WAZIRI MKUU AWATAKA WANAMIPANGO KUWA CHACHU YA MAGEUZI YA KIUCHUMI NA UTEKELEZAJI WA DIRA 2050
_▪️Asema bado kuna kazi ya kufanya kwenye eneo la tathmini na ufuatiliaji._
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka wanamipango, wachumi, na watendaji wote wa serikali kuongoza mageuzi ya kiuchumi kupitia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2026/27–2030/31).
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Septemba 17, 2026) alipokuwa akifungua na kuhitimisha Kongamano la Wanamipango Tanzania lililofanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Arusha (AICC) jijini Arusha, ambapo Waziri Mkuu amesisitiza kuwa kupitia utekelezaji wa Dira 2050 taifa limeingia katika awamu mpya ya utendaji kazi inayohitaji kasi, ujasiri, na utendaji wa “business unusual” (akimaanisha kufanya kazi bila mazoea) ili kufikia malengo yaliyowekwa.
“Tanzania imeanza rasmi utekelezaji wa Dira 2050 Julai Mosi, 2026, katika uzinduzi uliofanyika Julai 17. Lengo kuu ni kuijenga nchi kuwa na uchumi wenye thamani ya dola za Kimarekani trilioni moja na pato la mtu mmoja mmoja la dola 7,000 kwa mwaka ifikapo 2050.”
“Ili kufikia matokeo hayo, lazima tufanye kazi kwa kasi, tuache mazoea na tubadili mtazamo hasi uliojengeka dhidi ya sekta binafsi kwamba wao sio wazalendo, wakati utekelezaji wa Dira 2050 unaitegemea sekta binafsi kwa asilimia 70,” amesema Dkt. Mwigulu.
Ili kuchochea uwekezaji na ajira, Waziri Mkuu ameongeza msisitizo kwa kutoa wito wa kuipatia sekta binafsi heshima na fursa sawa na sekta ya umma ambapo amewataka wanamipango kutumia tafiti na taarifa sahihi kuingia kwenye mikataba ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) bila hofu.
Dkt. Mwigulu amewataka watendaji hao kuisaidia Serikali kujitegemea na kupanua wigo wa mapato ambapo amesema kutokana na kubadilika kwa mfumo wa rasilimali za kimataifa na kupungua kwa misaada na mikopo nafuu, kuna umuhimu wa nchi kupanua wigo wake wa mapato ya ndani na kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Rais ya Mfumo wa Kodi ili kuongeza kujitegemea.
Aidha, amewahimiza wanamipango na watendaji wa Serikali kuoanisha Sera, Mipango, na Bajeti ili kuhakikisha miradi yote ya kielelezo inakamilika kwa wakati, kwa bajeti iliyopangwa, na kwa viwango vinavyotakiwa, huku wakiepuka kubadili mipango kiholela au kuongozwa na dharura.
“Ninakumbuka nikiwa Waziri wa Fedha, wizara zinapitishiwa bajeti wakati wa Bunge la bajeti, lakini ndani ya mwezi Julai tu wizara zinakuja kuomba kubadili vipaumbele kwa kuwa mambo wanayopaswa kuyafanya hayamo kwenye bajeti waliyoiomba na kupitishiwa na Bunge,” amesisitiza Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu amewataka wataalamu wa tathmini na ufuatiliaji kutobaki na ujuzi/mifumo peke yao, bali watoke na kwenda kusimamia na kufuatilia mipango na utekelezaji wa miradi kwa ujasiri katika ngazi zote, mikoa, wilaya, na halmashauri ili kuzuia dharura na matumizi mabaya ya rasilimali.
“Moja ya eneo ambalo bado hatujafanya vizuri ni hili la tathmini na ufuatiliaji. Kwenye hili, bado tuna kazi ya kufanya. Ufuatiliaji lazima ujikite katika kuhakikisha miradi ya kielelezo na mipango yote iliyowekwa inaleta matokeo yenye tija, inakamilika kwa wakati, na inazingatia bajeti pamoja na viwango vilivyopangwa,” amehimiza Waziri Mkuu.
Awali, akimkaribisha Waziri Mkuu kuhutubia, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, alibainisha kuwa makongamano yajayo hayatakuwa tena ya kujadili mipango pekee, bali itajikita katika kutoa taarifa za matokeo halisi ya utekelezaji kwani Serikali imewezesha upatikanaji wa nyenzo zote za kisheria na kimkakati kwa wakati ili kuongoza nchi kwa miaka 25 ijayo.
Naye, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida, amesema kongamano hilo ambalo ni la pili tangu kuundwa upya kwa Tume ya Taifa ya Mipango mwaka 2023, limewakutanisha zaidi ya washiriki 1,300 kutoka mikoa yote 26 ya Tanzania Bara. Washiriki hao ni pamoja na wachumi, wataalamu wa takwimu, maafisa mipango, watafiti, watendaji kutoka wizara, sekretarieti za mikoa, mamlaka za serikali za mitaa, sekta binafsi, na wadau wa maendeleo, lengo likiwa ni kujenga jukwaa la kubadilishana uzoefu na kuimarisha mipango jumuishi.
SANGU AITAKA TALGWU KUJENGA UMOJA KUPITIA UCHAGUZI
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Clement Sangu, amekitaka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kuendesha uchaguzi wake kwa kuzingatia Katiba, demokrasia, uwazi, haki, usawa na amani.
Mhe. Sangu ameyasema hayo, leo Septemba 17, 2026, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa TALGWU katika Ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma, akisisitiza kuwa uchaguzi huo uwe fursa ya kuimarisha umoja na mshikamano badala ya kuwa chanzo cha mgawanyiko.
“Uchaguzi usiwe chanzo cha mgawanyiko, bali uwe fursa ya kuimarisha umoja na mshikamano. Baada ya matokeo kutangazwa, viongozi na wanachama wote wanapaswa kuendelea kushirikiana, kwa kutambua kwamba TALGWU ni kubwa kuliko mtu mmoja,” amesema Mhe. Sangu.
Amesema Serikali inatambua na kuheshimu uhuru wa vyama vya wafanyakazi na itaendelea kushirikiana navyo kupitia mfumo wa majadiliano ya pamoja katika kushughulikia changamoto na masuala ya maslahi ya wafanyakazi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TALGWU Taifa, Ndugu Tumaini Peter Nyamhokya, amesema viongozi wa Chama hicho wamejipanga kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa amani na utulivu, huku wakiahidi kuendelea kushirikiana na Chama cha Wafanyakazi Tanzania (TUCTA).
“Tunaishukuru Ofisi yako jinsi ilivyosimama nasi kwenye chaguzi za mikoa zikamalizika salama na kwa amani. Basi na huu wa Taifa pia, nikuhakikishie Mhe. Sangu, utamalizika vizuri,” amesema Ndugu Nyamhokya.
Mwisho.
ACT Wazalendo Yafanya Uteuzi wa Jina la Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
Global Publishers
September 17, 2026
0 views
0 Comments

Kamati ya Uongozi Taifa ya Chama cha ACT Wazalendo imefanya uteuzi wa jina la mwanachama anayependekezwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho, Kamati ya Uongozi Taifa ilifanya kikao maalum Jumatano, Septemba 16, 2026, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya ACT Wazalendo, Vuga, mjini Unguja.
Taarifa hiyo imesema katika kikao hicho, Kamati ya Uongozi Taifa, kwa mujibu wa Ibara ya 72(3)(f) ya Katiba ya ACT Wazalendo, imefanya uteuzi wa jina la mwanachama anayependekezwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, jina hilo litawasilishwa rasmi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa ajili ya kukamilisha utaratibu uliowekwa katika Ibara ya 39(1), (2) na (3) ya Katiba ya Zanzibar.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, ikiwa na tarehe ya Septemba 17, 2026.
Hatua hiyo inakuja wakati ACT Wazalendo ikiendelea kushiriki katika mchakato wa mazungumzo ya kisiasa Zanzibar. Hivi karibuni, Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, alisema chama hicho kiko tayari kushiriki katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, huku kikitoa mapendekezo kuhusu mambo mbalimbali yanayolenga kuimarisha maridhiano na mustakabali wa Zanzibar.
Taarifa ya ACT Wazalendo haikutaja jina la mwanachama aliyeteuliwa, hivyo jina hilo bado halijawekwa wazi katika taarifa hiyo.

TOL Gases Yafungua Toleo la Hisa za Haki Stahiki la Shilingi Bilioni 8.17

Dar es Salaam, Tanzania, Alhamisi tarehe 17 Septemba 2026: TOL Gases PLC imefungua Toleo la Hisa za Haki Stahiki lenye thamani ya Shilingi bilioni 8.17 kwa lengo la kugharamia upanuzi wa uwezo wake wa uzalishaji wa hewa ya Carbondioxide, hatua inayoashiria awamu mpya katika mabadiliko ya moja ya kampuni kongwe zaidi za gesi za viwandani na tiba nchini Tanzania.
TOL Gases PLC inatoa hisa mpya za kawaida 11,501,193 kwa bei ya Shilingi 710 kwa kila hisa, kwa wanahisa waliopo wenye sifa, ambapo wanahisa watastahili hisa mpya moja kwa kila hisa tano za kawaida walizokuwa nazo hadi Tarehe ya Kumbukumbu ya Jumatatu, tarehe 14 Septemba 2026.
Toleo hili linafunguliwa tarehe 17 Septemba 2026 na kufungwa tarehe 08 Oktoba 2026 saa 10:00 alasiri. Hisa mpya zitaorodheshwa na kuanza kuuzwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) tarehe 22 Oktoba 2026, kwa kuzingatia masharti husika ya uorodheshaji.
Uchangiaji huu wa mtaji unakuja wakati TOL ikihamia kutoka kipindi cha kujiimarisha kibiashara kuelekea mzunguko mpya wa uwekezaji, ukichochewa na ongezeko la mahitaji ya gesi za viwandani na tiba nchini Tanzania na masoko jirani.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, kampuni imerejesha faida, imeimarisha imani ya wateja na kuunganisha uwezo wake wa uzalishaji na usafirishaji. Mapato yameongezeka kwa wastani wa asilimia 9.5 kila mwaka kati ya mwaka 2020 na 2025, huku EBITDA ikiongezeka kwa 28% kati ya mwaka 2024 na 2025. Wakati huo huo, mahitaji yamezidi kujaribu uwezo uliopo wa TOL, huku baadhi ya fursa za kikanda zikizidi uwezo wake wa kusambaza.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TOL Gases, CPA Leonard Kitoka, asema Toleo la Hisa za Haki Stahiki linawakilisha mpito muhimu kutoka hatua ya kujenga upya biashara kuelekea uwekezaji kwa ajili ya awamu yake ijayo.
“Katika miaka mitano iliyopita, tumejenga upya TOL iliyo imara zaidi na yenye uwezo mkubwa wa kuhimili changamoto. Fursa iliyopo mbele yetu sasa ni kubadilisha maendeleo hayo kuwa uwezo wa ziada. Toleo hili la Hisa za Haki linatupatia njia ya kushughulikia pengo la muda mrefu la usambazaji, kuimarisha uaminifu wa huduma na kuiweka kampuni katika nafasi ya kukidhi mahitaji yanayoongezeka nchini Tanzania na kanda nzima.”
Fedha zitakazopatikana zitaelekezwa katika kukuza uwezo wa TOL wa uzalishaji wa hewa ya Carbondioxide (CO2) na miundombinu inayohusiana, ikiwemo usanifu, ununuzi, ufungaji na uanzishaji wa kiwanda kipya cha uzalishaji wa CO2 pamoja na mahitaji ya kiuendeshaji na kilogistiki yanayohusiana.
Uwekezaji huu unashughulikia changamoto halisi inayoikabili kampuni. Mahitaji yameongezeka kwa kasi zaidi kuliko uwezo uliopo wa uzalishaji, jambo linalopunguza uwezo wa TOL kukidhi kikamilifu mahitaji ya ndani na fursa za kikanda.
Mkurugenzi Mtendaji Bw. Daniel Warungu asema uwekezaji huu wa mtaji utaipatia TOL nafasi kubwa zaidi ya kuwahudumia wateja kwa uaminifu, huku ikijenga msingi imara wa uzalishaji kwa ajili ya ukuaji wa baadaye.
“Kimsingi, hii ni hadithi ya uwezo wa uzalishaji. Tumeimarisha biashara, tumeboresha uendeshaji wetu na kurejesha imani ya wateja, lakini sasa mahitaji yanajaribu kikomo cha kile ambacho msingi wetu wa sasa wa uzalishaji unaweza kutoa. Hatua inayofuata ni kuwekeza katika uwezo utakaoiwezesha TOL kuwahudumia wateja wetu kwa uaminifu zaidi na kushindania fursa ambazo kwa sasa hatuwezi kuzihudumia kikamilifu.”
Warungu amesema ukuaji wa TOL utaendelea kwenda sambamba na uwekezaji katika usalama, uendelevu na utawala bora.
“Kwetu, ukuaji lazima uende sambamba na uwajibikaji. Hii inamaanisha kiwango kilekile cha usalama katika kila kituo na kwa kila mteja, mtazamo wa ESG unaojenga thamani ya muda mrefu kwa wadau wetu huku ukichangia vyema katika jamii na mazingira, pamoja na utawala unaoakisi viwango vinavyotarajiwa kwa kampuni iliyoorodheshwa.”
Mradi huu wa CO2 ni sehemu ya mpango mpana wa kukuza uwezo wa uzalishaji.
TOL pia inajiandaa kuanzisha rasmi Kitengo kipya cha Kutenganisha Hewa chenye uwezo wa tani 13 kwa siku, kikiwa kimeungwa mkono na Clinton Health Access Initiative. Ikijumuishwa na kitengo kilichopo cha tani saba kwa siku, uwekezaji huu unatarajiwa kuongeza uwezo wa uzalishaji wa oxygen na nitrogen hadi kufikia takribani tani 20 kwa siku ifikapo mwishoni mwa mwaka 2026.
Uwekezaji huu ukiwa pamoja unalenga kuboresha unyumbufu wa uzalishaji na uaminifu wa usambazaji katika sekta zinazotegemea gesi za viwandani na tiba.
Mpango huu wa upanuzi hauishii kwenye uzalishaji tu. TOL inaongeza magari yake ya usambazaji na kujenga vituo vipya vya usambazaji vya kikanda katika mikoa ya Arusha na Mtwara, sambamba na kituo kilichopo cha Mwanza, ili kusogeza huduma ya uhakika karibu zaidi na wateja nchini Tanzania na kanda nzima.
Jukwaa la uzalishaji la TOL nalo limekua kwa hatua, kutoka EKAMA 1 hadi EKAMA 2, huku EKAMA 3 ikiwa katika hatua za mipango sambamba na kitengo kipya cha kutenganisha hewa, kama sehemu ya ujenzi wa uwezo uliowekwa katika mkakati wa kampuni wa 2025 hadi 2029.
Kwa sasa, TOL inasambaza bidhaa na huduma katika sekta za afya, chakula na vinywaji, uchimbaji madini, uzalishaji viwandani, ujenzi na matumizi mengine ya viwandani. Bidhaa zake ni pamoja na oksijeni, naitrojeni, hewa ya ukaa, asetilini, argoni, heliamu na gesi nyingine za viwandani na tiba, pamoja na mifumo ya gesi za tiba, huduma za kulehemu na kukata vyuma, na vifaa vinavyohusiana.
Historia ya kampuni hii inaanzia mwaka 1950, ilipoanza kufanya kazi Tanzania ikiitwa African Oxygen and Acetylene Company. Ilisajiliwa rasmi mwaka 1966 kama Tanzania Oxygen Limited, kisha ikabadilishwa jina na kuwa TOL Limited mwaka 1996, na baadaye TOL Gases Limited mwaka 2006, kabla ya kubadilika hadhi na kuwa kampuni ya umma iliyoorodheshwa (PLC) kama TOL Gases PLC mwezi Aprili 2024.
Leo hii, TOL inaunganisha uwezo wa uzalishaji, usambazaji na kiufundi ili kuwahudumia wateja nchini Tanzania na masoko ya kikanda, huku usalama, ubora na uhakika wa usambazaji vikiwa nguzo kuu za mfumo wake wa uendeshaji.
Kwa wanahisa, Toleo la Hisa za Haki linatoa fursa kadhaa kulingana na masharti yaliyoainishwa katika Prospectus. Wanahisa wenye sifa wanaweza kuchukua sehemu yote au sehemu ya haki yao, huku wale watakaochukua haki yao yote wakiweza kuomba hisa zisizochukuliwa na wenzao, kulingana na upatikanaji.
Tanzania Securities Limited (TSL) ndiyo Mshauri Mkuu wa Muamala na Wakala wa Udhamini, huku National Bank of Commerce Limited ikiteuliwa kuwa Benki Mpokezi
Wanahisa wenye sifa wanaweza kuthibitisha haki yao kupitia TSL, Programu ya DSE – Hisa Kinganjani, au kupitia Madalali wao wa Hisa. Wanahisa wenye sifa wanashauriwa pia kusoma kwa makini Prospectus ya Toleo la Hisa za Haki kabla ya kufanya maamuzi ya uwekezaji.
Warungu amesema Toleo la Hisa za Haki linapaswa kuangaliwa ndani ya muktadha mpana wa kampuni ya Kitanzania inayojenga uwezo wa uzalishaji unaohitajika kuhudumia uchumi unaokua.
“TOL imekuwa sehemu ya maendeleo ya viwanda nchini Tanzania kwa zaidi ya miongo saba. Jukumu letu sasa ni kuhakikisha kampuni ina uwezo wa uzalishaji, nguvu za kiufundi na ustahimilivu wa kubaki na umuhimu kwa miongo ijayo. Uwekezaji huu unahusu kujenga uwezo huo.”
Toleo la Hisa za Haki Stahiki linafungwa saa 10:00 alasiri, Alhamisi tarehe 8 Oktoba 2026. Wanahisa wanashauriwa kurejea Prospectus kwa masharti kamili, taratibu za maombi, taarifa za malipo na hatari zinazohusika.
Magic Wheel: Gurudumu la Bahati Lenye Mizunguko Ya Msisimko

Bahati ni kitu kisichotabirika, lakini kwenye Magic Wheel unaweza kuiona ikizunguka mbele ya macho yako. Meridianbet imekuja na mchezo unaoleka msisimko wa kasino, huku gurudumu likiwa mhusika mkuu wa burudani. Linapoanza kuzunguka, hakuna anayejua litakaposimama, na hali hiyo ndiyo inayofanya kila mzunguko ufuatiliwe kwa hamu hadi sekunde ya mwisho.
Gurudumu la Magic Wheel lina nafasi 56, zikiwemo namba 53 pamoja na nafasi tatu maalumu. Hii ina maana kwamba kila mzunguko una nafasi ya kuleta sapraizi mpya. Namba zinapita kwa kasi wakati gurudumu likizunguka, lakini matokeo hubaki kuwa siri hadi linapofika mwisho.
Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Ukiwa tayari kuingia kwenye mchezo, hatua zake ni rahisi. Chagua namba 1, 2, 6 au 11, weka dau lako na kisha subiri gurudumu lifanye kazi. Mfumo huu rahisi umeifanya Magic Wheel kuwa burudani inayoweza kueleweka kwa haraka, huku mvuto mkubwa ukiwa kwenye kusubiri matokeo.
Kwa wanaotaka kuongeza kipengele kingine cha sapraizi, Box Bonus inaingia uwanjani. Mabox matatu yanakupa chaguo kati ya low, medium au high odds, lakini yaliyomo ndani hayaonekani kabla ya kufanya uchaguzi. Hapo ndipo uamuzi mdogo unaweza kugeuka kuwa sehemu kubwa ya msisimko wa mchezo, kwani hujui utakutana na nini mpaka uchague.
Kwa kifupi, Magic Wheel imeleta mchanganyiko wa gurudumu, uchaguzi na sapraizi katika burudani moja. Kila raundi ni mpya, kila mzunguko una matokeo yake na kila mchezaji anaingia akitaka kuona kama bahati itamtabasamia safari hii. Kama unapenda michezo ya aina hii, Magic Wheel ndani ya Meridianbet ipo tayari kukupa burudani.
Betis, Getafe Kukutana Leo la Liga, Haya Ndio Yanayotarajiwa

Real Betis itakuwa mwenyeji wa Getafe katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania LaLiga utakaopigwa leo Alhamisi, Septemba 17, 2026, saa 20:00 usiku. Mechi hii ni ya raundi ya sita ya msimu wa La Liga na itachezwa uwanjani kwa Real Betis, mjini Sevilla.
Betis inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na mwanzo mzuri wa msimu, baada ya kushinda michezo mitatu kati ya minne ya kwanza ya LaLiga. Kikosi hicho pia kilipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Real Madrid Septemba 4, kabla ya kuongeza ushindi mwingine katika Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Lille.
Kwa upande wa Getafe, timu hiyo imekuwa ikipambana kupata matokeo thabiti katika mechi zake za hivi karibuni. Katika mchezo wake wa mwisho wa LaLiga, Getafe ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Deportivo de La Coruña, ikiwa ni sare yake ya pili mfululizo baada ya pia kutoka 1-1 dhidi ya Celta Vigo.
Betis itahitaji kutumia vizuri faida ya kucheza kwenye uwanja wake wa nyumbani, huku ikitakiwa kuwa makini na Getafe ambayo inajulikana kwa kucheza kwa nidhamu na ushindani mkubwa. Kwa Betis, ushindi unaweza kuiweka katika nafasi nzuri zaidi kwenye mbio za juu za msimamo, wakati Getafe itakuwa ikisaka pointi za kujiimarisha kwenye msimamo
Kwa upande wa Real Betis, timu inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na changamoto kadhaa za majeruhi wanaokosekana. Wachezaji kama Abde Ezzalzouli, Giovani Lo Celso, Diego Conde, Aitor Ruibal na Ismael Barea wote hawapo kwenye kikosi kutokana na majeraha.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Getafe nao pia hawajasalimika na tatizo la majeruhi nyotaz wao kama Andrés García, Abdel Abqar, Mario Martín, Chrisantus Uche na Juanmi wote wamepoteza fursa ya kucheza kutokana na majeraha mbalimbali.
Kwa ujumla, mchezo huu unatarajiwa kuwa ni vita ya pointi tatu, ambapo Betis inaweza kutegemea ubora wake wa kushambulia na kiwango kizuri ilichoonyesha mwanzoni mwa msimu, huku Getafe ikilenga kuvuruga mipango ya wenyeji na kuondoka na walau pointi moja.
SERIKALI INAWEKEZA KWENYE MADINI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA, KUONGEZA FURSA ZA AJIRA – PROF. SHEMDOE
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji na usimamizi wa rasilimali madini, kwa lengo la kuhakikisha utajiri wa madini unatumika kikamilifu katika kujenga uchumi wa taifa na kuongeza fursa za ajira kwa wananchi.
Prof. Shemdoe amesema hayo Septemba 16, 2026, akiwa Ruangwa mkoani Lindi, wakati akifungua Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji mkoani humo.
“Lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa sekta ya madini haibaki kuwa ya uchimbaji pekee, bali inakuwa kichocheo cha viwanda, teknolojia, ajira, biashara, ubunifu na maendeleo ya jamii,” amesisitiza Prof. Shemdoe.
Katika kuhakikisha lengo hilo linatimia, Prof. Shemdoe ameyataka makampuni makubwa yaliyowekeza katika sekta ya madini kuangalia namna bora ya kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya uchenjuaji wa madini mkoani Lindi, hususan katika maeneo yenye rasilimali hizo, ili wananchi wanaozunguka maeneo hayo wanufaike zaidi kupitia fursa za ajira.
Prof. Shemdoe amesema maonesho hayo ni jukwaa muhimu linalowaunganisha Serikali, wananchi, wawekezaji katika sekta mbalimbali za uchumi, wataalam pamoja na taasisi za kifedha, kwa ajili ya kujenga uelewa mpana kuhusu rasilimali zilizopo na fursa za uwekezaji, pamoja na namna sekta mbalimbali za uchumi, ikiwemo madini, zinavyoweza kuongeza ajira, mapato na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
“Nilipofika hapa nilitembelea mabanda mbalimbali yaliyowakutanisha wachimbaji wakubwa, wadogo, wanaoleta teknolojia, akina mama, vijana na taasisi za kifedha, ili wakitoka hapa watoke na fursa mbalimbali zinazotokana na uwekezaji katika sekta ya madini,” ameeleza Prof. Shemdoe.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Adam Kighoma Malima, amesema mkoa huo si maskini, bali changamoto ni wananchi wake kuwa maskini, kwani mkoa hauwezi kuitwa maskini wakati una utajiri wa madini mbalimbali, jambo aliloliona kupitia maonesho hayo.
Mhe. Malima ameahidi kuwa ofisi yake itaendelea kusimamia maonesho kama hayo ya madini ili yaendelee kuibua fursa na kuvutia uwekezaji utakaowanufaisha wananchi.
Aidha, Mhe. Malima amesema anatarajia kuwa ndani ya kipindi cha uongozi wa miaka mitano wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, mkoa wa Lindi utakuwa umetambua fursa zake, kuzipa kipaumbele na hatimaye kuwa miongoni mwa mikoa yenye mapato makubwa nchini.
Naye Mbunge wa Ruangwa ambaye pia ni Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, amesema Ruangwa ina kiwanda kikubwa cha graphite, huku akieleza kuwa madini yaliyopo wilayani humo si graphite, dhahabu na kopa pekee, bali yapo madini mengine mengi.
Mhe. Mmuya amesema kutokana na uwepo wa rasilimali hizo, Ruangwa imeendelea kunufaika na mapato yatokanayo na sekta ya madini, ambapo mwaka jana wilaya hiyo ilichangia kiasi cha shilingi bilioni 2.9.
Mixx, Zangof Waunganisha Nguvu Kuwezesha Asasi Za Kiraia Zanzibar

Zanzibar, Septemba 16, 2026 – Asasi za kiraia Zanzibar zitapata fursa ya kutumia huduma za kifedha za kidijitali kusimamia malipo, mishahara na fedha za taasisi kwa urahisi na uwazi zaidi, kufuatia makubaliano ya ushirikiano kati ya Mixx na Jukwaa la Asasi za Kiraia Zanzibar (ZANGOF).
Makubaliano hayo yatawezesha asasi zilizo chini ya ZANGOF kutumia huduma ya Mixx Business Suite kufanya malipo ya mishahara na wanufaika, pamoja na kusimamia miamala mingine ya taasisi kwa njia ya kidijitali. Asasi hizo pia zitaweza kupata huduma za mawasiliano na intaneti za Yas.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini iliyofanyika leo Zanzibar, Mrajisi Mkuu wa Asasi za Kiraia Zanzibar, Ahmed Khalid Abdalla, alisema matumizi ya teknolojia yanaweza kusaidia asasi kuboresha usimamizi wa fedha na utoaji wa huduma kwa wananchi.
“Asasi za kiraia zinafanya kazi moja kwa moja na wananchi katika maeneo mbalimbali. Tunataka kuona teknolojia ikitumika kurahisisha kazi zao, kuongeza uwazi katika usimamizi wa fedha na hatimaye kuboresha huduma zinazotolewa kwa wananchi,” alisema Abdalla.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx, Angelica Pesha, alisema ushirikiano huo utasaidia kupeleka huduma za kifedha za kidijitali karibu zaidi na asasi pamoja na jamii wanazozihudumia.
“Asasi hizi zinafanya kazi na wanawake, vijana, wajasiriamali na makundi mbalimbali katika jamii. Kupitia huduma zetu, tunataka kuwapa njia rahisi na salama zaidi za kusimamia fedha, kufanya malipo na kuweka akiba. Kwetu, ujumuishaji wa kifedha ni kuona huduma hizi zikimsaidia mwananchi kuboresha shughuli na maisha yake,” alisema Pesha.
Makubaliano hayo pia yanatoa fursa kwa vikundi vinavyofanya kazi na asasi za kiraia kutumia Kikoba cha Mixx, kinachowawezesha wanachama kuweka akiba, kuchangia, kununua na kuuza hisa pamoja na kukopeshana kwa njia ya kidijitali.
Mixx tayari inashirikiana na taasisi mbalimbali Zanzibar katika matumizi ya huduma za kidijitali, zikiwemo Idara ya Maendeleo ya Ushirika, ZARTSA, ZanBus na ZSTC, katika maeneo kama malipo ya wakulima, usafiri wa umma na huduma nyingine.
Makubaliano na ZANGOF yanatarajiwa kupanua matumizi ya huduma hizo kwa asasi za kiraia na vikundi vya kijamii Zanzibar.
Kajala Afichua Kilichotokea Baada Ya Harmonize Kutaka Ndoa, Wolper Afunguka

Mambo ya mapenzi yamechukua nafasi katika mazungumzo ya mastaa wa Bongo, huku majina ya Irene Uwoya, Jacqueline Wolper, Kajala Masanja na Aunty Ezekiel yakitajwa katika mjadala ulioibua maswali kadhaa kuhusu maisha yao ya kimapenzi.
Mjadala huo ulipomfikia Irene Uwoya, suala la kuwa na mpenzi lilionekana kuwa moja ya mada zinazomgusa zaidi. Irene alipohojiwa kuhusu mahusiano yake, alikanusha kwa msisitizo kuwa ana mtu, hali iliyozua shauku kwa waliokuwa wakifuatilia mazungumzo hayo.
Aunty Ezekiel, kwa upande wake, alitoa kauli iliyoonekana kuongeza utata katika mjadala huo, akigusia namna ambavyo mastaa wa A-List wanavyohusishwa na maisha binafsi ya Irene na hata suala la kumposti endapo wataamua kufanya hivyo.

WOLPER: “SITAKI MUME WANGU ATAJWE”
Kwa upande wa Jacqueline Wolper, mazungumzo yalihamia katika maisha yake ya ndoa, ambapo alionyesha kutopenda jina la mume wake kutajwa katika kipindi chao.
Hata hivyo, baada ya kauli hiyo, aliulizwa iwapo kuna uwezekano kwamba tayari ametengana na mume wake na kutakiwa kuweka wazi hali halisi ya uhusiano wao.

KAJALA AFUNGUKA KUHUSU HARMONIZE NA SUALA LA NDOA
Mambo yalizidi kuwa ya kuvutia baada ya jina la Harmonize kuingia kwenye mjadala kupitia Kajala Masanja.
Kajala alieleza kuwa Harmonize alitumia takribani miaka miwili kumshawishi hadi alipokubali kuwa naye katika uhusiano. Kwa mujibu wa maelezo yake, baada ya uhusiano huo kuanza, Harmonize alifika hatua ya kuzungumzia suala la ndoa.
Hata hivyo, Kajala alisema yeye ndiye aliyekataa kwa wakati huo, akieleza kuwa alitaka kujipa nafasi na muda zaidi kabla ya kufanya uamuzi mkubwa wa kuingia kwenye ndoa.
Katika mazungumzo hayo, Kajala pia alikabiliwa na maswali kuhusu tetesi za matatizo katika uhusiano wake na Harmonize. Wenzake walimtaka kutoa uhakika kuhusu hisia zake kwa rafiki yao, huku wakisisitiza kuwa wanataka kuona heshima na mapenzi yakidumishwa.
Walisema wamechoshwa kumuona Kajala akiumia kutokana na masuala ya mapenzi, hivyo kumtaka kuwa makini na maamuzi yake.
Pamoja na tetesi zinazoendelea kuhusu uwezekano wa Kajala na Harmonize kutengana, Kajala bado hajathibitisha rasmi kuwa wameachana, wala kuweka wazi chanzo cha madai hayo.
Wakati mashabiki wakiendelea kujiuliza kinachoendelea nyuma ya pazia, pia kumekuwa na taarifa kuhusu uwezekano wa Kusah na Harmonize kufanya “special appearance” katika kipindi hicho, jambo ambalo limeongeza hamu ya kujua kitakachojiri iwapo wawili hao watajitokeza.






