Massanza Apigwa Faini ya Mil 10, Bodi ya Ligi Yatembeza Faini Polisi na Geita Gold

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) leo Septemba 4, 2026 imetangaza adhabu mbalimbali dhidi ya klabu, viongozi na waamuzi kutokana na makosa yaliyotokea katika michezo ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/27.

Katika taarifa iliyotolewa Septemba 4, 2026, TPLB imesema adhabu hizo zimehusisha makosa ya nidhamu, kuchelewa uwanjani, kukiuka taratibu za mechi pamoja na udhibiti wa waandishi wa habari.

SINGIDA BLACK STARS NA POLISI TANZANIA KUPIGWA FAINI

Katika mchezo namba 017 kati ya Singida Black Stars na Simba SC, uliomalizika kwa Simba SC kushinda 2-1, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Singida Black Stars, Hussein Massanza, amefungiwa na kutozwa faini ya Sh milioni 10.

Massanza ameadhibiwa kwa kosa la kushutumu na kutoa lugha ya matusi kwa waamuzi wa kati na wa pembeni baada ya mchezo, kinyume na Kanuni za Ligi Kuu kuhusu udhibiti kwa maofisa habari wa klabu.

Kwa upande mwingine, Afisa wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Singida Black Stars, Pablo Almasi, naye amepigwa faini ya Sh milioni 10 kwa kosa la kusambaza machapisho kwenye ukurasa wake wa Instagram yaliyoletea madharau na kumkashifu mwamuzi wa mchezo kati ya Young Africans na Coastal Union, pamoja na kuikebehi teknolojia ya Football Video Support (FVS).

Aidha, Polisi Tanzania imepata faini ya Sh milioni 10 kwa kosa la kumjumisha mchezaji mmoja kwenye orodha ya wachezaji 21 kwa ajili ya mchezo dhidi ya Singida Black Stars, kinyume na taratibu za mashindano.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Singida Black Stars, Hussein Massanza.

NAMUNGO YAADHIBIWA KWA KUCHELEWA UWANJANI

Katika mchezo namba 032 kati ya JKT Tanzania na Namungo FC, uliomalizika kwa JKT Tanzania kushinda 2-1, Namungo FC imepewa Onyo Kali kwa kosa la kuchelewa kuwasili kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kwa ajili ya mchezo uliochezwa Agosti 29, 2026.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Namungo iliwasili uwanjani saa 1:55 usiku, wakati mechi ilipangwa kuanza saa 1:30 usiku, jambo ambalo ni kinyume na kanuni za Ligi Kuu kuhusu taratibu za mechi.

TPLB imewakumbusha timu zote kuzingatia kikamilifu kanuni hiyo.

GEITA GOLD YATOZWA SH MILIONI 10

Katika mchezo namba 033 kati ya Simba SC na Geita Gold, uliomalizika kwa Simba kushinda 2-0, Geita Gold imepewa Onyo Kali kwa kosa la maafisa wake kuchelewa kwa dakika 15 kufika katika kikao cha kitaalamu cha maandalizi na uratibu wa mchezo.

Pia, klabu hiyo imepigwa faini ya Sh milioni 10 kwa kosa la kuwakilishwa na maafisa wawili pekee katika kikao hicho, kinyume na matakwa ya kanuni za Ligi Kuu.

AZAM FC YAONYA, WATU WAWILI WAFUNGIWA

Katika mchezo kati ya Kagera Sugar na Azam FC, uliomalizika kwa Azam FC kushinda 2-0, Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imefuta adhabu ya kadi nyekundu aliyokuwa ameonyeshwa Gibril Sillah, mchezaji wa Azam FC, baada ya kujiridhisha kupitia picha kwamba tukio hilo halikustahili adhabu hiyo.

Hata hivyo, Mwamizi wa akiba wa mchezo huo, Greyson Buchard wa Kagera, amepewa Onyo Kali kwa kosa la kuonesha mapungufu ya kiuchezaji yaliyotokana na kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu.

Aidha, Azam FC imepewa Onyo Kali kwa kosa la kuwakilishwa na Kocha Msaidizi katika Mkutano wa Wanahabari siku moja kabla ya mchezo, kinyume na taratibu za Ligi Kuu.

KOCHA JOHN ZONGWE AFUNGIWA MIEZI 12

Katika taarifa hiyo, TPLB pia imetangaza kufungiwa kwa miezi 12 kwa aliyekuwa Kocha Mkuu wa IAA, John Zongwe.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Zongwe aliwasilisha ombi la kupunguziwa adhabu baada ya kufungiwa kwa kipindi cha miezi 12, akieleza kuwa amejifunza kutokana na adhabu hiyo na kuahidi kuwa balozi mzuri kwa makocha wengine.

Hata hivyo, TPLB imesema Zongwe alifungiwa baada ya kubainika kumchezesha mchezaji ambaye katika mchakato wa usajili wake alitumia jina la Joseph Ombeni, badala ya Bryson Urio, jambo lililokiuka taratibu za usajili wa wachezaji.

Zongwe pia alikuwa tayari ametumikia miezi sita ya adhabu hiyo, huku akizingatiwa katika uamuzi wa kumruhusu kurejea kwenye shughuli za mpira wa miguu.

TPLB imesisitiza kuwa hatua hizo zinalenga kuhakikisha klabu, viongozi, wachezaji na wadau wote wanazingatia kanuni za Ligi Kuu na taratibu za mchezo.

TPF NET YATAKIWA KUIJENGA IMANI KWA JAMII

DODOMA. 

Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma

MTANDAO wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF NET) umetakiwa kuongeza ushirikiano na wananchi pamoja na kuendeleza shughuli za kijamii zitakazosaidia kujenga imani na mahusiano bora kati ya Jeshi la Polisi na jamii.

Wito huo umetolewa leo jijini Dodoma na Kamishna Msaidizi wa Polisi Daniel Bendarugaho, alipokuwa akizungumza katika mkutano wa Polisi Wanawake uliofanyika kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa majukumu yao na kuangalia namna ya kuimarisha uhusiano na jamii.

Bendarugaho amesema askari wa TPF NET wanapaswa kutambua nafasi yao katika jamii na kuhakikisha wanakuwa mfano wa kuigwa kupitia utendaji wao, mienendo na namna wanavyoshirikiana na wananchi.

Amesema uhusiano mzuri kati ya polisi na wananchi ni muhimu katika kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya Jeshi la Polisi, hususan katika masuala ya ulinzi na usalama.

Kwa mujibu wa Bendarugaho, Polisi Wanawake wanapaswa kutumia shughuli mbalimbali za kijamii kama fursa ya kuwafikia wananchi, kuwasikiliza na kuelewa changamoto zinazowakabili katika maeneo yao.

Amesema hatua hiyo pia itasaidia kuongeza ushirikiano wa wananchi na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa na kushiriki katika jitihada za kuzuia uhalifu.

Kwa upande wake, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Mossi Ndozero amesema TPF NET imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na makundi mbalimbali ya kijamii katika kutekeleza shughuli zenye manufaa kwa wananchi.

Ndozero amesema miongoni mwa shughuli zinazofanywa na mtandao huo ni usafi katika shule, kuwatembelea wagonjwa hospitalini pamoja na kutoa misaada katika vituo vya watoto yatima.

Amesema shughuli hizo ni sehemu ya jitihada za Polisi Wanawake kuendelea kuwa karibu na jamii na kuonyesha kwa vitendo dhamira yao ya kushiriki katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Ndozero amesisitiza kuwa kuimarishwa kwa shughuli hizo kutasaidia kujenga mahusiano yenye tija kati ya Polisi Wanawake na jamii, jambo litakalochangia kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa majukumu ya ulinzi na usalama.

 

Tarehe Ya Diddy Kuachiwa Gerezani Yasogezwa Mbele Tena

Mwanamuziki na mfanyabiashara wa Marekani, Sean “Diddy” Combs, anatarajiwa kuachiwa huru Februari 5, 2028, baada ya tarehe yake ya kuachiwa gerezani kusogezwa mbele kwa mara nyingine.

Kwa mujibu wa rekodi za mfumo wa magereza wa Marekani, tarehe mpya ya kuachiwa Combs, mwenye umri wa miaka 56, sasa imewekwa kuwa Februari 5, 2028, ikiwa ni siku 15 mapema kuliko makadirio ya awali ya Februari 20, 2028.

Taarifa kuhusu mabadiliko hayo ziliripotiwa Septemba 3, 2026 na vyombo mbalimbali vya habari nchini Marekani, vikiwemo TMZ, People, Page Six, Hot 97 na Extra, baada ya tarehe hiyo kuonekana katika rekodi za mfumo wa magereza.

Combs kwa sasa anatumikia kifungo cha miezi 50 katika gereza la Federal Correctional Institution Fort Dix, lililopo New Jersey.

Tarehe yake ya kuachiwa imekuwa ikibadilika mara kadhaa katika miezi ya hivi karibuni. Awali, makadirio yalionesha angeachiwa baadaye mwaka 2028, kabla ya tarehe hiyo kusogezwa mbele hatua kwa hatua.

Mwezi Julai, makadirio ya kuachiwa kwake yaliwekwa Januari 2028, kabla ya kusogezwa hadi Februari 20, 2028. Mabadiliko hayo yalifuatia taarifa kuhusu mzozo uliodaiwa kutokea kati yake na mfungwa mwingine akiwa gerezani.

Sasa, rekodi mpya zinaonesha kuwa Februari 5, 2028 ndiyo tarehe inayotarajiwa ya kuachiwa kwake.

Hata hivyo, tarehe hiyo si ya mwisho na inaweza kubadilika tena. Mfumo wa magereza wa Marekani unaweza kurekebisha tarehe za kuachiwa kulingana na namna kifungo kinavyohesabiwa, ikiwemo muda aliotumikia na mikopo anayoweza kupata kwa mujibu wa taratibu za magereza.

Combs alihukumiwa kifungo cha miezi 50 baada ya kupatikana na hatia katika makosa mawili yanayohusiana na usafirishaji wa watu kwa madhumuni ya kujihusisha na ukahaba.

Pamoja na hukumu hiyo, baadhi ya madai yaliyowasilishwa dhidi yake yameendelea kupingwa, huku kesi yake ikiendelea kufuatiliwa kwa karibu na vyombo vya habari nchini Marekani.

Kwa sasa, macho yanaelekezwa kwenye tarehe mpya ya Februari 5, 2028, na iwapo itabaki kuwa tarehe rasmi ya kuachiwa kwa Diddy kutoka gerezani.

WMA YAIMARISHA ULINZI WA WANANCHI DHIDI YA VIPIMO VISIVYO SAHIHI.

NA CHAUSIKU SAID 

MATUKIO DAIMA MWANZA.

WAKALA wa Vipimo (WMA) imejipanga kuimarisha ulinzi wa wananchi dhidi ya matumizi ya vipimo visivyo sahihi kwa kuwafuata wafanyabiashara katika maeneo yao na kufanya uhakiki wa vifaa vinavyotumika katika shughuli mbalimbali.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanahudumiwa kwa ustahiki bila kuibowa na biashara kutokana na matumizi ya mizani na vipimo ambavyo havijahakikiwa na Wakala huo.

Akizungumza katika ufunguzi wa Maonesho ya 21 ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayoendelea katika viwanja vya furahisha Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Mkurugenzi wa Huduma Saidizi wa Wakala wa Vipimo (WMA), Christopher Mwakibinga, ameeleza kuwa wataendelea kusogeza huduma karibu na wananchi sambamba na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kutumia vipimo sahihi.

Mwakibinga amesema kwa sasa WMA haitasubiri wananchi au wafanyabiashara kufika katika ofisi zake, bali itawafuata katika maeneo yao ya biashara kwa lengo la kutoa elimu na kufanya uhakiki wa vipimo na kusisitiza umuhimu wa wananchi kuhakikisha wanatumia vifaa vya kupimia vilivyohakikiwa na Wakala wa Vipimo.

“Vipimo vilivyohakikiwa vinatambulika kwa urahisi kwa kuwa huwekwa alama maalumu pamoja na stika au stampu inayoonesha kuwa kifaa hicho kimekaguliwa,” Amasema Mwakibinga.

Mwakibimga amesema kuwa mbali na uhakiki wa vifaa vya kupimia, wanakagua bidhaa zilizofungashwa zinazozalishwa ndani ya nchi pamoja na bidhaa zinazoingia kutoka nje ya nchi kupitia mipaka mbalimbali.

Aidha, ametoa onyo kwa wafanyabiashara wanaochezea au kulegeza mizani, akisema vitendo hivyo ni ukiukwaji wa sheria na kwamba Wakala huo umejipanga kuchukua hatua dhidi ya wahusika.

Hata hivyo, ameleza kuwa wataweka mkazo pia katika utoaji wa elimu, akibainisha kuwa baadhi ya wafanyabiashara wanaweza kuwa wanakiuka sheria kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha.

Kwa mujibu wa Mwakibinga, ameeleza kuwa wafanyabiashara wanaokiuka sheria kwa kutofahamu watapatiwa elimu, lakini wale watakaobainika kufanya ukiukwaji huo kwa makusudi watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

*DKT. MWIGULU: IFIKAPO 2030 MWANZA–DODOMA KWA SGR*

_▪︎ Aagiza Wizara ya Fedha na Uchukuzi kuharakisha utekelezaji_*

*_▪︎ Aelekeza leseni za madini zisizoendelezwa kufutwa_*

*_▪︎ Asisitiza kupunguzwa kwa matumizi yasiyo ya lazima_*

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameiagiza Wizara ya Fedha na Wizara ya Uchukuzi, kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC), wakandarasi na taasisi zinazohusika na uhamasishaji wa fedha, kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya Reli ya Kisasa (SGR), akilenga kuona ifikapo mwaka 2030 wajumbe kutoka Mwanza na mikoa ya Kanda ya Ziwa wakisafiri kwa treni kutoka Mwanza hadi Dodoma.

Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Septemba 04, 2026) wakati akitoa hoja ya kuahirisha Bunge la 13, Mkutano wa Nne, jijini Dodoma.

“Naziagiza Wizara ya Fedha na Wizara ya Uchukuzi, zikishirikiana na Shirika la Reli, wakandarasi waliopewa kazi ya kujenga vipande hivi pamoja na wale waliopewa jukumu la kuhamasisha fedha za miradi hiyo, kupambana usiku na mchana,” amesema.

Amesema Serikali inalenga kuhakikisha vipande vya Mwanza–Isaka, Isaka–Tabora, Tabora–Kigoma na Makutupora–Dodoma vinaendelea kutekelezwa kwa kasi.

“Ikiwezekana, ifikapo mwaka 2030, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka Mwanza, Mara, Shinyanga, Geita na Kagera waje Dodoma wakiwa wamepanda SGR kutoka Mwanza hadi Dodoma,” amesema.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwigulu ameiagiza Wizara ya Madini kuchukua hatua za haraka na kali kwa mujibu wa sheria dhidi ya watu wanaoshikilia leseni nyingi za madini bila kuziendeleza, akieleza kuwa hali hiyo inawanyima Watanzania wengine, hususan vijana na wachimbaji wadogo, fursa ya kufanya shughuli za uchimbaji.

“Mheshimiwa Waziri, futeni leseni hizo kwa mujibu wa sheria na gaweni upya maeneo hayo kwa wawekezaji Watanzania, vijana wa Kitanzania na wachimbaji wadogo,” amesema.

Dkt. Mwigulu amewataka Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, watendaji wa Serikali na halmashauri kuhakikisha wanawasikiliza wananchi, wanatatua kero zao kwa wakati na kutoa mrejesho.

Amesema ziara za viongozi wakuu hazipaswi kuwa mbadala wa utatuzi wa kero za wananchi katika ngazi za kawaida za Serikali.

“Kwa msingi huo, nawaagiza tena watendaji wote wa Serikali kuweka utaratibu wa kuwasikiliza wananchi, kutatua kero zao na kutoa mrejesho,” amesema.

Aidha, Waziri Mkuu amezitaka taasisi za Serikali kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, ikiwemo gharama za uendeshaji wa magari, safari, mikutano, warsha na makongamano, akisisitiza umuhimu wa kuelekeza fedha kwenye vipaumbele vya maendeleo.

Amesema hatua hiyo ni muhimu hasa kutokana na mahitaji makubwa yanayotarajiwa katika sekta ya elimu kuanzia mwaka 2028.

“Tusipobadili tabia ya matumizi, watoto wetu wanaweza kurudi tena kusomea chini ya miti. Tusirudi huko. Tayari tumeshavuka,” amesema.

Dkt. Mwigulu pia amezitaka Kamati za Maafa kuanzia ngazi ya vijiji hadi taifa kujiandaa kukabiliana na mvua kubwa zinazotarajiwa katika baadhi ya maeneo nchini kuanzia wiki ya nne ya Septemba na wiki ya kwanza ya Oktoba 2026.

Amesema maeneo hatarishi yanapaswa kutambuliwa mapema, huku vifaa vya uokoaji, huduma za dharura na mifumo ya mawasiliano vikiwa katika hali ya utayari.

Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kutekeleza Bima ya Afya kwa Wote tangu Januari 2026 na amewataka Watanzania wenye uwezo kujiunga ili mfumo huo uweze kuwasaidia pia wananchi wasiokuwa na uwezo.

Amesema Serikali tayari imetenga zaidi ya Shilingi bilioni 48 kusaidia matibabu ya magonjwa ambayo Watanzania wengi hawawezi kumudu gharama zake.

Kuhusu maandalizi ya AFCON 2027, Dkt. Mwigulu amesema Serikali inaendelea na ujenzi na ukarabati wa viwanja, miundombinu ya usafiri, huduma za maji, umeme na afya, akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha Tanzania inanufaika kiuchumi kwa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

Aidha, amezitaka timu za Tanzania zitakazoshiriki mashindano ya CAF kufanya vizuri na kuwataka Watanzania kuweka mbele uzalendo kwa kuziunga mkono timu zote zinazowakilisha nchi.

Baada ya kutoa maelezo hayo, Dkt. Mwigulu ameomba Bunge la 13, Mkutano wa Nne, liahirishwe hadi Jumanne, Oktoba 27, 2026, saa 3:00 kamili asubuhi, litakapokutana tena katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

GEITA KUPATA MSUKUMO MPYA WA UWEKEZAJI KUPITIA UMEME

SHUGHULI za uzalishaji na uwekezaji mkoani Geita zinatarajiwa kupata msukumo mpya baada ya Serikali kuanza utekelezaji wa mradi wa Sh bilioni 63.19 wa kuongeza uwezo wa kusafirisha umeme kutoka Mpomvu hadi kituo cha GGM.

Mradi huo unahusisha ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 6.7, huku ukilenga kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya umeme linalotokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi katika eneo hilo.

Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, alisema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha miundombinu ya nishati inaendana na kasi ya ukuaji wa uchumi na mahitaji ya wananchi pamoja na wawekezaji.

Amesema uwekezaji katika miundombinu hiyo unatarajiwa kuongeza uhakika wa umeme na kutoa mazingira bora kwa shughuli za uzalishaji, jambo litakaloweza kuongeza ajira, mapato na kuvutia uwekezaji zaidi mkoani humo.

“Tunataka kuona umeme unaozalishwa nchini ukitumika kikamilifu kuchochea uzalishaji, kuongeza ajira, kuongeza mapato na kuvutia uwekezaji zaidi miradi huu ni kielelezo cha falsafa hiyo,” alisema Makamba.

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange, amesema utekelezaji wa mradi huo utachukua miezi 18 kuanzia siku ya kusainiwa kwa mkataba, akibainisha kuwa moja ya malengo yake ni kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya umeme kwa GGM.

Amesema GGM ni miongoni mwa wateja wakubwa wa TANESCO wanaochangia mapato makubwa kwa Shirika, hivyo kukamilika kwa mradi huo kutakuwa na manufaa kwa TANESCO, mteja huyo na uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Balozi Zuhura Bundala, amesema uwekezaji huo ni sehemu ya mkakati wa kuongeza uwezo wa Shirika kuhudumia mahitaji ya wateja na wakati huo huo kuweka msingi wa fursa mpya za uwekezaji na ajira.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini, Subira Mgalu, amesema hatua hiyo inaonyesha namna sekta ya nishati na madini zinavyoweza kushirikiana katika kuimarisha uchumi wa kisasa unaolenga kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashimu Komba, ameyemwakilisha Mkuu wa Mkoa, alisema Serikali ya mkoa iko tayari kushirikiana na mkandarasi ili kuhakikisha mradi unatekelezwa bila vikwazo na kukamilika kwa wakati.

Amesema kukamilika kwa njia hiyo mpya kutasaidia kuachia njia ya awali ya msongo wa kilovoti 33 kuendelea kunufaisha wananchi wa Geita na maeneo ya jirani, huku mfumo mpya ukiongeza uwezo wa kusafirisha umeme na kuwezesha shughuli za uzalishaji na uwekezaji kuendelea kukua.

Liverpool Kuivaa Ipswich Leo, Presha Ya Ushindi Yaongezeka

Ligi ya EPL kupigwa tena leo kwa Mchezo kati ya Ipswich Town wakiwakaribisha Liverpool katika uwanja wa Portman Road, katika raundi hii ya EPL. Liverpool wanaingia wakiwa bado hawajapata ushindi baada ya sare mbili za 2-2 dhidi ya Newcastle United na Nottingham Forest, hivyo presha ya kupata pointi tatu imeongezeka.

Kwa upande wa Ipswich Town, mwanzo wao unaonyesha uwezo wa kushindana nyumbani. Waliitandika Sunderland 2-1katika mchezo wao wa kwanza wa ligi kabla ya kupokea kipigo cha 5-2 kutoka Manchester United ugenini. Hata hivyo, ushindi huo wa nyumbani unaonyesha kwamba Liverpool hawawezi kuuchukulia mchezo huu kirahisi, hasa mbele ya mashabiki wa Ipswich.

Liverpool wanaonekana kuwa na changamoto kubwa zaidi katika safu yao ya ulinzi, baada ya kuruhusu mabao manne katika mechi mbili za kwanza za ligi. Kocha Andoni Iraola atahitaji kuboresha mpangilio wa timu bila mpira, huku akitafuta uwiano kati ya kushambulia na kujilinda.

Liverpool pia wameongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji kwa kumsajili Bradley Barcola kutoka PSG kwa ada inayoripotiwa kufikia £123 milioni, na anaweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachokabiliana na Ipswich.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kimbinu, Ipswich wanaweza kutumia nguvu ya uwanja wa nyumbani, mashambulizi ya haraka na mipira ya pembeni kujaribu kuisumbua safu ya Liverpool. Hata hivyo Liverpool, kwa upande mwingine, wanatarajiwa kutaka kumiliki mpira zaidi na kutumia kasi ya washambuliaji wao kuvunja ngome ya ulinzi ya IPSWICH.

Historia pia ipo upande wa Liverpool, ambao walishinda 2-0 walipokutana na Ipswich katika mechi yao ya kwanza baada ya kurejea EPL msimu wa 2024/25.

Kwa ujumla, Liverpool wanaonekana kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kushinda kutokana na ubora na uzoefu wa kikosi, lakini mwanzo wao wa msimu umeonyesha udhaifu ambao Ipswich wanaweza kuutumia.

Nandy Amtambulisha Linah Kwenye lebo yake ya African Princess

Global Publishers
September 4, 2026
90 views
0 Comments

CEO wa lebo ya muziki ya The African Princess, mwanamuziki Nandy (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mwanadada nguli wa muziki wa Bongo Flava, Linah Sanga.

CEO wa lebo ya muziki ya The African Princess, mwanamuziki Nandy, amemtambulisha rasmi mwanadada nguli wa muziki wa Bongo Flava, Linah Sanga, kuwa msanii mpya wa lebo hiyo.

Linah sasa anaungana na Pipi Jojo chini ya The African Princess, hatua inayofanya lebo hiyo kuwa na jumla ya wasanii watatu, akiwemo Nandy mwenyewe.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nandy amemkaribisha Linah ndani ya lebo hiyo huku akimuelezea kama “Ndege Mnana” na dada yake mpendwa.

“WELCOME THE AFRICAN PRINCESS LABEL OUR LOVELY SISTER NDEGE MNANA..! @linahafrica,” ameandika Nandy.

Kujiunga kwa Linah kunatarajiwa kuongeza nguvu katika safu ya wasanii wa lebo hiyo, huku The African Princess ikiendelea na dhamira yake ya kukuza na kuendeleza vipaji vya wasanii wa kike katika muziki wa Afrika.