Trump Atoa Kauli Mpya Kuhusu Iran, Asema Anaweza Kukutana na Pezeshkian

Global Publishers
September 21, 2026
0 views
0 Comments

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema yuko tayari kukutana na Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, huku akisema bado yuko katika hatua ya kufanya uamuzi kuhusu hatua inayofuata dhidi ya Tehran.

Trump alisema Jumapili kwamba mambo makubwa sana yanaweza kutokea kuhusu Iran, huku akionya Tehran kwamba inapaswa kuwa makini na kufuata masharti ya Marekani.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kukutana na Pezeshkian, ambaye yuko New York kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Trump alisema huenda akawa tayari kufanya hivyo.

Hata hivyo, kauli hiyo imekuja wakati mvutano kati ya Marekani na Iran ukiendelea kuwa mkubwa. Trump amesema chaguzi zinazokabili Marekani ni pamoja na kuendelea na mashinikizo ya kiuchumi, kuchukua hatua kali za kijeshi au kufikia makubaliano na Iran.

Kwa upande wa Iran, viongozi wake wameendelea kutoa tahadhari kwamba shambulio lolote jipya dhidi ya nchi hiyo linaweza kusababisha Tehran kuongeza ukubwa na aina ya silaha itakazotumia katika eneo hilo.

Wakati huohuo, Iran imeripotiwa kuwasilisha masharti kupitia wapatanishi kuhusu kurejeshwa kwa mazungumzo na Marekani pamoja na suala la usafirishaji kupitia Mlango wa Hormuz.

Kauli za Trump zinaonyesha kuwa, licha ya kuongezeka kwa vitisho na mvutano kati ya Washington na Tehran, bado kuna uwezekano wa diplomasia kutumika kama njia ya kutafuta makubaliano.

Mbaazi zaidi ya tani 100 zauzwa Pwani – HabariLeo

PWANI: ZAIDI ya tani 100 za mbaazi zilizokusanywa na wakulima wa Chalinze na Kibaha mkoani Pwani zimeuzwa zote katika mnada wa kwanza wa zao hilo, uliofanyika Kibaha kwenye ofisi za Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Pwani (CORECU).

Meneja wa CORECU mkoani humo, Hamis Mantawela, amesema mnada huo umehusisha mbaazi kilo 101,346, ambapo Chalinze zilikusanywa kilo 53,335 na Misugusugu, Kibaha, zilikusanywa kilo 48,011.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mnada huo, Mantawela amesema bei ya juu kwa kilo moja ya mbaazi zilizotoka Chalinze ilikuwa Sh1,300, huku za Misugusugu zikifikia Sh1,330 na bei ya chini ikiwa Sh1,300.

Amesema wakulima watalipwa fedha zao baada ya wanunuzi kuingiza malipo, akieleza kuwa utaratibu huo umekuwa ukisaidia kuhakikisha wakulima wanapata fedha zao kwa wakati.

“Tunapofanya mnada, wanunuzi ndani ya siku mbili wanaingiza fedha, hivyo na wakulima nao malipo hufanyika kwa haraka,” amesema.

Mantawela amewataka wakulima ambao bado wana mbaazi nyumbani kuzipeleka katika vituo husika ili ziingizwe kwenye minada na kuuzwa, badala ya kuendelea kuzihifadhi majumbani.

Kwa upande wake, mkulima na mjumbe wa Bodi ya AMCOS ya Maneromango, Kisarawe, Abdallah  Mwengia, amewataka wakulima wenye mbaazi majumbani kuzipeleka kwenye minada ili waweze kuziuza na kunufaika na mazao yao.

Akizungumzia mfumo wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), Mwengia amesema umeleta mabadiliko katika biashara ya mazao kwa kuwawezesha wakulima kunufaika zaidi na kilimo chao kupitia minada.

Amesema kabla ya kuanzishwa kwa mfumo huo, wakulima walikuwa wakikumbana na changamoto ya kudhulumiwa na madalali, hali iliyowafanya wasinufaike ipasavyo na mazao waliyolima.

Ameongeza kuwa kupitia mfumo huo, wakulima sasa wanapata malipo kwa wakati na kwa uwazi, huku wakipata fursa ya kufahamu bei ambazo mazao yao yameuzwa katika minada.-

Elizabeth Makune Aibuka Miss Universe Tanzania 2026

Global Publishers
September 21, 2026
0 views
0 Comments

DAR ES SALAAM: Elizabeth Makune kutoka Mwanza ametangazwa kuwa mshindi wa Miss Universe Tanzania 2026, baada ya kuibuka kidedea katika fainali ya mashindano hayo yaliyofanyika katika studio za Haddy Pro, Mbezi Beach Jogoo, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Septemba 21, 2026.

Makune, ambaye aliwakilisha Mkoa wa Mwanza, amejishindia zawadi ya Sh milioni 20 pamoja na taji la Miss Universe Tanzania 2026.

Elizabeth Makune kutoka Mwanza mshindi wa Miss Universe Tanzania 2026.

Katika nafasi ya tatu, Sandra Giovina kutoka Arusha ametangazwa kuwa mshindi wa tatu na kupokea zawadi ya Sh milioni 10.

Melinda Enok ameshika nafasi ya nne. Mbali na zawadi ya Sh milioni 5, Enok atapata fursa ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Humanity, yanayotarajiwa kufanyika Hong Kong.

Nafasi ya tano imekwenda kwa Mariam Cosmas kutoka Mwanza, ambaye amepokea zawadi ya Sh milioni 5. Cosmas pia ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss OURA.

Sita bora ya Miss Universe Tanzania 2026.

Katika tuzo nyingine zilizotolewa kwenye fainali hiyo, Merikai Wavi ametangazwa kuwa Miss Supranational Tanzania, akipokea zawadi ya Sh milioni 10.

Fainali hiyo imewakutanisha washiriki kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania, huku washindani wakipambana katika hatua mbalimbali za mashindano kabla ya majina ya washindi kutangazwa.

Ushindi wa Elizabeth Makune unamuweka katika nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika jukwaa la Miss Universe, huku washindi wengine wakipewa majukumu ya kuiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ya urembo ya kimataifa.

Faida za Maji ya Nazi kwa Wagonjwa wa Gauti Unazopaswa Kujua

Gout ni ugonjwa wa kimetaboliki unaosababishwa na kuongezeka kwa kiwango cha asidi ya uric (uric acid) kwenye damu. Asidi hii ikizidi, hutengeneza fuwele ndogo zinazojikusanya kwenye viungo, hali inayosababisha maumivu makali, uvimbe na joto kwenye viungo, hasa vidole vya miguu, magoti na vifundo.

Kwa mujibu wa Dkt. Nguyen Anh Duy Tung kutoka Kliniki ya Lishe ya Nutrihome, pamoja na kufuata matibabu ya daktari, wagonjwa wa gout wanashauriwa kupunguza vyakula vyenye purine nyingi, kunywa maji ya kutosha na kuzingatia mtindo bora wa maisha. Miongoni mwa vinywaji vinavyoweza kusaidia ni maji ya nazi.

Maji ya nazi yana virutubisho muhimu kama potasiamu, magnesiamu, vitamini C na elektrolaiti asilia, na yana uwezo wa kupunguza uvimbe mwilini. Yakinywewa kwa kiasi kinachofaa, hutoa faida zifuatazo:

1. Husaidia kuondoa asidi ya uric mwilini

Maji ya nazi yana tabia ya kuongeza mkojo kwa kiwango cha wastani. Hali hii husaidia figo kuchuja na kutoa asidi ya uric kupitia mkojo, hivyo kupunguza hatari ya fuwele kujikusanya kwenye viungo na kupunguza dalili za gout.

2. Hurejesha madini na kudumisha usawa wa pH mwilini

Yakiwa na potasiamu na bicarbonate, maji ya nazi husaidia kudumisha mazingira ya alkali kidogo mwilini, jambo linalosaidia kuzuia asidi ya uric kuganda na kutengeneza fuwele. Pia husaidia kurejesha elektrolaiti kwa wagonjwa wanaotumia dawa za kuongeza mkojo.

3. Hupunguza uvimbe na maumivu

Maji ya nazi yana antioxidants na enzymes zinazosaidia kupunguza uvimbe mdogo kwenye viungo vilivyoathiriwa na gout. Ingawa hayawezi kuchukua nafasi ya dawa, yanaweza kusaidia kupunguza maumivu na kuzuia mashambulizi ya mara kwa mara ya gout.

4. Hupunguza hamu ya vinywaji hatarishi

Vinywaji kama soda zenye sukari nyingi na pombe huongeza kiwango cha asidi ya uric. Maji ya nazi ni mbadala mzuri kwani hayana purine, yana sukari kidogo asilia na husaidia kupunguza hamu ya kunywa vinywaji visivyofaa kwa wagonjwa wa gout.

5. Husaidia afya ya figo

Wagonjwa wa gout wako kwenye hatari ya matatizo ya figo kutokana na mkusanyiko wa muda mrefu wa asidi ya uric. Kunywa maji ya kutosha, yakiwemo maji ya nazi, husaidia figo kuchuja damu vizuri na kutoa sumu mwilini.

Ushauri wa Daktari

Dkt. Tung anashauri wagonjwa wa gout wasinywe maji ya nazi kupita kiasi. Kiasi kinachopendekezwa ni nazi moja ndogo kwa siku, ikinywewa asubuhi au mchana. Inashauriwa kuepuka kunywa maji ya nazi usiku ili kuzuia kwenda haja ndogo mara kwa mara.

Watu wenye kisukari, matatizo ya madini mwilini au magonjwa ya figo wanapaswa kushauriana na daktari kabla ya kuanza kunywa maji ya nazi mara kwa mara.

Mbali na hilo, wagonjwa wa gout wanashauriwa:

  • Kupunguza ulaji wa protini za wanyama

  • Kuepuka pombe

  • Kufanya mazoezi mepesi mara kwa mara

  • Kudhibiti uzito wa mwili

  • Kufanya vipimo vya mara kwa mara vya asidi ya uric, sukari na mafuta kwenye damu

Kwa kufuata ushauri wa kitaalamu na mtindo bora wa maisha, maji ya nazi yanaweza kuwa nyongeza salama na yenye manufaa katika kudhibiti gout.

Mpigie Kura Godmuya, Kura Yako Ni Ushindi! – Tuzo za Samia Kalamu Awards 2026

Global Publishers
September 21, 2026
2,598 views
0 Comments

Mtangazaji wa @globaltvonline na @255globalradio, Godfrey Nathan @godmuya ameteuliwa kuwania tuzo za Samia Kalamu Awards 2026.

Sasa Godmuya anaomba support yako, mfuatiliaji wa Global TV, kwa kumpigia kura ili kufanikisha ushindi wake.

🗳️ MPIGIE KURA: GODFREY LUHILABAKE NATHAN
🔢 Kodi: 260246

Kura yako ni mchango mkubwa kwa Godmuya katika safari hii ya tuzo.

🙏 Piga kura, share na mwambie mwingine apige kura!

Ruvuma Yakanusha Taarifa za Ununuzi wa Coaster kwa Milioni 334

Global Publishers
September 21, 2026
1,002 views
0 Comments

Songea, Ruvuma: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa imefanya ununuzi wa gari aina ya Toyota Coaster kwa gharama ya Shilingi milioni 334, ikielezwa kuwa taarifa hizo zinalenga kupotosha umma kuhusu ununuzi wa gari hilo.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Septemba 20, 2026, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma imeeleza kuwa gari hilo lenye namba za usajili STN 7615 lilinunuliwa jipya kupitia Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA) kwa gharama ya Shilingi milioni 334, likiwa halijawahi kutumika.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ununuzi wa gari hilo ulifanyika kwa kuzingatia taratibu za ununuzi wa Serikali na lengo lake ni kuboresha usafiri wa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na wadau wa maendeleo wanapotekeleza shughuli za maendeleo kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.

Gari hilo lenye uwezo wa kubeba abiria 30 pia linatarajiwa kupunguza matumizi ya fedha za Serikali, kwa kuwa litatumika kama mbadala wa matumizi ya magari mawili hadi matatu katika safari moja yenye idadi kubwa ya wasafiri.

Ofisi hiyo imewataka watumiaji wa mitandao ya kijamii, wadau wa habari, wanahabari na wananchi kwa ujumla kutumia uhuru wa kujieleza kwa kuzingatia ukweli na uchambuzi wa jambo ili kuepusha taharuki inayoweza kusababishwa na taarifa zisizo sahihi.

Aidha, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma imewataka wananchi kupuuza taarifa zinazosambaa mitandaoni zenye nia ya kupotosha ukweli kuhusu ununuzi wa gari hilo, na kusisitiza kuwa itaendelea kusimamia masilahi ya umma kwa uadilifu, huku ikiwataka wananchi kuwa watulivu.

RC Ruvuma Azindua Basi Jipya La Shilingi Milioni 334

Ushauri wa JKT kwa vijana kuhusu matumizi ya mitandao – HabariLeo

KIGOMA: Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele amewahimiza vijana wa Kitanzania kutumia mitandao ya kijamii kwa uangalifu na kuwasilisha ujumbe wenye manufaa kwa jamii na taifa.

Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Mujibu wa Sheria kupitia “Operesheni Linda Amani” na vijana wa Kujitolea kupitia “Operesheni Nishati Safi”, yaliyofanyika katika Kikosi cha Kanembwa JKT mkoani Kigoma.

Amesema somo la uzalendo na uzalendo wa kidijitali katika silabasi za mafunzo ya JKT litaendelea kupewa kipaumbele na kuboreshwa, kwa lengo la kuwaelimisha vijana kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.

Meja Jenerali Mabele amesema vijana wanapaswa kuepuka kurekodi na kusambaza maudhui yasiyofaa, ikiwemo matusi na ujumbe unaoweza kuleta migawanyiko katika jamii. Badala yake, amewataka kutumia mitandao hiyo kutangaza biashara, kutoa elimu na kusambaza ujumbe wenye tija kwa taifa.

SOMA: JKT mambo safi matumizi nishati safi

Katika hatua nyingine, ameiishukuru Serikali kwa kuendelea kuliwezesha JKT kuboresha miundombinu katika vikosi vyake ili kuongeza uwezo wa kutoa mafunzo kwa vijana wengi zaidi.

Mafunzo hayo yalianza Septemba 8, 2026 na yamekuwa ya kwanza kwa vijana wa Kundi la Lazima (Mujibu wa Sheria) Operesheni Linda Amani na Kundi la Kujitolea Operesheni Nishati Safi kuhitimisha mafunzo yao kwa pamoja.

Mbeya wajiweka sawa kukabiliana na El Nino – HabariLeo

MBEYA; SERIKALI imetoa vifaa vya ujenzi wa barabara kwa ajili ya maandalizi ya kukabiliana na mvua za El Niño mkoani Mbeya.

Vifaa hivyo,ambavyo ni  makaravati ya chuma vitatumika katika barabara kuu sita zinazounganisha Mkoa wa Mbeya na mikoa jirani.

Akizungumza wakati wa kupokea vifaa hivyo,  Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Suleiman Bishanga, amesema vifaa hivyo vimeletwa kwa ajili ya kudhibiti na kurekebisha miundombinu ya barabara, iwapo mvua hizo zitasababisha madhara kwenye miundombinu hiyo.

“Tumejipanga kikamilifu kuhakikisha barabara zinapitika wakati wote na shughuli za usafirishaji wa watu na bidhaa haziathiriki katika kipindi chote cha mvua,”amesema Mhandisi Bishanga.

Agosti 18, mwaka huu, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitabiri uwepo wa mvua za El Nino kwa kuwepo ongezeko la mvua za vuli (Oktoba – Desemba) kuwa za juu ya wastani hadi wastani katika maeneo mengi nchini.

Mvua hizo zinatarajia kuanza wiki ya nne ya Septemba hadi wiki ya kwanza ya Oktoba 2026 katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria. Hii itasambaa taratibu katika maeneo mengine katika Oktoba 2026.

Miss Kanda ya Mashariki waanzisha mwendo – HabariLeo

PWANI: Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Khadija Nassir Ali, amesema serikali itaendelea kuunga mkono mashindano ya Miss Tanzania kwa kuwa yanaendana na jitihada za kukuza sanaa na kuweka mazingira ya vijana kutumia vipaji vyao kupata fursa za kiuchumi.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Miss Tanzania Kanda ya Mashariki uliofanyika Kisemvule, Mkuranga mkoani Pwani Khadija amesema shindano hilo linahitaji kuungwa mkono na wadau na kampuni mbalimbali kuwasaidia wasichana kutimiza ndoto zao.

Amewataka wawekezaji na kampuni mbalimbali kujitokeza kudhamini Miss Kanda ya Mashariki akisema ushirikiano wa sekta binafsi utasaidia kufanikisha shindano hilo ambapo fainali yake itakuwa Oktoba 10, mwaka huu.

“Mkuranga ni historia kwetu kuasisi jambo hili kubwa, ambalo linaenda sambamba na sera ya serikali katika kuhakikisha tunaendelea kukuza sanaa na kuweka mazingira wezeshi kwa sanaa za aina zote kuibua ajira mbalimbali kwa vijana wetu, ili kufanikisha wadau wasapoti,” amesema.

Naye Yusuf Hassan, Mkurugenzi wa Miss Tanzania Kanda ya Mashariki, amesema mashindano hayo yatahusisha warembo kutoka Morogoro, Lindi, Mtwara na Pwani, huku warembo 16 watakaofaulu usaili wakitarajiwa kuingia kambini kuanzia Oktoba Mosi kwa ajili ya mafunzo mbalimbali.

Yusuf amesema bado wanahitaji wadhamini zaidi kwa kuwa bajeti ya mashindano hayo inakadiriwa kufikia takribani Sh milioni 210, hivyo kuomba kampuni na taasisi kujitokeza kuunga mkono.

 

Kwa upande wake, Aidan Rico, mwakilishi wa Kamati ya Miss Tanzania iliyo chini ya Lamata Village Entertainment Company Limited, Miss Kanda ya Mashariki imekuwa kanda ya kwanza kuzindua mashindano yake na kuwashukuru waandaaji pamoja na wadhamini waliojitokeza, huku akitoa wito kwa wadau wengine na serikali kuendelea kuunga mkono tasnia ya urembo.