Lissu Ahoji Kisheria Maneno Yanayodaiwa Kuunda Kosa la Uhaini

DAR ES SALAAM, Septemba 24, 2026 — Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ameendelea kutoa majumuisho yake ya mwisho katika kesi ya uhaini inayomkabili, akisisitiza kuwa Mahakama inapaswa kutathmini kama maneno anayodaiwa kuyasema yanaweza, kwa mujibu wa sheria, kuunda kosa la jinai linalomkabili.

Lissu ametoa hoja hizo mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu, akiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, katika hatua ya mwisho ya kesi hiyo. Anashtakiwa kwa kosa la uhaini chini ya kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, kuhusiana na madai ya kuchochea umma kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Katika majumuisho yake, Lissu amesema hoja yake siyo tu kuhusu iwapo alitamka maneno yanayodaiwa na upande wa mashtaka, bali kama maneno hayo, yakitazamwa pamoja na mazingira yaliyotolewa, yanatimiza vipengele vinavyotakiwa kisheria kuthibitisha kosa la uhaini.

Amesema maneno yanayodaiwa kutamkwa katika mkutano wa Aprili 3, 2025, yakiwemo madai ya “tutazuia uchaguzi”, “tutahamasisha uasi” na “tutakinukisha vibaya”, hayajafafanuliwa na upande wa mashtaka kuhusu namna yanavyounda kosa la jinai.

Kwa mujibu wa Lissu, si wajibu wa mshtakiwa kufafanua kwa niaba ya upande wa mashtaka maana ya maneno hayo au kueleza kwa nini hayakuwa kosa. Amesema jukumu hilo liko kwa upande wa mashtaka kuonyesha kwa ushahidi kwamba maneno hayo yanatimiza masharti ya kosa analoshtakiwa.

Lissu pia amejikita katika hoja ya madai kwamba maneno yake yalilenga kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amehoji ni chombo gani au kiongozi gani wa Serikali anayedaiwa kutishiwa, akitaja kwa mfano Rais, Makamu wa Rais, Serikali yenyewe au taasisi nyingine.

Hoja hiyo inaendana na hoja aliyoiwasilisha katika siku ya kwanza ya majumuisho, ambapo alisema hati ya mashtaka haijaeleza kwa usahihi ni sehemu gani ya Serikali iliyodaiwa kutishiwa.

Lissu pia amesema katika maneno yanayodaiwa kutamkwa hakuna mahali ambapo ametaja Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais, Makamu wa Rais au kiongozi mwingine wa Serikali.

Kwa upande wake, upande wa mashtaka unasema mazingira na maudhui ya kauli hizo yanaonyesha dhamira ya kutishia Serikali na kuzuia uchaguzi.

Katika kuchambua ushahidi, Lissu amesema ushahidi wa baadhi ya mashahidi wa Jamhuri unatofautiana kuhusu maana ya maneno aliyodaiwa kuyasema.

Ametaja PW1, PW2 na PW16 kama mashahidi waliotoa tafsiri kwamba kauli hizo zilihusisha tishio kwa Serikali, huku akisema PW17, ambaye alikuwa katika mkutano huo, hakutoa tafsiri hiyo.

Kwa mujibu wa Lissu, PW17 alikuwepo kwenye mkutano wa Aprili 3, 2025 na alisikiliza yaliyokuwa yakijadiliwa, ikiwemo sera ya CHADEMA ya “No Reform, No Election.”

Lissu amesema ushahidi wa PW17 unaunga mkono hoja ya utetezi kwamba mkutano huo ulihusisha mjadala kuhusu sera ya chama na changamoto za mfumo wa uchaguzi.

“Kesi imejengwa kwenye hisia”
Lissu amesema anachopinga ni tafsiri ya upande wa mashtaka kwamba kauli hizo zilikuwa na nia ya kuitishia Serikali.

Amedai kuwa msingi huo unatokana na hisia au tafsiri ya mashahidi badala ya ushahidi unaoonyesha moja kwa moja nia hiyo.

Amesema ushahidi wa upande wa utetezi unaonyesha kuwa lengo lake lilikuwa kueleza msimamo wa CHADEMA kuhusu mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi na sera ya “No Reform, No Election”, na kwamba hakulenga kuitishia Serikali wala kuhamasisha vurugu.

Katika hatua hiyo, Lissu pia amesisitiza kuwa Mahakama inapaswa kuzingatia ushahidi uliotolewa na pande zote kabla ya kufikia hitimisho kuhusu nia yake.

Arejea kesi ya Freeman Mbowe
Lissu amerejea pia uamuzi wa Mahakama katika kesi iliyomhusu aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, akisema uamuzi huo una umuhimu katika hoja yake kuhusu ulazima wa hati ya mashtaka kueleza kwa uwazi tuhuma zinazomkabili mshtakiwa.

Amesema sheria inapaswa kumpa mtu anayeshtakiwa taarifa ya kutosha kuhusu kosa analodaiwa kutenda ili aweze kuandaa utetezi wake.

The Chanzo imeripoti kuwa Lissu alitumia pia uamuzi wa Isdory Patrice kuunga mkono hoja kwamba mshtakiwa anapaswa kupewa maelezo ya kutosha ya tuhuma ili aweze kujitetea ipasavyo.

Kesi iko hatua ya mwisho
Upande wa Jamhuri ulifunga ushahidi wake Agosti 17, 2026 baada ya kuwaita mashahidi 17 kati ya 30 waliokuwa wameorodheshwa. Mahakama baadaye iliamua kuwa Lissu ana kesi ya kujibu, na upande wa utetezi ukafunga ushahidi wake Septemba 18.

Kwa sasa, pande zote zinaendelea na majumuisho ya mwisho kabla ya jopo la majaji kufanya tathmini ya hoja na ushahidi uliowasilishwa.

Lissu amesema uamuzi wa kesi hiyo hautamhusu yeye pekee, bali unaweza pia kuweka msingi wa kisheria utakaozingatiwa katika kesi zijazo.

Stori na mwandishi Wetu

Haaland Kuongoza Mashambulizi ya Norway dhidi ya Denmark

Je unajua kuwa siku ya leo unaweza ukaondoka na kitita cha mkwanja wa maana ukibashiri mechi zako sasa. Mechi nyingi kupigwa kwenye viwanja mbalimbali huku wewe kwa dau dogo tuu unaibuka bingwa.

Norway atamleta kwake Denmark kwenye michuano hii ya UEFA Nations League ambapo wenyeji wanaingia kwenye mchezo huu wakihitaji kufanya mashambulizi zaidi kwenda kwa mpinzani kwani wana mshambuliaji hatari Duniani Erling Haaland na ni salaha kubwa sana kwenye kikosi hicho.

Ukiachilia kuwa na mshambuiliaji huyo, pia wana wachezaji wenye uwezo wa kuleta kasi pembeni na kusaidia kutengeneza nafasi, huku Martin Ødegaard akiwa muhimu katika kuunganisha kiungo na safu ya ushambuliaji.

Kinachoweza kuwa muhimu ni namna Norway itakavyomtafuta Haaland. Ikiwa Denmark itafanikiwa kumtenga na mipira, Norway inaweza kulazimika kutumia zaidi mashambulizi ya pembeni.

Huku Denmark wao wanaingia kwenye mchezo wakiwa na uzoefu mkubwa wa kucheza mechi za kiwango hiki. Hii si timu inayotegemea mchezaji mmoja pekee; nguvu yake kubwa ipo katika mpangilio wa timu, matumizi mazuri ya mpira na uwezo wa kucheza kwa nidhamu.

Mkwanja mrefu upo kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Eneo la kiungo litakuwa muhimu sana. Denmark ikifanikiwa kudhibiti tempo na kuwazuia Ødegaard pamoja na viungo wa Norway kupata nafasi ya kupiga pasi za mwisho, itapunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya Haaland.

Lakini Denmark pia lazima iwe makini inapopoteza mpira. Norway ina uwezo wa kubadilisha mchezo kutoka kujilinda kwenda kushambulia kwa kasi, hasa ikiwa Ødegaard atapata nafasi ya kuanzisha mashambulizi.

Mechi mbili za mwisho kukutana kati yao Denmark aliondoka na ushindi, hivyo hii ni mechi ya kisasi kwa kina Haaland na wenzake. Suka jamvi hapa.

Mechi nyingine ni hii ya Uholanzi dhidi ya Ujerumani huku timu zote mbili zikiwa zimejiandaa vyema kabisa kupata ushindi mnono kwenye hili Kundi lao ambalo wapo.

Timu zote mbili zina makocha wapya hivyo hii inakuwa mara yao ya kwanza kukutana ambapo kocha wa Uholanzi ni Xavi Hernandez ambaye amekabidhiwa kijiti cha kuinoa timu hiyo, huku kwa upande wa Ujerumani wao wana Jurgen Klopp ambaye anahitaji kurejesha matumaini kwa klabu hiyo kubwa Duniani.

Hii ni mechi ya kwanza wa Xavi Hernandez akiwa na Uhalonzi kama tunavyojua ni kocha ambaye anapenda timu icheze kwa kumiliki mpira na kushambulia lango la mpinzani inapopata nafasi hiyo. Lakini pia timu hiyo ina wachezaji wakubwa na wenye uwezo mzuri akiwepo Van Dijk, De Jong, Gakpo Memphis Depay na wengine wengi.

Vilevile kwa upande wa Jurgen Klopp hii ni mechi yake ya kwanza akiwa kama kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Ujerumani baada ya kuchukua mikoba ya Nagelsmann huku kocha huyo mwenye mafanikio makubwa akiwa ni tumaini kwenye Taifa hilo.

Ujerumani wakiwa kama washindi wa Kombe la Dunia 2014 wana wachezaji wenye uwezo mkubwa kabisa kama vile Joshua Kimmich, Musiala, Floarian Wirtz, Hevertz na wengine wengi ambao wanaungana kutengeneza kikosi hiki chenye uwezo mkubwa kabisa Duniani.

Uholanzi itataka kumiliki mpira na kujenga mashambulizi kwa utulivu, wakati Ujerumani chini ya Klopp inaweza kutafuta kutumia presha zaidi kwenda kwa mpinzani wao.

Kwa upande mwingine, kama Ujerumani itaruhusu Uholanzi kumiliki mpira kwa muda mrefu bila kuweka presha sahihi, De Jong, Reijnders na Gravenberch wanaweza kuanza kuutawala mchezo. Jisajili hapa.

Timu hizi mbili zimeshakutana sana na mara ya mwisho Ujerumani ndiye ambaye aliibuka mshindi. Je leo hii nani ataibuka na ushindi?. Odds Kubwa zipo kwenye mechi hii, hivyo bashiri sasa.

Video: Makonda Afichua Gharama za Tanzania Kuwa Mwenyeji Wa Afcon 2027

DAR ES SALAAM, Septemba 24, 2026 — Serikali ya Tanzania imelipa Dola za Marekani milioni 32, sawa na takriban Shilingi bilioni 74, kwa ajili ya kupata uenyeji wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda, amesema hayo leo, Septemba 24, 2026, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu uwekezaji wa Serikali katika sekta ya michezo na usimamizi wa nembo za taifa.

Kwa mujibu wa Makonda, fedha hizo ni sehemu ya gharama za kuipatia Tanzania uhalali wa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo, na si fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanja, barabara au miundombinu mingine.

“Tumelipa sisi taifa kuwa wenyeji wa AFCON milioni 32, sawa na takriban bilioni 74. Hii ni pesa ya kuwa tu mwenyeji,” amesema Makonda.

Makonda amesema Serikali pia ipo katika mazungumzo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuhusu malipo ya Dola za Marekani milioni 12, sawa na takriban Shilingi bilioni 30, kwa ajili ya kupata haki za matangazo ya televisheni za AFCON 2027.

Amesema uwekezaji huo unaangaliwa kwa mtazamo mpana zaidi ya michezo, ikiwemo kuitangaza Tanzania kimataifa, kukuza utalii na kuvutia wawekezaji.

“Fedha hizi sio za kujenga uwanja, sio za kununua maji, sio za kujenga barabara. Kama nchi tumelipa ili tupate uhalali wa ku-host haya mashindano,” amesema.

Ameongeza kuwa Tanzania inatarajia kutumia fursa ya mashindano hayo kuitangaza nchi na kuonyesha fursa zilizopo kwa wageni na wawekezaji watakaofika nchini.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, uwekezaji huo pia unalenga kuchochea shughuli za kiuchumi na kusaidia kuongeza fursa za ajira kwa vijana.

Akizungumzia suala la jezi ya Taifa Stars, Makonda amesema kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika kuiwakilisha Tanzania kwenye jukwaa la kimataifa, jezi ya timu hiyo inapaswa kupewa thamani na uzito unaostahili.

Amesema jezi ya Taifa Stars ni miongoni mwa alama zinazotambulisha Tanzania na hivyo suala la uzalishaji, utambulishaji na uuzaji wake linapaswa kufanyika kwa utaratibu rasmi.

Makonda amesisitiza kuwa jezi hiyo haipaswi kuchukuliwa kama bidhaa ya kawaida, bali inapaswa kuangaliwa pia kama sehemu ya nembo ya taifa na fursa ya kuitangaza Tanzania.

Kauli hiyo imekuja wakati Tanzania ikiendelea na maandalizi ya AFCON 2027, ambayo inatarajiwa kuwa moja ya matukio makubwa ya michezo yatakayoiweka nchi katika uangalizi wa kimataifa.

Amsha Nguvu ya Totem na Volcano Inayosubiri Mlipuko wa Mara 6,750

Global Publishers
September 24, 2026
24 views
0 Comments

Usiku unapokuwa kimya, Volcano bado huwa na nguvu zake ndani kabisa. Ndivyo ilivyo kwenye mchezo huu wa kasino kutoka Meridianbet, ambapo Totem Wild anaweza kujitokeza wakati wowote na kuleta kizidishi cha mara 2 au 3. Ni mwanzo wa safari ambayo kila raundi inaweza kuleta mabadiliko na kuongeza msisimko.

Kama Totem mmoja ni mwanzo, wawili au watatu kwenye mstari mmoja ni nguvu nyingine kabisa. Vizidishi vyake ujikusanya kwa pamoja na hii inafanya kiwango cha malipo kuendelea kupanda kadri nguvu hizo zinavyoungana. Hapo mchezo unaanza kupata ladha ya kweli, kwa sababu kila Totem anayefika anaweza kuongeza uzito wa tukio linalofuata.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Lakini kuna hatua ambayo inaweza kubadilisha kabisa mazingira, ni hatua ya kuamsha Volcano. Ikianza kulipuka, bonasi za mizunguko zinaingia na safari inaendelea kwa kasi mpya. Kila raundi inakuwa kama mlango mwingine wa sapraizi, huku Totem zaidi wakitafutwa ili kuongeza nguvu ya mlipuko.

Na mwisho wa safari hiyo kuna namba inayovutia macho, kizidishi cha mara 6,750. Hicho ndiyo kiwango ambacho mchezo unaweza kufikia, huku idadi kubwa ya Totem wanaoitikia wito ikimaanisha mlipuko wenye nguvu zaidi. Hakuna anayejua raundi inayofuata italeta nini, na hapo ndipo burudani inapopata ladha yake.

Sasa ni wakati wa kuamsha Totem na kuacha Volcano ifanye kazi yake. Fungua safari yako ndani ya Meridianbet, fuatilia vizidishi vikijikusanya na mizunguko ya bonasi ikimiminika.

Wananchi Pagwi waiomba Serikali kukamilisha zahanati – HabariLeo

TANGA: WANANCHI wa Kijiji cha Pagwi, wilayani Kilindi, mkoani Tanga, wameiomba Serikali kusaidia kukamilisha ujenzi wa zahanati yao ulioanza mwaka 2018 kwa nguvu zao wenyewe, wakieleza kuwa ukosefu wa huduma za afya karibu umekuwa changamoto kubwa, hususan kwa wanawake wajawazito.

Wananchi hao walisema hulazimika kutembea takribani kilomita nne kufuata huduma za afya katika vijiji jirani, huku hali ya barabara ikiongeza ugumu wa kuwafikisha wagonjwa hospitalini kwa wakati.

Walisema changamoto hiyo imekuwa na madhara kwa wajawazito, ambapo ndani ya mwaka huu wanawake watatu wamejifungua njiani wakati wakielekea kutafuta huduma za afya.

Akijibu kero hiyo, Mtendaji wa Kata ya Pagwi, Mustapha Msingwa, alisema Halmashauri tayari imetenga Sh milioni 20 kwa ajili ya kusaidia kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kilindi, Saleh Mhando, alisema kiasi kingine cha shilingi milioni 30 kimetengwa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.

Katika kuunga mkono juhudi za wananchi, Mhando ametoa shilingi laki tano pamoja na mifuko 50 ya saruji, ambayo itatumika katika hatua ya upigaji lipu ya jengo hilo.

Wananchi hao sasa wanasubiri kukamilishwa kwa fedha zilizotengwa na Halmashauri ili ujenzi wa zahanati hiyo uweze kukamilika na kuwawezesha kupata huduma za afya karibu na makazi yao.

Chagua Chaguo Lako na Bashiri Mechi za UEFA Nations League

Mechi za Mataifa mengi hatimaye zimewadia na timu kibao zimejiandaa kwaajili ya kukupatia maokoto ya maana. Je nani unampa nafasi kubwa ya kuondoka na ushindi?. Ingia kwenye akaunti yako na ubeti sasa.

Leo hii tutaenda kushuhudia mechi ya kibabe ya UEFA Nations League kati ya Uholanzi dhidi ya Ujerumani huku timu zote mbili zikiwa zimejiandaa vyema kabisa kupata ushindi mnono kwenye hili Kundi lao ambalo wapo.

Timu zote mbili zina makocha wapya hivyo hii inakuwa mara yao ya kwanza kukutana ambapo kocha wa Uholanzi ni Xavi Hernandez ambaye amekabidhiwa kijiti cha kuinoa timu hiyo, huku kwa upande wa Ujerumani wao wana Jurgen Klopp ambaye anahitaji kurejesha matumaini kwa klabu hiyo kubwa Duniani. Jisajili hapa.

Hii ni mechi ya kwanza wa Xavi Hernandez akiwa na Uhalonzi kama tunavyojua ni kocha ambaye anapenda timu icheze kwa kumiliki mpira na kushambulia lango la mpinzani inapopata nafasi hiyo. Lakini pia timu hiyo ina wachezaji wakubwa na wenye uwezo mzuri akiwepo Van Dijk, De Jong, Gakpo Memphis Depay na wengine wengi.

Mkwanja mrefu upo kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Jurgen Klopp hii ni mechi yake ya kwanza akiwa kama kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Ujerumani baada ya kuchukua mikoba ya Nagelsmann huku kocha huyo mwenye mafanikio makubwa akiwa ni tumaini kwenye Taifa hilo.

Ujerumani wakiwa kama washindi wa Kombe la Dunia 2014 wana wachezaji wenye uwezo mkubwa kabisa kama vile Joshua Kimmich, Musiala, Floarian Wirtz, Hevertz na wengine wengi ambao wanaungana kutengeneza kikosi hiki chenye uwezo mkubwa kabisa Duniani.

Uholanzi itataka kumiliki mpira na kujenga mashambulizi kwa utulivu, wakati Ujerumani chini ya Klopp inaweza kutafuta kutumia presha zaidi kwenda kwa mpinzani wao.

Kwa upande mwingine, kama Ujerumani itaruhusu Uholanzi kumiliki mpira kwa muda mrefu bila kuweka presha sahihi, De Jong, Reijnders na Gravenberch wanaweza kuanza kuutawala mchezo. Jisajili hapa.

Timu hizi mbili zimeshakutana sana na mara ya mwisho Ujerumani ndiye ambaye aliibuka mshindi. Je leo hii nani ataibuka na ushindi?. Odds Kubwa zipo kwenye mechi hii, hivyo bashiri sasa.

Mechi nyingine ni hii ya Norway dhidi ya Denmark ambapo wenyeji wanaingia kwenye mchezo huu wakihitaji kufanya mashambulizi zaidi kwenda kwa mpinzani kwani wana mshambuliaji hatari Duniani Erling Haaland na ni salaha kubwa sana kwenye kikosi hicho.

Ukiachilia kuwa na mshambuiliaji huyo, pia wana wachezaji wenye uwezo wa kuleta kasi pembeni na kusaidia kutengeneza nafasi, huku Martin Ødegaard akiwa muhimu katika kuunganisha kiungo na safu ya ushambuliaji.

Kinachoweza kuwa muhimu ni namna Norway itakavyomtafuta Haaland. Ikiwa Denmark itafanikiwa kumtenga na mipira, Norway inaweza kulazimika kutumia zaidi mashambulizi ya pembeni.

Huku Denmark wao wanaingia kwenye mchezo wakiwa na uzoefu mkubwa wa kucheza mechi za kiwango hiki. Hii si timu inayotegemea mchezaji mmoja pekee; nguvu yake kubwa ipo katika mpangilio wa timu, matumizi mazuri ya mpira na uwezo wa kucheza kwa nidhamu.

Lakini Denmark pia lazima iwe makini inapopoteza mpira. Norway ina uwezo wa kubadilisha mchezo kutoka kujilinda kwenda kushambulia kwa kasi, hasa ikiwa Ødegaard atapata nafasi ya kuanzisha mashambulizi.

Mechi mbili za mwisho kukutana kati yao Denmark aliondoka na ushindi, hivyo hii ni mechi ya kisasi kwa kina Haaland na wenzake. Suka jamvi hapa.

Wananchi Pagwi waiomba Serikali kukamilisha zahanati – HabariLeo

TANGA; WANANCHI wa Kijiji cha Pagwi, wilayani Kilindi, mkoani Tanga, wameiomba Serikali kusaidia kukamilisha ujenzi wa zahanati yao ulioanza mwaka 2018 kwa nguvu zao wenyewe, wakieleza kuwa ukosefu wa huduma za afya karibu umekuwa changamoto kubwa, hususan kwa wanawake wajawazito.

Wananchi hao walisema hulazimika kutembea takribani kilomita nne kufuata huduma za afya katika vijiji jirani, huku hali ya barabara ikiongeza ugumu wa kuwafikisha wagonjwa hospitalini kwa wakati.

Walisema changamoto hiyo imekuwa na madhara kwa wajawazito, ambapo ndani ya mwaka huu wanawake watatu wamejifungua njiani wakati wakielekea kutafuta huduma za afya.

Akijibu kero hiyo, Mtendaji wa Kata ya Pagwi, Mustapha Msingwa, alisema Halmashauri tayari imetenga shilingi milioni 20 kwa ajili ya kusaidia kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kilindi, Saleh Mhando, alisema kiasi kingine cha Sh milioni 30 kimetengwa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.

Katika kuunga mkono juhudi za wananchi, Mhando ametoa 500,000 na mifuko 50 ya saruji, ambayo itatumika katika hatua ya upigaji lipu ya jengo hilo.

Wananchi hao sasa wanasubiri kukamilishwa kwa fedha zilizotengwa na Halmashauri ili ujenzi wa zahanati hiyo uweze kukamilika na kuwawezesha kupata huduma za afya karibu na makazi yao.

 

WANANCHI IRINGA WATOA MAONI TOFAUTI KUHUSU UELEWA WA MVUA ZA EL NIÑO

 

Na Elamu Nyaulingo (UoI), Matukio Daima Media

IRINGA: Baadhi ya wananchi mkoani Iringa wameeleza uelewa wao kuhusu mvua za El Niño na madhara yake, huku wakisema mvua hizo zinaweza kusababisha mafuriko, kuharibu mazao, madaraja na miundombinu mingine endapo tahadhari hazitachukuliwa mapema.

Maoni hayo yametolewa na wananchi wa maeneo mbalimbali waliohojiwa na Matukio Daima Media, akiwemo Simon Msele, Marvin Fabian, Yohana Mhinga na Akolinari Kiungo.

Wananchi hao wameeleza namna wanavyozielewa mvua hizo pamoja na hatua wanazochukua au wanazopaswa kuchukua ili kukabiliana na madhara yanayoweza kujitokeza.

“Mvua za El Niño ni mvua kubwa zinazozidi kiwango cha mvua za kawaida ambazo tumekuwa tukizipata,” alisema Simon Msele, akieleza uelewa wake kuhusu mvua hizo.

Msele alisema moja ya hatua muhimu za kukabiliana na mvua hizo ni kuhakikisha mazingira yanakuwa safi, hususan kwa kusafisha mitaro iliyoziba ili kuruhusu maji kupita vizuri na kupunguza uwezekano wa mafuriko.

Alisema wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi, hasa mabondeni, wanapaswa kuchukua tahadhari mapema kwa kuhama kwenda maeneo salama ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na mafuriko.

Kwa upande wake, Marvin Fabian alisema anaelewa mvua za El Niño kuwa ni mvua zinazoweza kunyesha kwa muda mrefu bila kukatika, tofauti na mvua za kawaida.

Alitolea mfano mvua zinazoweza kuanza kunyesha asubuhi na kuendelea hadi jioni au usiku.

“Kwa kweli, sijajipanga kukabiliana nazo. Labda tutapokea tu hali itakapokuja,” alisema Marvin.

Wananchi wengine walisisitiza umuhimu wa kuhifadhi chakula, kusafisha mifereji na kujiweka katika maeneo salama ikiwa ni sehemu ya tahadhari dhidi ya madhara yanayoweza kujitokeza.

Akolinari Kiungo, mkazi wa Ilala, alisema wananchi katika eneo lake wameanza kuchukua tahadhari kwa kuandaa mifereji ya kupitisha maji na kuhifadhi chakula ndani ya nyumba.

Alisema hatua hizo ni muhimu kwa kuwa muda ambao mvua zinaweza kuendelea kunyesha hauwezi kujulikana ila mvua zikianza watajihami na kujilinda zaidi.

Tayari Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi utabiri wa msimu wa mvua za Vuli (Oktoba – Desemba) 2026, ikitoa angalizo la msimu huo kuathiriwa kwa kiwango kikubwa na hali ya El Niño yenye nguvu kubwa iliyotokana na joto la bahari kuwa Juu ya Wastani katika Bahari ya Pasifiki, hali itakayochagiza ongezeko la  Mvua za Vuli 2026 kuwa za Juu ya Wastani hadi Wastani katika maeneo mengi ya Ukanda wa Pwani ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki, Ukanda wa Ziwa Viktoria na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma.

BIMA YA AFYA YA SHILINGI ELFU 60,000 YAWAFIKIA WANALINDI KUPITIA VIKUNDI

 

NA HADIJA OMARY

LINDI

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeanzisha mpango wa bima ya afya kupitia vikundi, unaolenga kuwawezesha wananchi kupata huduma za matibabu kwa kuchangia shilingi elfu 60 kwa mwaka kwa kila mwanachama. Akizungumza kuhusu mpango huo, 

Meneja wa Bima ya Afya wa NHIF Mkoa wa Lindi Radhia Makono amesema mpango huo unalenga kuongeza wigo wa wananchi wanaonufaika na bima ya afya, ambapo mwanachama anatakiwa kuwa sehemu ya kikundi chenye wanachama wasiopungua 10, kiwe rasmi au kisicho rasmi mradi kitimize masharti.

Meneja huyo amesema kila mwanachama atatakiwa kuchangia shilingi elfu 60 kwa mwaka, na baada ya kukamilisha taratibu za uanachama ataweza kupata huduma za afya katika vituo na hospitali zilizosajiliwa na NHIF kwa kufuata mfumo wa rufaa kuanzia ngazi ya zahanati, kituo cha afya, hospitali ya wilaya na hatimaye hospitali ya mkoa pale huduma inayohitajika inapokosekana ngazi ya chini.

Amesema mpango huo ni fursa kwa wananchi, hususan wanaojishughulisha na shughuli za kiuchumi kupitia vikundi, kuwa na ulinzi dhidi ya gharama za matibabu ambazo wakati mwingine huwa mzigo kwa mtu mmoja au familia, hivyo amewataka wananchi kuunda au kujiunga na vikundi na kutumia fursa hiyo.

Baadhi ya wananchi mkoani Lindi wamepongeza kuanzishwa kwa mpango huo wakisema kiwango cha shilingi elfu 60 kwa mwaka kinawapa nafasi watu wengi wakiwemo wafanyabiashara wadogo, wakulima na wajasiriamali kumudu gharama za bima na kinawapa matumaini ya kupata matibabu bila kulazimika kutafuta fedha nyingi pindi wanapougua.

Hata hivyo, wananchi hao wameiomba Serikali na NHIF kuhakikisha huduma zinapatikana kwa ufanisi katika vituo vilivyosajiliwa ikiwemo upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, na kuwataka viongozi kuendelea kutoa elimu kuhusu namna ya kuunda vikundi, kujiandikisha na kutumia huduma kwa mfumo wa rufaa ili wananchi wengi waelewe manufaa ya mpango huo.

Makonda Atoa Msimamo Wake Kuhusu Umiliki wa Timu ya Taifa

Global Publishers
September 24, 2026
816 views
0 Comments

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Timu ya Taifa ni mali ya Nchi na si kampuni inayomilikiwa na mtu binafsi.

Akizungumza leo Septemba 24, jijini Dar es Salaam, Makonda amesema mamlaka ya Waziri katika kusimamia Sekta ya Michezo yanaongozwa na Sheria, Sera na Kanuni, huku akisisitiza kuwa Timu ya Taifa inawakilisha Nchi kila inaposhiriki mashindano ndani na nje ya Tanzania.

“Timu ya Taifa ni mali ya Nchi, si kampuni ya mtu. Ndiyo maana tumeikasimu na kuihudumia. Timu ikienda popote pale, ni Nchi inaenda,” amesema Makonda.

Aidha, Makonda amekosoa mtazamo wa baadhi ya watu wanaodharau mamlaka ya Waziri katika utekelezaji wa majukumu yake, akisisitiza kuwa Waziri ni mteule wa Rais na anawajibika kusimamia sekta aliyopewa kwa mujibu wa sheria.

“Wanamfanya kama Waziri wanamdharau, lakini huyo ni mteule wa Rais anayesimamia Wizara ambayo inakupa mkate,” amesema Makonda.