Hussein Idd Hussein (37), mlinzi wa Kampuni ya Ruge Security,mkazi wa Kayenzi Manispaa ya Morogoro, anashikiliwa na jeshi la polisi Morogoro kwa tuhuma za mauaji ya Feisal Yaqoob Ally (43), dereva wa gari aina ya Scania lenye namba za usajili T 680 EAY, mkazi wa Mbagala, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Andrew Kantimbo alisema tukio hilo limetokea Septemba 9, 2026 majira ya saa 12 Alfajiri, katika eneo la kituo cha mafuta Puma kilichopo Mtaa wa Viwandani, Kata ya Kihonda, Manispaa ya Morogoro.
Inadaiwa kuwa marehemu alikuwa akitoka jijini Dar es Salaam kuelekea jijini Mwanza, alipofika katika eneo hilo na alisimama katika kituo hicho cha mafuta aliegesha gari lake kwa ajili kwenda kuswali katika msikiti uliopo karibu na kituo hicho.
Inadaiwa kuwa baada ya kutoka msikitini akielekea kwenye gari lake mtuhumiwa ambaye ni mlinzi alimtaka kumlipa kiasi cha shilingi 15,000 kwa kumlindia gari,lakini marehemu alikataa na kupanda kwenye gari kwa nia ya kuondoka ndipo
mlinzi alipofyatua risasi kwa kutumia bunduki na kumpiga dereva na kichwani na kusababisha kifo chake hapo hapo.
Katika tukio lingine,jeshi la polisi mkoa wa Morogoro linawashikilia watuhumiwa saba kwa mauaji ya Zakaria Rashid Malika (57), Afisa Ardhi mkazi wa Kibaoni Wilaya ya Kilombero.
Mauaji ya afisa huyo ardhi yaliyotokea Julai 19, 2026 katika Kijiji cha Kapolo CCM, Kata ya Kibaoni, Tarafa ya Ifakara, Wilaya ya Kilombero ambapo alivamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake na kumshambulia na kitu chenye makali na kumsababishia majeraha kwenye mwili wake na ķupelekea kifo.
Kamanda Kantimbo alisema julai 20,2026 polisi walitoa taarifa na kuwataka wananchi kutoa ushilikiano wa kuwasaka watuhumiwa ambapo kwa nyakati na maeneo tofauti walikamatwa watuhumiwa hao saba.
“Polisi baada ya kupokea taarifa kuhusu tukio hilo, lilifanya jitihada za kuwatafuta watuhumiwa hao kwa kushirikiana na wananchi na Watu saba walikamatwa kwa tuhuma za kupanga na kuhusika katika mauaji hayo,”alisema.
Alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu za awwli za upelelezi kukamilika.
Polisi linatoa wito kwa wamiliki wa Kampuni za ulinzi kuaji walinzi wenye weledi na wanaozjua sheria,taratibu na kanuni za matumizi sahihi ya silaha wakati wa kutekeleza majukumu yao ili kuzuia madhara kama haya kutokea.
Pia limewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola.
Mwisho.
MATUKIO DAIMA MEDIA IMETEULIWA KUWANIA TUZO ZA SKA2026 TUNAOMBA KURA YAKO WAWEZA KUPIGA KURA LEO TENA NI KILA BAADA YA MASAA 24 UNARUDIA KUPIGA KURA HADI SEPT 30
Barcelona inaanza safari yake ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2026/27 kwa kuikaribisha Feyenoord kwenye Spotify Camp Nou, katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Mchezo huo utachezwa leo Jumatano, Septemba 9, saa 19:45 usiku. Hii ni mechi ya kwanza ya hatua ya ligi ya Champions League, hivyo ushindi wa nyumbani utakuwa muhimu kwa Barcelona kuanza kampeni yake kwa nguvu.
Barcelona inaingia kwenye mchezo huo ikiwa katika hali nzuri baada ya kuanza msimu wa La Liga kwa ushindi mfululizo. Katika mchezo wao wa mwisho, vijana wa Hansi Flick waliichapa Valencia 5-0 ugenini, matokeo yaliyoonyesha ubora mkubwa wa timu hiyo katika kushambulia. Lamine Yamal, Raphinha na Fermín López wamekuwa miongoni mwa wachezaji wanaovuta macho, huku ujio wa Rodri ukiongeza nguvu na uzoefu katikati ya uwanja.
Kwa upande wa Feyenoord, timu hiyo ya Uholanzi nayo haijaanza vibaya msimu huu, ikiwa bado haijapoteza katika mechi zake za mwanzo za Eredivisie. Hata hivyo, changamoto kubwa kwao itakuwa kucheza dhidi ya Barcelona kwenye uwanja wao wenyewe, ambako kasi ya pasi, presha ya juu na uwezo wa Barça kutumia nafasi ndogo unaweza kuwa tatizo. Feyenoord pia imeonyesha udhaifu wa kiulinzi katika baadhi ya michezo, jambo ambalo Barcelona inaweza kulilenga kupitia mawinga wake wenye kasi.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Kimbinu, mchezo huu unaweza kuamuliwa zaidi katikati ya uwanja. inatarajiwa kutaka kutawala mpira na kuilazimisha Feyenoord kurudi nyuma, wakati wageni wanaweza kutumia mashambulizi ya kushtukiza wanapopata nafasi.
Kwa Flick, changamoto itakuwa kuhakikisha timu yake haishambulii kwa wingi kiasi cha kuacha nafasi nyuma. Kwa Feyenoord, nidhamu ya ulinzi na uwezo wa kuhimili presha katika dakika za mwanzo vitakuwa muhimu sana.
Kwa ujumla, Barcelona inaonekana kuingia kwenye mchezo ikiwa na nafasi kubwa zaidi kutokana na ubora wa kikosi, form nzuri na faida ya kucheza mbele ya mashabiki wake. Lakini Feyenoord si timu ya kubeza na inaweza kuifanya mechi kuwa ngumu ikiwa itafanikiwa kuzuia Barcelona kupata nafasi mapema. Hivyo, macho yatakuwa kwa Yamal, Raphinha na Rodri kwa upande wa Barça, huku Feyenoord ikihitaji mchezo wa karibu na nidhamu ili kupata matokeo Camp Nou.
Global Publishers September 9, 2026 0 views 0 Comments
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratias Ndejembi, ameagwa rasmi na Menejimenti ya Wizara ya Nishati pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Dodoma, Jumatano, Septemba 9, 2026.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba, pamoja na viongozi wa Menejimenti ya Wizara na Wakurugenzi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu wa Rais amewaasa viongozi na watendaji hao kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wasaidizi wake, ili waendelee kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuwahudumia wananchi.
Aidha, Makamu wa Rais amewataka viongozi na watendaji hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi, uaminifu na uzalendo, akisisitiza kuwa misingi hiyo ni muhimu katika kuhakikisha Serikali inatimiza matarajio ya wananchi.
Amewahimiza pia kuendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za Serikali katika kutekeleza majukumu yao na kuhakikisha sekta ya nishati inaendelea kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.
VIJANA nchini wametakiwa kuzingatia suala la Amani na usalama kwa nchi yao ili fedha zinazotolewa kwa ajili ya shughuli za uwezeshaji wa miradi ya kiuchumi kwa vijana ziweze kutekelezwa na kuleta tija kwa vijana hao.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Wazo Mwang’onda alisema hayo wakati wenge wa uhuru ulipotembelea kikundi cha umoja wa madereva wa bodaboda Makere halmashauri ya wilaya Kasulu mkoani Kigoma ambapo alisema kuwa Amani na usalama ukivurugika nchini hakuna kijana yeyote atafaidika na mabilioni ya shilingi ynayotolewa na serikali kwa vijana hao.
Alisema kuwa serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya kuinua shughuli za kiuchumi za vijana lakini pia msisitizo umetolewa kwa halmashauri kutumia mapato ya ndani kwa ajili ya uwezeshaji wa shughuli za kiuchumi za vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ambapo halmashauri ya wilaya Kasulu kwa mwaka uliopita imetoa kiasi cha Zaidi ya shilingi Bilioni moja kwa ajili ya mpango huo.
Awali mwenyekiti wa kikundi cha madereva bodaboda Makere, George Kagoma alisema kuwa tangu mwaka 2018 kikundi hicho kilipoanzishwa hadi sasa kimekopeshwa kiasi cha shilingi milioni 70.5 kutoka mapato ya ndani ya halmashauri ya wilaya Kasulu na tayari kiasi cha shilingi milioni 50.0 kimerejieshwa.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa baada ya kumaliza mkopo uliobaki wanatarajia kuomba mkopo mwingine kwa ajili ya kununua basi la abiria kwa ajili ya kuimarisha shughuli zao za kiuchumi na kwamba kwa maisha yao yamekuwa na mafanikio makubwa kwa kuweza kujenga nyumba, kusomesha watoto wao na kuhudumia vizuri familia zao.
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameitaka Afrika kujenga uwezo wake wa ndani wa kugharamia, kusimamia na kuzalisha mahitaji muhimu ya huduma za afya, badala ya kutegemea misaada na mifumo ya nje kwa muda mrefu.
Dkt. Mwigulu ameyasema hayo leo, Jumatano Septemba 09, 2026, wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Huduma za Afya ya Msingi unaofanyika jijini Arusha, ukiwakutanisha zaidi ya washiriki 2,700 kutoka mataifa 27.
Amesema Afrika inapaswa kubadili namna inavyoelewa na kutekeleza dhana ya kujenga uwezo, akisisitiza kuwa haipaswi kuishia katika miradi midogo isiyojenga uwezo wa kudumu, bali iwekeze katika uzalishaji wa dawa, vifaa tiba, teknolojia na wataalamu.
“Enzi zile nikiwa Waziri wa Fedha nilikuwa nawaambia nchi za Afrika zimeshashuhudia muda mrefu sasa wa maisha ya misaada na misaada inayoelekezwa pengine katika maeneo ambayo yanatofautiana na malengo ya ndani ya nchi kwa jina la capacity building. Capacity building. Capacity building. Na ndio tunaishia chapati, mandazi, sambusa. Hatuwekezi kitu kitakachodumu na kikawa endelevu.”
Dkt. Mwigulu amesema malengo ya ndani ya nchi yanayokwenda sambamba na malengo ya maendeleo endelevu yanapaswa kuheshimiwa na washirika wa maendeleo, ili misaada na uwekezaji viweze kuacha matokeo ya kudumu katika maisha ya Waafrika.
Amesema Tanzania inaendelea kuweka nguvu katika kuimarisha huduma za afya, ikiwemo kuongeza miundombinu, rasilimali watu na utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, ambayo Serikali imeanza kutekeleza mwaka 2026.
“Tunapozungumza kuhusu afya ya msingi, tusizungumzie tu kujenga vituo vya afya. Tujenge pia uwezo wa nchi zetu kugharamia huduma hizo, kuzalisha mahitaji yake na kutumia teknolojia zetu wenyewe,” amesema.
Aidha, amesema Tanzania imeanza kuwekeza katika uwezo wa ndani wa uzalishaji wa dawa ili kupunguza utegemezi wa misaada na kuhakikisha upatikanaji wa dawa unaendelea kuwa wa uhakika hata wakati dunia inapokumbwa na changamoto zinazoathiri minyororo ya usambazaji.
Amesema Serikali pia itaendelea kuboresha mazingira ya watumishi wa afya, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba za watumishi na kuongeza ajira katika sekta hiyo.
Dkt. Mwigulu amesema mkutano huo unapaswa kuzaa hatua mahsusi zinazoweza kutekelezwa na kupimwa, badala ya kuishia katika mijadala na maazimio.
Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC), Dkt. Jean Kaseya, amesema Afrika ya mwaka 2026 si Afrika ya mwaka 1960 na kwamba wakati umefika kwa washirika wa maendeleo kubadili namna wanavyoshirikiana na serikali za Afrika.
Dkt. Kaseya amesema serikali za Afrika zinapaswa kuwa na umiliki na uelewa wa rasilimali zinazotolewa kwa ajili ya afya, huku fedha za washirika zikiendana na mipango ya kitaifa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa WHO, Profesa Mohammed Janabi, amesema changamoto kubwa si kukosa suluhisho, bali ni kukosa ujasiri wa kuyafadhili, nidhamu ya kuyatekeleza na uwajibikaji wa kuyadumisha.
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe, amesema Serikali itaendelea kuongeza uwekezaji katika afya ya msingi kwa kuwa ndiyo ngazi inayohudumia wananchi wengi zaidi.
Amesema asilimia 95.6 ya wajawazito wanaojifungua nchini wanapata huduma katika ngazi ya afya ya msingi, huku asilimia 86 ya mahudhurio ya wagonjwa wa nje katika vituo vya umma yakihudumiwa katika ngazi hiyo.
Profesa Shemdoe amesema kati ya vituo 8,288 vya afya vinavyomilikiwa na Serikali, vituo 7,946 sawa na asilimia 95.8 ni vya ngazi ya afya ya msingi, hivyo uwekezaji katika ngazi hiyo ni uwekezaji wa moja kwa moja kwa wananchi wengi.
Mkutano huo wa siku tatu unajadili namna ya kuimarisha huduma za afya ya msingi kuelekea upatikanaji wa huduma za afya kwa wote, kupitia ufadhili endelevu, ufanisi, ubora wa huduma, ubunifu, ushirikiano wa kikanda na kujenga mifumo ya afya inayostahimili majanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameagwa rasmi na Menejimenti ya Wizara ya Nishati pamoja na Taasisi zilizo chini yake katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Kambarage Treasury Square, Dodoma. Jumatano Septemba 09, 2026.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughukia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba, Menejimenti ya Wizara na Wakurugenzi wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu wa Rais amewaasa Viongozi na Watendaji hao kuendelea kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Wasaidizi wake ili waendelee kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia Watanzania.
Aidha, Makamu wa Rais amewataka Viongozi na Watendaji hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi, uaminifu na uzalendo ili kutimiza matarajio ya wananchi kwa Serikali.
Msanii maarufu wa muziki nchini Marekani, Taylor Swift, akiwa na mume wake, Travis Kelce.
Msanii maarufu wa muziki nchini Marekani, Taylor Swift, ameonekana akiwa na mume wake, Travis Kelce, katika ‘date night’ jijini New York, huku akivutia kwa muonekano wake mpya pamoja na gauni lenye thamani ya takribani TSh milioni 7.2.
Wanandoa hao, wote wenye umri wa miaka 36, walitoka Jumapili, Septemba 6, 2026, na kwenda kupata chakula katika mgahawa maarufu wa Kihindi, Ambassadors Clubhouse New York, uliopo eneo la NoMad, Manhattan.
Swift alivaa gauni refu la hariri lenye mistari kutoka kwa mbunifu Stella McCartney, likiwa na thamani ya takribani dola 2,800 (TSh milioni 7.2). Alikamilisha muonekano huo kwa mkoba wa mbunifu huyo pamoja na viatu vya Aquazzura vya rangi ya metali.
Mbali na gauni hilo, Swift pia alionyesha mtindo wake mpya wa nywele fupi, ambao aliutambulisha Agosti 15, 2026, alipohudhuria harusi ya wahandisi wa muziki, Oli Jacobs na Laura Sisk, nchini Uingereza.
Kwa upande wake, Kelce alivaa shati la mikono mifupi la rangi ya krimu lenye mistari, suruali ya kahawia pamoja na viatu vya rangi nyeusi na nyeupe. Alikamilisha muonekano wake kwa miwani myeusi.
Kwa mujibu wa chanzo kilichozungumza na jarida la PEOPLE, Swift na Kelce walikula katika sehemu ya chini ya mgahawa huo wakiwa pamoja na wanaume wengine wawili. Waliagiza aina mbalimbali za vyakula na vinywaji kutoka kwenye menyu.
WAMEFUNGWA NDOA MIEZI MIWILI ILIYOPITA
Kutoka kwao jijini New York kumekuja takribani miezi miwili baada ya Swift na Kelce kufunga ndoa katika Madison Square Garden Julai 3, 2026.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na takribani wageni 1,000, wakiwemo mastaa mbalimbali na watu mashuhuri kutoka tasnia ya burudani. Sherehe hiyo iliendeshwa na rafiki yao, Adam Sandler.
Wanandoa hao walionekana wakiwa wameshikana mikono walipojitokeza hadharani kwa mara ya kwanza baada ya ndoa, Julai 10, 2026, katika harusi ya aliyekuwa mchezaji mwenzake Kelce, JuJu Smith-Schuster.
Kumbuka: Thamani ya TSh milioni 7.2 ni makadirio kutokana na dola 2,800 na kiwango cha ubadilishaji kilichotumika kwenye uandishi huu.
Global Publishers September 9, 2026 888 views 0 Comments
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS), kwa niaba ya Ofisi ya Rais, inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo kujaza nafasi zifuatazo:
Afisa Rasilimaliwatu Mwandamizi – Nafasi 5
Ngazi ya Mshahara: PSRS 6
Sifa za Mwombaji
Mwombaji anatakiwa:
Kuwa na Shahada ya Kwanza katika Utawala wa Umma, Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Mipango na Usimamizi wa Rasilimaliwatu au fani nyingine zinazohusiana na hizo kutoka taasisi zinazotambuliwa na Serikali.
Kuwa na uzoefu wa kazi wa miaka saba (7) au zaidi katika usimamizi wa rasilimaliwatu.
Kuwa amefanya na kufaulu Human Resource Officer’s Proficiency Examination (PHR).
Kuwa mtumishi wa Umma ambaye amefanya kazi kwa mwajiri wake wa sasa kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu (3).
Kuwa tayari kujigharamia gharama za uhamisho.
Majukumu ya Kazi
Afisa Rasilimaliwatu Mwandamizi atakuwa na majukumu yafuatayo:
Kufuatilia na kusimamia uzingatiaji wa Sheria za Kazi, Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma (Standing Orders), kanuni, taratibu na miongozo ya utumishi.
Kutunza kumbukumbu za watumishi kwa mujibu wa taratibu na miongozo iliyowekwa.
Kushiriki katika maandalizi, utekelezaji na ufuatiliaji wa bajeti ya mwaka.
Kusimamia masuala ya watumishi na kuratibu pamoja na kuandaa vikao.
Kushughulikia na kusimamia masuala ya kinidhamu kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.
Kusaidia kukadiria na kupanga mahitaji ya rasilimaliwatu.
Kushiriki katika uchambuzi wa mahitaji ya mafunzo na maandalizi ya mipango ya maendeleo na mafunzo ya rasilimaliwatu (HRDT).
Kuandaa rasimu za nyaraka, maelekezo, matangazo na nyaraka nyingine zinazohusu masuala ya watumishi.
Kusimamia utekelezaji wa Mfumo wa Upimaji na Tathmini ya Utendaji Kazi wa Watumishi (PEPMIS).
Kutekeleza majukumu mengine atakayopewa na msimamizi yanayohusiana na kazi hiyo.
Masharti Muhimu kwa Waombaji
Mwombaji lazima awe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na asiwe na umri zaidi ya miaka 45.
Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha aina ya ulemavu wao kwenye mfumo wa maombi.
Waombaji wote wanatakiwa kuambatisha cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
Maombi yaambatane na vyeti vya elimu na vyeti vya kitaaluma vinavyohitajika kwa nafasi husika.
Testimonials, Provisional Results, Statement of Results pamoja na Result Slips za Kidato cha Nne na Kidato cha Sita hazitakubaliwa.
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanapaswa kuhakikisha vyeti vyao vimethibitishwa na mamlaka husika kama TCU, NECTA au NACTVET.
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa wawe na kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
Uwasilishaji wa taarifa au sifa za kughushi utasababisha hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya mhusika.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Maombi yote yanatakiwa kutumwa kwa njia ya kielektroniki kupitia Recruitment Portal ya Sekretarieti ya Ajira:
Mwombaji anatakiwa kuambatisha barua ya maombi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu na nyaraka nyingine zinazohitajika.
Barua ya maombi ielekezwe kwa:
KATIBU, OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA, S.L.P. 2320, Mtaa wa Mahakama, Tambukareli, DODOMA.
Mwisho wa Kutuma Maombi
17 Septemba, 2026
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Sekretarieti ya Ajira inawakumbusha waombaji kuwa ni marufuku kutoa au kupokea rushwa kwa lengo la kupata ajira au kupangiwa kituo cha kazi. Mchakato wa ajira unazingatia misingi ya haki, usawa na uwazi, kwa kuzingatia sifa zinazohitajika kwa nafasi husika.
Limetolewa na: KATIBU SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Shahidi wa nne wa upande wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, Brenda Rupia, amekamilisha kutoa ushahidi wake leo Septemba 9, 2026.
Rupia, ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, amekuwa akijibu maswali ya mawakili wa Serikali kuhusu hotuba mbalimbali za Lissu, ikiwemo kauli zinazodaiwa kuwa na maneno kama “tutahamasisha uasi”, “hakuna reforms, hakuna uchaguzi” na “tutakinukisha.”
Katika dodoso hilo, Wakili wa Serikali, Katuga, alimuuliza Rupia kuhusu video ya Lissu aliyosema aliiona kupitia YouTube ya Jambo TV. Shahidi alithibitisha kuiona video hiyo, akisema Lissu alikuwa amevaa vazi la combat, ingawa hakukumbuka rangi ya vazi hilo wala kama alikuwa amevaa miwani.
Rupia pia alikiri kuwa katika video hiyo kulikuwa na bendera ya Taifa, huku alipoulizwa kuhusu bendera ya CHADEMA akisema hakumbuki na kuomba sehemu hiyo ya ushahidi ifutwe.
Katika sehemu nyingine ya ushahidi, Rupia alikiri kwamba Lissu alitumia neno “uasi”, lakini alieleza kuwa kwa uelewa wake kauli hiyo ililenga kupinga sheria kandamizi.
Brenda Rupia, ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chadema.
Alipoulizwa kuhusu kauli ya CHADEMA ya “No Reforms, No Election”, Rupia alisema ilikuwa ni msimamo wa chama uliomaanisha kuwa bila mabadiliko hakutakuwa na uchaguzi, lakini akasisitiza kuwa chama hakikusema kingezuia uchaguzi.
Wakili Katuga pia alimuuliza shahidi kama Lissu alielekeza njia za kuvuruga uchaguzi au “kukinukisha”, ambapo Rupia alijibu kuwa alielekeza.
Kwa upande wake, Wakili Job alimuuliza Rupia kuhusu majukumu yake kama Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA. Shahidi alieleza kuwa moja ya majukumu yake ni kuratibu mawasiliano ya chama na umma kupitia vyombo vya habari, pamoja na kusimamia utendaji wa watu walio chini ya idara yake.
Rupia pia alieleza kuwa ana elimu ya Accounting na hakusomea uandishi wa habari, lakini akasisitiza kuwa anasimamia idara nzima ya mawasiliano ya chama.
Katika maswali ya Wakili Tawabu Issa Tawabu, Rupia alisisitiza kuwa kwa mtazamo wake Lissu hakufanya kosa, huku akisema mamlaka ya mwisho ya kuamua kama mtu ametenda kosa ni mahakama.
Alipoulizwa maana ya uhaini, Rupia alisema kwa uelewa wake ni kuisaliti nchi au kutaka kupindua serikali. Kuhusu uasi, alitoa tafsiri kuwa ni kitendo cha kikundi cha watu kupinga au kubadili mfumo wa nchi bila kufuata sheria.
Wakili Tawabu pia alimuuliza kuhusu umiliki wa maudhui yaliyotangazwa na Jambo TV. Rupia alisema maudhui hayo ni mali ya chombo husika cha habari na kwamba Lissu si mmiliki wa Jambo TV wala maudhui hayo.
Wakati wa maswali ya Wakili Cuthbert Mbiling’i, Rupia alikiri kuwa yeye ni kiongozi wa CHADEMA na kwamba amekuwa mwanachama wa chama hicho tangu mwaka 2013. Alikubali pia kuwa ushahidi anaoutoa ni wa kumtetea kiongozi wake, lakini akasema yeye ni “shahidi mwenye interest ya haki kutendeka”, si kwa sababu ya kumlinda Lissu bila kujali ukweli.
Rupia pia alithibitisha kuwa Lissu alitamka maneno “uasi” na “tutakinukisha”, lakini akasisitiza kuwa maneno hayo hayakuwa kosa kwa uelewa wake.
Katika maswali ya Wakili Winniwa, shahidi alieleza tafsiri yake ya neno “uasi” kuwa ni kupinga au kukataa kwa nguvu kubwa. Alipoulizwa maana ya “kukinikisha”, alisema linahusiana na kitu kunukia au kunuka vibaya, akitoa mfano wa mtu anayepika pilau na harufu yake kuwafanya wengine watambue kuwa kuna mtu anapika.
Baada ya mawakili wa Serikali kukamilisha maswali yao, Jaji alitangaza kuahirisha mwenendo wa kesi hadi kesho saa 3:00 asubuhi, huku upande wa utetezi ukiendelea na hatua zake katika kesi hiyo.
Shahidi wa tano wa upande wa utetezi anatarajiwa kuendelea na ushahidi katika hatua inayofuata ya kesi hiyo.
Baada ya kukamilika kwa hatua hiyo, majaji waliiahirisha kesi hiyo kwa muda wa saa moja na nusu, hadi saa 8:30 mchana, ambapo shahidi wa tano wa upande wa utetezi anatarajiwa kupanda kizimbani kuanza kutoa ushahidi katika kumtetea Lissu.
Katuga: Waambie majaji kama ulifanikiwa kuona video ya mwemyekiti kwenye mtandao wa youtube wa jambo Tv.
Brenda: Ndio nilifanikiwa kuiona.
Katuga: Mshtakiwa alikuwa ameonekana amevaa nini?
Brenda: Nguo za Chama Combat
Katuga: Alikuwa amevaa combat ya rangi gani?
Katuga: Alikuwa amevaa miwani?
Katuga: Ni kweli kwamba ndani ya kombat alikuwa amevaa tshirt nyeusi?
Katuga: Kama uliona hiyo video kwenye nyuma kulikuwa na bendera ya taifa na chama.
Brenda: Ndio ni kweli kulikuwa bendera ya taifa na chadema.
Katuga: Bendera ya Chadema ina rangi gani?
Brenda: Blue, nyeupe na nyekundu
Katuga: Waambie majaji kama unakumbuka mashahidi waliosema wameona hii video na unakumbuka ushahidi wao wakisema walimuona mwenyekiti akiwa amevaa miwani, kombat na nyuma yake kuna bendera ya taifa na chadema.
Katuga: Hawa mashahidi waliambia mahakama walimuona lissu amevaa kombat sasa wewe na hawa mashahidi nani alisema uongo
Katuga: Unajua vitu vingine ni virahisi kama hawa mashahidi wamesema kwamba alikuwa amevaa kombat na nyuma yake kuna bendera.
Brenda: Ni ushahidi wangu kwamba mwenyekiti alikuwa amesimama nyuma kuna bendera ya taifa ila kama kuna bendera ya chadema sikumbuki naomba mfute hiyo.
Katuga: Waambie majaji kama ulisikia akisema majaji ni maccm.
Katuga: Waambie majaji kama alisema mahakamani hakuendeki.
Katuga: Waambie majaji kama ukisikia watafanyaje watatuua si watanikamata na kunifungulia kesi ya uhaini?
Katuga: Wakati unamsikia mwenyekiti akisema atashtakiwa kwa uhaini hii kesi ilikuwa imefunguliwa?
Katuga: Una mamlaka gani kusema kesi hii ni ya uongo?
Brenda: Mahakama ndio ina mamlaka kisheria Mimi sina mamlaka
Katuga: Ulisikia akisema mapolisi wanaingia na kura feki kwenye vibegi mgongoni.
Katuga: Unajua kama mshtakiwa ana kesi ya kutoa taarifa uongo Kisutu?
Brenda: Naomba nikumbushe kama yapo.
Katuga: Waambie majaji kama mwenyekiti hakutaka hotuba yake ifikie umma.
Brenda: Sijui kama alitaka au hakutaka.
Katuga: Waeleze majaji kama unajua mh lissu ana vyombo vyake binafsi vya kutoa taarifa zake.
Brenda: Sijui kama ana vyombo binafsi.
Katuga: Waambie majaji wakati mwenyekiti anataka kutoa taarifa yake kwa umma huwa anafanya nini kuufikia umma?
Katuga:Unajua au hujui kwamba mwenyekiti akitaka taarifa ifike kwa umma anaongea na waandishi wa habari.
Brenda: Anafanya press conference.
Katuga: Kwa hiyo ni ushahidi wako kwamba bwana mshtakiwa njia pekee anayotumia kuchapisha taarifa yake kwa wananchi ni kupitia vyombo vya habari.
Katuga: Neno uasi lazima lielekezwe dhidi ya watu fulani.
Brenda: Ni dhidi ya mtu watu fulani ni sahihi.
Katuga: Waambie majaji hili neno tutahamasisha uasi ambalo unasema ulisikia mwenyekiti akilisema ilikua kuhamasisha uasi dhidi ya nani?
Brenda: Dhidi ya sheria kandamizi.
Katuga: Sasa waambie majaji ile kuhamasisha uasi dhidi ya sheria ilikuwa ni kuichana hii sheria.
Katuga: Hivi mabadiliko ya kisiasa yanafanywa na watu au taratibu za kisheria.
Brenda: Nguvu na mamlaka ni ya watu hivyo watu ndio wanafanya mabadiliko.
Katuga: Uasi unaenda dhidi ya mfumo na watu wenye mamlaka au dhidi ya sheria kandamizi.
Katuga: Aliposema tutahamasisha uasi waambie waheshimiwa mtazuia sheria zisifanye uchaguzi au mtazuia watu.
Brenda: Yalilenga sheria kubadilishwa.
Katuga: Waambie majaji kwamba sheria ndio zinashiriki kupiga kura.
Katuga: Unaenda kuzuia watu wasipige kura au sheria.
Katuga: Nani wanapiga kura?
Brenda: Watu wanapiga kura.
Katuga: Unapozuia uchaguzi unamanisha nini unazuia watu au?
Brenda: Unazuia mchakato mzima.
Katuga: Unajua au hujui kama chadema inaamini katika demokrasia
Brenda: Iko kwenye falsafa ya chama.
Katuga: Unajua Tanzania iko katika mfumo wa vyama vingi?
Katuga: Waambie majaji kama hii no reforms no election ilikuwa katika msimamo wa chama.
Katuga: Kuna ushahidi hapa mahakamani kwamba no reforms no election ni msimamo uliolenga kuzuia uchaguzi mpaka mabadiliko yafanyike.
Brenda: Sio kweli ni msimamo wa chama hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi.
Katuga: Niko sahihi kusema chadema ilimaanisha kama hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi.
Brenda: ilisema hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi haikusema itazuaia uchaguzi.
Katuga: Unafahamu uchaguzi upo kwa mujibu wa katiba?
Katuga: Waambie majaji kama unafahamu kubadili katiba ni mchakato.Waambie majaji kwa kuwa wewe unatuambia katiba ni mchakato na uchaguzi uko kwa mujibu wa katiba mlioanza kusema kama hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi na no reforms ilianza 2024.
Katuga: Iambie mahakama ilipanga vipi kuzuia uchaguzi katika hotuba yake.
Katuga: Alielekeza njia za kuvuruga uchaguzi?
Katuga: Alielekeza au hakuelekeza njia ya kukinukisha?
Katuga: Kwa jina langu nitakuwa sahihi nikisema wewe ni mnyawezi mwenzangu
Katuga: Waambie majaji kama ulikuepo siku ya kupiga kura na ulikua wapi
Brenda: Nilikuwepo nyumbani basi haya
Katuga: Una cheo gani kingine ndani ya chama?
Brenda: Mimi Katibu wa BAWCHA mkoa wa Kinondoni
Katuga: Waambie majaji kama ulikitaja cheo hicho
Katuga: Waambie majaji hii ni reforms ni election ililenga mabadiliko katika nyanja gani
Brenda: ililenga mabadiliko katika nyanja ya kisiasa
Katuga: Waambie majaji kama katika hituba ya mwenyeki kama ni ushahidi wako kwamba uliona hiyo video
Brenda: Ni kweli niliona hii video
Katuga: Je, ni kweli uliona kwenye mtandao wa kijamii wa Jambo
Katuga: Uliangakia youtube ya Jambo TV
Brenda: Nimesema mitandao ya kijamii twende na hiyo hiyo youtube
Katuga: Waambie waheshimiwa majaji kama nikikusikia sahihi ukisema neno kukinukisha ni slang sio neno rasmi
Katuga: Nitakuwa sahihi nilisema slang ni lugha isiyo rasmi inayotumika na kundi kwenye jamii
Brenda: Ndio kama hivyo utakuwa sahihi
Katuga: Waambie majaji kama katika ushahidi wako ulisema maana yake na inatumika na kundi gani
Brenda: Sikusema inatumika na kundi gani nilisema maana yake
Kataga: Kama nitakuwa sahihi ulisema kukinukisha ni kufanya kitu kinukie vizuri au vibaya ni slan au lugha rasmi
Katuga: Kitendo cha kufanya kitu kinukie kinaitwaje
Brenda: Kukifanya kinukie
Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema nimekinukisha
Katuga: Kwa kuwa hujataja ni kundi gani wanatumia hiyo slang nitakuwa sahahi nikisema inatumika na vijana wenu
Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema mtu akisema anaenda kukinukisha anaenda kufanya jambo lisilo la kawaida
Jaji: hilo litakuwa swali la mwisho
Katuga: Ukisema raisi wa Jamuhuri ya Muungano hajatajwa kwenye hotuba ya mwenyekiti
Katuga: Mheshimiwa jaji umenielekeza hilo ni swali la mwisho
Jaji: Tuna ahirisha mpaka kesho saa tatu asubuhi kesho tuwahi
Katuga: Kuna nyaraka mshitakiwa aliomba zimeshapitiwa naomba apokee
Lissu: Hawa watu wananipa nyaraka zangu kama kina nani sababu hawa ndio wananishitaki
Jaji: Kwa hiyo unazihitaji?
Lissu: Niliomba maana yake nazihitaji
Jaji: Naomba hizo nyaraka mshitakiwa apewe
Katuga: Nina maswali yasiyopungua hamsini na hayajirudii na nikiangalia ni saa kumi na moja kamili
Jiji: Wewe anza tunafidia dakika tano tulizopoteza asubuhi na tunafidia nusu saa tuliyopoteza asubuhi.
Job: Kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa kuna mahali sheria hiyo inaruhusu kuvuruga uchaguzi?
Job: Kwa kuwa kwenye majibu yako umeeleza mahakama unaunga mkono maneno yote yaliyoko kwenye hati ya mashitaka kitendo hicho ni ukiukwaji wa katiba ya Chadema
Brenda: Utakuwa hauko sawa
Job: Kwa lugha nyingine kama sio sahihi unawaeleza majaji swala la kuvuruga uchaguzi kukinukisha kama lilivyosemwa na mshitakiwa msingi wake ni ibara ya tatu tatu moja ya katiba ya chadema
Brenda: Wingi wake unatokana na msimamo wa chama
Brenda: Msingi wake unatokana na msimamo wa chama
Job: Msingi unatokana na ibara ya tatu moja tatu
Brenda: Ndio unatokana na ibara hiyo
Job: Umetoa tamko lolote kuhusiana na mwenendo wa kesi hii
Job: Una shida ya kumbukumbu?
Brenda: Hapana nimetoa matamko mengi ila sio specific kwenye kesi hii licha ya kwamba nimekuwa nikitoa maoni yangu juu ya mwenyekiti kuendelea kushikiliwa sababu ya nia ovu ya serikali
Job:Ulitoa hayao kupitia wapi
Brenda: Kupitia simu yangu na mitandao ya kijamii
Job: Ulikuwa unazungumza na nani
Brenda: Ukiwa mtandaoni uzungumza mbele ya kamera ya simu yako
Job: ila ulitaka umma wa watanzania wafuatilie na wajue
Brenda: Sikumbuki ilikuwa lini
Brenda: Kati ya mwaka huu na mwaka jana
Job: Una fahamu kutokujua sheria hakuondoi kosa
Job: Unafahamu jinai haifi
Job: utakubaliana na mimi tamko hilo ulilotoa ni kinyume cha sheria za nchi
Job: Naomba nishie hapa wenzangu waendelee
Job: Shahidi nina maswali machache…Kama nilikusikia vyema ulishiriki kwenue ule mkutano wa tarehe tatu april 2025
Job: Nataka uwaambie majaji mwenyekiti wa chama Tundu Lissu wakati anaongea na hadhara alipotamka haya maneno uliyosomewa hapa aliungwa mkono hakuungwa mkono?
Job: Umeiambia mahakama ulikuepo
Job: Hebu iambie mahakama hii majukumu yako mahususi
Brenda: Ni pamoja kusimamia itifaki kwenye mikutano ya ndani na ya hadhara iwapo Katibu Mkuu anakuwa hayupo
Job: Swali linaweza kuwa pana tuliweke hivi kwenye hiyo sehemu ya mawasiliano kazi yako nini
Brenda: Waheshimiwa Majaji kuhusiana na mawasiliano huwa na ratibu pale chama kinapohitaji waandishi wa habari ambao kupitia kwao chama kinawasiliana na umma.Lakini pia mimi ninasimamia utendaji wa kazi unaofanywa na watu chini yangu
Job: Watu walioko chini yako wanafanya nini kuhusiana na mawasiliano
Brenda: Wana alika waandisha wa habari wanawasiliana na viongozi wanawasiliana na umma kupitia vyombo vya habari. Wanataoa matangazo kwa niaba ya kurugenzi ya mawasiliano ya chama
Job: Kwa hicho ulivhosema ni sahihi kuwa moja ya jukumu lako ni kuhabarisha umma
Job: Utakubaliana na mimi kwamba moja ya sheria katika nchi hii inayosimamia maswala ya habari ni media service act
Job: Ukiwa kama mkurugenzi wa mawasiliano umesoma
Brenda: Watu walioko chini yangu
Job: Waambie majaji wewe umesoma nini
Job: Huna elimu kuhusiana na mambo ya habari na wewe sio mwandishi wa habari
Brenda: Hapana sijasomea uandishi wa habari
Job: Ndugu shahidi umewahi kusikia neno kishoka
Brenda: Sijawahi kusikia kwa kingereza ni nini
Job: Utakubaliana na mimi kwamba mtu yeyote anayefanya kazi ya kutoa huduma ya habari na hana sifa za kutoa hiyo kwa mujibu wa sheria anakiuka maadili ya habari?
Job: Ni sahihi unawaeleza majaji ukiwa unafanya kazi Chadema ya kuhabarisha umma huitaji kuwa na sifa zilizo ainishwa kwenye sheria kwamba yeyote yule sheria hii haimuhusu
Job: Ni sahihi kwamba mtu yeyote ambaye hana sifa za kutoa huduma ya habari anaweza kufanya kazi kwenye idara ya mawasiliano Chadema?
Job: Kama nimekusikia vizuri ukisema taaluma ya habari sio hitajio kwenye hiyo idara
Job: Kama sio sahihi wewe ambaye unafanya kazi pale unafanya kazi kikamisa na hujui chochote
Brenda: Sio kweli kwamba sijui chochote na siko peke yangu niko na idara
Job: hiyo nguvu ya umma imetafsiriwa vipi kwenye katiba yenu
Brenda: Waheshimiwa majaji sio vizuri sana kukariri vifungu lakini ni kushirikisha umma mambo yake ikiwa chaguzi na kushirikisha umma katika matukio katika maamuzi
Job: Hayo unayofafanua yameandikwa kwenye katiba
Brenda: Ni tafsiri yangu mimi kama brenda
Job: Nitakuwa sahihi nikikuambia wewe Brenda huijui vyema falsafa ya Chadema?
Brenda: Utakua hauko sahihi
Job: Kwa sababu umepatia au nimekosea
Brenda: Utakua hauko sahihi
Job: Nitaomba shahidi atusomee ibara ya tatu ya chama chao niweze kumuuliza maswali
Brenda: Falsa ya chama ni kuamini katika nguvu ya umma
Brenda: anasoma …………..
Job: Swali umeelewa sawa hiyo ibara
Job: Unaelewa kwamba nchi hii ina katiba
Job: Wewe kama Brenda ulimuunga mkono wakati anatamka yale maneno
Brenda: Ndio nilimuunga mkono
Job: Kwa kukubaliana naye
Brenda: Ninakubaliana naye na hata leo nakubaliana na hayo maneno
Job: Ni sahahi kwamba ibara ya tatu moja tatu inaelekeza Chadema kulinda katiba ya Tanzania
Job: Na utakubaliana mimi sheria ya uchaguzi hapa nchini Tanzania ni moja ya sheria iliyotungwa katika msingi huu wa kikatiba
Brenda: Nakubaliana na wewe
Job: Katika msingi huo swala la kuvuruga uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2025 ni ukikwaji wa katiba ya nchi?
Job: Hebu isaidie mahakama waambie majaji kabla ya uchaguzi mkuu ufanyike ni sahihi kwamba Tume ya Uchaguzi imekuwa na utaratibu wa kutoa kanuni ya maadili ya wanasiasa yanayopaswa kuasainiwa
Job: Wewe ukiwa kama mwenezi chadema ilisaini hizo kanuni mwaka 2020
Tawabu: Uliposema ameshitakiwa kwa uongo unadanganya
Brenda: Shitaka ni la uongo
Tawabu: Imo au haimo kwamba alichapisha jambo
Brenda: Hilo halimo jambo tv haijatajwa kwenye hati ya mashitaka
Tawabu: Kuna watu uliwataja wako kwenye sekretarieti
Brenda: Sikumtaja John Heche kwenye sekretarieti
Tawabu: Ulisema maudhui ni mali ya chombo husika cha habari
Brenda: Nilisema mmliki wa maudhui ni chombo husika cha habari na. mmliki namba moja atakuwa mkurugenzi wa chombo husika
Tawabu: Diamond, Mbosso na Mario una wafahamu?
Tawabu: Wanajihusisha na nini?
Tawabu: Kwa hiyo anachokisema Tundu Lissu kupitia Jambo TV sio cha kwake?
Brenda: Ndio sio cha kwake
Tawabu: Uliulizwa haya maneno yaliyoko kwenye hati ya mashitaka ni kosa sio kosa
Tawabu: Unakumbuka tafsiri ya uasi nakuopa kamusi utusomee tena
Brenda: Kitendo cha kuwapinga wenye mamlaka..Kitendo cha uvunjaji wa sheria kinachofanywa na kikundi cha watu wanaotaka kuziondoa mamlaka za nchi yao
Tawabu: Kwenye maneno ya huyu bwana neno uasi lilikuwpo halikuepo
Tawabu: Ulisema kwamba kufanya kitu kitoe harufu nzuri au mbaya sio kosa
Tawabu: Ukifuga kuku wakatia harufu mbaya sio kosa au ni kosa
Brenda: Sioni kama nin kosa waheshimiwa Majaji
Tawabu: Kuna kifungu kwenye pino kodi kinaongelea kutoa harufu mbaya je huoni unakinzanza na sheria
Brenda: Mimi sijui nifafanulie hiyo sheria
Tawabu: Nikikuambia kuna sheria inazuia watu wasitoe harufu mbaya utakubaliana na mimi
Brenda: Nisomee hiyo sheria mimi siwezi kukubali
Tawabu: Wewe ni mtaalamu wa hesabu
Brenda: Nimesomea account
Tawabu: Mtu akisema asilimia ina maanisha nini
Tawabu: Ukisema asilimia kubwa una maanisha nini
Brenda: Ni zaidi ya asilimia hamsini
Tawabu: Hawa zaidi ya asilimia hamsini ni wakina nani
Tawabu: Kuna mahala ulisema tarehe kumi mwezi wa sita kwengine tarehe 17 ulikuwa unatumia kalenda gani
Brenda: Nilikuwa ninamaanisha tarehe niliyoitaja
Tawabu: Ulikuwa unamaanisha aina gani ya kalenda
Brenda: Sijui aina ya kalenda
Tawabu: Ulipokuwa unatoa ushahdi ulirudia sana mwenyekiti wa chama mkurugenzi wa chama hapa Tanzania kuna vyama vingapi vya kisiasa
Tawabu: Unaweza kututajia hata viwili
Brenda: Chadema, ACT, Chauma
Tawabu: Ulikuwa unasema mkuregenzi wa chama na hukusema chama gani
Brenda: Waheshimiwa Majaji nilipoanza kujieleza nilisema mimi ni Mkurugenzi Mawasiliano na Uenezi Chadema
Tawabu: unakubali kwamba ulisema chama ila hukussema chama gani
Tawabu: Umetuambia wewe ni mkurugenzi wa mawasiliano na uenezi
Tawabu: Unaposema mshitakiwa sio mfanyakazi wa Jambo TV kwa nafasi yako unaweza kujua?
Brenda: Hapana siwezi kujua
Tawabu: Umetuambia kwamba neno uasi ilitokana na kauli ya G55 hao G55 waliongea wakati gani kwenye mkutano wenu
Brenda: Hawakuongea alikuwa anajibu waraka wao
Tawabu: Unakubaliana na mimi mahakama hii ni ya kisheria na sio kihisia
Brenda: Ndio ninakubalina
Tawabu: Ulisema umekamatwa na polisi lakini haujawahi kupelekwa mahakamani hivyo unaombaia mahakama uko tayari kama mambo yako yamekubalika
Brenda: Kama wanaona kama wanamashitaka niko tayari
Tawabu: Ni hayo tu waheshia majaji
Tawabu Issa Tawabu: Naomba utusomeee neno haki kwenye kamusi
Tawabu: Kwa hiyo hapo kamusi inasema haki ni kumpa mtu kile anachostahili
Brenda: Hiyo ni definitation moja
Tawabu: Huyu mwamba anashitakiwa kwa kukika kifungu cha 39 cha kanuni ya adhabu hiyo nakupa taarifa sasa kanuni ya adhabu ni sheria na mahakama inasimamia haki na hilo lipo kikatiba.
Tawabu: Uliposema huyu bwana hajatenda makosa ulitoa wapi hayo mamlaka ya kusema hivyo
Brenda: Mamlaka ndio yenye kauli ya mwisho
Tawabu: Wewe hayo mamlaka unayo
Brenda: Mamlaka ya kutoa kauli ya mwisho ni ya mahakama
Tawabu: Umeulizwa sana kuhusu maneno aliyosema mshitakiwa umewahi kuelewa maana ya uhaini ni nini
Brenda: Ni kuisaliti nchi yako kutaka kupindua serikali huo ndio uelewa wangu wa uhaini
Tawabu: Kwa kuwa umetuambia tafsiri yako ya uhaini kwa uelewa wako wa kawaida na kukiwa na tafsiri nyingine inayoweza kuthibitishwa na Mahakama na mtu akatendewa haki huna shida.
Tawabu: Umeulizwa sana kuhusu uasi kamusi ya kiswahili inasemaje kuhusu uasi
Brenda: Kitendo kinachofanywa na kikundi cha watu kubadili mfumo wa nchi yao bila kufuata sheria
Tawabu: Hivyo ni sahihi tafsiri ya uasi ndio hiyo
Tawabu: Kwa hiyo uasi ni kuvunja sheria
Brenda: Ni sahihi kwa moja ya fasiri
Tawabu: Nchi yetu ni ya kisheria au inaendeshwa kiimla
Tawabu: Na kinachofanyika hapa Mahakamani
Brenda: Haya ni ya kimahakama
Tawabu: Uliambia mahakama una uwezo wa kufanya miujiza
Klabu ya soka ya Young Africans (Yanga SC) imeanza utekelezaji wa mpango wake wa kuwekeza katika miundombinu ya kibiashara baada ya kubomoa rasmi jengo lake la zamani lililopo katika makutano ya Mtaa wa Mafia na Nyamwezi, Kariakoo, jijini Dar es Salaam.
Jengo hilo linatarajiwa kujengwa upya na kuwa jengo la kisasa la ghorofa 12, mradi unaolenga kuongeza vyanzo vya mapato ya klabu na kuimarisha uwezo wake wa kifedha kwa muda mrefu.
Hatua hiyo imekuja baada ya uongozi wa Yanga, chini ya Rais wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said, kutangaza zabuni ya wazi kwa makampuni makubwa ya ujenzi yenye sifa na uzoefu, ili kupata kampuni itakayoshirikiana na klabu katika utekelezaji wa mradi huo.
Uwekezaji huo ni sehemu ya mkakati wa Yanga wa kupanua shughuli zake nje ya uwanja wa soka, kwa kutumia mali na miundombinu kama chanzo cha mapato ya kibiashara.
Uwanja wa Jangwani nao wajengwa
Mbali na mradi wa Kariakoo, Yanga pia inaendelea na maandalizi ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 20,000 katika eneo la Jangwani, Dar es Salaam.
Mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano na GSM Group, ambaye ni mmoja wa washirika wakuu wa klabu hiyo katika uwekezaji na maendeleo ya miundombinu.
Bajeti ya Yanga yafikia Sh bilioni 36.01
Katika Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika Ukumbi wa Super Dome, Masaki, uongozi wa Yanga uliwasilisha mchanganuo wa kifedha wa klabu, ambapo wanachama waliidhinisha bajeti ya Sh bilioni 36.01 kwa matumizi ya klabu.
Bajeti hiyo imeongezeka kwa takribani Sh bilioni 3, kutoka Sh bilioni 33 zilizopangwa msimu uliopita, hali inayoonyesha kuongezeka kwa shughuli na mahitaji ya kifedha ya klabu.
Kwa ujumla, hatua za Yanga katika ujenzi wa jengo la Kariakoo na uwanja wa Jangwani zinaashiria mkakati wa klabu kujenga mali za kudumu na vyanzo endelevu vya mapato, sambamba na mafanikio yake ndani ya uwanja.