MAGAZETINI LEO JUMAMOSI SEPT 5/2026:KESI YA LISSU GOLUGWA ASHINDWA KUTHIBITISHA RIPOTI YA WAANGALIZI,MISURURU YA VIONGOZI INAVYOTAFUNA PESA

SAMIA KALAMU AWARDS 2026 -TUNAOMBA KURA ZA KUTOSHA CHOMBO CHETU CHA MATUKIO DAIMA MEDIA
1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI 
 MATUKIO DAIMA MEDIA (Kodi: 260215) kwa kutumia link hii hapa chini Kupiga kura
1;https://samiaawards.tz/mshiriki/260215
2:TUZO YA JINSIA,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 
BONYEZA LINK HII CHINI Kupiga kura⬇️
https://samiaawards.tz/mshiriki/260039
3:TUZO YA AFYA TANZANIA BARA
BONYEZA LINK HII CHINI Kupiga kura ⬇️
https://samiaawards.tz/mshiriki/260037
4:MWANDISHI WA HABARI ZA PICHA  
Bofya link hii chini KUPIGA KURA ⬇️⬇️
https://samiaawards.tz/mshiriki/260228
Kura yako ni mchango mkubwa sana kwa Matukio Daima Media . Tafadhali share pia kwa wengine ili kwa pamoja tusherekee ushindi wetu kwa kura za kishindo zaidi.
MATUKIO DAIMA MEDIA -NI YETU SOTE

 

Mpigie Kura Godmuya, Kura Yako Ni Ushindi! – Tuzo za Samia Kalamu Awards 2026

Global Publishers
September 5, 2026
984 views
0 Comments

Mtangazaji wa @globaltvonline na @255globalradio, Godfrey Nathan @godmuya ameteuliwa kuwania tuzo za Samia Kalamu Awards 2026.

Sasa Godmuya anaomba support yako, mfuatiliaji wa Global TV, kwa kumpigia kura ili kufanikisha ushindi wake.

🗳️ MPIGIE KURA: GODFREY LUHILABAKE NATHAN
🔢 Kodi: 260246

👉 Piga kura kupitia:
https://samiaawards.tz/mshiriki/260246

📌 Copy link hiyo kisha paste kwenye browser yako ili kumpigia kura.

Kura yako ni mchango mkubwa kwa Godmuya katika safari hii ya tuzo.

🙏 Piga kura, share na mwambie mwingine apige kura!

#SamiaKalamuAwards #VoteForGodmuya #Godmuya #GlobalTVOnline #255GlobalRadio

Beyoncé Atimiza Miaka 45, Aangaza Safari Yake Na Watoto Wake

MWIMBAJI maarufu wa Marekani, Beyoncé,  Septemba 4, 2026, anatimiza miaka 45 huku akisherehekea safari yake ya maisha na familia yake, hususan watoto wake watatu, Blue Ivy, Rumi na Sir.

Beyoncé, ambaye ni mshindi wa tuzo mbalimbali za Grammy na mtayarishaji wa vibao vingi vilivyofanya vizuri duniani, amekuwa akilinda kwa kiasi kikubwa maisha yake binafsi pamoja na familia yake.

Hata hivyo, katika miaka mbalimbali amekuwa akiwapa mashabiki wake fursa ya kuona baadhi ya nyakati zake za furaha akiwa na watoto wake, ambao amewapata pamoja na mume wake, mwanamuziki Jay-Z.

Moja ya kumbukumbu zilizowahi kuvutia mashabiki ni picha ya Beyoncé akiwa amewabeba mapacha wake, Rumi na Sir, katika picha iliyopigwa wakati wa Halloween na baadaye kushirikishwa katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa mwaka 2019.

Beyoncé pia amekuwa akionekana mara kwa mara akiwa na mtoto wake mkubwa, Blue Ivy, katika matukio mbalimbali ya kimataifa. Miongoni mwa matukio hayo ni mahudhurio yao kwenye uzinduzi wa filamu The Lion King jijini Hollywood mwaka 2019, ambapo mama na mwana walionekana wakiwa wamevalia mavazi yenye rangi nyeusi na fedha.

Familia hiyo pia imewahi kuonekana pamoja katika michezo ya NBA na hafla za tuzo za Grammy. Mwaka 2018, Beyoncé, Blue Ivy na mama yake Beyoncé, Tina Knowles, walihudhuria mchezo wa NBA All-Star mjini Los Angeles.

Katika Tuzo za Grammy za mwaka huo, Blue Ivy alivutia umakini baada ya kuonekana akiwaashiria wazazi wake wapunguze shangwe wakati wa hotuba, tukio lililoenea sana mitandaoni.

Beyoncé pia amewahi kuwashirikisha watoto wake katika safari zake. Katika makala maalumu Beyoncé Presents: Making The Gift ya mwaka 2019, mashabiki walipata nafasi ya kuwaona Beyoncé na Jay-Z wakiwa pamoja na watoto wao wakati wa safari barani Afrika.

Beyoncé alisema wakati huo kuwa kutembelea nchi za Afrika kwake kulikuwa jambo la kihisia, akieleza umuhimu wa watoto wake kufahamu asili na historia yao.

Mwaka 2023, Blue Ivy alianza kuonekana jukwaani akiwa na mama yake katika ziara ya Renaissance World Tour. Akiwa na umri wa miaka 11, Blue Ivy alisafiri katika maeneo mbalimbali duniani na kuendelea kuonyesha uwezo wake wa kucheza, hatua iliyomjengea umaarufu wake mwenyewe miongoni mwa mashabiki.

Safari hiyo pia ilionyeshwa katika filamu ya tamasha, Renaissance: A Film by Beyoncé, iliyowapa mashabiki picha za nyuma ya pazia za ziara hiyo.

Mwaka 2024, Beyoncé na Blue Ivy walionekana pamoja katika Tuzo za Grammy, kabla ya wawili hao kuonekana tena katika uzinduzi wa filamu Mufasa: The Lion King. Katika filamu hiyo, Blue Ivy alitoa sauti ya mhusika Kiara, binti wa Simba na Nala, ikiwa ni moja ya hatua kubwa katika safari yake ya kisanii.

Katika Tuzo za Grammy za mwaka 2025, Blue Ivy alisimama karibu na mama yake wakati Beyoncé akiweka historia kwa kushinda tuzo yake ya kwanza ya Album of the Year.

Familia hiyo iliendelea kuonekana pamoja katika Cowboy Carter Tour, ambapo Beyoncé aliwasogeza karibu watoto wake. Katika ziara hiyo, Rumi naye alipata nafasi ya kwanza kuonekana jukwaani katika uwanja mkubwa, akiambatana na mama yake na dada yake Blue Ivy wakati wa kuimba wimbo Protector.

Hivi karibuni, Blue Ivy pia aliungana na wazazi wake katika Met Gala ya mwaka 2026, akiwa amevalia gauni la Balenciaga pamoja na koti linaloendana nalo.

Beyoncé alisema wakati wa tukio hilo kuwa ilikuwa hisia za kipekee kwake kumuona binti yake akiwa sehemu ya tukio hilo kubwa la mitindo.

Katika kutimiza miaka 45, safari ya Beyoncé inaendelea kuonyesha si tu mafanikio yake katika muziki, bali pia nafasi kubwa ambayo familia yake imekuwa nayo katika maisha na kazi yake ya kisanii.

Jinsi ya Kuishi na Mwanaume Mkorofi Bila Kupoteza Amani Yako

Wapo wanaume wengi huwa wakorofi kwa wake zao au wapenzi wao na wanaume wa aina hii wapo wengi. Ukiwa na mwanaume wa aina hii na anakufanyiwa visa mbalimbali na ukorofi ujue kuna kitu labda anataka muachane au ana mchepuko ama ni hulka yake tu kuwa mkorofi.

Visa huwa haviishi sasa unatakiwa ujue jinsi ya kuishi naye; Mfano akianzisha ugomvi wa maneno unashauriwa kumuacha aendelee ili umsaidie kutoa yote ya moyoni wewe kaa kimya usimjibu,tena fanya kama unamsikiliza kwa makini, usiwe mwepesi kujitetea acha amalize yote
kama atakupa muda wa kujieleze muelezee taratibu kwa upendo.

Kama akianzisha mzozo ambao hujui chanzo chake wewe mnyamazie.Akimaliza kelele zake cha kufanya wewe anzisha jambo lingine kabisa mfano mwambie ulimmis sana na umemisi manjonjo yake kitandani tena kimapenzi kabisa ama mwambie muende matembezi au sehemu mliyozoea kwenda pamoja.

DAWA KUBWA YA MWANAUME MKOROFI NI KUWA MNYEYEKEVU.
Hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke mnyenyekevu hata ungekuwa umemkosea nini ukijishusha ukanyenyekea analainika labda awe na mapepo ndio unyenyekevu wako hautagusa moyo wake.

Mume hafokewi, mume hagombezwi, mume humfanyia jeuri na kiburi, akinuna na wewe unanuna asipokutafuta na wewe humtafuti, utapoteza ndoa yako au upendo.

Kama ni mume wako wa ndoa unaruhusiwa kumng’ang’ania kama ruba, kuwa na tabia ya kumpapatikia mmeo sio kujipendekeza bali ni kuonyesha mapenzi, wewe upo hapo?

Asipokutafuta akitoka nyumbani na kutowasiliana kwa muda mrefu, mtafute, asipoongea na wewe, ongea naye wewe kwa lugha ya mahaba sauti ya mahaba. Kufanya hivyo kutamfanya akupende Zaidi na kukufikiria kila anapokuwa mbali na wewe.

Kunyenyekea hakukugeuzi uonekane bwege, na ukapoteza nafasi yako ya kuwa mke, ila kiburi na jeuri ndio vitakufukuza kwenye hicho kiti na hiyo nafasi ya kuwa mke kuponyoka haraka sana.

Ujeuri weka pembeni! Hivyo ndivyo wanavyofanya waliodumu kwenye ndoa zao. Kwa maelezo haya machache kifupi ni kwamba unyenyekevu kwa mumeo ndio kujenga ndoa yako na ndio dawa pekee na kudumisha ndoa.

Nasisitiza kuwa mnyenyekevu sio kuwa mpumbavu ushauri muhimu ni kwamba panapotakiwa hekima na akili zitumie.

Makala na Elvan Stambuli, Global Digital

Fahamu Kanisa la ajabu Barcelona, Ujenzi wake Wachukua Miaka 140

Global Publishers
September 5, 2026
1,374 views
0 Comments

Ukiambiwa kuna kanisa ambalo ujenzi wake umechukua zaidi ya miaka 140 na bado haujakamilika, huenda ukashangaa. Lakini hali hiyo ipo katika jiji la Barcelona nchini Hispania, ambako kuna kanisa maarufu la Sagrada Família.

Ujenzi wa kanisa hilo ulianza mwaka 1882, kabla ya mbunifu Antoni Gaudí kuchukua jukumu la kuendeleza usanifu wake. Gaudí alilitumia sehemu kubwa ya maisha yake katika kulibuni na kulisimamia, lakini alifariki mwaka 1926 kabla ya kukamilika.

Baada ya kifo chake, ujenzi uliendelea kwa kutegemea michango na misaada ya watu binafsi. Hata hivyo, safari ya ujenzi haikuwa rahisi.

Mwaka 1936, wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Hispania, sehemu ya nyaraka, michoro na vielelezo vya Gaudí ziliharibiwa, jambo lililosababisha changamoto kubwa kwa waendelezaji wa mradi huo katika kujaribu kufuatilia maono yake ya awali.

Kutokana na ukubwa na ugumu wa usanifu wa jengo hilo, pamoja na mabadiliko yaliyotokea kwa miaka mingi, ujenzi umeendelea kwa hatua tofauti hadi sasa.

Sagrada Família liliwekwa wakfu mwaka 2010 na kutangazwa kuwa basilika ndogo, huku likifunguliwa rasmi kwa umma.

Kinacholifanya kanisa hilo kuwa la kipekee ni kwamba hata baada ya kutumika kwa ibada na kutembelewa na watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani, baadhi ya sehemu zake bado zinaendelea kujengwa.

Kwa hiyo, zaidi ya miaka 140 tangu kuwekwa jiwe la msingi, Sagrada Família bado linaendelea kuwa moja ya miradi mikubwa ya usanifu na ujenzi duniani, likibeba historia ndefu ya maono ya Antoni Gaudí na vizazi vilivyokuja baada yake.

Makala na Elvan Stambuli, Global Digital

*”SHERIA YA VIPIMO NI RAFIKI WA WOTE, MUUZAJI NA MNUNUZI”*

 *Na WMA – MWANZA* 

 Wakala wa Vipimo (WMA) umesisitiza kuwa ni rafiki wa muuzaji na mnunuzi na kwamba sheria ya vipimo haikuundwa kuwakomoa wafanyabiashara bali kuwasaidia kufanya biashara ya haki.

 Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 4, 2026 katika Siku ya Nane ya Maonesho ya 21 ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayoendelea katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.

Wakiizungumza kwa nyakati tofauti na wageni waliotembelea banda la WMA, Wataalamu wa Wakala wamesema lengo la uhakiki wa vifaa vya vipimo ni kulinda pande zote mbili.

“Muuzaji akitumia kipimo sahihi anajenga imani kwa mteja wake na kupata soko la uhakika. Na mlaji naye anapata thamani kamili ya fedha yake. Hapa hakuna mshindi na mshindwa. Sheria ya Vipimo ni msaada, sio adhabu” wamewaeleza wananchi.

Katika siku ya nane ya maonesho hayo, banda la WMA limeendelea kuwa kivutio kwa wafanyabiashara, wazalishaji na wananchi wa kawaida ambapo Wataalamu wameendelea kutoa elimu ya vipimo hususan jinsi ya kutambua vipimo halali pamoja na umuhimu wa kuhakiki vipimo mbalimbali ili kuepuka hasara katika biashara. 

WMA imesema ushiriki wake katika maonesho hayo ni sehemu ya mkakati wa kusogezwa kwa huduma kwa umma na kusikiliza changamoto za moja kwa moja kutoka kwa wadau. 

Wakala wa Vipimo umewahakikishia wananchi kuwa unaendelea kutoa huduma za uhakiki wa haraka katika Ofisi zao zilizopo mikoa yote ya Tanzania Bara na umewakaribisha kuendelea kutembelea banda lao katika Maonesho hayo hadi Septemba 6, 2026 yatakapofungwa.

 

Waziri Katambi Aagiza Dudu Baya Akamatwe, Afikishwe Mbele ya Sheria

Global Publishers
September 4, 2026
6 views
0 Comments

Dar es Salaam, Septemba 4, 2026 — Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ameliagiza Jeshi la Polisi kumtafuta na kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria msanii wa muziki Godfrey Tumaini maarufu Dudu Baya, baada ya kushindwa kuitikia wito wa Wizara hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, Katambi amesema Dudu Baya alitakiwa kufika katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya kutajwa katika tuhuma zinazohusiana na makosa ya jinai.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, msanii huyo aliitwa kwa mara ya pili, lakini bado hakufika katika ofisi za Wizara kama alivyotakiwa.

Katambi amesema Dudu Baya ameonekana kwenye mitandao ya kijamii akitoa kauli ambayo Waziri ameielezea kuwa ni ukaidi wa wito wa Serikali.

Kutokana na hali hiyo, Waziri Katambi ameliagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha msanii huyo anapatikana kokote aliko na kufikishwa mbele ya Jeshi hilo kwa ajili ya kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Agizo hilo linakuja wakati ambapo Dudu Baya amekuwa akizungumzia suala hilo kupitia mitandao ya kijamii, huku akieleza msimamo wake kuhusu wito alioupata kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Suala hilo limeendelea kuzua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, huku wadau na mashabiki wa msanii huyo wakisubiri hatua zitakazofuata baada ya agizo hilo la Waziri.

Rais Samia Afanya Uteuzi wa Viongozi Sita Katika Nafasi Mbalimbali

Dar es Salaam, Septemba 4, 2026 — Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi sita katika nafasi mbalimbali za umma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, baadhi ya uteuzi huo umejumuisha viongozi wapya kuchukua nafasi za waliomaliza muda wao.

Rais Samia amemteua Hamis Abdallah Mkunga kuwa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, akichukua nafasi ya Mick Kiliba, ambaye amemaliza muda wake.

Katika uteuzi mwingine, Rais Samia amemteua Prof. Alfred Said Sife kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), akichukua nafasi ya Prof. William Anangisye, ambaye pia amemaliza muda wake.

Aidha, Jaji Mstaafu Wilfred Peter Dyansobera ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), akichukua nafasi ya Edriss Mavura, ambaye amemaliza muda wake.

Rais Samia pia amemteua Prof. John Modestus Lupala kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi.

Katika uteuzi mwingine, Rais amemteua Mhandisi Abdallah Mohamed Mkufunzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Maji kwa kipindi cha pili.

Vilevile, Dkt. Henry Bethuel Mwanyika ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya TEHAMA, akichukua nafasi ya Prof. Leonard Mselle, ambaye amemaliza muda wake.

Taarifa hiyo imetolewa leo, Septemba 4, 2026, na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari S. Machumu.

Uteuzi huo unafanyika katika taasisi mbalimbali za umma zinazohusika na ajira, elimu, utatuzi wa migogoro ya kikazi, mipango ya matumizi ya ardhi, maji pamoja na TEHAMA.

*WAZIRI MAVUNDE AONGOZA KIKAO CHA UTATUZI MGOGORO WA HAKI MADINI NA HAKI ARDHI*

*Dodoma*

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde, akiongoza kikao cha utatuzi wa mgogoro wa haki madini na haki ardhi baina ya Kampuni ya Barrick na wachimbaji wadogo wa madini wa Tarime,Mkoani Mara.

Kikao hicho cha maridhiano, kimefanyika  leo tarehe 4 Septemba, 2026, jijini Dodoma ambapo Waziri Mavunde amezitaka pande zote mbili  kukaa na kujadiliana ili kuangalia namna ya bora ya kufika muafaka kwa kuzingatia maelekezo ya Sheria ya Madini Sura 123.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na  Mkuu wa Wilaya Tarime, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini,Katibu Mtendaji Tume ya Madini, Katibu Tawala Wilaya ya Tarime, Wawakilishi wa mgodi wa North Mara na walalamikaji.