Sh bilioni 2 zakabidhiwa kwa wanufaika wa utalii – HabariLeo

MOROGORO: MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imekabidhi Sh bilioni 2.47 kwa wanufaika wa mapato yatokanayo na shughuli za utalii kwa mwezi Julai 2026.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya TAWA mkoani Morogoro, Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA, Mlage Kabange, amesema Sh billioni 1,74 zimeelekezwa kwa Jumuiya 11 za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs); Sh millioni 354.94 kwa vijiji 18 na Sh millioni 379.2 kwa halmashauri 21 za wilaya.

Kabange amesema fedha hizo ni sehemu ya mapato yatokanayo na utalii ambayo hurejeshwa kwa jamii kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi na kuchochea utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mbali na hayo amesema katika mwaka wa fedha 2025/26 pekee, jumla ya Sh bilioni 12.17 zilitolewa kwa wanufaika wa shughuli za utalii.

Licha ya fedha hizo, TAWA imekabidhi ndege nyuki 27 kwa ajili ya kusaidia udhibiti wa wanyamapori wakali na waharibifu ambapo ndege 20 zimetolewa kupitia Mfuko wa Wanyamapori Tanzania (TWPF) mbili kutoka Bushman Safari Trackers Limited na tano kutoka TAWA.

Katika kuimarisha zaidi udhibiti wa wanyamapori wakali na waharibifu, TAWA imeongeza askari wapya 661 na kuwezesha Askari wa Vijiji 187 kushiriki katika shughuli hizo, sambamba na kuimarisha matumizi ya vitendeakazi na teknolojia.

Kabange amesema hatua hizo zinalenga kuhakikisha jamii zinapata manufaa ya moja kwa moja kutokana na uhifadhi, kuongeza ushiriki wa wananchi, kupunguza migongano kati ya binadamu na wanyamapori na kuchochea shughuli za kiuchumi.

Aidha, TAWA imetangaza namba maalum ya “TAWA NA JAMII” – 0800750440, kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano kati ya Mamlaka na wananchi katika kutoa taarifa na kuwasilisha changamoto zinazohusiana na shughuli za TAWA.

TBS yatoa mafunzo ya viwango Maonesho ya Madini Lindi – HabariLeo

LINDI; Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kuwa karibu na wajasiriamali wadogo nchini kwa kutoa elimu kuhusu viwango na ubora wa bidhaa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha kuzalisha bidhaa salama, zenye ubora na zinazoweza kushindana katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

TBS imetoa elimu hiyo katika Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji Lindi 2026, yanayofanyika Wilaya ya Ruangwa, Mkoa wa Lindi, ambapo wadau mbalimbali wamepata fursa ya kujifunza kuhusu viwango, taratibu za ubora wa bidhaa pamoja na umuhimu wa kuzingatia matakwa ya viwango katika uzalishaji na biashara.

Akizungumza katika maonesho hayo, Mhandisi Hemedy Hamim, Mkaguzi wa TBS Kanda ya Kusini, amesema TBS imeendelea kuwafikia wajasiriamali wadogo kwa kuwapatia elimu inayolenga kuwawezesha kuboresha bidhaa zao na kuingia katika masoko yenye ushindani.

Katika utekelezaji wa jukumu hilo, TBS imewatembelea na kuwapatia elimu wajasiriamali wanaojishughulisha na uzalishaji wa bidhaa za korosho, mafuta ya mwani, sabuni za mwani pamoja na Shower Jelly zinazotokana na mwani, huku ikiwahamasisha kuzingatia viwango vya ubora katika uzalishaji wao.

Hemedy amesema elimu hiyo pia inalenga kuwawezesha wajasiriamali kuelewa taratibu za kupata Alama ya Ubora ya TBS, ambayo ni muhimu katika kujenga uaminifu wa bidhaa kwa watumiaji na kuongeza uwezo wa bidhaa kufikia masoko mbalimbali.

TBS imeeleza kuwa kwa wajasiriamali wadogo, upatikanaji wa Alama ya Ubora unatolewa bila malipo, jambo linalolenga kuwawezesha wafanyabiashara hao wadogo kupata huduma za viwango na kuimarisha ubora wa bidhaa zao.

Katika kuwafikia kwa urahisi zaidi wajasiriamali hao, TBS imeshirikiana na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), ambapo ushirikiano huo umewezesha elimu ya viwango kuwafikia wajasiriamali wadogo wanaozalisha bidhaa mbalimbali, ikiwemo zile zinazotokana na mazao yanayopatikana katika maeneo yao.

TBS imewasisitiza wajasiriamali kutumia fursa hiyo kwa kuhakikisha bidhaa zao zinafuata taratibu zinazotakiwa na kupata Alama ya Ubora, kwani hatua hiyo inaweza kuongeza uaminifu wa bidhaa kwa walaji na kuwawezesha kutafuta fursa za masoko mapana zaidi.

Mmoja wa wajasiriamali walionufaika na elimu na huduma za TBS, Zena Adam, mbanguaji wa korosho kutoka Nachingwea, ambaye baada ya kufuata taratibu zilizowekwa na TBS alifanikiwa kupata Alama ya Ubora kwa bidhaa yake.

Zena ameishukuru TBS kwa elimu na maelekezo aliyopatiwa katika hatua mbalimbali, akieleza kuwa mafunzo hayo yamemsaidia kuelewa umuhimu wa ubora na taratibu zinazotakiwa katika uzalishaji.

Kwa mujibu wa  Zena, kupata Alama ya Ubora ya TBS ni hatua muhimu kwake kama mjasiriamali, kwani anaamini itasaidia kuongeza uaminifu wa bidhaa zake na kumfungulia fursa za masoko kutoka nje ya Mkoa wa Lindi hadi katika masoko ya kimataifa.

Kwa upande wake, Fatma Machalila, ambaye ni miongoni mwa wajasiriamali walionufaika na elimu hiyo, ameipongeza TBS kwa kuendelea kuwafikia wajasiriamali wadogo na kutoa elimu kuhusu uzalishaji wa bidhaa bora.

Ushiriki wa TBS katika Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji Lindi 2026 umeendelea kuonesha umuhimu wa taasisi hiyo kuwa karibu na wazalishaji na wajasiriamali, si kwa kutoa huduma za viwango pekee, bali pia kwa kutoa elimu inayowawezesha kuelewa namna ubora unavyoweza kuwa sehemu muhimu ya ukuaji wa biashara zao.

CCM yataka uwajibikaji miradi Temeke – HabariLeo

DAR ES SALAAM: Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM ambaye pia ni Mlezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kenani Kihongosi, ameitaka TARURA na uongozi wa Wilaya ya Temeke kuchukua hatua dhidi ya mkandarasi Group Six International Limited, kutokana na kutoridhishwa na utendaji wake katika ujenzi wa barabara.

Kihongosi ameyasema hayo wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Masaki, akieleza kuwa Temeke imepatiwa miradi ya barabara yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 92, inayohusisha zaidi ya kilomita 55, ambapo kilomita 32 ziko katika hatua za ujenzi.

Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Temeke, Mhandisi Janeth Mwandiga, amesema mkandarasi huyo anasimamia ujenzi wa barabara za Masuliza yenye urefu wa kilomita 4.04 na Kilimahewa kilomita 7.382, kwa gharama ya Sh bilioni 25.9.

Kwa upande mwingine, Mbunge wa Mbagala, Kakulu Burchard, amesema ujenzi wa hospitali ya ghorofa saba yenye thamani ya Sh bilioni 17.7 unaendelea, huku ukitarajiwa kuongeza upatikanaji wa huduma za afya, ikiwemo matibabu ya kibingwa.

Naye, Mbunge wa Temeke, Mariam Kisanga, amesema Serikali inaendelea kujenga shule za msingi na sekondari, ikiwemo majengo ya ghorofa, kwa lengo la kuboresha mazingira ya elimu.

Akihitimisha ziara yake kwa mkutano wa hadhara Masuliza, Tuangoma, Kihongosi amewataka wananchi kudumisha amani na mshikamano, akisisitiza umuhimu wa utulivu katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

 

MAGAZETINI LEO JUMATATU SEPT 21/2026:SAKATA LA KOROSHO CHINI YA KIWANGO CHA UBORA,WAHITIMU KIGONZOLE :WAZAZI WANA MCHANGO MKUBWA MAADILI KWA WATOTO

MAGAZETINI LEO JUMATATU SEPT 21/2026:SAKATA LA KOROSHO CHINI YA KIWANGO CHA UBORA,WAHITIMU KIGONZOLE :WAZAZI WANA MCHANGO MKUBWA MAADILI KWA WATOTO

 

 MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA 

 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)

TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

3:TUZO YA AFYA

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .

🚨ZIMEBAKI SIKU 9 ZOEZI KUFUNGWA

Wezesha Mzawa Insurance Broker Watangaza Nafasi Nne za Kazi

Kampuni ya Wezesha Mzawa Insurance Broker Limited imetangaza nafasi za kazi kwa Watanzania wenye sifa na uzoefu katika sekta ya bima, mauzo, masoko, biashara, uhasibu na nyanja zinazohusiana.

Nafasi zilizotangazwa ni Business Development Executive, Accountant pamoja na Insurance Sales Executives, huku waombaji wakitakiwa kutimiza vigezo vilivyowekwa kwa kila nafasi.

1. Business Development Executive

Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Kwanza katika Insurance and Risk Management, Sales and Marketing, Business Administration au fani nyingine inayohusiana, pamoja na uzoefu wa angalau miaka miwili katika sekta ya bima, maendeleo ya biashara, mauzo au masoko.

2. Accountant

Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Kwanza katika Accounting au Finance, pamoja na uzoefu wa angalau miaka miwili katika sekta ya bima. Sifa ya CPA ni nyongeza.

3. Insurance Sales Executives

Waombaji wanatakiwa kuwa na Cheti katika Insurance and Risk Management, Sales, Marketing, Business Administration au fani nyingine inayohusiana.

Uzoefu katika sekta ya bima na kazi za mauzo ni nyongeza.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi yao pamoja na viambatisho muhimu vilivyothibitishwa kupitia barua pepe au kwa anuani ya ofisi ya kampuni kabla ya Septemba 30, 2026.

Wezesha Mzawa Insurance Broker Limited
P.O. Box 7534, Sinza Mori
Global Group House/Building, Opposite Wanyama Hotel
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: [email protected]

RC Ruvuma Azindua Basi Jipya La Shilingi Milioni 334

Global Publishers
September 20, 2026
0 views
0 Comments

SONGEA, RUVUMA — Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, amezindua basi jipya aina ya Coaster lenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 334, lililonunuliwa kwa ajili ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

Basi hilo limekabidhiwa rasmi kwa ofisi hiyo kwa lengo la kuboresha huduma za usafiri na kurahisisha shughuli za kikazi, hususan safari za watumishi katika ziara mbalimbali.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika Ukumbi wa Songea Club, RC Ahmed amewataka madereva kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani, pamoja na kuhakikisha gari hilo linafanyiwa matengenezo kwa wakati.

Amesema fedha zilizotumika kununua basi hilo ni za walipa kodi, hivyo watumishi wana wajibu wa kulilinda na kuhakikisha linatumika kwa manufaa ya umma.

RC Ahmed amesisitiza kuwa kuharibika kwa gari hilo mapema kutakuwa hasara kwa wananchi ambao wamechangia kupitia kodi zao.

Kwa upande wake, Katibu Tawala Msaidizi wa Utawala na Rasilimali Watu, Joel Mbewa, amesema basi hilo litasaidia kupunguza changamoto za usafiri zilizokuwa zikiikabili ofisi hiyo.

Amesema basi hilo litatumika kusafirisha watumishi kwa pamoja wakati wa ziara mbalimbali, jambo ambalo litasaidia kupunguza gharama za misafara.

Mbewa ameahidi kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itahakikisha basi hilo linatunzwa ipasavyo, likifanyiwa service kwa wakati na kuendeshwa kwa kuzingatia sheria na kanuni zote za usalama barabarani.

WAHITIMU KIDATO CHA NNE KIGONZILE SEKONDARI WAWAPONGEZA WAZAZI, WAAHIDI KUFANYA VIZURI

Askofu wa kanisa la Romani Katoliki Jimbo la Iringa Romanus Mihali ambae alikuwa mgeni rasimi kwenye mahafali ya kidato cha nne Kigonzile Sekondari akimkabidhi cheti cha kuhitimu mwanafunzi Jimmy Edward Uphoro ,kulia ni mkurugenzi wa shule hizo Father Aidan Ulungi 

Na Matukio Daima Media , Iringa

WAHITIMU wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Kigonzile, Manispaa ya Iringa, wamewapongeza wazazi na walezi wao kwa kujitoa kuwasomesha katika shule hiyo yenye mazingira mazuri ya kujifunzia, huku wakiahidi kufanya vizuri katika Mtihani wa Taifa.

Wakizungumza  na Matukio Daima Media baada ya sherehe za mahafali zilizofanyika shuleni hapo jana, wahitimu Jimmy Edward Uphoro na Brian Baraka Mbangalala walisema wamejengwa vyema kielimu, kinidhamu na kimaadili katika kipindi chote cha miaka minne ya masomo yao.

Walisema tangu walipojiunga na Kidato cha Kwanza hadi kuhitimu Kidato cha Nne, hawajawahi kujutia uamuzi wa wazazi wao wa kuwapeleka kusoma katika shule hiyo kutokana na malezi bora na ufundishaji wenye weledi walioupata.

Uphoro alisema walimu wa shule hiyo wamekuwa wakitimiza wajibu wao kwa uadilifu na kujenga uhusiano wa karibu na wanafunzi, hali iliyowapa uhuru wa kuuliza maswali na kuomba msaada kila walipokutana na changamoto za kitaaluma au kijamii.

Alisema mazingira hayo yaliwasaidia wanafunzi kuongeza bidii katika masomo, kupenda kujisomea na kuelewa kwamba ufaulu mzuri haupatikani kwa bahati, bali unatokana na nidhamu, juhudi, ushirikiano na matumizi sahihi ya muda.

“Walimu wetu wamekuwa marafiki wa karibu wa wanafunzi. Kila tulipokwama katika jambo fulani tuliweza kuwafuata, kuwauliza na kupata majibu pamoja na maelekezo yaliyotusaidia kuendelea na masomo yetu,” alisema Uphoro.

Aliongeza kuwa njia bora ya kuwashukuru wazazi wao ni kufanya vizuri katika mitihani, kuendelea kuwa na tabia njema na kulitunza jina la shule hata baada ya kumaliza masomo yao.

“Kwa kujitolea kwa wazazi wetu kutusomesha hadi hapa tulipofika, zawadi kubwa tunayowaahidi ni kufanya vizuri katika Mtihani wa Taifa. Heshima kubwa kwa shule yetu ni sisi wahitimu kufaulu,” alisema.

Uphoro aliwashauri wazazi wanaotafuta shule zenye malezi bora, nidhamu na elimu yenye kiwango kizuri kuwapeleka watoto wao katika Shule ya Sekondari Kigonzile na Shule ya Msingi St. Dominic.

Kwa upande wake, mhitimu Brian Baraka Mbangalala alisema wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne kutokana na maandalizi waliyopata kutoka kwa walimu wao.

Aliomba wazazi, walezi na jamii kuendelea kuwaombea afya njema na mafanikio wakati wote wa maandalizi na kipindi cha kufanya mitihani yao.

Mbangalala alisema msaada wa wazazi haukuishia katika kulipa ada na michango mbalimbali, bali ulihusisha pia ushauri, maombi, ufuatiliaji wa maendeleo yao na kuwahamasisha kutokata tamaa walipokutana na changamoto.

Aliwahimiza wanafunzi wanaoendelea na masomo shuleni hapo kutumia vizuri nafasi waliyopewa, kuwaheshimu walimu, kusoma kwa bidii na kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha ndoto zao.

Awali, Mkurugenzi wa Shule za Kigonzile na St. Dominic, Padri Aidan Ulungi, alisema mafanikio yanayopatikana katika shule hizo yanatokana na ushirikiano mkubwa kati ya uongozi, walimu, wazazi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa elimu.

Alisema wazazi wameendelea kuonesha imani kwa shule hizo kwa kuwapeleka watoto wao kupata elimu, huku walimu wakijitahidi kuhakikisha wanafunzi wanapata maarifa, nidhamu na misingi bora ya maisha.

Padri Ulungi alisema shule hizo zitaendelea kuimarisha mazingira ya kufundishia na kujifunzia ili kuwajenga wanafunzi wenye uwezo wa kujitegemea, kulitumikia taifa na kukabiliana na ushindani wa kielimu na kiteknolojia.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Iringa, Romanus Mihali, aliwapongeza wazazi kwa kuendelea kuziamini shule hizo na kuwasihi kuwa mabalozi wa kuzitangaza kwa jamii.

Askofu Mihali alisema mafanikio ya taasisi za elimu yanahitaji ushirikiano wa wadau wote, hivyo akawaomba wananchi, waumini na wahitimu wa zamani kuendelea kuzisaidia shule hizo katika kuimarisha miundombinu na huduma za elimu.

Aliwataka waliosoma katika shule za St. Dominic na taasisi nyingine zinazosimamiwa na Kanisa kurejea na kutoa mchango wao kwa namna mbalimbali ili kuwasaidia wanafunzi wa sasa na vizazi vijavyo.

Vilevile, Askofu Mihali aliwapongeza walimu kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwaandaa wanafunzi kitaaluma na kuwajengea misingi ya nidhamu, uadilifu, uwajibikaji na hofu ya Mungu.

Aliwahimiza wahitimu kutambua kwamba kumaliza Kidato cha Nne si mwisho wa safari yao ya elimu, bali ni hatua muhimu inayowaandaa kuingia katika ngazi nyingine za masomo na maisha.

Pia aliwataka kuepuka makundi yasiyofaa, matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na tabia zinazoweza kuharibu malengo yao, huku akisisitiza umuhimu wa kusikiliza ushauri wa wazazi na walimu.

Aidha, Askofu Mihali alipongeza jitihada za Serikali ya Tanzania za kuendelea kuwekeza katika sekta ya elimu na kuiweka elimu miongoni mwa maeneo muhimu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Alisema kila mwananchi ana wajibu wa kushiriki katika utekelezaji wa dira hiyo kwa kuwa maendeleo ya taifa yanategemea uwepo wa jamii iliyoelimika, yenye maadili, ubunifu na uwezo wa kutumia maarifa kutatua changamoto.

Askofu Mihali alisema Kanisa Katoliki litaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine katika kutoa elimu bora inayolenga kumjenga mwanafunzi kitaaluma, kiroho, kimwili na kimaadili.

TANGAZO LA SHULE

Ruvuma Yakanusha Taarifa za Ununuzi wa Coaster kwa Milioni 334

Global Publishers
September 20, 2026
18 views
0 Comments

Songea, Ruvuma: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa imefanya ununuzi wa gari aina ya Toyota Coaster kwa gharama ya Shilingi milioni 334, ikielezwa kuwa taarifa hizo zinalenga kupotosha umma kuhusu ununuzi wa gari hilo.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Septemba 20, 2026, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma imeeleza kuwa gari hilo lenye namba za usajili STN 7615 lilinunuliwa jipya kupitia Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA) kwa gharama ya Shilingi milioni 334, likiwa halijawahi kutumika.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ununuzi wa gari hilo ulifanyika kwa kuzingatia taratibu za ununuzi wa Serikali na lengo lake ni kuboresha usafiri wa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na wadau wa maendeleo wanapotekeleza shughuli za maendeleo kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.

Gari hilo lenye uwezo wa kubeba abiria 30 pia linatarajiwa kupunguza matumizi ya fedha za Serikali, kwa kuwa litatumika kama mbadala wa matumizi ya magari mawili hadi matatu katika safari moja yenye idadi kubwa ya wasafiri.

Ofisi hiyo imewataka watumiaji wa mitandao ya kijamii, wadau wa habari, wanahabari na wananchi kwa ujumla kutumia uhuru wa kujieleza kwa kuzingatia ukweli na uchambuzi wa jambo ili kuepusha taharuki inayoweza kusababishwa na taarifa zisizo sahihi.

Aidha, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma imewataka wananchi kupuuza taarifa zinazosambaa mitandaoni zenye nia ya kupotosha ukweli kuhusu ununuzi wa gari hilo, na kusisitiza kuwa itaendelea kusimamia masilahi ya umma kwa uadilifu, huku ikiwataka wananchi kuwa watulivu.

Man City Yashinda 5-3, Haaland Aweka Rekodi Afunga Bao la 10

Global Publishers
September 20, 2026
0 views
0 Comments

MANCHESTER, England — Manchester City imepata ushindi wa mabao 5-3 dhidi ya Sunderland katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Etihad, Septemba 20, 2026, katika mchezo uliokuwa na drama kubwa.

Erling Haaland ndiye aliyehitimisha mchezo huo kwa kufunga bao la tano la City dakika ya 82, likiwa bao lake la 10 msimu huu. Ushindi huo umeifanya City kufikisha ushindi wa saba mfululizo chini ya kocha mpya Enzo Maresca.

Sunderland, licha ya kupoteza mchezo huo, ilitoa upinzani mkubwa huku mshambuliaji wake Brian Brobbey akifunga hat-trick. Mabao hayo yalikuwa ya kwanza kwake msimu huu, huku akiwa mchezaji wa kwanza baada ya miaka 19 kufunga hat-trick dhidi ya Manchester City na timu yake bado kupoteza mchezo huo.

City ilianza kupata bao kupitia Enzo Fernández ndani ya dakika 10, lakini Sunderland ilisawazisha dakika chache baadaye kupitia Brobbey.

Rayan Cherki aliirejesha City mbele kabla ya Brobbey kusawazisha tena. Antoine Semenyo kisha akaifungia City bao la tatu kabla ya mapumziko.

Katika kipindi cha pili, Semenyo aliongeza bao lake la pili na kuifanya City kuongoza 4-2. Hata hivyo, Brobbey alikamilisha hat-trick yake muda mfupi baadaye na kupunguza tofauti kuwa bao moja.

Sunderland iliendelea kutafuta bao la kusawazisha, lakini Haaland akamaliza matumaini hayo kwa kufunga bao la tano la City dakika nane kabla ya mchezo kumalizika.

Ushindi huo pia umeweka historia kwa Haaland, kwani Sunderland ndiyo ilikuwa timu pekee katika Ligi Kuu England ambayo alikuwa hajawahi kuifunga. Kwa bao hilo, sasa amefunga dhidi ya kila timu ya Premier League aliyokutana nayo.

Matokeo hayo yanaifanya Manchester City kuendelea na rekodi ya asilimia 100 ya ushindi katika michezo saba ya kwanza chini ya Maresca, huku ikipanda hadi kileleni ikiwa na tofauti ya pointi tatu.

Rais Samia Akutana na Makamu wa Rais Mstaafu wa Uganda

Global Publishers
September 20, 2026
30 views
0 Comments

 Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa kwenye mazungumzo na Dkt. Speciosa Kazibwe Wandira, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Uganda, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 20 Septemba, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Uganda, Dkt. Speciosa Kazibwe Wandira.

Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 20, 2026.

Mkutano huo ni sehemu ya shughuli za Rais Samia katika kuendelea kupokea na kufanya mazungumzo na viongozi na wageni mbalimbali wanaofika nchini Tanzania.