MAGAZETINI LEO IJUMAA SEPT 25/2026:MWANRI AONYA WANACCM WANAONUNUA UONGOZI…

 

 

 

MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA 

 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)

1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

3:TUZO YA AFYA

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .

🚨ZIMEBAKI SIKU 6 ZOEZI KUFUNGWA

v>

Rais Samia Aongoza Dhamira ya Afrika Kutokomeza Vifo Vya Mama na Mtoto

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepongezwa kwa uongozi wake mahiri katika kusukuma mbele ajenda ya Afrika ya kutokomeza vifo vinavyoweza kuzuilika vya mama na mtoto, huku bara hilo likikabiliwa na karibu asilimia 70 ya vifo vya akina mama duniani na takribani theluthi mbili ya vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano.

Akiwa Kinara wa Umoja wa Afrika katika Afya ya Mama na Mtoto, Rais Samia anaongoza ajenda ya “Malengo Matatu ya Sifuri” (Three Zeros) inayolenga kufikia sifuri ya kujifungulia nyumbani, sifuri ya vifo vinavyoweza kuzuilika vya mama na mtoto mchanga, pamoja na sifuri ya watoto wasiopata chanjo.

Ajenda hiyo imepewa msukumo katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Wakuu wa Nchi kuhusu Afya ya Mama, Mtoto Mchanga na Mtoto, iliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81), ukiwakutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali, viongozi wa taasisi za Umoja wa Afrika, mashirika ya kimataifa ya afya na washirika wa maendeleo.

Akiwasilisha ujumbe wa Rais Samia katika mkutano huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema ukubwa wa changamoto unahitaji Afrika kutoka kwenye ahadi na kuelekea katika hatua madhubuti zinazoweza kupimwa kwa maisha ya wanawake na watoto yanayookolewa.

Amesema, pamoja na hatua ambazo Bara la Afrika limepiga, Afrika bado inachangia karibu asilimia 70 ya vifo vya akina mama duniani na takribani theluthi mbili ya vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano, huku sehemu kubwa ya vifo hivyo ikiwa inaweza kuzuilika.

Makamu wa Rais amesema msukumo wa Rais Samia unalenga kuimarisha mifumo ya afya ya nchi za Afrika, kuongeza ufadhili wa ndani, kuboresha huduma za dharura na mifumo ya rufaa, kuongeza upatikanaji wa wahudumu wa afya wenye ujuzi na kuhakikisha takwimu zinatumika kufuatilia matokeo na kubaini maeneo yanayohitaji hatua zaidi.

 

Akielezea uzoefu wa Tanzania, Makamu wa Rais amesema uwekezaji katika huduma za afya ya msingi na za dharura kwa mama na mtoto mchanga, pamoja na kuimarishwa kwa mifumo ya rufaa ikiwemo M-Mama, unaonesha namna uongozi wa kisiasa, teknolojia na utoaji wa huduma kwa wananchi vinavyoweza kuunganishwa katika kuokoa maisha.

Hatua hizo zimekwenda sambamba na kuongezeka kwa wanawake wanaojifungulia katika vituo vya afya kutoka asilimia 51 mwaka 2015 hadi asilimia 81 mwaka 2022, mafanikio yanayoonesha uwezekano wa kubadili mwenendo wa vifo vya mama na mtoto pale uwekezaji unapounganishwa na utekelezaji katika ngazi ya jamii.

Makamu wa Rais alisema ajenda anayoiongoza Rais Samia pia inatoa uzito kwa suala la Afrika kujitegemea katika afya, akisisitiza kuwa mafanikio hayapaswi kupimwa pekee kwa uwezo wa bara kugharamia, kuzalisha au kununua mahitaji yake, bali pia kwa uwezo wa kuhakikisha huduma muhimu zinamfikia kila mama na mtoto kwa wakati na mahali wanapozihitaji.

Katika kufanikisha hilo, nchi za Afrika zimehimizwa kuimarisha uwajibikaji wa kisiasa, kuongeza uwekezaji wa ndani katika huduma zinazookoa maisha na kuhakikisha rasilimali zinafika hadi katika ngazi ya utoaji huduma.

“Dhamira ni kuhakikisha hakuna mama anayepoteza maisha kwa kukosa usafiri, damu, mhudumu mwenye ujuzi au huduma ya dharura; hakuna mtoto mchanga anayefariki kwa kukosa huduma inayoweza kuokoa maisha yake, na hakuna mtoto anayebaki bila chanjo kwa sababu mfumo wa afya haukuweza kuifikia familia yake,” amesema Mhe. Ndejembi.

Makamu wa Rais amesema kulinda uhai wa mama na mtoto si suala la afya pekee, bali ni uwekezaji katika rasilimali watu, uchumi na mustakabali wa Afrika, pamoja na kuwa sehemu muhimu ya utekelezaji wa Ajenda 2063 ya Bara la Afrika.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Africa CDC, Dkt. Jean Kaseya, alipongeza uongozi wa Rais Samia na kueleza dhamira ya Taasisi hiyo kuendelea kumuunga mkono katika jukumu lake la Kinara wa Umoja wa Afrika katika Afya ya Mama na Mtoto, huku akitaja hatua zilizopigwa na Tanzania kama mfano wa mafanikio yanayoweza kupatikana barani Afrika.

Takwimu za Africa CDC zinaonesha kuwa Tanzania imepunguza uwiano wa vifo vya uzazi kwa takribani asilimia 80, kutoka vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2016 hadi 104 mwaka 2022, hatua inayohusishwa na kuimarishwa kwa huduma za dharura za uzazi na watoto wachanga, mifumo ya rufaa, ongezeko la wahudumu wa afya pamoja na ufuatiliaji wa vifo vya mama na watoto.

Dkt. Kaseya alisema Africa CDC itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kusukuma mbele ajenda hiyo, akisisitiza umuhimu wa uongozi wa kisiasa, uwekezaji na mifumo imara ya afya katika kulinda uhai na ustawi wa mama na mtoto barani Afrika.

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Dkt. Adhanom Ghebreyesus amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuandaa mkutano huo na kuwa kinara wa Umoja wa Mataifa wa Afya ya Mama na Mtoto. Amesema katika kipindi cha miaka sita pekee, Tanzania imepunguza kiwango cha vifo vya kina mama kwa asilimia 81. Amesema kwa kuzindua mpango mkakati huo wa sifuri tatu (Three Zeros), Tanzania inaongoza kwa mfano na inapaswa kuungwa mkono.

Amesema Shirika la Afya Duniani limejidhatiti kusaidia kila nchi mwanachama kulingana na mazingira yake na kufikia malengo yake kwa kuimarisha viwango vya huduma za kitabibu vinavyotumiwa na wahudumu walio mstari wa mbele kuokoa maisha ya kina mama na watoto wachanga.

Kupitia nafasi yake kama Kinara wa Umoja wa Afrika katika Afya ya Mama na Mtoto, Rais Samia anasukuma dhamira ya kulifanya bara hilo kufikia hatua ambayo vifo vinavyoweza kuzuilika havitachukuliwa tena kuwa jambo lisiloepukika, huku kaulimbiu ya “Jiongeze, Tuwavushe Salama” ikibeba wito wa Afrika kwenda hatua ya ziada kwa ajili ya kila mama, mtoto mchanga, mtoto na kijana balehe.

Mkutano huo, umehudhuriwa na Viongozi kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Dkt. Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) Dkt. Jean Kaseya, Mwenza wa Rais wa Benin Bi. Nathalie Vilette Wadagni, Wadau wa Maendeleo wakiwemo, Gates Foundation, Global Fund, Gavi, UNFPA, Unicef, Suzan Thompson Buffett Foundation, Beginning Fund pamoja na Viongozi kutoka Umoja wa Afrika (AU).

 

OSHA, Bulyanhulu wapongezwa usalama kazini – HabariLeo

SHINYANGA: KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeipongeza Ofisi ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) pamoja na Mgodi wa Bulyanhulu kwa kuwekeza katika mifumo ya usalama na afya ya wafanyakazi, hatua inayolenga kuwalinda dhidi ya vihatarishi vinavyoweza kujitokeza katika mazingira ya kazi.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hawa Chakoma, wakati wa ziara ya kamati katika Mgodi wa Bulyanhulu mkoani Shinyanga, iliyolenga kufuatilia utekelezaji wa Sheria Na. 297 ya mwaka 2023 kuhusu Usalama na Afya Mahali pa Kazi, inayosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano.

Chakoma amesema ziara hiyo imelenga kutathmini namna wafanyakazi wanavyolindwa dhidi ya vihatarishi vinavyotokana na shughuli za uchimbaji wa madini, pamoja na ufanisi wa mifumo iliyowekwa kuwasaidia wafanyakazi wanaopata ajali au changamoto za kiafya wakiwa kazini.

“Tunataka kuona ni kwa namna gani wenzetu wa mgodi wanajaribu kuondoa vihatarishi kwa wafanyakazi, au kuwahudumia wanaopata changamoto hizo wakiwa mahali pa kazi,” amesema Chakoma.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Dkt. Evaline Wilbard Munisi, amesema Serikali kupitia OSHA imeendelea kuimarisha usimamizi wa usalama na afya mahali pa kazi kwa kufanya kaguzi, kutoa elimu na kuhakikisha waajiri wanazingatia matakwa ya sheria.

Dk Munisi amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026, jumla ya kaguzi 871 zilifanyika mkoani Shinyanga, huku wafanyakazi 7,969 wakifanyiwa vipimo vya afya.

Amesema pia jumla ya waajiri 102 walikidhi matakwa ya sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi na kupatiwa vyeti vya ithibati, wakati waajiri wengine walipewa maelekezo ya kufanya maboresho katika maeneo yaliyobainika kuwa na changamoto.

Katika upande wa mafunzo, Dkt. Munisi amesema jumla ya wafanyakazi 931 walipatiwa mafunzo kuhusu usalama na afya mahali pa kazi katika kipindi hicho.

Amesisitiza kuwa hatua hizo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha maeneo ya kazi yana mifumo madhubuti ya kuzuia ajali, magonjwa yatokanayo na kazi na madhara mengine yanayoweza kuhatarisha afya na usalama wa wafanyakazi.

Naye Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, amesema taasisi hiyo inaendelea kusimamia usalama na afya mahali pa kazi kwa kuhakikisha waajiri wanaweka mifumo madhubuti ya kuwalinda wafanyakazi dhidi ya vihatarishi.

Amesema OSHA pia inaweka mkazo katika utoaji wa elimu na uhamasishaji ili waajiri waelewe wajibu wao kisheria na waweze kutekeleza matakwa ya usalama na afya mahali pa kazi kwa ufanisi.

Ziara hiyo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake ya kufuatilia utekelezaji wa sheria pamoja na maagizo na maelekezo yaliyowahi kutolewa kuhusu uboreshaji wa usalama na afya mahali pa kazi.

RC CHALAMILA ATOA MWEZI MMOJA KWA WAFANYABIASHARA KUFUNGUA MITAA KARIAKOO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametoa agizo hilo wakati akifanya ziara ya kutembelea mitaa mbalimbali ya kariakoo wilaya ya Ilala na kutoa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo kwa wafanyabiashara wadogo kariakoo kuacha kufanya biashara barabarani na mbele ya maduka ya watu badala yake wao pia wafanye biashara zao kwenye vyumba vya maduka

Akizungumza leo Septemba 24, 2026 RC Chalamila amesema baada ya kufanya ziara amebaini uwepo wa changamoto ya wafanyabiashara wadogo kuweka meza zao juu ya mitaro ya maji, mbele ya maduka ya watu wengine pamoja na kuziba barabara hivyo amewataka wafanyabiashara hao wadogo kuhamia kwenye maduka ndani ya muda huo wa mwezi mmoja

Aidha RC Chalamila amemtaka RPC ilala kumkamata mmiliki wa jengo eneo la Kariakoo aliefanya utiririshaji wa maji taka, jambo ambalo ni kinyume na sheria huku akimuelekeza mkuu wa Wilaya ya Ilala kuendelea na oparesheni ya dhidi ya wanaofanya biashara juu ya mitaro ya maji

Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema wilaya hiyo imeendelea kutekeleza maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kulifungua Soko la kariakoo na kuhakikisha linapitika huku akieleza baadhi ya changamoto zilizopo kwenye eneo hilo ikiwemo wafanyabiashara kuziba mitaro, kuingiza majiko kupika kariakoo na kushusha mizigo kuziba njia

Vilevile Mwenyekiti wa wafanhabiashara wadogp maarufu kama machinga eneo la kariakoo Livingston Lusinde kwa niaba ya wafanyabiashara wadogo amesema wafanyabiashara wadogo wapo tayari kuondoka kariakoo na kwenda kufanya biashara eneo walilotengewa la Jangwani na kuiomba Serikali kueleza mchakato wa ujenzi wa soko hilo huku Mwenhekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara  kariakoo Severin Mushi akiipongeza Serikali kwa kuendelea kuiboresha kariakoo ikiwemo kuwaondoa wamachinga mbele ya maduka.

 

TARURA YAOKOA BILIONI 124 UJENZI MADARAJA YA MAWE NCHINI

Dar es Salaam 

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeokoa zaidi ya shilingi bilioni 124 kutokana na ujenzi wa madaraja kwa kutumia teknolojia ya mawe.

Kiasi hicho cha fedha kimeokolewa kutokana na ujenzi wa madaraja ya mawe 527 kwa gharama ya shilingi bilioni 47 ambapo kama yangejengwa kwa kutumia nondo na zege yangegharimu zaidi ya shilingi bilioni 171.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Madaraja ya Mawe TARURA Makao Makuu, Mhandisi Mshauri Pharles Ngeleja wakati akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega alipotembelea banda la TARURA katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wahandisi unaofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Sambamba na madaraja ya mawe, Mhandisi Ngeleja amemueleza Mgeni rasmi kuwa TARURA inajenga madaraja ya watembea kwa miguu “Suspension and suspended Bridge” kwenye barabara zilizosajiliwa na maeneo ambayo hayana mtandao rasmi wa barabara.

“TARURA tumeamua kujenga vivuko vya aina hii kwa ajili ya watembea kwa miguu lakini pia vina uwezo wa kutumika na waendesha baiskeli na bodaboda ambapo mpaka sasa vipo 80 na kwa kiasi kikubwa vimewasaidia wakulima kuyafikia masoko na huduma nyingine za kijamii kwa urahisi”, amesema Mhandisi Ngeleja.

Mhandisi Ngeleja ameongeza kuwa kwa sasa TARURA inatekeleza ujenzi wa vivuko hivyo mkoani Morogoro katika wilaya za Mvomero, Ulanga, Malinyi pamoja na wilaya ya Morogoro.

TARURA ambayo ni mdau mkubwa wa sekta ya ujenzi wa miundombinu ya barabara inashiriki katika Mkutano huo sambamba na kutoa elimu kwa wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu majukumu yake.

 

MAKAMU WA RAIS MHE NDEJEMBI AMEMWAKILISHA RAIS DKT SAMIA MKUTANO WA NGAZI YA VIONGOZI KUHUSU AFYA YA MAMANA MTOTO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Viongozi kuhusu afya ya Mama na Mtoto ulioandaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81) New York nchini Marekani.

 

Mkutano huo, umehudhuriwa na Viongozi kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Dkt. Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) Dkt. Jean Kaseya, Mwenza wa Rais wa Benin Bi. Nathalie Vilette Wadagni, Wadau wa Maendeleo wakiwemo, Gates Foundation, Global Fund, Gavi, UNFPA, Unicef, Suzan Thompson Buffett Foundation, Beginning Fund pamoja na Viongozi kutoka Umoja wa Afrika (AU).

 

Bulyanhulu yapongezwa usalama wa wafanyakazi – HabariLeo

SHINYANGA: KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeipongeza OSHA na Mgodi wa Bulyanhulu kwa kuwekeza katika mifumo ya usalama na afya mahali pa kazi, hatua inayolenga kuhakikisha wafanyakazi wanalindwa dhidi ya vihatarishi na wanapata huduma stahiki wanapopata ajali au changamoto za kiafya kazini.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hawa Chakoma, wakati wa ziara ya kamati katika eneo la Mgodi wa Bulyanhulu mkoani Shinyanga, iliyolenga kufuatilia utekelezaji wa Sheria Na. 297 ya mwaka 2023 kuhusu Usalama na Afya Mahali pa Kazi, inayosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano.

Chakoma amesema kamati hiyo imefanya ziara hiyo ili kutathmini namna wafanyakazi wanavyolindwa dhidi ya vihatarishi vinavyotokana na shughuli za uchimbaji wa madini, pamoja na mifumo iliyowekwa kuwasaidia wafanyakazi wanaokumbana na vihatarishi vinavyoweza kusababisha ajali au magonjwa wakiwa kazini.

“Tunataka kuona ni kwa namna gani wenzetu wa mgodi wanajaribu kuondoa vihatarishi kwa wafanyakazi, au kuwahudumia wanaopata changamoto hizo wakiwa mahali pa kazi,” amesema  Chakoma.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Dk. Evaline Wilbard Munisi, amesema Serikali kupitia OSHA imeendelea kufanya kaguzi na kutoa elimu kuhusu usalama na afya mahali pa kazi kwa wafanyakazi.

Dk Munisi amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026, jumla ya kaguzi 871 zilifanyika mkoani Shinyanga, huku wafanyakazi 7,969 wakifanyiwa vipimo vya afya mkoani humo.

Aidha, amesema waajiri 102 walikidhi matakwa ya sheria ya usalama na afya mahali pa kazi na kupatiwa vyeti vya ithibati, huku waajiri wengine wakipewa maelekezo ya kufanya maboresho katika maeneo yaliyobainika kuwa na changamoto.

Katika eneo la mafunzo, Dk Munisi amesema jumla ya wafanyakazi 931 walipatiwa mafunzo kuhusu usalama na afya mahali pa kazi.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, amesema OSHA inaendelea kusimamia usalama na afya mahali pa kazi kwa kuhakikisha waajiri wanaweka mifumo inayolinda usalama na afya za wafanyakazi.

Amesema OSHA pia inaweka mkazo katika elimu na uhamasishaji ili waajiri waweze kutekeleza wajibu wao kwa uelewa na kuzingatia matakwa ya sheria.

Ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Bunge katika kufuatilia utekelezaji wa sheria pamoja na maelekezo yaliyowahi kutolewa kuhusu uboreshaji wa usalama na afya mahali pa kazi.

VURUGU KILOSA: MTU MMOJA AFARIKI, ASKARI 3 WAJERUHIWA.

 

Na Matukio Daima Media, Kilosa

VURUGU zinazohusishwa na mgogoro kati ya wakulima na wafugaji wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro, zimesababisha vifo vya watu wawili katika matukio tofauti, kujeruhiwa kwa askari watatu na kuharibiwa kwa mali za Jeshi la Polisi.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro inaeleza kuwa tukio linaanzia Septemba 23, 2026, saa 7 mchana katika Mashamba ya Bondeni, Kitongoji cha Legeza Mwendo, Kijiji na Kata ya Tindiga, Tarafa ya Masanze, ambako Festo Selias Chaula maarufu kwa jina la Walter Mkulima alijeruhiwa vibaya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Andrew  Kantimbo akasema kuwa Festo alikatwa kichwani kwa kitu chenye makali na kupigwa kwa vitu butu sehemu mbalimbali za mwili wake na kupata majeraha makubwa yanayosababisha kifo chake katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Baada ya tukio hilo, Polisi lilifanya ufuatiliaji na kuwakamata Seletwi Samiji Mdamanya na Paulo Lukas Sumai, likiwatuhumu kuhusika na mauaji hayo. 

Wawili hao wanaelezwa kuwa ni wafugaji na wakazi wa Kijiji cha Malangali, Kata ya Tindiga.

Hata hivyo, wakati askari wakiwa wanawapeleka watuhumiwa Kituo cha Polisi Kilosa, kundi la watu linalodaiwa kuwa wakulima na kukadiriwa kufikia 200 lilidaiwa kufunga barabara na kuanza kuwashambulia askari waliokuwa wamewabeba watuhumiwa hao.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kantimbo, kundi hilo lilikuwa na silaha mbalimbali za jadi  likilenga kuwadhuru watuhumiwa hao jamii ya wafugaji.

Askari Polisi ikadaiwa walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi hao waliokuwa na visu, mapanga, mishale, mikuki, marungu na mawe.

Baada ya kundi hilo kutawanyika, Polisi walifanya ukaguzi na kumkuta mmoja wa wananchi, Kelvin Mhagama, mkulima na mkazi wa Kichangani, akiwa amejeruhiwa kwa kitu chenye makali sehemu mbalimbali za mwili wake.

Majeruhi huyo alipelekwa hospitali ya wilaya ya Kilosa, lakini alifariki Dunia akiwa anapatiwa matibabu.

Kamanda huyo wa Polisi amethibitisha licha ya kifo hicho, katika vurugu hizo, askari watatu walipata  madhara ikiwemo kujeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili baada ya kushambuliwa kwa silaha za jadi na wanaendelea na matibabu.

Vurugu hizo pia zimesababisha pikipiki ya Polisi yenye namba PT 3131 aina ya SANLG kuteketea kwa moto, huku gari la Polisi PT 5877 Toyota Hilux likiharibiwa baada ya kupigwa kwa mawe.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limewataka wakulima, wafugaji na wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na kutumia njia rasmi za kisheria katika kushughulikia migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Polisi pia wanaendelea na msako wa kuwakamata wote waliohusika na vurugu hizo na kujichukulia sheria mkononi katika tukio hilo.

NG’OMBE WAINGIA MIWA MTIBWA, WALINZI WAWILI WASHAMBULIWA

 

Na Matukio Daima, Mvomero.

Kundi la ng’ombe linalodaiwa kuingizwa katika mashamba ya miwa ya Kiwanda cha Sukari Mtibwa, Mvomero, limeibua vurugu baada ya walinzi wawili wa kiwanda hicho kushambuliwa na kujeruhiwa wakati wakijaribu kuwaondoa mifugo hiyo katika mashamba.

Tukio hilo limetokea Septemba 23, 2026 majira ya saa sita mchana katika eneo la D6, ndani ya mashamba ya miwa ya Kiwanda cha Sukari Mtibwa, Kata ya Mtibwa, Tarafa ya Turiani, Wilaya ya Mvomero.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Andrew Kantimbo, amesema walinzi hao walifanikiwa kulikata kundi la ng’ombe na kuanza kuwaswaga kuelekea Kambi ya Dumila One inayomilikiwa na kiwanda hicho kwa ajili ya utambuzi na hatua zaidi.

Hata hivyo, amesema zoezi hilo lilikumbana na upinzani kutoka kwa wafugaji waliodaiwa kuzuia walinzi na kuanza kuwashambulia kwa visu aina ya sime, marungu na fimbo.

Mashambulizi hayo yalisababisha walinzi Sayuni Ndika Nemes (25) na Sanula Masaga Msabila (36) kujeruhiwa. Wote ni walinzi wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa.

Katika tukio hilo.

Jeshi la Polisi limewakamata Sisone Lugaso Ndabali (20), Taturo Tetetea Shangalima (28) na Likua Kaika Ndikila (21), wote wakazi wa Kijiji cha Kambala, Kata ya Mkindo, Mvomero.

Polisi Mkoa wa Morogoro limewataka wafugaji kuacha kuingiza mifugo katika mashamba ya wakulima na kuacha kujichukulia sheria mkononi, likisisitiza matumizi ya taratibu na sheria katika kudai haki

Mwisho

Watanzania wanaorejea Afrika Kusini kutibiwa bure – HabariLeo

DAR ES SALAAM: HOSPITALI ya Rufaa ya Amana imeanzisha programu maalumu ya kuwasaidia Watanzania wanaorejea nchini kutoka Afrika Kusini kwa kutoa huduma za matibabu ya meno pamoja na ushauri nasaha na msaada wa kisaikolojia.

Daktari Kiongozi wa Hospitali ya Amana, Dk Mafele Ihoyelo, amesema mpango huo umeanzishwa baada ya kubaini baadhi ya Watanzania wanaorejea kutoka Afrika Kusini wakiwa na changamoto za meno, huku wengine wakihitaji msaada wa kisaikolojia ili waweze kuanza maisha mapya nchini.

Amesema huduma hizo zinalenga kurejesha afya ya kinywa kwa wanaokabiliwa na changamoto za meno, huku huduma za kisaikolojia zikilenga kuwasaidia wanaohitaji kurejesha matumaini na kuimarisha afya yao ya akili.

“Programu hiyo itatekelezwa kwa njia ya mtandao na inalenga kuwasaidia watu 100 katika awamu ya kwanza,” amesema.

Hospitali hiyo pia imezihimiza taasisi na wadau mbalimbali kujiunga na programu hiyo na kushirikiana katika kuwafikia watu wengi zaidi.

Kwa upande mwingine, Mohamed Msangi, Mtanzania anayeishi Pretoria/Johannesburg nchini Afrika Kusini, amesema Watanzania wanaorejea nchini wanahitaji kupokelewa vizuri na kusaidiwa kuanza maisha mapya badala ya kukumbana na masimango.

Msangi amesema bado kuna idadi kubwa ya Watanzania waliopo Afrika Kusini wanaohitaji kurejea nchini, lakini baadhi yao wamekuwa na hofu kuhusu namna watakavyopokelewa na kuanza maisha baada ya kukaa huko kwa muda mrefu.

Amesema baadhi ya Watanzania wameishi Afrika Kusini kwa zaidi ya miaka 15 hadi 32, huku wengine wakiwa wamejikita katika biashara na shughuli mbalimbali za kiuchumi, hivyo wanahitaji mazingira yatakayowawezesha kutumia ujuzi na uzoefu wao wanaporejea nchini.

Amesema hadi sasa Watanzania 543 wamekwisharejea nchini kupitia mpango huo, huku wengine 1,500 wakitarajiwa kurejea katika awamu zinazofuata. Wanaorejea wanajumuisha akina mama, watoto, vijana na wazee.

Kwa mujibu wa Msangi, changamoto za meno na afya ya kisaikolojia ni miongoni mwa mahitaji yaliyoonekana kwa baadhi ya wanaorejea, hivyo ushiriki wa Hospitali ya Amana na wadau wengine unaweza kusaidia kuwawezesha kuanza upya maisha yao nchini.