.

Aidha, Lissu alieleza kuwa anafahamu ratiba ya shauri hilo ilivyo na kwamba yeye pia anatamani shauri hilo lifikie hatua ya final submissions ili Mahakama ipate muda wa kutafakari na kutoa uamuzi.

Alisema iwapo mashahidi watafuata wito wa Mahakama, anaamini ushahidi wao hautachukua muda mrefu.

Upande wa mashtaka, kupitia Wakili Nassor Katuga, ulisema hauna pingamizi kuhusu kuahirishwa kwa kesi hiyo.

“Hata hivyo, tunaomba Mahakama hii imsisitize mshtakiwa mashahidi wake wafike kwa wakati,” alisema Katuga.

Kauli hiyo ilisababisha hali vicheko mahakamani, kabla ya Jaji Ndunguru kusisitiza kuwa mashahidi hao si “mashahidi wake” kwa maana ya kwamba ni jukumu la Mahakama kuhakikisha summons zinazingatiwa, huku akimkumbusha Lissu kuwa yeye ndiye anayetarajiwa kuwaleta mashahidi hao mahakamani.

Hatimaye, Jaji Ndunguru alitangaza kuwa shauri hilo limeahirishwa hadi Ijumaa tarehe 18, ambapo shahidi anayetarajiwa kufika mahakamani anatarajiwa kuendelea na hatua inayofuata ya ushahidi.

Katika hatua hiyo, Ramadhan Kingai anatarajiwa kufika Mahakamani Ijumaa kwa ajili ya kutoa ushahidi, ikiwa ni sehemu ya mwenendo wa shauri hilo.

Saudi Arabia Yatungua Drone ya Houthi Iliyolenga Anga ya Makkah

RIYADH, Saudi Arabia — Mfumo wa ulinzi wa anga wa Saudi Arabia umefanikiwa kutungua ndege isiyo na rubani (drone) iliyokuwa ikijaribu kuelekea katika anga ya mji mtakatifu wa Makkah, mamlaka za Saudi Arabia zimesema.

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa Muungano wa Kurejesha Uhalali nchini Yemen, Meja Jenerali Turki Al-Malki, drone hiyo ilidunguliwa majira ya saa 6:50 jioni kwa saa za Saudi Arabia, kusini mwa Makkah, kabla haijaingia katika anga ya mji huo.

Al-Malki amesema jaribio hilo ni hatua kubwa na limevuka kile alichokiita “mstari mwekundu”, kutokana na umuhimu wa Makkah kwa Waislamu duniani.

Makkah ni mji mtakatifu zaidi katika Uislamu na hutembelewa na mamilioni ya Waislamu kila mwaka kwa ajili ya ibada za Hajj na Umrah. Pia ni eneo ambalo lina umuhimu mkubwa katika utekelezaji wa moja ya nguzo tano za Uislamu, Hajj.

Muungano huo umeitaja hatua hiyo kama jaribio la makusudi la kuchochea hisia za mamilioni ya Waislamu, na kusema kuwa tukio hilo litaendelea kuwa sehemu ya rekodi ya ukiukaji unaodaiwa kufanywa na kundi la Houthi.

Tukio hilo si la kwanza kuhusisha shambulio linalolenga eneo la Makkah. Mwaka 2017, Saudi Arabia ilisema vikosi vyake vya ulinzi wa anga vilifanikiwa kulitungua kombora la balestiki lililorushwa kuelekea Makkah kutoka Yemen.

Kwa mujibu wa mamlaka za Saudi Arabia wakati huo, kombora hilo lilitunguliwa katika eneo la Al-Wasliya, mkoani Taif, na hakukuwa na taarifa za watu kujeruhiwa wala uharibifu wa mali.

Mvutano huo umeendelea huku Saudi Arabia ikiripoti mashambulizi mengine yanayohusishwa na Houthi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Siku ya Jumatatu, Saudi Arabia ilisema raia 13 walijeruhiwa baada ya maeneo ya raia katika Khamis Mushait, Abha na Taif kulengwa kwa makombora ya balestiki.

Wiki iliyopita, shambulio jingine lililoripotiwa katika miji na maeneo mbalimbali nchini Saudi Arabia lilisababisha zaidi ya watu 70 kujeruhiwa, wakiwemo wanawake na watoto.

Aidha, Saudi Arabia ilitangaza Ijumaa kusitisha kwa muda shughuli za East-West Pipeline, baada ya bomba hilo kulengwa katika mfululizo wa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani katika maeneo ya Riyadh na Madinah.

Mashirika ya nchi za Ghuba pamoja na taasisi mbalimbali za Kiislamu yalilaani shambulio hilo dhidi ya bomba na kueleza mshikamano wao na Saudi Arabia.