Ligi ya Mabingwa Kuanza Septemba 4, Simba na Yanga Kuwakilisha Tanzania

Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) inatarajiwa kuanza rasmi Septemba 4, 2026, huku Tanzania ikiendelea kuwakilishwa na vigogo wake, Simba SC na Young Africans SC.

Simba na Yanga zitaingia kwenye michuano hiyo zikiwa na kumbukumbu ya kutofanya vizuri katika msimu uliopita, ambapo timu zote mbili ziliishia katika hatua ya makundi.

Kwa msimu huu, kila timu inalenga kufanya vizuri zaidi na kusonga mbele katika hatua za juu za mashindano hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

YANGA KUANZA SEPTEMBA 5

Young Africans SC inatarajiwa kuanza safari yake ya Champions League Septemba 5, 2026, kwa kukutana na Gaborone United ya Botswana.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa majira ya saa 12 jioni, huku Yanga ikitarajiwa kuingia uwanjani ikiwa na lengo la kupata matokeo mazuri katika mchezo huo.

Gaborone United pia ina historia ya kuwa na uhusiano na soka la Tanzania, kwani timu hiyo iliwahi kunolewa na Dimitry Pantev, ambaye amewahi kuwa kocha wa Simba SC.

SIMBA KUKABILIA MIGHTY WANDERERS

Kwa upande wa Simba SC, timu hiyo inatarajiwa kushuka dimbani Septemba 6, 2026, dhidi ya Mighty Wanderers ya Malawi.

Mchezo huo umepangwa kuanza majira ya saa 9 alasiri.

Mighty Wanderers inaingia kwenye mchezo huo ikiwa imetoka katika kipindi cha mabadiliko baada ya kumtimua kocha wake kufuatia kipigo katika mchezo wa fainali ya ligi ya ndani nchini Malawi.

SIMBA NA YANGA ZATAKIWA KUWA MAKINI

Simba na Yanga zitaingia kwenye michuano hiyo zikiwa na kumbukumbu kwamba katika misimu iliyopita timu kubwa za Tanzania zimewahi kuondolewa na klabu ambazo hazikuwa na majina makubwa katika soka la Afrika.

Hali hiyo inafanya timu hizo mbili kuhitajika kuwa makini, hasa katika michezo ya ugenini, kwani hatua za awali za mashindano ya CAF mara nyingi zimekuwa na matokeo ya kushangaza.

Kwa Simba na Yanga, lengo kubwa msimu huu ni kuvuka hatua za awali na kuhakikisha zinaiwakilisha Tanzania kwa mafanikio zaidi katika michuano ya juu ya klabu barani Afrika.

Stori na Clever Alphonce | GPL

Antonio Rüdiger Afunga Ukurasa wa Ujerumani Baada ya Mechi 86

Global Publishers
September 2, 2026
30 views
0 Comments

Beki wa Real Madrid, Antonio Rüdiger, ametangaza rasmi kustaafu kucheza soka la kimataifa akiwa na timu ya taifa ya Ujerumani.

Rüdiger, mwenye umri wa miaka 33, amefikia uamuzi huo baada ya kutafakari kwa kina kuhusu safari yake ya kimataifa, akisema ameamua kutoa nafasi kwa kizazi kipya cha wachezaji wa Ujerumani.

Katika kipindi chake na timu ya taifa, Rüdiger amecheza jumla ya mechi 86, akiwa miongoni mwa mabeki waliokuwa na nafasi muhimu katika kikosi cha Ujerumani kwa miaka ya hivi karibuni.

Uamuzi huo unamaanisha kuwa Rüdiger hataendelea kuonekana kwenye kikosi cha Ujerumani katika michuano ijayo ya kimataifa, huku nafasi yake ikitarajiwa kuchukuliwa na wachezaji vijana wanaoibukia.

Hata hivyo, Rüdiger hajastaafu soka la klabu. Beki huyo bado anaendelea kuitumikia Real Madrid na ataendelea kuwa sehemu ya mipango ya klabu hiyo.

Real Madrid tayari iliongeza mkataba wake hadi Juni 30, 2027, hivyo Rüdiger anaendelea kuwa na majukumu ya klabu licha ya kufunga ukurasa wa soka la kimataifa.

Kustaafu kwake kunafunga rasmi sura moja muhimu ya maisha yake ya soka, huku akiwa ameacha rekodi ya mechi 86 akiwa amevalia jezi ya Ujerumani.

Na Erick Elibariki | GPL

Vitu Muhimu 9 vya Kuzingatia Wakati wa Kununua Gari

Kununua gari ni uamuzi mkubwa wa kifedha na unahitaji uangalifu mkubwa. Iwe unanunua gari jipya au lililotumika, kuna mambo muhimu ya kuzingatia ili kuhakikisha unapata gari lenye thamani bora, salama, na linalokidhi mahitaji yako. Hapa tunakuletea mwongozo wa vitu vya msingi vya kuzingatia.

1. Lengo la Gari na Aina Yake

Kabla ya kununua gari, fikiria unataka kulitumia kwa ajili gani:

  • Safari za mjini au za kila siku: magari madogo na ya uchumi wa mafuta ni bora.

  • Safari ndefu: magari ya kifamilia yenye faraja na engine yenye nguvu.

  • Biashara au usafirishaji: magari ya mizigo au van.

2. Matumizi ya Mafuta na Engine

Angalia engine size (cc) na ufanisi wake wa mafuta:

3. Gharama za Matengenezo na Vipuri

Gari linapokuwa na vipuri rahisi kupata na gharama za matengenezo ni za chini, litakuokoa pesa kwa muda mrefu. Fikiria gharama za bima, kodi, na vipuri vya badilisho.

4. Usalama na Teknolojia

Hakikisha gari lina vifaa vya usalama vinavyohitajika, kama vile:

Teknolojia ya kisasa pia huongeza faraja na urahisi wa kutumia gari.

5. Historia ya Gari (Kwa Magari Yaliyotumika)

Ikiwa unanunua gari lililotumika:

  • Hakikisha odometer haijachedwa.

  • Angalia kama gari limekuwa kwenye ajali kubwa au limeathiriwa na mafuriko.

  • Pata report ya gari au omba fundi akagua engine, gearbox, na chassis.

6. Hali ya Engine, Gearbox na Suspension

  • Engine: Hakikisha haimoshi vibaya au kutoa sauti zisizo za kawaida.

  • Gearbox: Gear inabadilika vizuri bila kukwaruza.

  • Suspension: Hakuna kutingisha vibaya au kugonga chini.

7. Mambo ya Umeme na Comfort

Angalia kama mfumo wa umeme unafanya kazi vizuri, AC inafanya kazi, windows zinafanya kazi, na vifaa vya burudani kama redio au touchscreen vyatumikia vizuri.

8. Test Drive

Test drive ni muhimu:

  • Pitia barabara yenye mashimo

  • Fanya acceleration na braking

  • Sikiliza kwa makini sauti zisizo za kawaida

Hii itakusaidia kubaini tatizo lolote kabla ya kununua gari.

9. Mmiliki na Makati ya Kisheria

  • Hakikisha kadi ya gari inasomeka vizuri na mmiliki halisi.

  • Hakuna deni la kodi au ushuru.

  • Makati yote ya kisheria lazima yawe safi ili kuepuka matatizo baadaye.

Kununua gari ni mchakato unaohitaji umakini. Kwa kuzingatia aina ya gari, gharama za mafuta, usalama, hali ya gari, na makaratasi, utakuwa na uhakika wa kufanya ununuzi sahihi, wa gharama nafuu, na salama kwa muda mrefu.

Tanzanite Queens Kukiwasha na Brazil, England na Canada Kombe la Dunia U-20

Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite Queens, imeondoka nchini kuelekea Poland tayari kwa fainali za Kombe la Dunia la FIFA U-20, zinazotarajiwa kuanza Septemba 5, 2026.

Tanzanite Queens imepangwa katika Kundi B, ambalo linaonekana kuwa na ushindani mkubwa baada ya Tanzania kukutana na mataifa yenye historia kubwa katika soka la wanawake duniani, Brazil, England na Canada.

Tanzania itaanza kampeni yake Septemba 5, 2026, kwa kucheza dhidi ya Brazil katika Uwanja wa Bielsko-Biala, kuanzia saa 11:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Baada ya mchezo huo, Tanzanite Queens itakutana na England Septemba 8 katika uwanja huo huo, ambapo mchezo huo utaanza saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi utakuwa dhidi ya Canada Septemba 11, 2026, katika Uwanja wa Arena Katowice, kuanzia saa 11:00 jioni.

Ratiba hiyo inawapa Tanzanite Queens mtihani mkubwa katika michuano hiyo, huku kila mchezo ukiwa muhimu katika harakati za kutafuta nafasi ya kufuzu hatua inayofuata.

Kocha Mkuu wa Tanzanite Queens, Bakari Shime, amesema ana imani na maandalizi ambayo timu hiyo imeyafanya tangu ilipoingia kambini Dar es Salaam.

Shime anaamini kikosi chake kina uwezo wa kufanya vizuri katika mashindano hayo na kufika hatua ya robo fainali, licha ya kukutana na wapinzani wenye uzoefu mkubwa katika soka la wanawake.

Kwa Tanzania, ushiriki wa Tanzanite Queens katika fainali hizo ni hatua muhimu katika historia ya soka la wanawake nchini, huku timu hiyo ikitarajiwa kupambana kuonyesha uwezo wake katika jukwaa kubwa la kimataifa.

Macho ya mashabiki wa Tanzania sasa yanaelekezwa Poland, ambako Tanzanite Queens itaanza safari yake ya kuandika historia katika Kombe la Dunia U-20.

Na Peter Jinni |GPL

Ebola Yazidi Kusambaa DRC, Vifo Vyakaribia 3,000 Afrika

Global Publishers
September 2, 2026
24 views
0 Comments

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inakabiliwa na ongezeko kubwa la maambukizi ya ugonjwa wa Ebola, huku idadi ya wagonjwa ikivuka 6,000 na vifo kufikia karibu 3,000.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na mamlaka za afya nchini humo, hadi Agosti 31, 2026, jumla ya wagonjwa 6,041 walikuwa wamethibitishwa kuwa na Ebola, huku watu 2,911 wakiripotiwa kufariki dunia.

Hali hiyo imeufanya mlipuko huo kuwa miongoni mwa milipuko mikubwa na yenye madhara zaidi kuwahi kutokea nchini DRC.

Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema katika taarifa yake ya Agosti 28 kuwa Ebola imeenea katika maeneo 60 ya afya yaliyopo ndani ya majimbo sita nchini humo.

Kwa mujibu wa WHO, kiwango cha vifo miongoni mwa watu waliothibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo kimezidi asilimia 48, hali inayozidisha wasiwasi kwa mamlaka za afya na jamii zilizo katika maeneo yaliyoathirika.

Mlipuko huo unahusishwa na aina ya Bundibugyo ya virusi vya Ebola, huku changamoto kubwa ikiendelea kuwa upatikanaji wa chanjo au tiba maalumu iliyoidhinishwa dhidi ya aina hiyo.

Juhudi za kudhibiti ugonjwa huo pia zimekumbwa na vikwazo kutokana na hali ya vita na ukosefu wa usalama katika baadhi ya maeneo, pamoja na kuhama kwa wananchi na ugumu wa kuwafikia baadhi ya jamii.

Hofu imeongezeka zaidi kutokana na kufunguliwa kwa shule katika baadhi ya maeneo yaliyoathirika, huku wazazi na walimu wakihofia mikusanyiko ya wanafunzi inaweza kuongeza hatari ya maambukizi.

Wataalamu wa afya wameendelea kutoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za haraka na kuimarishwa kwa juhudi za kukabiliana na mlipuko huo, ili kuzuia Ebola kusambaa zaidi ndani ya DRC na hatimaye kuvuka mipaka kwenda nchi jirani.

Stori na Na Nasra | GPL

Haakon Viii Aapa Kiapo Cha Katiba, Aanza Rasmi Utwala Wa Norway

Global Publishers
September 1, 2026
0 views
0 Comments

Mfalme mpya wa Norway, Haakon VIII, ameapa rasmi kuilinda Katiba na sheria za nchi hiyo katika hafla iliyofanyika Bungeni mjini Oslo, leo Jumanne, Septemba 1, 2026.

Haakon, mwenye umri wa miaka 53, ameingia madarakani baada ya kifo cha baba yake, Mfalme Harald V, aliyefariki Ijumaa akiwa na umri wa miaka 89 baada ya kutawala Norway kwa takribani miaka 35.

Katika hafla hiyo, Haakon aliweka kiapo cha kuongoza Ufalme wa Norway kwa kuzingatia Katiba na sheria za nchi. Kiapo hicho ni sehemu ya matakwa ya kikatiba kwa mfalme mpya na kinaashiria rasmi mwanzo wa utawala wake.

Haakon aliwasili Bungeni kutoka Ikulu ya Kifalme akiwa kwenye gari lililo wazi, huku baadhi ya viongozi wa familia ya kifalme wakishiriki katika hafla hiyo.

Mke wake, Malkia Mette-Marit, hakuhudhuria hafla hiyo kutokana na matatizo ya kiafya, wakati akiendelea kupona baada ya kufanyiwa upandikizaji wa mapafu.

Norway haitafanya sherehe ya kutawazwa rasmi kwa Mfalme Haakon VIII, kwa kuwa utaratibu huo ulifutwa nchini humo mwaka 1908. Badala yake, kiapo cha kikatiba ndicho kinachotumika kuashiria mwanzo wa utawala wa mfalme mpya.

Wakati huo huo, Norway inaendelea kuomboleza kifo cha Mfalme Harald V. Jeneza lake limewekwa katika eneo maalumu la kutembelewa na wananchi katika kanisa la Ikulu hadi Septemba 8.

Mazishi ya Mfalme Harald yanatarajiwa kufanyika mjini Oslo, Septemba 9, 2026.

Na Avia Remigius | GPL

Mwanamke Akamatwa kwa Tuhuma za Kumuua Mumewe – Video

Global Publishers
September 1, 2026
18 views
0 Comments

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limemkamata Jovita Bateguye Budyo, mwenye umri wa miaka 30, kwa tuhuma za kumuua mumewe, Abeli Charles, mwenye umri wa miaka 44, katika eneo la Mafisa, Morogoro Mjini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, tukio hilo lilitokea usiku wa Agosti 31, 2026, katika Mtaa wa Mafisa kwa Mambi, Kata ya Mafisa, Wilaya ya Morogoro Mjini, ambako mtuhumiwa na marehemu walikuwa wakiishi pamoja.

Taarifa inaeleza kuwa wawili hao walikuwa wakijiandaa kwenda kulala kabla ya kutokea kwa mgogoro wa kifamilia unaodaiwa kuhusishwa na suala la kunyimwa unyumba.

Inadaiwa kuwa mgogoro huo ulisababisha ugomvi, ambapo mtuhumiwa anadaiwa kumkata marehemu kwa kitu chenye ncha kali katika maeneo ya shingoni na kichwani.

Kutokana na majeraha hayo, Abeli Charles alifariki dunia.

Baada ya tukio hilo, Jeshi la Polisi lilimkamata Jovita na linaendelea na uchunguzi pamoja na hatua nyingine za kisheria kuhusu tukio hilo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limewataka wananchi kutumia njia salama katika kutatua migogoro ya kifamilia na mahusiano, badala ya kutumia nguvu au vitendo vya ukatili.

Aidha, wananchi wameshauriwa kuwashirikisha watu wanaowaamini, wazee wenye busara au vyombo vya sheria wanapokabiliwa na migogoro ili kuzuia matukio yanayoweza kusababisha madhara au kupoteza maisha.

Stori na Lailath Burhan | GPL

Video: Ndejembi Awasalimu Wananchi Moshi, Atoa Ahadi Kwa Rais Samia

Global Publishers
September 1, 2026
1,020 views
0 Comments


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amewasalimu wananchi wa Mbuyuni wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro, waliokusanyika kumpokea alipokuwa katika ziara binafsi mkoani humo leo, Septemba 1, 2026.

Akizungumza na wananchi hao, Makamu wa Rais amewasihi kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na yeye binafsi, ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Mhe. Ndejembi amesema kupitia nguvu ya maombi ataweza kumsaidia Rais Samia kwa hekima na utii katika kutekeleza majukumu ya kuwatumikia wananchi.

Aidha, amesema ataendelea kutekeleza wajibu wake kwa uadilifu, umakini na kujituma, huku akisisitiza utayari wake wa kushirikiana na viongozi pamoja na wananchi katika kutekeleza majukumu ya kitaifa.

Akizungumza kwa msisitizo, Makamu wa Rais amesema:

“Hatawazingua Wana wala hatamzingua Mama,”

kauli ambayo alisema aliitoa pia mkoani Dodoma kwa wananchi wa Chamwino mara baada ya kuapishwa.

Kabla ya kuelekea Mbuyuni, Makamu wa Rais aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambako alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wa dini pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kilimanjaro.

 

Vodacom Yaja na Ubunifu Mpya Kuelekea Tanzania 2050

Katika toleo la 12 la Wiki ya Ubunifu Tanzania (IWTz) 2026, Vodacom Tanzania imezidi kuonyesha jinsi mtandao, ubunifu na ujasiriamali vinavyochangia malengo ya Dira ya Maendeleo Tanzania 2050.

Tukio hili linakutanisha wabunifu wajasiriamali, watunga sera, watafiti, wawekezaji, vijana, wadau wa maendeleo na viongozi wa sekta binafsi chini ya kauli mbiu: “Kutoka Matarajio hadi Mageuzi: Kuibua Njia ya Tanzania Kuelekea Ustawi Jumuishi.”

Katika wiki hii, Vodacom imeshiriki katika mijadala mbalimbali kuhusu uchumi wa wabunifu wa maudhui, banda la maonyesho, mijadala na wanahabari na wadau, uzinduzi wa Vodacom Accelerator Season 5, pamoja na onyesho la moja kwa moja la usalama wa mtandao (cybersecurity) litakalofuatiwa na jopo la majadiliano.

Akizungumza katika majadiliano ya kuziunganisha Sauti za Watanzania: Watengeneza maudhui na Majukwaa Mtandaoni. Mkuu wa Idara ya Chapa na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Yvonne Maruma, alisema thamani ya mtandao inapaswa kupimwa kwa kile unachowawezesha watu kufanya.

“Mtandao ni hatua ya kwanza ya kushiriki katika uchumi wa kidijitali. Lakini thamani yake halisi iko katika kile unachowawezesha watu kufanya: kujifunza, kubuni, kujenga biashara, kufikia hadhira na kusikika,” alisema Maruma.

“Kwa kijana wa Kitanzania, simu janja inaweza kuwa darasa, soko, studio ya ubunifu na chombo cha biashara. Wakati Tanzania ikitekeleza Dira 2050, wabunifu wa maudhui wanapaswa kuonekana zaidi ya njia za kusambaza ujumbe; wao ni washirika wanaoweza kugeuza mawazo ya ujasiriamali, elimu, ujumuishaji wa kifedha na ubunifu kuwa hadithi ambazo watu wanaelewa, wanaziamini na kuzifanyia kazi. Hilo ndilo tunalomaanisha tunaposema Vodacom ni Zaidi ya Mtandao.”

Kupitia mpango wa Vodacom Youth Base (VYB), kampuni inaendelea kushirikiana na watengeneza maudhui mtandaoni na kuwasaidia kubaki mtandaoni wakati wakitengeneza na kusambaza maudhui kwa hadhira zao.

Mpango huu ni sehemu ya jitihada pana za Vodacom za kuhakikisha ujumuishaji wa kidijitali wenye maana, unaowawezesha watu si tu kuunganishwa mtandaoni, bali pia kushiriki, kushindana na kuongoza katika uchumi wa kidijitali.

Katika kilele cha wiki hii, Vodacom Tanzania itazindua programu ya Vodacom accelerator season 5, ambayo imelenga kuwasaidia wajasariamali wa Kitanzania kuanzia hatua zao za mwanzo za wazo hadi kuwa biashara imara. Uzinduzi huu utaambatana na hadithi ya mmoja wa wahitimu wa awali wa mpango huu aliyefanikiwa kutoka wazo hadi biashara.

Ushiriki wa Vodacom katika Wiki ya Ubunifu Tanzania unajengwa juu ya ushirikiano wake na UNDP Tanzania na unaunga mkono malengo ya Dira ya Maendeleo Tanzania 2050: uchumi wa viwanda wenye ushindani wa dola trilioni 1 za Marekani, unaoendeshwa na mtandao jumuishi wa usafirishaji, nishati, sayansi na teknolojia, utafiti na maendeleo, pamoja na mageuzi ya kidijitali.

Kesi ya Lissu Yaahirishwa, Mnyika Kuendelea Kudodoswa Kesho

Kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, imeahirishwa hadi kesho, huku Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, akitarajiwa kuendelea kujibu maswali kutoka upande wa Serikali.

Katika hatua za mwisho za mwenendo wa kesi leo, Mnyika alikabiliwa na maswali kuhusu uelewa wake wa sheria, majukumu yake kama Katibu Mkuu wa CHADEMA, pamoja na kauli na msimamo wa chama kuhusu uchaguzi na vurugu.

Wakili wa Serikali, Nzengeli, alimuuliza Mnyika kama yeye ni mtaalamu wa sheria, ambapo alijibu kuwa si mtaalamu wa sheria.

Mnyika pia alikataa kuwa hana uwezo wowote wa kuchambua nyaraka, akisema anaweza kuchambua mambo kwa uelewa wake, ingawa baadaye alikiri kuwa hana utaalamu wa kisheria.

MNYIKA AULIZWA KUHUSU DEMOKRASIA

Katika dodoso hilo, Mnyika alieleza kuwa endapo mtu anaamini uchaguzi ni wa haki na uhuru, lakini CHADEMA ina msimamo tofauti, mtu huyo anaweza kutokubaliana na msimamo wa chama.

Alisema kutokubaliana na msimamo wa CHADEMA ni suala la maoni ya mtu binafsi.

Wakili Job Mrema naye aliendelea kumuuliza Mnyika maswali akitumia Kamusi Kuu ya Kiswahili, Toleo la Tatu la mwaka 2022, katika kutafuta maana ya baadhi ya maneno yaliyotumika kwenye ushahidi.

Mnyika alithibitisha kuwa kamusi hiyo ni rasmi, ingawa si nakala pekee inayoweza kutumika kutoa tafsiri ya Kiswahili.

Mrema alimuuliza Mnyika kuhusu majukumu yake kama Katibu Mkuu wa CHADEMA.

Mnyika alisema jukumu lake ni kusimamia shughuli zote za kila siku za chama.

Alipoulizwa kama ameshindwa kutaja majukumu yake katika baadhi ya maswali yaliyoulizwa awali, Mnyika alikanusha na kusema amejibu maswali mengi, isipokuwa machache ambayo yalihitaji uelewa zaidi.

Mnyika pia alikanusha madai kwamba nafasi yake ya Katibu Mkuu imekuwa ya kusaidiwa au kwamba amekuwa akibebwa na Mwenyekiti wa CHADEMA.

MNYIKA AULIZWA KUHUSU “FUJO”

Katika sehemu nyingine ya dodoso, Mrema alimuuliza Mnyika maana ya neno “fujo.”

Mnyika awali alijibu kwa kusema, “Fujo ni fujo,” lakini baada ya kuombwa kueleza maana hiyo kwa mujibu wa kamusi aliyokuwa nayo, alisema fujo ni hali ya kutokuwepo kwa utaratibu mzuri au mpango, pamoja na hali ya ghasia na machafuko.

Wakili Mrema alimuuliza Mnyika kama kauli iliyotolewa na Lissu Aprili 3, 2025 kwamba “ataleta fujo” na “atakinukisha” ilikuwa ni fujo yenyewe.

Kutokana na muda, upande wa Serikali uliomba suala hilo liendelee kesho, na Jaji akaelekeza kuwa swali hilo litashikiliwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

“SIFAHAMU MIPANGO YA CHADEMA KUHUSU VURUGU”

Katika dodoso jingine, Wakili Katuga alimuuliza Mnyika kuhusu madai ya kuwepo kwa mipango ya vurugu kabla na wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Mnyika alisema hafahamu mipango hiyo.

Alipoulizwa kuhusu madai kwamba baadhi ya wanachama waliwahi kuzungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa kulikuwa na mipango iliyopangwa na kuratibiwa na chama, Mnyika alisema hafahamu.

Pia alisema hafahamu madai ya kuwepo kwa mifumo maalumu ya mawasiliano ambayo ingetumika iwapo mitandao ya simu ingezimwa.

MNYIKA AULIZWA KUHUSU VURUGU ZA UCHAGUZI

Katuga alimuuliza Mnyika kama anafahamu kuwa vurugu za siku ya uchaguzi zilidaiwa kuwa zilipangwa na kuratibiwa.

Mnyika alisema alisikia kuhusu madai hayo.

Alipoulizwa kuhusu watu waliokamatwa kuhusiana na vurugu hizo, Mnyika alisema anafahamu kuwa baadhi yao walikamatwa na baadaye wakaachiwa.

Hata hivyo, alipohojiwa kuhusu madai kwamba watuhumiwa walifanya fujo kituoni kutokana na kauli za kiongozi wao, Tundu Lissu, Mnyika alisema hafahamu.

LISSU AOMBA MWENENDO WA KESI

Baada ya kesi kuahirishwa, Tundu Lissu aliomba apewe mwenendo wa kesi ili aweze kuusoma akiwa aliko.

Upande wa Serikali unatarajiwa kuendelea na dodoso kwa Mnyika kesho, huku kesi ikiendelea kufuatiliwa kwa karibu kutokana na ushahidi unaohusu kauli za viongozi wa CHADEMA, uchaguzi wa mwaka 2025 na madai yanayohusiana na vurugu.